Tuesday, 25 January 2022

WADAU WA MASUALA YA ELIMU WAGUSWA NA MPANGO MKAKATI WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA)

Wadau kutoka sekta na Idara mbalimbali za Serikali wamekuta leo jijini Dar es Salaam kujadili rasimu ya mpango mkakati wa nne wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambao utatumika kwa miaka mitano hadi 2026. Katika kikao kazi hicho cha siku moja, wadau wamefurahishwa na jinsi ambavyo TEA imeweka vipaumbele katika mambo ya kimkakati ikiwemo TEHAMA.

Katika majadiliano hayo, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imepongezwa kutokana na jitihada zake za kusimamia na kuboresha miundombinu ya Elimu hasa katika mazingira ambayo ni magumu kufikika kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa.

Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI Bw. Musa Otieno ambaye alikuwa mmoja wa wadau katika kikao hicho amesema, TEA imefanya kazi nzuri sana ya kuboresha miundombinu ya shule ambapo imejenga madarasa, nyumba za waalimu, matundu ya vyoo, mabwalo ya vyakula pamoja na kununua madawati kwenye maeneo ya pembezoni mwa miji ambako ni ngumu kufikika.

Jitahada zote hizi zinalenga kusogeza huduma za sekta ya elimu karibu na wananchi ili kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kusoma karibu na mazingira anayoishi na hili linadhihirika wazi kwani mpango mkakati wa miaka mitano ijayo umebainisha kazi zinazooenda kufanyika katika kusimamia upatikanaji wa elimu bora, alisema Otieno

Nae mdau mwingine kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Gerald Sando, ameishukuru Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kazi zake na kusema kazi hizo ni endelevu na zinaonekana kwa macho.

Sando amesema, kazi za TEA zinagusa maisha ya wananchi moja kwa moja na kuongeza thamani kwenye maisha ya wale wa kipato cha chini kupitia mradi wa kuongeza ujuzi (SDF) ambao unafadhiliwa na TEA.

Kikao kazi cha kupitia rasimu ya mpango mkakati wa Mamalaka ya Elimu Tanzania (TEA) wa miaka mitano hadi 2026 kimefanyika jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu Bi. Bahati Geuzye.

Akitoa salaam za ukaribisho Mkurugenzi wa huduma za Taasisi Dr. Erasmus Kipesha ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho alisema, tangia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeanzishwa mwaka 2001, hii ni rasimu ya nne ya mpango mkakati.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Elimu Na. 8 ya mwaka 2001 ikiwa na jukumu la kusimamia uendeshaji wa Mfuko wa Elimu wa Taifa kwa lengo la kuongeza nguvu za Serikali katika kuinua upatikanaji wa elimu bora kwa usawa katika ngazi zote za elimu Tanzania Bara na elimu ya juu kwa Tanzania Zanzibar.

 
Mkurugenzi wa huduma za Taasisi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akitoa salaam za ukaribisho kwa wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria kikao kazi cha siku moja kujadili rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Bahati Geuzye akitoa hotuba ya ufunguzi katika kikao kazi cha siku moja cha kujadili rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA kwa wadau wa masuala ya elimu (hawapo pichani)

 Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao kazi cha siku moja wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.

Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao kazi cha siku moja wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bw. Musa Otieno akichangia maoni yake kuhusu rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA


Bw.Gerald Sando kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa – Dar es Salaam akitoa maoni yake kuhusu rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA.

Mkurugenzi wa huduma za Taasisi kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt Erasmus Kipesha akiwasilisha rasimu ya mpango mkakati wa miaka mitano wa TEA kwa wadau wa masuala ya elimu.


Share:

WASINDIKAJI NA WAZALISHAJI WA MAZIWA WAMETAKIWA KUHAKIKISHA BIDHAA HIZO KUWA BORA

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto SSI.Mbarak Alhaji Batenga ( kati kati), Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto Bw. Fadhili D. Alexander (Kushiro) na Meneja kanda ya Kaskazini (TBS) Bi Happy B. Kanyeka (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo kwa wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa. Mafunzo haya yanalenga kuwaelimisha wadau wa maziwa kuhusu viwango vya maziwa na bidhaa za maziwa , utaratibu wa kuthibitisha ubora wa maziwa na bidhaa za maziwa, kanuni bora na taratibu za kusindindika maziwa na bidhaa za maziwa pamoja na kanuni bora za ufugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Muhandisi Richard Runyango akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za Maziwa wilayani Arumeru.
Mhe. Runyango aliwataka washiriki kuzingatia mada zote zinazotolewa na kuzifanyia kazi ili waweze kuzalisha Maziwa na bidhaa za Maziwa bora zitakazoweza kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Hai Bw. Yassin A Zayumba akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa Bidhaa za Maziwa wilayani Hai.
Maafisa wa TBS wakitoa mada kuhusu faida na matakwa ya kiwango cha maziwa na bidhaa za maziwa pamoja na kaununi bora za usindikaji, vifungashio na ufungashaji wa maziwa na bidhaa za maziwa . Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha washiriki kuboresha na kuongeza thamani katika mnyororo wa uzalishaji wa bidhaa husika na hatimae kuzalisha bidhaa bora na salama.




************************


Wajasiriamali wanaojishughulisha na ufugaji, ukusanyaji, ubebaji na usindikaji wa maziwa na bidhaa za maziwa wameshauriwa kuzalisha na kusindika maziwa yenye ubora ili kufanikisha azma ya Serikali ya kukuza sekta ya viwanda nchini.




Ushauri huo ulitolewa na Bi Happy Kanyeka wakati wa mafunzo kwa wafugaji, wasindikaji, wasambazaji na wauzaji wa maziwa na bidhaa za maziwa yaliyofanyika katika wilaya za Kiteto (Manyara), Arumeru (Arusha) na Hai(Kilimanjaro)




Mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha wajasiriamali walio katika myororo wa thamani ya ufugaji, ukusanyaji wa maziwa ghafi, ubebaji na usindikaji wa maziwa na bidhaa za maziwa juu ya kanuni na matakwa ya msingi kuhusiana na shughuli wanazozifanya.




Akizungumza wakati wa mafunzo haya Bi Happy Kanyeka meneja wa kanda ya kaskazini (TBS) alisema, tunatambua kuwa sekta hii ya maziwa ina wajasiriamali wengi wadogo na wa kati ambao husindika na kupeleka sokoni maziwa na bidhaa za maziwa na walio wengi hufanya hivyo bila kufuata kanuni na taratibu zinazotakiwa hivyo kupelekea uwepo wa maziwa na bidhaa za maziwa hafifu sokoni pamoja na uharibifu na upotevu wa maziwa mengi sokoni.




“Kuna baadhi ya wasindikaji wa maziwa tayari walishaanza taratibu za kuthibitisha ubora wa bidhaa zao ili kukidhi matakwa ya viwango husika lakini kutokana na changamoto za kukosa elimu juu ya viwango imepelekea mchakato wa uthibitishaji ubora kuonekana mgumu hivyo basi katika mafunzo haya tumeelekezana kuhusu kanuni bora za usindikaji, kanuni bora za ufungaji, kanuni bora za afya, faida na matakwa ya kiwango cha maziwa na bidhaa za maziwa pamoja na utaratibu wa kuthibitisha ubora wa maziwa na bidhaa za maziwa” aliongeza Bi Kanyeka




Bi. kanyeka alisisitiza kuwa wilaya za Kiteto, Arumeru na Hai ni wilaya amabazo zinajihusisha na ufugaji wa ng’ombe wengi wakiwemo wa kienyeji na wa kisasa na usindikaji wa maziwa na bidhaa za maziwa ni moja ya shughuli inayofanya na wajasiriamali katika wilaya hizo.




“Mafunzo haya yametolewa katika maeneo muhimu sana yanayojishughulisha na Ufugaji wa Ng’ombe, usindikaji, usambazaji na uuzaji wa maziwa na bidaa za maziwa, pia ni azima ya serikali kukuza viwanda nchini endapo washiriki wa mafunzo haya watazingatia yale yote walioelekezwa taifa litakuwa na bidhaa bora na salama zitakazoweza kushindanishwa vyema katika sekta ya maziwa na bidhaa za maziwa ndani na nje ya nchi.”




Na katika kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi matarajio ya washiriki TBS imeshirikiana na taasisi nyingine ikiwemo SIDO, Bodi ya Maziwa (TDB) na TAMISEMI( ambao ni Afisa Afya, Afisa Mifungo, Afisa Biashara na Afisa Maendeleo ya Jamii)
Share:

Monday, 24 January 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 25,2022

Magazeti ya leo Jumanne January 25 2022


MAGAZETI MENGI ZAIDI TUNALETA HIVI PUNDE.....

Share:

JESHI LAPINDUA SERIKALI...RAIS WA BURKINA FASO HAJULIKANI ALIPO


Jeshi limesema hali mbaya ya usalama ndio iliolishinikiza kumuondoa madarakani rais Kabore


Jeshi nchini Burkina Fasso linasema kwamba limechukua mamlaka na kumuondoa madarakani rais Roch Kabore.

Tangazo hilo lilitolewa katika runinga ya taifa na afisa mmoja wa jeshi , ambaye alisema kwamba serikali na bunge limevunjwa.

Kufikia sasa haijulikani bwana Kabore yuko wapi , lakini afisa huyo amesema kwamba wale wote wanaozuiliwa wapo katika eneo salama.

Mapinduzi hayo yanajiri siku moja tu baada ya wanajeshi hao kudhibiti kambi za jeshi huku milio ya risasi ikisika katika mji mkuu wa Ouagadougou..

Mapema , Chama tawala cha peoples Movement PMP kilisema kwamba wote Kabore na waziri mmoja wa serikali walinusurika jaribio la mauaji.

Siku ya Jumapili, wanajeshi waasi walitaka kufutwa kazi kwa maafisa wa jeshi na kuongezwa kwa raslimali za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kundi ambalo halijasikika hapo awali, Vuguvugu la Patriotic for Safeguard and Restoration au MPSR, kifupi chake cha Kifaransa.

"MPSR, ambayo inajumuisha vitengo vyote vya jeshi, imeamua kusitisha wadhifa wa Rais Kabore leo," ilisema.

Kabla ya tangazo hilo, Muungano wa Afrika na Umoja wa Afrika Magharibi Ecowas walilaani kile walichokiita jaribio la mapinduzi nchini Burkina Faso.


Ecowas imesema kwamba wanajeshi watawajibikia usalama usalama wa Bw Kaboré iwapo lolote litatokea.
Rais Roch Kabore

Video kutoka mji mkuu inaonekana kuonyesha magari ya kivita - yanayoripotiwa kutumiwa na rais - yakiwa na mashimo ya risasi na kutelekezwa mitaani.

Huduma za mtandao wa simu za mkononi zimekatizwa, ingawa mtandao wa laini zisizobadilika na wi-fi ya nyumbani zinafanya kazi

Bw Kaboré hajaonekana hadharani tangu mzozo huo uanze lakini machapisho mawili yalionekana kwenye akaunti yake ya Twitter kabla ya afisa huyo kutangaza kuwa amepinduliwa.

Baadaye alitoa wito kwa wale waliochukua silaha kuziweka chini "kwa maslahi ya taifa". Hapo awali Bw Kaboré alipongeza timu ya taifa ya kandanda kwa ushindi wao katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Haijulikani ikiwa Bw Kaboré au mtu mwingine alichapisha tweets hizo.

Baadhi ya vyanzo vya usalama vinasema rais na mawaziri wengine wa serikali wanazuiliwa katika kambi ya Sangoulé Lamizana katika mji mkuu.

Siku ya Jumapili, mamia ya watu walijitokeza kuwaunga mkono wanajeshi hao na baadhi yao walichoma moto makao makuu ya chama tawala. Amri ya kutotoka nje wakati wa usiku imewekwa.

CHANZO - BBC SWAHILI
Share:

USAHA NA VIJIDUDU VILINITOKA, NILIVYORAMBA ASALI YA RAFIKI YANGU

 Niliishi katika kaunti ya Marsabit karibu na jirani yangu Kim ambaye alikuwa pia ni rafiki wangu wa dhati kwani alinisaidia mambo mengi maishani. 

Urafiki ule ulikuwa wenye kutamaniwa na wengi kwani hata watu wengi walisema kuwa tulikuwa marafiki lakini hiyo ilikuwa ni propaganda isiyo na msingi wowote.

 Siku ziliposonga, Kim alifanikiwa kupata jiko na hapo ikawa urafiki wangu na wake ukaanza kudidimia kwa kuwa wakati mwingi alitumia kukaa na mke wake. Hatungepata tena wakati wa kwenda kutazama mechi, kulewa vilabuni na kadhalika. 


Kwa wakati ule wote sikuwa nimefanikiwa kuoa kwani nilidhani kwamba wakati wangu murua haukuwa umefika. Kwa mara nyingi nilitembelea nyumba yao tukapiga gumzo na hata kushiriki vyakula kwa pamoja.

 Kwa vile Kim alikuwa akifanya kazi ya bawabu wa usiku ilikuwa ni fursa muhimu kwangu kupata upenyo hadi nyumbani mwake kupiga gumzo na mke wake kwa wakati wowote.

 Nilifanya mazoea ya kuingia kwenye nyumba ya Kim kila wakati alipokuwa katika shuguli za kazi usiku. Mke wake alikuwa mrembo ajabu mtoto wa kidigo aliyeumbwa akaumbika na hapo damu ilinichemka.

 Mara nyingi tulizungumza hadi usiku wa manane lakini hakuna kitu kama uhusiano kilinukia kwa ajili ya uoga flani. Baada ya wiki hivi mazungumzo yetu yalianza kubadilika kwani tulianza kuzungumzia mambo ya mapenzi.

 Dada yule alinielezea bayana kwamba hakufurahia kazi ya mume wake ya bawabu wa usiku kwani hali ile ilimwacha akisononeka na mwenye upweke. Alisema kuwa alitamani mume wake aiache kazi ile lakini hakuwa na budi kwa kuwa pato lao lilitoka kwenye kazi ile. 

Nilifahamu fika kwamba alikuwa akizungumzia suala zima la lungula na hapo nilijiambia akilini kuwa ni mimi pekee nilikuwa shujaa wa kumwondolea upweke wake wakati wa usiku. Mapenzi yetu na mke wa Kim yalinoga kwani hata tulianza kushiriki uroda. 

Nilirauka asubuhi na mapema kabla mume wake hajaingia ili kuepuka magombano au vita kwani nilikuwa nakula tunda la wenyewe. Nilifanya kitendo hiki kwa muda wa wiki tatu hivi.

 Kim hakugundua lolote wala hakuuliza mke wake chochote na hii ilinipa fursa ya kujiita kinara katika shughuli nzima hii ya kutafuna mke wake.

 Nilifahamu kwamba Kim asingegundua chochote. Baada ya siku majuma kadhaa mambo yalianza kuenda mrama. Usaha ulinitoka kwenye sehemu yangu ya siri huku ukiandamana na vijidudu vidogo mithili ya funza. Niligutushwa na mambo haya kwani hata sehemu zile zilikuwa kubwa ajabu hata kuvaa suruali ndefu ilikuwa ni mapigano kwa ajili ya uchungu.

 Nilijiambia moyoni kwamba Kim alikuwa ametembelea mahali ili kukinga mke wake kutokana na anasa. Hili lilikuwa ni kweli baada ya Joseph rafikiye Kim kuniambia kwamba Kim alikuwa amemfunga mke wake kushiriki mapenzi na mume mwingine na kwamba daktari aliyefanikisha suala hili lote alijiita Kiwanga.

 Niliposikia yale maneno machozi yalinitiririka kwa mpigo. Nilimwelezea Joseph anielekeze kwa daktari Kiwanga ili nirejeshe mambo kuwa kawaida. Nilipofika kwa ofisi za daktari Kiwanga alisema kuwa mtu aliyekuwa na uwezo wa kutatua shida yangu ni mume wa mke niliyeshiriki mapenzi naye na iwapo tu ningemuomba msamaha basi mambo yangu yangekuwa shwari. 

Nilifunga safari na kurejea kwangu na hapo siku iliyofuatia nilipiga moyo konde na kumtafuta Kim ili nimwombe msamaha. 

Alikubali kuzika mambo hayo kwenye kaburi la sahau na hali ikarejea shwari. Tangu siku ile mimi huona wake wa watu kama sumu. 

Daktari Kiwanga ana uwezo wa kutatua migogoro ya mashamba, kumaliza swala zima la wizi na mengineyo. Anatibu magonjwa kama vile kifua kikuu, kifaduro, msukumo wa damu na mengineyo kwa siku tatu tu. 

Kwa mengi zaidi wasiliana na Dkt. Kiwanga kutumia wavuti www.kiwangadoctors.com au kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama pia unaweza kupiga simu/WhatsApp kwa nambari +254769404965 kupata usaidizi.

Share:

WATAALAMU 422 WA TANZANIA BARA, ZANZIBAR WAPATIWA MAFUNZO YA ANWANI ZA MAKAZI


Muonekano picha ya vongozi na wataalam waliopo kwenye vituo vinne vya mikoa ya Mwanza, Mbeya, Tanga na Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) wakati akifunga mafunzo ya anwani za makazi na postikodi kwa wataalam hao kwa njia ya mkutano mtandao wakati akiwa ofisi za TTCL, jijini Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dorosela Rugaiyamu akizungumza kwa njia ya mkutano mtandao (video conference) na wataalam wa Halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wakati Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi kulia)  akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu kwa ajili ya kutekeleza anwani za makazi katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TTCL, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza kwa njia ya mkutano mtandao (video conference) na wataalam kutoka Halmashauri mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu hao  ya utekelezaji wa anwani za makazi katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TTCL, jijini Dodoma.

***
 
Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog, DODOMA.
KATIBU  Mkuu , Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amefunga mafunzo ya utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi huku akiwataka wataalamu hao kwenda kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo kwa kuweka namba za nyumba, majina ya mitaa na barabara kwenye halmashauri wanazotoka.

Dkt.Yonazi amezungumza hayo leo Jijini Dodoma kwenye  mkutano baina yake na wataalamu hao uliofanyika kwa njia ya mtandao(video conference) yaliyofanyika kwenye vituo vinne vya mkoa wa Mwanza, Mbeya, Tanga na Zanzibar na kuongeza kuwa zoezi hilo kinapaswa kutekelezwa nchi nzima na kukamilika ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi utasaidia kufungua kasi ya uchumi, utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi na kuifungua Tanzania kidijitali.

"Mkafanye kazi kwa ufanisi,ikiwa zoezi hili litafanikiwa mwananchi yeyote atatambulika duniani na anaweza kufikiwa na mteja kwa ajili ya kuuza bidhaa au huduma, hivyo kila mwananchi awiwe kuwa na namba ya nyumba, jina la barabara au mtaa anapoishi,” amesema 
 
Mbali na hayo  ametoa wito kwa kampuni, wadau mbali mbali na familia kuchangia utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi na kila mmoja awe balozi wa anwani za makazi na wataalam watoe taarifa kwa viongozi wao na Wizara iko tayari kuendelea kushirikiana kutekeleza hili
 
Kwa upande wake  Mratibu wa Kitaifa wa Anwani za Makazi na Postikodi wa Wizara hiyo, Mhandisi Jampyion Mbugi, amesema kuwa wataalam waliopatiwa mafunzo hayo ni wataalam wawili kutoka kwenye kila halmashauri nchi nzima ambapo inahusisha wataalam wa TEHAMA, Ardhi, Mipango Miji na Ramani.

Amesema, wataalamu hao wamepatiwa mafunzo hayo kwa muda wa wiki moja
kuanzia  Januari 17 hadi Januari 23 mwaka huu yanayolenga  utekelezaji wa anwani za makazi na postikodi ikiwemo kuweka namba za nyumba, jina la mtaa au barabara na kuweka taarifa za maeneo hayo kwenye mfumo wa kielektroniki wa NAPA .

"Jambo hili ni muhimu sana kwa kuwa litawezesha  wananchi  kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta na kutunza muda ,"amefafanua.
 
Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya wataalam wengine waliopatiwa mafunzo hayo, Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Kilindi, Tanga ndugu Anastius Biswalo Manumbu amesema wamepatiwa mafunzo hayo kwa vitendo na wataenda kuwafundisha wataalam wengine ili kuhakikisha kuwa anwani za makazi zinakamilika kwa wakati kuendana na azma ya Serikali .

"Tunawashukuru sana wawezeshaji kwani  tumeiva na sasa tupo tayari kutimiza wajibu wetu kwa vitendo na tutazingatia miongozo iliyopo ya uwekaji wa anwani za makazi na postikodi,"ameeleza.
 
Ufungaji huo wa mafunzo ya anwani za makazi na postikodi nchini, umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vituo vinne ambapo mafunzo hayo yametolewa kwa kuwashirikisha  wawakilishi wa wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa mikoa ya Tanga, Mwanza, Mbeya na Zazibar ambapo kwa upande wa Zanzibar waliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ndugu Amour Bakari

Aidha katika mafunzo hayo  jumla ya wataalam  422 wamepatiwa mafunzo ambapo wataalam 389 wametoka Tanzania Bara na 33 wametoka Zanzibar .

Share:

MAMA AJITOLEA KUMZALIA MTOTO MWANAE


MAPYA yaibuka! Pichani Maree Arnold (54) kutoka Australia ameamua kumbebea mimba mwanae huyo wa kumzaa Meagan (28) hivyo kumzaa mjukuu wake wa kiume mwenye afya njema tarehe 13 mwezi huu.

Imekuwaje? Meagan akiwa na miaka 17 aligundulika kuwa hana mfuko wa uzazi(uterus) hiyo ina maana kwamba hata period haingii kila mwezi na kamwe asingeweza kuja kubeba mimba na kuzaa, hata hivyo licha ya changamoto hiyo lakini madaktari waligundua bado ovaries zake zinafanya kazi hivyo baadaye akiamua bado anaweza kupata mtoto wake mwenyewe (biological child) ikiwa atatokea mwanamke mwingine wa kumsaidia kumbebea mimba.

2015 akakutana na jamaa pichani ambaye kwasasa ni mumewe, jamaa alipojua changamoto za mkewe wakakubaliana watafute mwanamke wa kuwasaidia kuwabebea mimba (surrogate) ambapo alipatikana nchini Canada kupitia agency flani, mimba ilibebwa na surrogate lakini mtoto akiwa na wiki 21 akafariki kisha janga la corona lilipoingia ndio kabisa Meagan akaanza kukata tamaa maana ilikuwa ngumu hata kusafiri nje ya nchi.

Maree alipoona binti yake huyo hana furaha muda mwingi sababu ya kuamini hatakuja kupata mtoto wake mwenyewe maishani, akafanya utafiti kidogo na kuambiwa licha ya kuwa tayari yeye ana miaka 54 na alishazaa watoto 5 lakini bado anaweza kumsaidia kumbebea mimba mwanae huyo wa kumzaa.

Maree alienda hospitali kupandikizwa embryo (kiinitete) kilichotokana na yai la mwanae na mkwe wake, alipandikizwa mara tatu lakini zote haikufua dafu ikashindikana kwa mara ya nne ndio ikakubali.

Kwa umri wake wa miaka 54 Maree tayari alikuwa hedhi imeshakoma(menopause) hivyo kabla ya kupandikizwa mimba hiyo ilibidi madaktari wampe dawa za ku-reverse process ya menopause na kujaribu kuuboresha mfuko wake wa uzazi uweze kubeba mtoto tena.

Maree akizungumza amesema mimba hii ilimfanya achoke zaidi kulinganisha na miaka 22 iliyopita alipobeba mimba ya mwisho ya mtoto wake halisi, lakini amesema amejisikia fahari kumsaidia mwnaae na kama muda ungekuwa unarudi nyuma basi angejitosa kumbebea mwanae mimba ya mtoto mwingine.

Kwa upande wa Meagan kwasasa furaha yake hailezeki baada ya kufanikiwa kuitwa mama kwa mtoto ambaye ni damu yake, aidha, pia amemshukuru sana mzazi wake kumbebea mimba.
Share:

MABASI YASIYO NA DEREVA KUANZA KUFANYA KAZI


NCHI ya Norway imesema inajiandaa kuanza majaribio ya mabasi ya abiria (ya umma) ambayo hayana dereva, kuanzia mweiz Aprili, mwaka huu.

Mabasi hayo ya umeme ambayo yametengenezwa na Kampuni ya nchini Uturuki ya Karsan yana uwezo wa kubeba abiria 50 na yana urefu wa mita 8, siti 21 na eneo kubwa la watu kusimama na kwa sasa yameanza majaribio katika eneo la Forus Business Park kabla ya maeneo mengine.

Wakati wa majaribio kutakuwa na madereva kwenye magari hayo kwa ajili ya kusimamia usalama na kusaidia kuweka vitu sawa kama kutakuwa na changamoto lakini baada ya muda wa majaribio yatakuwa yanasafirisha abiria bila kuwa dereva.

Majaribio hayo yatafanyika kwa muda wa miaka miwili katika majiji, miji na wilaya mbalimbali za nchi hiyo kabla ya kuanza kazi rasmi na kuiongezea Serikali ya nchi hiyo kipato huku ikitarajia kupunguza gharama za uendeshaji.

Majaribio hayo ya kwanza makubwa Barani Ulaya yatafanywa na Kampuni ya Vy kwa kushirikiana na Kampuni ya Kolumbus kwa kutumia teknolojia ya AI (Artificial Intelligence) na sensa kutoka Kampuni ya Adastec na teknolojia ya ufuatiliaji (monitoring technology) kutoka Kampuni ya Norway ya Applied Autonomy.
Share:

AKAA KWENYE MATAIRI YA NDEGE SAA 11 ANGANI


JESHI la Polisi wa Uholanzi wanasema wamempata mtu akiwa hai katika sehemu ya gurudumu la ndege iliyotua katika uwanja wa ndege wa Amsterdam wa Schiphol kutoka Afrika Kusini.

Safari za ndege kutoka Johannesburg hadi Amsterdam huchukua takriban saa 11, huku ndege ya mizigo ikiaminika kusimama mara moja, jijini Nairobi, Kenya.

Si jambo la kawaida sana kwa wanaopanda ndege kimagendo kuishi, kutokana na baridi na oksijeni kidogo kwenye miinuko ya juu. Umri na utaifa wa mwanaume huyo bado haujabainishwa, polisi wanasema.

“Mwanaume huyo alipatikana akiwa hai katika sehemu ya gurudumu upande wa pua ya ndege na alipelekwa hospitalini akiwa katika hali nzuri,” msemaji wa Polisi wa Kijeshi wa Uholanzi Joanna Helmonds aliambia shirika la habari la AFP.

“Inashangaza kwamba mtu huyo bado yuko hai,” alisema.

Kwa mujibu wa mtangazaji wa Uholanzi NOS, joto la mwili wa mtu huyo liliongezeka katika eneo la tukio na wakati gari la wagonjwa lilifika, aliweza kujibu maswali ya msingi.

Msemaji wa idara ya shehena ya mizigo Cargolux alithibitisha katika barua pepe kwa Reuters kwamba mtu huyo alikuwa kwenye ndege inayoendeshwa na Cargolux Italia.

Kulingana na data ya ndege, ndege pekee ya Cargolux ya mizigo kutoka Johannesburg hadi Schiphol Jumapili pia ilisimama Nairobi.

 Haijulikani iwapo mwanaume huyo alipanda ndege hiyo nchini Afrika Kusini au Kenya.
Share:

Sunday, 23 January 2022

Video Mpya : NYANDA MADIRISHA OBHADO 'MALIGANYA' - BHUHANGWA


Ninakualika kutazama Video Mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado ' Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo kutoka Kahama mkoani Shinyanga inaitwa Bhuhangwa iliyotengenezwa na Director Manwell. 

Tazama Video hapa chini

Share:

WATOTO WATATU WAFARIKI KWA KULA UYOGA NZEGA



 Katika hali ya kustaajabisha, watoto watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kudaiwa kula uyoga unaodhaniwa kuwa na sumu katika eneo la Igombanilo, Nzega Mkoani wa Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema waliokula chakula hicho ni mama na watoto wake ambapo mpaka sasa mama na mtoto mmoja wanaendelea vizuri na wameruhusiwa kutoka Hospitali.

Kamanda Abwao amewataja waliofariki dunia ni Happiness Greyson, Annastazia Greyson na Maria Greyson.
Share:

WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WAUAWA DODOMA


Watu watano wa familia moja wamekutwa wakiwa wameuawa nyumbani kwao eneo la Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Antony Mtaka pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Onesmo Lyanga wamefika eneo la tukio usiku wa kuamkia leo ambapo miili ya watu hao imekutwa ikiwa ndani ya nyumba yao walimokuwa wanaishi ikiwa tayari imeharibika.

Waliouawa katika tukio hilo ni Baba, mama, watoto wawili na mjukuu mmoja.

Akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka amelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza uchunguzi mara moja ili kubaini watu waliohusika kufanya mauaji ya watu hao watano wa familia moja.


Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi kuhusu vifo hivyo, ikiwemo kubaini watekelezaji wa tukio hilo la kikatili.
Share:

Waziri Bashungwa: Wakandarasi Wazembe Kutopatiwa Kazi Za Tarura


Na. Angela Msimbira, Njombe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff kuwaorodhesha makandarasi wote ambao wako kwenye rekodi ya kutokufanya vizuri na wababaishaji kufutwa na kutofanya kazi za TARURA nchi nzima.

Ameyasema hayo mapema leo wakati akikagua barabara ya Igosi –Ujindile-Wangama yenye urefu wa kilometa 16.9 iliyopo kata ya Wangama katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe ambayo inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe kutokana na Fedha za Tozo ya Mafuta.

Waziri Bashungwa amesema kuwa Makandarasi ambao hawafanyi vizuri wasiwe wanahamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, badala yake wapewe kazi makandarasi ambao wanauwezo wa kufanya kazi kwa viwango na kasi inayotakiwa.

“Serikali ya Awamu ya Sita inataka kupeleka huduma kwa wananchi kwa kuboresha mawasiliano ya miundombinu ya barabara hasa vijijini, Rais wetu anataka kuiboresha TARURA ili iweze kuhudumia watanzania, Makandarasi wanaofanya kazi kwa mazoea hawahitajiki kwa sasa “, amesema Waziri Bashungwa

Waziri Bashungwa amesisitiza kuwa moja ya vitu ambavyo vitafanyika kwa Makampuni na Makandarasi wazembe na rekodi zinaonyesha ni wazembe ameelekeza apelekewe taarifa zao ili wasipatiwe kazi za TARURA kwani Serikali itafanya kazi na Makandarasi watakaofanya kazi kwa weledi na kukamilisha miradi kwa wakati na ameelekeza kuwepo kwa kanzidata kwa ajili ya Makampuni na Makandarasi ambayo yanafanya kazi vizuri ili waweze kupatiwa kazi za TARURA.

Amesisitiza kuwa lengo la kuanzishwa kwa TARURA nchini ni kuhakikisha inawasaidia wananchi wa vijijini katika Suala zima la ujenzi wa miundombinu ya barabara ili kuwasaidia watanzania ambao ni wakulima kuwafungulia fursa za kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi, hivyo ni wajibu kutumia makandarasi wanaofanya kazi kwa uaminifu na kuhakikisha miradi wanayopatiwa na Serikali inakamilika kwa wakati.

Akiwasilisha taarifa kuhusu ujenzi wa barabara hiyo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Mhandisi Boniface Kasambo ameeleza kuwa barabara ya Igosi-Ujindile-Wangama ni muhimu kwa wanachi wa eneo hilo kwa kuwa inatumika kusafirisha mazao ya biashara ikiwemo parachichi, viazi na mbao kutoka mashambani Kata ya Wangama na Igosi kupeleka katika masoko ya Njombe Mji na Makambako kupitia barabara kuu ya Njombe -Makete.

Mhandisi Kasambo amesema ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuanza hivi karibuni, umeidhinishiwa zaidi ya shilingi milioni 400 na utajumuisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe, kuchimba mifereji na kujenga makalati.


Share:

Saturday, 22 January 2022

SERIKALI INAENDELEA KUYABAINI MAENEO YA MACHIFU NA KUYATUNZA ILI YAWE VIVUTIO NCHINI-RAIS SAMIA


********************

NA EMMANUEL MBATILO, KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Utamadunu,Sanaa na Michezo kuendelea taratibu,kuvikuza na kuviendeleza VIKUNDI vya burudani za kitamaduni ili vizalishe kazi za mikono za utamaduni.

Ameyasema hayo leo Rais Samia wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni Kilimanjaro lililoandaliwa na uongozi wa machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Rais Samia amesema tayari Serikali imeanzisha kanzi data sahihi inayohusu machifu, na imeshaanza kuweka taarifa Sahihi za machifu na mchango wao katika kupamabana na ukoloni.

"Serikali inaendelea kuyabaini maeneo ya kichifu na kimila na kuyatunza ili yawe sehemu za vivutio vya nchi yetu na kuibua, kuimarisha na kuhifadhi majengo na zana za zamani ili zibaki kuwa vielelezo vya Utamaduni wetu ". Amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Paulina Gekul amesema kuna umuhimu mkubwa kwa Watanzania kuendelea kutunza tamaduni zetu na kuachana na tamaduni potofu zinazofanywa na baadhi ya watu.

Amesema Serikali kupitia Wizara yake watandelea kutoa ushirikiano kwa machifu kutunza na kuenzi tamaduni zetu.
Share:

PAKUA APP MPYA YA MALUNDE 1 BLOG UPOKEE HABARI NA MATUKIO KWA URAHISI KWENYE SIMU YAKO


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:

UKIPOTEZA MKEKA UNALIPWA: SOMA HAPA JINSI YA KUOMBA BONUS UKILOST MKEKA WAKO

Habari njema kwa wadau wa kubeti ambao hupoteza mikeka yao mara kwa mara hapa nitakueleza namna ya kuomba utumiwe bonus  kama malipo ya mikeka yako uliyopoteza

Ofa hii inapatikana ndani ya kampuni ya kubet ya 22bet

Masharti ya kupata bonus hii,

👉 Ni lazima uwe umejisajili na >>22bet>>

👉Uwe umepoteza angalau mikeka 20 mfululizo

👉Katika timu zote ulizopoteza  timu ziziwe na ods juu ya 3.0 maana kuna watu watachagua timu yenye ods 12 ili walost makusudi na kuomba bonus.

👉Mikeka yote uliyolost iwe imewekwa ndani ya siku 30 sio zaidi ya hapo.

👉 Kila mkeka uliolost  stake yake ianzie $2 sawa na kama 4700 

👉Kumbuka  unatakiwa kuomba bonus hii kwa account moja tu, ikiwa unamiliki zaidi ya account 1 hutopewa na watagundua kupitia IP adress

Does your series of losing bets meet all the requirements? Then email us at support@22bet.com  account number and putting "Series of losing bets" in the subject line.

Kama umetimiza vigezo hivyo tuma barua pepe, na sehemu ya subject jaza account namba yako  na idadi ya mikeka uliyopoteza  utapokea malipo yako ndani ya muda mfupi, kumbuka email itumwe   kwenda  support@22bet.com  

   kUJISAJILI NA 22BET BOFYA >>>HAPA>>


Share:

SIASA ZILINIPIGA CHENGA, NILIAMBULIA PATUPU LICHA YA KUMWAGA HELA


Ama kwa hakika siasa hapa nchini Kenya huwa na wenyewe jinsi watu wanavyosema. Kila mara nilipowaona wanasiasa wakishinda viti mbalimbali hapa nchini nilidhani ni swala rahisi tu bora kujieleza.

 Nilifikiria tu wakati unapofanya mkutano wa kisiasa na wakati mwingine umati mkubwa wa watu ujitokeze ilikuwa ishara tosha kwamba ungeshinda kiti kile lakini hii haikuwa kweli kwani umati labda ulikuwa umekuja kula hela zako ama kusikia ajenda zako na mara nyingi wao huwa na mtu wao ambao wangependa kumpigia kura. 


Ama kwa hakika ulikuwa ni mchezo mchafu na ulio na watu waliouelewa. Mwaka mmoja nilisimama kiti cha ubunge wa kaunti na nikaona maajabu. 

Nilikopa hela za kampeni na kuwamwagia vijana, wazee na watu mbalimbali kwa ajili ya umaarufu ile niibuke bigwa kwenye debe. Mambo yalienda mrama kwani niliibukia limbukeni na nikawa mkia kwenye kinyang’anyiro hicho.


 Sikuwa na chochote cha kujivunia kwani nilikuwa nimepoteza hela pamoja na muda wangu kwa wakati mmoja. Nilingojea miaka mitano baadae na nikajitoza kwenye kiwanja tayari kuonyesha makali yangu ana mara hii nilidhania eti kwa vile nilimaliza mkia wakati uliopita, raia wenye eneo wadi ile wangenihurumia na kunipa kura.


 Kampeni zilichacha na hapo nilifahamu fika kwamba mambo yalikuwa mazuri kwani vijana na akina mama waliniahidi uungwaji mkono. Kiongozi wa chama chetu mara hii alibnifadhili kwani ajenda zangu zilienda sambamba na manifesto ya chama.


 Kila nilipoenda mashinani, watoto kwa vijana kwa wanawake wote waliimba jina langu. Nilifahamu huu ulikuwa ni mwamko mpya kwenye shughuli zangu za kisiasa. Ama kwa hakika ilikuwa ni siku njema ilyoanza kuonekana mapema. Siku ya kupiga kura ilifika na hapo nilifurahishwa na idadi ya watu waliojitokeza. Wakati wa matokeo ulipofika, nilipigwa na butwaa kwani wakati huu pia nilikuwa wa mwisho. 


Aibu ilinikumba nisijue la kufanya. Kila mtu alinikejeli na kuniita majina matusi. Wengine walisema kuwa nilikuwa naharibu pesa zangu nikijitosa kwenye ulingo huu wa siasa. 


Atafutaye hachoki lakini kwa wakati huu nilikuwa nimefikia kwenye ukingo wa swala zima la siasa. Nilipatana na mbunge Flani ambaye jina lake nalibana. Nilimuuliza siri yake kwenye ulingo wa siasa na akanielezea kwamba daktari Kiwanga alimsaidia akashinda kiti hicho kwa mpigo. 


Siku iliyofuatia nilienda ofisini kwa daktari Kiwanga kwa ushauri na usaidizi kwani ilikuwa imebaki ni mwaka mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu. Nilirejea kutoka kwa daktari Kiwanga na kurejelea shuguli zangu za kampeni. Mara hii umati mkubwa ulijitokeza kunishangilia kwa kishindo. 


Jambo hili lilitia wapinzani wangu kiwewe kwani ilikuwa ni ishara tosha mambo yalikuwa yamebadilika kwa uwezo wa daktari Kiwanga. Mara nyingi wapinzani wangu walitafuta sababu za kuniharibia lakini kwa kweli wimbi nilikuwa nalo kwa wakati ule.

 Hela nilimwaga kama ilivyokuwa kawaida yangu ili kuwarai raia waweze kunipigia kura. Siku ya kupiga kura ilipowadia nilijihisi kama niliyekuwa na mwamko mpya maishani. Nilipiga kura yangu asubuhi na mapema na nikarejea nyumbani kupumzika huku nikongoja matokea na mara hii nilikuwa na matumaini kuwa ningeibukia mshindi. 


Wakati wa matokea uliwadia na nilikuwa nimeketi ukumbini nikiwa ange kujua yote yaliyojiri kwenye uchaguzi ule. Matokea yalianza na hapo nilitangazwa kama mshindi na mbunge wa wadi. Nilipokezwa cheti kwa mpigo. Hakuna yeyote aliyepeleka kesi mahakamani kupinga kuchaguliwa kwangu kama mbuge wa wadi ile kwa wakati wowote. 


Ama kwa hakika daktari Kiwanga alikuwa ameimarisha azma yangu ya kuwa mwanasiasa. Daktari Kiwanga ana uwezo wa kusuluhisha mizozo ya ndoa,biashara kunawiri, kushinda kesi kotini na mengineyo. Ana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali kama vile kifua kikuu, kifafa, kifaduro na mengineyo kwa siku tatu pekee. Waweza kumpata Dkt. Kiwanga kupitia wavuti www.kiwangadoctors.com barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au piga simu kwa nambari +254769404965.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger