Saturday 11 July 2020

Katibu Mkuu Kilimo Apongeza Taasisi Za Uzalishaji Mbegu Nchini

...
Wizara ya Kilimo imezitaka taasisi na wakala zinazohusika na kazi ya uzalishaji mbegu bora za mazao kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji makubwa ya wakulima nchini.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa agizo hilo jana (10.07.2020) wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wakati alipofanya ziara ya kukagua shamba la uzalishaji mbegu Dabaga linalomilikiwa na serikali kupitia Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA)
 
“ Sasa ni matarajio ya serikali kuwa ASA mtaendelea kuzalisha mbegu bora kwa wingi na ubora ili kufikia malengo ya nchi kujitosheleza kwa mbegu  na kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima” alisema Kusaya
 
Katibu Mkuu huyo aliipongeza  Wakala wa Mbegu wa Taifa kwa kusema wanazalisha mbegu bora toka katika mashamba yake 11 yaliyopo nchini  na zinapatikana kwa bei rahisi hivyo kuwasaidia wakulima kutotumia gharama zaidi katika uzalishaji.
 
Ili kuongeza uzalishaji mbegu bora Kusaya ameagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu wa Taifa kuandaa andiko na kuliwasilisha wizarani kuhusu upatikanaji wa mfumo wa umwagiliaji ili mbegu zizalishwe kipindhi chote cha mwaka badala ya kutegemea mvua.
 
Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Mbegu Dabaga Edward Mbugi alieleza kuwa wamefanikiwa kuongeza upatikanaji wa mbegu nchini kutoka tani 587 mwaka 2015 hadi tani 1,436 mwaka 2019.
 
Aliongeza kusema wakala wa mbegu unamiliki maeneo yenye ukubwa wa hekta 12,188 kati yake hekta 8,348 ndio zinafaa kwa Kilimo hali iliyofanya kwa ushirikiano na kampuni binafsi kuweza kuchangia upatikanaji mbegu bora nchini kufikia asilimia 28 msimu wa 2019.
 
“  Katika makampuni yanayozalisha mbegu bora  nchini msimu wa 2018/2019 ASA ilishika nafasi ya pili kwa uzalishaji mbegu bora ndai ya nchi na  ya kwanza kwa uzalishaji wa baadhi ya mbegu mfano mpunga na alizeti” alisema Mbugi
 
Shamba la mbegu la Dabaga katika msimu huu kwa ushirikaiano na kampuni ya Seedco Ltd wamefanikwa kulima hekta 40 za mahindi chotara (UH 6303) zinazotarajiwa kutoa tani 120 za mbegu za mahindi bora.
 
Katibu Mkuu huyo alitembelea pia mashamba ya chai yawakulima wadogo wa kijiji cha Kidagala kujionea hali ilivyo ya zao hilo kutolimwa kikamilifu kutokana namgogoro wa kiwanda cha chai cha Kilolo kutofanya kazi
 
Katibu mkuu huyo aliwafahamisha wakulima hao kuwa serikali ya awamu ya tano itafanyia kazi madai yao ili kiwanda cha chai Kilolo kiweze kufanya kazi na kuwezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao
 
Akieleza sababu ya mashamba hauyo kugeuka pori,Mwenyekiti wa Kikundi cha Wakulima wa Chai Dabaga Venance Kihwaga alisema wawekezaji wanataka kiwanda kikianza kazi wakulima wasiwe wabia bali wazalishaji tu wa malighafi hali ambayo wakulima hawaitaki.
 
“ Tatizo wawekezaji wanataka umiliki wa soko la majani ya chai wapate asilimia 100 na wakulima wabakie kuwa manamba kwa kulima na kuuza tu.Hawataki wakulima washiriki kwenye mnyororo wa thamani hali inayopingwa na wakulima “ alisema Mwenyekiti Kihwaga
 
Akijibu malalamiko ya wakulima hao,Kusaya alisema atakutana na Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe ili wajadili na kuweka mkakati wa ukupata ufumbuzi wa kero hii iliyodumu muda mrefu sasa.
 
“ Tunataka kuona kiwanda hiki cha chai Kilolo kinafanya kazi na kuwanufaisha wakulima kwa uhakika wa soko.Nimekuja hapa baada ya kusikia malalamiko mengi,ninaahidi kushirikiana na makatibu Wakuu wenzangu wa Viwanda na wengine kupata suluhu.” Kusaya alisisitiza.
 
Mwisho



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger