Sunday, 11 April 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 12,2021






Share:

RAIS SAMIA NA MUSEVENI WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA BOMBA LA MAFUTA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha tamko la pamoja la yeye na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe baada ya hafla ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga
Maafisa wandamizi wa kampuni ya TOTAL ya Ufaransa wakiweka saini mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Dkt James Mataragio akiweka saini kwa niaba ya Tanzania mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga katika hafla iliyofanyika leo Ikulu ya Entebbe na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha ratiba ya hafla ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga baada ya yeye na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kuombwa na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya Total duniani Bw. Patrick Poyanne kufanya hivyo ili iwe kumbukumbu yake ya
siku hiyo ya kihistoria katika Ikulu ya Entebbe leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiweka saini kwenye kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe muda mchache kabla viongozi hao kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe baada ya hafla ya uwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakipata picha ya kumbukumbu na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Makampuni ya TOTAL duniani Bw. Patrick Pouyanner na viongozi waandamizi wa kampuni hizo mbili na kampuni hiyo katika Ikulu ya Entebbe baada ya hafla yauwekwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Bomba la Mafuta la Afrika
Mashariki litalotoka Hoima nchini humo hadi Tanga

Share:

TMA YATOA ANGALIZO LA MVUA KUBWA SIKU TATU MFULULIZO MIKOA 12 KUANZIA APRILI 12

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Aprili 11,2021, imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho Aprili 12 hadi Aprili 14  mwaka huu katika mikoa 15.

Katika taarifa iliyotolewa na TMA imeonyesha mvua hiyo yenye uwezekano wa wastani, itanyesha kesho Aprili 12, kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani inayojumuisha Visiwa vya Pwani,  Tanga, Lindi na Mtwara.

Pia mvua hiyo inatarajiwa kunyesh kesho kutwa, Aprili 13, katika mikoa hiyo n mikoa mingine kiwemo pia Iringa, Njombe, Ruvuma, Morogoro.


Aidha mvua hiyo inatarajiwa kunyesha Aprili 14  kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, shinyanga, Kigoma, Katavi, Rukwa, Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro

"Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji jambo linaloweza kuathiri shughuli za kiuchumi na ucheleweshwaji wa usafiri. Hata hivyo, TMA imewataka wananchi kuzingatia angalizo hilo,.

Taarifa hiyo inayoelezea hali ya hewa kwa siku nne kuanzia Aprili 12 imeonesha kuwepo kwa hali ya kawaida ya hewa kwa siku ya Aprili 15, 2021
Share:

WAFANYABIASHARA WADOGO MOROGORO WAPEWA MBINU ZA KUTIBU MAJI

 Wafanyabiashara wadogo katika soko la Mawenzi, soko la Madizini na soko la Mji Mpya yaliyopo katika manispaa ya mji wa Morogoro wamejengewa uwezo wa namna ya kutumia mbinu mbalimbali kutibu maji. Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na shirika la Raleigh Tanzania.

Mafunzo hayo yamefanyika Ijumaa Aprili 10, 2020 ambapo wafanyabisahara walifundishwa kwa vitendo mbinu mbalimbali za kutibu maji kwa lengo la kuhakikisha wanadumisha usafi na usalama wa afya zao na wateja wao kwa kutumia maji safi na salama. 

Akizungumza baada ya zoezi hilo (mwakilishi wa Raleigh Tanzania, Bi. Jovina Justus alisema baadhi ya mbinu walizofundishwa wafanyabiashara hao ni pamoja na kutibu maji kwa njia ya vidonge, kutibu maji kwa kutumia mitungi maalumu ya kuchujua maji, kuchemsha na kuchuja. Jovina aliongeza kwamba mbinu hizo ambazo nyingi ni za asili zitawasaidia wafanyabiashara hao kudumisha usalama wa afya zao kwa kuhakikisha wanatumia maji safi na salama.

“Mbinu hizi ambazo nyingi ni za asili zitawasaidia wafanyabiashara wa eneo hili kukabiliana na changamoto ya matumizi ya maji yasiyo safi na salama. Kwa sasa wafanyabiashara wengi hasa wafanyabiashara wanaofanya biashara ya kuuza chakula wanafahamu umuhimu wa maji safi na salama lakini pia wanafahamu namna ya kutibu maji”, alisema Jovina Justus.

Kwa upande wa wafanyabisahara hao walizungumza namna walivyonufaika na mafunzo hayo na kuwashukuru waandaaji Raleigh Tanzania kwa kuwaletea jawabu la maji safi na salama. 

“Mwanzo sikutaka kushiriki katika mafunzo haya kwani niliona kama napoteza muda wangu lakini nimejikuta nimechota maarifa mengi sana kwa muda mfupi. Nilikuwa nikisikia tuu kuhusu maji safi na salama lakini sikuwahi kuchukua hatua yoyote, kwa sasa nafahamu hasa nini cha kufanya ili kutibu maji. Kuanzia sasa siwezi kutumia tena maji ambayo hayajitibiwa kwani hakuna gharama yoyote ya kutibu maji”, alinukuliwa Bw. Felix Mwingizi mmoja ya washiriki wa mafunzo hayo. 

Mshiriki mwingine wa mafunzo hayo aliwaomba waandaaji wa mafunzo hayo kufikisha mafunzo hayo kwa wananchi wengi zaidi ili kusaidia kukabiliana na magonjwa yanayotokana na matumizi ya maji yasiyotibiwa.

“Mimi binafsi nimejifunza kwa vitendo namna ya kutibu maji, hii itanisaidia mimi na watu walionizunguka. Natamani mafunzo haya yangewafikia watu wengi zaidi hasa katika ngazi ya kaya ili kuzisaidia familia kujiepusha na magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo safi na salama”, alisema mshiriki huyo.

Mafunzo hayo ni sehemu ya kampeni iliyopewa jina la Kijana Ni Usafi inayotekelezwa na shirika la Raleigh Tanzania kwa lengo la kuhimiza usafi binafsi na usafi wa mazingira kwa vijana. Kampeni hiyo inayotekelezwa na Shirika la Msaada la Uingereza (UKAID) inalenga wanawake na wanaume wenye umri wa miaka 15-35. Kampeni hiyo inatarajia kuwafikia vijana 48,000 katika mikoa minne ambayo ni Iringa, Dodoma, Dar es salaam na Morogoro.

Mkoani Morogoro, lengo kuu la kampeni ni kuhimiza matumizi ya maji salama katika jamii. Sababu kubwa ni kwamba mkoa wa Morogoro umeathiriwa na magonjwa kama vile homa ya matumbo, kuhara na mlipuko wa kipindupindu mara kwa mara. Wanajamii wanaathirika kutokana na tabia ya kutumia maji yasiyo salama.

 Kampeni imepewa jina la "Tumia Maji Salama, Okoa Mkwanja" kuonesha vijana namna ambavyo matumizi ya maji salama yatawaepusha na gharama za kutibu magonjwa.

Share:

Rais Samia awasili Uganda, kushuhudia kusainiwa mkata bomba la mafuta


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassana, amewasili nchini Uganda kwa ziara ya siku moja ambapo pamoja na mambo mengine atashuhudia utiwaji saini kati ya Serikali ya Uganda na kampuni tanzu ya uzalishaji Mafuta ya Afrika Mashariki (EACOP).

Alipowasili katika Ikulu ya Entebe Rais samia Suluhu Hassan, amepokewa na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museven na kisha kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na kikosi cha jeshi cha nchi hiyo.

Katika ziara hiyo Rais Samia Suluhu Hassana atakuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais Museven kabla ya hafla ya kutiliana Saini baina ya EACOP na serikasli ya Uganda.

Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Chongoleani Jijini Tanga linatarajiwa kuanza kujengwa mara baada ya kukamilika kwa mikataba yote baina ya wadau wa wanaohusika na mradi huo.

Hii ni ziara ya kwanza kwa Rais Samia Suluhu Hassan nje ya nchi tangu aapishwe kuwa Rais wa Tanzania Machi 19,2021.


Share:

WAZIRI MKUMBO TUISIMAMIE KWA WELEDI SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA ILI KUKUZA UCHUMI NCHINI

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo,akizungumza kwenye kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake kilichofanyika  April 10,2021 jijini Dodoma,kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Exaud Kigahe (kulia) ni Katibu Mkuu wake Bw. Dotto James.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo,akifafanua jambo wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe ,akieleza jambo wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Dotto James akizungumza wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichoongozwa na Waziri Prof,Kitila Mkumbo kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah,akizungumza wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.

Sehemu ya watumishi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika April 10,2021 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo ,amewataka watumishi wa Wizara yake wote nchini kuimarisha sekta ya viwanda na biashara ili kukuza uchumi nchini na kutekeleza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26.

Prof.Mkumbo ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Menejimenti ya Wizara pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo,amesema kuwa majukumu ya wizara hiyo ni kutoa mwelekeo na utekelezaji wa kuinua uchumi wetu.

Prof.Mkumbo amesema kuwa Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 ni kuona Tanzania inahitimu na kuondoka kuwa nchi masikini inayotegemea kilimo na uchumi wa uzalishaji duni na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo Wizara ina mchango mkubwa katika kufanikisha azma hiyo.

“Uchambuzi wa maudhui ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26 unaonesha wazi kabisa nafasi ya Sekta ya Viwanda na Biashara,sisi kama Wizara tunatarajiwa kutoa mchango karibu kwa kila eneo la matokeo tarajiwa.”

Aidha amesema pia katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26, malengo sita kati ya mahsusi 12 yanahusu sekta ya viwanda na biashara, kati ya vipaumbele vitano vya mpango huo vitatu vinahusu wizara hiyo, katika Sekta 30 za mpango huo Sekta 6 zinahusu Wizara na katika hatua 156 hatua 54 zinahusu Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zina mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa taifa wa Maendeleo wa III wa miaka mitano 2021/22 – 2025/26, Hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo”

Hata hivyo, Prof.Mkumbo amesema kuwa hakusudii kutumia muda mwingi katika kutunga Sera, Sheria na mikakati na kuwa yeye analenga katika utekelezaji na kuona matokeo ya utekelezaji huo kwa kuchochea ukuaji wa haraka wa Sekta ya Viwanda na Biashara.

Prof.Mkumbo amewataka wataalamu wa Idara ya Sera na Mipango ya Wizara kusimamia uhuishaji wa nyaraka mbalimbali za kisera na sheria ili ziende na wakati na kuakisi maudhui ya Mpango wa tatu wa Maendeleo na maono ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Prof.Mkumbo amesema kuwa tunataka kuviendeleza viwanda hapa nchini lazima kuwa na kanzi data ya kisasa ya viwanda kwa kuzingatia kiwango cha uzalishaji na ajira, kuweka mazingira na masharti rahisi katika kukuza na kuchochea viwanda vidogo vidogo vinavyotumia teknolojia rahisi na ya kisasa na vilivyojikita vijijini na mijini,

Aidha Waziri Mkumbo ameongeza kuwa lazima tuwawezeshe na kuwahudumia wawekezaji katika viwanda vikubwa na vyenye tija katika uchumi na kuhuisha Mkakati wa Viwanda nchini,ikiwemo dhana ya EPZ na SEZ.

Amesema pia kusimamia kwa karibu miradi ya kielelezo iliyopo katika Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Taifa ambayo ni mradi wa Chuma wa Mchuchuma na Liganga, Magadi Soda wa Engaruka, ujenzi wa Kiwanda cha Sukari-Mkulazi na kanda Maalum za Uchumi na Maeneo Maalum ya Uwekezaji

Prof.Mkumbo amesema kuwa kuimarisha utafiti na matumizi yake katika maendeleo ya viwanda, ikiwemo kuwa na ushirikiano wa karibu na taasisi za utafiti na elimu ya juu na kupanua na kuboresha mahusiano na ushirikiano na taasisi za sekta binafsi.

“Naomba tumeimarisha ushirikiano na OR-TAMISEMI katika maendeleo ya viwanda vidogo vidogo, tunataka kuona uwezekano wa kuwaongeza majukumu maafisa biashara wa Halmashauri ili pia wasimamie viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao kwa kushirikiana na SIDO.”amesema Prof.Mkumbo

“Tunataka tunapokutana na wafanyabiashara tufanye mazungumzo yenye tija ya kubadilisha mikakati ya kukuza biashara na masoko, badala mikutano hiyo kutumika tu kama jukwaa la kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara.”

Pia naomba tuendelee kuzipitia kanuni za mamlaka za udhibiti zinazoonekana kukwamisha biashara, kuchochea na kuhamasisha tabia ya kujali wateja miongoni mwa watendaji wa Serikali wanaohudumia sekta mbalimbali za biashara.

Aidha, Prof. Mkumbo amesisitiza kuwa kuna haja ya watendaji wa wizara na taasisi kubadilisha mtizamo katika utendaji kazi na kuwa na “corporate thinking” na tabia ya kujali wateja kwa kuzingatia kuwa wadau tunaowahudumia ni wafanyabiashara.

Waziri Mkumbo amewataka wataalamu wa wizara hiyo kuhakikisha wanatoa ushauri wa kitaalamu wenye ushahidi wa kisayansi na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa wafanyabiashara

Share:

Updates : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ....IMEFANYIWA MABORESHO 2021

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 11,2021


























Share:

Saturday, 10 April 2021

Rais Samia apokea ujumbe maalum wa Rais Kenyatta leo Ikulu,mkoani Dar es Salaam.


Rais Samia Suluhu Hassan leo amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya uliowasilishwa na Waziri wa Michezo, Utamaduni na Urithi wa nchi hiyo Balozi Amina Mohamed.

Pamoja na kupokea ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Balozi Amina yaliyohusu dhamira ya Tanzania na Kenya kuendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari kuendeleza mambo mazuri yote yaliyokuwa yakifanywa na mtangulizi wake Hayati Dkt. John Magufuli na kutatua changamoto kati ya Tanzania na Kenya kwa kuwa nchi hizo ni ndugu, majirani na marafiki wa kihistoria.

Amewataka Mawaziri na Wataalam wa Tanzania na Kenya wanaounda Kamati ya Ushirikiano wa Pamoja ambao hawajakutana tangu mwaka 2016 kukutana mara moja ili kufanyia kazi masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano.

Rais Kenyatta amemwalika Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara rasmi nchini Kenya ili kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano.

Amemhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Kenya ipo tayari wakati wote kushirikiana na Tanzania kwa kuendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Amina aliongozana na Balozi wa Kenya hapa nchini Dan Kazungu.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger