Monday, 27 September 2021
Tanzia : NAIBU WAZIRI WILLIAM OLE NASHA AFARIKI DUNIA
DAKTARI ATUPWA JELA KWA KUMDUNGA MKEWE SINDANO YA MAPEPO

RAIS SAMIA AMUAPISHA MATHEW KIRAMA KUWA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA NA BALOZI MHE. TOGOLANI MAVURA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mathew Modest Kilama kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 27 Septemba, 2021.


MBUNGE AWATAKA WANAWAKE KUKATAA MAHUSIANO YA KINGONO NA WANAUME AMBAO HAWAJAFANYIWA TOHARA
DAKTARI AWAUA WATOTO WAKE WAWILI KWA KUWACHOMA SINDANO

TADB yatoa mkopo wa milioni 436 ujenzi kiwanda kusindika korosho Tanga
Na Mwandishi Wetu, Tanga
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeidhinisha mkopo wa kiasi cha shilingi 435,500,000/- kwaajili ya uanzishwaji wa kiwanda kidogo cha kusindika korosho ili kuliongezea thamani zao sambamba na kuongeza pato la taifa pamoja na kuinua pato la mkulima..
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Ubunifu katika mnyororo wa thamani wa zao la Korosho chini ya Taasisi ya Care Tanzania wilayani Mkinga,Jijini Tanga, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TADB,Bw Jeremiah Jeremiah Mhada alisema kuwa benki hiyo imeidhinisha mkopo huoambapo zitatumika katika ujenzi wa kiwanda na ununuzi wa mashine na vifaa mbalimbali za kuendesha kiwanda hicho.
“Fedha hizo zitatoka kwa awamu ikiwa ni kujenga miundombinu ya kiwanda na awamu ya pili kufadhili wakulima wa korosho pembejeo zitakazowawezesha kuzalisha korosho kwa tija na kupata bei nzuri sokoni,” alisema Bw.Mhada
Alieleza kuwa fedha ziizotolewa zitakwenda kusaidia katika kutengeneza ajira kupitia kazi ya ujenzi wa majengo ya kiwanda pia kukiwezesha kiwanda Mtaji wa kununua korosho kutoka kwa Wakulima wadogo wa Kilimo Viwanda Sigaya Limited.
“TADB imetoa mkopo huu kwa lengo la kuongeza thamani ya zao la korosho hali itakayopelekea kuongezeka kwa mapato ya wakulima wa korosho Wilayani Mkinga, alisema Bw.Mhada na kuongezea kuwa kiwanda hicho kitaongeza thamani ya zao na kuhamasisha wakulima kufanya kilimo cha korosho kutokana na uhakika wa soko.
Bw .Mhada alisisitiza kuwa majukumu ya TADB ni kuhakikisha mageuzi yanafanyika katika sekta ya kilimo na kuwabadilisha wakulima kutoka kilimo cha mazoea na kufanya kilimo biashara na kuwafanya waweze kupita hatua kiuchumi kupitia shughuli za kilimo na kuwaunganisha na masoko kupitia chama cha msingi cha ushirika cha DUGA.
“Uchakataji wa korosho hapa nchini utasaidia kuzalisha bidhaa nyingine kama mafuta kwa asilimia 15 ambayo hutumika kama dawa na matumzi ya viwandani jambo litakalopelekea kuongeza thamani ya zao la korosho hapa nchini,” alisema
Alieleza kwa sasa mafuta ghafi ya korosho yanauzwa katika soko la Umoja wa Ulaya, Marekani, Japan, Korea ambapo wasambazaji wakuu ni India na Brazil. Hivyo tukiweza kuzalisha wenyewe mafuta haya Tanzania itakuwa miongoni mwa wasambazaji wakuu wa bidhaa hiyo Duniani.
“Kwa mujibu wa ANSAF mwaka 2016/17 Tanzania ni namba 3 kwa uzalishaji wa korosho Duniani, sasa hivi ipo namba 4 kwa Afrika ambapo zaidi ya asilimia 90 inasafirishwa kama malighafi,” alisema Bw.Mhada
“TADB tutaendelea kuhamasisha kuongeza na kukuza uzalishaji nah ii ni muendelezo wa uwekezaji wa zaidi ya bilioni 33 ambazo zimetolewa katika mnyororo wa thamani wa uzalishaji, alieleza Bw.Mhada
Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha DUGA, Bw.Said Hassan Tuwano aliishukuru benki ya TADB pamoja na Wawekezaji walioamua kuwekeza katika Wilaya yao na kusema hii imeonyesha dhamira ya dhati ya kusaidia wakulima wadogo nchini.
“Nashukuru zaidi kwa kutupa asilimia 45 ya hisa kwenye kiwanda hivyo zaidi ya wakulima 200 tutakuwa sehemu ya kiwanda na tumejipanga kuhakikisha tunaongeza idadi ya wakulima mpaka kufikia 2,500 katika Wilaya yetu ili tunufaike wote,” alisema Bw.Tuwano
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Kanali Maulid Surumbu aliwataka wadau wote kutekeleza majukumu yao kuhakikisha uzalishaji wa zao la korosho unaongezeka pia kuhakikisha kiwanda kinakamilika ili uzalishaji uanze msimu ujao wa mavuno.
“Tunachotaka kutoka kwenu ni uwazi na uwajibikaji, niwahakikishe Serikali ipo pamoja na nyinyi kutoa mchango ili kuhakikisha tija katika uzalishaji inaongezeka na kufanya korosho yetu izidi kukubalika katika soko la ndani na masoko ya kimataifa jambo litakalo ongeza kipato kwa wakulima Wilayani Mkinga,” alisema Kanali Surumbu.
Rais Samia Awaasa Viongozi ALAT kutoa elimu ya Uviko 19
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa serikali za mitaa kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 kwa wananchi.
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi hao kutotumia mabavu katika utoaji wa chanjo bali kuwaelimisha wananchi wapate chanjo kwa hiari.
Rais ametoa kauli hiyo leo Septemba 27, 2021wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya serikali za mitaa- ALAT Taifa Mkoani Dodoma.
“Tulisema hili jambo ni la hiari, ukipita nyumba kwa nyumba anayetaka mchome asiyetaka usichome Lakini kubwa ninalotaka kusema mtu ana hiyari ya kukubali au kukataa na kama ana elimu ya kutosha ,hawezi kukataa”
Katika mkutano huo maalum Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi hao kushirikiana na kuondoa tofauti Zao ambazo nyingi hutokana na maslahi binafsi.
Serikali Yaitaka TPA Na Mscl Kuandaa Maegesho Ya Meli Ya Mv Mwanza Hapa Kazi Tu
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuandaa miundombinu ya maegesho ya meli kwa ajili ya meli mpya ya MV MWANZA “Hapa Kazi Tu” inayojengwa katika Bandari ya Mwanza.
Akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa meli hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema kuwa kazi za ujenzi wa meli hiyo kwa sasa zimefikia asilimia 53.8 na ifikapo mwezi Aprili, 2022 meli hiyo itaingizwa majini kwa mara ya kwanza na kuendelea kumaliziwa ujenzi wake ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2022 na baadae kufanyiwa majaribio na kukaguliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kabla ya kuanza kutoa huduma.
“Meli hii ni kubwa kuliko meli zote zinazofanya safari katika Ziwa Victoria kwani ina urefu wa mita 92.6, upana mita 17 na kimo mita 20, hivyo MSCL kwa kushirikiana na TPA hakikisheni miundombinu ya maegesho kwa ajili ya meli hii inaboreshwa ili meli itakapokuwa tayari iweze kuanza kazi mara moja kwani meli hii ni inatarajia kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma za usafiri wa maji katika Ziwa Victoria” amesema Kasekenya
Ameongeza kuwa hadi kufikia sasa Serikali tayari imemlipa mkandarasi zaidi ya asilimia 70 na kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo na kwamba kwa sasa kazi ya ujenzi wa meli hiyo inaendelea vizuri.
Aidha, Mhandisi Kasekenya amesema kuwa meli hiyo itakapokamilika itafungua fursa za kiuchumi na kibiashara kati ya jiji la wa Mwanza, mikoa jirani ya Musoma, Bukoba kupitia Bandari ya Kemondo Bay pamoja na nchi jirani za Uganda na Kenya.
Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Philemon Bagambilana amemueleza Naibu Waziri Kasekenya kuwa ujenzi wa meli ya MV MWANZA “Hapa Kazi Tu” unagharimu dola za kimarekani milioni 39 sawa na shilingi Bilioni 89.7 na umeenda sambamba na ujenzi wa chelezo kipya kinachotumika kwenye ujenzi wa meli hiyo ambacho pia kimegharimu dola za Kimarekani milioni15.
Bw. Bagambilana ameongeza kuwa Kampuni yake imekwishakamilisha ukarabati wa meli ya “New Victoria Hapa Kazi Tu” kwa gharama ya Shilingi Bilioni 25.5 na “New Butiama Hapa Kazi Tu” kwa Shilingi Bilioni 5.7 na tayari meli hizo zinaendelea kufanya kazi katika Ziwa hilo.
Naye, Kaimu Meneja wa Bandari ya Ziwa Victoria, Bw. Vicent Steven, amemueleza Naibu Waziri Kasekenya kuwa tayari TPA imeshafanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kupanua na kuboresha miundombinu ya maegesho yote yatakayopokea meli hiyo na kwamba kwa sasa wako kwenye hatua za manunuzi yatakayo wezesha kumpata mkandarasi atakayeifanya kazi hiyo.
Meli mpya ya MV MWANZA “Hapa Kazi Tu” inajengwa na wakandarasi kutoka kampuni ya GAS Entec Company na KANGNAM Corporation za Korea Kusini na itakapokamilika inatarajiwa kuwa na madaraja sita (6) yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200, magari madogo 20, magari makubwa 3 pamoja na mizigo tani 400 na hivyo inatarajiwa kuwa meli kubwa kuliko zote katika Ziwa Victoria.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
AOMBA APEWE DHAMANA MAHAKAMANI BAADA YA SEHEMU ZAKE ZA SIRI KUPOTEA

“Hakimu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mtoto wa Shekhe, Ustadhi huyo alinionya sana kuachana na Binti yake lakini sikusikia ndio chanzo cha sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti shamba kutuliza maumivu”.
Kutokana na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa Kompyuta akaguliwe na baada ya askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.
Hata hivyo Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa kumpata na kumtaka avumilie kwakuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shekhe alimuonya aachane na Binti yake akakaidi, Kesi iliahirishwa na itasikilizwa tena leo September 27,2021.
RAIS SAMIA ATANGAZA RASMI MADIWANI KUANZA KULIPWA POSHO KILA MWEZI
HII NDIYO FAIDA YA KU - RESTART SMART PHONE YAKO

BAADA YA KUCHEKWA SANA NA MAJIRANI, SASA BIBI YANGU ANAZAA

Naitwa Mohamed Peter mzaliwa wa Kijitopanga kule Tanzania ambako familia yangu pia imekita mizizi.
Nilimpata mrenbo flani ambaye tulianza maisha naye lakini kuna jambo moja lililotusumbua kwa muda mrefu. Tatizo hilo ni la kupata watoto.
Tumetafuta mtoto tangu mwaka jana lakini hatujafanikiwa. Mimba ya kwanza ilitoka kisha ya pili pia ikatoka tukabaki kwa masononeko.
Sijajua ni nini hasa mbaya lakini nilimpeleka bibi hospitalini ili afanyiwe uchunguzi lakini suluhu haikupatikana na ikafika wakati wa kuanza kulaumiana naye.
Nilimuambia kila mara simtaki sababu hawezi nizalia watoto hata nikamfukuza na akaenda kwao. Bila kuficha, amekuwa kwao kwa muda wa miezi nane nilipoambiwa anahudhuria matibabu ya kienyeji kwa daktri Kiwanga.
Hata nilipoambiwa hilo nilipuuzilia mbali lakini dadaangu akaniambia nitafute huyo bibi haraka huenda akafanikiwa kupata mtoto baada ya kupata matibabu kwa Kiwanga.
Kwa sababu nilimuheshimu dadaangu huyo nilimtuma amuite bibi yangu arudi. Na la kushangaza aliporudi tumekuwa naye kwa muda wa mwaka mmoja na tayari tumepata mtoto.
Kiwanga Doctors ni madaktari wa kiasili ambao wanaweza kutatuwa changamoto nyingi kama uzazi utasa na kadhalika. Tunapoongea nawe sasa hivi tunatafuta mtoto wa nne na maisha yetu ya ndoa inanawiri bila mvutano.
Kiwanga nimewaaamini. Kama unajuwa una matatizo na mapenzi, ndoa, kazi, cheo na magonjwa kwa nyumba yako mbona usitafute matibabu ya Kiwanga? Kiwanga Doctors ni shujaa wa mambo yote. Tuvuti au Website yao ni: www.kiwangadoctors.com; Simu: +254 769404965 au wasiliana kwa barua pepe yaani Email kwa: kiwangadoctors@gmail.com.
Sio lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi.
Sales Specialist (SA) at Alistair Group
Sales Specialist (SA) Are you someone with a “hunger for growth”, a “whatever it takes mentality” and understand the advantages of a team environment and what it takes to thrive in one? Are you someone who “Questions things” and “looks for improvements”? Do you have experience in taking a fast growing business to a […]
This post Sales Specialist (SA) at Alistair Group has been posted by Udahiliportaldaily
Get more post by visiting Udahiliportal.com
know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Social Performance Manager at Dangote
Description Develop, implement and maintain a consistent strategy on stakeholder’s engagement establishing cordial relationship with host communities and other relevant stakeholders. Key Duties and Responsibilities Manage, direct and inspire a team of independent professionals in order to achieve Departmental goals Manage identification, mapping and proactive engagements with stakeholders Negotiate and manage Community Development […]
This post Social Performance Manager at Dangote has been posted by Udahiliportaldaily
Get more post by visiting Udahiliportal.com
know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
MAZISHI YA ASKARI POLISI ALIYEFARIKI AKISHANGILIA MECHI YA SIMBA NA YANGA KUFANYIKE KESHO








Media and Communications Coordinator at Children in Crossfire
NOW RECRUITING TO DELIVER AN EXCITING EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT (ECD) NATIONAL PROGRAM! Children in Crossfire is a registered charity in Ireland that facilitates International Development and Development Education/Public Engagement activities. Our vision is a compassionate world where every child can reach his or her potential. We work in partnership with local organisations in Tanzania and […]
This post Media and Communications Coordinator at Children in Crossfire has been posted by Udahiliportaldaily
Get more post by visiting Udahiliportal.com
know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Senior Specialist Monitoring, Evaluation And Learning (MEL) at Children in Crossfire
NOW RECRUITING TO DELIVER AN EXCITING EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT (ECD) NATIONAL PROGRAM! Children in Crossfire is a registered charity in Ireland that facilitates International Development and Development Education/Public Engagement activities. Our vision is a compassionate world where every child can reach his or her potential. We work in partnership with local organisations in Tanzania […]
This post Senior Specialist Monitoring, Evaluation And Learning (MEL) at Children in Crossfire has been posted by Udahiliportaldaily
Get more post by visiting Udahiliportal.com
know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details







