Saturday 11 July 2020

Maabara Ya Kiwanda Cha Pareto Tanzania Kuchunguzwa-Kusaya

Serikali imetoa maelekezo kwa kiwanda cha Pareto Tanzania kuhakikisha kinaweka mazingira ya uwazi katika kupima kiwango cha sumu kwenye maua ili wakulima wapate bei nzuri ili kulinda maslahi ya wakulima nchini. 

Kauli hii ya serikali Imetolewa leo (11.07.2020 ) wilayani Mufindi na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati alipofanya ziara ya kukagua na kuongea na menejimenti ya kiwanda cha Pareto Tanzania ( Pyrethrum Company of Tanzania-PCT) kilichopo Mufindi mkoani Iringa. 

Kusaya alieleza kuwa serikali inazo taarifa za malalamiko ya wakulima wa zao la pareto kuwa wataalam wanaohusika na kupima viwango vya sumu kwenye maua wanatumia vipimo veye mashaka na kupelekea mkulima kupata bei ndogo za pareto hali inayosababisha wakate tama kuzalisha. 

“ Serikali imekuwa ikipokea malalamiko ya wakulima wake wa pareto kuhusu kiwanda hiki cha PCT kutumia vifaa vya maabara ya kupima viwango vya sumu kwenye maua ,jambo hili halikubaliki  ndio maana nimekuja hapa Mufindi” alisema Katibu Mkuu Kusaya 

Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo alitoa maelekezo sita ambayo kiwanda cha pareto na wadau wengine wanapaswa kuyazingatia ili mkulima apate haki kwa kazi anazozifanya 

Kwanza, ni lazima kiwanda kinapotengeneza kigezo cha kupima kiwango cha sumu kwenye maua kujua bei gani itatozwa yaani  ‘ K-Factor’ ishirikishe  Bodi ya Pareto ,wakulima na mmiliki wa kiwanda ili kuwe na uwazi na kulinda maslahi ya mkulima. 

Pili, wizara ya Kilimo itapelekea mtaalam wa maabara ya pareto toka TARI kwa ajili ya kusimamia upimaji wa kiwango cha sumu akiwakilisha serikali muda wote kwa kuangali kazi zinzvyofanyika kwenye maabara ya kiwanda  

Tatu, viwanda vyote vya pareto nchini katika kipindi cha miezi sita ijayo havitaruhusiwa kusafirisha nje ya nchi pareto ghafi badala yake vitatakiwa kuweka miundombinu ya kuzalisha bidhaa hapa nchini ili kulinda ajira za watanzania na kuwesaidia zao kuwa na bei nzuri 

Agizo la nne la seikali ni kuwa mashamba yote ya uzalishaji mbegu za pareto nchini lazima yasajiliwe na taasisi za utafiti wa Kilimo (TARI) na ile ya udhibiti ubora wa mbegu ( TOSCI).Lengo kuhakikisha wakuima wanapanda mbegu bora na zenye tija kwenye uzalishaji wa pareto nchini. 

Kusaya alitaja agizo la tano kuwa halmashauri zote zinazozalisha pareto ziratibu vituo vya ununuzi wa zao hilo na kuwa ni mmarufuku wanunuzi kwenda majumbani kununua pareto kwa wakulima sita halmashauri ziweke utaratibu wa wawekezaji kugawana kanda za uzalishaji pareto  na kuingia mikataba na wakulima wa maeneo hayo. 

Katibu Mkuu Kusaya alisema agizo la mwisho ni kuwa halmashauri nchini ziratibu na kuhamaasisha wakulima wa pareto kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kupata huduma za ugani kwa karibu na kuwezesha upatikanaji wa masoko. 

Kwa upande wake mwaklishi wa kiwanda cha Pareto Tanzania (PCT) Gerald Joseph alisema kiwanda kitaendelea kuhakisha kuwa kodi,tozo na ushuru unaotakiwa kulipwa unalipwakwa mujibu wa sheria na 
Aliongeza kusema kuwa watazingatia suala la vipimo na mizani  inayotumika kupima pareto ya wakulima inaendelea kuwa sahihi na kuwa wakulima wanapata bei inayostahili . 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda Tanzania John  Power alisema kiwanda chake kitaendele kuhakikisha kuwa wananunua pareto ya wakulima kwa mujibu wa bei ya soko na kuwa viwango vya ubora lazima vizingatiwe na wakulima wakati wa kuchuma maua ya pareto na kukausha. 

Akitoa uzoefu wake kuhusu sekta ya pareto nchini Mkurugenzi wa SAGCOT Center Ltd Dkt Godffrey Kirenga alisema ili mkulima azalishe zao bora la pareto lazima afundishwe vizuri kanuni bora za uzalishaji 

Dkt.Kirenga aliongeza kusema “ zao hili ndilo lenye uwezo wa kumpatia mkulima pato la uhakika kwani linalimwa kwa mwaka mzima “ katika maeneo ya mikao ya Iringa,Njombe ,Kilimanjaro ,Manyara na Mbeya 

Tanzania ndiye mzalishaji wa pili wa pareto kwa wingi na kupitia kiwanda hiki PCT  mwaka 2019 jumla ya tani  pareto 2,100 ziliuzwa nje na wakulima walilipwa Dola za kimarekani  Milioni 1.539  

Mwisho


Share:

MAGUFULI AMCHAGUA SAMIA SULUHU KUWA MGOMBEA MWENZA URAIS TANZANIA


Samia Suluhu Hassan
Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli amemchagua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM.

Magufuli amesema katika kipindi cha miaka mitano alichofanya kazi na Mama Samia kama makamu wa Rais amejifunza mengi na ameamua kuendelea naye katika awamu ya pili.

''Katika kipindi nilichofanya kazi na Mama Samia nimejifunza mambo mengi sana na kupitia yeye nawahikikishia nitakuwa mtetezi mzuri wa wanawake. Nimekuwa nikimtuma popote hakatai kama na nyie kina Mama mkitumwa hamkatai'', amesema.
Share:

JPM KUJENGAvKIWANDA KIKUBWA CHA KUKU NA KLINIKI YA KISASA YA MIFUGO SINGIDA


Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga Mpina akishiriki katika zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida ambapo Serikali imeahidi kuwezesha kujenga kiwanda kikubwa cha machinjio ya kisasa kitakacholisha Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga Mpina wa kwanza kulia akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Injinia Jackson Masaka na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida ndugu Beatus Choaji wakiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga akionyeshwa kifaa maalum cha kuchanjia mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi (mwenye kofia nyeusi) Luhaga akihutubia umati wa wadau wa mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.
Umati wa wadau wa mifugo wakati wa zoezi la uchanjaji wa mifugo kitaifa pamoja na wataalam wa mifugo lililofanyika leo kwenye kijiji cha Kinyangiri wilayani Mkalama mkoani Singida.


Na John Mapepele, Singida

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema Serikali inakusudia kuwezesha kujenga kiwanda kikubwa cha kisasa cha kuchakata nyama ya kuku kwenye Mkoa wa Singida kitakacholisha Tanzania na nchi mbalimbali duniani ambacho kitakuwa kinafanya uzalishaji ifikapo Desemba mwaka huu ili kuinua hali za wafugaji wa kuku wa Singida na kuongeza pato la taifa.

Mbali na kiwanda hicho, Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kujenga Kliniki bora ya kisasa ya mifugo kwenye Halmashauri ya Mkalama. 


Kliniki hiyo ni miongoni mwa Kliniki 30 ambazo zinazijengwa nchi nzima na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwenye Halmashauri mbalimbali.

Waziri Mpina ameyasema haya kwenye hotuba yake ya uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo za Mifugo Kitaifa kwenye kijiji cha Kinyangiri katika Wilaya ya Makalama mkoani Singida ambayo imelenga kutokomeza magonjwa mbalimbali ya mifugo (hususan magonjwa 13 ya kipaombele) ambayo yamekuwa kikwazo katika uzalishaji na biashara ya mifugo ndani na nje ya Tanzania.

“Tumeona hapa uzalishaji mkubwa sana wa kuku Singida, sasa ninaagiza mambo makubwa mawili Bodi ya Nyama na Dawati la linaloshughulikia Sekta Binafsi katika Wizara yangu kuwezesha kujenga kiwanda cha kuchakata nyama ya kuku na tutakizindua kikiwa kinatoa huduma ifikapo Desemba mwaka huu"Alisema

"Lakini la pili ninamuagiza Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko na Dawati la Sekta Binafsi kuunda vikundi na kuwaletea vitotoleshi vya kisasa ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa kuku ili kuwezesha upatikanaji wa malighafi za kiwanda kwa uhakika” alisisitiza Waziri Mpina.

Mpina amesema magonjwa mengi ya mifugo ni yale ya kuambikiza hususani yanayotokea kwa mlipuko na kusabisha vifo na hasara kubwa kwa wafugaji na kufafanua kuwa hadi sasa tayari, Serikali imekiimarisha kiwanda cha chanjo cha Tanzania Vaccine Institute (TVI) na kinazalisha aina sita (6) ya chanjo za kipaumbele na kitaanza kuzalisha aina nyingine tatu kufikia mwezi Desemba, 2020.

Mbali na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanza kutengeneza chanjo sita Mpina amesema mapinduzi na mageuzi makubwa yamefanyika ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Mifugo inatoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi na kwa mwananchi mmoja mmoja tofauti na awali ambapo sekta hiyo na wafugaji walidharaulika sana.

Ametaja baadhi ya mambo yaliyoboreshwa kwenye eneo la chanjo hapa nchini kuwa ni pamoja na Wizara yake kupitisha Mpango wa Ununuzi wa Chanjo za Mifugo kwa Pamoja (Vaccine Bulk Procurement Plan);

Serikali kutangaza Bei Elekezi ya chanjo aina 13 za magonjwa ya kipaumbele ambapo chanjo zimepungua bei kwa zaidi ya asilimia 60;

Amebainisha kuwa, Katika mwaka 2019/2020, Serikali katika kiwanda cha TVI imezalisha jumla ya dozi 53,851,850 za chanjo za magonjwa ya mlipuko na yanayovuka mipaka na chanjo hizi zote zimechanja mifugo.

Pia, Wizara imevutia wawekezaji na kiwanda kikubwa cha Hester Biosciences Africa Limited kinajengwa na kitakapokamilika kitakuwa kinazalisha aina 37 ya chanjo za wanyama.

Ameongeza kuwa katika mwaka 2019/2020, utoaji wa chanjo umeimarika ambapo Halmashauri 103 kati ya 185 sawa na asilimia 56 zimeshiriki kikamilifu katika kutoa chanjo kwa mifugo

Aidha Mpina amesema kutokana na mikakati ya Wizara yake ya kudhibiti utoroshaji wa mifugo kutoka nchni kwenda nchi za nje na udhibiti wa uingizaji holela wa bidhaa za mifugo nchini kupitia “Operesheni Nzagamba” Serikali ya awamu wa Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliweza kukusanya zaidi ya bilioni 50 kwa mwaka ukilinganisha na Shilingi bilioni 9.5 zilizokuwa zikikusanywa katika kipindi cha nyuma kwa mwaka.

Akitoa maelekezo kwa wataalam Waziri Mpina amewataka wataalmu wote wa mifugo ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Kata kuhakikisha uchanjaji wa mifugo unatekelezwa kikamilifu kulingana na kalenda ya chanjo kwa kuwa ni suala la kisheria ambapo amemtaka Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) kuhakikisha unasimamia jukumu hili na yeye kupatiwa ripoti ya chanjo hizo kila mwezi.

Pia amewataka Wataalamu wote wa mifugo kuhakikisha wanatoa elimu ya chanjo kwa wafugaji ili watambue umuhimu na faida za kuchanja mifugo yao na kwamba, Serikali imeshaandaa mazingira wezeshi ya upatikanaji wa chanjo kila mahali na kwa bei elekezi.

Amesema kulingana na Kalenda ya chanjo kitaifa, mwezi Juni mpaka Augosti, 2020 ni msimu wa chanjo za Homa ya Mapafu ya Ng'ombe, Homa ya Mapafu ya Mbuzi, Sotoka ya Mbuzi na Kondoo, Ugonjwa wa kutupa mimba na Ugonjwa wa Miguu na Midomo.

Hivyo, ametoa wito kwa madaktari wa mifugo wote nchini kuhakikisha kwamba chanjo hizi zinatolewa kikamilifu.

Aidha ameziagiza Halmashauri zote ambazo hazitowi huduma ya chanjo kwa mifugo yao kufanya hivyo mara moja kuanzia mwezi huu wa Julai, 2020.


Ripoti ya idadi ya mifugo na aina ya chanjo inayotolewa iwe inaletwa kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo (DVS) kila wiki.


Share:

BREAKING: Magufuli apitishwa kuwa Mgombea Urais 2020 Kupitia CCM

Mkutano Mkuu wa CCM umempitisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa tiketi ya CCM kwa kura 1,822 za wajumbe sawa na asilimia mia moja ya Kura zilizopigwa na hakuna Kura zilizoharibika.


Share:

Dereva Aliyesababisha Ajali Ya Basi La Prezdar Na Kusababisha Vifo Vya Watu 10 Akamatwa

NA DENIS MLOWE,IRINGA
JESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Iringa limefanikiwa kumkamata dereva wa basi la Prezdar Said Abas Said (30) aliyesababisha ajali eneo la mlima Kitonga iliyopelekea vifo vya watu 10 na majeruhi 36.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa, Juma Bwire alisema kuwa mara baada ya ajali hiyo dereva huyo alifanikiwa kukimbia na kwenda kujificha kwa baba yake mdogo maeneo ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Alisema kuwa Juni 27 katika mlima Kitonga wilaya ya Kilolo kulitokea ajali ya basi lenye namba za usajili T 326 CSX aina ya Yutong linalojulikana kwa jina la kibiashara Prezdar likifanya safari zake Iringa kwenda Dar na kusababisha vifo vya watu 10 na kujeruhi watu 36.

Kamanda Bwire alisema kuwa basi hilo liliacha njia kwenye mlima Kitonga na kutumbukia bondeni ambapo dereva wa basi alikimbia mara baada ya ajali hiyo na jeshi la polisi kumtaka mmiliki wake Neechi Msuya kuwapa ushirikiano wa kumpata dereva huyo.

Alisema kuwa mmiliki wa basi hilo, Neechi Msuya   (40) mkazi wa Dar es Salaam alijisalimisha kituoni Juni 30 mwaka huu ambapo jeshi la polisi liliendelea na msako wa kumtafuta dereva huyo hadi kumpata akiwa amejificha wilaya ya Mbarali.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na upelelezi na pindi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria za usalama barabarani.

Naye Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani  Mkoa wa Iringa Yusuph Kamota amewataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani hasa wanapokuwa katika katika mkoa wa Iringa na kuomba msaada kwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kupata maelekezo pindi wakiona hawaelewi kuhusu mlima Kitonga.

Alisema kuwa madereva wanatakiwa kutii sheria bila shuruti na endapo ikitokea ajali wajisalimishe kwa kifungu cha sheria za usalama barabarani namba 57 hata kama dereva  alikuwa amechanganyikiwa kiasi gani anapewa masaa 12 kuweza kujisalimisha.

Alisema kuwa mtu yoyote ambaye ni dereva asipojisalimisha ndani ya masaa kumi na mbili atakamatwa tu kwani jeshi lina mkono mrefu na macho makali kuweza kubaini wanaokimbia kama ambavyo wameweza kumkamata dereva wa basi la Prezdar.

Kamota alisema kuwa kwa upande wa kikosi cha usalama barabarani wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu ambayo imepunguza matukio ya ajali mkoani hapa na kufanya doria za barabarani usiku na mchana kwa lengo la kukabiliana na ajali.

Alisema kuwa vyanzo vya ajali viko vingi lakini makosa ya ajali yanasababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia asilimia 76 ya ajali hivyo vyanzo kama mwendo kasi, ulevi, kutofata sheria za usalama barabarani kwa ujumla vinadhibitiwa na jeshi hilo kwa njia ya doria.
 
‘’ Sisi kama jeshi tumejipanga vyema kabisa natoa wito kwa madereva wawe na tahadhari katika maeneo hatarishi kama mlima kitonga na bora uwe makini kuuliza kuliko kwenda kusababisha ajali ambazo zinasababishwa na madereva wazembe’’


Share:

Waziri Mhagama Azindua Mpango Wa Uendelezaji Wa Viwanda Vidogo Na Vya Kati Jijini Dodoma.


NA. MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua Mpango wa Uendelezaji wa Viwanda Vidogo na vya Kati wenye lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji wa ujuzi, masoko na mitaji katika miradi midogo na vya kati (SMEs) nchini.

Uzinduzi huo ulifanyika mapema Julai 10, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage Hazina Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe.

Pia ulihudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za SIDO, VETA, NEEC, NSSF na Banki ya AZANIA pamoja na Viongozi na Wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali za Sekta binafsi, Wajasiriamali na Wanafunzi kutoka Vyuo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mhagama amesema uwepo wa mpango huo utasaidia kuongeza kasi ya ujenzi na ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira wezeshi na kuandaa mazingira yenye mfumo wa kibiashara yatakayorahisisha kutengeneza uzalishaji wenye tija na kuunda soko la bidhaa utakaoboresha na kuinua maisha ya Watanzania.

“Serikali imetengeneza fursa za kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kujipatia kipato na kuhakikisha inatatua changamoto mbalimbali zinazokabili nguvu kazi ya taifa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa elimu na ujuzi wa kutosha pamoja na ukosefu wa mitaji na masoko ya uhakika wa bidhaa zinazozalishwa”,alisema Waziri Mhagama.

Waziri alifafanua kuwa mpango umejikita katika kuhakikisha kuwa wajasiriamali wanasaidiwa kuongeza ujuzi, kupata uzoefu na kuwawezesha kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na nje. Aidha, Mpango huu pia unalenga kuwezesha viwanda kupata vifaa vya kisasa  kama mitambo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji ili uwe na tija, kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kupanua shughuli za uzalishaji pamoja na kuongeza kinga za  hifadhi za jamii kwa wajasiriamali.

“Kupitia mpango huu wenye viwanda na wajasiriamali wamepanuliwa fursa ya kupata mitaji hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wengi wanaohitimu vyuo katika ngazi mbalimbali,”Alisistiza Waziri

Aliongezea kuwa, Mfumo unajikita kuwafika wananchi wote bila ubaguzi na matabaka ya aina yoyote kwa kuzingatia vigezo na masharti nafuu yaliyopo katika mfumo huu.

“Programu hii inavunja matabaka baina ya makundi mbalimbali katika jamii na kutoa fursa sawa kuanzia mtu binafsi hadi vikundi katika kuwapatia mitaji na ujuzi sawa hivyo tuiunge mkono kwani inawalenga Watanzania wote,” alisema

Aidha alibainisha sekta ya viwanda imeendelea kuwa na tija katika kuchangia ongezeko la Pato la Taifa kwa kuongezeka kwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ambapo Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2019 ilikuwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na asilimia 8.05 mwaka 2018, sawa na ongezeko la asilimia 0.45 na hii ni matokeo ya kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji viwandani katika kipindi hicho pamoja na kasi ya ukuaji wa thamani ya Uzalishaji Bidhaa Viwandani kwa mwaka 2019 ambayo ilikuwa ni Shilingi Trilioni 10.2 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 9.6 mwaka 2018, sawa na kasi ya ukuaji wa asilimia 5.8

Waziri aliendelea kutoa wito kwa taasisi husika kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu fursa zilizopatikana katika program na kuvitumia vyombo vya habari katika kueleimisha umma kwa malengo ya kuwafikiwa wengi pamoja na kuzitaka taasisi za kibenki kutoa mikopo kwa wajasiriamali kwa mifumo rafiki na inayofikika pamoja na kuutaka uongozo wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuwa na program za tathimin utekelezaji wa mpango kwa vipindi mbalimbali.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alieleza furaha yake ya uwepo wa mpango huo kwani umesadifu mikakakti ya nchi katika uendelezaji viwanda na kusema imekuja wakati mwafaka kwa kuzingatia imelenga sekta zenye tija katika kutoa ajira kwa watanzania wengi kwani imefungamanisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuwa ndizo zenye mchango mkubwa katika ajira.

“Ni hakika kuwa, kupitia Mpango huu wa uendelezaji wa viwanda, ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja katika  mnyororo mzima wa thamani wa sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji zitaongezeka na kupunguza changamoto mbalimbali zinazokabili jamii kutokana na ongezeko la wasio na ajira nchini,”Alisema waziri Bashungwa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’I Issa alisema, mpango umeainisha namna bora ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo la kukuza mitaji na kuimarisha vyanzo vyao vya mapato na kukuza akiba na mikopo.


Share:

Intaneti kwa njia ya simu inavyochagiza ukuaji wa uchumi jumuishi

Kisaka Msuya, UDBS
Hivi karibuni Benki ya Dunia imetangaza kuwa Tanzania imeingia rasmi kwenye uchumi wa kati ikiwa ni miaka mitano kabla ya kufikia ukomo wa muda uliokuwa umewekwa na serikali yaani 2025.

Tanzania imefanikiwa kufikia hatua hii kutokana na ukuaji imara wa uchumi. Kwa mfano, mwaka uliopita Tanzania ilirekodi ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7, hivyo kusaidia kuendelea kuwa miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.

Mafanikio ya nchi kufikia uchumi wa kati ni kitu cha kujivunia sana. Lakini ni muhimu kuhakikisha kuwa jitihada zaidi zinafanyika ili kuhakikisha kuwa faida ya mafanikio ya nchi yanawanufaisha Watanzania wote kwa usawa.

Uchunguzi wa hivi karibu wa wanazuoni kutoka Marekani umeonesha kuwa teknolojia ya kidigitali imekuwa nyenzo muhimu sana ya kuzisaidia nchi za Afrika kufikia ukuaji wa uchumi jumuishi. Utafiti wao umedadavua kuwa upatikanaji wa huduma ya intaneti kwenye simu hukuza upatikanaji wa taarifa za fursa mbalimbali kujikwamua kiuchumi, mtandao wa ajira, fursa za kazi na kipato jumuishi. 

Kwa miaka ya hivi karibuni usambaaji wa huduma ya intaneti nchini umekua sana na kufikia asilimia 46. Ukuaji huo umechangiwa pia kwa kiasi kikubwa na kampuni za watoa huduma za mawasiliano ya simu nchini.

Watoa huduma hawa wamefanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa wanaziba ombwe la upatikanaji wa mtandao wa intaneti kati ya maeneo ya mjini na vijijini. Sasa ni wazi kuwa kusaidia jamii za vijijini kupata huduma ya intaneti ya uhakika ni jambo muhimu sana katika kupunguza utofauti kati ya jamii hizo mbili.

Mbali na hilo, kuwa na huduma ya intaneti ya uhakika ni njia muhimu ya kusaidia kufanikisha uwepo wa fursa za kiuchumi kwa ambao walikuwa wameachwa nyuma. Kwa mfano, huduma ya fedha ya Kampuni ya Tigo (Tigo Pesa) inawasaidia wale wote ambao hawakuwa na uwezo wa kupata huduma za benki kama kupata mikopo na kuweka akiba, ambayo mwisho wake inasaidia kukuza huduma ya fedha jumuishi.

Tigo inaendelea kufanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa inaziba utofauti wa kidijitali uliopo sasa. Simu yao mpya ya gharama nafuu ya Kitochi 4G inamuwezesha mtumiaji kukamilisha mawasiliano pamoja na kuperuzi mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp.

Wakati nchi ikiwa imefungua ukurasa mpya kuelekea ukuaji mkubwa wa uchumi na maendeleo, tuangazie kwa mapana namna ambazo kampuni za simu zinaweza kuendelea kuwa na mchango mkubwa katika kufikia mafanikio.

Kwa kuwekeza katika miundombinu ya kizazi kijacho, kampuni za mawasiliano ya simu zinaweza kuendelea kuboresha usambazwaji wa huduma ya intaneti na kuhakikisha Watazania wengi zaidi wananufaika na huduma za simu. Tuendelee kuwa na matumaini kuwa sekta hii itapata msaada inaohitaji kupitia sheria na kanuni rafiki na vichocheo vya uwekezaji kwani kwa kufanya hayo, tutaweza kukahakikisha kuwa mafanikio yanawagusa Watanzania wote.


Share:

Katibu Tawala (DAS) Handeni Afariki Dunia Katika Ajali Mbaya....Watatu Wanusurika Akiwemo Mbunge

Aliyekuwa Katibu Tawala (DAS) Boniface Maiga Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga amepoteza maisha katika ajali huku watu watatu wakijeruhiwa akiwemo Mbunge wa Jmbo la Handeni Omary Kigoda ambaye amevunjika vidole viwili vya mkono wa kulia wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa yake dereva wa gari la Mbunge wa Handeni Omary Kigoda, Peter Mganga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba usiku katika eneo la Vikonji Dodoma.

Amesema chanzo cha ajali hiyo imetokana na mwendokasi aliokuwa dereva wa basi baada ya kulipita sehemu yenye kona kitendo ambacho si sahihi.

Dereva huyo wa mbunge amesema baada ya dereva wa basi kulipita katika eneo hilo lenye kona kali alimuwashia taa ili aweze kupunguza mwendo gari ila dereva wa basi hilo hakupunguza spidi na ndipo wakavana uso kwa uso.

“Katika ajali hii dereva na kondakta wa basi wote wamefariki nilijaribu kumwashia taa nyingi ili apunguze spidi lakini cha kushangaza kama hajaziona ilibidi sisi tupaki pembeni ndipo mwendo aliokuwa nao ililazimu kulivaa gari letu hasa upande wa kulia aliokuwa amekaa mheshimiwa mbunge na DAS wetu aliyefariki,”alisema Mganga.

Amesema mara baada ya ajali hiyo DAS alipoteza maisha hapo hapo huku wao wakikimbizwa katika hospitaliti ya Chamwino kwajili ya matibabu ambapo Mbunge alilazimika kufanyiwa upasuaji wa vidole hivyo wakahamishiwa katika hospitali ya Mkoa Dodoma (General Hospital).

Mganga amesema baada ya kupata matibabu wawili waliruhusiwa kutoka hospitalini hapo saa kumi na moja alfajiri huku mbunge Kigoda akibaki kuendelea na matibabu ya vidole alivyoumia.

Amesema katika gari hiyo ya mbunge Kigoda walikuwa watu wanne akiwemo yeye Dereva wa Mbunge Peter Mganga, Mbunge Omary Kigoda, Mbelwa Saidy ambaye ni ndugu yao pamoja na Boniface Maiga (DAS) aliyepoteza maisha na kueleza kuwa mwili wa marehemu upo katika hospitali hiyo ya Mkoa.

Credit:Majira


Share:

LIVE: Mkutano Mkuu Wa CCM Wa Taifa

LIVE: Mkutano Mkuu Wa CCM Wa Taifa


Share:

Katibu Mkuu Kilimo Apongeza Taasisi Za Uzalishaji Mbegu Nchini

Wizara ya Kilimo imezitaka taasisi na wakala zinazohusika na kazi ya uzalishaji mbegu bora za mazao kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji makubwa ya wakulima nchini.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa agizo hilo jana (10.07.2020) wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wakati alipofanya ziara ya kukagua shamba la uzalishaji mbegu Dabaga linalomilikiwa na serikali kupitia Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA)
 
“ Sasa ni matarajio ya serikali kuwa ASA mtaendelea kuzalisha mbegu bora kwa wingi na ubora ili kufikia malengo ya nchi kujitosheleza kwa mbegu  na kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima” alisema Kusaya
 
Katibu Mkuu huyo aliipongeza  Wakala wa Mbegu wa Taifa kwa kusema wanazalisha mbegu bora toka katika mashamba yake 11 yaliyopo nchini  na zinapatikana kwa bei rahisi hivyo kuwasaidia wakulima kutotumia gharama zaidi katika uzalishaji.
 
Ili kuongeza uzalishaji mbegu bora Kusaya ameagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu wa Taifa kuandaa andiko na kuliwasilisha wizarani kuhusu upatikanaji wa mfumo wa umwagiliaji ili mbegu zizalishwe kipindhi chote cha mwaka badala ya kutegemea mvua.
 
Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Mbegu Dabaga Edward Mbugi alieleza kuwa wamefanikiwa kuongeza upatikanaji wa mbegu nchini kutoka tani 587 mwaka 2015 hadi tani 1,436 mwaka 2019.
 
Aliongeza kusema wakala wa mbegu unamiliki maeneo yenye ukubwa wa hekta 12,188 kati yake hekta 8,348 ndio zinafaa kwa Kilimo hali iliyofanya kwa ushirikiano na kampuni binafsi kuweza kuchangia upatikanaji mbegu bora nchini kufikia asilimia 28 msimu wa 2019.
 
“  Katika makampuni yanayozalisha mbegu bora  nchini msimu wa 2018/2019 ASA ilishika nafasi ya pili kwa uzalishaji mbegu bora ndai ya nchi na  ya kwanza kwa uzalishaji wa baadhi ya mbegu mfano mpunga na alizeti” alisema Mbugi
 
Shamba la mbegu la Dabaga katika msimu huu kwa ushirikaiano na kampuni ya Seedco Ltd wamefanikwa kulima hekta 40 za mahindi chotara (UH 6303) zinazotarajiwa kutoa tani 120 za mbegu za mahindi bora.
 
Katibu Mkuu huyo alitembelea pia mashamba ya chai yawakulima wadogo wa kijiji cha Kidagala kujionea hali ilivyo ya zao hilo kutolimwa kikamilifu kutokana namgogoro wa kiwanda cha chai cha Kilolo kutofanya kazi
 
Katibu mkuu huyo aliwafahamisha wakulima hao kuwa serikali ya awamu ya tano itafanyia kazi madai yao ili kiwanda cha chai Kilolo kiweze kufanya kazi na kuwezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao
 
Akieleza sababu ya mashamba hauyo kugeuka pori,Mwenyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Chai Dabaga Venance Kihwaga alisema wawekezaji wanataka kiwanda kikianza kazi wakulima wasiwe wabia bali wazalishaji tu wa malighafi hali ambayo wakulima hawaitaki.
 
“ Tatizo wawekezaji wanataka umiliki wa soko la majani ya chai wapate asilimia 100 na wakulima wabakie kuwa manamba kwa kulima na kuuza tu.Hawataki wakulima washiriki kwenye mnyororo wa thamani hali inayopingwa na wakulima “ alisema Mwenyekiti Kihwaga
 
Akijibu malalamiko ya wakulima hao,Kusaya alisema atakutana na Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe ili wajadili na kuweka mkakati wa ukupata ufumbuzi wa kero hii iliyodumu muda mrefu sasa.
 
“ Tunataka kuona kiwanda hiki cha chai Kilolo kinafanya kazi na kuwanufaisha wakulima kwa uhakika wa soko.Nimekuja hapa baada ya kusikia malalamiko mengi,ninaahidi kushirikiana na makatibu Wakuu wenzangu wa Viwanda na wengine kupata suluhu.” Kusaya alisisitiza.
 
Mwisho



Share:

Habari Zilizopo Magazeti ya Leo Jumamosi July 11

















Share:

Friday 10 July 2020

WATUHUMIWA MAUAJI YA WATU WANNE MGODINI KAHAMA WAKAMATWA


Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, SACP Mihayo Msikhela akionesha baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa kwenye msako wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji.

Na Damian Masyenene–Shinyanga Press Club Blog

Wiki chache baada ya tukio la mauaji ya watu wanne katika mgodi wa wachimbaji wadogo uliopo eneo la namba 4, Kijiji cha Wisolele Kata ya Segese Tarafa ya Msalala katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga kwenye Plant ya kuchenjua Dhahabu ya Dakires, Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwanasa watuhumiwa 13 na vielelezo mbalimbali.

Tukio hilo la mauaji lilitokea Juni 30, 2020 saa 2:00 usiku, ambapo walinzi wawili wa kampuni ya Sekepa inayolinda Plant hiyo, Juma Jigwasanya na Lusajo Michael pamoja na Mwendesha Mtambo wa Plant, Raphael Kipenya na Msimamizi Mkuu wa plant hiyo,Daniel William waliuawa kwa kugongwa na kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na watu wasiojulikana.

Ambapo baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi nchini liliamua kufanya msako kuwasaka watuhumiwa wa uvamizi na mauaji hayo na operesheni hiyo ilikamilika jana Julai 9, 2020 Alfajiri.

Akitangaza matokeo ya msako huo wa siku 10 kwa waandishi wa habari leo Julai 10, 2020 katika kituo cha Polisi Bugarama halmashauri ya Msalala, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, SACP Mihayo Msikhela amesema kuwa baada ya taratibu za upelelezi kukamilika watapelekwa mahakamani haraka iwezekanavyo, huku Jeshi hilo likiendelea kuwatafuta baadhi ya watuhumiwa waliokimbia ili nao wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

“Baada ya tukio Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi lilianza msako wa kuwatafuta wahalifu hao, tutaendelea kufanya operesheni na misako kwenye migodi yote ya uchimbaji madini ili kubaini mtandao wote wa watuhumiwa wanaojihusisha na matukio kama haya,” alisema.

Amesema katika tukio hilo mhanga mmoja, Exavery Mboya (21) ambaye alikuwa mwendesha mitambo kwenye plant hiyo alinusurika baada ya kujeruhiwa na kuwekwa pamoja na marehemu baada ya watuhumiwa kuamini kuwa ameuawa, ambapo majeruhi huyo amelazwa hospitali ya Mji Kahama na afya yake imezidi kuimarika.

SACP Msikhela alitaja vielelezo vilivyokamatwa katika opereseheni hiyo vikihusishwa na tukio hilo la mauaji, kuwa ni mchanga viroba saba visivyo na mnaso wa dhahabu (vimeshachenjuliwa) iliyoibiwa kwenye plant hiyo Kilo 464.76, viroba vinne vya Carbon vyenye dhahabu Kilo 385.34 vikiwa kwenye hatua ya kupelekwa kwenye kinu kwa ajili ya kuchenjuliwa, pikipiki tano zikiwemo nne zilizotumika mzigo na moja ambayo mmoja wa watuhumiwa alikimbia na kuitelekeza.

Vingine ni Bunduki aina ya Shotgun yenye serial namba9025817, namba ya usajili TZCAR103855 ambayo iliporwa kwa mlinzi mmojawapo aliyeuawa siku ya tukio ikiwa na risasi mbili baadae kutelekezwa umbali wa mita 400 kutoka kwenye eneo la tukio.
Kamanda Msikhela amesema pia wamekamata panga moja, ambapo msako huo ulianza Juni 30, mwaka huu na kumalizika juzi (Alhamisi) alfajiri ambao watuhumiwa hao ni wale waliosuka mpango, walioutekeleza, waliosafirisha mizigo na waliohifadhi mizigo.

Hata hivyo Kamanda Msikhela ametoa wito kwa mamlaka zinazoshughulikia utoaji wa nyaraka na vibali vya kusafirisha mchanga kwenda kuuchoma ili kupata dhahabu, ni vyema wakatoa vibali baada ya kujiridhisha uhalali wa mchanga huo hasa kwa kufika kwenye Plant, kubaini mmiliki halali au mchanga husika ili kuepuka kutoa vibali kwa wahalifu.
Viroba vya Carbon ya Dhahabu vilivyokamatwa kwenye operesheni hiyo.
Bunduki aina ya Shot Gun na Panga vilivyokamatwa vikihusishwa na tukio hilo la mauaji.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, SACP Mihayo Msikhela (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha Polisi Bugarama halmashauri ya Msalala, kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba.
SACP Msikhela akionyesha baadhi ya vielelezo vinavyohusiana na tukio hilo.
Sehemu ya viroba vilivyonaswa vyenye Carbon ya kuchenjulia Dhahabu
SACP Mihayo Msikhela (kushoto) akionesha risasi mbili zilizokutwa kwenye bunduki aina ya Shot Gun iliyotumika kwenye tukio la mauaji.
SACP Msikhela akionesha sehemu ya vielelezo mbalimbali vilivyonaswa kwenye msako huo zikiwemo pikipiki tano zilizotumiwa na watuhumiwa kutekeleza mpango wao wa uvamizi mgodini.
SACP Msikhela akitoa maelezo mbalimbali kuhusu vielelezo vilivyonaswa kuhusiana na tukio hilo la mauaji.

Picha zote na Damian Masyenene

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB CLOG
Share:

Picha : EMMANUEL NTOBI, SALOME MAKAMBA WARUDISHA KWA KISHINDO FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI KUPITIA CHADEMA

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Ntobi (aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngokolo na Mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Shinyanga) na Salome Makamba (aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum) wamerudisha kwa kishindo Fomu za kuomba kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 10,2020.

Makada hao wa CHADEMA wamewasili katika Ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini wakisindikizwa na misafara ya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wanaendesha magari na pikipiki huku wakiwa wamebeba bendera za chama hicho sambamba na matarumbeta ya hapa na pale.

Mara baada ya kuwasili katika ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, watia nao walikabidhi fomu za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa na chama chao kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini kisha wakapata nafasi ya kuelezea mbele ya wanachama wa CHADEMA malengo yao ya kuomba chama kiwapitishe kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.

Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala amesema zoezi la kurudisha fomu kwa wanachama wa CHADEMA waliotia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini ni leo Ijumaa Julai 10 saa 10 kamili jioni.

“Zoezi linalofanyika leo ni kupokea fomu za wanachama wetu waliojitokeza kuomba kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Shinyanga ambapo majina ya waliojitokeza yatajadiliwa katika mkutano wa chama na atapatikana mgombea mmoja”,amesema Ndatala.

Ameyataja majina ya wanachama wa CHADEMA waliochukua fomu kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kuwa ni Emmanuel Ntobi, Samson Ng’wagi, Mchungaji Jilala Fumbuka, Nicholaus Luhende, Hassan Salim pamoja na Zainab Kheri Zena Gulam wanaowania nafasi ya Ubunge Viti Maalum.

Ndatala amesema zoezi la wanachama wa CHADEMA kurudisha fomu za kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini limeenda sambamba na kumdhamini Tundu Lissu kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Ntobi (aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngokolo na Mwenyekiti CHADEMA mkoa wa Shinyanga) akiwasili katika ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 10,2020 wakati akirudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akizungumza wakati wa kupokea fomu za wanachama wa CHADEMA waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akizungumza wakati wa kupokea fomu za wanachama wa CHADEMA waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Emmanuel Ntobi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Emmanuel Ntobi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akionesha fomu ya Emmanuel Ntobi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba  chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Emmanuel Ntobi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Samson Ng'wagi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Samson Ng'wagi kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Samson Ng'wagi akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Salome Makamba akiwasili katika ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini kurudisha fomu ya  kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Salome Makamba kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Salome Makamba kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Salome Makamba akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Salome Makamba akieleza sababu zilizomsukuma kuomba chama chake kimpe ridhaa ya kugombea  Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Joseph Ndatala  akipokea fomu ya Zena Gulam kuwania nafasi ya Ubunge Viti Maalum Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mtia nia kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA  Zena Gulam akieleza sababu zilizomsukuma kugombea  Ubunge Viti Maalum Jimbo la Shinyanga Mjini.
Awali Makada wa CHADEMA wakiendelea na shamra shamra nje ya ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini.
Awali Makada wa CHADEMA wakiendelea na shamra shamra nje ya ofisi za CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini.
Msanii Mussa Jumanne akitoa burudani wakati makada wa CHADEMA wakirudisha  fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Msanii Mussa Jumanne akitoa burudani wakati makada wa CHADEMA wakirudisha  fomu kuomba kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger