Friday 30 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 31, 2024

Share:

PROGRAMU YA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYABIASHARA WA NDANI YA BARRICK YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita akiongea katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo
***
Katika mwendelezo wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa ndani kupitia mafunzo yanayotolewa na kampuni ya Barrick nchini kupitia Programu yake ya kuendeleza biashara za ndani ili ziweze kunufaika na sekta ya madini (Local Business Development Programme), Wajasiriamali wapatao 150 kutoka wilaya za Msalala, Kahama na Nyang’hwale, wanapatiwa mafunzo ya biashara ya wiki mbili ambayo yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.

Mafunzo haya ambayo yanafanyika katika hoteli ya Kitapela, yanayotolewa na wataalamu mbalimbali wa masuala ya kibiashara yamelenga kuwawezesha wajasiriamali waliopo katika maeneo yanayozunguka mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu kuweza kuchangamkia fursa za kibiashara na kunufaika na uwekezaji wa mgodi huo sambamba na kupata maarifa zaidi ya kuendesha biashara zao kitaalamu.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, aliipongeza Barrick Bulyanhulu kwa kuendesha mafunzo hayo na kuwataka washiriki kutoka kata tatu zinazozunguka Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, kuchangamkia fursa za mikopo ya asilimia 10, inayotolewa halmashauri zote ili kujikwamua kiuchumi.

“Mnaoshiriki mafunzo kupitia program hii muyazingatie kikamilifu ili muweze kuwa na vigezo vya kuchangamkia biashara zilizopo mgodini na kupata ujuzi wa kufanya biashara zenu kwa weredi nje ya mgodi”, alisema Mhita.

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Victor Lule, alisema Kampuni ya Barrick inaamini kwamba msingi wa maendeleo ndani ya jamii unatokana na watu na hatua sitahiki kwenye fursa zinazopatikana ndio sababu ya kuwekeza katika programu hii ili kuwahamasisha kuzitambua fursa hizo.

Aidha alisema Mgodi wa Barrick Bulyanhulu unajivunia kuona idadi kubwa ya washiriki wa mafunzo hayo wanatokea katika kata mbalimbali jirani na mgodi ambao watanufaika na mafunzo yanayotolewa kupitia program hii ili waweze kuchangamkia fursa za kibiashara mgodini sambamba na kukuza biashara zao.


Mafunzo hayo yanaendeshwa na washauri wabobezi wa masuala ya kibiashara kutoka sekta ya umma na binafsi, ambapo yanatarajiwa kuwaongezea wafanyabiashara hao ujuzi, maarifa, mbinu na uwezo wa kubaini fursa mpya za kibiashara ndani na nje ya nchi ili kuweza kufikia malengo yao - wakizingatia vigezo, masharti, sheria na kanuni za Serikali na Kampuni ya Barrick ambayo inaendesha shughuli zake nchini kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Tangu Programu hii ianzishwe tayari imewafikia wafanyabiashara mbalimbali waliopo maeneo jirani na migodi ya Barrick North Mara na Bulyanhulu na yamewawezesha baadhi yao kuchangamkia fursa migodini na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara.

Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo, Anastazia Ibrahim, kutoka Nyang’hwale, alisema matarajio yao ni kupata ujuzi utakaowawezesha kuchangamkia fursa za kibiashara zinazojitokeza sambamba na kuendesha biashara zao kitaalamu na kufuata sheria za nchi.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Victor Lule akiongea wakati wa hafla wa uzinduzi wa mafunzo hayo.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Siraji Nalikame kutoka kampuni ya Impacten akitoa Mfunzo kwa washiriki
MenejaMahusiano na Mazingira wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu,Agapit Paul akiongea na washiriki wa mafunzo hayo
Mkufunzi Rashidi Mwakatuma kutoka Impacten akitoa mafunzo kwa Washiriki wa Mafunzo haya.
Mkufunzi kutoka Jukwaa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Wilaya ya Kahama, Jozaka Bukuku akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi

Washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi

Washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi
Makundi mbalimbali ya washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduzi
Makundi mbalimbali ya washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduzi
Makundi mbalimbali ya washiriki na wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wakati wa uzinduzi
Share:

SILLO AWATAKA VIONGOZI WA DINI KULINDA AMANI NA MAADILI







Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amewataka viongozi wa dini nchini Tanzania kuendelea kukemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili katika jamii na visivyoendana na neno la Mungu ili kulinda mila na desturi nzuri za nchi yetu na kujenga taifa lenye upendo na amani

Sillo amesema hayo katika Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 150 ya Utume Ulimwenguni yaliyofanyika katika kanisa la Waadventista wa Sabato (SDA ) lililopo Mamba Myamba wilayani Same, mkoani Kilimanjaro leo Agosti 29, 2024

Amesema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kujihusisha katika kuendelea kulinda amani ya nchi yetu na kufanya amani ya nchi kuwa jambo la kwanza

"Ikiwa tunawafundisha watu kumtii Mungu ambaye ni chanzo cha amani ya kweli basi tunapaswa kuwafundisha waumini umuhimu wa kuendelea kuilinda amani". Amesema

Aidha Mhe. Sillo alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha Wananchi kuwa Mwaka huu mwezi Novemba kutakuwa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kuhuisha taarifa zao katika daftari la Wapiga kura

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Waadvestista Wasabato Jimbo kuu la Kaskazini mwa Tanzania, Mark Malekana ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano mzuri wanaoutoa kwa viongozi wa dini. 

Ameongeza kuwa kanisa litaendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika masuala ya Ustawi wa Jamii ili amani iendelee kutamalaki na kujenga taifa lenye ustawi
Share:

Thursday 29 August 2024

WAKULIMA WA DENGU MANYARA WATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA SAHIHI ZA KUPOKELEA MALIPO YAO


Wakulima wa dengu wanaohudumiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Rift Valley (RIVACU LTD) Mkoani Manyara wametakiwa kuhakiki na kukabidhi taarifa zao za kupokelea fedha zikiwa hazina makosa kwa Makatibu wa Vyama vyao, ili kuepusha ucheleweshwaji wa malipo kwa wakulima ambao taarifa zao zina mapungufu.

Rai hiyo imetolewa na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga, kwenye mnada wa nne wa zao la dengu uliofanyika katika ghala la Gendi.

Cheliga amesema kuwa wanunuzi wamekuwa wanalipa fedha za mnada kwa wakati na mkulima anapaswa kupokea fedha hizo ndani ya masaa 72 baada ya mnada kufanyika ila kumekuwa na changamoto ya kukosewa kwa taarifa za wakulima hali inayosababisha baadhi kuchelewa kupokea malipo.

Kwa upande wake Meneja wa RIVACU, Upendoel Valentine, amewaomba wakulima kuzingatia usafi na ubora ili waendelee kupata bei nzuri kwenye soko hilo la dengu.

“Niwaombe Wakulima kuzingatia usafi na ubora wa dengu na niwatake muendelee kuleta dengu katika maghala kwani bei inayopatikana sokoni sasa hivi ni nzuri na tuache kuuza kwa walanguzi kwasababu tunapishana na bei iliyo nzuri kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani," amesema Upendo.

Mkoani Manyara minada mitatu ya dengu imefanyika katika ghala la Endagaw wilaya ya Hanang, Gendi wilaya ya Babati na Maretadu wilaya ya Mbulu na wakulima wamekubali kuuza dengu hizo kwa Ghala la Endagaw Kilo 322,333 kwa bei ya wastani ya Shilingi 1,814, Ghala la Gendi Kilo 210,669, kwa bei ya wastani ya Shilingi 1,818 na Ghala la Maretadu Kilo 225,165 kwabei ya wastani ya Shilingi 1,756.

Share:

Tuesday 27 August 2024

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 28,2024

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger