Tuesday, 17 October 2017

SABABU KUBWA ZILIZOFANYA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA ZAIDI YA 44000 KUKOSA VYUO VIKUU AWAMU YA KWANZA NA PILI 2017/2018

...
Habari zenu,

Kwa mara nyingine tena baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kusikika,tumerudi kwa kasi isiyopimika.

Leo tunapenda kuzungumzia kuhusu sababu zilizofanya wanafunzi wengi wakose nafasi za kuchaguliwa vyuo vikuu katika awamu ya kwanza na ya pili 2017/2018.

Awali kabla ya yote mfumo wa udahili ulikuwa chini ya TCU kwa miaka kadhaa hapo nyuma ambapo wanafunzi walikuwa wakiomba kupitia TCU,kwa mwaka huu ahali imekua tofauti baada ya wanafunzi ana wazazi wengi kulalamika kuwa TCU imekuwa ikiwapangia vyuo ambavyo hajachagua na kuifanya serikali kuelekeza kuwa sasa wanafunzi wataomba vyuo moja kwa moja chuoni.

Nikianza na hili,TCU imekuwa ikipangia watu vyuo vikuu ambao walikua na sifa ndogo ,Kwa mfano mtu una E E ambazo ni minimu qualification za kujiunga chuo na umeomba vyuo vya 5 lakini kutokana na ushindani unakosa chuo hivyo TCU wanaamua ili usikose chuo wanakupangia kozi yoyote ambayo itakufaa chuoni.

Watu wengi walilalamikia hili bila kujua dhumuni la TCU kufanya vile wakati ule,sasa wanafunzi wameomba moja kwa moja chuoni kozi mbalimbali na imekua ni kilio kikubwa sana kwa sababu vyuo vimekua (hasa vyenye majina makubwa) vikidahili wanafunzi wenye maksi za juu tu. na kuwafanya wanafunzi wengi hasa wenye sifa za kwenda chuo kikuu namaanisha D D AU C E kukosa nafasi katika kozi walizoomba.

SABABU KUBWA iliyowafanya wanafunzi wengi wakose vyuo ni ushindani mkubwa uliopo katika kozi husika na vyuo husika walivyoomba wanafunzi.

Kwa takwimu za haraka ni kwamba asilimia zaidi ya 80 ya wanafunzi walioomba vyuo mwaka huu walioomba vyuo kama SUA,UDSM,DUCE,MUCE,SAUT,UDOM na MUHAS  na kuvifanya vyuo hivi vichukue wanafunzi wenye ufaulu wa juu na wengi wao kukosa.

Hivyo ninazidi kuwashauri wanafunzi ambao bado hawajapata vyuo vikuu waombe vyuo ambavyo ambavyo wanadhani havina ushindani kuliko kukosa chuo na kukaa nyumbani,kwa sababu maisha ya mtaani ni magumu sana na huwezi jua  mwakani vigezo vikawaje.

Na kwa wale waliopata kuchaguliwa nawapongeza na kuwasihi wakasome kwa moyo wote na wakelewe darasani ili elimu watakayoipata waje waitumie mtaani kujiajiri.

Taarifa hii imendaliwa na 
MMILIKI WA MASWAYETU BLOG
(Blooger boy)

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger