Monday, 20 April 2020
WANNE WADAKWA NA DAWA ZA KULEVYA NYUMBANI KWA CHIKU SHINYANGA MJINI
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia wanaume watatu na mwanamke mmoja kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine katika mtaa wa Majengo, Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema watu hao wamekamatwa Aprili 19,2020 baada ya askari polisi kupata taarifa za kiintelejensia.
“Askari walifika nyumbani kwa mtuhumiwa Chiku Tungu na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo na dawa hizo ambazo ni pinchi 08 za heroine pamoja na rizla, kitezo, kigae na kisu kimoja”,amesema Kamanda Magiligimba.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hassan Ibrahim (22), mkazi wa Majengo, Juma Omary (26), mkazi wa Ngokolo, Abdalah Hemed (23), mkazi wa Majengo pamoja na mwanamke mmoja aitwaye Chiku Tungu (57), mkazi wa Majengo.
“Watuhumiwa wanahojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani. Natoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uuzwaji, utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevya ili kuikinga jamii dhidi ya dawa hizo”,amesema Kamanda Magiligimba.
Marekani Waandamana Kupinga Marufuku Ya Kutotoka Nje Kisa Corona
Waandamanaji nchini Marekani wameingia mitaani katika majimbo kadhaa wakishinikiza magavana kufungua uchumi wa majimbo yao kwa kuondosha amri ya kutokutoka nje.
Marufuku hiyo ya kutokutoka nje imewekwa katika majimbo yote ya Marekani ili kudhibiti kusambaa kwa janga la virusi vya corona, hali iliyotikisa uchumi wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi duniani.
Maaandamano yameripotiwa jana Jumapili katika majimbo ya Arizona, Colorado, Montana na Washington, huku mwendelezo wa maandamano hayo ukitarajiwa leo Jumatatu.
Hasira juu ya marufuku hizo imeongezeka nchini humo huku waandamanaji wakitaka masharti yalegezwe.
Rais wa Marekani Donald Trump ameonesha dalili za kukubaliana na maandamano hayo.
Kwa sasa, Marekani ndiyo kitovu cha janga la ugonjwa wa virusi vya corona duniani. Hata hivyo kuna dalili kuwa maambukizi yanafikia kileleni nchini humo na kasi ya maambukizi kuanza kushuka katika baadhi ya majimbo.
-BBC
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA ASKOFU GETRUDE RWAKATARE
PROF.OLE GABRIEL AWATAKA WATALAAM WA MIFUGO KUACHA KUKAA MAOFISINI

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (Wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye maombi mafupi ya kuliombea taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona muda mfupi kabla ya kuanza kukagua josho la mifugo lililopo mnada wa awali wa Buzirayombo uliopo Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato na wakala wa majengo (TBA) leo kwenye eneo la mnada wa wa awali wa Buzirayombo unapotarajiwa kufanyika ujenzi wa majengo ya kisasa ya mnada wa upili .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Leonard Mwaisabula akielezea manufaa ya mnada wa upili wa Buzirayombo kwa upande wa halmashauri hiyo pindi utakapoanza kazi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel leo alipofika Wilayani humo kwa ajili ya kukagua eneo itakapojengwa miundombinu ya mnada huo.

Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Geita Mhandisi Gladys Jeffa mapema leo akifafanua hatua ambazo mpaka sasa ofisi yake imefikia kabla ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya mnada wa Upili wa Buzirayombo unaotarajiwa kuanza kabla ya mwezi Julai mwaka huu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati), Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) mkoa wa Geita Mhandisi Gladys Jeffa (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Leonard Mwaisabula wakielekea kwenye josho la mifugo lililopo ndani ya mnada wa awali wa Buzirayombo wakati wa ziara yake ya kukagua eneo hilo la mnada leo

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akipokea maelezo ya namna utakavyokuwa mnada wa Upili wa Buzirayombo baada ya kukamilika kwake kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Majengo (TBA) Bw. David Luoga leo alipofika kwenye eneo hilo kwa ajili ya kukagua.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel akisoma maelezo ya kibao cha ufunguzi wa kliniki ya Mifugo iliyopo Wilayani Chato ambako alifika leo kwa ajili ya kukagua miundombinu ya kliniki hiyo inayotarajiwa kukarabatiwa upya kwa ushirikiano baina ya Halmashauri ya Wilaya hiyo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
........................................................................................
Na.Mwaandishi wetu,Chato
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka wataalam wa sekta ya mifugo kote nchini watumie muda mwingi kwenda kuwahudumia wafugaji badala ya kukaa ofisini.
Prof. Ole Gabriel ameyasema hayo mara baada ya kufika kukagua moja ya kliniki za mifugo iliyopo Wilaya ya Chato Mkoani Geita leo ambapo amemshauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Leonard Mwaisabula kutenga kiasi cha fedha cha kuanza ukarabati wa kliniki hiyo na Wizara yake itamuunga mkono kwa kukamilisha hatua zilizobaki.
"Ni kweli Wizara ina mpango wa kukarabati kliniki zote za Mifugo hapa nchini lakini kipaumbele chetu cha kwanza ni kwa zile halmashauri ambazo zitakuwa zimeshaanza ukarabati kwa kutumia fedha za mapato yao ya ndani hivyo kama Chato mkianza mapema Wizara pia itawapa kipaumbele na hatimaye muwe mfano kwa wengine" Aliongeza Prof. Ole Gabriel.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Leonard Mwaisabula amesema kuwa halmashauri yake itayafanyia kazi ushauri huo kwa sababu wana shauku kubwa ya kuona kliniki hiyo inafanya kazi.
"Nimepokea ushauri wako Mhe. Katibu Mkuu na kesho tutakutana kwa ajili ya kuangalia mchanganuo wa fedha tulizokuwa tumetenga kwenye idara ya mifugo ili kuona namna tunavyoweza kuanza na ukarabati wa kliniki hii kwa sababu kwetu ina umuhimu Mkubwa sana" Alisema Bw. Mwaisabula.
Mara baada ya kutoka kwenye eneo hilo Prof. Olr Gabriel alielekea kwenye eneo la mnada wa Buzirayombo unapotarajiwa kujengwa mnada mkubwa wa upili ambako alioneshwa kuridhishwa na usanifu wa michoro inayoonesha namna mnada huo utakavyokuwa baada ya kukamilika kwake.
"Lakini pia nimeona eneo hili la mnada litakuwa linajumuisha pande mbili zinazotenganishwa na barabara hivyo Mkurugenzi kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo (TBA) ni lazima muangalie namna ya kufanya ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama wakati wote wakiwa kwenye eneo la mnada" Aliongeza Prof. Ole Gabriel.
Pia alipendekeza kutokana na michoro ya mnada huo kuonesha ni wa kisasa ni lazima kuwe na mfumo mzuri wa matangazo ndani ya eneo la mnada, kituo kizuri cha Polisi kitakachofanya kazi kwa saa 24, Mfumo wa kibenki na huduma za afya zitakazowanufaisha wananchi wote watakaokuwa karibu na eneo hilo la mnada, Runinga kubwa itakayoonesha kila kinachoendelea Mnadani hapo na mfumo mzuri wa kuhifadhi idadi na aina ya bidhaa na huduma zinazopatikana mnadani hapo ili kuwe na utaratibu wa kupata taarifa zote muhimu ndani ya muda mfupi
Kwa upande wake Meneja wa TBA Mkoa wa Geita Mhandisi Gladys Jeffa aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ushirikiano Mkubwa iliowaonesha mpaka sasa ambapo aliahidi kufanya kazi nzuri itakayokamilika kwa wakati.
"Tunataka kuhakikisha mpaka kufika mwisho wa Mwezi Mei tuwe tumekamilisha na kuwasilisha hii hatua ya michoro yote ya mnada huu na tunataka kabla ya kuvuka mwaka huu wa fedha mkandarasi awe site" Alisisitiza Mhandisi Jeffa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Bw. Leonard Mwaisabula alisema mradi huo kwao una manufaa makubwa kwa sababu utaongeza kiasi cha makusanyo ya fedha za ndani na hivyo kuiwezesha Halmashauri kuboresha miundombinu ya huduma mbalimbali za jamii kama vile Elimu na afya.
Pierre Liquid (Peter Mollel ) akutwa na Virusi Vya Corona
Msanii wa Maigizo na Mchekeshaji ‘Pierre Liquid’ amethibitisha kuwa na virusi vya corona vinavyosababisha homa kali ya Mapafu
Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti la Mwanaspoti Pierre amesema kwa sasa yupo hospitali ya Amana akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.
Akieleza namna alivyogundulika kuwa ana corona,amesema hii ni baada ya kwenda kupima wiki iliyopita hospitali ya Temeke.
“Nina bosi wangu wa karibu ambaye kapata ugonjwa huu na kwa kuwa mara nyingi tuko naye alinishauri na mimi nikapime kwa nia njema ili kama ninao nipate matibabu mapema na kuepuka kuwaambukiza wengine.
” Hivyo nilienda hospitali ya Temeke, wakanipima ndipo nilipokutwa ninao na kuletwa hapa Amana ambapo kwa sasa ni moja ya kituo cha wagonjwa,”amesema Pierre.
Alipoulizwa anadhani ni wapi kaupatia, amesema “Huu ugonjwa mimi nitakuwa nimembukizwa nikiwa baa hakuna sehemu nyingine kwa kuwa ndio maeneo yangu ya kujidai,”.
Source : Mwanaspoti
Waliofariki Kwa Virusi Vya Corona Marekani Wafika 40,565
Ripoti ya kutoka Chuo kikuu cha Johns Hopkins imesema kuwa takriban kesi za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani imefikia 764,265 huku idadi ya vifo ikiwa ni zaidi ya 40,565.
Barani Afrika, kesi za maambukizi zimefika 21,317 pamoja na idadi ya vifo 1,080 mpaka kufikia leo Aprili 20.
Barani Afrika, kesi za maambukizi zimefika 21,317 pamoja na idadi ya vifo 1,080 mpaka kufikia leo Aprili 20.
Mbali na hizo takwimu duniani kote inakdiriwa kuwa na kesi 2,408,304 zilizothibitishwa huku waliopona wakikadiriwa kufikia 629,066 na vifo vikikadiriwa kufikia 165,105
Watu 16 wauawa katika shambulio la risasi Canada
Watu 16 akiwemo Ofisa wa polisi mwanamke wameuawa katika shambulio la risasi lililoendeshwa na mtu mwenye silaha katika kijiji kidogo cha Nouvelle-Écosse, Mashariki mwa Canada, kabla ya kudhibitiwa na polisi.
Haya ni mauaji mabaya kuwahi kutoka nchini Canada tangu miaka thelathini iliyopita.
Kwa muda wa saa 12 za makabiliano, polisi ilizingira kituo cha mafuta, na mshambuliaji anadaiwa kuwa ameuawa, huku shambulio la muuaji huyo likigharimu maisha ya watu 16.
Ofisa wa polisi mwanamke mwenye miaka 23 ya uzoefu ni miongoni mwa watu waliouawa.
Sababu za mshambuliaji Gabriel Wortman, 51, kutekeleza shambulio hilo hazijajulikana bado.Mshambuliaji alitumia gari linalofanana na magari ya polisi
Haya ni mauaji mabaya kuwahi kutoka nchini Canada tangu miaka thelathini iliyopita.
Kwa muda wa saa 12 za makabiliano, polisi ilizingira kituo cha mafuta, na mshambuliaji anadaiwa kuwa ameuawa, huku shambulio la muuaji huyo likigharimu maisha ya watu 16.
Ofisa wa polisi mwanamke mwenye miaka 23 ya uzoefu ni miongoni mwa watu waliouawa.
Sababu za mshambuliaji Gabriel Wortman, 51, kutekeleza shambulio hilo hazijajulikana bado.Mshambuliaji alitumia gari linalofanana na magari ya polisi
Wawili Wafariki Dunia Kahama Wakituhumiwa Kuwa Ni Wezi
SALVATORY NTANDU
Wanaume wawili ambao hawajafahamika Majina wala Makazi wenye umri kati ya 20-25 wanaodhaniwa ni wezi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamepoteza Maisha wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji kahama baada ya kushambuliwa na watu wenye hasira kali baada ya kuwakamata wakiwa na mali zinazodaiwa kuwa ni za wizi.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa Aprili 20 mwaka huu na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba imesema kuwa tukio hilo limetokea jana katika Mtaa wa Majengo baada ya kukamtwa na wananchi wakiwa na Televisheni (1)aina ya Tandar na Radio (1) ya Subwoofer mali ya Ayoub Kingi mkazi wa mtaa huo ambazo wanatuhumiwa kuziiba.
“Watu hawa walikamatwa na wananchi wakiwa wamebeba mali hizo zenye thamani ya shilingi laki 345,000 na kisha kushambuliwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali za miili yao na wananchi waliojichukulia sheria na kisha kupelekwa katika hospitali ya Mji kahama na walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu,”alisema Kamanda Magiligimba.
Kamanda Magiligimba alisema kuwa Chanzo cha tukio ni hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi baada ya kuwatuhumu watuhumiwa kuwa ni wezi na juhudi za kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo zinaendelea.
TANZIA: Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto Getrude Rwakatare Afariki Dunia
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto (Mikocheni B Assemblies of God ) Mchungaji Dkt.Getrude Rwakatare amefariki dunia Alfajiri ya leo.
Kwa mujibu wa mtoto wake Muta Rwakatare amesema marehemu alikuwa akisumbuliwa na Presha.
"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.
"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Muta.
Sunday, 19 April 2020
Katibu Mkuu aipongeza Muhimbili kubuni vazi la wataalamu kujikinga na virusi vya Corona
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainab Chaula ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ubunifu wa kushona vazi (PPE) kwa ajili ya Wataalamu wa Afya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona wakati wa kutoa huma kwa wagonjwa.
Dkt. Chaula ametembelea kiwanda kidogo cha kutengeneza mavazi hayo na kuona jinsi yanavyotengenezwa na kuwashauri MNH waendelee kuzalisha mavazi mengi ili kutosheleza mahitaji ya Wataalamu wa hospitali hiyo.
“ Leo nimekuja hapa kuwatia moyo kwa kazi kubwa mnayoifanya. Sisi Kama Serikali tunaichukulia Kama jambo jema hasa kipindi hiki cha mapambano ya COVID-19,” amesema Dkt. Chaula.
Katibu Mkuu, Dkt. Chaula ameiagiza Muhimbili kupeleka vazi Hilo katika mamlaka za kuthibitisha ubora wake ili vazi hilo lianze kutumika rasmi na wataalamu.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai amesema ameishukuru Serikali kwa kutambua ubunifu wa mavazi hayo na kwamba wataongeza juhudi kutosheleza mahitaji ya Wataalamu.
Dkt. Swai amesema gharama za kutengeneza vazi moja si kubwa kwani wametumia shilingi 30,000 ukilinganisha na vazi lililothibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo moja linagharimu shilingi 350,000.
“ Vazi lililothibitishwa na kupitishwa kutumika na WHO ni shilingi 350,000 hadi shilingi 550,000, inategemea umelinunua kutoka nchi gani, “ amesema Dkt. Swai.
Amesema ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, imewatia moyo kwani ameona jinsi mafundi wanavyotegeneza vazi hilo kwa ustadi wa hali ya juu na hivyo huwezi kuona tofauti kati ya vazi lililothibitishwa na WHO na vazi lililotengenezwa na MNH.
“ Katibu Mkuu ameagiza tumpelekee mavazi manne pamoja na Lile lililothibitishwa na WHO ili apeleke Shirika la Viwango Tanzania (TBS), TMDA na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili kuthibitishsha Viwango,” amesema Dkt.Swai.
Wenye Virusi Vya Corona Nchini Kenya Wafika 270....Ni Baada ya Wengine 8 Kuongezeka Leo
Fisi Ajeruhi Watu Wawili Kahama Mkoani Shinyanga
Wakazi wawili wa Kijiji cha Ngogwa halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga wamenusurika kuuawa baada ya kushambuliwa na Fisi wakati wakijaribu kumfukuza fisi huyo aliyekuwa amevamia kundi la mbuzi katika kijiji hicho.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Aprili 19, 2020 Afisa mtendaji wa Kata hiyo Upendo Shirima alisema tukio hilo limetolea leo saa mbili asubuhi ambapo Fisi huyo alivamia zizi la Mbuzi kabla ya wananchi kuanza kumpiga na ndipo alipowajeruhi sehemu za mikononi wananchi hao ambao wamepelekwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama kwa matibabu.
Aliwataja walioshambuliwa Fisi huyo kuwa ni Pamoja na Donald Simoni (27) na Furaha Ngusa (46) na ameiomba Wizara ya Maliasili kutenga siku maalumu ili kwenda kuwawinda fisi hao ambao wamekuwa ni wengi kwa wakati huu.
“Tunaomba tu watu wa maliasili watusaidie kufanya oporesheni juu ya wananyama hao maana kutokana na mvua hizi Maji yameingia kwenye mapango yao hali ambayo inawafanya waje kwenye makazi ya watu”alisema Shirima.
Alisema kuwa watu wameanza kupata hofu kutokana na wananyama hao kuanza kuvamia nyakati za mchana kwani walizoea kuwaona wakivamia mifugo wakati za usiku.
Diwani wa Kata ya Ngogwa Kamuli Mayuga alisema baada ya kuwafikisha hospitalini wamepatiwa matibabu kwa kushonwa nyuzi kwenye majereha na kuruhusiwa kuerejea nyumbani huku akiwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari.





































