DAKTARI mmoja nchini Uingereza ambaye ni raia wa Misri, Hossam Metwally amehukumiwa kwenda jela miaka 14 baada ya kukutwa na hatia ya kumdunga mke wake sumu akiwa katika harakati za ‘kumuondoa mapepo’ yaliyokuwa yakimsumbua.
Hossam mwenye umri wa miaka 34, alipewa adhabu hiyo baada ya kumdunga mke wake Wilson sindano ya sumu aina ya Nicortin kwa lazima akidai anamtoa mashetani nyumbani kwao katika eneo la Grimsby.
Kufuatia ushahidi uliotolewa katika Mahakama ya Sheffield, Metwally alidaiwa kumshutumu mke wake kuwa na ‘majini ndani ya mwili wake.
Daktari huyo alipatikana na makosa nane ikiwemo kujaribu kumuua mke wake, ulaghai na pia kutazama picha za utupu baada ya kunaswa na kamera za siri alizoziweka katika ndani ya kliniki yake ya kibinafsi.
Metwally alikamatwa baada ya Wilson kupatikana akiwa mahututi na kupoteza fahamu mnamo Julai 4, 2019 na kulazimka kulazwa.
Kufuatia uchunguzi uliofanywa na polisi, ilibainika kuwa kiwango kikubwa cha sumu za nircotics, zikiwemo zile za aina ya ketamine, propofol na fentanyl zilitumika.
Hata hivyo, jambo la kushangaza zaidi ni kwamba daktari huyo bingwa wa upasuaji, hakuonyesha kujutia kitendo hicho alipokuwa akijitetea kortini.
0 comments:
Post a Comment