Thursday, 22 April 2021
Picha : RAS SHINYANGA, DC MBONEKO WAUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA FLAVIANA KIFIZI
RAIS SAMIA AONYA WANAOCHONGANISHA MITANDAONI KIFO CHA MAGUFULI....AWATULIZA WENYE MASHAKA NAYE
COSOTA YAMTOZA FAINI YA MILIONI 5 MWIGIZAJI WA FILAMU KWA KUGHUSHI NYARAKA ZA UMILIKI
| Kaimu Meneja Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka (katikati) akikemea tabia ya la kughushi nyaraka za umiliki unaofanya na baadhi ya wanatasnia ya filamu nchini kwa lengo la kujipatia fedha kinyume na taratibu za Hakimiliki leo Aprili 21, 2021 katika kikao cha usuluhishi kilichofanyika katika Ofisi za COSOTA Jijini Dar es Salaam kati ya Mwigizaji Sabrina Abdallah (kushoto) aliyeghulishi umiliki wa kazi Filamu ya ‘Mama Nongwa’ inayomilikiwa na Bw. Jotham Ngulika (kulia) baada ya Sabrina kukiri kufanya kosa hilo kwa kupatiwa filamu hiyo na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman) kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam. |
|
Mwigizaji Sabrina Abdallah (kushoto) akikiri na kuomba msamaha kwa kosa la kughushi nyaraka mbalimbali za umiliki wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ na kuisajili COSOTA kama mmiliki kinyume na sheria umiliki wa kazi Filamu ya ‘Mama Nongwa’ inayomilikiwa na Bw. Jotham Ngulika (kushoto) kwa kusema filamu hiyo alipewa na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman), leo Aprili 21,2021 wakati wa kikao cha kupata suluhu ya mmiliki halali wa kazi hiyo baada ya kazi hiyo kuwasilishwa na watu wawili kufanyiwa usajili, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam, katikati Kaimu Meneja Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka |
Mmiliki wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ Bw. Jotham Ngulika (kulia) akiishukuru COSOTA kwa kufanikisha kumpata kurudisha ummiliki wa kazi yake baada ya Sabrina Abdallah kukiri kosa la kughushi umiliki wa kazi hiyo na kuisajili kinyume na sheria na kuomba msamaha leo Aprili 21,2021 wakati wa kikao cha kupata suluhu ya mmiliki halali wa kazi hiyo baada ya kazi hiyo kuwasilishwa na watu wawili kufanyiwa usajili, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za COSOTA Dar es Salaam, katikati ni Kaimu Meneja Idara ya Usajili na Ugawaji wa Mirabaha COSOTA Bw.Philemon Kilaka na kushoto ni ya Mwigizaji Sabrina Abdallah aliyeghushi kazi hiyo na kuisajili.
Na Anitha Jonas – COSOTA, Dar es Salaam
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania yamtoza faini ya shilingi milioni tano Mwigizaji wa Filamu kwa kughushi nyaraka mbalimbali za filamu isiyo ya kwake na kuisajili kama mmililiki halali.
Akizungumza katika kikao hicho cha kupata suluhu ya Mmiliki halali wa Filamu ya ‘Mama Nongwa’ iliyokuwa imesajiliwa COSOTA na Mwigizaji Sabrina Abdallah kwa kughushi umiliki na mikataba mbalimbali, Kaimu Meneja Idara ya Usajili na Ugawaji Mirabaha COSOTA Bw. Philemon Kilaka alisema kitendo alichokifanya mwigizaji huyo ni kosa kisheria na ni ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi ikiwepo Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai.
Katika kikao hicho kilichofanyika leo Aprili 21,2021 Jijini Dar es Salaam baada ya mmiliki wa Filamu hiyo Bw.Jotham Ngulika kufika kusajili kazi hiyo na kuonekana filamu hiyo ilikwisha sajiliwa na Mwigizaji huyo kama mmiliki halali.
"Kitendo alichokifanya Sabrina cha kughushi nyaraka mbalimbali ikiwemo mkataba wa Muongozaji,(Director),Mkataba wa Mwandishi wa stori pamoja na Mkataba wa Mpiga picha huku akiwa anafahamu kuwa ni kosa,tunampa onyo kali pamoja na faini hiyo na akirudia kosa hili tunamfutia uanachama, hii ikawe fundisho kwa watu wengine wenye kufikiria kufanya hivi au wenye tabia
kama hii,’’alisema Bw.Kilaka.
Kwa upande wa Mwigizaji huyo Sabrina Abdallah alikiri kufanya kosa hilo la kusajili filamu hiyo kwa kughushi mikataba mbalimbali kinyume na sheria, ambapo alieleza kuwa filamu hiyo alipewa na Mpiga picha wa kazi hiyo (Cameraman).
"Nakiri kweli nimefanya kosa la kughushi nyaraka mbalimbali kuhusu umiliki wa kazi hii hivyo naomba msamaha kwa mmiliki wa kazi hii na COSOTA kwa usumbufu niliyosababisha na ahidi kuwa balozi wa kukemea matumizi ya kazi usiyo na umiliki nayo bila ridhaa ya mmiliki,"alisema Sabrina.
Halikadhalika nae Mmiliki wa Filamu hiyo Bw. Jotham Ngulika aliishukuru COSOTA kwa kufanikisha kurudisha umiliki wa kazi yake na kufanikisha kumpata mhusika aliyekuwa amesajili kazi hiyo kwa kughushi kinyume na utaratibu.
Wito wa COSOTA kwa wadau wa kazi za ubunifu ni kuacha kuibiana kazi kwani hilo kosa kisheria na linahatarisha ukuaji wa kisekta .
Syria, Israel zashambuliana tena Kwa Makombora
Syria na Israel zimeshambuliana tena kwa makombora, huku kila upande ukidai kudunguwa la mwenzake mapema alfajiri ya leo.
Jeshi la Israel limesema kombora lililorushwa kutoka Syria limepiga karibu na kinu cha nyuklia katika mji wa Negev ulio kusini mwa Israel.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, nalo lilijibu kwa kuishambulia mitambo ya ulinzi na iliyorusha kombora hilo nchini Syria.Kwa upande wake, vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kwamba jeshi la anga limeyadunguwa makombora ya Israel yaliyokuwa yameelekezwa kwenye viunga vya mji mkuu, Damascus.
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Syria, wanajeshi wake wanne wamejeruhiwa na kuna madhara madogo kwenye eneo makombora hayo yalipoangukia.
Inashukiwa kuwa mashambulizi yaliyoelekezwa nchini Israel yamefanywa na vikosi vitiifu kwa Iran nchini Syria, kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel wiki iliyopita dhidi ya kinu cha nyuklia nchini Iran.
Serikali kuajiri watumishi 44,096
Wizara ya Nchi Ofisi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2021/22 inatarajia kuajiri watumishi wa umma wapya 44, 096.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi Aprili 22, 2021 Waziri wa wa wizara hiyo, Mohamed Mchengerwa, wakati akiwasilishwa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/22.
Mchengerwa amesema kada ya elimu wataajiri watumishi wapya 10,297, afya 11,215, kilimo 1,383, mifugo 1,250, uvuvi 733, Jeshi la Polisi 1,782, Magereza 843, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji 512 na watumishi wapya wa hospitali za mashirika ya kidini na hiari 1,240.
Ameongeza kuwa serikali itaajiri watumishi 14,841 wa kada mbalimbali ikiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu vyote vya umma nchini pamoja na kada nyingine ambazo haziko kwenye sekta zilizoainishwa awali.
Hata hivyo, amesema watumishi 92,619 wa kada mbalimbali watapandishwa vyeo na watumishi 2,360 watabadilishwa kada katika utumishi.
Amebainisha kuwa maelekezo yatakayotolewa wakati huo ni kuchambua na kuhakiki madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma 17,699 yenye thamani ya Sh37.47 bilioni na kuchukua hatua ipasavyo.
Shilole athibitisha kufunga ndoa na mpenzi wake Rommy
Msanii Zuwena Mohamed 'Shilole' amethibitisha kufunga ndoa ya siri na mume wake Rajab Issa maarufu kama Rommy kama ambavyo ilikuwa inaelezwa na baadhi ya vyombo mbalimbali.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram muda mfupi uliopita Shilole ameandika hilo baada ya kufunga ndoa na mume wake.
"Alhamdulillah tumemaliza salama, rasmi ni mume na mke niliechukuliwa kwa furaha na upendo wa juu 'Officially Husband and Wife happily taken and very much in love' kwasasa unaweza kuniita Mrs Rajab Issa (Rommy) Yarabbi iwe salama".
Kabla ya hapo Shilole alikuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Uchebe na waliachana mwaka jana baada ya ugomvi mkubwa uliotokea kwenye ndoa.
Waasi nchini Chad watishia kumng'oa mtoto wa Rais Deby
Waasi nchini Chad wametishia kumng’oa madarakani mtoto wa Rais aliyeuawa baada ya kuteuliwa kuwa kiongozi wa mpito nchini humo.
Kundi la waasi ambalo jeshi limelilaumu kwa mauaji ya Rais Idriss Deby Itno, limesema kuwa wapiganaji wake wanaelekea katika mji mkuu wa N’Djamena wakati huu. Waasi hao wanaojulikana kama “Front for Change and Concord”, wamesema katika taarifa kuwa Chad sio nchi ya kifalme.
Hali ya wasiwasi ilitanda mapema jana Jumatano juu ya umbali wa kiasi gani waasi hao watakuwa wameukaribia mji mkuu wa N’Djamena, mji wenye idadi ya watu milioni 1, na iwapo jeshi lingeendelea kuwa tiifu kwa Mahamat Deby baada ya kifo cha baba yake aliyedumu madarakani kwa miongo mitatu.
Haijabainika wazi walikofika waasi hao, japo taarifa za ujio wao zimezua hofu katika mji wa N’Djamena, ambao uliwahi kushambuliwa na kundi lingine la waasi mnamo mwaka 2008.
Maafisa wa baraza la kijeshi wamesema mapambano ya kuwania udhibiti wa nchi bado hajakwisha.
Bunge latengua kanuni ili viongozi wapate fursa ya kuingia Bungeni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama ametoa hoja ya kutengua hoja hiyo kufuatia ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye leo atalihutubia Bunge.
Kabla ya hoja hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alieleza kuwa ujio wa rais utakuwa na wageni wengi hivyo baadhi watalazimika kuingia ndani ya ukumbi kutokana na unyeti wa nafasi zao.
Akisoma orodha ya wageni watakaoingia ukumbini Ndugai amesema ni makamu wa Rais, Dk Philip Mpango; Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi; Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais Zanzibar.
Wengine ni jaji mkuu wa Tanzania, jaji mkuu wa Zanzibar, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na Spika wa Baraza la Wawakilishi.
SPIKA NDUGAI : WABUNGE HAKUNA KUVAA TAI NYEKUNDU LEO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
MYP EAL position at International School of Tanganyika
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
We seek teachers who are passionate about educating young minds and who can demonstrate resourcefulness and flexibility. Tanzania is a wonderful country, with outstanding opportunities for individuals and families. Teachers who thrive here tend to be active and intrepid and are often called upon to show a good sense of humour. We seek clear commitment […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Lifeguard/Swimming Instructor at International School of Tanganyika
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Title Lifeguard/Swimming Instructor Category (cf Policy 5.101) Support Staff Reports to: Principal Department: Physical Education Job Holder Start date: Immediately IST Foundational Documents IST Mission Challenging, inspiring and supporting all our students to fulfil their potential and improve the world IST Vision IST will be a global leader in the education of […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Free 12,625 Apprenticeship Training Opportunity (Nafasi 12,625 za Mafunzo ya Ufundi Stadi) by Tanzania Government
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Announcement about Apprenticeship Training Opportunity 2021 Tanzania is an East African country known for its vast wilderness areas. They include the plains of Serengeti National Park, a safari mecca populated by the “big five” game (elephant, lion, leopard, buffalo, rhino), and Kilimanjaro National Park, home to Africa’s highest mountain. Offshore lie the tropical islands of […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
RIPOTI YA CAG YAWAVURUGA MADIWANI KISHAPU...WAAZIMIA KUMSIMAMISHA KAZI MWEKA HAZINA, DED ATAKA WOTE WAJITATHMINI
HAKUNA JAMBO BAYA MWANAUME KULETA MWANAMKE KWAKO
Wanawake tunakutana na shida na changamoto mbalimbali katika ndoa zetu,kuna shida ambazo zinasababishwa na waume zetu na shida nyingine chanzo chake unakuta ni familia kutoka kwa upande wa mme wako.









