Mbunge wa Ndanda Mkoani Mtwara (CHADEMA), Cecil Mwambe amejiuzulu nafasi hiyo na kutangaza kuhamia CCM
Mwambe amefikia uamuzi huo leo Februari 15, 2020 katika makao makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es salaam
Mwambe amefikia uamuzi huo leo Februari 15, 2020 katika makao makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es salaam
Takribani miezi miwili iliyopita, Mwambe alijitosa kugombea uenyekiti wa Chadema akichuana na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
Akizungumza kuhusu uamuzi wake huo Mwambe amesema vyama vya upinzani nchini vina safari ndefu ya kujenga demokrasia ya kweli, hivyo ameona atakuwa anajidanganya na kuwadanganya wapiga kura wake kubaki katika vyama vya namna hiyo wakati bado anatamani kuwatumikia wananchi wa Ndanda.
Mwambe alijiunga Chadema mwaka 2015 akitokea CCM ambako jina lake lilikatwa katika mchakato wa kura ya maoni kuwania kupitishwa kugombea ubunge
0 comments:
Post a Comment