Saturday 27 November 2021

Theatre Nurse at Maternity Africa

Theatre Nurse    Maternity Africa (MA) is a local non- governmental organization in Tanzania, devoted to making child birth safe through maternity services and treatment of obstetric fistulae and other birth related injuries. We serve the poorest, most vulnerable rural communities by providing free, quality reproductive health care. All programmes have been developed to have […]

This post Theatre Nurse at Maternity Africa has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Senior Electrician at Kilombero Valley Teak Company

Senior Electrician   Introduction The Kilombero Valley Teak Company Ltd. (KVTC) is a forestry company located in the Kilombero and Ulanga Districts of the Morogoro Region. The Company manages teak plantations and natural woodlands and processes timber in a factory located at Mavimba in the Ulanga District. KVTC Currently has one (1) vacancy for a […]

This post Senior Electrician at Kilombero Valley Teak Company has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Tanzia : MMILIKI WA ZAHANATI YA MITI MIREFU MJINI SHINYANGA Dkt. SAHARI AFARIKI DUNIA

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 27,2021


Magazetini leo Jumamosi November 27,2021







Share:

VIONGOZI WA TAKUKURU MIKOA 28 WAKUTANA KUTATHMINI UTENDAJI KAZI ...TAKUKURU YAAGIZWA KUWEKA MASANDUKU YA MAONI KUHUSU VIASHIRIA VYA RUSHWA OFISI ZOTE

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa 
akiongea wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyia Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Salum Hamduni akiongea na viongozi mbalimbali wa Taasisi hiyo kwenye mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyia Jijini Dodoma.
Viongozi wa TAKUKURU kutoka mikoa 28 nchini wakiwemo Wakuu wa vitengo na wakurugenzi wasaidizi wa Taasisi hiyo wakiwa kwenye mkutano

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog -Dodoma.

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo kwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa nchini(TAKUKURU) kuhakikisha inaweka masanduku ya maoni kuhusu viashiria vya rushwa katika taasisi zote za serikali pamoja na wizara ili kuweza kupokea maoni ya wananchi juu ya viashiria vya rushwa katika taasisi hizo.

Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hay o Novemba 25,2021 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU ambao unatoa fursa kwa viongozi wa TAKUKURU kutathimni utendaji wa kazi wa mwaka mzima uliopita kwa mujibu wa sharia ya kuzuia na kupambana na rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Waziri Mchengerwa amesema viongozi walio wengi hawatambui kuwa nchi ni ya wananchi hivyo TAKUKURU ina nguvu kubwa katika kupambana na viongozi wasio waaminifu.

"Ndugu zangu maono na fikra zenu zifanye kazi kwa kugusa mioyo ya wananchi wa kawaida katika kupigania vita dhidi ya maadui wa haki, maadui wa haki ambao wamegawanyika katika sehemu kuu tatu, Ujinga, Maradhi na Umasikini,"amesisitiza.

Vilevile ,Mchengerwa amewaagiza viongozi hao kufatilia vyema utekelezaji wa miradi yote ya kimaendeleo inayoendelea hapa nchini na wahakikishe kuwa kusiwepo na mianya ya rushwa.

“Utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo umegubikwa na udanganyifu ninyi kama TAKUKURU kiongozi wa kila wilaya apimwe namna anavyoweza kusimamia matumizi ya fedha katika kila Wilaya na niseme tu kwamba hili ni jukumu letu sote katika kusimamia,

“Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan alivyofungua hizi fursa za uchumi hakumaanisha watu watumie fedha hizo vibaya na kutumia nyaraka za uongo kuhusu gharama zinazotumika katika miradi hiyo tumieni mkutano huu kujadili malengo na muhakikishe kusiwepo na mianya ya uchepushaji wa fedha hizo kwaajili ya matumizi binafsi katika kila mradi”,amesema Mchengerwa.


Mbali na hayo ametumia nafasi hiyo kumtaka Mtendaji mkuu wa TAKUKURU nchini Salumu Hamduni,kuhakikisha anatumia nafasi yake kuudhihirishia ulimwengu na watanzania wote kuwa anastahili majukumu haya kwa kufanya kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa pasipo kumuonea wala kumpendelea mtu yeyote, kuboresha taswira na kuimarisha mifumo ya utendaji kazi za taasisi huku ukilinda maslahi ya Taifa.

" Mheshima Rais anaamini kuwa kwa umoja wenu na kwa ushirikiano na viongozi pamoja na watumishi wengine wa TAKUKURU mtaisaidia Serikali anayoiongoza kuijenga Tanzania ambayo wananchi wake watanufaika na rasilimali za umma na kupata huduma bora pasipo kuombwa au kutoa rushwa,


Tumieni nafasi hii kujenga nguzo kuu za serikali za kuinua na kukweza ufanisi wa uwajibikaji uwe na watumishi wa umma wenye miiko ya maadili kwa ustawi na maendeleo ya jamii na Taifa, taasisi hii ni nanga ya Taifa letu kwa usalama wa tija ya kutoa wajibu wa uwazi na ukweli wa kuchangia utawala bora, mkizembea tunaanguka wote na mkiwa imara na kutimiza wajibu wenu ipasavyo, tunainuka wote,"amesema Mchengerwa.

Pamoja na hayo amewataka watumishi wa Taasisi hiyo kuacha woga na kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii hivyo matendo yao yanapaswa kuwa safi .

“Wito wangu kwenu ni kwamba tathmini yetu iwe ya kina na tutazame namna tutakavyoweza kujipambanua katika kila Wilaya namna bora ya utendaji”, amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Salumu Hamduni,amesema wametekeleza majukumu na kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 jumla ya shilingi billion 29.3 ziliokolewa na kwamba billion 11 .2 ziliokolewa kwa mfumo wa fedha taslim na utaifishaji mali na kiasi cha bilioni 18 zilidhibitiwa kabla hazijatumika.

Ameeleza miradi ya kimaendeleo 1,188 yenye thamani ya bilioni 714.17 katika sekta ya afya maji elimu ziliweza kufatiliwa na kuona makosa ambayo wameyachukulia hatua.

“Tumeelimisha katika ngazi ya Makao Makuu pamoja na wakuu wa TAKUKURU, kuzuia vitendo vya rushwa kuelimisha, kushirikisha jamii pamoja na kuwafikisha watuhumiwa Mahakami kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya mashtaka ambapo majalada 1,053 yalichunguzwa na kukamilishwa na majadala 339 yaliwasilishwa kwa Mkurugenzi wa mashitaka kuomba kibali cha kuwafikisha mahakani ambapo kesi mpya zilipatikana 542, na kesi 541 zilitolewa uamuzi ambapo Jamhuri iliweza kushinda kesi 345”,amesema Hamduni

Kutokana na hali hiyo amesema wao wakiwa na dhamana ya kupinga masuala ya rushwa nchini wataendeleza juhudi kuelimisha umma kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na kuzuia mianya ya rushwa.

"Tunatambua wapo wananchi ambao hawajafikiwa,tunaendeleza jitihada za kuwafikia wananchi na hasa waliopo vijijini n kuendelea kutoa kipaumbele zaidi katika kuzuia vitendo vya Rushwa ikiwemo kuwaelimisha wananchi ili wafahamu haki zao katika upatikanaji wa huduma, madhara ya rushwa na jinsi ya kutoa taarifa za rushwa,"amefafanua Hamduni.

Mbali na hayo ameeleza kuwa Taasisi hiyo ina wajibu sahihi usiopoka haki za wasio na kasoro za kupata haki za Uhuru wa dhamana na kwamba hakimu haki ndiye atajenga sifa nzuri za kuthaminika nyinyi ni taasisi ya utalawa Bora kwa Serikali ya awamu ya sita.

" Ni imani yetu kuwa wananchi wakiwa na ufahamu wa kutosha kuhusu Rushwa na madhara yake basi itawarahisishia kukabliana nayo kwakuwa hawatatoa wala hawata sita kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa,elimu hiyo itawafunua zaidi macho wananchi, kutambua vitendo vya rushwa vinavyoweza kutokea katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutoa taarifa kwenu na kwa mamlaka nyingine zinazohusika,"ameeleza Mtendaji huyo Mkuu wa TAKUKURU nchini.
Share:

Friday 26 November 2021

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MASOMO YA ZIADA KWA WANAFUNZI KIPINDI CHA LIKIZO 'WAPUMZIKE, TUNAWAHARIBU KUSOMA MUDA WOTE'

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Ummy Mwalimu amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote nchini kuhakikisha wanasimamia suala la wanafunzi kupumzika wakati wa likizo ili kuwapatia watoto muda wa kujifunza masuala mengine ya kijamii.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo baada ya kupata maelekezo ya kisera kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknojia, Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako ambaye amemtaka kulisisitiza suala hilo ili wanafunzi hao waweze kupata muda wa kupumzika kipindi cha likizo.


Akihutubia kwenye Mahafali ya 29 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo,Waziri Ummy amesema watoto wanatakiwa kupumzika majumbani kipindi cha likizo ili waweze kusaidia kufanya kazi ndogondogo nyumbani, kusoma dini na kusaidia kufanya biashara ndogo za kuwasaidia wazazi pale wanapokuwa likizo.


“Sasa hivi elimu imegeuzwa kama biashara, watoto wamekuwa wakisoma masomo ya ziada mpaka kipindi cha likizo, hawapumziki, pia wazazi huchangia fedha kwa ajili ya masomo hayo ya ziada, watoto hawafaulu kwa kusoma muda mrefu, hivyo nawaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanalisimamia hili,” amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema, Serikali imepanga muda wa vipindi wa saa nane, ikiamini muda huo wanafunzi wataweza kujifunza kwa kina masomo yote yaliyopangwa kwa siku, hivyo amewataka Wakurugenzi kuwaelekeza wakuu wa shule kusitisha masomo ya ziada mpaka saa mbili usiku Jumatatu hadi Jumapili.

"Ninaagiza kusitishwa mara moja kwa kuwa hatuwajengi watoto,tunawaharibu kwa kuwachosha kusoma muda wote bila kupata muda wa kupumzika,"amesema Waziri.

Chanzo - Dira Makini Blog
Share:

SERIKALI YASITISHA UHAMISHO KWA WATUMISHI 'KIPAUMBELE KWA WALIO TAYARI KUFANYA KAZI VIJIJINI'

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog Dodoma.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amesema kwa sasa amesitisha masuala ya uhamisho kwa Watumishi wa umma wanaotaka kuhamia kwenye Majiji na kukataa kuishi vijijini na badala yake ataendelea kutoa nafasi za kubadilishana vituo vya kazi pale inapobidi.

Hayo yamejiri hivi karibuni Jijini Dodoma wakati wa mahafali ya 13 ya Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) huku Waziri huyo akisisitiza kuwa hali hiyo itatoa nafasi kwa wananchi wa pembezoni kupata huduma wanazostahili ikiwemo elimu na afya .

Amesema,sehemu za vijijini kuna uhaba mkubwa wa watumishi wa kada mbalimbali kutokana na watumishi wengi kukimbilia kufanya kazi Mjini na kwamba ili kumaliza tatizo hilo lazima wahitimu wote wawe tayari kuajiriwa na kupelekwa sehemu yoyote yenye uhitaji.

"Nimesitisha na nitaendelea hivyo mpaka tutakapofanya msawazo wa watumishi lazima ningalie kwa nini Ukerewe kuna walimu 100 wakati Kinondoni kuna walimu 2,000 tutaangalia mahitaji na waliopo ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuhamisha,"amesema.

Aidha ameeleza kuwa ili kuwapa hadhi wanayostahili watumishi,Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya Vijijini ikiwemo kuanzisha Shule zenye mchepuo wa Kiingereza ili Watumishi wanaohitaji watoto wao kusoma shule hizo wapate fursa hiyo hali itakayo saidia kuacha kutamani kuishi Mjini.

Ametilia mkazo kuwa ili kukidhi mahitaji ya ajira nchini,Serikali itatoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu walio tayari kufanya vijijini huku akiwataka wanachuo wa chuo hicho (LGTI)wanaomaliza muda wao kujiandaa kisaikolojia kuishi maeneo yoyote watakapo pangiwa ili kuisaidia jamii.

"Mnapopata ajira muwe tayari kwenda kufanya kazi kwenye halmashauri za pembezoni (vijijini) na sio mkishapata tu mnaanza kuomba uhamisho kurudi Mjini,lazima mjifunze maisha ni popote mnapaswa kuridhika"amesisitiza

Aidha amesema Mamlaka ya Serikali za Mitaa itaendelea kuajiri wataalam wanaohitimu LGTI kwa kuwa wamepikwa kutumika vyema kwenye Serikali za Mitaa.

'Lazima tuwe wakweli,kwa sasa Serikali itatoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu walio tayari kufanya kazi Halmashauri za Vijijini ambapo kuna mahitaji makubwa ya Watumishi wa kada mbalimbali na si vinginevyo,"amesema Waziri Ummy na kuongeza;

“Watu wa kijijini pia wanahitaji huduma zenu, hivyo watumishi wanahitajika kwenda kufanya kazi maeneo hayo na sio kunga’ang’ania kubakia mjini wakati wote, kila mtu anataka Dodoma Jiji, Kinondoni, Arusha Jiji, Mwanza Jiji nani akae Mpimbwe, Uvinza, Kilindi, Rufiji,” amehoji Waziri huyo.

Wakati huo huo amesema Serikali itaendelea kuboresha na kutatua changamoto zilizopo Chuoni hapo ili kuboresha huduma za kijamii na kuongeza umakini wa masomo kwa wanachuo hao.

Amesema katika bajeti ya 2022/2023 watatenga fedha kea ajili ya Ujenzi wa bweni moja lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 ili wanafunzi wakae kwenye mazingira ya Chuo ambayo ni salama.

Aidha alisema atapigania ujenzi wa barabara ya lami kutoka Ihumwa hadi Hombolo kurahisisha hali ya usafiri na kukuza uchumi .

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Profesa Joseph Kuzilwa ameiomba Serikali kuwezesha ujenzi wa barabara ya Ihumwa - Hombolo kwa kiwango cha lami ili kuweza kufika kiurahisi chuoni hapo tofauti na sasa ambavyo miundombinu hairidhishi.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Dk. Mpamile Madale amesema chuo hicho kinakua siku hadi siku na kuongeza udahili na wanafunzi waliohitimu mwaka 2021 ni 6,021.

Share:

WADAU WA SEKTA YA KILIMO DUNIANI WAWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI KUFUATILIA SHUGHULI ZINAZOTOLEWA NA WADAU

 Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

WADAU wa Sekta ya Kilimo duniani wamewataka Viongozi wa Serikali kufuatilia shughuli mbalimbali wanazozitoa  ikiwemo mafunzo , mikopo inayotolewa kwaajili ya Wakulima ili kutekeleza azimio la Malabo la wakulima katika  kilimo chenye tija na manufaa kwa Taifa.

Haya yamebainishwa  Wakati wa Kongamano la Malabo Policy Learning Event (MAPLE) lilifanyika kwa njia ya Mtandao ( Video Conference) lililofuatiliwa moja kwa moja na wadau mbalimbali kutoka bara la Afrika , wakulima wadogo kutoka wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma katika  hafla iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Action   Aid Tanzania.


Wadau hao wamesema bado kuna changamoto katika utekelezaji wa tamko la Malabo kwa kuwa baadhi ya Viongozi kutokuwa wafuatiliaji wa shughuli zinazotolewa kwa ajili ya wakulima pamoja na mapitio ya Sekta ambayo hayajafanyika kwa kipindi cha miaka minne.


Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Mkurugenzi wa Kilimo na Maendeleo Vijijini, Dk Godfrey Bahiigwa, amesema licha ya miaka sita ya utekelezaji wa Azimio la Malabo, kuna nchi chache tu ambazo zimehimiliki tangu kupitishwa.


Kwa Upande wake Mkuu wa Kilimo na Mazingira kutoka Shirika la Maendeleo la AU, Mamadou Diakhite, amesema nchi nyingi za Afrika bado zinapambana na marekebisho ya sera huku ulimwengu ukiendelea kupambana na janga la Covid-19.


Hata hivyo, amezitaka nchi zote wanachama wa AU kuzingatia tamko la Malabo kama ajenda ya kimataifa ikiwa kumaliza umaskini ni jambo la kutatanisha.


Akizungumza kwa niaba ya sekta binafsi,  Nana Honey  amesema  ilikuwa injini kuu katika shughuli za Kilimo na uwekezaji kuna uhitaji wa  wanasayansi zaidi ambao wanaweza kufanya tafiti zenye manufaa.


Aliendelea  kwa kusema ipo  haja ya kuwa na rasilimali fedha utosha, uwekezaji katika sekta binafsi yenye uthabiti pamoja na mifumo mizuri ya kutambua mifumo ya lishe bora.


Tamko hilo   lilipitishwa mwaka 2014 lakini utekelezaji wake rasmi ulianza mwaka 2015, Azimio la Malabo lililotiwa saini na Serikali za Afrika mwaka 2014 liliwakilisha kujitolea tena kwa kanuni na malengo ya Mpango Kamili wa Maendeleo ya Kilimo Afrika (CAADP) iliyopitishwa mapema mwaka 2003 chini ya Azimio la Maputo.


Mwaka 2003, viongozi wa nchi za umoja wa Afrika [ AU] walikubaliana katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, kutenga kima cha chini cha asilimia 10 ya bajeti yao yote ya kitaifa kwa sekta ya kilimo ili kuhakikisha usalama wa chakula na kukabiliana na umaskini wa vijijini ifikapo mwaka 2015, Wakati wa Mkutano wa Maputo, huko nyuma. , Tanzania iliwakilishwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.


Mpango uliobatizwa jina la CAADP ulibuniwa na ulilenga kuhakikisha kuwa sekta hiyo inakua kwa kiasi kikubwa.


CAADP ni mfumo wa sera ya Afrika kwa ajili ya mabadiliko ya kilimo, uzalishaji mali, usalama wa chakula na lishe, ukuaji wa uchumi na ustawi kwa wote. Katika Mkutano wa AU wa Maputo, viongozi walitoa tamko la kwanza kuhusu CAADP kama sehemu muhimu ya Ushirikiano Mpya wa Maendeleo ya Afrika (NEPAD).


Baadaye mwaka 2014, tamko la Malabo lilikwenda mbali zaidi kwa kubainisha malengo na shabaha mahususi zinazopaswa kufikiwa ndani ya kipindi cha miaka kumi. Malengo hayo ni pamoja na kumaliza njaa, kuongezeka mara tatu kwa biashara ya bidhaa na huduma za kilimo baina ya nchi za Afrika, kuimarisha ustahimilivu wa maisha na mifumo ya uzalishaji, na kuhakikisha kuwa kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza umaskini.

Share:

WAZIRI WA KILIMO PROFESA ADOLF MKENDA ATEMBELEA SHAMBA LA MICHIKICHI NCHINI UGANDA




Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda alipotembelea kitalu cha kuoteshea miche ya michikichi katika shamba la Oil Palm Uganda Limited, katika ziara ya kikazi nchini Uganda. Kushoto ni Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu

Baadhi ya wafanyakazi wakipanda miche kwenye shamba la michikichi katika shamba la Oil Palm Uganda Limited nchini Uganda ambako Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda alitembelea jana.
Miche iliyooteshwa katika shamba la Oil Palm Uganda Limited nchini Uganda.
Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda akiangalia mbegu za mchikichi alipotembelea kitalu cha kuoteshea miche ya michikichi katika shamba la Oil Palm Uganda Limited, katika ziara ya kikazi nchini Uganda. Kushoto ni Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa Chimagu.

..................................................

Na Mwandishi Wetu, KAMPALA 

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, amezuru kikazi Uganda na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Viwanda na Uvuvi, Frank Tumwebaze pamoja na timu ya wataalamu kutoka Tanzania na Uganda.

 Katika ziara hiyo, Waziri Mkenda ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye na wataalamu wa kilimo kutoka Wizara ya Kilimo na Mkoa wa Kigoma. 

Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa ya kimkakati katika uzalishaji wa zao la michikichi nchini.

 Ziara hiyo imelenga kuimarisha uhusiano wa Uganda na Tanzania katika sekta ya kilimo ili kukuza tija ya uzalishaji wa mazao kwa kutumia mbinu bora za kilimo, ikiwa ni pamoja na kuimarisha utafiti wa kilimo na upatikanaji wa mbegu bora. Katika mazungumzo yao hayo jana Waziri Mkenda alieleza jitihada zinazofanywa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan za kukuza uchumi kwa kuimarisha uhusiano chanya na nchi jirani kama Uganda.

 “Tumekuja Uganda kwa kuwa tunafahamu sisi ni ndugu na uhusiano wetu una historia ndefu. Marais wetu wote wawili, Rais Yoweli Museven na Rais Samia Suluhu Hassan wanafanya kazi nzuri ya kuimarisha uhusiano uliopo na kukuza uchumi wa nchi zote mbili," alisema.

 Waziri Mkenda alisisitizia Wizara ya Kilimo ipo katika mkakati kabambe wa kuhakikisha nchi inaondokana na dosari ya uhaba wa mafuta ya kula na kutumia fursa ya ziara hiyo kujifunza namna ambavyo Uganda imepiga hatua kubwa ya kilimo cha michikichi.

 Alisema hatua hiyo itaongeza hamasa kwa uwekezaji mkubwa wa kilimo hicho nchini na kulimwa kwa tija na kupunguza uhaba wa mafuta ya kula kwa kiwango kikubwa na kushusha bei kwa mtumiaji. 

“Katika ziara hii nimeongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kwa kuwa Kigoma ni mkoa mmojawapo wa kimkakati kwa kilimo cha michikichi.

 "Kuja kwake huku kutawezesha kujionea na kujifunza ili kwenda kuwahamasisha wakulima wetu kulima kwa tija," Prof. Mkenda alisema. Ziara hiyo pia ilihusisha kutembelea mashamba makubwa ya mchikichi, viwanda vya uchakataji wa mafuta ya mawese na kujifunza mfumo mzima wa ulimaji na utunzaji wa michikichi na hadi kupata mafuta ya mawese.

 Kampuni ya Wilmer yenye matawi katika nchi zaidi ya 25, ina nia ya kuongeza uzalishaji Tanzania katika kuzalisha mafuta yatokanayo na michikichi, alizeti na mazao mengine.

 Kampuni hiyo imejenga kiwanda cha mchele mjini Morogoro chenye uwezo wa kukoboa mpunga tani 200 kwa siku, kilichofunguliwa rasmi na aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk. John Pombe Magufuli mapema mwaka huu.

 Waziri wa kilimo, Mifugo, Viwanda na Uvuvi wa Uganda, Tumwebaze, alimshukuru Waziri Mkenda na timu yake kwa kuamua kutembelea Uganda na kuonyesha undugu na urafiki wa nchi hizo mbili. 

Aliongeza kuwa Uganda iko tayari kuendelea kuimarisha uhusiano na Tanzania katika sekta ya kilimo na kutaka wataalamu wa kilimo wa nchi zote mbili kuharakisha uundwaji kamati ya pamoja ya kilimo ili kutekeleza makubaliano ya ushirikiano wa pamoja katika kilimo yaliyotiwa saini Septemba 6, 2019 jijini Dar es Salaam.

 “Tumekubaliana nchi zetu kushirikiana katika mambo mbalimbali kwenye sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa mbegu bora, masoko, utafiti na mengineyo. 

"Tumefurahi sana kwa ujio huu wa Waziri wa Kilimo wa Tanzania kwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano hayo," alisema Waziri Tumwebaze.

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wilmar anayesimamia Afrika, Santhosh Pilai, alisema kampuni hiyo iko tayari kuongeza uwekezaji mkubwa zaidi Tanzania ili kumhakikishia mkulima soko pamoja na kuondoa vikwazo vya uhaba wa mafuta ya kula Tanzania.

 “Tumefanya uwekezaji katika nchi zaidi ya 20 Afrika, Asia na Marekani na kwa Tanzania tuwekeza kiwanda kikubwa pale Morogoro na tunataka kuwekeza zaidi Tanzania. Zaidi ya vijana 400 wameajiriwa katika uwekezaji huo," alisema Pilai
Share:

ZALISHENI NYAVU KWA KUZINGATIA UBORA -NAIBU WAZIRI ULEGA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ofisini kwake ambapo amemueleza mipango waliyonayo ya kuhakikisha wanaongeza uzalishaji wa samaki kupitia ufugaji kwa kutumia vizimba. Mhe. Ulega alifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku mbili. 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (Mb) akisikiliza maelezo ya namna nyavu za kuvulia dagaa zinavyotengenezwa wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza nyavu cha Ziwa Net kilichopo katika Kijiji cha Kanyama wilayani Magu mkoa wa Mwanza. 


Picha ya pamoja ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega na Viongozi na watumishi wa kiwanda cha Ziwa Net kilichopo katika Kijiji cha Kanyama wilayani Magu mkoa wa Mwanza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho. 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akikagua ujenzi wa mwalo wa Ihale wilayani Busega mkoa wa Simiyu ambapo amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo kwa wakati. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Gabriel Zacharia na Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe. Simon Songe. 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wananchi wa Kijiji cha Ihale wilayani Busega mkoa wa Simiyu mara baada ya kukagua mwalo wa Ihale ambapo amewataka wananchi kushirikiana na serikali katika kulinda rasilimali za uvuvi. 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akikagua miundombinu iliyopo katika Kituo cha kupumzishia Mifugo cha Lamadi wilayani Busega mkoa wa Simiyu ambapo amewaagiza Viongozi kuendelea kulilinda eneo hilo na kwamba uangaliwe uwezekano wa kukiboresha Kituo hicho ili kiweze kufanya kazi kama zamani. 


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiangalia mabondo wakati alipotembelea kiwanda cha kuchakata mabondo cha Pesca Perch kilichopo wilayani Magu mkoa wa Mwanza. 

...................................................

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekitaka kiwanda cha kuzalisha nyavu za kuvulia dagaa cha Ziwa Net kuzalisha nyavu hizo kwa kuzingatia ubora. 

Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuona namna uzalishaji wa nyavu hizo unavyokwenda ambapo uongozi wa kiwanda hicho umetakiwa kuzingatia ubora katika uzalishaji wa nyavu lakini pia kuhakikisha wanazalisha nyavu za kutosha ili wavuvi wasipate shida kuzitafuta. 

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ulega amempongeza mwekezaji huyo wa Kiwanda cha Ziwa Net kwa uamuzi wake wa kujenga kiwanda hicho lakini pia kwa kutoa ajira nyingi kwa wanawake ambapo kati ya waajiriwa 18 wanaweke ni 15. Vilevile amewasihi kuhakikisha wanazingatia misingi ya ajira na kuhakikisha hakuna unyanyasaji wa watumishi. Lakini pia amewashauri kuendelea kuwekeza katika utengenezaji wa nyavu za aina nyingine zikiwemo za kuvulia samaki pamoja na nyavu maalum za kutengenezea vizimba vya samaki. 

Vilevile amewasihi uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanajitangaza lakini pia kuwaalika wadau kuja kuona namna nyavu zinavyozalishwa ili pia waweze kutoa maoni yao kuhusu nyavu hizo. 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Salum Kali amesema uwepo wa kiwanda hicho ni muhimu sana kwa wavuvi kwa kuwa itawarahisishia upatikanaji wa nyavu kwa bei nafuu. Lakini pia itapunguza uvuvi haramu kwa kuwa wavuvi watakuwa wakitumia nyavu sahihi. 

Meneja Masoko wa kiwanda cha Ziwa Net, Bi. Christina Melkior amesema lengo la kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kurahisisha upatikanaji wa nyavu za dagaa kwa wavuvi, kukuza na kutangaza zana bora za uvuvi pamoja na kufungua fursa ya ajira kwa vijana watakao ajiriwa katika kiwanda hicho. Pia amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha vipande 66 vyenye urefu wa mita 75 na upana wa mita 3.2 kwa siku ambapo uzalishaji kwa mwezi ni vipande 2000. 

Naibu Waziri Ulega pia ametembelea mwalo wa Ihale kukagua maendeleo ya ujenzi wa mwalo huo na kuzungumza na wavuvi, Kituo cha kupumzisha Mifugo cha Lamadi wilayani Busega mkoa wa Simiyu na kiwanda cha kuchakata mabondo cha Pesca Perch wilayani Magu mkoa wa Mwanza.
Share:

SERIKALI YAIAGIZA TAKUKURU KUWEKA MASANDUKU YA MAONI TAASISI ZOTE ZA SERIKALI

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo kwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa nchini[TAKUKURU]kuhakikisha inaweka masanduku ya maoni kuhusu viashiria vya rushwa katika taasisi zote za serikali pamoja na wizara ili kuweza kupokea maoni ya wananchi juu ya viashiria vya rushwa katika taasisi hizo.

Mhe. Mchengerwa ametoa maagizo hayo Novemba 25,2021 jijini Dodoma katika mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU ambao unatoa fursa kwa viongozi wa TAKUKURU kutathimni utendaji wa kazi wa mwaka mzima uliopita kwa mujibu wa sharia ya kuzuia na kupambana na rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.

Waziri Mchengerwa amesema viongozi walio wengi hawatambui kuwa nchi ni ya wananchi hivyo TAKUKURU ina nguvu kubwa katika kupambana na viongozi wasio waaminifu.

Hivyo,Waziri Mchengerwa ameiagiza TAKUKURU kuandaa masanduku katika taasisi zote ili kubaini wapokeaji rushwa katika taasisi hizo huku akibainisha kuwa katika mwaka huu ,serikali imetoa kibali cha ajira mpya 350 kwa TAKUKURU.


Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini [TAKUKURU]Kamishna wa polisi , SALUM RASHID HAMDUNI amesema hadi sasa TAKUKURU imeshashinda kesi za rushwa 345 na kushindwa kesi 156 huku ikiokoa Tsh.bilioni 29.3 .

Ikumbukwe kuwa ,mwaka 1971 ilitungwa sheria ya kuzuia Rushwa Na.16 ili kukabili tatizo la rushwa nchini ,baada ya miaka mitatu ,Januari 15,1975 serikali ilianzisha kikosi cha cha kuzuia rushwa chenye dhamana ya kutekeleza sharia Na.16/1971 na kilikuwa chini ya jeshi la polisi na mwaka 1991 sheria ya kuzuia Rushwa Na.16/1971 iliboreshwa ili iendane na wakati na ikaitwa Taasisi ya Kuzuia Rushwa [TAKURU] na wengi walizoea kama PCB ,na ilipofika mwaka 2007 ilibadilishwa kuwa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU].

Hivyo mabadiliko haya yaliendana na ongezeko la Wigo wa kushughulikia makossa ya rushwa kutoka makosa 4 na kuwa makossa 24 chini ya sharia ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007 inayotumika hadi sasa.
Share:

eGA YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZINAZOANZISHA MIFUMO YA TEHAMA BILA IDHINI YA MAMLAKA HIYO


Meneja wa Huduma za sheria mamlaka ya Serikali Mtandao[eGa] ACP. Raphael Rutahiwa

Na Faustine Gimu Galafoni, Dodoma.
Mamlaka ya Serikali Mtandao [eGa] imezitaka taasisi za umma zinazoanzisha mifumo ya Tehama bila idhini ya mamlaka hiyo kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu zilizoanzishwa na mamlaka hiyo.

Hayo yamesemwa leo Novemba 26,2021 jijini Dodoma na Meneja wa Huduma za sheria mamlaka ya Serikali Mtandao[eGa] ACP. Raphael Rutahiwa wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambapo amesema taasisi zote za Umma zinapotaka kuanzisha mifumo lazima ziwasililiane na Mamlaka hiyo.

“mamlaka inaelekeza taasisi yoyote ya umma isijenge au kuendeleza mradi wa wowote wa TEHAMA bila kupata idhini ya mamlaka,pia inasisitiza kutoa taarifa mara kwa mara kwa mamlaka katika utekelezaji pia sheria inasisitiza kujenga mifumo kwa kutumia wataalam wa ndani”amesema.

Aidha,amesisitiza kutumia wataalam wa ndani katika kuokoa gharama pamoja na kulinda usalama zaidi wa kimfumo.

Pia meneja huyo wa Huduma za sheria eGa ametoa msisitizo kwa taasisi zote za kiserikali kuzingatia sheria Na.10 ya mwaka 2019 ya mamlaka serikali mtandao kuwa na utayari wa kuweka miundombinu ya TEHAMA pindi zinapoanzisha majengo ili kuepusha gharama zinazoweza kujitokeza baadae.

“Sheria inaelekeza kwamba tunapoelekea TEHAMA inaenda kutumika kila sehemu ,hivyo panapokuwa na mpango wa ujenzi wa miundombinu mfano majengo,reli,barabara ,madaraja lazima pawepo utayari wa mifumo ya TEHAMA ,kwa kufanya hivyo tunashirikiana na taasisi husika ,isiwe kesho kutwa ukitaka kujenga mfumo wa TEHAMA ubomoe ukuta ,mfano pale Dar Es Salaam barabara ya Mwendokasi kama unaelekea BRT ile barabara inajengwa kwa zege lakini ikifika muda ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA panakuwa na gharama nyingine “amesema.

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019.

Ni taasisi yenye mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma.

Kuanzishwa kwa Mamlaka hii mwaka 2019 kunaendeleza afua za Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na kuchukua sehemu ya mipango yake kwa sababu majukumu ya taasisi hizi yanafanana ingawa yanatofautiana katika mamlaka ya utendaji.

Mamlaka ya Serikali Mtandao ni taasisi iliyoirithi Wakala ya Serikali Mtandao iliyoundwa Aprili 2012 kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 Sura ya 245 ya mwaka 1997 yenye jukumu na Mamlaka ya Kuratibu, Kusimamia na Kukuza Jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.

Kabla ya kuanzishwa Wakala ya Serikali Mtandao, matumizi ya TEHAMA Serikalini yalikuwa yanaratibiwa na kusimamiwa na Idara ya Usimamizi wa Mifumo (DMIS) iliyopo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambayo kwa sasa ni Idara ya Huduma za TEHAMA Serikalini (DICTS).

Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 imeainisha majukumu na mamlaka yanayoiongoza Mamlaka ya Serikali Mtandao katika utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini Tanzania.
Share:

AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA TISHIO ZAIDI CHARIPOTIWA AFRIKA KUSINI


Wanasayansi nchini Afrika Kusini wameingiwa na wasiwasi wa aina mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa hivi karibuni na kinachotajwa kujibadili kwa kasi kubwa na kuenea kwa haraka miongoni mwa vijana na ripoti zinasema hata chanjo haziwezi kukikabili.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Joe Phaahla amesema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi ndani ya siku tano zilizopita na aina hiyo mpya ya kirusi ndiyo inahofiwa kuchochea kupanda kwa maambukizi, Wanasayansi nchini humo wanajaribu kutathimini ni asilimia ngapi ya maambukizi mapya ambayo yamesababishwa na aina mpya ya kirusi.

“Wakati timu ya wanasayansi wakifanya utafiti na kutupa taarifa zaidi mwishoni mwa juma tutakuwa na uwezo zaidi lakini bila shaka, tunaona kwamba kutokana na uzoefu wa miezi 21 iliyopita au zaidi, tunaweza kutabiri jinsi hali itakavyokuwa, kama nilivyosema, hasa wakati Delta ilivyoanza Gauteng, unaweza kuwa na uhakika kwamba watu watapoanza kutembea katika wiki chache zijazo kirusi kitakuwa kila sehemu”,wamesema

Kirusi hicho aina ya B.1.1.529, pia kimeripotiwa nchini Botswana na Hong Kong miongoni mwa wasafiri waliotoka Afrika Kusini, Wataalamu wa WHO watakutana leo kutathmini kirusi hicho na kuona kama watakipatia jina la kigiriki.
Share:

DED NICE MUNISSY : WAZEE WA KIMILA WASHIRIKWISHE KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy 
***
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy amewataka wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga  kuwatumia wazee wa kimila katika mapambano ya kupinga ukatili kwa halmsahuri ya wilaya ya Shinyanga.

Munissy ametoa rai hiyo Novemba 24, 2021 wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa asasi za kiraia na shirika la Mfuko wa Wanawake Tanzania(WFT) kuhusu tathmini ya utekelezaji wa MTAKUWWA katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Alisitiza kuwa wazee wa kimila katika halmashauri ya Shinyanga wanaheshimika na wana kundi kubwa la watu hivyo ni jambo la muhimu kwa wadau kutambua ushiriki wao katika kutokomeza ukatili kwa mkoa wa Shinyanga.

Alieleza kuwa itakuwa ni kazi rahisi katika utekelezaji wa kutokomeza ukatili iwapo wazee wa kimila watapewa elimu ili watambue mila zipi ni nzuri na mbaya.

 "Tusikubali kuendelea kujielimisha wenyewe kila wakati,semina kama hizi ni muhimu na wazee wa kimla kushirikishwa kila mara kwa ajili ya kuleta mabadiliko", alisema Munissy.

"Historia ya miaka mitatu wa halmashauri ya Shinyanga kuhusu ukatili kwa wanawake na watoto imepungua tofauti na miaka ya nyuma. Changamoto ni uhaba wa watumishi ili kuweza kusaidia kutokomeza ukatili kwa halmashauri yetu",aliongeza.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje alizitaka asasi za kiraia kuweka juhudi za kuwatumia waganga wa kienyeji katika kupinga ukatili kwa kuwa ni kundi linalokusanya watu wengi kwa matibabu ikiwa ni wanawake na watoto.

"Jamii yetu inaamini, kutambua ma kuwapa heshima wazee wa kimila,tusipowapa nafasi kwa kuwapa elimu, juhudi zetu zitachelewa kuwakomboa watoto na wanawake. Halmashauri yetu ipo tayari kuweka bajeti juu ya maeneo yanayohitaji bajeti katika kupinga ukatili kwa halmashauri yake",alisema.

Mkurugezi wa shirika la ICS,Kudely Sokoine alisema masuala ya mila na desturi ni mzizi wa ukatili na jamii ya watu inaheshimu sana wazee wa kimila hivyo ni muhimu kubadili mitizamo na kupata matokeo kwa mikakati kwa kujikita zaidi kwa wazee wa kimila
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Nice Munissy akiwa ukumbini
Afisa kutoka WFT Neema Msangi akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngasa Mboje
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Estomine Henry akielezea namna klabu hiyo inashiriki katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omary akizungumza katika mafunzo hayo.
Mkurugezi wa shirika la ICS,Kudely Sokoine akifuatilia mafunzo ukumbini
Share:

ASKARI MAGEREZA AJILIPUA NDANI YA NYUMBA YAKE



Wakaazi wa Lessos eneo bunge la Kwanza, Kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya waliamkia habari za kusikitisha kumhusu askari jela (magereza) aliyejilipua ndani ya nyumba yake Jumatano, Novemba 24 usiku. 

Elias Kipchumba Too ambaye alikuwa zamuni usiku alitoroka kutoka kituo chake cha kazi akiwa na bunduki aina ya G-3 ambayo alitumia kukatiza maisha yake.

Afisa wa gereza la kati la Kitale Julius Kaliakamur, alithibitisha kutokea kwa kisa hicho na kusema kuwa askari huyo mwenye umri wa miaka 25 hakuacha kijibarua chochote cha kueleza sababu za kujitoa uhai. 

Kwa mujibu wa ripoti ya K24, afisa huyo hakuonesh dalili zozote za kutatizika kimawazo.

 “Elias alikuwa zamu jana usiku. Kisha akatoka kisiri akiwa na bunduki yake, baadaye ikagundulika hakujulikana alipo na tukaingiwa na wasiwasi. Tulikimbia hadi nyumbani kwake eneo la Lessos na tukampata amefariki dunia," Kaliakamur alisema.

 Alifichua kuwa afisa huyo ambaye amekuwa akihudumu kwa miaka mitatu alikuwa ameomba uhamisho suala ambalo Huduma ya Magereza ya Kenya ilikuwa ikishughulikia.

"Uhamisho ni wa kawaida katika utumishi, tulipokea maombi yake ya uhamisho na kupeleka kwa mkuu wa gereza la mkoa ambaye alikuwa akiyashughulikia" aliongeza. 

Alimtaja afisa huyo kuwa mtu mkarimu ambaye alitekeleza majukumu yake mara moja na alisikitishwa mno na hatua yake kujitia kitanzi. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Cherangany Nursing Home ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

 Kwingineko afisa wa GSU Jumanne, Novemba 23 aliuawa kwa kupigwa risasi na mwenzake katika hali isiyoeleweka huko kijiji cha Mitete eneo la Laikipia Magharibi.

 Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Laikipia John Nyoike alisema maafisa hao wawili walikorofishana katika kambi ya GSU eneo hilo kabla ya mmoja wao kutwaa bunduki yake na kumvamia mwenzake. 

Baada ya tukio hilo, afisa huyo aliyekuwa amejihami alikusanya mali yake ikiwemo bunduki aliyotumia katika kumshambulia mwenzake na kisha akaondoka.

 Juhudi za kumkamata afisa huyo ambaye aliingia mafichoni baada ya tukio hilo ziliambulia patupu kwani alikuwa akitoroka huku akiwafyatulia risasi wenzake waliokuwa wakimfukuza.

Kamanda wa polisi alisema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha shambulio hilo huku msako dhidi yake ukianzishwa.

Chanzo - Tuko News
Share:

BINTI AMSHTAKI DAKTARI KWA KUZALIWA


Picha ya Evie Toombess

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Evie Toombess (20) amefungua kesi dhidi ya Daktari aliyemsaidia mama yake kujifungua kwa madai ya kwamba yeye hakustahili kuzaliwa.

Evie alizaliwa na tatizo la 'Spina Bifida' ambalo husababishwa na kutokukua vizuri kwa uti wa mgongo wa mtoto akiwa tumboni, pamoja na kuzaliwa na tatizo hilo Evie ni maarufu katika mchezo wa kuruka na farasi nchini Uingereza.

Evie anasema kama Dkt Phillip Mitchell angemshauri mama yake kutumia virutubisho vya 'Folic Acid' basi mama yake asingebeba ujauzito na yeye asingezaliwa na tatizo la 'Spina Bifida' ambalo humfanya kuvaa mirija masaa 24.
Share:

MSALALA WAZINDUA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA....JAMII YATAKIWA KUEPUKA KUMALIZA KESI KIENYEJI

Wana Mabadiliko wakiwa wamebeba bango linaloonesha mfumo wa maisha ya mwanamke katika familia na jamii wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jamii imetakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi panapotokea matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kutoa ushahidi mahakamani badala ya kumaliza kesi kienyeji ili kuwezesha kufikiwa kwa maamuzi ya kimahakama yanayolenga kukomesha matukio ya ukatili katika jamii.

Hayo yamebainishwa Novemba 25,2021 wakati uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala yaliyofanyika kwenye kata ya Lunguya mkoani Shinyanga yakiongozwa na kauli mbiu ‘Ewe Mwananchi Komesha Ukatili wa Kijinsia Sasa’.


Kupitia uzinduzi huo wa Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na UNFPA wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Msalala wametakiwa kuacha tabia ya kumaliza kesi kifamilia bila kulishirikisha jeshi la polisi hali inayosababisha kuendelea kutokea kwa matukio hayo.


Akitoa taarifa za mwenendo na matukio ya ukatili katika halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, Msaidizi wa Mkuu wa Upelelzi Halmashauri ya Msalala Inspekta Costantine Challe amesema matukio ya ukatili wa kijinsia katika halimashauri hiyo yamepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na takwimu za miaka ya nyuma.


“Tunatoa wito sisi kama jeshi la polisi kuacha kabisa kupeana ng’ombe au kushawishiana katika maeneo ya kaya zenu na kumalizia kesi zenu huko, kesi zote naomba ziende kituo cha polisi lakini pia tunaomba mtoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili hizo kesi ziende mbele kwani jeshi la polisi pamoja na ninyi lengo letu ni moja tu kupambana na ukatili”, amesema Challe.

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi Benedicto Manwali ambaye ni Diwani wa kata ya Lunguya ameitaka jamii kuutambua mchango wa wanawake katika shughuli za maendeleo katika jamii na kwa ngazi ya familia.

“Niwapongeze TGNP kwa kuendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa jamii na ni imani yangu kuwa ukatili huu utatoweka kabisa hapo baadae. Ni vyema tukatambua kuwa familia yenye maendeleo inatakiwa mama awepo kwani ni mchangiaji mzuri wa shughuli za maendeleo”,amesema Manwali.

“Vituo vya taarifa na maarifa kwa kushirikiana na hawa wasaidizi wa kisheria katika kata zetu wanafanya kazi nzuri ya kupinga matukio ya ukatili. Natoa wito kwa wanawake mkifanyiwa matukio ya ukatili msirudi nyuma endeleeni kutoa taarifa za matukio ya ukatili”,amesema Manwali.


Aidha amelipongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na wana jamii kupunguza matukio ya ukatili ikiwemo mauaji ya vikongwe akisema matukio hayo yamepungua ukilinganisha na hapo awali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga John Shija ameomba kuwepo kwa utaratibu maalumu utakaosaidia kupatikana kwa takwimu za matukio ya ukatili serikalini tofauti na hali ilivyo sasa.

“Kwa uzoefu wa shughuli ambazo zinaonekana zinafanyika ukiangalia takwimu hizi zimesambaa, tunaona takwimu za polisi,takwimu za Vituo vya taarifa na maarifa na takwimu za wasaidizi wa kisheria. Ombi langu ni kwamba tuwe na njia moja ya kupata takwimu zilizo sahihi leo hapa tungekuwa na takwimu moja ingetupa dira nzuri hivyo ni vizuri tukatengeneza mlango mmoja ambao utatusaidia kupata takwimu za halmashauri zinazohusu matukio ya ukatili wa kijinsia”,amesema Shija.

Katibu Msaidizi wa kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Mbunge amesema bado jamii haijaona umuhimu wa kusomesha mtoto wa kike ambapo baadhi ya wazazi wanaona watoto wa kike ni kama fursa ya kupata mali ikiwemo ng'ombe na wengine wamekuwa wakithubutu hadi kuwashawishi watoto wao wafeli kwenye mitihani ili waolewe.

Hata hivyo amesema vituo vya taarifa na maarifa vinaendelea kutoa elimu kwa jamii kuona umuhimu wa kupeleka watoto shule na kuelimisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.


ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni rasmi Diwani wa kata ya Lunguya Benedicto Manwali akizungumza Novemba 25,2021 wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala yaliyoandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na UNFPA kwenye kata ya Lunguya mkoani Shinyanga 
Mgeni rasmi Diwani wa kata ya Lunguya Benedicto Manwali akizungumza Novemba 25,2021 wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala yaliyofanyika kwenye kata ya Lunguya mkoani Shinyanga yakiongozwa na kauli mbiu ‘Ewe Mwananchi Komesha Ukatili wa Kijinsia Sasa’.
Mwenyekiti wa Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga John Shija wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Mwenyekiti wa Huduma ya Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga John Shija wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Mkuu wa Upelelezi Halmashauri ya Msalala Yohana Mafie  akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Mkuu wa Upelelezi Halmashauri ya Msalala Yohana Mafie akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Msaidizi wa Mkuu wa Upelelzi Halmashauri ya Msalala Inspekta Costantine Challe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Katibu Msaidizi wa kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Shilela, Joseph Mbunge akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Mwana mabadiliko akiwa amebeba bango lenye ujumbe 'Wanawake turuhusiwe kufuata mahari'  wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wana vituo vya taarifa na maarifa wakiwa wamebeba mabango wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala
 
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala
Mchezo wa  Igizo ukiendelea kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Igizo likiendelea kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala 
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika halmashauri ya Msalala
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger