Tuesday, 4 February 2020

Marekani yamaliza mafuzo ya kijeshi na kukabidhi vifaa kwa JWTZ

...
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson amekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 18 (Tsh bilioni 41.6) kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama sehemu ya Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Afrika (African Peacekeeping Rapid Reaction Program – APRRP).

Ubia wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Afrika (APRRP), ni ubia kati ya Marekani na nchi sita za Afrika ambazo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Senegal na Ghana wenye lengo la kujenga uwezo na utayari wa kutoa msaada wa kiuongozi na vifaa kwa oparesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU).

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, wakufunzi wa Kimarekani wamekuwa wakifanya kazi na kikosi cha JWTZ ambacho ni sehemu ya Kikosi cha Kimataifa cha Kulinda Amani ili kukijengea uwezo wa kushiriki katika operesheni za kulinda amani, utoaji misaada ya kibinadamu na huduma wakati wa majanga iwe nchini Tanzania na barani kote.

“Marekani itaendelea kuwa mbia imara wa JWTZ,” amesema Patterson katika hafla ya makabidhiano, na kuongeza kuwa “tutaendelea kuisaidia APRRP pamoja na mafunzo ya awali ya askari walinda amani wa Kitanzania.”


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger