Sunday, 25 April 2021
TSC QUEENS BINGWA BONANZA LA MEI MOSI






Na Veronica Simba - TSC
Timu ya Mpira wa Pete kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC Queens), imetwaa ushindi wa kwanza katika bonanza maalum la michezo kwa Taasisi za Serikali, lililofanyika Aprili 24 mwaka huu, jijini Dodoma.
TSC Queens ilitwaa ushindi huo baada ya kuwabwaga washindani wao kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa waliochuana nao vikali katika ngazi ya fainali kwa magoli 25 kwa moja.
Awali, Timu hiyo machachari ilipambana na Timu kutoka Wizara ya Fedha na kufanikiwa kuwachakaza mabao 29 kwa 05, hatua iliyowawezesha kufuzu kuingia ngazi ya fainali.
Akizungumzia siri ya ushindi huo wa kishindo, Mlezi wa TSC Queens ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimaliwatu, Shani Kamala alisema ni kutokana na kujituma katika kufanya mazoezi ya mara kwa mara.
“TSC tunathamini michezo kwani tunaamini ina mchango mkubwa katika kujenga afya za watumishi wetu. Ndiyo maana sisi kama viongozi tumeweka mikakati ya kuhakikisha watumishi wanafanya mazoezi mara kwa mara na kushiriki katika michezo mbalimbali,” alifafanua.
Wakati huohuo, Timu ya Mpira wa Miguu kutoka TSC (TSC Sports Club) waliibuka washindi wa tatu baada ya kuwachabanga mikwaju 5 ya Penalti wapinzani wao ngazi ya nusu fainali, Timu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa ambao waliambulia mikwaju 2 tu.
Kwa upande wake, Kapteni wa TSC Sports Club, Bitwalihat Magota amesema kikosi chake Kiko vizuri isipokuwa wanahitaji kuongeza zaidi mazoezi na mbinu za kimchezo.
Bonanza hilo liliandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi, ambayo huadhimishwa tarehe moja ya kila mwezi Mei.
Saturday, 24 April 2021
SIMBA SC YAPAA KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA...YAITWANGA GWAMBINA FC 1-0 MISUNGWI
MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WAANDAMANA

MCHEZAJI WA SOKA SOSPETER MAIGA AFARIKI DUNIA AKIFANYA MAZOEZI MUSOMA MJINI
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ASHIRIKI MKUTANO WA 37 WA DHARURA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KWA MTANDAO.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof Shukran Manya (kulia) na Mkurugenzi Mkurugenzi Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara Bw. Ali Gugu (kushoto) wakishiriki Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akisikiliza kwa makini mjadala wakati wa Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof Shukran Manya ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 23 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Mkutano huo wa 37 ulilenga kujadili uendelezaji wa Sekta ya Viwanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia maelekezo yaliyopita ya Wakuu wa Nchi na Baraza la Mawaziri la Jumuiya kupitia mikutano mbalimbali iliyopita na kwa kuzingatia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha, Mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zote sita (6) Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Sudani Kusini ulikuwa chini ya uenyekiti wa Jamhuri ya Kenya na Katibu wa Mkutano huo alitoka nchi ya Burundi.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), aliyeambatana na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof. Shukurani Manya (Mb.) ulijumuisha Maafisa Waandamizi kutoka Wizara za Viwanda na Biashara; Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Kilimo; Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) na Wizara Madini.
Pia, Mkutano huo wa 37 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ulitanguliwa na mkutano ngazi ya Watendaji Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika sekta hizo uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 22 Aprili, 2021 na ngazi ya Wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mahsusi katika eneo la Viwanda uliofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 20 hadi 21 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, uliopo katika Mji wa Magufuli Mtumba, Jijini Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya wataalamu katika mkutano huo uliongozwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na ulihudhuriwa na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Madini, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Chama cha wazalishaji nguo na bidhaa za nguo Tanzania (TEGAMAT) na Mfamasia Mkuu wa Serikali.
SITAKI WALA SITAMANI KUITWA MWANAUME MASURUALI TENA MWAKA HUU
Niliweza kupata GPA ya 3.5 kutoka chuoni kwangu.Nilitafuta kazi kwa mwaka mmoja bila mafanikio ila sikuweza kukata tamaa kwa sababu nilikuwa na vigezo vya kutosha kupata kazi nzuri.
Kulingana siku zinasonga mbele ilinibidi nipate mwenza wangu wa kuishi nae na family yangu ilisimamia Harusi yangu mwanzo hadi mwisho.Tuliishi na amani na upendo na mke wangu nikiwa bado nazidi kutafuta ajira.
Mungu si Athumani niliweza ajiriwa kwa department ya IT (Information Technology) katika kampuni flani hapa Jijini. Nilichapa kazi kwa bidii kubwa sana ili niweze kupata hata cheo kwa sababu mshahara wangu ulikuwa hautoshi kabisa kulingana na mahitaji yangu.
Hali yangu ilikuwa ngumu sana kimaisha na mke wangu kabadilika ,amani na upendo ukakosekana kwa nyumba kisa sina pesa ya kuacha hata nyumbani kwa ajili ya kupata chakula.
Mke wangu alikuwa akaniomba pesa ya Saloon ili apendeze sina kila kukicha maisha yangu baada ya kusonga mbele kimaendeleo yalikuwa yanarudi nyuma.Niliweza kubana pesa yangu na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ila pesa bado haionekani,sababu kubwa zaidi nilikuwa nafanya kazi mbali sana na ninapoishi ,nilikuwa napanda gari 2 tofauti kufika kazini na 2 tofauti kurudi nyumbani.
Nusu ya mshahara wangu ulikuwa unaishia katika usafiri.Mwisho wa mwezi nikipokea mshahara wangu najikuta nina madeni katika maduka mbalimbali hapa mtaani kwangu.Nilikuwa najitahidi kulipa hivyo kabla ya kufika katikati ya mwezi mimi pesa sina tena.
Mke wangu aliweza kunivumilia kwa kila namna ila ilifika hatua ndiyo akasema, Sitaki wala sitamani kuishi na mwanaume masuruali mwaka huu.
Ni baada ya kutoka kazini ndipo aliniambia kuwa mtoto wetu anaumwa hivyo inahitajika kuchukuliwa Hospitali ndiyo nikasema sina pesa,iliniuma sana lakini sikuwa na namna lazima nimwambie ukweli kuwa mfukoni sina chochote.
Ndipo nikampiga rafiki yangu Datius ili anikope Tshs 100,000 Datius arinitumia TShs 200,000 wakati niliomba Tshs 100,000 Nilikutana na Datius University na baada ya masomo alifanikiwa kufanya kazi katika kampuni ya Vodacom mkoa wa Tanga kama meneja.
Kesho yake niliamua kufungua moyo wangu na kumwambia rafiki yangu kuwa nimefanya kazi kwa miaka 3 sasa ila sipanishwi cheo kazini kwangu. Mshahara wangu mdogo na mambo mengine.
Rafiki yangu alinieleza mtu ambaye alimsaidia kupata nafasi ya kuwa Meneja wa mkoa wa Tanga akiwa bado kijana mdogo hata bila kufanya kazi kwa kampuni hiyo kwa muda mrefu. Alinipatia namba hii +254 769404965 ya Dr. Kiwanga nikajieleza kadiri nilivyoweza,pia Dr. Kiwanga akaniuliza maswali kidogo kuhusu kazini kwangu nikamjibu pia.
Hapo Dr. Kiwanga ndiyo alisema kuwa atanisaidia na Promotion spell na kuniambia ndani ya masaa 24 nitakuwa nimepata majibu sahihi. Baada ya chakula cha mchana Boss alikuja kwa Department yetu na kutupa taarifa kuwa tuna kikao saa 4:30 za jioni.
Muda ulipotimia wote na department mbalimbali tulijumuika na kusubiri kipi Boss anataka kusema. Ndipo alipoanza kutuambia kuwa Meneja wa kampuni amehamishiwa mkoa wa Pwani kulingana na mambo ya family na atakaye chukua nafasi yake ni Dickson Kato ambaye ni mimi.
Nilishtuka na kufurahi sana,nikasimamishwa ili niweze kutoa neno nikatoa na kutoa ahadi mbalimbali kwa kampuni. Baada ya wiki 2 nikapewa nyumba pamoja na gari. Maisha yangu kwa sasa yamejaa furaha na upendo.
Natoa shukrani zangu za dhati kwa kiwangadoctors bila kusahau rafiki yangu Datius. Dr. Kiwanga aliniambia anaweza kusaidia mtu akiwa mbali bila kufika ofisini kwake Kenya-Nakuru. Pia alisema kuwa anatatua shida mbalimbali kama Kurudisha mpenzi,kuwa na mvuto kwa mwanaume,kuinua biashara yako,nguvu za kiume,kupata mimba kwa waliokosa,kunasa mwizi na Kusafisha Nyota.
Unaweza kumpata Dr. Kiwanga kwa kumpigia/WhatsApp +254 769404965 au tembelea website yao www.kiwangadoctors.com
JITIBU TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KUTUMIA FULL POWER.. UUME MDOGO ZAT 50 NDIYO SULUHISHO
Zanzibar yasitisha safari za baharini
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesitisha usafiri wa baharini na shughuli nyinginezo za baharini kuanzia leo Jumamosi, saa tatu asubuhi hadi pale taarifa nyingine zitakapotolewa na mamlaka husika.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema serikali imefikia uamuzi huo ili kuchukua tahadhari ya dhidi ya Kimbunga Jobo.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kimbunga hicho kipo umbali wa kilomita 200 kutoka Kisiwa cha Mafia kikisafiri kwa kasi ya kilomita 18 kwa saa.
TMA imeeleza kuwa kasi hiyo imepungua kutoka ile iliyokuwa ikitarajiwa kutokana na kimbunga hicho kuingia katika mazingira yenye upepo kinzani.
Waziri Biteko Atoa Wito Mabenki Ya Ndani Kuungana Kukopesha Wawekezaji
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampuni kubwa na ndogo zinazowekeza kwenye sekta ya madini.
Waziri Biteko ametoa wito huo tarehe 23 Aprili, 2021 alipokutana na uongozi wa juu wa Benki ya NMB uliofika kwa nia ya kutaka kujua maeneo ya ushirikiano baina ya wizara na benki hiyo ili waweze kushiriki katika kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini kwa kutoa mikopo kwa wawekezaji hao.
“Niwasihi sana ndugu zangu, unganeni mfanye kazi kwa pamoja Benki hii itatoa asilimia 20 nyingine 30, 40, 10 kwa mwekezaji na hivyo manufaa ya uwekezaji kupitia sekta ya madini yataonekana zikikopwa nje ya nchi manufaa wanapata mataifa mengine” alisisitiza.
Amesema wizara imekuwa ikipokea wawekezaji wengi wenye changamoto za mitaji na wakielekezwa kukopa kwenye benki za ndani kutokana na sera yetu ya local content wanakiri benki za ndani hazina uwezo wa kukopesha kiasi cha pesa wanachokihitaji.
Akizungumza katika kikao hicho Waziri Biteko ameweka wazi kuwa biashara ya uchimbaji wa madini inahitaji mtaji mkubwa na kubainisha sifa kuu tatu za biashara hiyo kuwa ni biashara inayohitaji mtaji mkubwa (capital intensive), muda wa kutosha mpaka kuona matokeo pamoja na uwepo wa rasilimali watu ya kutosha.
Biteko ameushukuru uongozi wa Benki ya NMB kwa kuona umuhimu wa kufika na kuzungumzia masuala ya muhimu kama ya mitaji na kuona kuwa Sekta ya Madini ni mahala wanapoweza kuwekeza fedha zao.
Aidha, amesema Wizara pamoja na taasisi zake wako tayari kufanya kazi bega kwa bega na benki za ndani na kuwaongoza mahala penye viashiria vizuri ili waweze kuwekeza pesa zao na kukiri kuwa wizara yake haitakuwa tayari kuziingiza benki katika kutoa mikopo mahala ambapo kuna viashiria hatarishi vya hali ya juu maana haipendi benki hizo kupata hasara. “Kazi ya wizara ni kuzishauri benki nasisi tutafanya hivyo” alisisitiza.
Akibainisha maeneo ambayo yana viashiria vizuri katika biashara ya madini Biteko amesema ni pamoja na eneo la uchakataji wa madini, uongezaji thamani wa madini biashara ya madini na kubainisha kuwa katika hatua hizo tayari mwekezaji anakuwa na uhakika wa kile anachokifanya hivyo ni rahisi kuuza madini aliyonayo na kupata pesa ya kulipia deni la mkopo aliouchukua.
Ameitaka Sekta ya Benki kushirikiana na wizara katika kusukuma gurudumu la maendeleo na kusema kazi haiwezi kwenda mbele wala kujulikana kusipokuwa na ushirikiano baina ya sekta hizo mbili. Tushirikiane kwa pamoja, tusukume gurudumu, sekta iende mbele ili sote tuone manufaa, alisema.
Akibainisha vipaumbele vya wizara, Biteko amesema kuwa kwanza ni kutengeneza ajira kwa watanzania. Amebainisha kuwa endapo kuna leseni imetolewa kwa mwekezaji na haifanyiwi kazi leseni hiyo inanyang’anywa na kupewa wachimbaji wadogo walio tayari kufanya kazi.
Pili amesema kipaumbele kingine ni kubadilisha mtazamo wa wachimbaji wadogo katika suala zima la nidhamu ya pesa. Katika hilo ameitaka benki hiyo kuendesha mafunzo mbalimbali kwa wachimbaji wadogo katika eneo hilo ili kuwawezesha na kuwasaidia kuweza kufanya kazi kwa weledi na baadaye walipe kodi zitakazochangia katika maendeleo ya nchi.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila ameutaka uongozi wa benki hiyo kuwasilisha chati inayoonesha viwango vya chini na vya juu vya mikopo inayoweza kutolewa na benki hiyo kwa wawekezaji ili pindi wawekezaji wenye nia ya kukopa wanapotembelea ofisi yake wanakuta taarifa hizo muhimu na kufanya mawasiliano.
Aidha, ameishauri benki ya NMB kujihusisha na biashara ya bima na kukiri kwamba biashara hiyo ni fursa ya wazi na itawawezesha kutengeneza pesa na kuendeleza benki yao kiurahisi.
Akiwasilisha hoja zake kwa uongozi wa wizara, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ameanza kwa kutoa pongezi kwa Sekta ya Madini na kusema kwamba sekta ya madini imeibeba nchi hususani katika kipindi cha janga la corona katika suala zima la kuiingizia nchi pesa za kigeni. Amesema sekta hii imekuwa ni tegemeo sana katika suala zima la pesa za kigeni. “Sisi tupo kwenye sekta ya fedha hivyo tunaona namna sekta hii ilivyokuwa mkombozi” amesisitiza.
Amesema awali benki ya NMB ilikuwa ikisita kuingiza mkono wake kwenye sekta ya madini lakini kutokana na namna bora zilivyowekwa katika suala zima la mnyororo wa biashara ya madini benki hiyo imeamua kuingia na kutoa mikopo ili kuwawezesha wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kufanya biashara kwa ufanisi ambapo mpaka sasa tayari benki hiyo imetoa mikopo ya shilingi bilioni 10 kwa wachimbaji wadogo.
Aidha, amesema benki hiyo ikishirikiana na benki kutoka Afrika ya Kusini wametoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 22 kwa mgodi wa Uchimbaji Mkubwa wa madini wa Geita (GGM).
Zaipuna amebainisha kuwa, kwa sasa benki yao ina mtaji wa shilingi trilioni 1.1 ambapo ameonesha imani yake ya kuchangia katika miradi mikubwa ya uchimbaji na kuboresha maisha ya watanzania.
Amesema benki yake inaweza kutoa mkopo wa kiasi cha shilingi bilioni 240 bila shida yoyote.
Amekiri kuwa biashara ya madini ina changamoto kubwa katika kuielewa, kutokana na changamoto hiyo benki hiyo imefanya jitihada ya kuwasaidia watumishi wake kuielewa biashara ya madini kwa kuandaa mafunzo kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwepo wizara na taasisi zake ili kuwajengea uwezo na uelewa wa namna biashara ya madini inavyofanyika.
Akihitimisha mazungumzo yake Ruth Zaipuna amesema ofisi yake ipo tayari kuisikiliza wizara kadri itakavyoona inafaa kuona ni maeneo yapi yapewe kipaumbele ili waweze kushirki katika kulisukuma gurudumu la maendeleo kupitia benki anayoisimamia.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Yahya Samamba amekiri kufanya mafunzo kwa wataalamu wa benki hiyo na kuwaelimisha juu ya mnyororo mzima wa biashara ya madini unavyofanyika.
TMA yasema kimbunga Jobo kimekuwa hafifu
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kimbunga Jobo kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani.
Taarifa iliyotolewa na TMA leo Jumamosi Aprili 24, 2021 imeeleza kuwa kimbunga hicho kimekuwa hafifu na kinasafiri kwa kasi ya kilometa 18 kwa saa baharini tofauti na spidi ya kilometa 60 kwa saa iliyokuwa imetabiriwa awali.
TMA imesema kimbunga hicho kilichopo Bahari ya Hindi kwa sasa kipo umbali wa kilomita 200 mashariki mwa kisiwa cha Mafia.
“Kimbunga hafifu cha Jobo kinatarajiwa kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache hususan ya ukanda wa Pwani kadri kinavyosogea nchi kavu kwa siku ya leo Aprili 24 na kesho Aprili 25, 2021,” inaeleza taarifa hiyo.
Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani ikiwemo kisiwa cha Mafia, Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja.
Aidha TMA imetahadhalisha kuwa uwepo wa kimbunga hafifu baharini, unatarajiwa kusababisha mawimbi makubwa.
ASKOFU AKIRI HADHARANI KUCHOVYA ASALI YA MKE WA ASKOFU MWENZAKE
PADRE LIVINUS AFARIKI DUNIA
MTANDAO WA WANAWAKE, KATIBA, UONGOZI, NA UCHAGUZI WACHAMBUA HOTUBA YA RAIS SAMIA…WATOA TAMKO
SAFARI ZA KWENDA, KUTOKA ZANZIBAR BAHARINI ZASITISHWA TAHADHARI YA KIMBUNGA JOBO... TMA YATOA NENO


















