Monday 27 September 2021

AOMBA APEWE DHAMANA MAHAKAMANI BAADA YA SEHEMU ZAKE ZA SIRI KUPOTEA

...

 

Mshtakiwa Faraji Ramadhani mwenye umri wa miaka 27 ameiomba Mahakama imruhusu ajidhamini mwenyewe kutokana na sehemu zake za siri kutoweka hivyo kupata maumivu makali anapokuwa Mahabusu.

“Hakimu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mtoto wa Shekhe, Ustadhi huyo alinionya sana kuachana na Binti yake lakini sikusikia ndio chanzo cha sehemu zangu za siri kupotea, nikiwa nyumbani natumia dawa za miti shamba kutuliza maumivu”.

Kutokana na malalamiko hayo Hakimu Manase aliamuru mtuhumiwa huyo aliyefikishwa Mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa Kompyuta akaguliwe na baada ya askari kumkagua ilibainika anachokisema ni kweli.

Hata hivyo Hakimu Diana Manase wa Mahakama hiyo ya Mwanzo Jijini Mbeya aligoma kumruhusu kujidhamini kwa madai akitoroka hawezi kujua wapi kwa kumpata na kumtaka avumilie kwakuwa tatizo kalitafuta mwenyewe maana shekhe alimuonya aachane na Binti yake akakaidi, Kesi iliahirishwa na itasikilizwa tena leo September 27,2021.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger