Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wametoa Elimu ya miundombinu ya barabara kwa wananchi 300 waliotembelea kwenye banda lao kupitia Maadhimisho ya Utumishi wa Umma Mkoani Dodoma ambapo wananchi hao wamepatiwa ufafanuzi wa miradi mbalimbali ya barabara katika maeneo yao
Hayo yamesemwa Mkoani na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma TARURA Catherine Sungura, amesema wananchi waliotembelea kwenye banda letu tumewahudumia na kusikiliza changamoto zao ambapo tunaenda kuzitatua kupitia mameneja waliopo maeneo husika.
Aidha sungura ameongeza kuwa Tarura inaendelea na ujenzi wa barabara ya zege kimara King'ong'o Dar es salaam hivyo unaendelea vizuri, na Meneja wa TARURA amewahakikishia wananchi kuwa kilomita 1.6 pekee ndizo zimebaki kukamilishwa, huku mita 800 zikitarajiwa kujengwa mwanzoni mwa mwaka mpya wa fedha kuanzia Julai na sehemu iliyobaki kukamilishwa katika awamu inayofuata.
"Nitoe wito kwa wananchi kuwa tarura itaendelea kuhakikisha miundombinu ya barabara inaboreshwa ili kurahisisha mawasiliano na usafiri kwa wananchi kwani barabara hizo zinachochea Upatikanaji wa Maendeleo ya uchumi nchini "Amesema Afisa sungura"
Hata hivyo sungura amewataka wananchi wote waendelee kutembelea kwenye banda la tarura waweze kujipatia elimu ya Miundombinu ya barabara zinazoendelea kujengwa nchini.


0 comments:
Post a Comment