TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AWAMU YA TATU YA UDAHILI
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatangaza kuwa Awamu ya Pili ya Udahili wa waombaji wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 10 Oktoba 2017. Kutokana na waombaji wengi kutochaguliwa kwa sababu mbali mbali, Tume itafungua maombi kwa Awamu ya Tatu kuanzia tarehe 18 hadi 22 Oktoba 2017 na siyo 16 hadi 18 ya awali.
Tume inapenda kusisitiza yafuatayo:
a) Awamu hii itawahusu waombaji waliokosa nafasi kwenye Awamu ya Kwanza na ya Pili kutokana na ushindani au kukosa sifa katika programu walizoomba;
b) Waombaji waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja; wanatakiwa kuamua mara moja kwa kuchagua chuo kimoja tu na hatimaye kukiarifu chuo husika;
c) Awamu hii haitawahusu waombaji wapya (ambao hawajawahi kutuma maombi katika awamu mbili zilizopita);
d) Waombaji ambao hawatathibitisha uchaguzi wao au kujithibitisha zaidi ya chuo kimoja hawatatambuliwa na Tume katika udahili wa mwaka 2017/18
e) Waombaji kuwasiliana moja kwa moja na mara kwa mara na vyuo husika kwa masuala yote yanayohusiana na zoezi la udahili badala ya kuja TCU.
f) Waombaji wote kutembelea Tovuti za vyuo ili kufahamu hatima ya maombi yao. Aidha, Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi na kuthibitisha ni ule ule uliotumika katika awamu mbili zilizopita za Udahili.
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
0 comments:
Post a Comment