Saturday 30 March 2019

Kikwete aitaka Taasisi ya Sayansi za Bahari wilayani Pangani kuwekeza kwenye utafiti

Rais Mstaafu na Mkuu wa Chuo kikuu cha DSM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema ili nchi iweze kuendelea na kuwa na uchumi mzuri ni lazima iwe na watafiti wenye uwezo wa kugundua vitu mbalimbali vitakavyo iwezesha Serikali kutatua changamoto za wananchi bila kutegemea nchi nyingine

Dk Kikwete  amesema hayo Machi 29 alipofanya ziara ya kutembelea kituo  cha Utafiti na mafunzo ya ufugaji wa samaki kilichopo Pangani mkoani Tanga kilicho chini  ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)

“Uwekezaji katika utafiti ndio kichocheo kikubwa ambacho
kinaweza kuwapa mafanikio makubwa muweke msukumo kwenye suala hilo kwani ndilo litakalowapa mafanikio makubwa.

“Nimefurahi sana kwamba taasisi hii ipo kwa ajili ya bahari eneo la viumbe vya majini hakuna taasisi nyingine kubwa kushinda nyie mkibaki kuangalia viumbe vya baharini majini na kusahau na vilivyopo maji baridi kutakuwa na ombwe lakini nafurahi hapa mmeanza kufanya utafiti
wa viumbe wa maji baridi,” Amesema.

Dkt Kikwete amesema taasisi hiyo imeanzishwa kwa ajili ya taaluma kubwa ya viumbe vya bahari huku akiwataka watumie taaluma hiyo kuingiza kwenye viumbe wa maji baridi.

Awali akizungumza wakati akisoma risala Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Bahari Dkt Magreth Kyewalyanga amesema malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kutoa mafunzo ya uvunaji endelevu na uzalishaji wa mazao ya samaki bahari.

Amesema katika tafiti za uzalishaji wa mazao ya bahari taasisi hiyo ilianza na kilimo cha mwani na uzalishaji katika miaka ya 80 ikifuatiwa na tafiti za ufugaji wa smaki aina ya mwatiko ikiwemo uzalishaji wa lulu kwenye miaka ya 2000 na hatimaye utafiti wa perege kuanzia mwaka 2009.

Aidha amesema mazao mengine yanayofanyiwa utafiti na majaribio ni pamoja na majongoo bahari ,kaa koko, chaza, Spirulina nk, ambapo tafiti hizo ndio zimechangia sana katika kuwapa ukuaji wa uzalishaji wa viumbe mbalimbali baharini hapa nchini

Naye Mkuu wa wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah
Amesema uwepo wa chuo hicho ni faraja kubwa sana kwao na kitakuwa kichocheo cha maendeleo kwa wakazi wa wilaya hiyo


Share:

Je wewe ni Mmiliki wa Gari? Ni Fundi Magari au Muuza Spea? ...Hapa Tunahabari Njema Inayokuhusu

Habari njema kwa wamiliki wa Magari, mafundi na Wauza Spea za Magari. EDRIVE PRO wamekeletea mfumo ambao unawaunganisha pamoja na pindi gari lako likiharibika popote ulipo hutapata tena tabu ya kuhangaika kutafuta fundi au maduka ya spea.

www.edrivepro.co.tz ni mfumo wa kufanya na kusimamia utengenezaji wa magari online.

1. Katika mfumo huu wamiliki wa magari, maduka ya spare, na mafundi wanajisajiri ama wanaweza kusajiliwa kwa kuwasiliana na mtoa huduma wetu kwa e-mail edriveprotz@gmail.com

2. Baada ya kujisali kulingana nafasi yako [ mmiliki wa gari, muuza spare, fundi ama mwandika makala juu ya magari] msimamizi wa mfumo atakuthibitisha katika mfumo na utatumiwa e-mail na mfumo.

Baada ya kudhibitishwa utaweza kupata huduma za uuzaji wa spare, matengenezo ya magari kwa wamiliki wa magari na mafundi kupata fursa za mateja wapya mtandaoni nchi nzima.

3. Kutokana na wahusika wote katika mfumo huu kuwa wamesajiliwa, huduma katika mfumo huu ni nafuu na za uhakika.

Karibuni mjisajili katika www.edrivepro.co.tz


Share:

Rais Magufuli na Amiri Jeshi Mkuu atunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya 146 wa JWTZ Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Dkt John Magufuli, leo Machi 30, 2019, amewatunuku Kamisheni Maofisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Rais Magufuli amewatunuku Kamisheni katika cheo cha Luteni USU maafisa hao wanafunzi ambao idadi yao ilikua 146.

Hafla ya utunukiwaji kamisheni kwa Maafisa hao imefanyika katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.



Share:

Kituo cha kuzalisha na kusambaza umeme cha Mlandizi Chateketea kwa Moto

Kituo cha kuzalisha na kusambaza umeme cha Mlandizi mkoani Pwani kimeungua moto kufuatia mlipuko uliotokea kwenye transfoma.

Taarifa iliyotolewa na TANESCO inasema chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika na uchunguzi unaendelea.  


Share:

MWANAMKE 'ALIYEFARIKI' MWEZI DISEMBA AJIFUNGUA MTOTO

Mtoto akiwa kwenye mashine ya kumpatia joto

Mwanamke mmoja mwenye miaka 26 amejifungua mtoto wa kiume siku ya Alhamisi licha ya kutangazwa kuwa ni mfu toka Disemba.

Mwanamichezo wa kimataifa, bi Catarina Sequeira alipatwa na shambulio kali la pumu akiwa nyumbani kwake.

Bi Sequeira amezikwa Ijumaa, siku moja baada ya mtoto kutolewa tumboni mwake.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Salvador, amezaliwa baada ya kukua kwa wiki 32 tumboni mwa mama yake kwa wiki 32, na sasa yupo chini ya uangalizi kwenye hospitali ya watoto.

Hii ni mara ya pili nchini Ureno kwa mtoto kuzaliwa kutoka kwa mama ambaye ni 'mfu wa ubongo'.

Sequeira ambaye alikuwa mwanariadha wa mbio za mitumbwi amekuwa akisumbuliwa na pumu toka utoto wake.

Aliwahi kuiwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa wakati wa uhai wake.

Shambulio lililochukua uhai wake lilimpata akiwa na mimba ya wiki 19, hali iliyomfanya kupoteza fahamu. Siku chache akiwa chumba cha wagonjwa mahututi hali ilizidi kuwa mbaya na akatangazwa kuwa 'mfu wa ubongo' Disemba 26. Madaktari wakamuwekea mashine ya kusaidia kupumua ili mtoto tumboni aweze kuishi. Mashine hiyo iliwekwa kwa siku 56.
Sheria ya kutoa viungo yaamua 'kesi' hii

Madaktari wanasema malengo yalikuwa ni kusubiri mpaka Ijumaa ambapo ujauzito huo ungefikisha wiki 32, lakini mfumo wa hewa wa mama huyo uliharibika ghafla na kulazimisha upasuaji ufanyike Alhamisi ili mtoto atolewe.

Wiki 32 ndiyo kipindi ambacho madaktari wanansema mtoto anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuishi.
Mkuu wa kitengo cha maadili cha hospitali hiyo, Filipe Almeida, ameelezea kuwa maamuzi ya kumuacha mtoto aendelee kukuwa kwenye tumbo la mama yake yalifikiwa kwa pamoja na familia ya mama huyo, kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kipinga kwa maandishi sheria ya kutoa viungo vyake baaa ya kufariki.

"Kuwa mtoaji wa viungo si tu kuwa na nafasi ya kutoa ini au mapafu, lakini pia inahusu kuwa na uwezo wa kujitoa ili mtoto wako aishi," Almeida ameuambia mtandao wa Observador.

Baba wa mtoto huyo alitaka azaliwe, kama ilivyokuwa kwa familia nzima ya marehemu.

Hata hivyo mama wa Sequeira, bi Maria de Fátima Branco, ameiambia televisheni moja ya Ureno kuwa alimuaga binti yake Disemba 26, na uamuzi wa kumuacha mtoto huyo azaliwe umefikiwa baada ya baba yake, Bruno, amekuwa akitaka kuwa baba kwa muda sasa.

Mtoto huyo amezaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.7kg na anatazamiwa kubaki hospitali kwa walau wiki tatu zijazo.

Mwaka 2016, mtoto mwengine ajulikanaye kama, Lourenço, alizaliwa jijini Lisbon baada ya kukaa kwa wiki 15 baada ya mama yake kufariki.
Chanzo - BBC
Share:

JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA WAGANGA WA JADI 19 WAKIWA NA NYARA ZA SERIKALI




Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limedai kuwakamata waganga wa Jadi 19 ambao wamekuwa wakipiga ramli chonganishi na kusababisha kuendelea kuwepo kwa matukio ya mauaji ya wananchi ambayo yamekuwa yakitokana na imani potofu za kishirikina.


Hayo yamebainishwa leo Machi 30,2019 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema katika misako mbalimbali ambayo inaendelea kufanyika na jeshi hilo ili kukabiliana na uhalifu pamoja na kupunguza mauaji yatokanayo na imani potofu za kishirikina, wamefanikiwa kuwakamata waganga hao 19 pamoja na watuhumiwa wengine 16 wakiwa na vitu vya wizi na madawa ya kulevya.

“Waganga hawa wa jadi tumewakamata pia wakiwa na nyara za serikali ambazo hutumia kupigia ramli chonganishi ambayo ni mikia ya nyumbu, ngozi ya kenge, ngozi ya simba, kucha za simba, mayai ya mbuni, kichwa cha kenge, jino la ggiri, pamoja na bundi mmoja ambaye tukimtoa hapa atakimbia,”amesema Kamanda Abwao.

“Pia katika msako mwingine tumefanikiwa kukamata watuhumiwa saba (7) wakiwa na mali za wizi ambazo ni pikipiki 2, mashine 3 za kunyolea saluni za kike, Tv 5, Radio Sabwoofer  5, Deki 5, King’amuzi kimoja, komputa moja, Friji moja, baiskeli 3, pamoja na watuhumiwa wengine tisa (9) wanawake wakiwa na madawa ya kulevya aina ya bangi uzito wa kilogramu 35 na heroine gramu 195,”ameongeza.

Aidha Kamanda amesema watuhumiwa wote hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi za Kisheria, ili liwe fundisho kwa watu wengine ambao hawataki kuzitii sheria za nchi.

Pia ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga, kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa dhidi ya waharifu, wakiwamo na wanganga wa jadi ambao wamekuwa wakitoa tiba kwa kupiga Ramli Chonganishi, ili mkoa ubaki kuwa salama kwa kudumisha amani na utulivu.

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (ACP) Richard Abwao akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa juu ya misako ambayo wanaendelea kuifanya ya kukamata wahalifu, wauza madawa ya kulevya pamoja na waganga wa Jadi ambao wamekuwa wakitoa tiba kwa kupiga ramli chonganishi na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia kutokana na imani za kishirikina.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (ACP),Richard Abwao akionyesha nyara za serikali ambazo zimekuwa zikitumiwa na Waganga wa Jadi kinyume na Sheria na kutoa tiba kwa kupiga ramli chonganishi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao akionyesha dhana ambayo hutumiwa na waganga wa Jadi kutibia wateja wao na kupiga ramli Chonganishi inayo sababisha mauaji ya kishirikina kwa watu wasio na hatia wakiwamo wazee.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao, akionyesha madawa ya kulevya aina ya Bangi Kilogramu 35 ambayo wameyakamata kutoka kwa wanawake 9 waliokuwa wakifanya biashara hiyo zikiwamo na Heroine Gramu 195.

Nyara za serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia ramli chonganishi.

Nyara za serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia ramli chonganishi.

Afisa wa jeshi la polisi akionesha nyara za Serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia Ramli Chonganishi.

Nyara za Serikali pamoja na dhana ambazo hutumiwa na Waganga wa Jadi kupigia ramli chonganishi.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakichukua matukio ya wahalifu waliokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo wakiwamo na Waganga wa Jadi ambao hutoa tiba kwa kupiga ramli chonganishi inayosababisha mauaji ya kishirikina kwa watu wasio kuwa na hatia.

Waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakiendelea na uchukuaji wa matukio.

Vitu vingine vya wizi vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi.

TV pamoja na Pikipiki ya wizi ambayo imekamatwa na Jeshi la Polisi SANLG yenye namba za usajili MC 187 BEM.

Vitu vingine kama unavyoona vikiwa vimekamatwa katika msako huo wa Jeshi la Polisi ndani ya siku nne kwa mkoa mzima ambapo zoezi hilo ni endelevu ili kuhakikisha mkoa unabaki kuwa salama.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga (ACP) Richard Abwao, akitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo, kuacha Tabia ya kupenda kwenda kutibiwa kwa Waganga wa Jadi, bali waende kwenye huduma za kiafya kupatiwa matibabu sahihi na siyo kwenda kupigiwa Ramli Chonganishi.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Share:

Live | Magufuli Akiwatunuku Kamisheni Maofisa Wapya JWTZ

Live | Magufuli Akiwatunuku Kamisheni Maofisa Wapya JWTZ


Share:

Mbowe Kuongoza Kamati Kuu ya CHADEMA Leo

Kamati Kuu ya chama kikuu  cha upinzani nchini (Chadema) leo inakutana ili kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa hali ya siasa nchini.
 
Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza kuwa, kikao hicho ni cha siku moja na kilichofanywa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema toleo la mwaka 2016.

Kikao hicho kitaongozwa na Mbowe, ikiwa ni baada ya kukosa vikao kadhaa kutokana na kuwekwa rumande katika Gereza la Segerea tangu Novemba mwaka jana mpaka alipopata dhamana tarehe 7 Machi 2019.

Kazi zinazotarajiwa kufanywa na kamati hiyo ni pamoja na kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa kisiasa nchini, na kisha kuchukua mwelekeo baada ya mjadala wa taarifa hiyo.




Share:

JINSI KAZI ZINAVYOUA NA WATU NA HAWAJALI

Jeffrey Pfeffer anaposema kuwa ''kazi zinawaua watu na hakuna anayejali,'' hasemi kwa njia ya mafumbo.

Anasema kwa hakika kabisa kutokana na utafiti alioufanya kwa miongo kadhaa, nchini Marekani na duniani kwa ujumla.

Profesa Pfeffer kutoka shule ya biashara ya Chuo cha Stanford na mwandishi na mwandishi msaidizi wa vitabu 15 kuhusu muundo wa kampuni na masuala ya uongozaji rasilimali watu, ametoa hoja katika kitabu chake cha hivi karibuni kiitwacho , ''Kufa kwa ajili ya Mshahara'' Jinsi mifumo ya kazi inavyoathiri na hata kusababisha kukatisha maisha ya watu.

Katika kitabu hicho anazungumzia tuko la Kenji Hamada, mwenye miaka 42 aliyekufa kwa mshtuko wa moyo akiwa kwenye dawati lake kazini jijini Tokyo.Nilifanya kazi saa 72 kwa wiki na ilikua inanichukua saa mbili kufika kazini.

Kabla ya kifo chake, alifanya kazi siku 40 mfululizo bila kupumzika na mjane wake anasema Kenji alikuwa na msongo mkubwa

Huu ni moja kati ya mifano iliyokuwa kwenye chapisho lake, ambapo mwandishi anaeleza madhara ya mfumo wa kazi ambao wakati mwingine ''si ya kibinaadamu'' kutokana na majukumu makubwa ya kazi.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowekwa na Pfeffer,nchini Marekani, asilimia 61 ya wafanyakazi wanaona kuwa msongo umewafanya waumwe na asilimia 7 wanasema walilazwa kutokana na sababu zinazohusiana na kazi.

Makadirio yake ni kwamba msongo una uhusiano na vifo vya wafanyakazi 120,000 wa Marekani.Wafanyakazi hupoteza maisha kutokana na majukumu mengi ya kazi

Kwa mtazamo wa kiuchumi, msongo umewagharimu waajiri zaidi ya dola za Marekani 300,000 kwa mwaka nchini Marekani.

Katika kitabu chako umeeleza kuwa kuna mfumo wa ufanyaji kazi unaowaua watu.Ni ushahidi gani ulionao kuhusu hili na ni kwa jinsi gani mfumo wa kisasa wa ufanyaji kazi unawaathiri waajiriwa?

Kuna ushahidi wa madhara ya kiafya.Saa nyingi za kufanya kazi,kupunguzwa kazi, kukosa bima ya afya, masuala ya kiuchumi, migogoro kwenye familia na maradhi.

Kazi sasa imekua si ya kibinaadamu.Kwa upande mwingine, makampuni yameacha kuwajibika kwa ajili ya wafanyakazi wao.

Lakini changamoto za kiuchumi zimeongezeka, hofu ya kukosa ajira pia inaongezeka.

Katika Benki za uwekezaji, kwa mfano, kuna namna ya ufanyaji kazi, unakwenda nyumbani kwako kuoga na kurejea ofisini.

Katika mfumo huo, waajiriwa wengi huingia katika uraibu wa madawa, kwa sababu wanaishia kutumia Cocaine na madawa mengine ili wawe macho.

Mfanyakazi wa kiwanda, rubani wa ndege, mwendesha lori, wana idadi ya saa za kufanya kazi.

Lakini kuna kazi nyingine hakuna saa maalumu za kazi.

Nchini Marekani, sababu ya tano ya vifo ni sehemu ya kazi.

Lakini nani anawajibika kwa vifo hivi?

Waajiri na serikali zinawajibika kwa kutochukua hatua yoyote kuhusu suala hili.

Ni kazi kubwa tunapaswa kufanya kitu kwa ajili ya kukomesha hili.Lakini hatutaweza kufanya chochote kama mtu mmojammoja.

Kama unataka kutatua tatizo yapaswa kuwa katika utaratibu ambao utatoka kwa mtindo wa sheria.

Mazingira mabaya ya kazi husababisha maradhi kama vile sukari na shinikizo la damu.

Lakini tukizungumzia gharama,makampuni yanaweza kuleta hoja kuwa kufanya mabadiliko katika mfumo wa kazi kutaathiri kipato cha kampuni.

Hii si kweli, anasema Profesa Pfeffer.''Tunajua kuwa watu walio katika msongo wa mawazo wako katika nafasi kubwa ya kuacha kazi''.Tunajua kuwa wafanyakazi wasio sawa kisaikolojia hawawezi kuizalishia kampuni inavyopaswa''.

Alitolea mfano kuwa inafahamika kuwa Marekani na Uingereza zaidi ya 50% ya siku za kazi hupotea kwa sababu ya wafanyakazi kutokuwepo kutokana na msongo wa kazi.

Hivyo kuna athari kubwa kwa mfanyakazi mgonjwa anayekwenda kazini na asifanye kazi kama anavyotakiwa.Hali hii huigharimu kampuni.Wafanyakazi wanapaswa kuzijali afya zao

Wafanyakazi wanapaswa kujijali

Kwa upande wa wafanyakazi, Profesa ameandika kuwa watu wajijali.Lakini ameulizwa swali kuwa itakuwaje ikiwa muajiriwa akadai kuboreshewa mazingira ya kazi na kuna uwezekano akaishia kufukuzwa?

Je mazingira ya kazi yatabadilishwaje?

Profesa anasema, kwanza waajiriwa wanapaswa kujali afya zao.

Ikiwa unakwenda kazini, mahali ambapo huwezi kuoanisha maisha ya kazi yako na familia, unapaswa kuacha kazi hiyo.

Jambo jingine ni kwamba watu wanapaswa kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa.
Chanzo - BBC
Share:

RADI YABOMOA NYUMBA NA KUUA MTU RUKWA

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 30




Share:

Friday 29 March 2019

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatoa tahadhari ya mvua nchini

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari ikiwemo mafuriko.

 Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha leo Ijumaa Machi 29 hadi Aprili 2, 2019 na kwamba zinaweza kuleta athari kwenye makazi ya watu.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

Pia zinaweza kuleta shida katika usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Mamlaka hiyo imesema kuanzia leo hadi Machi 31, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na Morogoro.

Imeeleza kuwa Aprili Mosi hadi Aprili 2, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

TMA imeshauri Menejimenti ya Maafa na watoa huduma za dharura pamoja na wadau wengine kuchukua hatua za kuweka mipango stahiki kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger