Thursday, 16 April 2020

MWILI WA MWANAHARAKATI WA HAKI ZA WATU WENYE UALBINO JOSEPHAT TORNER WAZIKWA MKOANI SIMIYU

Mazishi ya Mwili wa Mwanaharakati wa kutetea Haki za watu wenye ualbino Josephat Torner Nkwabi (42) yamefanyika leo mchana Alhamis Aprili 16,2020 katika kijiji cha Mwamwenge kata ya Imalamate wilaya ya Busega mkoani Simiyu alikozaliwa.

Josephat Torner Nkwabi amefariki dunia Siku ya Sikukuu ya Pasaka Aprili 12,2020 majira ya saa mbili usiku baada ya kugongwa na Hiace 'Daladala' akivuka barabara jijini Mwanza .



Share:

Serikali yazindua mpango maalumu wa kutoa elimu ya afya Dar es Salaam

Serikali imezindua mpango maalumu wa kutoa elimu ya afya kwa umma katika Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kuwapo kwa ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Corona ikiwa ni mwendelezo wa kuwafikia watu wengi katika ngazi ya mtaa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizundua mpango wa elimu ya afya kwa umma kwa siku 20 ambao utaongozwa na vikundi vya kijamii kwa kushirikiana na Red Cross chini ya Wizara ya Afya.

Waziri Ummy amesema lengo la kuzindua mpango huo ni kukata mnyororo wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona Kati ya mtu na mtu kwa kutumia vikundi vya kijamii ambavyo vitaelimisha na kutoa taarifa sahihi kwa Jamii kuhusu ugonjwa wa Corona.

“Vikundi hivi vya kijamii, vitashirikiana na Wizara ya Afya na Red Cross na UNICEF kutoa elimu ya afya kwa umma.

Magari 18 yatatumika kwa siku 20 na yatakwenda katika maeneo ya masoko, stendi za mabasi na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri amefafanua kuwa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, vikundi vya kijamii vitakwenda katika maeneo ya nyumba za ibada kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kutoa elimu ya afya kutokana na kuwapo kwa ongezeko la ugonjwa wa Covid-19.

“Niwatoe hofu Watanzania, tutashinda hii vita endapo kila mmoja katika Jamii atazingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri amesema mbali ya Elimu ya afya kutolewa katika Mkoa wa Dar es Salaam, pia vikundi vya kijamii vitakwenda katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza na Arusha kwa ajili ya kutoa elimu ya afya kwa umma kuhusu kujikinga na maambukizi ya ugonjwa Corona.

“Serikali inawashukuru Watanzania kuhusu suala la kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, wameelewa, wamepokea hili vizuri sana, hata katika ngazi ya Kijiji nje ya nyumba wameweka ndoo ya maji na sabuni, kwa hili tunawashukuru Sana Watanzania na tunawatia moyo wa kuendelea kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni,” amesema Waziri.

Waziri amewasisitiza Watanzania kuepuka mikusanyiko na misongamano ili kukabiliana na ugonjwa huo Kama walivyofanya kwenye hatua ya kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Elimua ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya, Dkt. Ama Kasangala amesema atahakikisha elimu kwa Jamii inatekelezwa ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini.

“Nitashirikiana na Red Cross na wenzangu wa kitengo cha elimu ya afya kwa umma ili kuhakikisha Mipango ya utoaji wa elimu kwa wananchi inatekelezeka,” amesema Dkt. Kasangala.


Share:

Wananchi Waaswa Kutochoka Kusafisha Mikono Kwa Sabuni Na Maji Safi Yanayotiririka ili Kukabiliana na Virusi Vya Corona

Na WAMJW- Tunduma Songwe
Kaimu Meneja wa forodha Mikoa ya Songwe na Mbeya Ndg. Anangisye Mtafya amewataka Wasafiri na wafanya biashara wa maeneo ya mipakani kutochoka kusafisha mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka wakati wote ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Ameyasema hayo leo wakati akipokea vifaa vya kunawia mikono vilivyo tolewa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau wa Project CLEAR katika ofisi za forodha zilizo katika mpaka wa Tanzania na Zambia Tunduma Songwe.

“Kunawa mikono ndio silaha yetu kubwa, ambayo tunajivunia, maji safi yanayotiririka na sabuni ndio silaha kubwa, nawa ukiwa nyumbani, nawa ukiwa katika biashara zako, nawa ukiwa kazini, nawa nawa nawa,” alisema

Aliendelea kusisitiza kuwa, baadhi ya silaha za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huu haziitaji pesa nyingi ili kupambana nao, huku akisisitiza watu kuacha tabia za kusalimiana kwa kushikana mikono katika maeneo yote ya kazi, mtaani na majumbani.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima ameeleza kuwa, zaidi ya watu 121,000/ wamepoteza maisha kutokana na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona, na kuweka wazi kuwa zaidi ya watu 1,900,000/ wakiwa na maambukizi ya ugonjwa huo.

“Zaidi ya watu 1,900,000 Duniani wameambukizwa na virusi hatari vya Corona, na kati ya hao watu 121,000 wamepoteza maisha, huu ni ugonjwa ambao unaua kwa idadi kubwa sana, toka tuanze karne ya hii ya 21 hakuna ugonjwa ambao umeua watu wengi kwa muda mfupi kama Corona ” alisema

Aliendelea kusema kuwa, Wataalamu wa masuala ya Afya wanashauri kuwa, kila mtu ahakikishe anasafisha mikono angalau sio chini ya mara 14 kila siku, ili kuviangamiza virusi vya ugonjwa wa Corona endapo vitakuwa katika mikono muda wowote.

“Tunasema angalau katika siku moja, unawe mikono yako sio chini ya mara 14, hii itasaidia kuacha mikono yako safi na salama muda wote” alisema

Nae Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya Serikali na raia wote katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona, huku akiwaasa wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali katika kujikinga, ikiwemo kuepuka msongamano maeneo yote, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka.

Uhamasishaji huu unafanywa kupitia kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR kwa kushirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery unaendelea katika Mkoa wa Songwe, kisha kuelekea Mkoa wa Rukwa.


Share:

Corona Yasababisha Wafanyabiashara Kuchelewa Kuagiza Sukari Kwa Wakati, Serikali Yaingilia Kati Yatatua Changamoto Hiyo

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imewahakikishia watanzania kuwa hakuna upungufu wa sukari Tanzania hivyo wananchi hawapaswi kuwa na wasiwasi wa aina yoyote ile.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo Jijini Dodoma leo tarehe 16 Aprili 2020 wakati akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa bei ya sukari.

Amesema kuwa kila mwaka serikali imekuwa makini katika kutathmini mahitaji ya sukari kwa wananchi kadhalika uwezo wa viwanda vya ndani katika uzalishaji.

Bashungwa amesema ni kweli bei ya sukari imepanda lakini haisababishwi na upungufu wa sukari bali imesababishwa na waagizaji kushindwa kuagiza kwa wakati kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu unayosababishwa na kirusi cha Corona.

Ili kukabiliana na kadhia hiyo serikali imetoa vibali vya jumla ya Tani 40,000 kwa kampuni 4 za wazalishaji ambapo kila kampuni imeagiza Tani 10,000

Waziri Bashungwa amesema kuwa tayari sukari iliyokwisha ingia bandarini kupitia kampuni ya Kagera Sugar ni Tani 9,990 na imeanza kutolea bandarini tangu jana jioni.

Kadhalika tarehe 24, 28 na 30 kampuni ya Mtibwa Sugar itaingiza jumla ya Tani 10,000. Kampuni ya Kilombero Sugar itaingiza jumla Tani 1,624 hivi karibuni kutoka Malawi na Msumbiji huku Tani 1,800 ikiagizwa kutoka Afrika Kusini.

Sambamba na hayo amesema kuwa wiki ya kwanza ya mwezi Mei  Kampuni ya Kilombero Sugar itaingiza Tani 7,276 huku tarehe 15 Mei kampuni ya TPC itaingiza Tani 5,000 na Tarehe 30 Mei Tani 4,500 zitaingia nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amesema kuwa Wizara inatarajia kuomba nyongeza ya Tani 58,000 ili kukidhi mahitaji ya sukari kufikia Juni 2020

Hata hivyo amesema kuwa Asilimia 80% ya sukari ambapo kwa mujibu wa Takwimu mahitaji ya sukari inayotumiwa majumbani ni kiasi cha Tani 4,700,000 ambapo kati ya hizo Tani 378,000 zinazalishwa nchini.

Bashungwa amesema kuwa Hiyo ni hatua kubwa kwa nchi na serikali katika mkakati wa kuimarisha uchumi wa viwanda huku wawekezaji wengi wakiendelea na mchakato wa uongezaji tija na uwezo wa uzalishaji

Kadhalika wakulima wamekuwa na mtazamo mkubwa katika kuzalisha miwa kwa wingi ambayo wataipeleka katika viwanda vya kuchakata sukari na Katika kipindi cha hivi karibuni serikali itafikia uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo kuwa na ziada ya skari itakayouzwa nje ya nchi.

MWISHO


Share:

RC Wangabo awatahadharisha vibarua wa miradi ya serikali juu ya Corona

Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewatahadharisha mafundi na vibarua wa mradi wa ujenzi wa vihenge unaojengwa na serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kuwa makini na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona kwa kufuata maelekezo ya wataalamu afya wawapo katika eneo la kazi na wanaporudi kwenye familia zao.

Amesema kuwa afya ya kila mmoja ni muhimu kutokana na mchango wake katika kujenga nchi na hivyo kuwataka kuwa makini kwa kunawa kila mara hali iliyopelekea kumuagiza meneja wa mradi huo kwa niaba ya Wakala wa majengo nchini (TBA) Mhandisi mkazi Haruna Kalunga kuhakikisha eneo hilo la kazi kunakuwa vifaa vya kutosha vya kunawia maji na sabuni kwa kukanyaga kwaajili ya wafanyakazi na kuondoa ndoo zilizopo ambazo koki zake hazina usalama.

“Afya yako ni ya Msingi sana, na familia yako na sisi sote kwa ujumla wake, kwa maana wewe mtu mmoja ukiugua Corona utaweza kuusambaza kwa watu wengi sana, na wote hapa mnaweza mkafutika ndani ya wiki moja tu, sasa mtakuwa mmeiweka nchi mahali pabaya na mradi wenyewe utasuasua, kwahiyo mjihadhari na ugonjwa huu hatari wa Corona, lakini mchape kazi msiogope kuchapa kazi,” alisema.

Aidha, alitoa pongezi kwa mkandarasi wa mradi huo Unia araj kutoka nchini Poland kwa kusaidiana na mkandarasi mzawa Elerai kutoka Arusha pamoja na meneja wa mradi huo TBA pamoja na mafundi wa mradi huo kwa kufanya kazi ndani ya wakati mbali na hali ya hewa kutokuwa Rafiki kwa ujenzi huo na hivyo kuwataka kuongeza kasi ili kukamilisha ujenzi huo ifikapo tarehe 9.3.2021.

“Ningependa ratiba hiyo izingatiwe, tusirudi nyuma tuongeze kasi kwa kiwango ambacho mradi huu tunataka umalizike mapema, utakuwa na manufaa makubwa sana kwasababu uwezo wa kutunza nafaka zetu kimkoa utaongezeka kutoka tani 30,500 za sasa mpaka kufika tani 55,500 utakuwa ni uwezo mkubwa, kwahiyo hata wakulima wetu watahamasika kulima mahindi zaidi wakijua kwamba NFRA itaweza kuyanunua na kuyahifadhi kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi,” Alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa TBA Mhandisi Mkazi Haruna Kalunga alisema kuwa ujenzi huo utajumuisha majengo 13 ambapo ujenzi wa vihenge 6 vikubwa na vihenge 2 vidogo pamoja na miundombinu yake itachukua asilimia 70 ya mradi huku asilimia 30 ikibebwa na majengo saidizi.

“Kuna Jengo la utawala, kuna jengo la kupikia na kulia chakula, kuna jengo la kutunzia vifaa na dawa, kuna jengo la maabara kwaajili ya upimaji wa hizo sampuli ambazo zitakuwa zinaingia hapa, kuna vihenge 6 vikubwa na vihenge vidogo kwaajili ya usafi vyenye jumla ya tani 20,000 na pia tuna ghala la kuhifadhia mazao lenye uwezo wa kubeba tani 5,000,” alisema.

Kwa mkoa wa Rukwa mradi huo utagharimu Dola za Kimarekani 6,019,399.00 wakati mkandarasi huyo akifanya kazi katika mioa mingine ya Manyara na Katavi ambapo jumla ya gharama yake ni $20,280,906.00 ambapo hadi sasa mkandarasi huyo ameshalipwa $ 10,175,714.22.


Share:

Wagonjwa Wote Na Wanaokwenda Kuwaona Wagonjwa Moi Watakiwa Kuvaa Barakoa (Mask)




Share:

Wenye Virusi Vya Corona Zanzibar Wafika 24....Ni Baada ya Wengine 6 Kuongezeka Leo

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya 6 wa virusi vya Corona, idadi inayofanya kufikia wagonjwa 24 visiwani humo.




Share:

Finance & Administrative Manager Job at Jane Goodall Institute

Finance & Administrative Manager Job at Jane Goodall Institute Job Description Organization Overview: Founded in 1977, the Jane Goodall Institute (JGI) USA is an international non-governmental organization that continues Dr. Goodall’s pioneering work on chimpanzee ecology and behavior. Its mission is to promote wildlife conservation, in particular chimpanzee sustainability, through research, education, and community conservation. The breadth of… Read More »

The post Finance & Administrative Manager Job at Jane Goodall Institute appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Manager, Bancassurance Vacancy at Stanbic Bank Tanzania Limited

Manager, Bancassurance Overview Job ID: 48396 Job Sector: Banking Country: Tanzania Region/State/Province/District: Dar es Salaam Region Location: Dar es Salaam Job Details Bancassurance Job Purpose Primarily to manage and grow the Bancassurance department by acquiring new customers and servicing current customers in a profitable manner. To increase the penetration of the Bancassurance solutions into the bank customer base… Read More »

The post Manager, Bancassurance Vacancy at Stanbic Bank Tanzania Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Country Director at BBC Media Action

Country Director   Location: Dar es Salaam, Tanzania Reports to: Regional Director, Africa (based in London) Contract duration: 36 months (with the possibility of extension) BBC Media Action in Tanzania BBC Media Action is currently implementing several multi-year projects in Tanzania addressing themes such as gender equality, civic engagement, responsible parenting and humanitarian response. We do this by combining… Read More »

The post Country Director at BBC Media Action appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head, Business Banking Job at Stanbic Bank Tanzania Limited

Head, Business Banking Overview Job ID: 48398 Job Sector: Banking Country: Tanzania Region/State/Province/District: Dar es Salaam Region Location: Dar es Salaam Job Details Retail & Business Banking Job Purpose Provide a sales and professional financial advisory service function to the branch based banking market, increasing market penetration through the management of a portfolio of accounts and proactively identifying… Read More »

The post Head, Business Banking Job at Stanbic Bank Tanzania Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Resource Mobilizer and Grants Manager at Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT)

Resource Mobilizer and Grants Manager at Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT)   Vacancy: Resource Mobilizer and Grants Manager Ref: 2020-01 Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT) is a locally registered organisation first established in 1994. It is the largest indigenous provider of ophthalmic and rehabilitation services in the country. CCBRT aims to be the leading… Read More »

The post Resource Mobilizer and Grants Manager at Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Senior Technical Specialists – Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity at Tetra Tech International Development Services

Tetra Tech International Development Services (https://ift.tt/2xle9Na), headquartered in Arlington, VA is currently accepting expressions of interest from qualified candidates for various senior technical specialists to provide technical and managerial oversight for the anticipated 5-year USAID-funded Tuhifadhi Malias Deadline Date: Saturday, 09 May 2020 Organization: Tetra Tech Country: United Republic of Tanzania ili Activity (TMA). The USAID Tuhifadhi Maliasili… Read More »

The post Senior Technical Specialists – Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity at Tetra Tech International Development Services appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Chief of Party- Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity | Tetra Tech International Development Services 

Tetra Tech International Development Services (https://ift.tt/3epyyqL headquartered in Arlington, VA is seeking to hire a qualified Chief of Party to lead all technical and administrative aspects of an anticipated 5-year USAID-funded biodiversity conservation initiative. The purpose of the activity is to support and strengthen capacity in Tanzania for biodiversity conservation in a manner that i) increases private sector engagement… Read More »

The post Chief of Party- Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity | Tetra Tech International Development Services  appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Director of Administration and Finance – Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity at Tetra Tech International Development Services

Tetra Tech International Development Services (http://www.tetratech.com/intdev) headquartered in Arlington, VA is currently accepting expressions of interest from qualified candidates for various senior technical specialists to provide technical and managerial oversight for the anticipated 5-year USAID-funded Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA). The USAID Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA) is anticipated to be a five-year contract to address dynamics that threaten habitat connectivity and… Read More »

The post Director of Administration and Finance – Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity at Tetra Tech International Development Services appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Knowledge Management and Learning Lead- Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity

Tetra Tech International Development Services (https://ift.tt/1JGwAiR), headquartered in Arlington, VA is currently accepting expressions of interest from qualified candidates for a potential Knowledge Management and Learning Lead position on the USAID funded Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA). The USAID Tuhifadhi Maliasili Activity (TMA) is anticipated to be a five-year contract to address dynamics that threaten habitat connectivity and the long-term presence of… Read More »

The post Knowledge Management and Learning Lead- Tanzania Tuhifadhi Maliasili Activity appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

ALIYEPIGA SIMU KWA WAZIRI WA AFYA AKIDANGANYA ANA UGONJWA WA CORONA AKAMATWA SHINYANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba 
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mussa Jackson Kisinza, (25) mkazi wa kijiji cha Mwakitolyo namba 02 wilaya ya Shinyanga kwa  kutoa taarifa ya uongo kwa kumpigia simu na kumdanganya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuwa ana ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba baada ya kijana huyo kutoa taarifa kuwa ana ugonjwa wa Corona timu ya madaktari inayotoa huduma eneo la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (vijijini) kuhusiana na ugonjwa wa Covid 19 ilifika eneo la kijiji cha Mwakitolyo namba 02 ili kutoa huduma kwa mtu huyo lakini mtu huyo alizima simu yake na kusababisha timu hiyo ya madaktari kushindwa kumpata hivyo kusababisha taharuki. 

“Hivyo Aprili 15,2020 majira ya saa moja kamili asubuhi kikosi kazi cha askari wa makosa ya kimtandao walifika eneo la Mwakitolyo namba 02 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Mussa Jackson akiwa anaendelea na shughuli zake za machimbo na kumfikisha zahanati ya kijiji cha mwakitolyo namba 02”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Timu ya madaktari ilimfanyia vipimo vya awali vya magonjwa nyemelezi yanayoashiria kuwepo kwa uwezekano wa mtu kuwa na ugonjwa wa Covid 19 lakini hakuwa na dalili za magonjwa hayo”,ameongeza Kamanda Magiligimba. 

Amesema baada ya kuhojiwa mtuhumiwa amekiri kutoa taarifa hiyo na kwamba baadaye aliamua kuiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja vunja. 

“Natoa wito kwa wananchi kuacha masihara juu ya ugonjwa Covid 19 na mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo juu ugonjwa huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger