Friday, 18 August 2023
Thursday, 17 August 2023
MKOA WA TANGA UNA CHANGAMOTO KUBWA YA MATUKIO YA AJALI ZA BARABARANI HUSUSANI ZA WANAFUNZI
Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo akielezea Mpango Kazi wa Usalama Barabarani
Mmoja wa madereva waliokiuka sheria za usalama barabara Avishai kushoto akiandika maelezo ya kutokurudia kosa la kutokusimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu baada ya kukamatwa kwa kosa hilo leo na kufikishwa kwenye mahakama ya watoto iliyokuwa ikishikiliza kesi za madereva waliovunja sheria za barabarani kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Tanga William Mwamasika
Mahakama ikiendelea
| Elimu ikitolewa kwa waendesha bodaboda |
Wanafunzi wakifiatilia mahakama hiyo
Na Oscar Assenga,TANGA
JESHI la Kitengo cha Usalama barabarani mkoani Tanga limesema kwamba mkoa huo una changamoto kubwa ya matukio ya ajali hususani kwa watoto na wanafunzi wanapotoka majumbani kwenda shuleni na wanaporejea.
Hayo yalibainishwa leo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga (RTO) Wiliam Mwamasika wakati wa kuelezea mpango kazi wa Usalama barabara kwa Jiji la Tanga unaendeshwa na Shirika la Amend Tanzania ambao umefikia asilimia 90.
Kabla ya kueleza mpango huo kulishuhudiwa uendeshaji kesi katika Mahakama ya Watoto( Mahakama Kifani) kwa madereva waliovunja sheria za usalama barabarani kwa kutosimama maeneo yenye alama za watembea kwa miguu yanayotumiwa kuvuka wanafunzi.
Mpango huo umekwenda sambamba na kufadhili mafunzo kwa waendesha bodaboda 300 katika Jiji la Tanga ili kuweza kuzijua sheria za usalama barabarani na namna ya kuweza kuziepuka.
Alisema mara nyingi ajali hizo zimekuwa zikisababishwa na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kutokana na baadhi yao kushindwa kufuata sheria za usalama barabarani
Alisema kufuatia uwepo wa changamoto hiyo, Jeshi hilo limendelea kujipanga na kuimarisha usalama hususani kwenye vivuko wavyovukia wanafunzi nyakati za asubuhi wanapovuka ikiwa ni mkakati wa kutokomeza ajali ambazo zimekuwa zikipoteza ndoto zao.
“Kwa kweli sisi kama Mkoa wa Tanga tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatokemeza ajali za barabarani hususani kwa watoto na wanafunzi kwa kuhakikisha kila siku hususani nyakati za asubuhi kuna kuwa na askarti wa usalama kwenye vivuto vya watembea kwa miguu kwa lengo kuondosha ajali hizo”Alisema
Alisema watumiaji wa vyombo vya moto wamekuwa wakipuuzia sheria za usalama barabarani licha ya kuzifahamu hivyo ni jukumu la kila mwananchi sasa wahakikishe wanazingatie na kufuata sheria za usalama ili kuweza kupunguza ajali
Awali Meneja wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo alisema hilo limetekeleza Mpango Kazi wa Usalama Barabarani kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa asilimia 90 huku likitumia nafasi hiyo kueleza hatua mbalimbali za kuutekeleza mpango huo ikiwemo kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa 350 wa shule za msingi.
Alisema Shirika hilo linajishughulisha na usalama barabarani nchini tangu mwaka 2009 na kwa ufadhili wa Shirika la Fondation Botnar jijini Tanga, shirika hilo limekuwa likishirikiana na Halmashauri ya Jiji katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo ya shule.
“Pia kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi,kuanzisha klabu za usalama barabarani na mahakama kifani za watoto, mafunzo kwa madereva pikipiki , kuandaa makongamano ya wadau wa usalama barabarani, kufanya tafiti huhusu ajali za barabarani, na kuandaa Mpango Kazi wa usalama barabarani kwa Jiji hilo”Alisema
Akizungumzia Mpango Kazi huo wa usalama barabarani wenye lengo la kuboresha safari salama na endelevu kwa jiji la Tanga alisema ulizinduliwa Novemba 11 ,2022 na tangu ulipozinduliwa kuna mambo kadha yametekelezwa.
Alisema baada ya uzinduzi huo amesema shirika la Amend limefanikia kuzindua miundumbinu katika shule tatu za msingi za Shaaban Robert, Mabawa na Majengo.
“Mpaka sasa tumetoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi 3,501 wa shule za msingi Mabawa, Majengo and Shabaan Robert na wengine 3,247 wa shule za sekondari Toledi, Kihere and Kiomoni”Alisema
“Tumeanzisha klabu mbili za shule za usalama barabarani katika Shule ya Msingi Usagara na klabu ya usalama wa baiskeli katika Shule ya Sekondari Usagara, yenye watoto 20 katika kila klabu na tumetoa mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto hawa, baada ya kuhitimu kuwa mabalozi, wakipokea vyeti katika hafla ndogo”Alisema
"Shughuli za vilabu hivi zimejumuisha mafunzo, midahalo ya usalama barabarani, michezo, mijadala ya mezani na kushiriki katika kampeni za vyombo vya habari na mafunzo ya msasa kwa madereva wa pikipiki 350 kufanya jumla ya madereva waliopata mafunzo haya kufikia 950."
Kalolo alisema Februari mwaka huu wamesambaza vifaa vya kufundishia usalama barabarani kwa maofisa maendeleo ya jamii katika kata 22 kati ya 27 za Jiji la Tanga.
MWisho.
TAMKO LA KULAANI KUSHAMBULIWA KWA WAANDISHI WA HABARI
Tukio hilo lilihusishwa kujeruhiwa kwa Waandishi wa habari wafuatao, Ferdnand Shayo (ITV), Dennis Msacky (Media Brain),Habib Mchange (Jamvi la Habari),Elia Kinian (Channel Ten),Janeth Joseph (Mwananchi), Dickson Busagaga (Clouds Media) na Mkalimani wao Lengai Ngoishiye,
Waandishi hao walikutwa na madhila hayo wakati wakitekeleza majukumu yao ya kikazi ya kutafuta taarifa za wamasai wanaoishi Ngorongoro na kutaka kuhama kwa hiari yao toka Kijiji cha Enduleni kilichopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
OJADACT inaamini kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha pamoja na Mamlaka nyingine za ulinzi na usalama zitawatafuta na kuwakamata watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria ili wawajibishwe na iwe funzo kwa watu wengine wenye nia ovu dhidi ya waandishi wa habari.
Pia OJADACT inawakumbusha waandishi wa habari na vyombo vya habari kufanya tathimini ya ulinzi na usalama wa maeneo wanayotakiwa kwenda kufanya kazi zao ili kupungunza madhila yanayoweza kuwapata na pia OJADACT inatia pole majeruhi wote.
Edwin Soko
Mwenyekiti, OJADACT
Julai Agosti 17, 2023
JUMLA YA WAZABUNI 4,350 WAMEJISAJILI KWENYE MFUMO WA NeST.
MIAKA 20 YA PEPFAR: KITUO CHA BIKIRA MARIA MAMA WA TUMAINI - MASANGA KIMBILIO SALAMA LA TOHARA KINGA KWA WANAUME
JK ATETA NA KAMATI YA SADC-TROIKA ANGOLA
*Na Mwandishi Wetu, Angola*
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, (SADC Panel of Elders) akiwa pamoja na Viongozi wanaounda Kamati ya Utatu ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC- TROIKA) wakijiandaa na Mkutano wa Kamati hiyo unaofanyika leo tarehe 16 Agosti, 2023, Luanda, Angola.
Viongozi hao ni pamoja na Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa SADC TROIKA, Mhe. Haikande Hichilema wa Zambia ambaye anatarajiwa kuchukua Uenyekiti wa Kamati hiyo na Mhe. Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Kamati hiyo ya SADC TROIKA. Pichani pia ni Mhe. Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Lesotho (wa pili kutoka kulia) na Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Magosi (wa kwanza kushoto).
Rais Mstaafu Kikwete amewasilisha katika Kamati hiyo ya SADC TROIKA Ripoti ya Kamati ya Uangalizi (Oversight Committee) anayoiongoza katika kufuatilia hatua za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kiasiasa ulipo katika Ufalme wa Lesotho.
DAWA ITAKAYOKUSAIDIA KUJIKINGA NA MAADUI ZAKO!

Maadui wamekuwa wakiumiza wasio na hati katika maisha yetu, ubaya ni kwamba ni vigumu sana kufahamu maaduni wetu, hivyo naweza kusema maadui wetu tunaishi nao katika kazi, biashara na hata mahusiano.
Jina langu ni Fadhili kutokea Nyeri, nina miaka 24, katika familia yangu tulipitia changamoto nyingi sana kiasi kwamba nilitaka hadi kukimbia nyumbani maana changamoto zilikuwa haziishi.
Kila mara utakuta wazazi wanaumwa, natumia fedha zangu zote kuwatibu hadi nakosa nauli ya kwenda kazini, hilo likiishi mara utasikia kuna changamoto nyingine kubwa ipo ambayo inahitaji fedha kuitatua.
Kila siku maisha yakawa ni kurudi nyuma badala ya kusonga mbele, hakuna jambo la kimaendeleo ambalo kama familia tuliweza kulifanya.
Hata wadogo zangu wote hawakuweza kwenda shule, wengine wa kike walipata na ujauzito wakiwa hapo hapo nyumbani bila ya kuolewa na hata wanaume waliowapa ujauzito waliwatelekeza, hivyo kazi ikawa tena kwetu kama familia kuwahudumia.
Kuna siku niliweza kusikia tangazo katika redio kuwa African Doctors anaweza kuikinga familia na maadui, nilitegemea sikio kwa makini hadi pale Mtangazaji alipotaja namba yake ambayo ni +254 769404965. Nilinakili namba hiyo ili baadaye niweze kumpigia.
Hatimaye niliweza kuwasiliana naye na kumuelezea kuhusu shida yangu, aliniambia ningoje baada ya muda, alinipigia na kuniambia kuna jirani yetu ambaye mara nyingi huwa anakuja nyumbani kwetu ndiye ambaye anatuchezea mchezo huo.
African Doctors alinipatia dawa ya kuweza kujikinga na adui huyu na kweli nashukuru dawa yake imeweza kuzaa matunda maana tangu wakati huo huyu jirani haji tena nyumbani kwetu kwa madai ni mgonjwa lakini mimi najua langu moyoni kuwa dawa ya African Doctors imeweza kufanya kazi yake vilivyo.
Tangu wakati huo hakuna chochote kile ambacho kimeweza kuleta shida pale nyumbani, mambo yamekuwa yakienda sawa kama ambavyo tulipanga na kutarajia.
Kumbuka African Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.
Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.
Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.
Mwisho.
Wednesday, 16 August 2023
AFYA CHECK , OFISI YA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA KUZINDUA KAMBI MAALUMU YA MATIBABU BURE




Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo akizungumza


TAASISI ya Afya Check kwa kushirikiana na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Tanga wanatarajia kuzindua kambi maalum ya kupima afya bure kwa wananchi wa Jiji la Tanga kwa siku tano ikiwa ni mpango wa kuihamasisha jamii kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara ili pale wanapogundulika kuwa na matatizo mbalimbali waweze kupata matibabu ya haraka.

































