Saturday, 15 February 2020

AU yaimairisha maandalizi ya mlipuko wa virusi vipya vya Corona

...
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) cha Umoja wa Afrika kimetangaza kwamba kinazidi kuimarisha juhudi ili kujiandaa na uwezekano wowote wa mlipuko wa virusi vipya vya korona vinavyosababisha nimonia (COVID-19).

Katika mkutano wake na wanahabari wa kila wiki, mkurugenzi wa Africa CDC Dkt John Nkengasong, amesema kituo kinaratibu juhudi na shughuli za maandalizi ya bara na kuitikia uwezekano wowote wa mlipuko wa COVID-19. 

Nkengasong amesema kikosi kazi cha Afrika juu ya virusi vipya vya korona kimeanzishwa miongoni mwa shughuli nyingine ili kuwezesha Afrika kujiandaa na kuwa na uwezo wa kuitikia endapo utatokea mlipuko.

Kikosi kazi cha Afrika, ambacho kinajumuisha wataalamu kutoka Afrika nzima kinaratibiwa na nchi tano zikiwemo Senegal, Kenya, Morocco, Nigeria na Afrika Kusini, ili kusimamia maeneo matano makubwa ya uangalizi, kuzuia na kudhibiti maambukizi, usimamizi wa matibabu ya wagonjwa wenye maambukizi makubwa ya virusi vipya vya korona, mawasiliano ya hatari na usimamizi wa jamii.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger