Wednesday, 15 April 2020

ANUSURIKA KUFA KWA KIPIGO AKITUHUMIWA KUIBA NDOO YA KUNAWA MIKONO KUJIKINGA CORONA SHINYANGA MJINI

Mmoja wa wananchi akimdhibiti "kibaka" asikimbie baada ya kudaiwa kuiba ndoo ya maji kwa ajili ya kunawa mikono ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona. (Picha na Suleiman Abeid, Timesmajira, Shinyanga)

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

KIJANA mmoja mjini Shinyanga ambaye hakufahamika jina wala makazi yake mara moja amenusurika kufa baada ya kushambuliwa kwa kipigo na wananchi wenye hasira akituhumiwa kuiba ndoo inayotumika kwa ajili ya watu kunawa mikono kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambalo limetokea maeneo ya mjini kati leo saa 2.20 asubuhi, kijana huyo anadaiwa kuiba ndoo hiyo kwenye moja ya vibanda vya mama Lishe maeneo ya mtaa wa Ikelenge mjini Shinyanga.

Mashuhuda hao wamefafanua kuwa, wakati akielekea maeneo ya Soko Kuu la mjini Shinyanga kwa ajili ya kutafuta mteja wa kumuuzia ndoo hiyo, mmiliki wake alibaini kuibiwa ndoo hiyo na kuanza kumfuatilia huku akiomba msaada kwa baadhi ya wananchi waliokuwa maeneo ya viwanja vya ofisi za CCM ambao walimuona na ili kujihami, alianza kukimbia akiwa na ndoo aliyoiba na kuingia ndani ya eneo la Soko Kuu la mjini Shinyanga.

Akiwa katika harakati za kujinusuru na kipigo, aliamua kukimbilia ndani ya jumba la wauzaji wa nafaka mchanganyiko ambapo alidakwa na wafanyabiashara na kulazimika kuitupa chini ndoo hiyo huku akijitetea kwa bidii kwamba yeye siyo mwizi lakini watu wenye hasira walimuadhibu kwa kipigo lakini alipopata upenyo aliwatoroka na kukimbilia mtaani.

Baada ya kukimbia, watu wenye hasira walimkimbiza huku wakimshambulia kwa kutumia mawe na fimbo lakini baadaye walipomkamata, waliamua kumpeleka kituo cha Polisi ili kunusuru asiuawe na watu hao.
Share:

Manager, Client Coverage Job opportunity at Stanbic Bank Tanzania

Job Details Client Coverage – Corporate & Investment Banking Job Purpose Define and execute strategic client plans that will ensure the development of strong business relationships and the delivery of profitable and integrated Standard Bank products and services, with the purpose of ensuring client profitability, increased revenue, risk optimisation and consistent service delivery. Client strategic plan development &… Read More »

The post Manager, Client Coverage Job opportunity at Stanbic Bank Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wagonjwa Wapya Sita (6)wa Corona Waongezeka Zanzibar Na Kufikia Wagonjwa 18






Share:

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI ILIYOSABABISHA VIFO 18 PWANI




Share:

AJALI YA COASTER,LORI YAUA WATU 18,KUJERUHI 15 PWANI


Watu 18 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahwewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo iliyohusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster imetokea leo Jumatano Aprili 15, 2020 asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

Amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15 na majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.
Share:

Procurement Officer at International Rescue Committee Kibondo, Tanzania

Requisition ID: req8826 Job Title: Procurement Officer Sector: Supply Chain Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: No Location: Kibondo, Tanzania Job Overview Job Description The Procurement Officer is responsible for the efficient coordination and management of procurement functions for IRC’s office. The position holder will procure Program supplies, services and equipment, whilst ensuring good practices and maintaining audit-compliant records. You will… Read More »

The post Procurement Officer at International Rescue Committee Kibondo, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Country Manager at Infobip Dar es Salaam, Tanzania

Company Description At Infobip we dream big. We value creativity, persistence and innovation, passionately believing that it is through teamwork that we can all reach greater heights. Since 2006, we have been innovating at the edge of technological possibilities and are now shaping global communications of the future. Through 60+ offices on six continents, Infobip’s platform is used… Read More »

The post Country Manager at Infobip Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Individual Consultancy at UNICEF Tanzania-Value of Neonatal Life in Mbeya and Kaskazini Pemba Regions, Tanzania

Individual Consultancy -Value of Neonatal Life in Mbeya and Kaskazini Pemba Regions, Tanzania Job no: 530571 Position type: Consultancy Location: Tanzania,Uni.Re Division/Equivalent: Nairobi Regn’l(ESARO) School/Unit: United Republic of Tanzania Department/Office: Dar Es Salaam, United Rep. of Tanzania Categories: Child Protection, Health, Monitoring and Evaluation, Planning, Social and Economic Policy, Statistics and Monitoring, Programme Management Apply now UNICEF works in some of the world’s toughest places,… Read More »

The post Individual Consultancy at UNICEF Tanzania-Value of Neonatal Life in Mbeya and Kaskazini Pemba Regions, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Education Officer Job at International Rescue Committee Kasulu, Tanzania

Education Officer Job at International Rescue Committee Kasulu, Tanzania Requisition ID: req8823 Job Title: Education Officer Sector: Education Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: No Location: Kasulu, Tanzania Job Description Background The International Rescue Committee (IRC) responds to the world’s worst humanitarian crises and helps people to survive and rebuild their lives. Founded in 1933 at the request of Albert Einstein,… Read More »

The post Education Officer Job at International Rescue Committee Kasulu, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Project Leader / Deputy Chief of Party – Tanzania PS3+ at Abt Associates Dar es Salaam, Tanzania

Organization Overview The International Development Division focuses on improving the lives and economic well-being of people in lower and middle-income countries. We command technical expertise in health, agriculture, climate change, food security and governance—as well as in international evaluation. Our multi-layered health portfolio includes policy, health promotion and disease prevention, health finance, and health systems management. In partnership… Read More »

The post Project Leader / Deputy Chief of Party – Tanzania PS3+ at Abt Associates Dar es Salaam, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

SUA EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: MIZENGO PINDA CAMPUS-KATAVI & SUA MAIN CAMPUS-MOROGORO

EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: MIZENGO PINDA CAMPUS-KATAVI & SUA MAIN CAMPUS-MOROGORO The Management of Sokoine University of Agriculture (SUA) invites suitable qualified Tanzanians to apply for positions of Assistant Lecturers and Tutorial Assistants. All applications should be addressed to the Deputy Vice Chancellor (Administration and Finance), P.O. Box 3000, CHUO KIKUU, MOROGORO two weeks from the date of this advertisement. The application letters should indicate… Read More »

The post SUA EMPLOYMENT OPPORTUNITIES: MIZENGO PINDA CAMPUS-KATAVI & SUA MAIN CAMPUS-MOROGORO appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano April 15





















Share:

Tuesday, 14 April 2020

SHULE ZOTE NA VYUO KUENDELEA KUFUNGWA TANZANIA...SHEREHE ZA MUUNGANO NA MEI MOSI ZAAHIRISHWA KUKABILIANA NA CORONA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SHULE ZOTE NA VYUO KUENDELEA KUFUNGWA – MAJALIWA
*Sherehe za Muungano, Mei Mosi zaahirishwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.

 

Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima, hivyo maeneo hayo yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia majumbani kwao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameagiza sh. milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia, Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema elimu ya tahadhari ni muhimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. “Kama si lazima kutoka, wananchi waendelee kutulia majumbani mwao.”

Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kusimamia utoaji wa elimu ya kujikinga na virusi hivyo hasa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ikifuatiwa na Zanziba. “Ni muhimu wananchi wake wakapewa tahadhari juu ya namna ya kijikinga.”

Waziri Mkuu ameagiza kuwa wataalamu wanaosimamia utoaji wa huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wa watu wenye maambukizi ya COVID-19, wakiwemo madaktari wote wapewe vifaa vya kijikinga ili kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema watu waliokutana na wagonjwa waendelee kufuatiliwa kwa umakini na wahusika wawashirikishe viongozi wote hadi wa ngazi za chini na kwamba athari za kiuchumi zinazojitokeza kufuatia ugonjwa huo ziendelee kuchambuliwa.

Machi 17, 2020 na Machi 18, 2020, Serikali ilitangaza kuzifunga shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu kwa muda wa siku 30 na kwamba wanafuzi wa kidato cha sita waliopaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 nao wangepaswa kusubiri Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri Mkuu pia alisisitiza kuwa mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo ya lazima imesitishwa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli nyingine za kijamii. 

Alizitaka wizara na taasisi zizitishe semina, warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini ambayo inahusisha washiriki toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi makubwa, wanashauriwa wasitishe safari hizo,” alisisitiza.

Akielezea hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA,                      
JUMANNE, APRIL 14, 2020.
Share:

NHIF TANGA WATOA HUDUMA NJE YA OFISI KUKABILIANA NA CORONA

 MENEJA WA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Senkrani Mohon Singh aliyefika kwenye ofisi zao kupata huduma za bima ambapo kwa sasa wanatoa huduma zao nje ya ofisi ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusuanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.
 MENEJA WA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimsikiliza mmoja wa wateja wao leo wakati wakitoa  huduma nje ya ofisi zao ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusuanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.
 MENEJA WA Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akimsikiliza mteja wao kama alivyokutwa leo
 Huduma zikiwa zinaendelea kwenye ofisi za nje kama inayoonekana huku wateja wengine wakiwa foleni


Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga Mrisho Mponela akiendelea na kazi nje ya ofisi zao

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga imelazimika kuhamisishia ofisi nje ili kuweza kutoa huduma kwa wananchi wanaokwenda ikiwa ni sehemu ya kupunguza mkusuanyiko na kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambao kwa sasa unaitikisa dunia.

Blog ya Kijamii ya Malunde 1 Blog ililishuhudia baadhi ya huduma zikitolewa nje ya ofisi na wananchi wakiendelea kupata huduma mbalimbali ambapo Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu alikuwa akiongoza zoezi la kusikiliza wateja.

Akizungumza na Meneja wa NHIF Mkoa wa Tanga Ally Mwakababu alisema kwamba dhamira kubwa ni kuonyesha jamii juu ya kujali na kupambana na ugonjwa wa Corona lakini pia kuwasiliana na wateja wao kwenye eneo lenye nafasi kubwa kwenye hewa kuliko kufanya kazi kwenye ofisi ambapo wanakuwa wamejifungia.

Alisema hapo kila mtu anakaa kwenye nafasi yake kwa mita mbili na mita moja na nusu kati ya mtu na mtu na mazingira salama na wanapata hewa nzuri kutokana viti kuwa mbalimbali ili kuweza kuwafanya wateja kuwa kwenye mazingira mazuri ikiwemo eneo ambalo watu wananawa mikono kwa kutumia sanitize ambayo kila anakuja kuhudumiwa anapatiwa.

Alisema kwamba wao kama mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kiio kwa na kuonyesha kuitikia mwito wa serikali kupitia Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwamba suala la ugonjwa wa Corona sio la utani tena ni lazima lichukuliwe kwa umakini mkubwa.

“Hivyo kutokana na hilo na ndio maana tumeamua kutoa ofisi nje kwa lengo la kuweza kuwasiliana na wateja wetu kwenye eneo kubwa na kila mtu anakaa kwa nafasi kwa mita mbili au moja na nusu lakini mazingira salama huku kila mtu anayekwenda kuhudumiwa lazima anaweze kunawa mikono kwa kutumia Santinze”Alisema Meneja Mwakababu.

Hata hivyo alisema kwamba pamoja na kuendelea kutoa huduma mbalimbali lakini eneo kubwa ambalo wanalihimiza ni mpango wa toto afya kadi ambao unawawezesha watoto kuweza kunufaika na matibabu pindi wanapokuwa wakiugua hivyo wameendelea kulihamasisha kwenye maeneo mbalimbali.

Meneja huyo alisema kwamba dhamira kubwa ya mfuko huo ni kuhakikisha inawafikia wananchi wote kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ili waweze kujiunga nao na hatimaye kuweza kunufaika na huduma za matibabu pindi wanapokuwa wakiugua.
Share:

Wagonjwa Wa Corona Nchini Kenya Wafika 216....Ni Baada ya Wengine 8 Kuongezeka Leo

Idadi ya waathirika wa Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 216, baada ya hii leo kuthibitisha visa vipya nane, ambapo watano ni raia wa Kenya na watatu ni raia kutoka Mataifa mengine.


Share:

Rais Yoweri Museveni Wa Uganda Aongeza Siku Zingine 21 Za Wananchi Kubaki Majumbani Mwao Ili Kukabiliana Na Corona

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza siku nyingine 21 kuanzia kesho April 15 hadi April May 05,2020 za Watu kuendelea kubaki nyumbani na kutofanya shughuli ambazo zilipigwa marufuku hapo awali ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Mpaka sasa watu 54 wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi hivyo na kati yao wanne wamepona. Hakuna kifo kilichoripotiwa kufikia sasa.

Machi 31, Museveni alitangaza marufuku ya watu kutokutoka nje kwa siku 14, ambazo zilikuwa zinaisha leo Aprili 14.

Hii leo, Museveni amesema bado wanahitaji muda zaidi wa kupambana na virusi hivyo na watu waendelee kusalia majumbani mwao.

“Kwakuwa tumeongeza siku 21 za kubaki nyumbani, tutaendelea kugawa chakula kwa makundi mawili, wale ambao walikuwa wanategemea pato la siku kuendesha maisha na wale ambao hawawezi kujitafutia chakula (walemavu, Wazee nk), wenye mishahara kila mwezi hii misaada haiwahusu”- Amesema Museven


Share:

Sudan Kusini yakumbwa na mlipuko wa Homa ya Manjano

Shirika la Afya Dunia (WHO) limetangaza mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Manjano Kusini mwa Sudan Kusini, katika eneo la Kajo-keji, mkoa unaopakana na Uganda.

WHO imetahadharisha kuwa uwezekano wa ugonjwa huo kusambaa kwa watu wengi ni mkubwa kutokana na kurejeshwa nchini humo kutoka Uganda watu walioyakimbia makazi yao.

Aidha, udhaifu wa sekta ya afya nchini humo, marufuku ya kusafiri uliyowekwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, na mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zinatoa mazingira rafiki kwa mbu wanaosambaza ugonjwa huo kuzaliana, zimetajwa kuwa ni sababu zinazoweza kuchangia kusambaa kwa Homa ya Manjano.

Wizara ya afya nchini humo kwa kushirikiana na WHO imetangaza kuzindua kampeni ya kutoa chanjo kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika, na kuanzisha mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapatiwa chanjo ifikapo 2022.

Mei 2003 Sudan Kusini ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo, ambapo visa 178 viliripotiwa na kupelea vifo 27 katika Mkoa wa Imatong.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger