Thursday 2 January 2020

Upande wa Jamhuri wakataa Kabendera kumzika Mama yake...Mahakama Kuamua

Upande wa Serikali umempa pole Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi huku ukipinga maombi yake ya kutaka ashiriki Ibada ya mazishi ya mama yake.

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Kabendera anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha alipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.

“Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba,”amesema Wankyo.

Wankyo amedai kuwa maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia Mkurugenzi wa Mashitaka hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

“Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini mahakama isifungwe mikono,” amesema.

Kuhusu mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefika hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP).

Kukataliwa kwa Kabendera kushiriki mazishi ya Mama yake, kumeibuka kutokana na maombi aliyoyatoa Kabendera kupitia Mawakili wake akiwemo Jebra Kambole.

Wakili Kambole amedai wanaiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Changombe majira ya mchana.

Kambole ameieleza mahakama kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha.

“Kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake tutakuwa tumemuadhibu adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza na ni vizuri akatoa heshima ya mwisho,”ameeleza.

Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.

“Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho,” ameomba.

Baada ya kutoa hoja hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.


Share:

Waandamanaji waondoka eneo la ubalozi wa Marekani, Iraq

Waungaji mkono wa makundi ya kijeshi nchini  Iraq yanayoungwa mkono na Iran ambao waliovamia maeneo ya viunga vya ubalozi wa  Marekani na kurusha mawe katika maandamano ya siku mbili wameondoka jana(01.01.2020).

Hatua  hiyo  imewezekana  baada  ya  Marekani kupeleka  vikosi vya  ziada na  kutishia  kuchukua  hatua  dhidi  ya  Iran. Lakini  wachambuzi wa masuala  ya  kisiasa  wanaonya  kuwa  hali  hiyo  inaweza  kuwa  na athari  za  kudumu  katika  sekta tete  ya  usalama  nchini  Iraq pamoja  na  mahusiano  ya  kidiplomasia.

Waandamanaji , ambao wamekasirishwa  na  mashambulizi  ya anga  ya   vikosi  vya  jeshi  la  Marekani  dhidi  ya  kundi linaloungwa  mkonom na  Iran  la  Hezbollah  ambapo  kiasi  ya  watu 25 waliuwawa, walirusha  mawe katika  jengo  la  ubalozi  wakati wanajeshi wa   jeshi  la  Marekani  waliokuwa  katika  mapaa ya jengo  hilo  wakifyatua  mabomu  ya  kutoa  machozi kuwatawanya.

Ilipofika  mchana , wengi walionekana  kutii wito  wa  kujiondoa kutoka  katika  eneo  hilo, uliotolewa  na  kundi  la  wanamgambo  wa Kishia linaloongoza  vikundi  vya umma  vya  mapambano PMF, ambalo  lilisema  ujumbe  wa  waandamanaji  tayari  umesikika.

Vijana walitumia  matawi  ya miti  ya  mitende kufajia  mtaa  mbele ya  eneo  la  ubalozi  wa  Marekani. Wengine  walikusanya  vifaa hivyo na magari yaliwasili  kuvichukua.

Maandamano  hayo  yameonesha mabadiliko  mapya  katika  kivuli cha  vita  kati  ya  Marekani  na  Iran  vinavyotokea  katika  eneo  la mashariki  ya  kati. Rais Donald Trump  ambaye  anakabiliwa  na kampeni  ya  uchaguzi  mwaka  2020, ameishutumu  Iran kwa kuchochea  ghasia  hizo. 

Ametishia  siku  ya  Jumanne  kuchukua hatua  dhidi  ya  iran lakini  alisema  baadaye  kuwa  hataki  vita. 

Makamu  ya  rais  katika  taasisi  ya  Charles Koch  anayehusika  na utafiti  na  sera Will Ruger  amesema  hatua Marekani  inazochukua kuibinya Iran hazitafanyakazi:

"Moja ya  matatizo  hapa  ni  kwamba  sio tu shambulio la  roketi  la jeshi  la  Marekani ndio lililochochea mzozo  huu, lakini  pia  kile tulichoshuhudia  jana katika  ubalozi wa  Marekani mjini  Baghdad, nafikiri  hii inaonesha  kwamba  kampeni  kubwa  ya  shinikizo ambayo  utawala  wa  Trump  umekuwa  ukitumia dhidi  ya  Iran haifanyikazi kupunguza  wasi  wasi. Na haifanyi Iran kutulia. Badala yake  inaleta  uhasama na  changamoto nyingi kwa  mahusiano."
 
Iran , ikiwa  katika  hali  mbaya  ya  kiuchumi kutokana  na  vikwazo vya  kuumiza  vilivyowekwa  na  Trump, imekana  kuhusika. 

Ghasia hizo  zilitokana  na  mashambulizi  ya  anga  siku  ya  Jumapili dhidi ya  vituo  vya  kundi  la  Kataib Hezbollah kwa  kulipiza  kisasi  kwa mashambulizi  ya  makombora  ambayo  yalisababisha  kifo  cha mkandarasi  wa  Marekani  kaskazini  mwa  Iraq wiki  iliyopita.

Marekani imesema  wanadiplomasia wako salama na inapeleka  mamia  ya  wanajeshi wa ziada  katika  eneo  hilo. 

Wizara ya  mambo ya kigeni ya  Marekani imesema  jana  kuwa  waziri wa  mambo  ya  kigeni Mike Pompeo  ameamua  kuahirisha  ziara  yake  kwenda  Ukraine, Belarus , Kazakhstan, Uzbekistan, na  Cyprus  na  kubakia  mjini  Washington ili  kufuatilia  hali  nchini  Iraq.

-DW


Share:

Polisi adaiwa kukatwa sehemu za siri na mkewe

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Flora Adamu (23), mkazi wa Shinyanga Mjini, kwa tuhuma za kumkata mumewe sehemu za siri, ambaye ni askari Polisi mwenye Namba H, 8980 Pc Kazimiri, kwa madai ya kumtuhumu kutokuwa muaminifu katika ndoa.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alimtuhumu mumewe kuwa ana  nyumba ndogo.

Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Deborah Magiligimba, alisema tukio hilo limetokea Desemba 28 mwaka jana, majira ya saa 6:30 usiku wakati wanandoa hao wakiwa wamelala.

Alisema wakiwa wamelala, ghafla Flora aliamka na kuanza kumnyatia, huku akiwa ameshika kitu chenye ncha kali kisha kumkata mumewe sehemu za siri na kumjeruhi vibaya.

“Baada ya askari huyu kukatwa uume wake alikimbizwa kwenye Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga ili kupatiwa matibabu ya haraka, ambapo alilazwa kwa muda wa siku mbili  kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea kujiuguza kidonda,” alisema  Kamanda Magiligimba.

“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mwanamke alikuwa akimtuhumu mume wake kuwa ana nyumba ndogo, ndipo akaamua kuchukua kitu chenye ncha kali kisha kuanza kuukata uume wa mumewe na kumjeruhi vibaya,” aliongeza.

Aidha, kamanda huyo alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke huyo, na kwamba uchunguzi ukikamilika, atafikishwa mahakamani.


Share:

Papa Francis aomba radhi kwa kumchapa kibao muumini Aliyemvuta kwa Nguvu

Papa Francis ameomba radhi kwa kumpiga kibao mkononi mwanamke mmoja aliyemvuta kwa nguvu wakati akisalimiana na waumini katika mkesha wa mwaka mpya. Papa amesema alikosa uvumilivu na kwamba kitendo kimeweka mfano mbaya.

Papa alikuwa akisalimiana na watoto na mahujaji na wakati akigeuka mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye umati wa watu waliokuwa karibu aliuvuta mkono wa Papa kwa nguvu karibu amuangushe.

Hali iliyomfanya Papa kugeuka na kumpiga makofi mawili mkononi mwanamke huyo kwa hasira.


Badaye Papa alikiri kwamba alishindwa kujizuia na yeye pia huwa anakosea kama binadamu wengine.

Hivyo anaomba radhi kwa kitendo hicho kwa muumini huyo na kila mtu.

Kitendo cha Papa cha kumzaba makofi ya mkononi mwanamke huyo, kimezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, hasa Twitter, wengi wakimuunga mkono Papa.


Share:

DC Njombe ataka amani isichezewe

Na Amiri kilagalila-Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri,ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuwa sehemu ya kuilinda amani ya Tanzania ili kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla na kuendelea kuifanya tanzania kuwa ndio sehemu pekee yenye amani ya uhakika Duniani.

Pamoja na hayo amewakaumbusha wananchi wa mkoa wa Njombe kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani hapo baadaye mwaka huu

Ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini wa kanisa la Angricana dayosisi ya Tanganyika magharibi lililopo mtaa wa Mji mwema mjini Njombe wakati wa ibada ya mwaka mpya ambapo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kulinda amani.

“Tusichezee amani watanzania wenzangu,kuna watu wachache ambao hawajui amani kwamba ni pamoja na uhai wako,amani hii ambayo ndio msingi wa taifa letu,tusithubutu kuivuruga kwa wakati wowote wala kwasababu yeyote wala kwa ushawishi wa aina yoyote ile”alisema Ruth Msafiri

Aidha ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kujitokeza kujiandikisha na kuhakiki katika daftari la mpiga kura, zoezi lililo anza hii leo na kumalizika januari 5,2020 mkoani humo.

Mchungaji wa kanisa hilo Ayub Haule amesema uwepo wa amani katika taifa hutoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo ni vema kila mtanzania kuwa sehemu ya kulinda amani ya Tanzania

“Tunao uchaguzi mkuu wa nchi hii ambao tunategemea kabisa kama amani ilivyoendelea kudumu ndivyo tutakavyofanya,tunapokuwa tunauona mwaka huu tuone ambavyo tunaweza kupambana na adui mkubwa anayetusakama katika mkoa wetu nae ni maambukizi ya VVU”alisema mchungaji Ayub Haule

Nje ya ibada baadhi ya waumini  wamekiri kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuilindi amani iliyopo.

Mwaka 2019 umekamilika hapo jana ambapo watanzania waliungana kwa pamoja kuukaribisha mwaka mpya 2020 ambapo walio wengi wamekuwa wakituma maombi yao kwa Mungu ili mwaka huu 2020 uwe mwaka wa mafanikio makubwa katika maisha yao


Share:

PAPA FRANCIS AOMBA RADHI KWA KUMCHAPA VIBAO MUUMINI

Share:

BITEKO AKAMATA KIWANDA BUBU CHA UCHENJUAJI DHAHABU SHINYANGA


Ndani ya kiwanda bubu kilichokamatwa na kufungiwa na waziri wa Madini Dotto Biteko.
Baadhi ya mifuko zaidi ya 25 ya cabon iliyokamatwa kabla ya kuchenjuliwa katika kiwanda hicho.
Maafisa madini wakifunga kiwanda bubu cha Uchenjuaji dhahabu katika kijiji cha Bunango wilayani Kahama.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumaza na mwenyekiti wa kitongoji cha Mnara wa voda Masoud Bakari kijiji cha Bunango katika kata ya Bugarama.

Na Salvatory Ntandu - Kahama
Licha ya serikali kuboresha sekta ya madini kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga imebainika kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu ikiwemo kuanzisha viwanda bubu na kuikosesha serikali mapato.

Hayo yalibainishwa Januari Mosi mwaka 2020 Waziri wa Madini Dotto Biteko katika ziara yake ya siku mmoja ya kushitukiza katika kijiji cha Bunango katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya kubaini kiwanda bubu cha kuchenjua dhahabu kilichopo katikati ya makazi ya watu.

“Kiwanda hiki kipo hapa katika nyumba hii tangu mwezi julai mwaka 2019 huku kikiendelea kufanya kazi,serikali imepoteza mabapo mengi tutachukua hatua kali za kisheria kwa miliki wa mtambo huu na nyumba hii”,alisema Biteko.

Sambamba na hilo Biteko aliwataka viongozi wa vijiji na Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya madini ambazo zinafanyika katika makazi ya watu ambao hawana vibali wanaoikosesha serikali mapato.

“Niwaagize viongozi wa mkoa wa Shinyanga kuthibiti vitendo vya biashara haramu ya madini ambavyo vinaendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali kwani mpaka sasa tumeshakamata viwanda bubu viwili vya uchenjuaji wa dhahabu ili kutokomeza vitendo hivi", alisema Biteko.

Hata hivyo Biteko aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Bunango Kajanja Kajanja na Mke wa mwenye nyumba iliyobainika kuwa na mtambo wa kuchenjulia dhahabu aliyefahamika kwa jina mmoja la Shule kuhusiana na kuhusishwa na tukioa hilo.

Masoud Bakari Balozi wa kitongoji cha mnara wa voda alisema alishatoa taarifa kwa mamlaka za kisheria kuhusiana na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo lake lakini hakuona hatua zozote zikichukuliwa kwa wahusika.

“Kiwanda hiki kipo katika nyumba hii tangu julai mwaka jana kuna vijana wageni wanne ambao walikuwa wakifanyashughuli ya kuchenjua dhahabu hapa viongozi wote wa eneo hili wanajua tumelalamika sana kuhusiana kumwagwa ovyo kwa maji yenye kemikali kwenye makazi yetu”,alisema Bakari.

Katika ziara hiyo mifuko zaidi ya 35 imekamatwa ikiwa na Cabon zinadhaniwa kuwa na madini ya dhahabu katika kiwanda hicho huku mashine hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 500 za Cabon ikiwa tayari imewekewa mzigo kwa ajili ya kuanza kazi.

Share:

Biteko Akamata Kiwanda Bubu Cha Uchenjuaji Dhahabu Shinyanga.

SALVATORY NTANDU
Licha ya serikali kuboresha sekta ya madini kwa wafanyabiashara wadogo wa madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga imebainika kuwa wapo ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchenjuaji wa madini ya dhahabu ikiwemo kuanzisha viwanda bubu na kuikosesha  serikali mapato.

Hayo yalibainishwa Januari Mosi mwaka 2020 Waziri wa Madini Dotto Biteko katika ziara yake ya siku mmoja ya kushitukiza katika kijiji cha Bunango katika Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya kubaini kiwanda bubu cha kuchenjua dhahabu kilichopo katikati ya makazi ya watu.

“Kiwanda hiki kipo hapa katika nyumba hii tangu mwezi julai mwaka 2019 huku kikiendelea kufanya kazi,serikali imepoteza mapato  mengi tutachukua hatua kali za kisheria kwa miliki wa mtambo huu na nyumba hii”alisema Biteko.

Sambamba na hilo  Biteko aliwaka viongozi wa vijiji na Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanawafichua wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara haramu ya madini ambazo zinafanyika katika makazi ya watu ambao hawana vibali wanaoikosesha serikali mapato.

“Niwaagize viongozi wa mkoa wa Shinyanga kuthibiti vitendo vya biashara haramu ya madini ambavyo vinaendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali kwani mpaka sasa tumeshakamata viwanda bubu viwili vya uchenjuaji wa dhahabu ili kutokomeza vitendo hivyi alisema Biteko.

Hata hivyo  Biteko aliagiza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Bunango Kajanja Kajanja na Mke wa mwenye nyumba iliyobainika kuwa na mtambo wa kuchenjulia dhahabu aliyefahamika kwa jina mmoja la Shule kuhusiana na kuhusishwa na tukioa hilo.

Masoud Bakari Balozi wa kitongoji cha mnara wa voda alisema alishatoa taarifa kwa mamlaka za kisheria  kuhusiana na uwepo wa kiwanda hicho katika eneo lake lakini hakuona hatua zozote zikichukuliwa kwa wahusika.

“Kiwanda hiki kipo katika nyumba hii tangu julai mwaka jana kuna vijana wageni wanne ambao walikuwa wakifanyashughuli ya kuchenjua dhahabu hapa viongozi wote wa eneo hili wanajua tumelalamika sana kuhusiana kumwagwa ovyo kwa maji yenye kemikali kwenye makazi yetu”alisema Bakari.

Katika ziara hiyo mifuko zaidi ya 35 imekamatwa ikiwa na Cabon zinadhaniwa kuwa na madini ya dhahabu katika kiwanda hicho huku mashine hiyo yenye uwezo wa kubeba kilo 500 za Cabon ikiwa tayari imewekewa mzigo kwaajili ya kuanza kazi.

Mwisho.


Share:

Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya Latoa Ufafanuzi Kuhusu Jeneza Kukutwa Sokoni Soweto.

Ni kwamba mnamo tarehe 21/12/2019 mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MASUOD MUSA MOHAMED [47] mfanyabiashara na mkazi wa makambako mkoani Njombe aliletwa kwa gari ya wagonjwa [Ambulance] katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu na mnamo tarehe 23/12/2019 majira ya 05: 00 alfajiri mtu huyo alifariki dunia na ndipo mmoja wa ndugu yake aitwaye HAMIS MUSSA HAMAD [61] mkazi wa Pambogo Iyela Jijini Mbeya aliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika msikiti wa MASJID TAUFIQ uliopo Block Q Soweto kwa ajili ya kuoshwa na kuswaliwa ambapo baada ya shughuli hizo kukamilika mwili wa marehemu ulihifadhiwa kwenye jeneza lililokuwa msikitini hapo na kisha kusafirishwa kuelekea Makambako kwa mazishi ambapo siku hiyo hiyo majira ya saa 18:00 jioni ulizikwa.

Baada ya kumaliza mazishi jeneza hilo lilibaki kwenye msikiti wa Makambako baada ya kukosa usafiri wa kulirudisha Mbeya kwa siku hiyo. 

Mnamo tarehe 31/12/2019 ALLY MOHAMED Mkazi wa Makambako alimkabidhi jeneza dereva wa lori ili aweze kulileta hapa Mbeya na kumpatia namba ya simu ya HAMIS MUSSA HAMAD ili alipokee jeneza hilo.

 Aidha lori hilo lilikuwa limebeba mzigo wa nyanya ambapo baadhi zilikuwa zinashushwa soko la Soweto na zingine zinapelekwa Songwe, hivyo majira ya saa 01:00 usiku wa kuamkia tarehe 01.01.2020 dereva huyo alifika Soweto na kushusha nyanya pamoja na jeneza lakini alipompigia HAMIS MUSA HAMAD mtu ambaye aliyeambiwa kuwa atalipokea jeneza hilo hakuweza kupatikana hewani hivyo ilimlazimu dereva huyo kukaa mpaka saa 04:00 usiku wa tarehe 01.01.2020 bila mafanikio na ndipo aliamua kumuachia mmoja wapo wa walinzi wa sokoni hapa ili ikifika saa 05:00 alfajiri kipindi cha swala aweze kuwakabidhi jeneza msikitini hapo.

Sambamba na hilo alimuachia namba ya simu ya mpokeaji kwa ajili ya mawasiliano na kisha dereva aliondoka kwenda Songwe lakini mlinzi huyo alilitelekeza jeneza hilo pale liliposhushwa na kuondoka zake hali iliyosababisha taharuki kwa wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, limefuatilia kwa karibu suala hili na nitumie nafasi hii kukanusha habari zilizokuwa zimeenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitando ya kijamii kwani uhalisia wa suala hilo ni huu, hivyo niwatake wafanyabiashara na wananchi wa mkoa wa Mbeya kuendelea na kazi/biashara zao kama kawaida.


Share:

ADAIWA KUKUTWA NA MIHURI 56 YA SERIKALI IKITUMIKA KUGHUSHIA NYARAKA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia ABRAHAM  OBEDI [55] wakala wa bima ya GTM na Mkazi wa Isanga Jijini Mbeya akiwa na mihuri hamsini na sita [56] ya idara mbalimbali za serikali na ofisi binafsi ambayo imeghushiwa na kuhifadhiwa katika ofisi yake ya Stationaries.

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 17:00 jioni huko maeneo ya Mtaa wa Sokoine uliopo Kata na Tarafa ya Sisimba Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kupata taarifa na kisha kufanya msako mkali na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa pamoja na vielelezo.

Baadhi ya mihuri na nyaraka alizokutwa nazo mtuhumiwa ni kama ifuatavyo:-

1.Mhuri wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko Kata ya Ruanda,

2.Mhuri wa Afisa biashara wa Halmashauri ya Mbeya,

3. Access Bank Tawi la Mbeya,

4.Mamlaka ya Mapato Mbeya [TRA]

5. Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbeya Mjini,

Aidha mtuhumiwa alikutwa pia na  Kompyuta moja aina ya Accer, Stika za bima, Poss Machine na nyaraka mbalimbali vikiwemo vyeti vya wanafunzi ambao vimeghushiwa. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia AGREY MASHAKA @ MBOTO [25] Mkazi wa Kilambo Wilayani Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi kavu kilogramu thelathini [30].

Mtuhumiwa alikamatwa Disemba 31, 2019 majira ya saa 14:45 mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanya msako mkali huko Kitongoji cha Kilambo, Kata ya Njisi, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bangi hiyo. 

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi January 2



















Share:

Wednesday 1 January 2020

Iran yamuita afisa wa Uswisi kujadili kile inachosema ni "uchokozi wa Marekani" kwa Iraq

Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema serikali yake imemuita afisa wa ubalozi wa uswisi ambayo inawakilisha matakwa ya Marekani nchini humo kulalamika juu ya uchokozi wa Marekani katika taifa jirani la Iraq. 


Kulingana na taarifa kutoka wizara hiyo, Jamhuri ya kiislamu ya Iran imelaani vikali matamshi ya kichochezi yanayoweza kusababisha vita yanayotolewa na maafisa wa Marekani ambayo ni ukiukwaji wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa. 

Rais wa Marekani na maafisa wengine wa taifa hilo wameilaumu Iran kwa shambulio la roketi lililisababisha kifo cha mkandarasi mmoja wa Marekani Kaskazini mwa Iraq Ijumaa iliyopita. 

Pia wameishutumu Iran kuhusika na uvamizi uliofanywa katika Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na waandamanaji waliojawa na hasira kufuatia shambulio la kulipiza kisasi la Marekani, Magharibi mwa Iraq lililowauwa wanamgambo 25. 

Wizara ya kigeni ya Iran hata hivyo imeitaka Uswisi iikumbushe Marekani kwamba Iran ni nchi huru.


Share:

Masauni apiga marufuku Mawakili Nje ya Ofisi za NIDA

Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni amepiga marufuku watu wanaojiita mawakili na kuwatoza wananchi kiasi cha  fedha kinachozidi shilingi Elfu Kumi  wakidai ni ada ya kupewa nyaraka mbadala ya cheti cha kuzaliwa ikiwa ni hitajio la msingi kwa wananchi wanaofika ofisi mbalimbali nchini za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)

Akizungumza baada ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Mkoa wa Morogoro walioitaka Serikali kuweka bayana kama kupata vitambulisho vya taifa lazima ulipe hela,Naibu Waziri Masauni alisema vitambulisho hutolewa bure hakuna haja ya kulipa gharama yoyote huku akipiga marufuku wananchi kutozwa fedha nje ya ofisi za NIDA

“Kuanzia sasa kila Ofisi ya NIDA itakuwa na mawakili wa serikali wataohusika na kuandaa pamoja kuhakiki nyaraka mbalimbali za wananchi wanaokuja kwa ajili ya vitambulisho vya taifa na ninatoa maelekezo kwa nchi nzima katika ofisi za NIDA kuwaondoa watu wanaowaandalia wananchi nyaraka hizo kwanza hatuwatambui kama ni maafisa sheria sahihi au la na wanaweza kuwathibitisha watu ambao sio raia wakapata vitambulisho kama raia” alisema Masauni

Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema wao kama mkoa wako tayari kuleta mawakili wa serikali katika ofisi hizo za NIDA huku akiwaasa wananchi kwenda sehemu sahihi wanapofika kutafuta vitambulisho katika ofisi hizo.

“Serikali ipo kuhakikisha zoezi la utolewaji namba na vitambulisho vya taifa linamalizika ndani ya siku 20 zilizoongezwa na Rais Magufuli na kama mkoa tunayafanyia kazi maelekezo ya Naibu Waziri Masauni na kuanzia kesho mawakili wa serikali watakuwepo hapa kuhakiki na kutengeneza nyaraka za serikali kwa wananchi” alisema RC Sanare

Nae Afisa Usajili wa  NIDA Mkoa wa Morogoro,James Malimo amesema katika Mkoa wa Morogoro na Wilaya zake jumla ya vitambulisho 347,466 kati ya 849,436 vimezalishwa huku maombi 237.236 yakikwama kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo waombaji kukosa vigezo vya uraia,mihuri ya wadau na viambata.


Share:

Monitoring, Learning and Evaluation (MLE) Manager at Project Concern International Musoma, TZ

Monitoring, Learning and Evaluation (MLE) Manager at Project Concern International Musoma, TZ PCI is a non-profit organization dedicated to preventing diseases, improving community health, and promoting sustainable development worldwide. With support from United States Department of Agriculture (USDA), PCI Tanzania will be implementing the final phase of Food for Education (FFE) programming in the Mara region (2017-2021). The… Read More »

The post Monitoring, Learning and Evaluation (MLE) Manager at Project Concern International Musoma, TZ appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TRA Yavunja Rekodi Nyingine Kwa Kukusanya Trilioni 1.987 Desemba 2019

Na Veronica Kazimoto-Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa mara nyingine, imevunja rekodi kwa kukusanya jumla ya kiasi cha sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019 ambayo ni rekodi ya kwanza kufikiwa tangu kuanzishwa kwake ikilinganishwa na rekodi ya mwezi Septemba, 2019 iliyokuwa sh. trilioni 1.767. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa, makusanyo hayo ya mwezi Desemba 2019 ni sawa na ufanisi wa asilimia 100.20 kutoka katika lengo la kukusanya kiasi cha sh. trilioni 1.983 kwa mwezi huo.

“Ni kweli kwamba, kitaalam, miezi tofauti hailinganishiki moja kwa moja. Hata hivyo, kwa makusanyo haya ya sh. trilioni 1.987 kwa mwezi Desemba 2019, TRA imevunja rekodi yake yenyewe iliyoiandika mwezi Septemba 2019 ambapo ilikusanya jumla ya sh. trilioni 1.767 ikiwa ni sawa na asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya sh. trilioni 1.817 katika kipindi hicho,” alisema Dkt. Mhede.

Akizungumzia makusanyo ya kipindi cha Robo ya Pili ya mwaka 2019/20 inayohusisha mwezi Oktoba, Novemba, na Desemba yenyewe, Kamishna Mkuu Mhede amesema kuwa, TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya sh. trilioni 4.972 sawa na ufanisi wa asilimia 97.49 ya lengo la kukusanya jumla ya sh. trilioni 5.100.

“Makusanyo haya ya robo ya pili ya mwaka 2019/20 ni sawa na ukuaji wa asilimia 19.78 ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha Robo ya Pili ya mwaka 2018/19 ambapo Mamlaka ilikusanya sh. trilioni 4.151 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 87.59 kutokana na lengo la kukusanya mapato kiasi cha sh. trilioni 4.739 katika kipindi hicho,” alifanunua Kamishna Mkuu Mhede.

Ameeleza kuwa, kwa upande wa makusanyo ya mapato ya Serikali kwa mwezi Oktoba 2019, TRA ilikusanya kiasi cha sh. trilioni 1.484 na Novemba 2019, Mamlaka ilikusanya sh. trilioni 1.501 sawa na ufanisi wa asilimia 93.98 na asilimia 97.59 kutoka katika malengo ya kukusanya sh. trilioni 1.579 na sh. trilioni 1.538 kwa mwezi Oktoba na Novemba 2019.

Kamishna Mkuu Mhede ameongeza kuwa, makusanyo hayo ni muendelezo wa kiashiria cha wazi kwamba Walipakodi na Watanzania walio wengi wameendelea kuelewa, kukubali, na kuitikia wito wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya maendeleo ya Taifa zima.

“Kwa kuwa Walipakodi wengi wameitikia wito wa kulipa kodi kwa mujibu wa Sheria, ni rai yangu kwamba asiwepo mlipakodi hata mmoja ambaye atathubutu kubaki nyuma. Ni busara wafanyabiashara wote wakaungana na kundi kubwa la Washindi, yaani, kundi kubwa la wanaolipa kodi kwa hiari, kwa ukamilifu, na kwa wakati, alisisitiza Dkt. Mhede.

Pia, amewashukuru walipakodi waliolipa kodi kwa wakati na hivyo kupelekea kuongezeka kwa makusanyo ambayo yatapelekea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

“Kwa namna ya kipekee, napenda kuwashukuru Walipakodi wote waliolipa kodi ya Serikali na kupelekea Mamlaka kufikia makusanyo haya ya kihistoria kwa mwezi Desemba 2019. Pia, tunaishukuru sana Serikali ikiwa ni pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Taasisi za Maendeleo, na Sekta Binafsi kwa kuendelea kuipatia TRA ushirikiano stahiki katika kutekeleza majukumu yake ya kukadiria, kukusanya, na kuhasibu mapato ya Serikali,” Alisema Kamishna Mkuu Mhede.

Aidha, ametoa wito kwa wamiliki wote wa majengo nchini kujitokeza kulipia kodi za majengo ili kuepuka usumbufu wa kulipa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo amesema kuwa, kwa sasa viwango ni rafiki na vinalipika kwa urahisi.

Amevitaja viwango hivyo kwa mwaka kuwa ni sh. 10,000 kwa nyumba ya kawaida, sh. 50,000 kwa kila sakafu ya nyumba ya ghorofa katika Majiji, Manispaa, na Halmashauri za Miji, na sh. 20,000 kwa jengo la ghorofa katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya.

MWISHO.


Share:

ASKARI POLISI AKATWA UUME NA MKEWE SHINYANGA

Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Askari polisi aitwaye Kazimir (28) mkazi wa Shinyanga Mjini amenusurika kifo baada ya sehemu zake za siri kukatwa na kitu chenye ncha kali akiwa amelala na mkewe Flora Adam (23) kutokana na kile kinadaiwa ni wivu wa mapenzi 'mme kuwa na mchepuko'. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Desemba 28,2019 majira ya saa 6 na nusu usiku wakati wamelala ambapo ghafla alikatwa na kitu chenye ncha kali katika uume wake. 

“Wakiwa wamelala mke wake Frola Adam aliamka na kunyatia na kuchukua kitu chenye ncha kali na kumkata mmewe sehemu zake za Siri na kumjeruhi vibaya na kumsababishia maumivu makali”,amesema Kamanda Magiligimba. 

“Baada ya tukio hilo Pc Kazimir alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa siku mbili na badaye aliruhusiwa”,ameeleza. 

Amesema chanzo tukio hilo kuwa ni wivu wa kimapenzi jambo linalosadikiwa kwamba mme wake alikuwa na nyumba ndogo.  

“Tunamshikilia Frola Adam (23) kwa tuhuma ya kumkata mume wake sehemu za siri na baada uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili”,amesema Kamanda Magiligimba.
Share:

Head; Business Banking at NMB Tanzania

Reporting Line: Chief, Retail Banking Job Purpose To builds an effective network of internal and external relationships, such as community and industry relationships, to actively acquire new clients and/or expand existing clients and enhance the client experience. Leverages reporting and sales tools to proactively identify and successfully convert sales opportunities To Manage risk/return and drives quality for new… Read More »

The post Head; Business Banking at NMB Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger