Mkali wa R&B Bongo, Ben Pol.
KACHAA mkali wa R&B Bongo, Ben Pol muda wowote kuanzia sasa anatarajia kuelekea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ kwenda ku-shoot video zake mbili mpya.Ben ameliambia Championi Jumatano kuwa akiwa ‘bondeni’ atatengeneza video mbili za nyimbo zake hizo mpya.
Moja inaitwa Ningefanyaje, aliyoimba na mwanadada mrembo wa Kenya, Avril na nyingine amempa shavu msanii mahiri wa Kenya, Nameless.Aidha, ameongeza kuwa Kampuni ya Gorilla Films chini ya Director, Justin Campos, aliyetengeneza video kali ya Nusu Nusu ya Joh Makini ndiye atakayefanya naye kazi hiyo kwa muda wa wiki moja na nusu.
“Muda wowote tangu sasa nitaenda Sauz ku-shoot video zangu mbili na kampuni ya Gorilla Films, kila kitu kimekaa sawa na tutatumia muda kama wa wiki na nusu hivi kukamilisha kila kitu. Nameless nishaongea naye na nitakutana naye hukohuko kumaliza kazi,” alisema Ben Pol.
0 comments:
Post a Comment