Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza ongezeko la bei kwa mafuta yanayoingilia Bandari ya Dar es Salaam.
Mabadiliko hayo yanatokana na kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani na ongezeko la bei katika soko la dunia.
Taarifa ya Ewura kwa mwezi Februari, 2020 inaonyesha lita moja ya petroli imepanda kwa Sh20 huku dizeli ikiongezeka kwa Sh74 na mafuta ya taa Sh44.
Ikilinganishwa na bei zilizokuwapo Januari 2020, bei za jumla ya petroli imeongezeka kwa Sh20.01 kwa lita, dizeli imeongezeka Sh74.21 na mafuta ya taa Sh43.96 kwa lita moja.
0 comments:
Post a Comment