• Home
  • About
  • Support
  • Contact
  • Advertise

MASWAYETU BLOG

  • Home
  • Business
    • Internet
    • Market
    • Stock
  • Downloads
    • Dvd
    • Games
    • Software
      • Office
  • Parent Category
    • Child Category 1
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • Featured
  • Health
    • Childcare
    • Doctors
  • Uncategorized
Menu
  • Home
  • Business
    • Internet
    • Market
    • Stock
  • Downloads
    • Dvd
    • Games
    • Software
      • Office
  • Parent Category
    • Child Category 1
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • Featured
  • Health
    • Childcare
    • Doctors
  • Uncategorized

Monday, 19 April 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 19,2021

 Unknown     06:55:00     NEWS     No comments   

























 


Share:
Read More →

Sunday, 18 April 2021

SIMBA SC YAICHAPA MWADUI FC 1 - 0 KAMBARAGE

 Unknown     17:55:00     NEWS     No comments   

 Bao pekee la Nahodha John Raphael Bocco leo limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Bocco amefunga bao hilo dakika ya 66 kwa kichwa akimalizia mpira uliounganishwa kwa kichwa pia na beki Mkenya, Joash Onyango kufuatia kona ya winga Mghana, Bernard Morrison kutoka upande wa kulia.

Ushindi huo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 52 baada ya kucheza mechi 22 na kurejea nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi mbili na Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.
Share:
Read More →

Cosota Yatoa Somo La Hakimiliki Kwa Maprodyuza Wa Muziki

 Unknown     16:55:00     NEWS     No comments   

 


Anitha Jonas – COSOTA
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki, Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare atoa elimu kwa Watayarisha wa Muziki nchini (Maprodyuza) kwa kuwaeleza umuhimu wa kusimamia haki zao na  kuingia mikataba na wasanii pale wanapokuwa wanafanya kazi zao.

Mtendaji huyo  ametoa elimu hiyo katika kikao cha Uzinduzi wa Chama cha Umoja wa Maprodyuza Tanzania (Tanzania Producers and Composers Association) kilichofanyika Aprili 17, 2021 Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanya uchaguzi  wa viongozi pamoja na kuweka mikakati ya namna ya kuendesha chama hicho ambacho kimeanzishwa hivi karibuni.

"Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inaweka  ulinzi katika kazi za Sanaa na usimamizi madhubuti  wa Hakimiliki na serikali inataka sekta ya Sanaa ikue na kuendana na kipato na siyo mtu anakuwa na umaarufu wa jina halafu kipato chake kinakuwa hakiendani na umaarufu wake "alisema Bibi Doreen.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo wa TPCA  Bibi. Doreen alieleza kuhusu Mfuko wa Sanaa na Utamaduni ambao  unatarajia kuzinduliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na pale utakapozinduliwa utawanufaisha wadau wote wa sekta ya Sanaa na Utamaduni kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu, pamoja na kusaidia kutoa ufadhili wa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika kuimarisha ujuzi katika kazi zao.

Kwa upande wa Muanzilishi wa Chama hicho Prodyuza P-Funk Majani alitoa ombi kwa COSOTA  la kusambaza sampuli za Mikataba  na fomu za Usajili na kutaka Studio zote nyaraka hizo ili mteja anapokwenda kuandaliwa kazi ahakikishe anasaini mkataba na studio pamoja na kujaza fomu ya COSOTA studio, ili ulinzi wa kazi kuanza katika ngazi ya chini.

Aidha, nae mmoja wa Maprodyuza hao Quick Raca atoa maoni kuwa ya kuiomba COSOTA kuwa na mfumo wa kusimamia matumizi ya kazi za wanamuziki kwa kutoa msisisitizo  kwa Makampuni  yaliyosaini mikataba na wasanii peke yao kwa kazi zinazohusisha haki za "Maproducer"  makampuni hayo sasa yaingie mikataba pia na ‘Producers’ ili yaanze kulipa na "producers", na kuanzia sasa  utaratibu wote upitie COSOTA vilevile  matumizi ya kazi za muziki kwenye mitandao yote ilipwe na wanaotumia, halikadhalika Televisheni na Redio zisipige au kuonyesha kazi ya Muziki kama haijapita kukaguliwa BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania na kusajiliwa COSOTA.

Pamoja na hayo Maprodyuza hao waliridhia ushauri wa kuanza  kujisajili kwenye chama chao na pia kujisajili COSOTA na kusajili kazi zao COSOTA na  kwa taasisi zinazowasimamia pamoja na kuanza kuwa na utaratibu wa kutumia mikataba katika kazi zao.

Halikadhalika  Doreen  aliahidi  kuwa COSOTA itatoa  sampuli ya mikataba   hiyo bure na zitakabidhiwa TPCA ili kuweza kuwafikishia wadau hao. Pia aliwasisitiza kuwa umoja wao ukiwa imara na wenye manufaa wadau wengi wanaweza kujiunga na kunufaika zaidi.hivyo ni vyema wajenge misingi imara ya kukuza tasnia hiyo kwa lengo la kuweza kunufaika vyema na kazi zao.



Share:
Read More →

Mfumo wa Masoko ya Madini Umeongeza Makusanyo Serikalini

 Unknown     16:55:00     NEWS     No comments   


Na Steven Nyamiti, Kahama.
Imeelezwa kuwa, Wizara kupitia Tume ya Madini kupanga  bei elekezi ya kuuza madini Nchini umesaidia wauzaji na wanunuzi kuondoa ulanguzi wa bei, na kuchochea wachimbaji kuleta madini yao kwa wingi kwenye masoko ya madini Nchini.


Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Kimadini Kahama Fabian Itaru tarehe 17 April, 2021 katika ziara yake na wanahabari kutembelea Masoko ya Madini, Vituo vya ununuzi wa Dhahabu na maeneo ya machimbo ya Dhahabu wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.


Ameeleza kuwa, kuanzishwa kwa masoko ya madini kumefanya Dhahabu yote kuingia kwenye mfumo wa soko na malipo halali ya Serikali kukusanywa kwa wakati.


"Kuanzishwa kwa masoko haya kumeongeza mapato kwa Serikali. Ofisi ya madini kipindi cha nyuma ilikuwa inapewa lengo la kukusanya bilioni 45 kwa Mwaka ambapo kabla ya kuanzishwa masoko hayo Mwaka 2016 hatukuwahi kufikia lengo, lakini baada ya kuanzishwa masoko ya madini malengo ya Ofisi ya Madini Kahama kupitia Tume ya Madini yamefikia lengo.Mwaka huu tumepangiwa kukusanya bilioni 79 ambapo hadi sasa tumekusanya bilioni 72 sawa na wastani wa asilimia 91" ameeleza Itaru


Amefafanua kuwa, Makusanyo hayo yametokana na masoko ya Madini, shughuli nyingine za Wachimbaji wadogo, Kodi za leseni zinazolipwa, mrabaha na ada za ukaguzi zitokanazo na uzalishwaji wa Dhahabu Kahama.


Naye, Mjiolojia Samuel Baruti kutoka Tume ya Madini akizungumza Katika kituo cha Ununuzi Madini Mwime Kahama, amewaeleza wanahabari kuwa, huko nyuma hali ilikuwa ngumu Sana kwa wachimbaji wadogo kabla Serikali haijaanzisha utaratibu wa masoko.


Amesema kulikuwa na watu wanafanya biashara mitaani na kujipangia bei tofauti na kipindi hichi ambacho Serikali inapanga bei elekezi ili mchimbaji mdogo aweze kuona faida ya uchimbaji wake.


Ameeleza kuwa, miaka ya nyuma mfaidika mkubwa alikuwa mfanyabiashara wa madini lakini baada ya kuanzisha mfumo wa masoko umefanya  wafanyabiashara kukusanyika eneo moja katika soko la madini.


Kwa Upande Meneja  wa Umoja  wa Kwenye Mashamba  Ilindi  Mwime Joseph Nalimi, akieleza kwa niaba ya wachimbaji wadogo Mwime ameiomba wizara kuwasaidia  wachimbaji wadogo ili  waweze kukopesheka na kupata udhamini wa mabenki, kutengeneza miundombinu ya machimbo ya Mwime, na kupata ripoti ya kijiolojia ya maeneo yao ili waache kuchimba kwa kubahatisha.


Nalimi, ameishukuru ofisi ya madini Mkoa wa Kimadini Kahama kwa kuanzisha vituo vya uuzaji na ununuzi Dhahabu karibu na maeneo ya machimbo ambavyo vimesaidia kupata soko la uhakika la Dhahabu




Share:
Read More →

Waziri Aweso Amtumbua Kigogo Wa Moruwasa

 Unknown     16:55:00     NEWS     No comments   

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewasimamisha kazi vigogo wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (Morowasa) ili kupisha uchunguzi wa wa tuhuma ambazo zinawakabili huku akiagiza watumishi wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Vigogo waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba,Afisa Maji wa Bonde la Wami Ruvu Bwana Simon Ngonyani huku akiagiza watumishi wengine waliokuwa vinara wa kueneza chuki na kuleta taharuki badala ya kufanya kazi nao wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Waziri Aweso aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambapo alisema kuwa Mkurugenzi wa Moruwasa pamoja na tuhuma nyingine za kiutumishi lakini alisaini mkataba wa fedha nyingi na wakandarasi bila kushirikisha Wizara na hata bila uwepo wa Katibu Mkuu kinyume na taratibu.

Huku Afisa  wa Bonde akisimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya utumishi.


Share:
Read More →

WAZIRI AWESO AWASHA MOTO MOROGORO AMTUMBUA KIGOGO WA MORUWASA

 Unknown     14:55:00     NEWS     No comments   

 


 

Na Mwandishi,Morogoro

  

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewasimamisha kazi vigogo wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (Morowasa) ili kupisha uchunguzi wa wa tuhuma ambazo zinawakabili huku akiagiza watumishi wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

 

Vigogo waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Mhandisi Tamimu Katakweba,Afisa Maji wa Bonde la Wami Ruvu Bwana Simon Ngonyani huku akiagiza watumishi wengine waliokuwa vinara wa kueneza chuki na kuleta taharuki badala ya kufanya kazi nao wachukuliwe hatua za kinidhamu.

 

Waziri Aweso aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambapo alisema kuwa Mkurugenzi wa Moruwasa pamoja na tuhuma nyingine za kiutumishi lakini alisaini mkataba wa fedha nyingi na wakandarasi bila kushirikisha Wizara na hata bila uwepo wa Katibu Mkuu kinyume na taratibu.

 

Huku Afisa  wa Bonde akisimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya utumishi.

 

Mwisho.

Share:
Read More →

Rais Samia Afanya Uteuzi Wa Mkuu wa Itifaki na Mkurugenzi Mkuu wa eGA

 Unknown     12:55:00     NEWS     No comments   


 Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Yusuf Mndolwa kuwa Balozi.

Pamoja na uteuzi huo, Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Mteule Mndolwa kuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi Mteule Mndolwa anachukua nafasi iliyoachwa na Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi Mteule Mndolwa ataapishwa Jumatatu aprili 19, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Wakati huo huo Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Benedict Ndomba kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

Kabla ya uteuzi huo Ndomba alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu na Operesheni wa eGA na anachukua nafasi ya Dkt. Jabir Kuwe ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Uteuzi wa viongozi hao umeanza Aprili 17, 2021.


Share:
Read More →

Vijana 854 wa JKT walioandamana kwenda Ikulu watimuliwa

 Unknown     12:55:00     NEWS     No comments   


Mkuu wa majeshi nchini Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema vijana 854 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kuandamana kwenda Ikulu wakishinikiza kuajiriwa jeshini  wamesitishiwa mikataba yao na kurudishwa majumbani.

Mabeyo ameeleza hayo jana Jumamosi Aprili 17, 2021 katika hafla ya kuwatunuku kamisheni maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mjini Dodoma.

"Aprili 8,  2021 vijana wetu wa JKT wapatao 854 walianzisha mgomo,  kukataa kufanya kazi maeneo mengine  na kufanya maandamano kwenda Ikulu kwa madai ya kutaka kumuona rais ili wadai kuandikishwa jeshini kama walivyoahidiwa na aliyekuwa rais wa Tanzania,  John Magufuli."

"Vijana hao ni kati ya vijana 2400 walioahidiwa kuandikishwa jeshini na walifanya uamuzi huo baada ya jeshi kuamua kuwapunguza katika kazi ya ujenzi wa Ikulu Chamwino baada ya kazi kupungua ili waende kufanya kazi katika maeneo mengine lakini wao wakapinga kwa madai wangekosa kuandikishwa jeshini, " amesema Mabeyo.

Amebainisha kuwa jeshi halikuwa na lengo hilo na limelazimika kusitisha mikataba yao kwa kuwa kosa walilolifanya ni sawa na uasi na hauvumiliki.

Ameeleza kuwa pamoja na  kufanya uchunguzi  wa kwa nini walifanya hivyo,  jeshi limeamua kutafakari upya mpango wa kuchukua vijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na JKT.


Share:
Read More →

Waziri aiagiza OSHA kufanya tathmini ya maeneo ya kazi yenye ajali,magonjwa mengi

 Unknown     11:55:00     NEWS     No comments   


Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameagiza Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kufanya tathmini ya maeneo ya kazi yanayoongoza kwa matukio ya ajali na magonjwa pamoja na kubainisha visababishi vyake ili kuwezesha uandaaji wa mkakati wa kudhibiti visababishi hivyo.

Ametoa agizo hilo alipokuwa akifungua kikao cha pili cha baraza la wafanyakazi wa OSHA kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022.

“Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu inaonesha taasisi yenu imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambayo yametokana na maboresho mbali mbali ambayo yamekuwa yakifanyika na serikali ikiwemo kuondoa baadhi ya tozo ambazo zilionekana kuwa kero.Hivyo, nawaagiza kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuweza kufikia lengo letu la kupunguza ajali na magonjwa yatokanayo na kazi na kuleta ustawi wa Taifa letu,” alieleza Mhagama.

Waziri huyo wa Nchi aliwashauri wajumbe wa kikao hicho kufanya majadiliano katika kikao hicho kwa hekima na busara na hatimaye kutoka na maazimio muhimu ambayo yatafanyiwa kazi ili kutimizi malengo ya taasisi.

Aidha, aliitaka taasisi ya OSHA kuendelea kubuni mifumo mbali mbali ya Tehama ambayo itaboresha utoaji wa huduma kwa wadau pamoja na kuweka taratibu za huduma ambazo ni rafiki kwa wadau ili kuendana na maelekezo ya serikali.

Awali wakati akimkaribisha Waziri ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika kikao hicho, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema maboresho ambayo yamekuwa yakifanyika na serikali katika sekta ya biashara na uwekezaji ikiwemo kuondoa baadhi ya tozo, yamepelekea taasisi hiyo kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza usajili wa maeneo ya kazi kutoka 5,300 hadi 20,000 kwa kipindi kati ya mwaka wa fedha 2014/2015 na 2020/2021.

Kwa upande wao mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Taifa, Fidelis Athuman na Mjumbe wa Baraza hilo, Joyce Mwambungu, wameipongeza serikali na uongozi wa OSHA kwa maboresho ya utendaji ambayo yamekuwa yakifanyika kutokana na ushirikishwaji wa watumishi kupitia vikao vya mara kwa mara vya baraza la wafanyakazi.

Kikao hiki ambacho ni cha pili cha baraza la nne la wafanyakazi wa OSHA pamoja na masuala mengine, kilikuwa na agenda kuu ya kupitia bajeti ya mwaka  wa fedha ujao (2021/2022).

Mabaraza ya wafanyakazi katika taasisi mbali mbali za umma yapo kwa mujibu wa Sheria Na. 19 ya Mabaraza ya mwaka 2003 ambayo iliundwa kupitia Waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 1970. Lengo likiwa ni kuleta ushirikishwaji baina ya menejimenti na watumishi katika kufanya maamuzi yanayohusu utendaji wa taasisi husika.


Share:
Read More →

Utumishi Kusimamia Utekelezaji Ahadi Za Masuala Ya Kiutumishi Kwenye Ilani Ya Ccm Ya Mwaka 2020

 Unknown     11:55:00     NEWS     No comments   


Na. James K. Mwanamyoto
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Watumishi wa Ofisi yake kusimamia utekelezaji wa ahadi za masuala ya kiutumishi na utawala bora zilizoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 ili kuhakikisha Sekta ya Umma inaimarika na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi yake uliofanyika jijini Dodoma.

Mhe. Ndejembi amelitaka baraza hilo kupitia na kuchambua Ilani kwa kina na kubaini ahadi zinazohusu Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa ufanisi mkubwa ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

Akihimiza utekelezaji wa Ilani katika Taasisi za Umma, amewataka Watumishi wa Umma kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi ili kuiwezesha Serikali kutekeleza ahadi ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Ndejembi amesema, licha ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi kufanya kazi kwa weledi katika kutekeleza Ilani, lakini wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanabadili mtazamo hasi dhidi yao kwani malalamiko mengi yanayowasilishwa Utumishi yanatokana uzembe wa Watumishi wa Taasisi nyingine.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa baraza, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bi. Agnes Meena amemuahidi Mhe. Ndejembi kuwa, Utumishi itahakikisha inaishauri vizuri Serikali kutekeleza Ilani na kuongeza kuwa, watumishi wataendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuiwezesha ofisi kufikia malengo yake.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imefanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi kwa mujibu wa sheria, ambapo Taasisi za Umma zinapaswa kukutana kupitia mpango na bajeti itakayowasilishwa Bungeni, kabla Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijapitisha bajeti husika kwa ajili ya utekelezaji.


Share:
Read More →

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo April 18

 Unknown     06:55:00     NEWS     No comments   


Share:
Read More →

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 18,2021

 Unknown     05:55:00     NEWS     No comments   








 

     
    Share:
    Read More →

    Saturday, 17 April 2021

    WANANCHI WACHANGIA MADAWATI 336, SH. MILIONI 5.6 SHULE YA SEKONDARI SOLWA , DC MBONEKO APONGEZA

     Unknown     21:55:00     NEWS     No comments   

    Muonekano wa madawati yaliyotolewa na wananchi kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa

    Na Shinyanga Press Club Blog
    Wananchi wa Kata ya Solwa wilayani Shinyanga wameamua kutengeneza madawati 336 na kuyakabidhi katika shule ya Sekondari Solwa iliyokuwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madawati kwa lengo la kutatua kero hiyo ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini.

    Mbali na msaada huo wa madawati, Wananchi hao wamechangia zaidi ya Sh. 5,600,000 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo ili kupunguaza uhaba uliopo kwa sasa.

    Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na Shinyanga Press Club Blog wakati wakikabidhi madawati hayo wazazi hao waliotengeneza madawati zaidi ya 336 kwa gharama ya shilingi 23,6000,000 ikiwa ni nguvu zao wenyewe, wamesema wameamua kufanya hivyo ili kutokomeza upungufu wa madawati uliokuwepo awali ukisababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini.

    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje amesema halmashauri iko tayari kutoa fedha za kukamilisha maabara ya shule hiyo, huku akimtaka Kaimu Mkurugenzi kufikisha suwala hilo panapohusika ili fedha hizo ziandaliwe mapema na kutolewa ili wanafunzi wa masomo ya sayansi wafanye vizuri katika masomo yao.

    Naye, Diwani wa Kata ya Solwa, Awadhi Abood amesema licha ya wananchi kutengeneza madawati hayo 363 kwa nguvu zao wenyewe na kuchangia Sh. Milioni 5.6 za ujenzi wa vyoo vya wanafunzi, lakini pia wameweka mpango kazi wa kujenga madarasa manne zaidi kwa nguvu zao wenyewe ambapo mchanga na mawe tayari wameshakusanya.

    Mkuu wa shule ya Sekondari Solwa, Thomas Manembe amesema kuwa msaada huo wa madawati umeifanya shule kuwa na ziada ya madawati 61.

    Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ambaye pia ni Menyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo, amewapongeza wananchi hao kwa juhudi zao za kusaidia na kutatua matatizo yanaisibu jamii yao, ambapo ametoa agizo wanafunzi watoro katika shule zote za wilaya hiyo wafuatiliwe na kurudi shuleni maramoja.

    Vilevile, Mboneko ametoa onyo kwa baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuwatupia mapepo wanafunzi haswa wasichana kwa lengo la kuwasababishia kufanya vibaya katika mitihani yao ya kuhitimu wakiwa na malengo kuwaozesha na kujipatia mali.

    DC Mboneko pia amewataka wanafunzi wa shule hiyo kutumia nafasi ya elimu kutimiza malengo na ndoto zao kwa kuacha tamaa za kimwili zinazosababishwa na watu wasio na malengo mazuri juu yao.
    Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kushoto) na baadhi ya viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakiwa wameshikilia kiti ambacho ni sehemu ya msaada uliotolewa na wananchi
    Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ngasa Mboje (kushoto) wakiwa wameshikilia dawati ambalo ni sehemu ya msaada wa madawati 336 yaliyotolewa na wananchi kwa ajili ya shule ya Sekondari Solwa
    Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kushoto) na baadhi ya viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakiwa wameshikilia kiti ambacho ni sehemu ya msaada uliotolewa na wananchi
    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (kushoto) akimkabidhi msaada wa madawati, Mkuu wa Shule ya Sekondari Solwa, Thomas Manembe (kulia)
    Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Solwa baada ya kukabidhi msaada wa madawati uliotolewa na wananchi wa kata ya Solwa
    Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza shuleni hapo baada ya kukabidhi msaada huo uliotolewa na wananchi wa Kata ya Solwa

    Sehemu ya madawati 336 yaliyotolewa na wananchi wa kata ya Solwa kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Solwa
    Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi msaada huo
    Diwani wa Kata ya Solwa, Awadhi Abood akizungumza wakati za zoezi la kukabidhi msaada huo shuleni hapo
    Mkuu wa Shule ya Sekondari Solwa akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati 336 kutoka kwa wananchi, msaada ambao umeiwezesha shule hiyo kumaliza tatizo la madawati na kuwa na akiba ya madawati 61

     CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG
    Share:
    Read More →

    NAMNA NILIVYOMKAMATA MME NA BEST YANGU WAKILA URODA KITANDANI KWANGU

     Unknown     21:55:00     NEWS     No comments   
    Share:
    Read More →
    ← Newer Posts Older Posts → Home
    Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

    Popular Posts

    • MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
      Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa na watu wengi,ni kuhusu ...
    • UPDATED:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
      Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa m...
    • NECTA:HAYA HAPA MATOKEO DARASA LA SABA 2017
      NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2017 EXAMINATION RESULTS ANGALIA MATOKEO YAKO KWA KUBONYEZA MKOA WAKO HAPO CHINI, ...
    • MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 10,027 WALIOKOSEA KUJAZA FORM ZA MIKOPO BODI YA MIKOPO 2016/2017
        KUONA MAJINA HAYO   << BONYEZA HAPA--PDF >>
    • BREAKING NEWS:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MWAKA WA MASOMO 2016/2017
        Bodi ya mikopo ya elimu ya juu wametangaza majina ZAIDI YA 20000 ya wanafunzi waliopata mkopo 2016/2017. Kama utahitaji kuangaliziwa j...
    • MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
      Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa ma...
    • MPYA:HAYA HAPA MAJINA (KATIKA PDF) WANAFUNZI SPECIAL DIPLOMA WALIOPANGIWA KURUDI UDOM &VYUO VINGINE 2016
      >>> CLICK HERE FOR LIST OF SELECTED STUDENT - UDOM (53.28 kB)<<<  CLICK HERE FOR LIST OF SELECTED STUDENTS - TEACHER ...
    • ANGALIA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWAPAMOJA NA APPLICATIONS FOR ADMISSION INTO NON DEGREE (DIPLOMA AND CERTIFICATE) PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017-NACTE
                        Nacte wametoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kuchaguliwa  katika vyuo mbalimbali  afya,ualimu ,kil...
    • MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
      Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa ma...

    Unordered List

    Pages

    Blog Archive

    • ▼  2026 (268)
      • ▼  April (79)
        • KAGERA KUNUFAIKA NA MPANGO WA MKOA WA AFYA MOJA
        • DKT. MAULID AONGOZA KIKAO CHA BODI YA CHUO CHA MAJI
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 29,2026
        • KUTANA NA MTABIBU WA NY0TA ZA BINADAMU, BINGWA WA ...
        • WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BELARUS AWASILI NCHINI K...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 28,2026
        • MARIDHIANO YATALIPONYA TAIFA NA KUDUMISHA AMANI NA...
        • WENZA WA MAJAJI WAWAFARIJI WAGONJWA WA SARATANI DAR
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 27,2026
        • WATANZANIA WATAKIWA KUENZI MISINGI YA MUUNGANO
        • TAIFA GESI YATOA ELIMU YA MATUMIZI SALAMA YA GESI ...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 26,2026
        • WANANCHI SHINYANGA WAPOKEA RIPOTI YA JAJI CHANDE K...
        • WAFANYABIASHARA SOKO LA NAMANGA KAHAMA WALALAMIKIA...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 25,2026
        • MKUTANO WA KIKANDA WAJADILI USALAMA NA BIASHARA YA...
        • Video Mpya : SHINJE ORIGINAL - YA MOTO BALAA
        • TAMCU YAIMARISHA UCHUMI WA WAKULIMA TUNDURU KWA UN...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 24,2026
        • HAMU YA MARIDHIANO: VIONGOZI WA DINI NA WANASIASA ...
        • AMANI YATAJWA KAMA MTAJI WA MAENDELEO NA USTAWI WA...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 23,2026
        • RAIS SAMIA ASHIRIKI KONGAMANO LA KITAIFA LA MAMA N...
        • MASHAHIDI 553 WAMELETA USHAHIDI KWA KIAPO NA MAAND...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 22,2026
        • UVCCM BUKOBA YATOA VIFAA VYA MICHEZO KUELEKEA MASH...
        • UVCCM BUKOBA YATOA VIFAA VYA MICHEZO KUELEKEA MASH...
        • TUMUOMBEE RAIS, TULIOMBEE TAIFA-MASHILI
        • DIWANI WA KATA YA KILIMANI JIJINI DODOMA AANZA ZIA...
        • BARRICK BULYANHULU YAKABIDHI TREKTA WILAYA NYANG’W...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 19,2026
        • WACHIMBAJI WA MADINI MWAKITOLYO WALIA NA TOZO MPYA...
        • RAIS SAMIA AMERIDHIA MILIONI 544 ZILETWE BAHI KUJE...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 18,2026
        • OFISI YA AFISA MADINI MKAZI MKOA WA SINGIDA YATOA ...
        • MTANDA AAGIZA UKAGUZI MKALI WA MAZINGIRA MWANZA
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 17,2026
        • TANZANIA YAONESHA MAFANIKIO YA MAGEUZI SEKTA YA AF...
        • JAJI MKUU MSTAAFU: TANZANIA INA UWEZO WA KUTATUA C...
        • NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AWASILI BRAZIL KUKUZA DIPLOM...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 15 2026
        • CRDB YAWAPA DILI NONO WATEJA: WASHINDI KUSAFIRI MA...
        • SANGU APIGILIA MSUMARI TUNU ZA TAIFA: ASEMA AMANI ...
        • LALJI FOUNADATION YAENDESHA KAMBI YA MATIBABU YA M...
        • AMANI NA MARIDHIANO: NGUZO KUU INAYOIFUNGULIA SIDO...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 13, 2026
        • Video Mpya : MAMA USHAURI - MILEMBE
        • Video Mpya : YOGATI - MAISHA
        • MOIL ENERGIES YAIPONGEZA TRA KWA MFUMO MPYA WA ULI...
        • PROF. SHEMDOE AELEKEZA WAFANYABIASHARA SOKO LA SIM...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 11,2026
        • MWANAMKE CHUMA MAENDELEO GROUP YATOA MSAADA KWA WA...
        • MUYINGA AISHUKIA CHADEMA KUHUSU KIINI CHA VURUGU Z...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 10, 2026
        • SANGU ASISITIZA UMUHIMU WA TAASISI ZA KIDINI KATIK...
        • GAVANA TUTUBA :TANZANIA IMEPIGA HATUA MIFUMO YA MA...
        • JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI N...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 9,2027
        • SERIKALI YAINUA UTALII WA TIBA: WAGONJWA WA NJE WA...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 8,2026
        • BARRICK NORTH MARA YAWEZESHA VIJANA TARIME KUANZIS...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRILI 7,2026
        • TUME YA UCHUNGUZI YAONGEZEWA MUDA TENA HADI APRILI...
        • POLISI TANGA WAOKOA VIJANA 87 WALIOINGIZWA KWENYE ...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 6,2026
        • UKOMAVU WA KISIASA: RAIS SAMIA AZIBA MAKOVU YA UCH...
        • MALUNDE 1 BLOG INAKUTAKIA SIKUKUU NJEMA YA PASAKA!
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 5,2026
        • MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA SHINGO SHINYANGA
        • KAHAMA KUCHEKA KWA NGUVU JUMAMOSI HII !! LIVE COME...
        • BAGAMOYO YAVUTA WAWEKEZAJI, MAOMBI 48 YAPOKELEWA
        • DKT. GWAJIMA ATOA WITO KWA JAMII NA WAZAZI KUSHIRI...
        • Video Mpya : JINASA MADEBE - MAJIVUNO
        • SERIKALI YAPANUA WIGO WA MAFUNZO NA FURSA ZA AJIRA...
        • POLISI YAJIDHATITI KUHAKIKISHA USALAMA NA UTULIVU ...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 2,2026
        • Wimbo Mpya : MALIGANYA MADIRISHA - YAKALE
        • PROF. SHEMDOE AWASILISHA RANDAMA YA MAKADIRIO YA M...
        • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 1,2026
      • ►  March (62)
      • ►  February (55)
      • ►  January (72)
    • ►  2025 (993)
      • ►  December (73)
      • ►  November (67)
      • ►  October (72)
      • ►  September (92)
      • ►  August (82)
      • ►  July (84)
      • ►  June (76)
      • ►  May (92)
      • ►  April (86)
      • ►  March (91)
      • ►  February (83)
      • ►  January (95)
    • ►  2024 (1017)
      • ►  December (89)
      • ►  November (89)
      • ►  October (73)
      • ►  September (94)
      • ►  August (86)
      • ►  July (85)
      • ►  June (86)
      • ►  May (94)
      • ►  April (92)
      • ►  March (101)
      • ►  February (30)
      • ►  January (98)
    • ►  2023 (1772)
      • ►  December (99)
      • ►  November (101)
      • ►  October (130)
      • ►  September (102)
      • ►  August (150)
      • ►  July (162)
      • ►  June (165)
      • ►  May (178)
      • ►  April (172)
      • ►  March (188)
      • ►  February (162)
      • ►  January (163)
    • ►  2022 (1846)
      • ►  December (173)
      • ►  November (161)
      • ►  October (190)
      • ►  September (188)
      • ►  August (185)
      • ►  July (146)
      • ►  June (116)
      • ►  May (130)
      • ►  April (126)
      • ►  March (120)
      • ►  February (136)
      • ►  January (175)
    • ►  2021 (7035)
      • ►  December (284)
      • ►  November (598)
      • ►  October (641)
      • ►  September (638)
      • ►  August (619)
      • ►  July (616)
      • ►  June (617)
      • ►  May (637)
      • ►  April (581)
      • ►  March (621)
      • ►  February (539)
      • ►  January (644)
    • ►  2020 (7392)
      • ►  December (597)
      • ►  November (589)
      • ►  October (586)
      • ►  September (618)
      • ►  August (680)
      • ►  July (625)
      • ►  June (614)
      • ►  May (591)
      • ►  April (606)
      • ►  March (632)
      • ►  February (624)
      • ►  January (630)
    • ►  2019 (7895)
      • ►  December (611)
      • ►  November (643)
      • ►  October (673)
      • ►  September (664)
      • ►  August (679)
      • ►  July (677)
      • ►  June (619)
      • ►  May (725)
      • ►  April (622)
      • ►  March (477)
      • ►  February (604)
      • ►  January (901)
    • ►  2018 (409)
      • ►  December (388)
      • ►  August (1)
      • ►  July (1)
      • ►  June (2)
      • ►  May (2)
      • ►  April (7)
      • ►  March (2)
      • ►  February (1)
      • ►  January (5)
    • ►  2017 (450)
      • ►  December (1)
      • ►  November (1)
      • ►  October (119)
      • ►  September (7)
      • ►  August (2)
      • ►  July (10)
      • ►  June (23)
      • ►  May (28)
      • ►  April (39)
      • ►  March (16)
      • ►  February (77)
      • ►  January (127)
    • ►  2016 (2803)
      • ►  December (246)
      • ►  November (198)
      • ►  October (274)
      • ►  September (286)
      • ►  August (251)
      • ►  July (233)
      • ►  June (260)
      • ►  May (309)
      • ►  April (210)
      • ►  March (233)
      • ►  February (264)
      • ►  January (39)
    • ►  2015 (1416)
      • ►  December (24)
      • ►  November (102)
      • ►  October (186)
      • ►  September (89)
      • ►  August (80)
      • ►  July (229)
      • ►  June (197)
      • ►  May (61)
      • ►  April (266)
      • ►  March (105)
      • ►  February (50)
      • ►  January (27)
    • ►  2014 (1347)
      • ►  December (21)
      • ►  November (33)
      • ►  October (51)
      • ►  September (43)
      • ►  August (40)
      • ►  July (202)
      • ►  June (287)
      • ►  May (328)
      • ►  April (159)
      • ►  March (61)
      • ►  February (118)
      • ►  January (4)

    Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger