Friday 25 April 2014

KADINDA ‘AMMISS’ JACK PATRICK


MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda ameonesha hisia zake hadharani baada ya kutupia picha ya rafiki yake kipenzi, modo Jack Patrick mtandaoni na kuonesha kuwa amemkumbuka.
Modo Jack Patrick.
Jack alikamatwa nchini China akidaiwa alikuwa amebeba madawa ya kulevya ambapo kabla hajaondoka, walikuwa wakishirikiana kikazi na mwanamitindo huyo ambaye amemwambia mwandishi wetu kuwa waliishi kama ndugu.
Mwanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda.
“Jack Patrick alikuwa zaidi ya rafiki, tuliishi vizuri, tumekula good time pamoja na mambo mengine mengi, sitaki kuongelea ishu yake iliyompata lakini kimsingi namkumbuka sana,” alisema Kadinda.
Share:

ANGALIA PICHA ZA MAUAJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA SUDAN YA KUSINI,TUITUNZE AMANI YETU.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI


http://www.ufukunyuku.blogspot.com/ 
Umoja wa Mataifa unasema kuwa vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan Kusini viliwaua mamia ya watu kwa sababu ya kabila lao wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, watu hao walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa wanahifadhiwa kama vile msikitini, makanisani na hospitalini.Umoja huo umesema kuwa watangazji katika baadhi ya vituo vya redio walitumia lugha ya chuki na uchochezi na kuwataka watu wa kabila fulani kuondoka mjini humo huku wakiwashauri wanaume kuwabaka wanawake.




Share:

Thursday 24 April 2014

PICHA:VIKOSI VYA ULINZI NA USALAM VIKIENDELEA NA MAZOEZI KWA AJILI YA SIKU YA MUUNGANO

Share:

TAZAMA KIONJO CHA WIMBO MPYA WA OMMY DIMPOZ NCHINI MAREKANI



Ommy Dimpoz a.k.a Poz kwa poz ameamua kuwaonjesha kionjo cha wimbo wake mpya unaokuja ambao video yake imefanywa nchini Marekani Na producer mkali nchini humo.
Kupiti Account yake ya Instagram Ommy dimpoz aliweka kionjo cha Video hii na kusema ndio cha wimbo huo unaosubiriwa na Wapenzi wa Muziki wa Bongo fleva Kwa Hamu Kubwa.

Watch Here

Share:

BATULI: MUDA WAKUVAA NUSU UCHI SASA...

Msanii wa Bongo Movies Ametoa ushauri kwa waigizaji wenzake wa kike kuwa Muda wa kuvaa nusu uchi na kupiga picha kuzitupia kwenye mitandao ili kupata umaarufu umekwisha, siku hizi ukivaa nusu uchi unaonekana Malaya tu...Amewaasa kuwa wafanye kazi na kutoa kazi zinazouzika sokoni ...Amewaambia kuwa wajifunze kutoka kwake kwani huwa anavaa vizuri uwezi kukuta picha zake za uchi uchi mitandaoni
Share:

MAFURIKO WILAYA YA KYELA JIJINI MBEYA NI HATARI TUPU!!

 
See more pics...

Mbunge wa Kyela Dr. Mwakyembe akikagua Barabara iendayo Bandari ya Kiwira
 Baadhi ya watu wakigangaika kupita juu ya maji hayo yaliyotokana na Mafuriko

 Baadhi ya watu mbalimbali wakiwa wanashuhudia Mafuriko
 Gari Likiwa limekwama katika tope lililotokana na Mafuriko hayo, hili ni eneo la Bujonde 
Share:

DIAMOND AHAHA KUTAFUTA COLLABO NA BEYONCE



Hii Habari nimeisoma katika Gazeti moja Jana kuwa Diamond anahangaika kuwasiliana na Beyonce ili wafanye Wimbo Pamoja , Inasemekana Diamond alitafuta Number ya Beyonce kwa bahati nzuri akaipata na kumpigia simu na kumweleza anachotaka ila Beyonce akamkatiza na Kumuuliza huna Manager ? na Kisha kukata simu ..kwani Maswala ya Kazi Kwake lazima yapitie kwa Manager akiwa na Maana kuwa Manager wa Diamond Awasiliane na Manager wa Beyonce ndio Waanzia hapo kama kikieleweka poa , Mhh Goodluck Brother kama ni kweli na Ufuate Protocol
Share:

Wednesday 23 April 2014

VIDEO:TAZAMA HII(KUHUSU NDOA)


Share:

The Frenchman turned home Fabio Coentrao's cross in the first half to seal a win against Pep Guardiola's side, who dominated possession but failed to find a breakthrough

Real Madrid 1-0 Bayern: Benzema gives Ancelotti's men slender first-leg advantage

KARIM BENZEMA REAL MADRID BAYERN MUNICH CHAMPIONS LEAGUE 04232014
Getty Images
A solitary strike from Karim Benzema was enough to give Real Madrid a 1-0 win over Bayern Munich in the first leg of the Champions League semi-final.

The France international poked home Fabio Coentrao's cross in the first half for the only goal of the game to inflict only a second defeat in the competition for Pep Guardiola's side.

Bayern bossed possession but failed to create many meaningful chances, and Madrid could have won more comfortably had Cristiano Ronaldo and Angel Di Maria kept their composure with clear openings in the first 45 minutes.

Share:

MBEYA CITY YAAGIZA NDEGE YA CHINI...


MBEYA City imemaliza Ligi Kuu Bara kwa kushika nafasi ya tatu na sasa imeanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao kwa maana na usajili pamoja na kutengeneza miundombinu yake, likiwamo suala la usafiri kwa kununu basi la kisasa litakalokuwa ‘ndege ya chini’.
Mikakati mingine ya miundombinu hiyo ni kujenga uwanja wao. Kwa suala la uwanja, inatarajia kuanzisha kazi ya kuujenga katika eneo la Iwambi mjini Mbeya. Eneo lao limeelezewa kuwa na ukubwa ekari 15.
Ukija kwenye suala la usafiri ambalo linatarajia kukamilika muda si mrefu kutoka sasa, klabu hiyo inatarajia kununua basi jipya la kisasa lenye huduma zote ndani. Basi hilo litakuwa ama Yutong au Higer.
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe, ameliambia Mwanaspoti kuwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo ndiyo mmiliki wa timu hiyo, imeshatangaza tenda kwa kampuni mbalimbali zinazouza magari baada ya kuweka wazi sifa za basi wanalolihitaji.
“Tulitangaza mara ya kwanza, hakukuwa na kampuni iliyojitokeza, tukarudia ndipo kampuni tatu zimejitokeza na hivyo itapendekezwa kampuni moja kulingana na makubaliano yatakayofanyika,” alisema Kimbe.

“Tupo katika hatua za mwisho za ununuzi wa basi la timu, tutahitaji moja lenye hadhi tunayoitaka, fedha zipo.”

Source.. Mwanaspoti
Share:

MAIGE "KUWA NA SEREKALI TATU TANZANIA ITAINGIA KATIKA MAAJABU YA DUNIA"

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Almas Maige amesema endapo wajumbe wa Bunge hilo watapitisha muundo wa Serikali tatu, nchi itaingia katika kitabu cha maajabu ya dunia cha Guiness Book of Records.

“Hili litakuwa shirikisho la pekee hapa duniani lenye marais wengi katika nchi mbili, linaweza kuingia katika kitabu cha maajabu cha Guiness kwa kuwa na marais wengi katika nchi maskini sana,” alisema.


Mjumbe huyo alisema amejaribu kufuatilia hoja za wanaounga mkono muundo huo na kufananisha na nchi za Marekani na Nigeria, lakini akasema katika nchi hizo Rais wa nchi ni mmoja.

“Mimi nimejaribu kuwafuata wanaofananisha na Marekani na Nigeria, wameshindwa kusema katika nchi hizo mbili Rais ni mmoja tu hakuna wingi wa Rais kutokana na majimbo,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, mjumbe huyo aliwashangaa wajumbe wanaotokana na kundi la Ukawa kujigeuza kuwa wachunguzi wa kijinai kwa kuhoji uhalali wa saini ya muasisi wa Muungano, Abeid Aman Karume.

“Mimi nawashangaa sana wanasiasa hawa na wanasheria wa Ukawa wamejigeuza Forensic Expert (wachunguzi wa jinai). Mimi ningewaunga mkono kama wangeenda kuwauliza watoto wa marehemu,” alisema.

Aliongeza kusema: “Watoto wa marehemu wapo Zanzibar… Yupo Aman Karume aliyekuwa Rais wa Zanzibar na yuko Balozi Ali Karume na yuko pia mama Karume. Kwa nini hawawaulizi,” alihoji.

“Mimi ningefurahi sana kama wangeenda kuwauliza wanafamilia sahihi hii ni ya baba yenu? Au je, mheshimiwa mama hii ni sahihi ya mumeo? Wangekataa ndipo tungewaunga mkono,” alisisitiza.

Mjumbe huyo alisema kinyume chake, Ukawa wanavaa gamba la elimu ambayo hawana na vilevile hawajui maana na tafsiri sahihi iliyoandikwa miaka 50 iliyopita.

“Taaluma ya sasa ingeweza kugundua wino uliotumika una umri gani na kuondoa kero hiyo kama ni ya juzi au jana au kama imeghushiwa,” alisema mjumbe huyo na kuongeza kusema:

“Wataalamu wa Forensic (uchunguzi wa kijinai) wangeweza kugundua wino huo una miaka 50. Wanafanya kitu ambacho hawakijui na wanadhalilisha Watanzania.”

Mjumbe huyo alisema yeye anaunga mkono muundo wa Muungano wa Serikali mbili na kuwa Serikali tatu ni sawa na mtu kunywa sumu.
Share:

AJALI MBAYA YA MAGARI MANNE YATOKEA MKOANI IRINGA

Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio..
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.
BASI aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya jana. Tukio hilo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace.  
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
Share:

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA IVUMWE MBEYA YATEKETEA KWA MOTO



Mwenyekiti wa Bodi wa Kwanza Dr Victory Kanama akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Ndugu Fatma Asenga pamoja na mmoja wa walimu wa shule  hiyo kuangalia namna jnaga hilo la moto lilivyo teketeza mabweni katikia shule hiyo ya Ivumwe yenye mchepuko wa  Wavulana na Wasichana.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga akizungumza juu ya mipango ya dharula itakayo fanywa ili kuokoa janga hilo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo Dr Victory Kanama akizungumza juu ya tukio hilo.


Na EmanuelMadafa,Mbeya

Bweni Moja  la Wavulana lenye vyumba zaidi ya  Sita  katika shule ya Sekondari ya Ivumwe  inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea leo April 23  majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya   wakati wanafunzi hao wakiwa madarsani kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Akizungumza katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi wakati teyari wanafunzi wakiwa madarasani.

Amesema taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo.

Amesema mara baada ya kupata habari hizo   walitoa taarifa kwa kikosi cha zimamoto ambacho kilifika mara moja na kuanza juhudi za kuuzima moto huo.

Amesema pamoja na kikosi hicho cha zimamoto kufika shuleni hapo mapema na kuzima moto huo lakini teyari moto huo ulikwisha teketeza asilimian kuwabwa ya mali zilizomo katika mabwani hayo.

Amesema kwa kiwango kikubwa vitu vingi vimeteketea kwa moto huo   hususani vitanda na magodoro ambayo ndiyo yaliyoungua vibaya  pamoja na vitu vingine vya wanafunzi hao.

Aidha kwa mujibu wa Dakta Kanama hakuna mwanafunzi yoyote aliye poteza maisha kutokana tukio hilo licha ya mmoja wa wanafunzi kujeruhiwa mkononi na kitu kinacho dhaniwa kuwa ni kioo katika harakati za kuokoa vitu ambapo teyari amekwisha fikishwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Fatma Asenga amesema mabweni hayo yalichukua jumla ya wanafunzi 160  ambao ni wavulana huku chanzo cha moto huo kikiwa bado bado hakijajulikana.

Amesema  kwa sasa juhudi zinazofanyika na Chama kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo  ili kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwahifadhi wanafunzi hao.

Amesema litatengwa darasa moja kwa muda ambalo litatumika kama bweni wakati wakiendela kufanya utaratibu mwingine.
Share:

MBUNGE MTATA WA CCM DR. HAMIS KIGWANGWALLA AFUNGUKA TENA LEO SOMA HAPA LIVE!!

Hamisi Kigwangalla
"Leo nilikuwa kwenye mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na Twaweza. Chief discussants tulikuwa mimi nikimuwakilisha KM wa CCM Ndg. Kinana, Mzee Warioba na Ndg. Julius Mtatiro.
Nilichojifunza kutokana na kauli za Mwenyekiti wa Tume Mzee Warioba ni kuwa, mapendekezo ya Serikali 3 yalijengwa kwenye msingi wa hoja nyepesi, na zaidi ilikuwa ni hisia na utashi wa Tume. Maswali; nani aliwapa mamlaka hayo? Sheria? Hayakujibika!"
Share:

HANDAKI LA AJABU LAONEKANA ENEO LA KITANZINI IRINGA.. SHUHUDIA


Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo

Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake Mtandao huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi. 


Handaki hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo. 
Akizungumza mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo.


Ameeleza kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani. 

Anazidi kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza kuendelea kutokana na kuzibwa.


Mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa nyumba ambayo handaki hilo limeonekana

Mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio:
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo. 

Nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo? 
Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.
Share:

NISHA: SIJAWAHI KUCHUKULIWA NA PEDESHEE

SALMA Jabu maarufu kama Nisha, ni mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri katika kiwanda cha filamu Tanzania. Amefanya kazi nyingi zinazomfanya kuwa mmoja wa mastaa wanaoongoza kwa kushiriki katika movie nyingi.
Salma Jabu 'Nisha'.
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta na kufanya naye mahojiano maalum kuhusu mambo mbalimbali yanayohusiana na sanaa yake.
Risasi: Mambo vipi Nisha?
Nisha: Poa kabisa, niambie
Risasi: Unaizungumziaje sanaa yako kwa ujumla wake?
Nisha: Sanaa yangu ni safari ndefu sana na naamini ndiyo kwanza nipo robo yake.
Kuna mambo mengi magumu, mojawapo ni kupata vikwazo vya hapa na pale, pia wapo baadhi yetu wanapata labda skendo, badala ya kuwahukumu wenyewe, lakini tunachukuliwa kuwa wote ndivyo tulivyo jambo ambalo siyo kweli.
Mtu unatamani kuwa fulani, lakini unawekewa vikwazo kwa sababu tu ya ule msemo wa samaki mmoja akioza, basi wote wameoza.
Risasi: Vipi kuhusu soko la bidhaa zetu?
Nisha: Soko ni zuri sana, ni kujua tu mashabiki wako wanapenda nini basi.
Risasi: Unadaiwa wewe una fedha sana, kuna mtu yuko nyuma yako?
Nisha: Sina mtu nyuma yangu, pesa ni juhudi zako mwenyewe, kikubwa nafanya kazi kwa bidii, napenda sana kazi yangu, alhamdulilah sasa nimekuwa na kampuni yangu mwenyewe ya kuandaa filamu (Nisha’s film production).
Nisha katika pozi.
Kwa mfano nimeandaa filamu kama Tikisa, Pusi na Paku, Kashfa na Gumzo na zingine. Hiyo ndiyo siri ya hizo pesa wanazozitaja, napenda kuweka akiba kwa kufungua mradi, saluni yangu na duka la samani, ndiyo vinaendesha maisha ya kawaida ya nyumbani.
Risasi: Umri unaenda, vipi umeolewa?
Nisha: Nina mtu alhamdulilah, Inshaalah niombeeni dua, sijawahi sumbuliwa kwani mimi mapema nimeanza kujiajiri mwenyewe.
Risasi: Umejaaliwa kupata mtoto?
Nisha: Sina watoto ila napenda watoto, kila mtoto ni wangu inshaallah nataka kuanzisha familia, nasubiri Mwenyezi Mungu ajibu kwani kila kitu kimeandikwa na yeye, mimi siwezi jua lini, saa na wapi.
Risasi: Kuna maneno juu ya wasanii kujirahisisha kwa watu wenye fedha, wanaoitwa mapedeshee, unazungumziaje?
Nisha: Mimi sijawahi kuwa na pedeshee wala simuhitaji, nakuwa na mtu kwa mapenzi ya kweli, awe maskini au tajiri ilimradi moyo wangu umempenda, kikubwa tabia na maelewano na anipende kwa dhati.
Risasi: Unafikiri kwa nini baadhi ya wasanii na wasichana wengine wanaamua kujiuza?
Nisha: Wengine wanashindwa kujiajiri kwa kukosa mtaji (kwa wasiokuwa nao nawaombea wapate) wanaojiuza ni tamaa,
kutojitambua na kukosa malengo, mimi nina malengo na siku moja niwe mfano kama Oprah Winfrey na kadhalika, sijaridhika kwa nikipatacho, nafanya kazi kwa bidii ili kupata zaidi Inshaalah.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger