Tuesday 28 September 2021

SHIRIKA LA C4C LATAMBULISHA MABALOZI NA WADAU KUSHUGHULIKIA MASUALA YA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

...

Na  Mapuli Misalaba, Shinyanga
Shirika la Citizens 4 Change (C4C) Jamii kwa ajili ya Mabadiliko limewatambulisha mabalozi na wadau mbalimbali zaidi ya 70  watakaoshughulikia masuala ya ukatili kwa wanawake na watoto  katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 
Kikao hicho kimejumuisha  viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya ulinzi na usalama kwa watoto pamoja na wanawake  ili kuwatambulisha na kuwapa maelekezo ya hatua ambayo wanapaswa kuanza nayo katika kukomesha ukatili kwa watoto na wanawake 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mipango na Utaratibu Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Idara ya  maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale amewaomba wadau hao kushirikiana na serikali katika kukomesha ukatili kwa wanawake na watoto kwa kupata matokeo ya kumaliza ukatili unaofanyika hasa katika wilaya ya Shinyanga mjini.

“Ninyi sasa ni viongozi tunaomba mtatusaidia sana iwe ni Halmashauri ya mfano kwa masuala ya ukatili kwa watoto na wanawake kuyamaliza ili viongozi wengine waje kujifunza kutoka kwenu nawaomba mshirikiane na serikali katika kufanya kazi”,alisema

Kwa upande wake Dkt. Kate Mcalpine ambaye ni Kiongozi na Mtaalamu wa utafiti wa ukatili kwa wanawake na watoto Shirika la Citizens 4 Change (Raia kwa ajili ya mabadiliko) amesema lengo la Shirika hilo kufika Mkoa wa Shinyanga ni kumaliza ukatili na kuonesha njia nzuri ya kulinda usalama wa watoto na wanawake.

“Nia yetu ni kuonesha kwamba watu wa Shinyanga waseme sasa ukatili basi lakini tunataka tuoneshe njia ya nzuri ya kulinda usalama kwa watoto na wanawake njia hii ipo moyoni mwetu “amesema Dkt. Kate 

Dkt. Kate amesema Shirika la Citizens for Change lipo nchi ya Tanzania na Uganga ambapo linafanya kazi kwa kutumia njia ya ujumbe kuwasiliana na watu ambao wanania ya kulinda usalama wa watoto na wanawake ili kutatua ukatili kwenye jamii 

Amewaomba wananchi wote kujisajili  na shirika la Citizens 4 Change (C4C) kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *149*46*11#  ambapo amesema huduma hii ni bure kabisa ili kuwa raia anayewalinda watoto na wanawake dhidi ukatili.

Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Muhoja amesema baadhi ya maeneo ukatili umepungua ambapo amesema changamoto kubwa ni mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni   amewataka wananchi kuacha matendo ya ukatili .

“Kwa hali ya ukatili katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa sasa ukatili umepungua na ukatili mkubwa ambao upo kwa sasa hivi ni mimba za utotoni pamoja na ndoa za utotoni nitoe wito kwa wananchi tuache matendo ya ukatili kwa sababu ukatili hauna faida na wale ambapo wanaendelea kufanya majirani watoe taarifa mapema sehemu husika ili kuwashughulikia hao watu”,amesema

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger