Habari yenu wadau wapendwa wa blog hii ya MASWAYETU BLOG wadogo hamjambo?wakubwa shikamoni.
Kwanza kabisa nipende kuwapongeza wale
wote waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali ndani na nje ya Bongo
yetu hii.Hongereni sana kwani nyie ni baadhi ya vijana wengi waliokosa
nafasi hizo;
Leo napenda kuzungumzia mada kubwa
kuhusu ubadilishaji wa kozi uingiapo chuoni,Kutokana na vijana wengi
kuchaguliwa kozi ambazo hawazitaki,mfano mtu alikuwa anataka kusomea
ualimu akajikuta kachaguliwa hotel management au mwingine alikuwa
anataka kusomea udakatari akajikuta kachaguliwa Ualimu LEO nitaelezea
njia ambazo unaweza kuzifanya ili uweze kuadilisha kozi na kusoma kozi
unayoitaka;
Zifuatazo ni njia hizo;
1.KUBADILI KOZI SIKU YA KWANZA YA REGISTRATION
UFIKAPO CHUONI.
UFIKAPO CHUONI.
-Hii ni kati ya njia ambazo ni nyepesi sana ambayo itakufanya usome kozi unayotaka kusoma tofauti na uliyochaguliwa,ukifika
siku ya kwanza
chuoni.Wakati wa kusajiliwa utakuta kila kozi na sehemu yake,wewe nenda
moja kwa moja sehemu wanayosajili kozi utakayotaka kuhamia,then ongea na
yule anaesajili mwombe kwa upole atakusikiliza tu,usifanye papara
kusajili,MADHARA ya njia hii ni kwamba itaweza ikakupa usumbufu kwenye
mkopo baadae.
2.KUBADILI KUPITIA TCU.
-Hii pia inaweza ikakufanya uame kozi
unayotaka kuhama na kuhamia unayotaka kusoma,cha kufanya fata maelekezo waliyotoa tcu jinsi ya kuhama chuo kwa kubonyeza hapa>>>>>TARATIBU ZA KUHAMA CHUO
3.NJIA YA TATU NI KUANDIKA BARUA
-Njia hii ndio njia inayokubalika
kiofisi lakini kuhamishwa kwake kiukweli ni vigumu sana kwani unaweza
ukakauta wanaohamishwa kati ya wanafunzi 2000 ni 20 tu,na nikati ya njia
ngumu na ndefu sana kwani inaweza kukuchukua takribani wiki 4 hadi
kuhamishwa.KIKUBWA FIKA MAPEMA CHUONI HAPO.
Makala hii imeandaliwa na;
INNOCENT THE BLOGGER BOY(hata mimi nilifanikiwa kubadilisha kozi niliyochaguliwa)
MMILIKI HALALI WA MASWAYETU BLOG
Kama unaswali Ni follow instagram,then ni inbox,search>>>>MASWAYETU BLOG
0 comments:
Post a Comment