Na Exaud Msaka Habari
Baraza la vijana la chama
cha Demkocrasia na maendeleo chadema
BAVICHA wametoa siku tatu kwa jeshi la polisi nchini kumwachia Mwenyekiti wa
baraza hilo PATROBAS KATAMBI aliyekamatwa jana mkaoni mwanza pamoja na
kuwakamata wahusika wote waliohusika na kifo cha Mwenyekiti cha CHADEMA mkoani
GEITA Bwana ALPHONCE MAWAZO huku wakisema kuwa kama hayo hayatafanyika
watalazimika kulipa kisasi.
Akizungumjza na
wanahabari mchana wa leo jijini Dar es salaam katibu wa uenezi wa baraza hilo
Taifa Bwana EDWARD SIMBEYE amesema kuwa kwa sasa vijana na wanachama wa chadema
wamechoka na mauaji ya viongozi wa chama
hicho huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wahusika hivyo sasa wameamua
kuhakikisha kuwa wanajilinda wenyewe ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wahusika wa
tukio la Geita na kuwakamata kama polisi watakuwa wameshindwa kufanya hivyo kwa
muda muafaka..
Akizungumzia tukio la
jana mkoani mwanza amesema kuwa wakati jana mwili wa marehemu MAWAZO ukiwasili
katika hospitali ya BUGANDO kwa ajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa uchunguzi
zaidi Polisi walipanga njama za kuutorosha mwili wa marehemu kwa ajili ya
kwenda kuuzika kimya kimya jambo ambalo amesema wanachama na viongozi wa
CHADEMA walishtuka na kuamua kulinda mwili huo na ndipo ilipotokea vurugu
iliyopelekea kiongozi wa vijana taifa kukamatwa na polisi bila sababu yoyote ya
msingi.
Amesema kuwa
inashangaza kuona jeshi la polisi likiwa
katika mstari wambele kuhangaika juu ya mwili wa Marehemu ALPHONCE MAWAZO
wakati iko wazi kuwa wakati anauawa na wananchi polisi walikuwepo eneo la tukio
na kushindwa kutoa hata msaada wa gari kwa ajili ya kumpeleka hospitalini
lakini jana polisi walipata gari la kuja kumtorosha katika hospitali hiyo jambo
ambalo amesema limekuwa likifanywa na polisi kila mara yanapotokea matukio ya
mauaji kana haya.
Kiongozi huyo amesema
ni lazima jeshi la polisi sasa waeleze ukweli kama sio wao na serikali ya CCM
wanaohusika na mauaji ya viongozi wa chadema Basi waweke wazi ni nani hasa
anayefanya unyama huo juu ya Democrasia ya Tanzania.
Aidha katika hatua
nyingine vijana hao wametangaza rasmi kuwa baada ya siku tatu na polisi
kushindwa kuwaachia huru viongozi wao na kuwakamata wauaji wa MAWAZO
wamewaagiza vijana wote wa Tanzania kukusanyika kwa wingi mkaoni mwanza kwa
ajili ya kushinikiza kuwaachia viongozi wao pamoja na kulinda mwili wa marehemu
ALPHONCE MAWAZO ambao umelazwa katika hospitali ya Bugando mkoani mwanza.
Marehemu ALPHONCE
MAWAZO aliuawa na wananchi mkoani GEITA baada ya kushambuliwa na wananchi
waliokuwa na sialaha za jadi ambao hadi sasa hakuna taarifa rasmi inayoeleza
hali halisi ya mauaji hayo.
0 comments:
Post a Comment