Idadi ya waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini China imeongezeka kwa vifo 89 na kufikia watu 811.
Mmarekani na Mjapani pia ni miongoni mwa waliokufa. Watu hao ni raia wa kwanza wa kigeni kufa tangu kuzuka kwa mripuko huo.
Shirika la afya duniani limesema kumekuwa na jumla ya maambukizi 34,800 duniani kote.
Eneo lililoathirika zaidi ni China Bara, ambako kumethibitishwa watu 34,546 walioambukizwa.
Raia watano wa Uingereza akiwemo mtoto wamegundulika kuwa na virusi hivyo nchini Ufaransa.
Waziri wa Afya wa Ufaransa Agnes Buzyn amesema raia hayo waliambukizwa na raia mwingine wa Uingereza ambae katika siku za hivi karibuni alikuwa nchini Singapore.
0 comments:
Post a Comment