WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji wajiepushe na vitendo vya kuomba rushwa na urasimu usiokuwa wa lazima katika kuwahudumia wawekezaji ili kujenga imani baina ya sekta binafsi na sekta ya umma
Pia, Waziri Mkuu amezitaka Wizara na taasisi zote zinazohudumia wawekezaji kuhakikisha wanawezesha wawekezaji katika maeneo yao kwa kutoa huduma na taarifa muhimu kwa wakati.
Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Aprili 16, 2021) wakati akihitimisha hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa 2021/2022 mwaka wa Fedha 2021/2022, Bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema tarehe 6 Aprili 2021, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Tanzania akiwaapisha Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa baadhi ya Taasisi za Serikali alisisitiza masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji na vibali vya kazi.
“Mheshimiwa Rais aliielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu kuimarisha huduma za pamoja (One Stop Centre), kushughulikia malalamiko kuhusu kodi, kuondoa vikwazo katika uwekezaji, kuhamasisha uwekezaji kupitia mazungumzo, ushawishi, kudhibiti rushwa na kuondoa urasimu kwenye maombi ya vibali vya kazi”.
Amesema maelekezo hayo ya Mheshimiwa Rais yenye kujali maslahi mapana ya nchi hii yalikwenda sambamba na uamuzi wake wa tarehe 31 Machi 2021 wa kuunda rasmi Wizara ya Uwekezaji chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa Wizara hiyo inasimamia kikamilifu masuala ya uwekezaji.
Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kueleza hatua mbalimbali za utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia kuhusu Wizara ya Uwekezaji ambazo tayari zimechukuliwa kuwa ni pamoja na pamoja na kuandaa Muundo wa Wizara ambao utaainisha majukumu na mgawanyo wa Idara na Taasisi zitakazokuwa chini ya uwekezaji.
“Hatua ya pili ni kupitia Sera ya Uwekezaji ya mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 1997 ili kubainisha maeneo yenye kuhitaji maboresho ambapo tayari tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996 imekamilika na kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Maendeleo ya Uwekezaji ili kuimarisha uratibu, usimamizi, uhamasishaji na ufuatiliaji wa masuala ya uwekezaji nchini”.
Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa hatua hizo kutaiwezesha Serikali kushiriki kikamilifu katika mikutano na majadiliano ya jumuiya za kikanda yanayohusu masuala ya uwekezaji ikiwemo maandalizi ya Sera ya Uwekezaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pia, Waziri Mkuu ameongeza kuwa hatua hizo zitaiwezesha Serikali kushiriki katika utungaji wa Sera za Uwekezaji kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Itifaki ya Uwekezaji ya Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika.
“Kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji na uchumi shindani nchini kwa kutekeleza programu mbalimbali za kuimarisha mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuandaa mfumo wa kielektroniki wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wawekezaji (Online Investors Feedback Platform)”.
“Kutatua changamoto za wafanyabiashara kupitia Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kwa kuratibu majadiliano ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kutoa elimu na hamasa kuhusu huduma zitolewazo kwenye Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja (One Stop Facilitation Centre-OSFC).”
Amesema kupitia hatua hizo, Serikali itaweza kuimarisha mifumo ya usajili wa miradi na kutoa Cheti cha Vivutio (Certificate of Incentives), kuunganisha mifumo inayotumika TIC na makao makuu ya Taasisi na kuboresha mfumo wa kuchakata rufaa za vibali vya kazi na ukaazi kwa njia ya mtandao.
“Nitumie fursa hii tena kuwakumbusha watendaji wenzangu wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kuhakikisha kuwa muundo na mifumo ya masuala ya uwekezaji inakamilika ndani ya muda ulioelekezwa na Mheshimiwa Rais”.
(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Friday, 16 April 2021
Majaliwa: Watendaji Jiepusheni Na Rushwa
Waziri Mkuu Awatoa Wasiwasi Watanzania ......Ni Kuhusu Mfumo Wa Kuyaendeleza Makao Makuu Ya Nchi Dodoma
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu Watanzania kuhusu kuendelezwa kwa Makao Makuu ya nchi Dodoma kwa kuwaeleza kwamba Serikali imeweka mfumo mzuri utakaohakikisha yanajengwa kuendana na mipango ya maendeleo ya Jiji la Dodoma.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 16, 2021) wakati akihitimisha hoja ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Bungeni jijini Dodoma.
Amesema mfumo huo, unahusisha Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma ambacho kinajumuisha wajumbe kutoka Wizara na Taasisi za Serikali. “Kikosi Kazi hicho kina jukumu la kushauri namna bora ya kupanga na kuendeleza Mji wa Serikali na Jiji la Dodoma kwa ujumla”.
Waziri Mkuu amesema utekelezaji huo, unahusisha miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na maji, kiwanja cha ndege, barabara na utoaji wa huduma za jamii. “Niwahakikishie Watanzania wote kuwa Dodoma inaendelea kujengwa”.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wabunge na Watanzania warejee kauli ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa waendelee kushikamana, kusimama na kuwa wamoja kama taifa, kuoneshana upendo na undugu, kudumisha amani yetu, kuenzi utu wetu, uzalendo wetu, utanzania wetu na kutazama mbele kwa matumaini na kujiamini.
“Huu si wakati wa kunyoosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele. Kwa msingi huo, tuendelee kudumisha na kuilinda amani ya nchi yetu ikiwa ni sehemu ya kuenzi jitihada za waasisi wa Taifa hili. Tutumie muda mwingi kwa kazi zaidi za kujipatia kipato na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja.”
Vilevile, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatakia Waislamu wote nchini mfungo mwema na wenye mafanikio wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ulioanza katikati ya wiki hii. “Nitoe rai kwamba tutumie kipindi hiki kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuibariki nchi yetu na watu wake”.
“Kadhalika, tumuombe Mwenyezi Mungu awajalie viongozi wetu hekima na busara ili waendelee kuliongoza Taifa letu kwa haki, kujenga umoja na mshikamano, kudumisha amani katika nchi yetu pamoja na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii”.
(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
WATANZANIA TUMUUNGE MKONO RAIS WETU MHE.SAMIA SULUHU-BW.FESTO
Kijana Mzalendo Bw.Frank Festo (Kulia)akiwa pamoja na rais wa Chuo cha Bahari (DMI) Bw.Salim Awali wakionesha stika yenye ujumbe "MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE".

Kijana Mzalendo Bw.Frank Festo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam baada ya kukutana kwaajili ya uzinduzi wa stika yenye ujumbe "MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE".
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
NA EMMANUEL MBATILO
Ili kuweza kuunga mkono Juhudi za Rais Mhe.Samia Suluhu Hassani, Kijana Mzalendo Bw.Frank Festo amezindua stika yenye ujumbe "MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE". Lengo kuhamasisha mshikamano, umoja, upendo, amani na furaha kama kipaumbele cha Rais Mhe.Samia Suluhu.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Bw.Festo amesema sote kwa pamoja tunapaswa kumuunga mkono ili kuweza kufanikisha kuiongoza Tanzania katika amani na upendo tulionayo toka zamani.
"Tusikae pembeni kwa kuchungulia na kumsikiliza eti huyu mama ataweza?.Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake ipasavyo ndiyo njia pekee ya kumuunga mkono Mama yetu mpendwa". Amesema Bw.Festo.
Aidha Bw.Festo amesema stika hiyo itasambazwa nchi nzima kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, vyombo vya usafiri, kutembelea ofisi za Umma na Binafsi,Bunge, Shule,Vyuo na nyumba za ibada ikiwa lengo ni kuhakikisha ujumbe huo unamfikia kila mtanzania mahali popote alipo.
Pamoja na hayo Bw.Festo amesema kuwa pamoja na taifa letu kujaliwa rasilimali nyingi, rasilimali kubwa tuliokuwa nayo ni amani na hatuna mbadala wa amani.
Kwa upande wake rais wa Chuo cha Bahari (DMI) Bw.Salim Awali amewasihi viongozi ambao wamepewa dhamana serikalini kufanya kazi kwa bidii bila kumkatisha tamaa Rais kwa masirahi ya nchi yetu.
"Sisi kama vijana tunamuahidi Rais wetu tutaliendeleza taifa hili kwa umoja na kumshauri ni nini kifanyike ili tuweze kufika sehemu ambayo tunaitaka kwasababu kiongozi wetu Rais Mhe.Samia ni mtu ambaye anapokea ushauri na ni mtu ambaye msikivu". Amesema Bw.Awali.
MBUNGE NEEMA LUNGANGIRA AIKUMBUSHA SERIKALI KUHUSU UMUHIMU WA LISHE BORA KWA MAENDELEO YA TAIFA
Jobs at NGARA District Council
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Various Jobs at NGARA District Council April, 2021. Ngara District is one of the eight districts of the Kagera Region of Tanzania. It is bordered to the north by Karagwe District, to the east by Biharamulo District, to the south by the Kigoma Region, to the northeast by Muleba District and to the we […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
WAFANYABIASHARA WAOMBWA KUWA NA HURUMA MWEZI WA RAMADHAN
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo
**
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaomba wafanyabiashara nawatoa huduma mbalimbali mkoani humo kutopandisha gharama za mazao na mahitaji mbalimbali katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kuwahurumia Waislamu wanaoendelea na mfungo wa Mwezi wa Ramadhan.
“Niwaombe sana wafanyabiashara na watoa huduma, hiki sio kipindi cha kujineemesha ni kipindi cha tafakari, ni kipindi cha kuwa Pamoja, kipindi cha kuhurumiana, kipindi cha sadaka, sio kipindi cha kuona kwamba sasa ni kipindi cha kupata mapato zaidi, niwaombe msiongeze bei za vyakula, niwaombe msiongeze bei za huduma mbalimbali, mwaka jana mlinisikiliza, hali ilikuwa nzuri, ni matarajio yangu hata mwaka huu pia, bei za vyakula sokoni, viazi, mihogo, sukari na bidhaa nyingine hazitapanda,”
“Lakini kama itatokea watu wataokwenda kinyume, niwatahadharishe, serikali ipo na itafuatilia kila mahali, ili tusitese watu ambao tayari wanajitesa, mtu anajinyima, anashinda njaa, anakula jioni ile na wewe unaamua kumtesa zaidi, kuwabebesha mzigo mkubwa zaidi, hii haikubaliki, tuhurumiane, tupendane, bila ya shaka ujumbe huu utafika kwa kila mwananchi na kila mwanarukwa,” alisisitiza.
Mh. Wangabo alitoa ujumbe huo tarehe 14.5.2021 ambapo Waislamu kote nchini walikuwa wameuanza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kipindi cha siku 30 ama 29 kutemea mwandamo wa mwezi.
Field Officers (18 Posts) at Ifakara Health Institute
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job Summary Position: Field Officers (18 Posts) Reports to: Research Officer/Project Leader Work station: Tanga District (Tanga Municipality), Kaliua District (Tabora) and Sengerema District (Mwanza) Apply by: April 23rd 2021 Institute overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Technology Procurement & Asset Manager at NBC
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
NBC is the oldest serving bank in Tanzania with over five decades of experience. We offer a range of retail, business, corporate and investment banking, wealth management products and services. Job Summary The role is responsible to ensure that new and existing IT Assets and Services are procured and renewed cost-effectively. It will also ensure […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Programme Finance Assistant at UNCDF
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Eligibility criteriaCandidate age: between 18 and 29 throughout the entire duration of their assignment. Applicants must be nationals of or legal residents in the country of assignment. Description of task Assist in financial management activities of the office – 25% Support the preparation of the various financial reports based on our reporting calendar. Ensure that […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Senior Finance and Admin Manager at REDESO
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
About REDESO: Relief to Development Society (REDESO) is a Tanzanian National Non-Governmental Organization dully registered under the Society Ordinance of 1954 with registration number S.O. No. 9459. The organization is engaged in Humanitarian and Community Development projects implemented under the humanitarian to development nexus concept. In the areas of our operation, Local Government has been […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Deputy Director Finance at International Rescue Committee
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Requisition ID: req14307 Job Title: Deputy Director Finance Sector: Finance Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: Yes Location: Dar es Salaam, Tanzania Job Description The International Rescue Committee responds to the world’s worst humanitarian crises and helps people whose lives and livelihoods are shattered by conflict and disaster to survive, recover and gain control of their future. We […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
MKAGUZI MKUU WA MIGODI AIDHINISHA MPANGO WA UCHIMBAJI MADINI WA GGML MWAKA 2021
Inventory and Asset Assistant at ICAP
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Job no: 495106 Work type: Regular Full-Time Location: Tanzania – Dar es Salam Categories: Finance/Administration ICAP at Columbia University, a global health leader situated within the Columbia University Mailman School of Public Health in New York City, seeks Inventory and Asset Assistant to be based in Dar es Salaam, Tanzania. Inventory and Asset Assistant with safety, efficiency and customer […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Information System (IS) Specialist at Médecins Sans Frontières
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
JOB VACANCY – INFORMATION SYSTEM (IS) SPECIALIST Médecins Sans Frontières (MSF) is an international, independent, medical humanitarian organisation that delivers emergency aid to people affected by armed conflict, epidemics, natural disasters and exclusion from healthcare. MSF offers assistance to people based on need, irrespective of race, religion, gender or political affiliation. MSF […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Commercial Specialist at U.S. Embassy Dar es Salaam
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
The U.S. Mission in Dar es Salaam is seeking eligible and Qualified applicants for the position below. Position Title: Commercial Specialist Vacancy Number: DaresSalaam-2021 -018 Duties 25% – Trade facilitation through business matchmaking, including identifying potential partners (incl., distributors, agents, etc.) The incumbent identifies potential distributors, representatives, joint venture partners, or other professional contacts […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Mechanic Cum Driver at HJFMRI
This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content
Join us in our efforts to end the HIV epidemic in Tanzania. Be part of the winning team to advance global health and save the lives of people living with HIV. About HJFMRI Tanzania Program The Walter Reed Program Tanzania (WRP-T) is a collaborative effort that supports PEPFAR-funded HIV prevention and treatment activities in the […]
This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details
Senior Financial Analyst at HJFMRI