Wednesday, 10 June 2020

Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya 15

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188

ILIPOISHIA
“Ila sijui kwa nini aliye wapa kazi hakuhitaji kunia kwa kutumia watekaji wake. Ila nina hisi ana hitaji siku moja aje kuitoa roho yangu kwa mikono yake mwenyewe. Ila kabla ya yeye kufanya hivyo basi nita hakikisha kwamba nina itoa roho ya kibaraka wake aliye mpatia pesa za kwenda kuwalipa majambazi kisha nitaitoa roho yake. Au una semaje mke wangu hilo si wazo zuri eheee?”
Nabii Sanga alizungumza huku akimkazia macho mke wake. Taratibu mrs Sanga akakaa kitandani huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga kwani kila kitu kinacho zungumwa na mume wake kina muhusu yeye.


ENDELEA

Mrs Sanga aka mtazama mume wake kisha akamjibu kwa kutingisha kichwa akimaanisha kwamba hajakubaliana na jambo hilo.
“Kwa nini sasa una kataa ikiwa mtu ameamua kunifanyia ubaya? Ameamua kuniteka na kuhitaji kunia, je ile risasi walio piga kwenye kioo cha mbele kama ingenipata ningekuwa wapi leo hii?”
“Ila mume wangu sisi ni watumishi wa Mungu. Samehe saba mara sabini”
“Sio katika hili, ndio maana hata Mungu mwenyewe ali mpa ujasiri Daudi kwenye kumpiga Goliath na kumuua. Laiti kama wangesamehe saba mara sabani, ingekuwa ni hali tete kwa Daudi na watu wake. Hivyo na mimi nitafanya hivyo nina imani kwamba Mungu atakuwa pamoja nami kwani sikuanza mimi. Ila yeye aliye ianzisha hii vita basi atanifanya mimi niweze kuimaliza”
Mrs Sanga akaka kimya huku moyo wake ukiwa umepoteza amani kabisa.
“Hivi una habari kwamba Tomas ame kamatwa na askari?”
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake usoni kwa macho ya udadisi.
“Weeee!!”
Mrs Sanga alijifanya ana shangaa, ila kukamatwa kwa Tomas ana tambua na anacho kiomba kwa Mungu ni Tomas kuto mtaja katika sekeseke hilo la utekaji.
“Amekamatwa, sijui ame fanya kosa gani. Ila nikitoka kwenye kikao na waandishi wa habari nitapita kituoa cha polisi kumuona na ikiwezekana nimuwekee dhamana”
“Kweli mume wangu?”
Mrs Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake.
“Ndio mbona ume furahi sana?”
“Hamna, kitu mume wangu”
“Ila kama atakuwa amefanya kosa kubwa lisilo hitajika dhamana. Nitamuacha akafie huko jela”
“Mmmm”
“Ndio na ikiwezekana alipe kwa matendo yake aliyo yafanya.”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza maneno hayo akatoka chumbani humu na kumuacha mke wake akizidi kupoteza amani.
    Majira ya saa tatu sekretari wa mchungaji Sanga akafika nyumbani hapo. Akamkuta nabii Sanga akiwa tayari amesha jiandaa kwa ajili ya kuelekea kwenye kikao na waandishi wa habari.
“Tupitie kwenye ofisi za tigo nahitaji kurudisha laini yangu iliyo potea”
“Sawa baba mchungaji”
Nabii Sanga akaondoka na sekretari wake huyo huku akimuacha mke wake akiwa katika hali tete. Wakafika katika ofisi za Tigo, kila aliye muona nabii Sanga alijawa na furaha kubwa sana. Watu wengi waliguswa sana na tukio la kutekwa kwake. Laini yake ika rudishwa kwa haraka na wala hakuchajiwa kiasi chochote cha pesa. Akasali na baadhi ya wafanyakazi pamoja na wateja alio wakuta eneo hilo kisha akaondoka na kuelekea eneo la kanisani kwake ambapo ndipo alipo andaa mkutano na waandishi wa habari. Akiwa ndani ya gari nabii Sanga akampigia Clayton, rafiki yake wa karibu anaye uza magari ya kifahari ndani na nje ya Tanzania.
“Pole sana kwa matatizo ndugu yangu”
“Nashukuru sana. Niambie hapo ofisini kwako kuna gari gani nzuri?”
“Ahaa kuna land cruser new model. Harriel new model. Benzi, BMW X5 na X6. Kuna Audi Q7. Kwa ufupi zipo gari za kifahari. Gari ya bei ya chini ni milioni tisini”
“Sawa sawa. Sasa nakutumia namba ya binti mmoja atafika hapo ofisini kwako na achague gari yoyote ya bei yoyote kisha uta niambia ni kiasi gani na nitakupitishia cheki hapo”
“Sawa ndugu yangu. Nitumie niweze kumpigia”
“Sawa, ila maswala ya usajili yote mkamilishie. Pia mtafutie dereva wa kumrudisha na hiyo gari hadi nyumbani kwa maana hafahamu kuendesha. Jina lake ana itwa Magreth”
“Sawa sawa ndugu yangu nita fanya hivyo”
“Nashukuru”
Nabii Sanga akakata simu yake na kumtumia Clayton namba ya Magreth. Wakafika kanisani, waandishi wa habari wakaanza kuwashambulia kwa kuwapiga picha toka wakiwa wana ingia getini hapo.  Nabii Sanga akashuka kwenye gari na kuwapungia mkono waumini wake wengi ambao wamekusanyika kanisani hapo kuhakikisha wana mpa mapokezi mazuri nabii wao.
“Karibu sana nabii”
Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo alizungumza. Nabii Sanga akaelekea ofisini kwake, akaitazama ofisi hii na kujikuta akizidi kupandwa na hasira ya kumchukia mke wake. Kwani ameigeuza ofisi yake kuwa ndio eneo la kufanyia ngono.
‘Mungu nipe moyo wa uvumlivu na hekima katika hili.’
Nabii Sanga alizungumza huku akianza kuomba. Ikamchukua dakika ishirini za kusali, akiwa peke yake ofisini hapo, kisha akamruhusu sekretari wake kuingia.
“Tayari wamesha jiandaa?”
“Ndio wana kusubiria wewe tu”
“Sawa”
Nabii Sanga akajiweka sawa koti la suti na kuingia katika ukumbi wa mikutano midogo midogo katika kanisa lao. Mkutano na waandishi wa habari ukaanza. Nabii Sanga akaanza kuelezea jinsi alivyo tekwa na majambazi hao huku akiongopea kwamba siku hiyo alikuwa ana toka kanisani na kuelekea nyumbani kwake pasipo kupita mahala popote. Akaelezea ni jinsi gani  majambazi hao walivyo kuwa wana pokea amri kutoa kwa mtu ambate aliwapa kazi hiyo.
“Nabii Sanga akajipa maujiko ya kuongopea jinsi alivyo toroka katika ngome ya majambazi hao na kurudi jijini Dar es Salaam. Akaenda mbali zaidi ya kusema kwamba aliwasiliana na RPC na kumuomba aweze kumletea vijana wake sehemu alipo kuwepo na vijana hao wakafanya kazi hiyo ya kumchukua huku wakiwa na bosi wao huyo kisha wakamrudisha nyumbani kwake.”
“Mara baada ya kumsikia baba yetu hapa wa kiroho nina karibisha maswali machache kisha ata ingia kanisani kuwasalimia waumini wake wana msubiri kwa hamu sana.”
Sekretari alizungumza na kuwafanya waandhishi wa habari washindane kwa kunyoosha mikono.
“Ehee pole dada”
“Kwanza nitangulize pole sana nabii Sanga. Je katika kusikia sikia mazungumzo ya watekaji hao. Uliweza kuhisi au kusikia nani ni muhusika wa kukuteka wewe?”
Nabii Sanga akatazama mtangazaji huyo huku akilini mwake akimtafakari mke wake. Mwanamke ambaye alipata naye tabu kwenye shida na raha na leo hii ndio amekuwa adui yake.
                                ***
    Mrs Sanga sanga kila wazo analo jaribu kulitafakari kichwani mwake ili kujinasua kwenye tatizo linalo mkabili ana jikuta anashindwa kabisa kupata suluhisho. Akawasha tv ya chumbani kwake na kukuta mume wake akiwa mubashara kwenye kituo cha televisheni. Swali la muandishi wa habari kuhusiana na nani aliye mteka likamfanya mrs Sanga kuzidi kutetemeka kwani ana tambua tayari mume wake amesha fahamu ukweli.
“Ehee Mungu asinitaje huyu mwanume. Nitaiweka wapi sura yangu. Sitaki kwenda jela na umri huu”
Mrs Sanga alizungumza huku akiwa ameifumbata kwa pamoja mikono yake.
“Simfahamu kwa kweli”
Jibu la nabii Sanga likamfanya mrs Sanga kushusha pumzi zinto huku matumaini ya kuto ingia kwenye mikono ya sheria ikimtawala kichwani mwake.
“Nabii je walikupatia mateso?”
“Hapana nina imani mtu aliye toa agizo la mimi kukamatwa alihitaji nisipatiwe mateso.”
Mrs Sanga akaendelea kutazama mahojiano hayo ya mume wake na waandishi wa habari. Yalipo karibia kuisha, akaingia bafuni, akaoga kwa haraka kisha akarudi na kuvaa nguo zake.
“Nabii mbona huja ongozana na mke wako katika siku muhimu kama hii ya leo?”
Mrs Sanga akastuka na kusitisha zoezi la kujipaka mafuta mwilini mwake. Akamtazama mume wake anaye malizia mahojiano na waandishi hao wa habari.
“Kuna kazi ya kifamilia kidogo ana ishuhulikia. Nawashukuru na Mungu awabariki sana nyote mulio funga na kuomba kwa ajili yangu.”
Nabii Sanga mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo. Mahojiano yakaishia hapo na akaondoka ukumbini hapo. Mrs Sanga akazima tv hiyo kisha akamalizia zoezi lake la kujiandaa. Alipo hakikisha kwamba yupo vizuri, akaingiza baibui lake la siri katika pochi yake kubwa kishaa katoka ndani humo.
“Mama leo tupike nini?”
Mfanyakazi wa ndani alimuuliza Mrs Sanga.
“Chochote ambacho baba yenu ata jisikia kula. Mimi natoka”
Mrs Sanga akamuacha dada huyo wa kazi njia panda. Mrs Sanga akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo huku kichwani mwake akifikiria ni wapi ambapo ata kwenda kukaa japo kwa siku kadhaa pasipo kupata usumbufu wa mtu yoyote anaye mfahamu.
“Lazima Tomas akikutana na mume wangu ata muambia ukweli”
Mrs Sanga alizungumza mwenyewe huku akizidi kusonga mbele. Akafika benki ya crdb, akatoa kiasi cha milioni kumi na kurudi nacho kwenye gari.
“Pesa hii itanitosha”
Mrs Sanga alizungumza huku akiondoka eneo hilo la benki huku akilini mwake akiwaza sehemu sahihi ya yeye kutuliza kichwa chake ni Bagamoyo kwenye hoteli yoyote ya kitalii ambayo ata ona ina mpendeza kwa yeye kuishi.
                                    ***
Magreth na Sheby wakafika katika ofisi ya magari waliyo elekezwa na Clayton. Kila mmoja aka shangaa uwepo wa magari ya kifahari ambayo yapo kwenye car show room hiyo.
“Mmmm!! Magreth hapa ndipo ulipo elekezwa kweli?”
“Ndio Sheby kwani vipi?”
“Mmm mbona magari yote ni ya garama sana?”
“Wewe twende kwa wahusika bwana”
Wakaingia kwenye ofisi hiyo, wakasalimiana na sekretari waliye mkuta eneo la mapokezi. Akauliza ni wapi alipo bwana Clyaton.
“Wewe ndio Magreth”
“Ndio mimi”
“Basi ingia ofisi hiyo hapo”
“Sawa”
Magreth akaingia kwenye ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo ya magari. Akamkuta mzee mmoja mwenye umri una karibiana na nabii Sanga, akasalimiana naye kisha hawakuona haja ya kupoteza muda zaidi. Wakaelekea kwenye eneo yalipo wekwa magari hayo.
“Ameniambia uchague gari lolote utakalo”
“Lolote?”
“Ndio kuwa huru.”
“Sheby njoo unisaidie kuchagua gari ndugu yangu”
Wote watatu wakaanza kuzunguka kwenye magari hayo huku kila gari ambalo Magreth ana liona ana tamani kulichagua hilo.
“Jamani yote mbona ni mazuri?”
“Yaa yote ni mazuri. Wewe chagua kitu ambacho roho yako itapenda kwa kweli”
“Ila Audi ni nzuri kwa mtoto wa kike”
Sheby alishauri huku akimuonyesha Magreth gari hiyo yenye rangi nyeupe na inayo ng’ara vizuri.
“Kweli hili ni gari zuri, ni bei ngapi?”
“Audi Q7 ni dola laki moja na ishirini, hii ni model mpya ya mwaka huu.”
“Mmm parefu hapo”
Sheby alizungumza huku akitazama gari hilo.
“Nimelipenda hili”   
Magreth akachagua gari hilo la kifahari aina ya Audi Q7
“Sawa, basi taratibu zote za usajili za hili gari nita shuhulikia, pia tuta kukabidhi kwa dereva atakaye kusaidia kuliendesha gari hili hadi nyumbani kwako”
“Sawa nashukuru sana”
“Tuelekee ofisini kwa ajili ya kuandikishana”
Magreth na Clayton wakaingia katika ofisini. Magreth akajaza fomu zote na kukabidhiwa funguo zake.
“Hilo gari ni jipya kabisa yaani ni zero kilomita.”
“Yaani nina hamu ya kuingia ndani ya gari hilo, hembu ngoja nikafungue”
Magreth akatoka ofisini humo na kukimbilia kwenye gari lake akafungua mlango na kuingia ndani. Furaha ambayo imemtawala hakika hajawahi kuipata toka kuja kwake duniani. 
                            ***
    Nabii Sanga akaingia kanisani kwake. Waumini wake walio jitokeza kumuona kwa siku hiyo waka simama na kuanza kumshangilia huku wote wakiwa wamejawa na furaha sana. Nabii Sanga akawashukuru waumini wake hao, kisha baada ya hapo, akaongoza sala fupi ya kumshukuru Mungu. Kutokana siku hiyo sio siku ya ibada kanisani hapo, nabii Sanga akaagana na waumini wake kisha akaondoka na kuianza safari ya kuelekea polisi huku akiongozana na dereva wa kanisa hilo.
“Ndio RPC nina kuja ofisi kwako”
“Sawa tena nilikuwa nina fwatilia mazungumzo yako kwenye televishion na nikawa nina subiria umalize kuzungumza ili tuwasiliane”
“Sawa baada ya dakika kadhaa nitakuwa hapo”
Nabii Sanga akakata simu. Wakafika kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam. Nabii Sanga akapokelewa na RPC na wakaeleka ofisini kwake.
“Karibu sana mzee”
“Nashukuru. Ehee niambie ume fikia wapi katika kutafakari kwako”
“Ahaa…kumpoteza ina wezekana na nimesha andaa mpango mzima wa kuhakikisha kwamba ana kufa kifo ambacho hakuna mtu yoyote atakaye tilia mashaka na hata kama ikitokea wakatilia mashaka basi uchunguzi ukifanyika hakuna mtu ambaye ata weza kugundua lolote”
“Je ni kiasi gani cha pesa uta hitaji kwa shuhuli hiyo?”
“Kutokana wewe ni mzee wangu na tuna fahamiana kwa kipindi kirefu na ume toka kwenye matatizo. Nipatie milioni ishirini tu zita nitosha”
“Sawa sawa nitakupatia. Nina omba jambo moja unisaidie”
“Jambo gani?”
“Nina hitaji kuonana na kijana huyo kabla ya kufa kwake”
“Sawa hilo halina shaka mzee”
RPC akampigia askari mmoja na kumuagiza amuingize Tomas katika chumba cha mahojiano. Baada ya zoezi hilo kukamilika, nabii Sanga na RPC wakelekea katika chumba hicho.
“Kamera na sound record katika chumba hicho zote zime zimwa kwa hiyo utakacho kizungumza hapo kitaishia ndani humo. Mimi nipo hapa mlangoni nina kusubiria”
RPC alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Sawa”   
Nabii Sanga akaingia ndani ya chumba hicho na kumfanya Tomas ashtuke sana kwani hakutarajia kumuona nabii Sanga kwa wakati kama huu kwa namna moja ama nyingine alihisi kwamba Rama D na wadogo zake watakuwa wamemuua, kwani aliwashuhudia rafiki zake hao wakifa peke yao pasipo uwepo wa nabii Sanga.
                                                                                                ITAENDELEA
Haya sasa, nabii Sanga amekutana na mwizi anaye iba asali yake katika mzinga wake. Je ata mfanya nini Tomas, kijana aliye muamini sana? Endelea kufatilia kisa hichi cha kusisimua, usikose sehemu ya 16
 


Share:

MTOTO WA MIAKA 4 AUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINYANGA...MUUAJI NAYE AUAWA

Picha haihusiani na habari hapa chini

Na mwandishi wetu- Shinyanga Press Club blog
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la James Mhoja(36)ameuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuua kwa kumkata mapanga mtoto Emmanuel John(4) wakati akicheza na watoto wenzake nyumbani kwao.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Joseph Paul amesema tukio hilo lilitokea jana Juni 9 majira ya saa 9 alasiri kwenye Mtaa wa Ndala Manispaa ya Shinyanga, wakati mtoto huyo alipokuwa anacheza nje ya nyumba yao ndipo mtu huyo alimvamia na kumshika kisha kuanza kumkata mapanga.

"Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto huyo naye aliuawa na wananchi kwa kumponda mawe na katika uchunguzi wetu wa awali,tumebaini alikuwa anatatizo la ugonjwa wa akili na bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili"amesema kaimu Kamanda Paul.
Share:

TANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI NA KIBIASHARA ZINAZOLETWA NA TPDC



Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akikata utepe leo kushiria uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania ( Tan Oil.) kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu uzinduzi huo ulifanyika kijiji cha Michungwani kata ya Segera wilayani
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akikata utepe leo kushiria uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania ( Tan Oil.) kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu uzinduzi huo ulifanyika kijiji cha Michungwani kata ya Segera wilayani

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio akizungumza wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi huo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Handeni,Athumani Malunda akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 MKUU wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo
 AFISA wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gibson George akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo
Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi huo
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu



WANANCHI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara ambazo zinaletwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) kupitia miradi yake katika sekta ya mafuta na gesi ambayo inakuja mkoani humo. 

Hayo yamebaishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),Dk James Mataragio pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigela jana katika kijiji cha Michungwani kata ya Segera wilayani hapa katika hafla fupi ya uzinduzi wa kituo cha kuweka mafuta kinachoendeshwa na kampuni tanzu ya shirika hilo Tan Oil. 

Akizungumza katika hafla hiyo,Dk Mataragio amesema kuwa shirika hilo limeingia rasmi katika mkakati wake wa kufufua biashara ya mafuta ambayo ilikuwepo tangu shirika hilo lilipoanzishwa mwaka 1969 kabla ya kusitisha huduma hizo.


Amesema kuwa mkakati huo sio lengo la serikali kuua kampuni binafsi za mafuta bali ni kuingia katika ushindani wa biashara ya mafuta ikiwemo uagizaji wa mafuta kupitia mfumo wa pamoja wa uagizaji wa mafuta(BPPA),kudhibiti bei ya mafuta ,kuwa na takwimu za matumizi ya nishati hiyo pamoja na usambazaji kwa ujumla. 

Amesema kuwa wanatarajia kuzindua vituo vingine sita vya aina hiyo baada ya kuzindua vituo vingine viwili Musoma mkoani Mara na Segera wilayani Handeni mkoani hapa. 

Aidha,amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Shirika hilo litajenga vituo vingine 100 katika maeneo mbalimbali nchini katika Halmashauri za Wilaya sambamba na ujenzi wa matenki makubwa ya kuhifadhia mafuta katika mikoa mbalimbali hapa nchini.


Mkurugenzi huyo aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Tanga,Dar es salaam,Morogogo,Dodoma,Mbeya na Isaka-Kahama kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari nchini(TPA) ili kuunguza msongamano wa wfanyabiashara kuchukua mafuta sehemu moja pamoja na kupunguza misongamano ya magari lengo likiwa ni kulinda miundombinu ya barabara. 

“TanOil inachukua kazi zote za iliyokuwa kampuni ya mafuta ya Copec sasa tunaingia rasmi katika biashara ya mafuta, lengo si kuziondoa kampuni binafsi za mafuta bali ni kuleta ushindani, kudhibiti bei, kuwa na takwimu sahihi za mafuta na kuagiza mafuta kwa ujumla (BPPA),” alisema. 

Kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga,amesema kuwa baada ya kampuni ya Tullow kuwauzia hisa zao kampuni ya mafuta ya Total,sasa kampuni hiyo itamiliki hisa hizo kwa asilimia 66.7 na wamefikia muafaka na mradi utaanza mapema mwakani . 

Amefafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Juni,wataanza kutangaza zabuni za ujenzi wa mradi kwa kampuni mbalimbali,mwezi Desemba watapitia kampuni hizo ili kujua gharama za mradi na ujenzi wa mradi huo utasimamiwa na Shirika la Mafuta la Uganda(NOC),Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) na kampuni ya CNOOC. 

“Ujenzi wa bomba la mafuta uliokuwa uanze ulikwamishwa na mazungumzo ya kodi kati ya kampuni za mafuta kwa hiyo kuanzia mwaka huu mwezi Jui tutaanza kutangaza zabuni hadi mapema mwakani kazi zitaanza,hivyo wananchi wa mkoani Tanga kupitia miradi ya TPDC changamkieni fursa za kiuchumi na biashara,”alisema. 
 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliwashukuru TPDC kwa kuanzisha vituo hivyo mkoani humo nawataka wananchi kutoa ushirikiano wa ulinzi katika vituo hivyo kutokana ni mali ya serikali na kuwasisitiza kuanzisha shughuli za uwekezaji zaidi na kjipatia fursa za ajira kupitia miradi ya TPDC ikiwemo kufunguliwa vituo vya mafuta,gesi na mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi(EACOP). 

Pia, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Daudi Mayeji kuharakisha mchakato wa taarifa ya tathmini ya eneo ambalo TPDC watajenga tenki kubwa la kuhifadhia mafuta ili wananchi walipwe fidia na ujenzi uanze haraka. 

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema kuwa katika mradi wa bomba la mafuta(EACOP)wilaya hiyo inapitiwa na bomba hilo kwa urefu wa kilometa 54,na eneo la kambi kubwa itakayojengwa Handeni lina ukubwa wa ekari 51 na tayari wananchi wa Misima wamekubali kuondoka kupisha ujenzi huo. 

Kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta vya TPDC,amesema wilaya hiyo ina maeneo mengi ya uwekezaji hivyo amekubali kutoa eneo popote pindi TPDC wakitaka kwa ajili ya ujenzi huo. 

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Handeni,Athumani Malunda aliwaomba TPDC kujenga vituo vingine viwili kama hivyo wilayani humo katika maeneo ya Mkata na Handeni mjini na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji ikibidi kuwapa eneo. 
Share:

Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Ya Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi CCM Jijini Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 10 Juni 2020.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa Hamasa ya maendeleo pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 10 Juni 2020 kabla ya kuanza kwa Kikao hicho. PICHA NA IKULU


Share:

POLISI MOROGORO WABAINI HEKARI 100 ZA MASHAMBA YA BANGI..RPC ATOA SIKU 2 VIONGOZI WA VIJIJI WAJIELEZE

Na Jackline Lolah - Malunde 1 blog Morogoro

Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Willbroad Mutafungwa amewataka wananchi wanaojihusisha na kilimo cha bangi kuacha mara moja huku akitoa siku mbili kwa viongozi wa vijiji vitano mkoani Morogoro kujisalimisha polisi baada ya operesheni iliyofanywa na jeshi hilo kubaini hekari 100 za mashamba ya bangi.

Kamanda Mtafungwa alitoa agizo hilo jana wakati wa operesheni maalum ya kusaka watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu vya kuzalisha na kuuza bangi kinyume na sheria.

Alisema mashamba hayo zaidi ya hekari 100 yamebainika umbali wa kilomita 30 kutoka eneo la makazi ya watu katika kijiji cha Misengele, Tarafa ya Doma.

"Ndani ya wiki moja kuanzia tarehe 1juni hadi tarehe 8 mwezi Juni mwaka huu tumefanya oparesheni maalumu ya kudhibiti dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 12 wa makosa mbalimbali ya bangi ambapo vilivyopatikana ni viroba 5 na nusu, misokoto 160 ya bangi na puli moja na nusu, kete 10 za bangi na gari yenye namba za usajili T. 572 CFN aina ya Toyota Brevis rangi ya silva, pikipiki 2 aina ya houjue na ekari 100 ya mashamba ya bangi",amesema. 

“Natoa siku mbili kwa viongozi hawa wa jijiji vya Bunduki, Misengere, Kododo, Vinile, na Yowe, kata ya Doma, wilayani Mvomero, vinavyozunguka bonde la Mto Mgeta kujisalimisha kituo cha polisi wenyewe ili watuambie walikuwa wapi miaka yote mambo haya yanafanyika katika maeneo yao pasipo kutoa taarifa yoyote,” alisema Mutafungwa.

Alisema eneo hilo lililopo karibu na mto Mgeta, lipo ndani ya hifadhi ya msitu asilia wa Misengele na kuzitaka mamlaka zinazohusika na uhifadhi wa maeneo hayo kuweka uangalizi wa karibu kujua shughuli zinazoendelea.

“Eneo hili ni hifadhi hairuhusiwi mtu yeyote kufika ama kuendesha shughuli za kibinadamu, lakini katika operesheni kufuatilia taarifa za uchunguzi inabainika uwapo wa mashamba haya makubwa ilhali viongozi wa vijiji wapo na wamenyamaza,” alisema Kamanda Mtafungwa.

Kamanda Mtafungwa alisema katika operesheni hiyo inayoendelea watu 12 wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.


Share:

DKT.SHEIN : SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR (SMZ) INATEKELEZA HAKI ZA BINADAMU KWA KUTOA AFYA NA ELIMU BURE

Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali inatekekeleza utawala bora kwa wananchi kwa kuwapatia huduma za jamii zikiwemo elimu na  afya zinazotolewa bure.

 Akizungumza alipokutana na ujumbe wa watendaji wa juu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Ikulu Zanzibar, Dkt. Shein alisema kuwa Serikali inatakeleza kwa vitendo dhana ya utawala bora ikiwa ni utekelezaji wa dhana iliyoasisiwa na Hayati. Abeid Aman Karume baada ya Mapinduzi ya Mwaka 1964.

“Lengo kuu la mapinduzi wakati huo lilikuwa ni kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa kwa kila mwananchi hapa Zanzibar, kwa hiyo Hayati. Abeid Aman Karume aliiongoza Zanzibar kulete haki hizo ikiwemo elimu, afya na ardhi ambapo kabla ya hapo huduma zilikuwa zinatolewa kwa madaraja, hasa sekta ya afya na elimu daraja A lilikuwa la Waingereza, B lilikuwa la zile familia za kisultani, C watu wa katikati na D watu wa kawaida ambao kimsingi walikuwa wanapata huduma mbovu, kwa hiyo suala la utekelezaji wa haki za binadamu lina historia kwa hapa Zanzibar”, alisema Dkt.Shein.

Alibainisha kuwa baada ya Mapinduzi wananchi walianza kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu, kuanzia darasa la kwanza hadi la nne na kuanzia darasa la tano kulikuwa na malipo ambayo yalimnyima mwananchi wa hali za chini haki hiyo.

 Kwa upande wa ardhi, Dkt. Shein alisema kuwa ilikuwa ni ngumu kwa wananchi wa Zanzibar kumiliki ardhi kabla ya mapinduzi kwani ardhi iligawiwa kwa wageni na wenyeji kuwa wafanyakazi wa mashamba ya wageni, lakini baada ya mapinduzi kila mwananchi alikuwa na uhuru na haki ya kutumia ardhi kwa mujibu wa sheria.

Alifafanua kuwa mambo hayo matatu ni ishara ya kwamba SMZ imeanza utekelezaji wa Utawala bora na Haki za Binadamu mara tu baada ya kuidai haki  hiyo kwa wakoloni, na hii ilileta furaha kwa kila Mzanzibar kupata haki zake za msingi kama vile ardhi, afya na elimu bure amabapo mpaka sasa Serikali inatoa huduma hizo bure kwa asilimia 100.

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa chini ya Uongozi wa Rais. Shein utawala bora na utekelezaji wa haki za binadamu umeonekana wazi  kwa kuwa hadi  sasa Serikali yake inatoa huduma za afya na elimu bure kwa kila mwananchi.

“Mhe. Rais kutokana utekelezaji wa utawala bora na  haki za binadamu,  Zanzibar imeendelea kuwa na amani, lakini pia wananchi wameendelea kupata huduma za afya na elimu bure, hii ndiyo dhana ya utawala bora”, Jaji Mwaimu.

Alibainisha lengo la kumtembelea kuwa  ni kuweka ukaribu na Serikali yake ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu ya tume hiyo ambayo   ni kufuatilia utekelezaji wa haki za  msingi za wananchi.

Aidha, Jaji Mwaimu aliipongeza SMZ kwa kushughulikia vizuri janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona, kwani  Serikali hiyo ilikuwa bega kwa bega na  wananchi kwa kuwapa moyo wa kufanya kazi huku wajikinga na maradhi hayo na mpaka sasa janga hilo limepungua kwa kiasi  kikubwa.

“Serikali imechukua  hatua kubwa kushughulikia janga la corona na tunashukuru kwamba viongozi wote wa pande zote mbili mmekuwa na busara kubwa kwenye mapambano hayo pamoja na maagizo yaliyokuwa yanatolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ikiwemo kufungia watu ndani, lakini nyinyi mlisema watu wafanye kazi na sasa tumeshinda”, Jaji Mwaimu.

Mwisho


Share:

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Ateta Na Madereva Wa Malori, Namanga

Na WAMJW- Arusha.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha na kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto zinazowakumba.

Dkt. Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga.

“Nimekuja kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa ” alisema.

Aidha, Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho, Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na kusema anawapenda sana.

Mbali na hayo Dkt. Mollel alisema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Nae, dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya Bw. Abdullah Hassan amesema kuwa, kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka Kenya kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na ugonjwa wa Corona jambo ambalo sio kweli.

“Tunaishi maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha zaidi, sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili.

Kwa upande wake, Japhet Jeremiah alisema kuwa, wamekuwa wakiombwa kiasi cha shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, hali aliyeweka wazi kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania.

“Sisi kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tumeambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na sijawai tumia dawa yoyote mpaka sasahivi” alisema


Share:

Azimio La Kumpongeza Rais Magufuli Kwa Mapambano Dhidi ya Corona Lapita Kwa Kishindo Bungeni

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge limefanya   azimio La Kumpongeza  Rais   Wa  Jamhuri Ya  Muungano  Wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kwa Namna Alivyoliongoza Taifa  Katika Mapambano Dhidi Ya Janga La UgonjwaWa Corona (Covid-19)


Akiwasilisha  azimio  hilo  jana  Juni 9,2020 Bungeni   jijini  Dodoma  mbunge wa VITI MAALUM  Esther  Mmasi  amesema  katika  kukabiliana  na  ugonjwa   wa Corona  Rais alitumia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo  kukataa    kuiga  mtindo  wa kufunga mipaka  na  kuwafungia  wananchi  wake wasitoke nje tofauti na viongozi wa Mataifa mengine waliofunga  mipaka  ya nchi zao na  kuzuia watu wao kutokanje    (lockdown) .

Hivyo Mhe.Mmasi amesema kwa  kuzingatia hali hiyo, Rais Magufuli  aliruhusu  shughuli za kiuchumi  na  baadhi  ya  shughuli za kijamii    ziendelee  kwa  tahadhari  na  kuwahimiza wananchi kuzingatia  maelekezo na miongozo  ya wataalam.

Wakichangia Michango yao kuhusu mjadala wa  azimio hilo la kumpongeza Rais,baadhi ya Wabunge akiwemo Mbunge wa Rombo Mashariki Joseph Selasini amesema Rais Magufuli amesaidia kuondoa hofu kwa Watanzania ,mbunge wa Viti Maalum Christina Ishengoma akitoa pongezi kwa kuruhusu ibaada huku Mbunge wa Viti Maalum  Nagma Giga   akisema Rais Magufuli amekuwa Mzalendo wa Kweli kwa Taifa la Tanzania.
==>>Lisome Tamko Zima Hapo Chini


Share:

Mbunge wa Nkasi CCM, Ally Kessy Ataka Rais Magufuli Aongezewe Muda....Spika Ndugai Amjibu

Mbunge wa Nkasi CCM, Ally Kessy ameliomba Bunge kumuongezea muda wa kutawala Rais John Magufuli hata kama yeye Rais hataki kwa kubadili Ibara inayoweka kikomo cha kipindi cha urais.

Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Kessy kuileta hoja hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika Bunge la 12 ambapo ameahidi kulishughulikia.

“Mheshimiwa Keissy ngoja tuende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Keissy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,”  Amesema  Spika Job Ndugai

Itakumbukwa kuwa Rais Magufuli amekwisha kataa hadharani wazo la kuongeza muda wa kuongoza nchi.



Share:

Dkt. Abbasi: Watakaoshindwa Kufuata Mwongozo Afya Michezoni Watachukuliwa Hatua Kali.

Na Kelvin Kanje, Mwanza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi,  tarehe 9 Juni, 2020, ameendelea na ziara ya kukagua, pamoja na mambo mengine, utayari wa viwanja mbalimbali vya soka kabla ligi hazijaanza.

Akiwa jijini Mwanza jana Dkt. Abbasi aliwaeleza wadau wa michezo kuwa Serikali imechukua uamuzi mgumu wa kufungua michezo yote nchini na tayari ratiba za mechi mbalimbali katika Ligi Kuu ya Soka Nchini imetoka na timu zimeanza mazoezi, vilevile Serikali imetoa ruksa kwa mashabiki watakaotaka kuhudhuria  viwanjani waruhusiwe kwa taratibu maalam.

Katika hatua nyingine Dkt. Hassan Abbasi amesisitiza kuzingatiwa kwa Muongozo wa Afya Michezoni ikiwemo mashabiki na wachezaji kunawa kwa maji tiririka na sababu au kutumia vipukusi kabla ya kuingia viwanjani, kupimwa joto na mashabiki kukaa kwa kuachiana mita moja na kusisitiza yeyote atakayekiuka taratibu hizo atachukuliwa hatua stahiki ikiwemo viwanja husika kufungiwa kutumika kwa ligi.

“Tumefanya mazungumzo na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Katibu Tawala wa Mwanza na wadau mbalimbali na wote wako tayari kuhakikisha yale yote ambayo Serikali imeagiza kwenye mwongozo yanazingatiwa,” alisema Dkt. Abbas wakati akiongea na wadau wa michezo Mkoani Mwanza akiwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Katika ziara hiyo Dkt. Abbasi ameambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Yusuf Singo na walitembelea pia kukagua viwanja vya CCM Kirumba na Nyamagana.

Katika hatua nyingine, leo akiwa Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza na baadaye mkoani Shinyanga, Dkt. Abbasi amewapongeza wadau binafsi waliojenga viwanja vya Gwambina (Misungwi); na Uwanja wa Mwadui Complex na uwanja mwingine mpya vilivyoko Shinyanga Mjini.

“Uwekezaji huu ni mkubwa na umechangia juhudi za Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya michezo namwagiza Mkurugenzi wa Michezo awaletee wataalamu wetu ili washirikiane nanyi utaalamu katika baadhi ya maeneo hasa utunzaji wa nyasi za viwanja," aliagiza.


Share:

Wanunuzi Wa Kahawa Marufuku Kununua Kahawa Usiku

Na: Allawi Kaboyo
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi msimu wa Kahawa wa mwaka 2020/2021 ikiwa ni pamoja na kutangaza bei  ya malipo ya awali shilingi 1200 kila kilo ya kahawa ya maganda kwa  Vyama Vikuu vya Ushirika vya KCU 1990 Limited,  KDCU Limited na Ngara Farmers.

Mkuu wa Mkoa Gaguti akitangaza ufunguzi wa msimu katika  Chama cha  Msingi cha Mabira Wilayani Kyerwa Juni 9, 2020 alisema kuwa jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha mkulima analindwa haki zake asipunjwe katika bei  pia muda wa kupata malipo yake uwe mfupi kutoka wiki moja hadi masaa 48 tangu mkulima kufikisha kahawa yake katika Chama cha Msingi.

Gaguti amewataka wafanya biashara ya kahawa ambao wapo tayari kununua kahawa ya wakulima wa kahawa katika mkoa huo kuhakikisha wanafanya biashara hiyo mchana kweupe bila kuwahujumu wakulima kwakuwa kahawa na biashara halali na hakuna sababu ya kuuzwa gizani.

“Niwaombe wafanyabiashara wenye nia ya kunua kahawa yetu fanyeni biashara hii mchana kweupe maana hata wakulima wanavuna mchana kweupe, nielekeze tu katika mkoa wa Kagera sitaruhusu biashara ya kahawa kufanyika usiku hii sio biashara haramu” Alisisitiza Mkuu wa mkoa Gaguti.

Mkuu wa Mkoa Gaguti alitumia fursa hiyo kurudia kauli yake kuwa kama kuna mfanyabaiashara yeyote ambaye yupo tayari kununua kahawa kwa wakulima kwa bei nzuri ajitokeze na kutangaza bei yake ili akapatiwe kahawa.

 “Kufikia tarehe 8.06.2020 tumepokea maombi ya wafanyabiashara wanane na kati ya hao wawili tu waliwasilisha maombi kwa barua na mmoja ndiye aliomba kununua kahawa kwa shilingi 1100 tu.”  Alieleza Mkuu wa Mkoa Gaguti.

Mkuu huyo wa Mkoa pia alitoa rai kwa wakulima kuhakikisha wanatunza ubora wa kahawa yao kabla ya kuipeleka katika  Vyama vya Msingi ili kuhakikisha kahawa kutoka Mkoani Kagera inafika kwenye soko ikiwa na ubora unaotakiwa  ambapo katika msimu huu 2020/2021 zinatarajiwa kukusanywa takribani kilo milioni 60 juu ya kiasi cha msimu uliopita ambapo zilikusanywa kilo milioni 52.

Naye Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Japhet Justine katika hafla hiyo ya ufunguzi wa msimu wa kahawa mwaka 2020/2021 alisema kuwa Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vimekuwa viaminifu tangu mwaka 2018 benki ya TADB ilipoanza kuvipa mkopo ambapo msimu wa mwaka 2018 Benki hiyo ilitoa   bilioni 30 na zililipwa zote, msimu 2019 Benki ilitoa bilioni 23 na zote zililipwa.

“Aidha, msimu huu wa 2020/2021 tayari tumeweka shilingi  bilioni  7.7 katika akaunti za Vyama Vikuu vya KDCU Limited na KCU 1990 Limited kwaajili ya kukusanya kahawa ya wakulima na bila kuchelewesha malipo yao. Ndiyo maana baada ya kuona uaminifu wa vyama hivyo vikuu tumeamua kupunguza riba kutoka asilimia 12 na mwaka huu tunatoa mkopo kwa asilimia tisa tu (9%).” Alifafanua Bw. Japhet

Kuanzia Juni 9, 2020 wakulima wa zao la kahawa Mkoani Kagera wanahamasishwa kuanza kukusanya kahawa katika Vyama  vyao vya Msingi na fedha ya malipo ya awali ipo tayari kwaajili ya  kuwalipa.


Share:

Nyavu Haram 110, kokoro 2 na timber 32 Zakamatwa Na Kuteketezwa Wilayani Busega

Jumla ya Nyavu 110, kokoro 2 na timber 32 zilizokuwa zinatumika katika uvuvi haram zimekamatwa na kuteketezwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Busega. 


Vifaa hivyo vimekamatwa kati ya tarehe 19/05/2020 na 04/06/2020 katika vijiji vya Nyakaboja kata ya Kabita na Maega Kata ya Kalemela.

Uvuvi haram umekuwa changamoto ukanda wa Ziwa Viktoria, hivyo Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Busega imeanza kupambana na wavuvi wanaotumia vifaa visivyokubalika kwenye shughuli za uvuvi ili kuzuia uharibifu wa rasimilimali kwenye Ziwa Viktoria.

Kwa upande mwingine Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imewataka wavuvi wote wilayani humo kufuata sheria za uvuvi kwa kufanya shughuli zao za uvuvi kwa kufuata utaratibu uliowekwa na serikali, kwani uvuvi haram umekuwa moja ya changamoto kwenye ukusanyaji wa mapato yanayotokana na shughuli za uvuvi.


Share:

TAKUKURU Makao Makuu Kuwahoji Wabunge 69 wa CHADEMA Kuhusu Matumizi Ya Fedha Za chama

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, inatarajia kuwahoji wabunge 69 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, 
 
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 10 Juni 2020 na Doreen Kapwani, Afisa Uhusiano wa Takukuru imesema mahojiano hayo yatafanyikia Makao Makuu ya taasisi hiyo Dodoma na yatakamilika wiki ijayo.

“Ni kweli kuwa Takukuru imewaita waheshimiwa wabaunge wa Chadema na waliowahi kuwa wabunge wa chama hicho kwa ajili ya mahojiano.”

“Hatua hii ni muendelezo wa uchunguzi wa malalamiko dhidi ya matumizi mabaya ya fedha nza Chadema unaoendeshwa na Takukuru ambapo hatua iliyopo sasa ni kuwahoji wabunge 69,” amesema Doreen


Share:

Halmashauri Zatakiwa Kuwa Na Operesheni Maalum Ya Upimaji Ardhi

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameziagiza halmashauri nchini kufanya operesheni maalum ya kupima na kumilikisha ardhi ili kuwawezesha wananchi kuwa na hati miliki kwenye maeneo wanayoyamiliki.

Dkt Mabula alitoa maagizo hayo jana kwa nyakati tofauti katika wilaya za Tarime na Musoma mkoani Mara alipokutana na uongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi wa wilaya hizo wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani humo.

Alisema, ni lazima halmashauri zifanye opresheni maalum ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ili kuwawezesha wananchi kuwa na hati miliki zitakazowawezesha kuzitumia kwenye sughuli za kimaendeleo na wakati huo kuiwezesha serikali kukusanya mapato kupitia kodi ya pango la ardhi.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Mabula, pamoja na wizara ya Ardhi katika Bajeti yake ijayo ya 2020/2021 kuwa na mpango wa kupima kila kipande cha ardhi kupitia miradi ya Benki ya Dunia na Benki ya Exim-Korea lakini halmashauri zina wajibu kuhakikisha ardhi inapimwa na kumilikishwa.

Alizitaka halmashauri za wilaya na zile za miji kutenga bajeti kwa ajili ya kazi ya kupanga na kupima maeneo na kusisitiza kuwa, zoezi hilo lisiishie katika upimaji pekee bali lifikie hatua ya umilikishaji ardhi kwa kuwapatia wananchi hati.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, vifaa kwa ajili ya kazi za upimaji vipo kwenye baadhi ya Ofisi za Ardhi za Mikoa na kuongeza kuwa kinachotakiwa ni halmashauri kuwasiliana na ofisi hizo ili kuvitumia kwenye kazi ya upimaji.

Alisema, kwa halmashauri zenye wataalam wachache wa sekta ya ardhi zinaweza kuazima wataalam  kutoka maeneo mengine ikiwemo Ofisi za Ardhi za Mikoa na kubainisha kuwa kinachotakiwa ni wakurugenzi kutenga pesa ya kujikimu kwa wataalam watakaofanya kazi ya upimaji.

‘’Mnaweza kuazima wataalam kutoka maeneo mengine kama ile vofisi za ardhi za mikoa na cha msingi hapa ni kwa Mkurugenzi kutenga fedha za kuwalipa wataalam watakaoenda kufanya kazi’’ alisema Dkt Mabula.

Akigeukia suala la migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali, Dkt Mabula amezitaka halmashauri kushirikiana na ofisi za ardhi za mikoa zilizoanzishwa hivi karibuni ili kuatua migogoro ya ardhi kwenye maenro yao na kubainisha kuwa ofisi za ardhi za mikoa zisipotumika ipasavyo basi itakuwa haina maana kuanzisha ofisi za ardhi za mikoa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri aliipongeza Wizara ya Ardhi kwa hatua inazochukua katika kushughulikia migogoro ya ardhi nchini ambapo aliiomba ofisi ya Kamishna wa Ardhi mkoa wa Mara kuyachukua matatizo ya ardhi ya wilaya yake na kuyafanyia kazi ili kuleta suluhu miongoni mwa wananchi wenye migogoro.


Share:

Serikali Kurudisha Zao La Shahiri Na Kutatua Adha Katika Zao La Zabibu

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma
Serikali imekutana na wadau wa zao la shahiri na zabibu kwa lengo la kurejesha zao la shahiri na kutatua changamoto zilizopo katika sekta ndogo ya Zabibu ili kuweza kukuza soko la mazao hayo na kuinua kipato cha wakulima wake.
 
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe katika Mkutano uliyohudhuriwa na wanunuzi wa zao la zabibu na shahiri pamoja na wakulima wa mazao hayo.
 
Aidha Mhe. Bashe amesema kuwa kwa sasa wakulima wa shahiri hawana soko, hivyo ni vyema kwa msimu ujao wakulima walime zao la shahiri.
 
Mhe. Bashe ameuagiza uongozi wa kiwanda cha Tanzania Breweries (TBL) kufunguliwaa au kukikodisha kiwanda cha Kilimanjaro ambacho kipo mikononi mwao ili kianze kazi mara moja.
 
“Lengo ni kutaka wakulima waweze kulima kwa msimu ujao na sisi serikali tutahakikisha mikataba inakuwa sawa kwa pande zote mbili kwa mnunuzi na mkulima na uwazi wa mikataba hiyo ili kila mmoja kunufahika katika zao hilo”, ameeleza Mhe. Bashe.
 
Hata hivyo katika mkutano huo Mhe. Bashe amewataka wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa na warajis wa vyama vya ushirika watakapo saini mikataba hiyo na Serikali ishirikishwe kikamirifu ili kulinda maslahi ya mkulima na wanunuzi.
 
Kwa zao la zabibu Mhe.Bashe amesema msimu wa kilimo unaanza mwezi wa nane hivyo Serikali inahitaji uhakika wa masoko na wanunuzi wanatakiwa kusema namna ambavyo watanunua zao la zabibu .
 
“Hatutaki wakulima wa zabibu mwezi wa nane wakati wa kuvuna wapate shida ya masoko na nahitaji kujua kwa mwezi huo tutavuna kiasi gani . Njia pekee itakayotusaidia ni kuingia mkataba na wakulima” ameweka wazi Mhe. Bashe.
 
Kwa kuongezea Mhe. Bashe ametoa wito kwa wakulima kutotegemea zao moja bali wajikite pia kwenye mazao mengine na kuwataka kampuni ya wanunuzi kununua shahiri kwa wakulima wote .
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi.Theresia Mahongo amesema zao hili ni zao la kibiashara linalowaingizia uchumi wakulima hivyo ametoa rai kwa wanunuzi kuongeza tani kwa zao la shahiri kwani wakulima wanalima zaidi ya tani 8,000 zinazohitajika
 
Mkurugenzi wa Tanzania Bruweries (TBL) Bw.Philip Redman amesema kwa msimu ujao wa 2021,wameingia mkataba na wakulima 300 na kiwanda kina uwezo wa kuchukua tani 5,000 kwa mwaka.
 
Kwa upande wa Serengeti Breweries (SBL) Mkurugenzi wa Mahusiano Bw.John Wanyancha amesema kuwa kwa msimu ujao wanatarajia kuchukua tani 3,000 kwa wakulima 60.
 
Huku Mkulima wa shahiri Bw. Domisiani William kutoka Karatu ameeleza changamoto wanazokumbana nazo ni mapato na bei ndogo ya zao hilo pia ameiomba Serikali kuongeza tani kwani wakulima wanalima zaidi.


Share:

Viwanja Vinauzwa Bei nafuu: Bunju na Mapinga

Viwanja Bei nafuu: Bunju na Mapinga

Kwa Mapinga; viwanja vipo (Mji mpya) karibu na Kimere resort, km 2 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road).
Hapa vipo viwanja vya:
15/15 bei million 3,
20/20 bei million 6
20/30 bei million 8
20/40 bei million 11
Nusu eka bei million 26
Eka moja bei million 50
Huduma za umeme na maji zipo.

Kwa Bunju; vipo viwanja 4 na Kila kiwanja kina ukubwa wa 25/40 na bei ya kila kiwanja ni tsh 30 million.

Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki.
Hakuna dalali, mpigie mhusika: 0757100236


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger