TAARIFA KWA UMMA

YAH:
KUTOSHIRIKI AWAMU YA PILI YA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

Tafadhali husika na somo hapo juu.


Mtakumbuka kuwa Chama chetu kwa kushirikiana na vyama vingine vinavyoounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) tuliamua kutoka katika Bunge maalum la Katiba baada ya CCM kuamua kukiuka utaratibu wa mchakato wa kupata katiba mpya kama ulivyoainishwa katika sheria ya mabadiliko ya Katiba na kuweka Mkakati wa kupitisha Rasimu ya CCM ya serikali mbili.


Pamoja na juhudi ambazo tumeendelea kuzifanya kama Chama na UKAWA, hadi sasa bado CCM wanaonekana hawana dhamira ya dhati ya kuurejesha mjadala wa Katiba Mpya kwa kuheshimu maoni ya wananchi kama yalivyoratibiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuwekwa katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa katika Bunge Maalum.