Saturday, 17 April 2021

Kampuni Ya Israel Yaanza Mazungumzo Ya Awali Ya Uwekezaji Katika Sekta Ya Mifugo Nchini


Na. Edward Kondela
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amekutana na kufanya mazungumzo ya awali na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Holding ya nchini Israel Bw. Avi Postelnik yenye lengo la kuwekeza hapa nchini kupitia sekta mbalimbali zikiwemo za mifugo na uvuvi.

Akizungumza jana (16.04.2021) mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yao ya awali katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo jijini Dar es Salaam, Prof. Gabriel amesema katika mazungumzo yao wameainisha fursa kubwa zilizopo hapa nchini ikiwemo ya unenepeshaji mifugo na uongezaji thamani wa bidhaa zitokanazo na mazao ya mifugo.

Amesema nchi ya Israel ina ng’ombe ambao wana uwezo wa kutoa lita 40 hadi 50 za maziwa kwa siku moja na kwamba Bw. Postelnik amewaona ng’ombe wa aina hiyo hapa nchini katika Mkoa wa Kagera.

“Kwa bahati nzuri tayari kosaafu hiyo ya ng’ombe ameiona hapa Tanzania katika Mkoa wa Kagera na tuna dume la ng’ombe kutoka nchini Israel, ambalo lipo katika Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) kilichopo Mkoani Arusha.” Amefafanua Prof. Gabriel

Aidha, ameongeza kuwa mkakati mzuri ukiwekwa baina ya Tanzania na Israel katika kukuza sekta ya mifugo hapa nchini, wafugaji wanaweza kupata faida kubwa hasa baada ya Israel kuwa na teknolojia ya kutengeneza malisho ya mifugo kwa kutumia mabaki ya mazao ya mifugo.

Katika mazungumzo hayo wamegusia umuhimu wa masoko ya bidhaa za mifugo na uvuvi, ambapo wamekubaliana kuwa na masoko ya bidhaa za mifugo na uvuvi katika nchi mbalimbali kutatoa hamasa zaidi kwa wafugaji na wavuvi kuzalisha zaidi bidhaa zao.

Katika mazungumzo hayo ya awali ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Holding ya nchini Israel Bw. Avi Postelnik wamesema eneo ambalo wanalipa kipaumbele kwa sasa katika sekta ya mifugo ni ufugaji wa ng’ombe na uzalishaji wa mazao yatokanayo na ng’ombe ukifuatiwa na ufugaji wa kuku.

MWISHO.


Share:

Watumishi Wizara ya Habari wametakiwa kuwa wabunifu kufikia malengo ya Serikali


Na Eleuteri Mangi-WHUSM, Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ametaka watumishi wa Wizara hiyo kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao hatua inayoboresha utendaji kazi na kufikia malengo ya Serikali.

Waziri Bashungwa amesema hayo leo Aprili 17, 2021 Jijini Dodoma katika kikao cha wafanyakazi wa Wizara hiyo chenye lengo la kuwakaribisha viongozi wapya pamoja na kufanya kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo.

“Wizara hii ni ya furaha kulingana na sekta zake, nasisitiza upendo, uaminifu  na ushirikiano  na kuchapa kazi kwa weledi  na kuongeza ubunifu katika kazi tunazofanya kwa maslahi ya Taifa hili” amesema Waziri Bashungwa.


Aidha, Waziri Bashungwa amesisitiza kuwa Viongozi na watumishi wa Wizara hiyo ni lazima kufanya kazi kwa bidii na jitihada katika maeneo yao ya kazi kwa kuungaanisha nguvu kwa kuwa wanasifa kwenye nafasi zao ili Wizara hiyo iweze kufika mbali zaidi katika kuwatumikia Watanzania.

“Naamini katika ushirikiano, sisi viongozi wenu tunachotarajia ni kuona mnaendelea kuwa wazalendo, wachapakazi, wabunifu na kuwa watu mnaowekeza katika bidii ya utendaji na sio majungu, fitna na uzembe kazini” amesema Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa ameongeza kuwa Wizara yake tayari imetekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kuhusu kufungulia Vyombo vya Habari hususan Online TV ambapo maagizo hayo yameyatekeleza kwa kushirikiana na Wizara ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano kupitia Mamlaka ya Mawasilano Tanzania (TCRA).

Kwa upande wake Naibu Waziri katika Wizara hiyo Mhe.Pauline Gekul amemshukuru Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kumpa ushirikiano  na kutoa matokeo anayotarajia.

Naibu Waziri Gekul amewasisitiza watumishi hao kushirikiana katika kufanya kazi kwasababu Wizara hiyo ni nyeti na inagusa maisha ya watu kupitia sekta zake na kuikumbusha jamii kuzingatia utamaduni pamoja na kuimarisha na  kuenzi mila na desturi za nchi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amekuwajulisha watumishi hao kuwa Bajeti ya Wizara inaendelea kuongozeka mwaka hadi mwaka ikiwemo Bajeti ya Maendelo pamoja na ile matumizi mengine.

Kwa mwaka ujao wa fedha wa 2020/2021 Wizara inatarajia kuwa na ongezeko la Bajeti ya Fedha za maendeleo kufikia Bilioni 20 kutoka  shilingi Bilioni 7.7 Mwaka uliopita na fedha za matumizi mengine zimeongezeka na kutoka Shilingi Bilioni 11 kwa mwaka 2019/2020 na inatarajiwa kufikia Bilioni 14 kwa mwaka ujao wa Fedha 2020/2021  amabazo zimetengwa kutekeleza majukumu ya Wizara hiyo.



Share:

Ukurasa wa historia wageuka Cuba: Raul Castro kuachia ngazi


Katika siku chache, Fidel Castro hatakuwa tena madarakani nchini Cuba: kongamano la Chama cha Kikomunisti, ambalo lilifunguliwa jana Ijumaa, litasitisha miongo sita ya utawala wa kidugu ambao sasa unaachia kizazi kipya nafasi.

Baada ya kifo cha Fidel Castro mnamo mwaka 2016, kustaafu kwa Raul, ambaye hivi karibuni atatimiza umri wa miaka 90, ambaye alimkabidhi kijiti cha uongozi wa nchi Rais Miguel Diaz-Canel, 60, ukurasa wa kihistoria kwa kisiwa hicho na wakaazi wake unabadilika, ambapo karibu wakaazi wote wa Cuba hawaijui familia yoyote katika uongozi wa nchi hiyo kuliko ile ya wanamapinduzi maarufu.

"Raul hatakuwa kiongozi wa chama tena, lakini ikiwa kuna tatizo Raul atakuwepo, hajafa", Ramon Blande, mwanaharakati wa kikomunisti, 84, amesema.

Kuanzia  jana saa 3:00 asubuhi (sawa na saa7:00 mchana ), wajumbe zaidi ya mia moja wa chama kimoja, kutoka majimbo yote, watakutana kwa siku nne hadi siku ya Jumatatu  katika mji mkuu, kwenye vikao mbalimbali, kujadili maswala makubwa ya nchi.

Uteuzi wa Bwana Diaz-Canel kama katibu mpya wa kwanza, wadhifa muhimu zaidi nchini Cuba, unatarajiwa kufanyika siku ya mwisho, Jumatatu.

 

-RFI




Share:

Urusi yaijibu Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake


Urusi imewataka wanadiplomasia 10 wa Marekani kuondoka nchini humo katika hatua ya kulipiza kisasi baada ya Marekani kuwafukuza wanadiplomasia 10 wa Urusi kwa madai ya udukuzi na kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka uliopita.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema John Sullivan, ambaye ni balozi wa Marekani nchini Urusi, anapaswa kurudi nyumbani katika kile walichosema ni kwa mashauriano zaidi.

Kupitia taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema huu ni wakati wa Marekani kuonyesha ukomavu wake wa kiakili na kugeuza mkondo wao wa kugombana.

Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa ina uwezo wa kuiumiza zaidi Marekani kuichumi na kupunguza idadi ya wanadiplomasia wa Marekani nchini Urusi hadi 300, japo kwa sasa haitachukua hatua hiyo.

Uamuzi wa Urusi, ukiwa sehemu ya mpango mpana wa kulipiza kisasi, uliidhinishwa na Rais Vladimir Putin kama jibu kwa Marekani baada ya serikali ya Joe Biden kuiwekea vikwazo Urusi.

Hata hivyo licha ya Moscow kujibu kwa haraka na kuweka hatua ambazo zinanuia kupunguza ushawishi wa Marekani nchini Urusi, Urusi imeacha mwanya wa mazungumzo uliopendekezwa na Rais Joe Biden aliyetaka kufanyika mkutano kati yake na Putin ili kujadili masuala kadhaa.

Credit:BBC



Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Awataka Watanzania Kuwalinda Vijana


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuhusika na ulinzi wa watoto kwa kuweka mipango itakayoondoa mazingira yanayowafanya vijana balehe kuwa na tamaa ya vitu na kushawishika kujiingiza kwenye ngono katika umri mdogo.

”Suala la mimba za utotoni limekuwa mwiba kwa kipindi kirefu. Limekuwa likiwanyima wasichana wengi fursa ya kukamilisha malengo yao katika maisha. Hali hii haikubaliki lazima kila mmoja kwa nafasi yake aweke mikakati ya kuwawezesha watoto wa kike kumaliza masomo yao”.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 17, 2021) wakati wa uzinduzi wa Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo kwa Vijana Balehe katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, jijini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu amesema programu za kuelimisha Vijana Balehe kuhusu madhara ya kuanza ngono mapema ziandaliwe ili washiriki kikamilifu katika masomo na masuala mengine ya maendeleo kwa kuwawezesha kupata taarifa sahihi.

Waziri Mkuu amesema takwimu za Elimu Msingi Tanzania (BEST – 2020) zimeonesha kuwa jumla ya watoto 1,135 katika shule za msingi na 5,340 katika shule za sekondari waliacha shule kwa sababu ya mimba hadi Desemba, 2020”.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha changamoto zinazolikabili kundi hilo zikiwemo za magonjwa ya kuambukizwa, upungufu wa taaluma sahihi za kujiajiri na kuajiriwa, matumizi ya dawa za kulevya, ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wadau wote wa masuala ya afya na maendeleo ya vijana balehe nchini kubuni na kuandaa afua zilizofanyiwa utafiti zenye kuleta matokeo chanya katika kutokomeza mimba za utotoni.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya ihakikishe kuwa vijana balehe watakaothibitika kuwa na maambukizi ya VVU wanaunganishwa na huduma za tiba na matunzo ili wawe na afya njema itakayowawezesha kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

“Natoa rai kwa viongozi wenzangu, wataalamu na wadau wote mnaohusika na Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe nchini kuhakikisha kuwa ajenda hii inatekelezwa kwa vitendo ili hatimaye kutatua changamoto zinazowakabili vijana wetu ifikapo 2024/2025”.  Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema ajenda hiyo imeandaliwa kwa lengo la kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma rafiki za afya na kuondoa vikwazo vya maendeleo kwa vijana balehe nchini.

”Ajenda hiyo imejikita katika nguzo sita ambazo ni kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, kutokomeza mimba za utotoni, kuzuia ukatili wa kimwili, kingono na kisaikolojia, kuboresha  lishe, kuhakikisha watoto wa kike na kiume wanabaki shuleni na kuwajengea vijana balehe ujuzi na uwezo wa kuzifikia fursa mbalimbali za kiuchumi”.

Amesema katika kusaidia vijana balehe kupata fursa ya kujiendeleza kiujuzi na kiuchumi, ajenda hiyo inaelekeza kutanua wigo kwa programu ya ujuzi mwepesi (soft skills) kupitia Vyuo vya Elimu ya Ufundi (VETA) na vyuo vingine vya ufundi (Post Primary Training Colleges) kwa ajili ya vijana wanaomaliza shule za msingi ili kuwawezesha kupata maarifa na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kujiajiri na kuajiriwa.

Waziri Dorothy amesema ajenda hiyo haina lengo la kuanzisha afua au programu mpya zinazokinzana na programu zilizopo katika sekta nyingine bali imelenga kuimarisha na kuboresha uratibu wa pamoja katika utekelezaji wa afua mbalimbali zinazohusu mahitaji mahsusi ya vijana wa rika balehe katika maeneo ya kimsingi yaliyoainishwa.


Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza

 Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linafanya Upelelezi Na  Ufuatiliaji Mkali Kufuatia Matukio Mawili Yaliyo  Tokea Kwa Nyakati Tofauti Katika Wilaya Ya  Nyamagana.

Tukio La Kwanza,
Tarehe 16.04.2021 Majira Ya 08:00 Hrs Katika Mtaa Wa Ipuli,  Kata Ya Mahina, Wilaya Ya Nyamagana, Ulikutwa Mwili Wa Mtu Mmoja Anayekadiriwa Kuwa Na Umri Wa Miaka 35, Akiwa Ameuawa Na Kutelekezwa Eneo La Makaburi. Jeshi  La Polisi Linaendelea Na Upelelezi Wa Kina Ili Kubaini  Wahusika Na Kuwakamata Na Kuwafikisha Maakamani Haraka Iwezekanavyo. Mwili Wa Marehemu Umehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Bugando Kwa Uchunguzi Zaidi.

Tukio La Pili,
Tarehe 16.04.2021 Majira Ya 06:00hrs Huko Maeneo Ya Bukaga,  Kata Ya Kishiri, Wilaya Ya Nyamagana, Vijana Wawili Jinsi  Ya Kiume Ambao Bado Kufahamika Utambulisho Wao, Wanaokadiriwa Kuwa Na Miaka Kati Ya 18-23, Waliuawa Kwa Kushambuliwa Sehemu Mbalimbali Za Miili Yao Kwa  Kupigwa Mawe Na Kundi La Watu Ambao Baadae  Walitawanyika Na Kukimbia Waliwatuhumu Watu Hao  Kujihusisha Na Matukio Ya Wizi. Eneo La Tukio Kulikutwa  Kuku Watano Na Pikipiki Yenye Usajili Mc 607 Cpk Mali  Walizotuhumiwa Kuiba. Miili Ya Marehemu Imehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Bugando Kwa Uchunguzi Na Utambuzi.  Msako Mkali Unaendelea Maeneo Yote Ilikukamata Wale  Wote Waliohusika Na Mauaji Hayo Kwa Kujichukulia Sheria  Mkononi.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawataka Waanch  Kuacha Vitendo Vya Kujichukulia Sheria Mkononi Kwani  Kufanya Hivyo Nikutenda Kosa La Jinai. Na Wale Wote  Waliohusika Kwa Mauaji Hayo Watakamatwa Na  Watafikishwa Mahakamani.

Imetolewa Na;
Muliro J. Muliro- Acp
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza.



Share:

MTOTO WA MIAKA 7 ADAIWA KUBAKWA NA BABU YAKE BIBI AKIWA AMELAZWA HOSPITALI



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba

Na Damian Masyenene, SHINYANGA

WAKATI Taifa na wanaharakati mbalimbali wakiendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto, matukio ya udhalilishaji na ukatili kwa watoto yameendelea kuripotiwa mkoani Shinyanga.


Ambapo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Juma Emmanuel (53) mkazi wa Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga kwa kosa la kubaka. 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo imetolewa leo Aprili 17, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Aprili 16, mwaka huu katika maeneo ya Ndembezi mjini Shinyanga, ambapo mtuhumiwa huyo alimbaka mtoto mwenye umri wa miaka 7 ambaye ni mjukuu wake.

Taarifa hiyo ya jeshi la polisi imeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni mmonyonyoko wa maadili, ambapo mtuhumiwa alimchukua mtoto huyo usiku kutoka chumba cha kulala watoto na kumpeleka kwenye chumba chake kisha kumuingilia kimwili.

“Mnamo Aprili 16, 2021 majira ya saa nne asubuhi jeshi la polisi mkoa wa shinyanga lilipokea taarifa kuwa maeneo ya ndembezi, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 07 (jina linahifadhiwa) alibakwa na mtuhumiwa huyo ambaye ni babu yake….Mtuhumiwa alipata nafasi ya kufanya kitendo hicho wakati mke wake akiwa amelazwa hospitali kwa matibabu,” amesema ACP Magiligimba.

Hata hivyo, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika, huku jeshi hilo likitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto vikomeshwe.


Share:

WAZIRI MKUU ATAKA LISHE IWE AJENDA SHULENI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipata maelezo ya shughuli zinazofanywa na Taasisi ya "Msichana Initiative" kabla hajazindua Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana balehe jijini Dodoma leo tarehe 17/04/2021.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana balehe jijini Dodoma leo tarehe 17/04/2021.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia KItabu cha Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo kwa vijana balehe jijini Dodoma leo tarehe 17/04/2021.

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akipata maelezo ya shughuli zinazofanywa na Taasisi ya "Msichana Initiative" kabla hajazindua Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana balehe jijini Dodoma leo tarehe 17/04/2021
Washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Ajenda ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo yaa Vijana balehe wakifuatilia matukio mbalimbali leo tarehe 17/04/2021.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana balehe jijini Dodoma leo tarehe 17/04/2021.





Na Mwandishi Wetu Dodoma

 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika Afya  na Maendeleo kwa Vijana Balehe ili kupata Taifa lenye nguvu kazi endelevu.

 

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati akizindua Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo kwa Vijana Balehe.

 

Ajenda hiyo ya kitaifa nimejikita katika nguzo sita ambazo ni kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kudhibiti mimba za utotoni, kuboresha lishe kwa vijana, kuzuia ukatili wa kimwili na kisaikolojia, kuhakikisha watoto wa kike na kiume wanakwenda shule na kumaliza masomo yao na kuwawezesha vijana balehe wanapata ujuzi na maarifa ya kuchangamkia fursa za kiuchumi.

 

Akizungumza kuhusu lishe bora amesema agenda  itawasaidia vijana hasa kundi la vijana katika kuimarisha nguvu na akili kwa kundi hili ambalo linatarajiwa kuwa nguzo ya Taifa.

 

" Suala la lishe liwe ni ajenda kwenye shule zetu, kila shule iwe na bustani ya mboga mboga, hii itasaidia vijana kufahamu umuhimu wa lishe salama na kuweza kujitegemea na kuelimisha  jamii" alisema Majaliwa.

 

Aidha, amezitaka Wizara zinazosimamia Ajenda hiyo kusimamia kikamilifu utekelezaji wake ili kuhakikisha lengo linafikiwa kwa ufanisi mkubwa na kuwasaidia vijana.

 

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema masuala ya lishe bado hayapewi kipaumbele kwani asilimia kubwa ya wanawake wenye umri wa kuzalisha wanakabiliwa na  tatizo la lishe duni.

 

Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika Afya na Maendeleo kwa Vijana balehe  inatekelezwa chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, kazi, Ajira na watu wenye ulemavu na Wizara ya Elimu.

 

Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ajenda hii itatekelezwa katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara na baadaye kuendelezwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

 

Lengo mahsusi la ajenda hii ni  kuwawezesha kundi la vijana kati ya miaka 10 na 19 kuimarisha Afya zao ili kuwa wazalishaji bora na nguvukazi ya Taifa.

 

MWISHO

Share:

SIMBA SC : TUNAIJUA MWADUI, HATUWACHUKULII POA.....MWADUI NAYO YATAMBA KUINUKA KESHO

Mratibu wa Simba SC, Abbas Ally

Na Damian Masyenene, SHINYANGA
 
MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Wekundu wa Msimbazi Simba, wamesema kuwa hawatowadharau wapinzani wao katika mchezo wa kesho, Mwadui FC, bali wataingia uwanjani kwa lengo moja la kupata alama tatu ili kuwa na uhakika wa kuutetea ubingwa wao msimu huu.

Simba SC watakaribishwa kesho (Jumapili) katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na wenyeji wao, Mwadui FC kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, huku wenyeji wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda bao 1-0 timu hizo zilipokutana uwanjani hapo msimu uliopita.

Akizungumza leo uwanjani hapo katika maandalizi ya mchezo wa kesho, Mratibu wa Simba SC, Abbas Ally amesema kikosi chao takimekuja kikamilifu kupambana na Mwadui na wanafahamu vyema namna wapinzani wao walivyo wasumbufu wanapokuwa uwanja wa nyumbani.

“Tuna historia isiyo nzuri katika mchezo wa mwisho hapa, …Mwadui wamekuwa wasumbufu wakiwa hapa nyumbani kwao, naamini watatumia nguvu nyingi kupata matokeo ili kujinusuru hapo walipo, hivyo itakuwa mechi ngumu, lakini lengo letu ni kutafuta alama tatu ili tuwe katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wetu,” amesema.

Mratibu huyo ameeleza kuwa, kutokana na upinzani mkubwa unaokuwepo baina ya timu hizo, tayari Kocha Mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi, Didier Gomez anazo taarifa ya kilichojiri katika mchezo wa mwisho uwanjani hapo, hivyo anauchukulia mchezo huo kwa umuhimu mkubwa na amezungumza na wachezaji kuupa umuhimu na kushinda.

Hata hivyo, Abbas ameeleza kuwa katika kuhakikisha wanapata ushindi kwenye michezo yao mitatu ya Kanda ya Ziwa baina ya Mwadui FC, Kagera Sugar na Gwambina FC, timu hiyo imekuja na nyota wote 28 wa kikosi hicho.
Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Salhina Mjengwa

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Salhina Mjengwa amekiri kuwa wanakutana na timu bora yenye mwendelezo mzuri ndani na nje ya nchi, lakini wamejiandaa vyema kuikabili Simba na kupata matokeo mazuri yatakayowapa matumaini ya kujinusuru na janga la kushuka daraja, huku akibainisha kuwa wachezaji wake wote wako kwenye hali nzuri na hakuna majeruhi.

“Wachezaji wako katika hali nzuri, kuelekea kesho asilimia 90 tumekamilisha maandalizi yote kuikabili Simba. Ni kweli tunacheza na timu bora, mabingwa watetezi na timu yenye mwendelezo mzuri, tunafahamu wanakuja kwenye uwanja usio rafiki, pamoja na kwamba mwenendo wetu siyo mzuri lakini hatuchezi vibaya, tunataka kuanzia kwao kupata alama tatu,” amesema. 
Nahodha wa Mwadui FC, Mussa Mbise

Naye Nahodha wa Mwadui FC, Mussa Mbise amesema kwa sasa morali ndani ya kikosi chao ni kubwa na kwa wiki nzima wamejiandaa vyema kwa ajili ya Simba, hivyo ana matumaini watashinda kesho.

“Timu yetu ni nzuri tunakosa tu mwendelezo mzuri tumekuwa na bahati mbaya tu ya kukosa matokeo, tunawaheshimu Simba lakini tutafanya vizuri. Wana Shinyanga watarajie matokeo mazuri,” ameeleza. 



Share:

SHIREFA YATANGAZA VIINGILIO MWADUI VS SIMBA, YAWATAKA MASHABIKI KUJITOKEZA KWA WINGI

Mwenyekiti wa Shirefa, Said Mankiligo

Na Damian Masyenene, SHINYANGA 
CHAMA cha Soka Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kimesema kuwa maandalizi yote ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) baina ya Mwadui FC NA Simba SC utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga yamekamilika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa SHIREFA, Said Mankiligo, hali ya uwanja wa CCM Kambarage ni nzuri, maandalizi ya uuzaji tiketi yamekamilika, huku akibainisha kuwa wenyeji Mwadui FC wameahidi ushindi kwa Wana Shinyanga, hivyo akwaomba mashabiki wa timu zote mbili kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo.

Mankiligo ameeleza kuwa viingilio vya mchezo huo vitakuwa Sh 5,000 kwa mzunguko na Sh 10,000 kwa jukwaa kuu (VIP), ambapo milango ya uwanja huo itafunguliwa saa 6 mchana na tiketi zitauzwa katika mageti manne.

“Maandalizi yote yamekamilika, hali ya uwanja ni nzuri, kazi kwa timu tu kuonyesha ufundi wao. Tayari timu zote zimeshawasili, tunawakaribisha mashabiki wote kufika kwa wingi kuzishuhudia timu zao.

“Kikubwa Zaidi, naomba timu zote mbili zituonyeshe burudani iliyo bora, wananchi wa Shinyanga wanayo hamu ya kuona burudani, tunaiombea Mwadui iweze kupata alama tatu na tunajua wamejiandaa kwa ajili ya hilo.

“Mwadui wametuahidi kwamba watakwenda kupambana kufa kupona na kuonyesha kwamba siyo timu ya kudharauliwa kama inavyoonekana. Na wameahidi kwamba watafufukia kwa Simba,”
amesema.




Picha zikionyesha maandalizi mbalimbali ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga utakaotumika kwa mchezo wa ligi kuu kati ya Mwadui FC na Simba SC kesho




Share:

KAMANDA MUTAFUNGWA ATOA ONYO KWA MADEREVA WALEVI NCHINI

 


KAMANDA wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Wilboard Mtafungwa amewataka ametoa onyo kali kwa madereva wa malori na mafuso hapa nchini ambao wamekuwa wakiendesha magari nyakati za usiku wakiwa wamelewa waache tabia hiyo mara la sivyo watajikuta wakiishia kwenye mikono ya sheria.

Mtafungwa aliyasema hayo akiwa mkoani Tanga wakati alipokuwa akiongea na madereva ,sambamba na watoa huduma wa mabasi juu ya masuala ya usalama barabarani  kwenye kituo cha Stendi ya Mabasi Kange na eneo la Mabanda ya Papa alipozungumza na madereva wa malori.

Alisema kwamba wapo baadhi ya madereva ambao wamekuwa wakiendesha magari hayo wakitokea Dar es Salaam wanasubiri mpaka gizo liingie kwa kisingizio kwamba serikali,Jeshi la Polisi itakuwa imelala wanakaa sehemu wanaanza kunywa pombe matokeo yake wanakwenda kuendesha magari wakiwa wamelewa.

“Madereva mnaoendesha Malori ,Mafuso wakiwa wamelewa ndugu zangu niwaambie kwamba maisha yenu yana thamani kubwa sana na kuishi ni mara moja hakuna kuishi mara mbili lazima mjali maisha yenu wewe umetoka na fuso Dare s Salaam unasuburi  mpaka giza liingie kwa kisingizio kwamba serikali itakuwa imelala polisi sasa wewe ulali unakaa sehemu unaanza kunywa na pombe matokeo yake unakuja kuendesha gari ukiwa umelewa”Alisema

Alisema kwa  sasa hayo wamekwisha kuyabaini na wameweka utaratibu wa kuwakagua hata nyakati za usiku RTO pelekeni askari wakiwa wamevaa kiraia au sare  wahakikisheni wanawakagua mpaka usiku lori ambalo linatiliwa walisimamishe wapime ulevi madereva kwa sababu wanavyo vya kutosha wakigundua wamekunywa pombe wamelewa wamakatwe wakae ndani mpaka pombe zake ziishe na baadae wawapeleke mahakamani.

Kamanda Mtafungwa alisema hatua hizo ni kubwa na hawataki zichukuliwe wanataka kila mtu athamni kazi anayofanya lakini niwaambie wale walevi kaeni chonjo hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yenu kutokana na kutokufuata sheria zilizopo.


Share:

SHEREHE ZA KUTUNUKIWA KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI KUNDI LA 01/17 SHAHADA YA SAYANSI YA KIJESHI NA KUNDI LA 68/20 PAMOJA NA MAHAFALI YA KWANZA YA SHAHADA YA SAYANSI YA KIJESHI KWA MAAFISA WANAFUNZI KUNDI LA 01/17 IKULU CHAMWINO DODOMA

 

 Viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Viongozi waandamizi wa Serikali, na Wananchi mbalimbali waliohudhuria Hafla hiyo inayofanyika leo April 17,2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 17,2021


















Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA WASAIDIZI WA OFISI YAKE BINAFSI



Share:

Friday, 16 April 2021

DKT. EDWARD HOSEAH ACHAGULIWA KUWA RAIS WA TLS


Dkt. Edward Hoseah
***
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimefanya uchaguzi wa Rais ambapo Dkt. Edward Hoseah ameibuka mshindi wa nafasi hiyo kwa kupata kura 297 katika uchaguzi uliojaa ushindani mkali.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Aprili 16, 2021 Jijini Arusha, mshindani wa karibu wa Dk. Hoseah Flaviana Charles amepata kura 223.

Dk. Hoseah amewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wake mwaka 2015.

Kwa ushindi huo Dk. Edward Hoseah sasa anachukua nafasi ya Rais wa TLS anayemaliza muda wake Dk. Rugemeleza Nshala ambaye naye alichukua kijiti cha kuiongoza TLS kutoka kwa mtangulizi wake Fatma Karume.

 Chanzo- EATV
Share:

Watumishi Wa Umma Tumieni Jitihada Binafsi Kutoa Huduma Bora Kwa Wananchi


Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma nchini kutumia jitihada binafsi katika kutekeleza majukumu yao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akiwa kwenye ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mhe. Ndejembi amesema ni vema Watumishi wa Umma wakatathmini mchango wao binafsi katika Utumishi wa Umma ili waweze kuwa na tija katika utoaji wa huduma kwa umma.

“Ukiwa Mtumishi wa Umma uliyejitoa kuwahudumia Watanzania unapaswa kujiuliza unataka kufanya nini ili kutimiza malengo yako na ya Taasisi kwa ujumla,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Kuhusiana na madai mbalimbali ya kiutumishi, Mhe. Ndejembi amewaambia watumishi hao kuwa, wakati Serikali inayafanyia kazi madai yao ni vema wakatekeleza wajibu wao kikamilifu ili madai yao yawe na thamani inayolingana na huduma wanayoitoa.

Aidha, amewasisitiza Wakuu wa Idara na Vitengo katika Taasisi za Umma kuwasilisha mpango kazi kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi zao utakaoziwezesha Idara na Vitengo pamoja na Taasisi kutekeleza majukumu kikamilifu.

Katika kuhimiza uwajibikaji unaozingatia maadili ya kiutumishi, Mhe. Ndejembi amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Chamwino Bw. Athman Masasi, kumpa barua ya onyo Mpima Ardhi wa Halmashauri hiyo, Bw. Charles Laseko kwa kosa la kushinikizwa na Afisa Usalama kuweka alama ya mpaka kwenye Kiwanja ambacho kimeuzwa na Jiji kwa mtu mwingine.

Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger