Thursday 1 August 2019
Wednesday 31 July 2019
Waziri Mkuu Majaliwa Akagua Maandalizi Ya Mapokezi Ya Wajumbe Wa Mkutano Wa Sadc Kwenye Kiwanja Cha Ndege Cha Julius Nyerere
Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31, 2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.
“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.
Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.
Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.
Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.
“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, JULAI 31, 2019.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Awataka Wadau Wa Mazingira Kutekeleza Sheria,kanuni,na Taratibu Za Mazingira.
MAKAMU wa Rais SAMIAH SULUHU HASSAN amewataka wadau wa mazingira kutekeleza Sheria,Kanuni na maandiko ili kuhimiza utunzaji wa rasilimali misitu na kurahisisha upatikanaji wa rasilimali za maji.
Akizindua jukwaa la maendeleo endelevu kuhusu usimamizi bora wa misitu kwa upatikanaji wa rasilimali maji endelevu leo jijini Dodoma Makamu wa Rais amesema misitu ndio chanzo kikubwa cha rasilimali maji hivyo isipotunzwa na kusimamiwa vizuri watakuwa wanahatarisha upatikanaji wa maji kwa matumizi ya kijamii,kibiashara na kuimarisha mazingira.
Ametaja mambo yanayosababisha athari kubwa kwa uhai wa rasiliamli maji kuwa ni kilimo kisichokuwa endelevu,ujenzi holela,uchomaji mkaa,ukataji kuni,uvunaji haramu wa magogo na ufugaji usiozingatia kanuni.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira GEORGE SIMBACHAWENE amesema haridhishwi na hali ya mazingira ilivyo na kuwataka wadau hao kupeleka fedha katika mazingira yanayoharibika badala ya kutumia kwenye makongamano.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dodoma dokta BINILITH MAHENGE amesema ni vyema jamii ikijikita katika kulinda na kutunza mazingira na kwa viongozi kutekeleza yale wanayoazimia.
Naye mkuu wa taasisi ya uongozi profesa JOSEPH SEMBOJA amesema sekta ya maji na misitu ni muhimu hivyo ni vyema sera, mikakati na taasisi zinazohusu sekta hiyo zikafungamana ili ziweze kufnaya kazi kwa ufanisi.
Jukwaa la maendeleo endelevu lilianzishwa mwaka 2012 ili kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji na misitu ili waweze kujadili mpango wa maendeleo endelevu.
KISANDU ACHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA MANISPAA YA SHINYANGA
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga John Kisandu
Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga
Diwani wa Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga John Kisandu (CCM) amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, na kumshinda mpinzani wake Zena Gulamu (Chadema).
Uchaguzi huo wa Naibu Meya umefanyika leo Julai 31,2019 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani wa kumchagua Naibu Meya pamoja na Kamati mbalimbali, ambazo zitasimamia utekelezaji wa maendeleo ya Manispaa hiyo, ikiwamo kamati ya fedha ya kudumu, uchumi, elimu na afya, miundombinu, ukimwi, maadili pamoja na Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT).
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, amesema John Kisandu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka mshindi kwa kupata kura 15, dhidi ya mpinzani wake Zena Gulam kutoka Chadema ambaye amepata kura tano ,ambapo wajumbe waliopiga kura walikuwa 20.
Akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, Kisandu ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani hao na kuwa kitu kimoja katika kuisimamia halmashauri kwa maslahi mapana ya wananchi na kuwaletea maendeleo.
Aidha madiwani hao wameendelea kujadili ajenda mbalimbali zikiwamo za afya, elimu, maji, miundombinu, fedha, kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa hiyo.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Diwani wa Kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM John Kisandu, akiomba kuchaguliwa kuwa Naibu Meya kwa mara nyingine tena, ambapo alishinda kiti hicho kwa kura 15.
Diwani wa viti wa maalumu Manispaa ya Shinyanga Zena Gulamu kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema(, akiomba kuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga, ambapo alipata kura tano.
Madiwani wakipiga kura kumchagua Nibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga.
Upigaji kura ukiendelea.
Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.
Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga.
Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.
Upigaji kura ukiendelea wa kumchagua Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga.
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akijipigia kura ya kuchaguliwa kuwa Naibu Meya kwa mara nyingine.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akimtangaza diwani wa Kata ya Chibe John Kisandu kuwa mshindi wa Kiti cha Unaibu Meya kwa mara nyingine.
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti hicho tena, na kuwataka madiwani kushirikiana kwa pamoja kusimamia maendeleo ya halmashauri.
Madiwani wakiendelea na baraza mara baada ya kumaliza kuchaguzi wa Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga na wajumbe wa kamati mbalimbali.
Madiwani wakiendelea na baraza.
Baraza la madiwani likiendelea.
Baraza la madiwani likiendelea.
Diwani wa Kata ya Kitangili Hamisi Ngunila (CHADEMA), akizungumza kwenye baraza hilo.
Diwani wa Kata ya Ndala Wiliamu Shayo(CHADEMA) akizungumza kwenye baraza.
Baraza likiendelea.
Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.
Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye baraza la madiwani.
Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu, akifunga mkutano wa mwaka wa baraza la madiwani na kuwataka watendaji na madiwani kila mtu awajibike kwenye nafasi yake ili kuleta maendeleo kwenye manispaa hiyo.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Call for Papers: UNESCO Regional Conference on Africa 2019 – Accra, Ghana (Funded)
Call for Papers: UNESCO Regional Conference on Africa 2019 – Accra, Ghana (Funded), Call for Abstracts – Assessing challenges and opportunities towards effective governance of diversity in Africa. UNESCO is opening a call for abstracts in preparation of a Regional Conference on the theme: Governance of Diversity: Challenges and Opportunities for Sustainable Development and Peaceful Coexistence in Africa,… Read More »
The post Call for Papers: UNESCO Regional Conference on Africa 2019 – Accra, Ghana (Funded) appeared first on Udahiliportal.com.
Wananchi 144 Jijini Dodoma Wakabidhiwa Hatimiliki Kwa Masharti Nafuu.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amekabidhi hati ya viwanja kwa wananchi 144 wa Kata ya Tambukareli ambao maeneo yao yalitwaliwa na Serikali.
Kunambi amekabidhi hati hizo leo Julai 31,2019 kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakihangaika takriban miaka mine hadi sasa.
Kunambi amefafanua kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma itahakikisha kila Mwananchi anapata haki yake kama ambavyo Rais Dk John Magufuli amekuwa akisisitiza kuwatetea wanyonge.
” Leo hii hapa kuna zoezi la kutoa viwanja kwa wananchi ambao ni wahanga wa maeneo yao ambao awali inadaiwa yalitwaliwa na iliyokua mamlaka ya ustawishaji Makao makuu na kuwaacha ndugu zetu hawa wakiwa hawana maeneo.
” Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi na sisi kama Jiji tulifanya tathimini ya jumla na kuona ndugu zetu hawa wana haki ya kulipwa fidia maeneo yao na hivyo leo tumemaliza kero yao ya muda mrefu kwa kuwagaia viwanja bure na watakacholipia wao ni zile tozo za kawaida za kikatiba,” amesema Kunambi.
Kunambi amesema katika mwaka 2018 wa Fedha tayari wameshatoa hati miliki 5000 na kuwa Jiji la kwanza Nchi nzima ikifuatiwa na Ilemela jijini Mwanza
.
” Ili tuweze kumaliza matatizo yote Dodoma basi Jiji linapaswa kutoa viwanja kwa mtindo huu wa leo kwa viwanja 5000 ambavyo vitatugharimu Shilingi Bilioni nne kwa hali ya kawaida sawa na kujenga vituo vya afya 8.
” Leo hii hawa wananchi ambao wako 144 tumewapa viwanja bure kwa maana watalipa tu zile gharama za kisheria takribani laki saba kwa kiwanja ambacho angeweza kulipa Shilingi Milioni saba. Hii ni kuonesha jinsi gani Serikali ya Dk Magufuli inatetea haswa wanyonge,” amesema Kunambi.
Hata hivyo Kunambi amesema badala ya Mwananchi kutoa gharama ya Tsh. milioni saba anapunguziwa na kutoa Laki saba pekee kwa kiwanja na utoaji wa fedha hizo ni kwa masharti nafuu kutoa kwa awamu ndani ya miezi 6.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Juma Mazengo akizungumza kwa niaba ya madiwani jiji la Dodoma amemshukuru Mkurugenzi wa Jiji kwa namna alivyolivalia njuga suala lao na kuweza kumaliza kero ya wananchi wake ambao wameteseka kwa miaka minne.
” Nimshukuru Mhe Rais kweli tumeona jinsi gani anatetea wanyonge. Hii inaonesha jinsi gani anaziishi ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni, tunayo furaha sana na hakika tumeona heshima tuliyopewa na Serikali yetu,”amesema Mhe. Mazengo.
Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo
Makusanyo Ya Kodi Kwa Kipindi Cha Mwaka Wa Fedha 2018/19
Ikumbukwe kwamba, katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ambao utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili (2). Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo. Awamu hii ya kwanza iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 Januari 2019 imeendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, na CD/DVDs yamekamilika. Hivo mfumo huu wa ETS kwa awamu hii ya pili, unatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 1 Agosti, 2019.
Lengo kuu la kubandika stempu hizi za kielektroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa Ushuru wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya mapato stahiki.
Ni matumaini ya TRA kuwa, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja, na umma kwa ujumla wataendelea
kutoa ushirikiano kwa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Richard M. Kayombo
KAIMU MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
MKUU WA MKOA WA MARA AZINDUA KAMPENI YA 'NYUMBA NI CHOO'
Makerere University Mak Graduate Admission Lists for 2019/20 Academic Year
makerere graduate admission list 2019 admission list makerere university postgraduate admission list makerere university graduation list 2019 makerere university masters admission 2019 makerere university graduate admission 2019/20 makerere university admission list 2019/20 makerere university graduation list 2019 pdf
The Directorate of Research and Graduate Training (DRGT), Makerere University has released the admission lists for postgraduate applicants successfully admitted for the 2019/20 Academic Year. The lists include those of candidates admitted to eight colleges of Makerere University. Additional lists will follow.
Please see the Downloads below for admitted students listed by College.
For further enquiries please contact
The Directorate of Research and Graduate Training (DRGT),
Level 4 Senate Building
Makerere University
P.O. Box 7062 Kampala
Telephone: +256 (414) 691-937
Email: drgt[at]rgt.mak.ac.ug
DOWNLOADS & ESSENTIAL ATTACHMENTS
Attachment | Size |
---|---|
PDF icon | 767.99 KB |
PDF icon | 458.19 KB |
PDF icon | 569.6 KB |
PDF icon | 702.9 KB |
PDF icon | 832.5 KB |
PDF icon | 404.66 KB |
PDF icon | 298.74 KB |
PDF icon |
The post Makerere University Mak Graduate Admission Lists for 2019/20 Academic Year appeared first on Udahiliportal.com.