Thursday, 22 April 2021

Picha : RAS SHINYANGA, DC MBONEKO WAUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA FLAVIANA KIFIZI

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Flaviana Kifizi
***
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko wameungana na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi (40) aliyefariki dunia Aprili 19,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam akiumwa kichwa.

Akizungumza wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 nyumbani kwa Lubaga Mjini Shinyanga, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema Flaviana alijituma na kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha wananchi wa Shinyanga wanapata huduma ya maji safi na salama.

“Taarifa za kifo cha Flaviana zimetushtua sana kama mkoa. Niwaambie tu kuwa hakuna kazi ngumu kama kuwa kiongozi wa taasisi inayohusika kwa sababu maji hayana mbadala. Flaviana alitamani kila eneo, kila uchochoro wa Shinyanga upate huduma ya maji. Tumefanya naye kazi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha wananchi wa Shinyanga wanapata maji”,amesema Msovela ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa SHUWASA.

“Flaviana alikuwa msimamizi mzuri na kiungo mzuri katika mkoa wa Shinyanga. Alikuwa msikivu na alipenda kuwa na maamuzi ya pamoja na ndiyo maana SHUWASA imekuwa ikifanya vizuri na imeendelea kukua. Naomba tuenzi mambo aliyoyasimamia na kuyaanzisha na alitamani yafanyike”,ameongeza Msovela.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko amesema Flaviana hakubagua watu na alikuwa rafiki wa kila mtu na alitimiza wajibu wake kikamilifu na kuipa sifa nzuri SHUWASA kwa kujali wananchi.

“Kifo cha Flaviana ni pigo kwetu serikali na wananchi kwa ujumla. Flaviana alishirikiana na viongozi wa serikali na wadau katika kuwapatia huduma ya maji wananchi. Hata kama kazi ilikuwa ngumu ukimuagiza kufanya yeye alifanya.Mama yake na Flaviana ni Jasinta na mimi naitwa Jasinta, alikuwa ananiita mama. Naomba tumuenzi kwa mazuri aliyofanya”,amesema Mboneko.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi amemwelezea Flaviana kuwa alikuwa kiongozi Jembe aliyefanikiwa kujenga misingi imara SHUWASA hivyo watamkumbuka kutokana na usikivu,utendaji kazi na bidii yake katika kazi.

“Flaviana alipenda sana kazi yake. Hakuwa Mhandisi lakini alikuwa anafanya kazi kama amesomea uhandisi. Ameitumikia SHUWASA kwa zaidi ya miaka 10 mwanzo akiwa Meneja wa Rasilimali na utawala kisha Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA”,ameongeza Jilumbi.

Mazishi ya mwili wa marehemu Flaviana Kifizi yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa Aprili 23,2021 jijini Mwanza.

Marehemu Flaviana Kifizi alizaliwa mwaka 1981, ameacha mtoto mmoja wa kike.

ANGALIA PICHA HAPA
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizungumza wakati akiongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizungumza wakati akiongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Parokia ya Lubaga, Philemon Chikala akiongoza Ibada ya Kumuombea mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SHUWASA, Mwamvua Jilumbi (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akimfariji  (Precious) ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Afisa Habari wa KASHWASA, Dkt. Mwidima Peter akitoa mwongozo wa kuaga mwili wa marehemu Flaviana Kifizi
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akifuta machozi wakati akiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 
Waombolezaji wakiaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 

Kushoto ni Mkurugenzi wa KASHWASA, Mhandisi Joshua Mgeyekwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa msibani

ZIFUATAZO NI PICHA ZA WADAU MBALIMBALI WAKITOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka za maji nchini akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Julieth Kayovela akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. Luther Mneney akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Shinyanga akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Mwakilishi wa Benki ya NMB akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Afisa Habari wa KASHWASA, Dkt. Mwidima Peter akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Mwakilishi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), Sam Bahari akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Meneja wa KUWASA, akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (Patrobas Katambi), Samwel Jackson akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Diwani wa kata ya Lubaga akitoa salamu za rambirambi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga.
Wafanyakazi wa SHUWASA wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA), Flaviana Kifizi leo Alhamis Aprili 22,2021 Lubaga Mjini Shinyanga. 

Share:

RAIS SAMIA AONYA WANAOCHONGANISHA MITANDAONI KIFO CHA MAGUFULI....AWATULIZA WENYE MASHAKA NAYE

Na Damian Masyenene
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na maneno yanayozushwa na baadhi ya watu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii juu ya sababu za kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk. John Magufuli.

Rais Samia amesisitiza kuwa Hayati Magufuli alifariki kwa tatizo la Moyo lililokuwa likimsumbua kwa zaidi ya miaka 10.

Akilihutubia bunge la 12 leo Aprili 22, 2021 bungeni jijini Dodoma, Rais Samia amewataka wale wote wenye mashaka na kifo cha Hayati Magufuli na wana taarifa za msingi basi wafike kwenye vyombo husika watasikilizwa, lakini vinginevyo watasakwa na kuchukuliwa hatua.

Rais Samia amesisitiza kuwa wanaofanya uzushi huo wanafanya uchonganishi kwenye taifa na kutaka kuvuruga amani na utulivu wa nchi. 
 
"Nimekuwa nikiona kwenye mitandao taarifa za uchonganishi, taarifa tuliyopewa na madaktari wetu kwa kifo cha mpendwa wetu ni matatizo ya moyo aliyoishi nayo kwa zaidi ya miaka 10

"Kama wana taarifa za maana waje tuwasikilize, vyombo vya upelelezi na uchunguzi vipo waje tuwasikilize, tofauti na hapo wanaleta uchonganishi. Waache kuleta uchonganishi ndani ya nchi. Niwaambie kuwa tutawatafuta 

"Kama wanajizatiti wanafanya hivyo wanadhani hatutowapata, basi warudi kwa mungu wajiulize wanavyofanya hivyo wangeambiwa wao hivyo wangekubali?," ameonya. 

WALIOANZA 'KULEGEA'
Katika hatua nyingine, Rais Samia ameeleza kuwa baada ya kifo cha Hayati Dk. John Magufuli, baadhi ya watendaji wa Serikali, wawekezaji na nidhamu vimeanza kulegea kutokana na watu kuamini kuwa kuondoka kwa JPM mambo yatakwama.

Rais Samia amesema kuwa baadhi ya watendaji wameanza kulegea na kukosa ufanisi, wizi wa mali za umma umeshamiri, wawekezaji waliokuwa kwenye majadiliano na serikali wameanza kurudi nyuma, hivyo amebainisha kuwa MWENDO NI ULE ULE na mambo yatakwenda sawia kadri ya yalivyoahidiwa.

 WENYE MASHAKA NA RAIS
Rais Samia pia amebainisha kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wake kutokana na jinsia yake na namna atakavyoyatimiza yale aliyoyasema. 

Ambapo, amewatoa wasiwasi na kueleza kuwa anao uzoefu wa kutosha kwenye shughuli za serikali na chama chake (CCM) kwani Mwenyezi Mungu hakuumba ubongo hafifu kwa mwanamke na ubongo makini kwa mwanaume, wote wamezaliwa sawa. 

"Nataka niwahakikishieni kuwa nimekuzwa kwenye jamii makini na nina uzoefu wa kutosha kwenye shughuli za serikali na chama changu cha siasa. Najiamini kuwa ninao uwezo wa kuliongoza taifa langu. 

"Haya niliyoyasema hapa siendi kukaa na kuyatekeleza peke yangu, nitashirikiana na watanzania wote katika Nyanja tofauti. Tushirikiane katika kulijenga taifa letu," amesema.
Share:

🔴LIVE: Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Bunge, Aprili 22, 2021

 ðŸ”´LIVE: Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Bunge, Aprili 22, 2021

Share:

COSOTA YAMTOZA FAINI YA MILIONI 5 MWIGIZAJI WA FILAMU KWA KUGHUSHI NYARAKA ZA UMILIKI

Kaimu Meneja  Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka (katikati) akikemea tabia ya la kughushi nyaraka za umiliki unaofanya na baadhi ya wanatasnia ya filamu nchini kwa lengo la kujipatia fedha kinyume na taratibu za Hakimiliki leo Aprili 21, 2021  katika kikao cha usuluhishi kilichofanyika katika Ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam kati ya Mwigizaji Sabrina Abdallah (kushoto) aliyeghulishi umiliki wa kazi Filamu ya ‘Mama Nongwa’ inayomilikiwa na Bw. Jotham  Ngulika (kulia) baada ya Sabrina kukiri kufanya kosa hilo kwa kupatiwa filamu hiyo na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman) kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam.

Mwigizaji Sabrina Abdallah (kushoto) akikiri na kuomba msamaha kwa kosa  la kughushi nyaraka mbalimbali za umiliki wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ na kuisajili  COSOTA kama mmiliki  kinyume na sheria umiliki wa kazi Filamu ya ‘Mama Nongwa’ inayomilikiwa na Bw. Jotham  Ngulika (kushoto) kwa kusema filamu hiyo alipewa na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman), leo Aprili 21,2021 wakati wa kikao cha kupata suluhu ya mmiliki halali wa kazi hiyo baada ya kazi hiyo kuwasilishwa na watu wawili kufanyiwa usajili, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam, katikati Kaimu Meneja  Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka

Mmiliki wa  Filamu ya ‘Mama Nongwa’  Bw. Jotham  Ngulika (kulia) akiishukuru COSOTA kwa kufanikisha kumpata kurudisha ummiliki wa kazi yake baada ya Sabrina Abdallah kukiri kosa la kughushi umiliki wa kazi hiyo na kuisajili kinyume na sheria  na kuomba msamaha leo Aprili 21,2021 wakati wa kikao cha kupata suluhu ya mmiliki halali wa kazi hiyo baada ya kazi hiyo kuwasilishwa na watu wawili kufanyiwa usajili, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Meneja  Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka na kushoto ni ya Mwigizaji Sabrina Abdallah aliyeghushi kazi hiyo na kuisajili.

Na Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania yamtoza  faini ya shilingi milioni tano Mwigizaji wa Filamu kwa kughushi nyaraka mbalimbali za filamu isiyo ya kwake na kuisajili kama mmililiki halali.

Akizungumza katika kikao hicho cha kupata suluhu ya Mmiliki halali wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ iliyokuwa imesajiliwa COSOTA na Mwigizaji Sabrina Abdallah kwa kughushi umiliki na mikataba mbalimbali, Kaimu Meneja Idara ya Usajili na Ugawaji Mirabaha COSOTA Bw. Philemon Kilaka alisema kitendo alichokifanya mwigizaji huyo ni kosa kisheria na ni ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi ikiwepo Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo Aprili 21,2021 Jijini   Dar es Salaam baada ya mmiliki wa Filamu hiyo Bw.Jotham Ngulika kufika kusajili kazi hiyo na kuonekana filamu hiyo ilikwisha sajiliwa na Mwigizaji huyo  kama mmiliki halali.

"Kitendo alichokifanya Sabrina cha kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo mkataba wa Muongozaji,(Director),Mkataba wa Mwandishi wa stori pamoja na Mkataba wa Mpiga picha huku akiwa anafahamu kuwa ni kosa,tunampa onyo kali pamoja na faini hiyo na akirudia kosa hili tunamfutia uanachama, hii ikawe fundisho kwa watu wengine wenye kufikiria kufanya hivi au wenye tabia

 kama hii,’’alisema Bw.Kilaka.

Kwa upande wa Mwigizaji huyo Sabrina Abdallah alikiri kufanya kosa hilo la kusajili filamu hiyo kwa kughushi mikataba mbalimbali kinyume na sheria, ambapo alieleza  kuwa  filamu hiyo alipewa na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman).

"Nakiri kweli nimefanya kosa la kughushi nyaraka mbalimbali kuhusu umiliki wa kazi hii hivyo naomba msamaha kwa mmiliki wa kazi hii na COSOTA kwa usumbufu niliyosababisha na ahidi kuwa balozi wa kukemea matumizi ya kazi usiyo na umiliki nayo bila ridhaa ya mmiliki,"alisema Sabrina. 

Halikadhalika nae Mmiliki wa Filamu hiyo Bw. Jotham Ngulika aliishukuru COSOTA kwa kufanikisha kurudisha umiliki wa kazi yake na kufanikisha kumpata mhusika aliyekuwa amesajili kazi hiyo kwa kughushi kinyume na utaratibu.

Wito wa COSOTA kwa wadau wa kazi za ubunifu  ni kuacha kuibiana kazi kwani hilo kosa kisheria na linahatarisha ukuaji wa kisekta .

Share:

Syria, Israel zashambuliana tena Kwa Makombora

Syria na Israel zimeshambuliana tena kwa makombora, huku kila upande ukidai kudunguwa la mwenzake mapema alfajiri ya leo. 

Jeshi la Israel  limesema kombora lililorushwa kutoka Syria limepiga karibu na kinu cha nyuklia katika mji wa Negev ulio kusini mwa Israel.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, nalo lilijibu kwa kuishambulia mitambo ya ulinzi na iliyorusha kombora hilo nchini Syria.Kwa upande wake, vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kwamba jeshi la anga limeyadunguwa makombora ya Israel yaliyokuwa yameelekezwa kwenye viunga vya mji mkuu, Damascus. 

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Syria, wanajeshi wake wanne wamejeruhiwa na kuna madhara madogo kwenye eneo makombora hayo yalipoangukia. 

Inashukiwa kuwa mashambulizi yaliyoelekezwa nchini Israel yamefanywa na vikosi vitiifu kwa Iran nchini Syria, kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel wiki iliyopita dhidi ya kinu cha nyuklia nchini Iran.

Share:

Serikali kuajiri watumishi 44,096

Wizara ya Nchi Ofisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2021/22 inatarajia kuajiri watumishi wa umma wapya 44, 096.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 22, 2021 Waziri wa wa wizara hiyo, Mohamed Mchengerwa, wakati akiwasilishwa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Mchengerwa amesema kada ya elimu wataajiri watumishi wapya 10,297, afya 11,215, kilimo 1,383, mifugo 1,250, uvuvi 733, Jeshi la Polisi 1,782, Magereza 843, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji 512 na watumishi wapya wa hospitali za mashirika ya kidini na hiari 1,240.

Ameongeza kuwa serikali itaajiri watumishi 14,841 wa kada mbalimbali ikiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu vyote vya umma nchini pamoja na kada nyingine ambazo haziko kwenye sekta zilizoainishwa awali.

Hata hivyo, amesema watumishi 92,619 wa kada mbalimbali watapandishwa vyeo na watumishi 2,360 watabadilishwa kada katika utumishi.

Amebainisha kuwa maelekezo yatakayotolewa wakati huo ni kuchambua na kuhakiki madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma 17,699 yenye thamani ya Sh37.47 bilioni na kuchukua hatua ipasavyo.

Share:

Shilole athibitisha kufunga ndoa na mpenzi wake Rommy

Msanii Zuwena Mohamed 'Shilole' amethibitisha kufunga ndoa ya siri na mume wake Rajab Issa maarufu kama Rommy kama ambavyo ilikuwa inaelezwa na baadhi ya vyombo mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram muda mfupi uliopita Shilole ameandika hilo baada ya kufunga ndoa na mume wake.

"Alhamdulillah tumemaliza salama, rasmi ni mume na mke niliechukuliwa kwa furaha na upendo wa juu 'Officially Husband and Wife happily taken and very much in love' kwasasa unaweza kuniita Mrs Rajab Issa (Rommy) Yarabbi iwe salama".

Kabla ya hapo Shilole alikuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Uchebe na waliachana mwaka jana baada ya ugomvi mkubwa uliotokea kwenye ndoa.

Share:

Waasi nchini Chad watishia kumng'oa mtoto wa Rais Deby

 Waasi nchini Chad wametishia kumng’oa madarakani mtoto wa Rais aliyeuawa baada ya kuteuliwa kuwa kiongozi wa mpito nchini humo.

Kundi la waasi ambalo jeshi limelilaumu kwa mauaji ya Rais Idriss Deby Itno, limesema kuwa wapiganaji wake wanaelekea katika mji mkuu wa N’Djamena wakati huu. Waasi hao wanaojulikana kama “Front for Change and Concord”, wamesema katika taarifa kuwa Chad sio nchi ya kifalme.

Hali ya wasiwasi ilitanda mapema jana Jumatano juu ya umbali wa kiasi gani waasi hao watakuwa wameukaribia mji mkuu wa N’Djamena, mji wenye idadi ya watu milioni 1, na iwapo jeshi lingeendelea kuwa tiifu kwa Mahamat Deby baada ya kifo cha baba yake aliyedumu madarakani kwa miongo mitatu.

Haijabainika wazi walikofika waasi hao, japo taarifa za ujio wao zimezua hofu katika mji wa N’Djamena, ambao uliwahi kushambuliwa na kundi lingine la waasi mnamo mwaka 2008.

Maafisa wa baraza la kijeshi wamesema mapambano ya kuwania udhibiti wa nchi bado hajakwisha.

Share:

Bunge latengua kanuni ili viongozi wapate fursa ya kuingia Bungeni

Bunge la Tanzania leo Alhamisi Aprili 22, 2021 limetengua kanuni ya 160 (1) ya kanuni za kudumu za chombo hicho cha kutunga sheria ili kuruhusu baadhi ya wageni kuingia ukumbini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,  Jenister Mhagama ametoa hoja ya kutengua hoja hiyo kufuatia ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye leo atalihutubia Bunge.

Kabla ya hoja hiyo,  Spika wa Bunge,  Job Ndugai alieleza kuwa ujio wa rais utakuwa na wageni wengi hivyo baadhi watalazimika kuingia ndani ya ukumbi kutokana na unyeti wa nafasi zao.

Akisoma orodha ya wageni watakaoingia ukumbini Ndugai amesema ni makamu wa Rais,  Dk Philip Mpango; Rais wa Zanzibar,  Dk Hussein Ali Mwinyi;  Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais Zanzibar.

Wengine ni jaji mkuu wa Tanzania, jaji mkuu wa Zanzibar, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na Spika wa Baraza la Wawakilishi.

Share:

SPIKA NDUGAI : WABUNGE HAKUNA KUVAA TAI NYEKUNDU LEO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kutovaa tai nyekundu, wakati wa kikao cha saa 10:00 jioni, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge.

“Napenda kuwakumbusha waheshimiwa wabunge, siku anapokuja kiongozi mkuu wa nchi (bungeni), basi haishauriwi sana kuvaa tai nyekundu”. Amesema Spika

“Nadhani tunakubaliana, ile red inabakia na wenye mamlaka, kwa hiyo ni vizuri kuyajua haya mambo,baadae jioni tutakapo rudi, ukivaa tai nyekundu utarudia getini” amesema spika Ndugai.

Majira ya saa 10:00 jioni hii leo, Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kushika wadhifa huo Machi 19,2021.
Share:

MYP EAL position at International School of Tanganyika

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

We seek teachers who are passionate about educating young minds and who can demonstrate resourcefulness and flexibility. Tanzania is a wonderful country, with outstanding opportunities for individuals and families. Teachers who thrive here tend to be active and intrepid and are often called upon to show a good sense of humour. We seek clear commitment […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Lifeguard/Swimming Instructor at International School of Tanganyika

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

  Title Lifeguard/Swimming Instructor Category  (cf Policy 5.101) Support Staff Reports to: Principal Department: Physical Education Job Holder Start date: Immediately   IST Foundational Documents   IST Mission Challenging, inspiring and supporting all our students to fulfil their potential and improve the world IST Vision IST will be a global leader in the education of […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

Free 12,625 Apprenticeship Training Opportunity (Nafasi 12,625 za Mafunzo ya Ufundi Stadi) by Tanzania Government

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Announcement about Apprenticeship Training Opportunity 2021 Tanzania is an East African country known for its vast wilderness areas. They include the plains of Serengeti National Park, a safari mecca populated by the “big five” game (elephant, lion, leopard, buffalo, rhino), and Kilimanjaro National Park, home to Africa’s highest mountain. Offshore lie the tropical islands of […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

Share:

RIPOTI YA CAG YAWAVURUGA MADIWANI KISHAPU...WAAZIMIA KUMSIMAMISHA KAZI MWEKA HAZINA, DED ATAKA WOTE WAJITATHMINI

Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye baraza la madiwani Kishapu kulia ni mkurugenzi halmashauri hiyo Emmanuel Johnson na kushoto ni Anderson Mandia makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson akizungumza kwenye baraza la madiwani kulia ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu na kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese akizungumza kwenye baraza hilo.
Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa ukumbini
Katibu wa CCM wilaya, Lucas Nyanda akizungumza kwenye kikao hicho 

Na Suzy Luhende, Kishapu
Wiki kadhaa baada ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuipa hati ya mashaka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Madiwani wa halmashauri hiyo kwa kauli moja wameazimia kumsimamisha kazi Mweka hazina wa halmashauri hiyo, Deus Ngelanizya kwa kosa la kushindwa kusimamia mapato ya mwaka wa fedhan 2020/2021 na kusababishia halmashauri hiyo kuwa ya mwisho kitaifa kwenye makusanyo ya nusu mwaka.

Pia Makosa mengine ni kudharau maagizo ya madiwani na kuisababishia halmashauri kupata hati ya mashaka kwa mwaka 2019 /2020.

Madiwani hao pia wamemtaka Afisa Mipango wa halmashauri hiyo Mang'era Mang'era kujitathmini utendaji wake wa kazi kwa sababu ana jukumu la kufuatilia mipango yote ya halmashauri hiyo.

Maazimio hayo yamefikiwa jana Aprili 21,2021 kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo baada ya baraza hilo kukaa kama kamati na kujadili juu ya wafanyakazi hao.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mondo amesema wameamua kutoa maazimio hayo kwa sababu wameshindwa kusimamia kikamilifu mapato ya halmashauri hiyo, hali ambayo wameisababishia kupata hati ya mashaka na kuwa ya mwisho kitaifa.

"Tumekuwa tukiwaagiza wasimamie kukusanya mapato ya ndani lakini hawasimamii kikamilifu, hivyo tumeona tuwaazimie ili wasiendelee kudharau. Hili litakuwa ni fundisho na kwa watendaji wengine wa halmashauri hii kwani mapato ni roho ya halmashauri hivyo tunatakiwa kuwajibika kila mmoja ili kuhakikisha mapato yanaongezeka", alisema Jijimya.

Diwani wa kata ya Mwamalasa Bushi Mpina alisema wameamua kuwaazimia watumishi hao kwa sababu hawasimamii fedha kikamilifu, fedha zinaingia lakini hawajui zinaenda wapi hivyo wameona ukusanyaji unaofanywa sio sahihi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emmanuel Johnson amesema kama inatokea changamoto ya kusababisha hati ya mashaka idara ya fedha ilitakiwa kusaidiwa, kutoa ushauri na kuwa weledi katika suala la mapato, pia unahitajika ushirikiano wa hali ya juu katika kusimamia mapato.

"Kama miongoni mwetu ameazimiwa mwenzetu kwa changamoto ya kusababisha hati ya mashaka inatakiwa tujitathimini wote, kwani tulitakiwa kuwasaidia idara ya fedha na kuzingatia weledi na taaluma zetu kwa sababu suala la mapato ni letu sote, tunatakiwa tushirikiane ili kuondokana na changamoto hii",alisema Johnson.

Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese amesema ni jambo la aibu kuona halmashauri hii ina kuwa ya mwisho kitaifa na kupata hati ya mashaka, hivyo watumishi wote wanatakiwa kujituma katika kusimamia mapato na kuongeza vyanzo mbadala kwa ajili ya kuongeza mapato.

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Lucas Nyanda amewapongeza kwa kusimamia vizuri maendeleo ya wananchi kwa sababu sifa ya kiongozi ni kuonyesha njia, lakini katika kusomeka kwa kupata hati ya mashaka haikutakiwa kufikia hatua hiyo, ni vizuri kutengeneza mazingira mazuri ili mapato yaweze kuongezeka.

"Ni aibu kubwa kwa sisi wanakishapu kupata hati ya mashaka hatutakiwi kufikia hatua hii hivyo kwa hili mliloliazimia na watumishi wengine watajisimamia, dhamila yetu ni kuendelea kushikamana tunatakiwa kuwa na mazingira mazuri ya kuweza kuongeza kipato chetu",amesema Nyanda.
Share:

HAKUNA JAMBO BAYA MWANAUME KULETA MWANAMKE KWAKO

 Wanawake tunakutana na shida na changamoto mbalimbali katika ndoa zetu,kuna shida ambazo zinasababishwa na waume zetu na shida nyingine chanzo chake unakuta ni familia kutoka kwa upande wa mme wako.

Mimi kwa majina naitwa (Mariamu) umri wa miaka 35 na mwenyezi Mungu ametujaria tumepata watoto 3. Mmoja ni mtoto wa kiume ambaye ni mtoto wetu wa kwanza na waliobaki ni wasichana.

Mwanzo kabisa ndoa yangu ilikuwa imejaa furaha, amani na upendo muda wote, mme wangu alikuwa ananipenda na kunipa kila ninachokitaka kutoka kwake.

Baada ya miaka 3 kupita mme wangu alianza kuwa na tabia ambazo mimi nilikuwa sijazoea tangu tuoane. Ilifika wakati hataki nishike simu yake, Password ya simu anabadilisha kila wakati na zaidi alivyokuwa akitoka kazini anakuwa busy na simu yake.

Jinsi siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo mme wangu alikuwa ana badilika ilifika hatua hata kitandani hataki maneno yangu.

Alivyoanza tabia ya kukataa maneno yangu kitandani ikabidi nimuulize mme wangu wapi nimemkosea ili niweze kujirekebisha ila jibu nililopewa ni kwamba sijakosea popote.

Nilibaki mdomo wazi baada ya kuniambia hivyo,ilinibidi nianze kufuatilia taratibu mme wangu kwa nini anakuwa hivyo.

Nilianza kutegeshea simu yake akienda kuoga au akiwa anaongea na simu ili niweze kupata jibu ila jitihada zangu hazikufanikiwa tu.

 Nilianza kutafuta usaidizi kwa marafiki zangu ndipo rafiki yangu akaniambia kuna Dr. Kiwanga anaweza kunisaidia kwa nini mme wangu anafanya hivyo.

Rafiki yangu alizidi kuniambia kuwa Dr. Kiwanga ndiye alimsaidia kupata kazi baada ya kutafuta kazi kwa miaka 3 biLa kufanikiwa ila sasa anafanya kazi nzuri na anapata matunda ya kazi yake.

Ilibidi nimuombe namba ya Dr. Kiwanga ambayo ndiyo hii +254 769404965 na website yao www.kiwangadoctors.com.

 Nilichukua simu yangu na kumpigia Dr. Kiwanga nikamueleza tabia ya mme wangu alivyo kwa sasa, pia nikamuomba kuwa nahitaji kujua shida ni nini, ndipo Dr. Kiwanga akaniambia kuwa atanisaidia na spells ya marriage spell kisha akasema kwa muda wa masaa 24 nitakuwa nimeisha pata jibu.

Baada ya kuambiwa hivyo nilipanda gari na kurudi kwangu “Kericho" kutoka ofisini kwa Dr. Kiwanga “Nakuru" ili niweze kufika nyumbani kabla ya mme wangu hajatoka kazini kwake.

Nilifika Kericho muda wa saa kumi na moja jioni na kuelekea kwangu, nilipokaribia mlangoni kwangu nikaona viatu vya mme wangu sikuweza kushtuka sana maana alikuwa anajua nimeenda kutembelea rafiki yangu ambae anaishi Nakuru.

Nilipotoa kateni mlangoni nikaona viatu vya mwanamke nikahisi kuwa kuna mgeni ila sebuleni sikuweza ona mtu ndipo nikasikia sauti ya mwanamke kwenye chumba chetu. Nilipoingia chumbani nikamuona mme wangu akiwa na secretary ambaye wanafanya kazi kwa ofisi moja wote wapo uchi.

 Machozi yalinitoka na kuishiwa nguvu, yule mwanamke akavaa nguo zake na mme wangu kisha wakatoka chumbani na kuniacha natoa machozi na moyo kuniuma.

Baada ya nusu saa nikagundua kuwa hata mme wangu hayupo na hiyo siku hakurudi nyumbani. Kesho yake mme wangu akarudi nyumbani wala hakuniomba msamahaa zaidi nilivyomuuliza akaniambia kama nimechoka nirudi kwetu ila nilivyo watazama watoto wangu 3 nikajisemea”moyoni wapi niende na hawa watoto na nikiwaacha malezi gani watapata mimi bila kuwepo mama yao”.

 Kesho yake niliwasiliana na Dr. Kiwanga kwanza nikamshukuru kwa sababu nimepata jibu kwa nini mme wangu alikuwa anatoka kazini amechelewa na kwa nini alikuwa hataki maneno yangu kwa muda wa miezi 9 kisha nikamuomba tena Dr. Kiwanga kuwa nahitaji mme wangu arudi nyumbani na aachane na yule secretary, Akaniambia nirudi ofisini kwake bila kukawia nilikwenda Nakuru tena na kupewa dawa na kuniahidi kuwa siku 3 nitaona mabadiliko ya mme wangu.

Nilifuata maelekezo niliyopewa vizuri na siku ya 2 mme wangu alitoka kazini kwake mapema ,alivyofika nyumbani aliniita chumbani na kuniomba msamaha na kuniambia kuwa mama yake ndiyo alimwambia kuwa mimi ni mwanamke gani ambaye hata kazi sina ila mme wangu akaniahidi kuwa hatarudia hiyo tabia maana yeye ndiyo alinichagua mimi bila kuwa na shindikizo la mtu yoyote.

 Na kwa sasa maisha yangu yamejaa furaha, amani na upendo kama ilivyokuwa mwanzo. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa kiwangadoctors kwa kazi yao nzuri. pia natoa wito kwa mwenye shida ya Magic ring,Magic wallet,Promotion kazi,kupata kazi,kupata mpenzi wasiliana na Dr. Kiwanga atakusaidia pia Dr Kiwanga alizidi kuniambia kuwa anatibu magonjwa sugu kama Sukari,Pressure,TB na Syphilis. Unaweza kumpata Dr. Kiwanga kwa namba +254 769404965 au tembelea website yao www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger