|
|
|
OFISI
YA RAIS
|
Anuani ya Simu: “TAMISEMI”
|
Tawala za MKOA na
|
||
Simu Na:
(026) 2322848, 2321607
|
Serikali za Mitaa,
|
||
2322853, 2322420
|
Jengo la Mkapa,
|
||
Nukushi:
(026) 2322116, 2322146
|
2 Barabara ya hospitali,
|
||
2321013
|
|
S.L.P. 1923,
|
|
41185 DODOMA.
|
|||
|
|
|
|
Unapojibu
tafadhali taja:
|
|
||
Kumb. Na. CD.
162/355/01
|
30
Oktoba, 2017
|
TANGAZO LA KUITWA KAZINI
OR
TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali za kada za
Afya walioomba kazi kuanzia tarehe 25/07/2017
hadi tarehe 30/08/2017 kuwa mchakato
wa kuwapangia vituo vya kazi umekamilika.
Aidha,
mnatakiwa kuripoti katika vituo vya kazi mlivyopangiwa katika muda wa siku kumi
na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili mkiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo
kuanzia kidato cha nne na kuendelea kwa ajili ya kuhakikiwa na mwajiri kabla ya
kupewa barua ya ajira.
Orodha
ya majina ya waliopangiwa vituo vya kazi inapatikana kupitia tovuti ya OR
TAMISEMI www.tamisemi.go.tz.
Hakutakuwa
na mabadiliko ya vituo, watakaoshindwa kuripoti katika muda uliopangwa, nafasi
zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika.
Kwa
wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakupata nafasi hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi
zitakapotangazwa. Nafasi za Wauguzi na Wahudumu wa Afya zitatangazwa mara baada
ya kukamilisha zoezi la uchambuzi na uhakiki wa vyeti.
Waajiri
wote mnaelekezwa kuwapokea, kuhakiki vyeti na kuwafanyia mafunzo elekezi
(Induction Course) kabla ya kuwapangia vituo vya kazi.
Limetolewa na:-
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
OR – TAMISEMI
30/10/2017
KUYAONA MAJINA HAYO
>>>BONYEZA HAPA--PDF<<<
0 comments:
Post a Comment