Monday, 13 April 2020

Buyer at Airtel

Buyer Airtel Tanzania PLC is looking for a suitable  candidate  for the Buyer Position .The incumbent will be responsible for executing procurement activities in the best practice and be a link between supplies and internal customers, while ensuring value for company money spend.Key deliverables;1. Ensure right price and good quality of products2.Procure from the right vendor/Supplier3.Ensure that customers get… Read More »

The post Buyer at Airtel appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAMLILIA JOSEPHAT TORNER

Josephat Torner enzi za uhai wake


SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI MSIBA WA JOSEPHAT TORNER

Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mdau wa haki za watu wenye ualbino Josephat Torner (40) ambaye amefariki dunia Aprili 12,2020 kwa ajali ya  gari /kugongwa na Hiace ‘Daladala’ akivuka barabara jijini Mwanza.

Josephat Torner atakumbukwa kwa ushirikiano wake mkubwa SPC na waandishi wa habari kwa ujumla katika kutetea na kulinda haki za watu wenye Ualbino mkoani Shinyanga na maeneo mbalimbali nchini hususani mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ilikuwa inasifika kwa mauaji ya watu wenye ualbino.

SPC imeshiriana na Josephat Torner kutetea haki za Watu wenye Ualbino tangu akiwa Afisa Mahusiano na Habari wa Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS) na hata alipoanzisha Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Utetezi wa haki za Watu wenye Ualbino iitwayo Foundation of Josephat Torner Europe Aid (FOJOTEA) akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa taasisi hiyo tumeendelea kushirikiana naye.

Kupitia taarifa hii Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kinatuma salamu za pole za rambirambi kwa Chama Cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (Tanzania Albinism Society – TAS), Familia ya Josephat Torner na FOTOJOA kwa kumpoteza ndugu Josephat Torner.

Tukiwa wadau wa kutetea haki za Watu Wenye Ualbino,tunasikitika kwa pamoja na ndugu,jamaa na marafiki kufuatia msiba huu mzito.

Bwana alitoa,Bwana ametwaa,Jina la Bwana Lihimidiwe

Imetolewa leo Jumatatu Aprili 13,2020 na:
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC)
Kadama Malunde
Share:

Matarajio ya Hali Mbaya ya Hewa kwa siku Tano zijazo na Athari zinazoweza kutokea




Share:

WAGONJWA WA CORONA TANZANIA WAFIKA 46....NI BAADA YA WENGINE 14 KUONGEZEKA





Share:

Tanzia : MWANAHARAKATI WA HAKI ZA WATU WENYE UALBINO JOSEPHAT TORNER AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI


Josephat Torner enzi za uhai wake

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi wa Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na Utetezi wa haki za Watu wenye Ualbino iitwayo Foundation of Josephat Torner Europe Aid (FOJOTEA) ambaye amewahi kuwaAfisa Mahusiano na Habari wa Chama cha watu wenye Ualbino nchini Tanzania (TAS),Josephat Torner (40) amefariki dunia baada ya kugongwa na Hiace ‘ Daladala’ akivuka barabara jijini Mwanza.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema Josephat Torner amefariki dunia jana Aprili 12,2020 majira ya saa mbili usiku baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T263 CZQ Toyota Hiace Daladala. 

“Josephat Torner mkazi wa Gana Mwanza ambye ni mtu mwenye ualbino aligongwa na Daladala na kufariki dunia katika barabara ya Makongoro eneo la Kifua wazi karibu na Rock City Mall kata ya Kirumba iliyoendeshwa Emmanuel Mwanasalaha”,amesema Kamanda Muliro. 

“Daladala hiyo iliyokuwa inatokea Mjini kwenda Nyakato ilimgonga Josephat Torner ambaye alikuwa akivuka barabra kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine",amesema Kamanda

Kamanda Muliro amesema dereva wa gari hiyo alikimbia na kutelekeza gari na Jeshi la polisi linamshikilia mmiliki wa gari hiyo huku juhudi za kumtafuta dereva wa gari zikiendelea.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu April 13





















Share:

Sunday, 12 April 2020

MAMLAKA YA USALAMA WA ANGA NCHINI TANZANIA YAFUTA SAFARI ZOTE ZA NDEGE ZA ABIRIA ZA KIMATAIFA ILI KUKABILIANA NA CORONA

Mamlaka ya Usalama wa Anga nchini imefuta safari za ndege zote za abiria za kimataifa na kuweka vikwazo zaidi kwa ndege maalum za mizigo zitakazoruhusiwa kutua nchini. Hii ni hatua nyingine ya kupambana na Ugonjwa wa Covid-19.




Share:

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA BORIS JOHNSON ALIYEKUWA AMELAZWA ICU KWA CORONA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoka hospitali baada ya kupona virusi vya corona lakini atapumzika kwanza kabla ya kuanza kurejelelea majukumu yake.

Johnson, 55, alipelekwa St Thomas' hospital, mjini London, Jumapili - siku ya 10 baada ya kupatatikana na virusi hivyo.

Alikuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku tatu kabla ya kurejeshwa kwenye wodi ya kawaida Alhamisi.

Kulingana na taarifa iliyotolewa, Waziri Mkuu ataendelea kupumzika katika makazi ya Chequers.
Idadi ya watu waliokufa kwa virusi vya corona  nchini Uingereza inasemekana kupita 10,000 hadi kufikia Jumapili.


Share:

Kesi ya pili ya kifo cha Ebola yaripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeripoti kesi ya pili ya kifo cha Ebola katika kipindi cha siku tatu baada ya nchi hiyo kupitia muda wa zaidi ya majuma sita bila ya kuripotiwa kesi mpya ya maambuzo ya Ebola.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza habari hiyo na kueleza kwamba, aliyeaga dunia kwa Ebola ni binti wa miezi 11 ambaye anasadikiwa kuambukizwa na mgonjwa aliyeaga dunia kwa maradhi hayo Ijumaa ya juzi huko katika mji wa Beni.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, leo amhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitarajiwa kutangaza rasmi kumalizika kabisa ugonjwa huo katika nchi hiyo ambao umeua zaidi ya watu 2,200.


Share:

Waziri wa Kilimo Awahakikishia Watanzania Mavuno Ya Mazao Yatakuwa Ya Kutosha

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imeendelea kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula ili watu wake wawe na nguvu ya kufanya kazi kufikia uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kauli hii ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Tarehe 11 Aprili 2020 mkoani Songwe wakati akikagua mashamba ya wakulima mashambani.
 
Akiwa katika Kijiji cha Idiwili na Iyula mkoani humo Waziri Hasunga ameridhishwa na hali ya ustawi wa mazao ya wakulima shambani hivyo kuwahakikishia wananchi kuwa kutakuwa na mavuno ya kutosha katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 kwani wakulima wengi wameitikia wito wa serikali wa kuongeza tija na uzalishaji wa mazao.
 
Waziri Hasunga amesema kwa miaka mitatu  sasa serikali ya imeendelea kuhakikisha nchi inazalisha mazao mengi na ya kutosha ya chakula kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wizara ya kilimo na taasisi zake.
 
Alibainisha kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula mwaka 2019 ulishuka ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo nchi ilizalisha tani milioni 16.8 hivyo katika msimu huu wa mwaka 2020 nchi itazalisha mazao ya kutosha na kuwa na utoshelevu mkubwa wa chakula
 
Amewapongeza wakulima nchini kwa kuitikia wito na maelekezo ya serikali katika kuhakikisha uzalishaji nchini unaendelea kuongezeka hususani kwenye mazao ya chakula na biashara.
 
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga ameigiza Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kuhakikisha inaharakisha upatikanaji na usambazaji wa mbolea aina ya UREA ambayo imeadimika kwa wakulima.
 
Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amebainisha mkakati wa serikali wa kuongeza uzalishaji wa zao la Pareto ambapo umeanza mkakati wa makusudi wa kuanzisha shamba la pareto katika Kijiji cha Idiwili Mkoani Songwe kwa ajili ya uvunaji wa mbegu ili kuongeza kiasi cha mbegu kwani idadi ya wakulima inaongezeka kila siku. 
 
Tanzania imejaaliwa kuwa na mifumo mbalimbali ya kilimo yenye misimu ya tabia nchi inayotofautiana na hali za ekolojia ya kilimo inayofaa kwa uzalishaji wa mazao.  Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni pamoja na mahindi, mtama, lulu, mpunga, ngano, jamii ya kunde (hasa maharage), mihogo, mbatata, ndizi mbichi na ndizi za kuiva.  

Vyakula mbalimbali vya biashara vinavyozalishwa ni pamoja na kahawa, pamba, korosho tumbaku, katani, pareto, chai na miwa.

Mbegu za mafuta ni pamoja na karanga, alizeti na ufuta. Kilimo cha bustani hujumuisha mazao kama vile mbogamboga, matunda, maua na viungo vya chakula. Karafuu ni zao kuu la biashara kwenye visiwa vya Zanzibar.


Share:

Dudu Baya Aitwa Tena Kuhojiwa BASATA

Baraza la sanaa Taifa (Basata)  limemuandikia barua  mwimbaji maarufu nchini, Godfrey Tumaini 'Dudubaya' kumuita ili kwenda kujieleza  kutokana na kutumia lugha isiyo ya staha kwenye mitandao ya kijamii.
 
Dudubaya anatakiwa kuripoti keshokutwa Jumanne kwenye ofisi za makao makuu ya Baraza hilo.
 
Mwimbaji huyo ameiposti barua hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kukubali wito huo siku ya Jumanne.


Share:

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya

KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia Pamoja na vifaa vya kutengenezea noti hizo.

Ni kwamba mnamo tarehe 11.04.2020 majira ya saa 00:30 usiku huko eneo la Sokoni, Kata ya Kyela Kati, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.

Jeshi la Polisi mkoani hapa lilimkamata JOHN FRANCIS [22] mfanyabiashara na mkazi wa Olofea – Kyela akiwa na noti bandia dola za kimarekani 09 kila noti sawa na dola 100 kama zingekuwa halali sawa na dola 900 zikiwa na Na. LB399120505B, noti za Zambia Kwacha 40 kila noti sawa na noti za Zambia kwacha 100 kama zingekuwa halali sawa na kwacha 4,000. kati ya noti 20 zina Na. EH122082777 na noti nyingine 20 zina Na. EH122082854.

Wakati huo huo katika misako inayoendelea katika maeneo mbalimbali, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya lilimkamata PETER MWAKAMENYA [37] Mkazi wa Mbalizi akiwa na noti bandia 07, noti 02 Tshs.10,000/= Na.HJ5091884 na Tshs.5,000/= Na.EY2592056, noti 02 dola za Kimarekani 200 Na.LB39120505BBZ kama zingekuwa halali sawa na dola 200, noti 03 za Zambia Kwacha Na.EH122082777, EH12208254, EH122082777 kila moja sawa na Kwacha 100 kama zingekuwa halali sawa na Kwacha 300. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUPATIKANA NA MALI YA WIZI.
Mnamo tarehe 10.04.2020 majira ya saa 11:00 Asubuhi huko Mtaa wa Relini, Kitongoji na Kata ya Bwawani, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ZEZE CHARLES [29] mkazi wa Bwawani akiwa na Pikipiki Na. MC 417 CAR Sinorai, Chasis Na. LD3PCK6J5J2004712 mali ya wizi. Thamani ya Pikipiki ni Tshs. 2,200,000/=. Upelelezi unaendelea.

KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 10.04.2020 majira ya saa 15:30 Alasiri huko maeneo ya sheli ya Tanganyika iliyopo Mtaa wa Sokoni, Kata ya Makongolosi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi waliwakamata KULWA WATSON [42] na STEWARD CHARLES [25] mchimbaji madini wote wakazi wa Makongolosi wakiwa na bhangi kilogramu 03. Watuhumiwa ni wauzaji na watumiaji wa bhangi.


Share:

Tusherekee Pasaka Tukichukua Tahadhari Dhidi Ya Corona: RC Mtaka

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka leo ameshiriki ibada ya Pasaka katika makanisa tofauti mjini Bariadi na kuwasisitiza waumini na wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu kutulia, kuepuka safari zisizo za lazima na kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali.

Mtaka ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akitoa salamu za Pasaka za Mkoa aliposhiriki ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John, Parokia ya Mtakatifu Luka, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Bariadi Mjini na Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania (AICT) leo Aprili 12, 2020.

“Nimeona watu wananawa mikono utaratibu huu usiishie kwenye nyumba za ibada na maeneo ya kutolea huduma, uende mpaka nyumbani,tunapokuwa kwenye nyumba za ibada pia tuzingatie umbali katika ukaaji wetu na wakati wa kupokea huduma za kiroho: pasaka hii tutulie majumbani tuepuke safari zisizo lazima na tufuate maelekezo ya Serikali.” alisema Mtaka.

Aidha, pamoja na kuwasisitiza wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima Mtaka ametoa wito kwa jamii kuona namna ya kuwasaidia zaidi wazee, watoto  na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu kuepuka zaidi mikusanyiko hiyo ili kuwaondolea hatari ya kupata maambukizi kutokana na hali ya kinga zao za mwili.

Katika hatua nyingine Mtaka amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao kujisomea kwa bidii kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona hususani wale wa madarasa ya Mitihani ya Kitaifa kwa kuwa mitihani hiyo bado ipo na itafanyika.

Sambamba na hayo Mtaka amewaasa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutunza chakula ambacho kimepatikana mwaka huu na kutokiuza kwa matumizi ambayo si ya lazima hususani katika kipindi hiki ambacho chakula kinauzwa kwa bei ya chini huku akiwasisitiza kujiunga na Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii ili waweze kupata unafuu katika huduma za matibabu.

Kwa upande wao viongozi wa makanisa akiwemo Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John, Peter Mkunya, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Luka, Martine Jilala, Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha na Mchungaji wa AICT, Amosi Ndaki wamesema wametumia Maadhimisho ya Kufufuka kwa Yesu Kristo(Pasaka) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na Janga la Corona na kuendelea kuwakumbusha waumini kuzingatia maelekezo ya viongozi wa Serikali na wataalam wa afya.

Koga Mihama na George Lyimo ni miongoni mwa waumini waliohudhuria ibada ya pasaka wameishukuru Serikali kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa kujikinga na Maambukizi ya CORONA huku wakitoa wito kwa wananchi wote kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali ili Maambukizi ya Virusi vya Corona yaishe nchini Tanzania.

MWISHO


Share:

Wenye Virusi Vya Kenya Nchini Kenya Wafika 197

Idadi ya visa vya waathirika wa ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 197, baada ya hii leo kutangaza visa vipya sita.


Share:

Watu 20,000 Wafariki Kwa Corona Nchini Marekani

Washington, Watu 1,920 wamekufa nchini Marekani kutokana na virusi vya corona katika kipindi cha saa 24 zilizopita na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza duniani kwa idadi kubwa ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa wa COVID-19

Taarifa iliyochapishwa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins imeonesha idadi ya vifo nchini Marekani imepindukia watu 20,000 ambayo ni kubwa ikilinganishwa na vifo 19,500 vilivyotokea nchini Italia.

Kulingana na takwimu zilizopo, taifa hilo pia linaongoza kwa visa vya maambukizi ya virusi vya corona na hadi sasa kuna idadi ya watu 527,111 waliothibitika kuambukizwa.

Wakati huo huo, idadi jumla ya maambukizi ya virusi vya corona duniani imepindukia watu milioni 1.7 leo, na virusi hivyo tayari vimesababsiha vifo vya zaidi ya watu 107,000 tangu vilipozuka kwa mara ya kwanza nchini China, Disemba iliyopita.


Share:

MCT watoa pole vifo vya wanahabari TBC,...Watoa Tahadhari Ya Corona

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetoa salamu za pole kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayub Rioba, familia nzima ya televisheni hiyo na wafiwa wote kwa misiba ya wanahabari wake.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga ilieleza kuwa Baraza lipo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

Shirika hilo limepoteza wafanyakazi wake watatu katika kipindi cha wiki moja.

==>>Hapo chini ni Taarifa ya MCT
Baraza la Habari Tanzania (MCT) linatoa salamu za pole kwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dr. Ayub Rioba, familia nzima ya TBC, na wafiwa  wote kwa misiba ya hivi karibuni kituoni hapo. Baraza liko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.

MCT inachukua nafasi hii kuwakumbusha viongozi wa vyombo vya habari, wahariri na wanahabari wote kuzingatia mwongozo tulioutoa hivi karibuni kuhusu kujikinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya Corona wakati wakiwa kazini, na jinsi ya kuandika habari za janga hilo kwa weledi.

MCT inasisitiza kuwa janga “limeshaingia chumbani” hivyo ni vyema pale mwanahabari anapojisikia dalili zinazohusiana na maambukizi ya Corona atoe taarifa kwa mhariri wake mara moja na achukue hatua  za tahadhari ikiwemo kutokwenda kazini na kwenda hospitalini au kwenye kituo cha afya mara moja.

Baraza linapenda pia kuwasisitizia viongozi wa vyombo vya habari kuchukua hatua za kuwalinda wafanyakazi wao wote kama inavyoelekezwa na wataalamu wetu.

Tuchukue tahadhari na Mungu atuepushe na madhila zaidi.

Kajubi D. Mukajanga

Katibu Mtendaji


Share:

MKE ALIYEFUKUZWA KWA KUTOMPIKIA MMEWE AMCHOMA KISU MME WAKE SHINYANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Mwanaume aitwaye Mpemba Gamba (48) mkazi wa Uzogole kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga amejeruhiwa kwa kukatwa na kisu ubavuni na mke wake aitwaye Suzana Richard akilazimisha kurudi kwa mumewe baada ya kufukuzwa sababu za kutompikia mme wake. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea Aprili 11,2020 majira ya sita usiku katika maeneo ya Uzogole, Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga. 

“Mpemba Gamba ambaye ni mkazi wa Uzogole akiwa nyumbani alijeruhiwa kwa kukatwa na kisu ubavuni upande wa kulia na mke wake aitwaye Suzana Richard. Chanzo cha tukio ni ugomvi uliotokana na mtuhumiwa kulazimisha kurudi kwa mumewe kwani alifukuzwa siku tatu zilizopita kwa sababu za kutompikia mumewe”,ameeleza Kamanda Magiligimba 

Amesema mtuhumiwa alikimbia mara baada ya tukio hilo juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea na majeruhi alipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga na kuruhusiwa, hali yake inaendelea vizuri. 

“Natoa wito kwa wananchi hususani wanandoa na wote walioko katika mahusiano ya kimapenzi waache kujichukulia sheria mikononi bali wafike polisi ofisi za dawati la kijinsia na watoto pale wanapokuwa na migogoro kwenye ndoa zao kwa msaada zaidi wa kusikilizwa na kupatiwa suluhu ya migogoro yao badala ya kujichukulia sheria mikononi”,amesema.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger