Monday, 14 October 2019

Dawa Komesha Ya Maumbile Madogo , Nguvu Za Kiume Na Magonjwa Mengineyo

*NGETWA MIX*/
√Hii ndio dawa bora ya mitishamba kiboko ya maumbile Madogo(KIBAMIA) Hurefusha na kunenepesha maumbile  mafupi pia  yaliyoingia ndani kutokana na kitambi ama kuathirika na punyeto

*πŸ“ŒSUPER MORINGA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
πŸ”–(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri   ilio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
πŸ”–(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
πŸ”–(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
πŸ”–(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
πŸ”–(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
πŸ”–(3)Ngiri/
πŸ”–(4)Kama umejichua sana punyeto/
πŸ”–(5)Kisukari/
πŸ”–(6)Presha ya kupanda na kushuka/
πŸ”–(7)Vidonda vya tumbo,/
.
Na haya yote husababisha/
πŸ“Kuishiwa kwa nguvu za kiume πŸ“Œ/
. _______________________
Bado hujachelewa dawa hizi ni mpya kabisa  ni tofaut na ulizo wahi kutumia pia zimeonesha mafanikio kwa watu wengi sana/

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
DR .SELEMANI OMARY ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM , PIA UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO  NDANI NA NJE YA NCHI .SIMU NO:/
*πŸ“ž+255788468114*


Share:

Rais Magufuli amkabidhi Naibu Mkurugenzi wa Takukuru ripoti ya miradi 107 yenye Dosari

Rais   Magufuli amemkabidhi naibu mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo ripoti ya miradi 107 iliyobainika kuwa na dosari.

Miradi hiyo ilibainika kuwa na kasoro ilipotembelewa kwa ajili ya kuzinduliwa na kukaguliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofikia kilele chake leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.

Rais Magufuli amekabidhi ripoti hiyo leo katika maadhimisho ya kilele hicho na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere yaliyofanyika mkoani Lindi.

Awali, kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Mzee Mkongea Ally alimkabidhi Rais Magufuli ripoti ya miradi ya Sh90.28 bilioni iliyokutwa na dosari.

“Sogea hapa mbele nikukabidhi ripoti hii, zege halilali. Naikabidhi hii ripoti ukafanye ukaguzi kila ukurasa, kila nukta na ukachambue wale wote wanaohusika wapelekwe mahakamani. Usisite wapeleke mahakamani,” amesema Rais Magufuli wakati akimkabidhi Brigedia  Jenerali Mbungo ripoti hiyo.


Share:

MTOTO AZIKWA AKIWA HAI

Mtoto huyo anapata matibabu hospitalini

Mtoto mchanga wa kike amepatikana akiwa amezikwa hai katika kaburi la kina kifupi kaskazini mwa India, mkuu wa polisi afichua kisa hicho.

Abhinandan Singh amewaambia wanahabari kuwa mtoto huyo alipatikana na mwanakijiji aliyekuwa ameenda kumzika mtoto wake aliyefariki baada ya kuzaliwa.

Mtoto huyo aliyekuwa amewekwa ndani ya chunguu na kuzikwa katika shimo la futi tatu, amekimbizwa hospitali ambako anapokea matibabu.

Polisi imeanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

"Tunajaribu kutafuta wazazi wa mtoto huyo kwani tunashuku huenda hatua hiyo ilifikiwa kutokana na idhini yao," Bw. Singh aliwaambia wanahabari katika jimbo la Uttar Pradesh.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa polisi, mwanakijiji mmoja wlimpata mtoto huyo alipokuwa akifukua kaburi la kumzika mwanawe aliyefariki baada ya kuzaliwa.

"Walipokuwa wanaendelea na shughuli ya uchimbaji kaburi kijiko cha kutoa mchanga katika shimo liligonga chungu kilichokuwa kimezikwa fiti tatu. walilopokitoa walipata ndani kuna mtoto," Bw Singh alieleza.

"Polisi walimpeleka mtoto huyo katika hospitali iliyo karibu ambako anaendelea kupokea matibabu."

Suala La kijinsia nchini India linatajwa kuwa katika hali mbaya zaidi duniani.

Wanawake mara nyingi hubaguliwa katika jamii hukiu watoto wa kike wakichukuliwa kama mzigo wa kiuchumi, hasa katika jamii masikini.

Wanaharakati wa kutetea usawa wa kijinsia wanasema watoto wa kiume wanapendelewa zaidi kuliko wa kike.

Japo mimba za watoto wakike mara nchini hutolewa baada ya wazazi kubaini jinsia ya mtoto kupitia kiliniki zilizopigwa marufuku, visa vya watoto wa kike kuawa baada ya kuzaliwa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.
Chanzo - BBC
Share:

Rais Magufuli Aaahidi Kuendelea Kumuenzi Mwalimu Nyerere

Rais  Magufuli ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere bila uoga wowote kwa kutekeleza mambo mbalimbali ambayo alitamani kuyafanya enzi za uhai wake.

Ametoa ahadi hiyo leo Jumatatu Oktoba 14, alipokuwa akihutubia wananchi katika hafla ya maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru, kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na wiki ya vijana kitaifa inayofanyika katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.

“Serikali ninayoingoza itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa, kuheshimu tunu za mwenge pamoja kuendelea kuwathamini vijana ikiwemo kuwateua kushika nafasi mbalimbali za uongozi na wito wangu kwa vijana watakaoteuliwa kushika nafasi hizo wajitahidi kufanya kazi kwa bidii na uzalendo mkubwa,”.

“Tumejitajidi kumenzi Baba wa Taifa kwa kupambana na vitendo vya rushwa, wizi, ubadhilifu wa mali za umma mambo ambayo aliyachukua enzi za uhai wake na katika hilo tumeanzisha kitengo maalumu cha mahakama cha kushugulikia mafisadi pia tumeondoa watumishi hewa takribani 20,000 na wafanyakazi wenye vyeti vya kughushi takribani 14,000,”

“Ili kuendelea kuenzi mchango mkubwa uliotolewa na Baba wa Taifa hatuna budi kuwafundisha vijana wetu kuhusu mambo muhimu ambayo yalisimamiwa na baba wa Taifa katika uhai wake ikiwemo uzalendo, uaminifu, nidhamu, uchapakazi na moyo wa kujitolea kwani tusipofanya hivyo tutakuwa tumeliangamiza taifa letu kwasababu vijana ni kundi kubwa na ndio viongozi wa leo na kesho,” amesema Rais Magufuli.

Aidha amewataka Watanzania kumuishi Mwalimu Nyerere kwa kutimiza maono yake aliyotamani kuyatimiza, kusimamia miiko ya azimio la Arusha pamoja na kudumisha umoja bila kubaguana kwa dini waka kabila.


Share:

Picha : RAIS MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,KUMBUKIZI YA MIAKA 20 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu Ndugu Mzee Mkongea Ally kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi
leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Jukwaa kuu na viongozi wengine wa kitaifa sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alizoongoza katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Wabunge wa Lindi na Viongozi wengine wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama "Harmonize" ama "Konde Boy" kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine wakiserebuka na Msanii Rajabu Abdul Kahali maarufu kama Harmonize ama Konde Boy kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali
wakati wa sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Vijana wa Halaiki wakijenga maumbo mbalimbali
wakati wa sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Vijana wa Halaiki katika sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Kikundi cha utamaduni cha Dege la Jeshi kikitumbuiza kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14,2019
Wanewnguaji wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT) wakitumbuiza kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019
Msanii wa Kizazi Kipya Kala Jeremiah akitumbuiza kwenye sherehe za Kilele za Mbio za Mwenge, Wiki ya Vijana na Kumbukizi ya Miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere zilizoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Michezo wa Ilulu Mjini Lindi leo Jumatatu Oktoba 14, 2019.PICHA NA IKULU
Share:

62 Merit Scholarship for studies at The University of Dar es Salaam for the 2019/2020 academic year.

62 Merit Scholarship for studies at The University of Dar es Salaam for the 2019/2020 academic year. The University of Dar es Salaam is pleased to announce 62 merit-based scholarships, 52 for undergraduate and 10 postgraduate students (at the Master’s Level) for the 2019/2020 academic year. Successful candidates will register for studies at the University of Dar es… Read More »

The post 62 Merit Scholarship for studies at The University of Dar es Salaam for the 2019/2020 academic year. appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Gender and Micro finance Specialist at Enabel

Vacancy Enabel – Belgian Development Agency Gender and Microfinance Specialist – Kigoma Region. Background of the job position The Belgian Development Agency, Enabel, mobilizes its resources and its expertise to eliminate poverty in the world. ENABEL contributes to the efforts of the international community and works towards a society that provides present and future generations with enough resources to… Read More »

The post Gender and Micro finance Specialist at Enabel appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Job Opportunities at Standard Chartered

Branch Sales and Service Executive – (1900024796) Job: Retail Banking Primary Location: Africa & Middle East-Tanzania-Dar es Salaam Schedule: Full-time Employee Status: Permanent Posting Date: 04/Oct/2019 Unposting Date: 18/Oct/2019 ! About Standard Chartered We are a leading international bank focused on helping people and companies prosper across Asia, Africa and the Middle East. To us, good performance is about… Read More »

The post Job Opportunities at Standard Chartered appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jobs at CRDB Bank PLC, October 2019

CRDB Bank PLC is looking for suitable person to fill a vacant position of Senior Manager; Financial Crime Compliance in the Department of Risk & Compliance at the Head Office, in Dar es Salaam. Senior Manager; Financial Crime Compliance Job Purpose: Support to define the bank’s AML & Sanctions Monitoring strategy and goals across the bank, providing guidance… Read More »

The post Jobs at CRDB Bank PLC, October 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

11 Nurse Midwives Jobs at Ifakara Health Institute

Position: Nurse Midwife (11 Posts) Reports to: Study Coordinator/Supervisor Work station: Simiyu Apply by: October 15, 2019 Institute overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, training and services, the Institute’s work now spans a… Read More »

The post 11 Nurse Midwives Jobs at Ifakara Health Institute appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Field Supervisor at Ifakara Health Institute

Position: Field Supervisor (1 Post) Reports to: Study Coordinator Work station: Simiyu Apply by: October 15, 2019 Institute overview Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, training and services, the Institute’s work now spans a… Read More »

The post Field Supervisor at Ifakara Health Institute appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MREMBO AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI KUPITIA DIRISHANI

Mwanamke mweusi nchini Marekani ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi kupitia dirisha la chumbani kwake Jumamosi asubuhi , baada ya jirani yake kuiomba polisi iangalie hali yake.

Atatiana Jefferson, mwenye umri wa miaka 28, amekuwa akiishi katika makazi ya Fort Worth, mjini Texas na mpwa wake mwenye umri wa miaka minane.

Jirani yake alipiga simu kwa polisi wasio wa dharura baada ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa mlango wa mbele ya nyumba yake ulikuwa wazi usiku.

Polisi wametoa picha za tukio , ambazo zinaonyesha afisa mmoja wa polisi akifyatua risasi dakika chache baada ya kumuona.

Picha hizo zinaonyesha polisi wakisaka makazi yake, baada ya kubaini umbo la mtu kwenye dirisha. Baada ya kumtaka mtu waliyemuona kunyoosha mikono juu, afisa mmoja wa polisi alifyatua risasi kupitia kwenye dirisha la kioo.

Idara ya polisi ya Fort Worth imesema katika taarifa yake kwamba afisa ambaye ni mzungu ''alihisi tisho" wakati alipoamua kumimina risasi.

Polisi huyo amepewa likizo huku uchunguzi ukiendelea , wamesema maafisa wa polisi.

Ufyatuaji huo wa risasi ulitokea majira ya saa nane na nusu usiku kwa saa za Texas.

Ingawa imefanyiwa uhariri video ya tukio inaonyesha maafisa wakijitambulisha kuwa wao ni maafisa wa polisi.

Picha hizo za video hata hivyo hazionyeshi ndani ya makazi , lakini zinaonyesha silaha ambayo polisi wanasema waliipata ndani ya chumba cha Atatiana Jefferson.

Haiko wazi ikiwa Bi Jefferson alikuwa ameshikilia silaha wakati huo, lakini kumiliki silaha ni kinyume cha sheria kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika Texas.

Polisi wanasema maafisa walitoa huduma ya dharura ya matibabu kwa Bi Jefferson kwenye eneo la tukio , lakini alitangazwa kuwa amekufa kwenye makazi yake.

Bi Jefferson mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akicheza michezo ya video na mpwa wake kabla ya kwenda kuangalia ni nini kilichokuwa kinasababisha kelele nje ya dirisha, kwa mujibu wa wakili anayeiwakilisha familia.Polisi wametoa picha ya silaha iliyobainika ndani ya chumba cha Bi Jefferson

"Mama yake alikuwa ameugua sana hivi karibuni , kwa hiyo akitunza nyumba na kufurahia maisha yao ," Wakili Lee Merritt alisema kwenye ukurasa wa Facebook. "Hapakuwa na sababu ya kumuua . Hakuna .Lazima tupewe haki."

Bi Jefferson alikuwa mhitimu wa chuo kikuu ambaye alikuwa akifanya kazi katika duka la mauzo ya vifaa vya maabara , aliongeza.

Ufyatuaji risasi huo umekuja chini ya wiki mbili baada ya afisa wa polisi aliyekuwa katika mapumziko kufungwa kwa kumpiga risasi mwanaume mweusi Bothan Jean, na kumuua katika makazi yake ya Dallas yaliyoko kilomita takriban 55 kutoka eneo la tukio la mauaji ya Bi Jefferson.

Mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic Beto O'Rourke kutoka Texas amezungumzia kujusu kifo cha Bi Jefferson.

"Huku tukiomboleza kifo na wapendwa wa Atatiana, lazima tudai uwajibikaji na ahadi ya kupambana hadi wakati ambapo hakutakuwa na familia inayokumbwa na mkasa kama huu tena ," alituma ujumbe wake katika Twitter.

Chama cha Kitaifa cha maendeleo ya watu wenye rangi (NAACP) kimekitaja kifo cha Bi Jefferson kama "kisichokubalika".

Jirani aliyewaita polisi kwa jina James Smith, mwenye umri wa miaka 62, amesema kuwa binafsi aliangalia nyumba ya muathiriwa kabla ya kuwaita polisi , lakini hakuona kama kulikuwa na mtu ndani yake. but failed to spot movement inside.

"Ninatetemeka. Ninahasira. Nina jazba kubwa .Na ninahisi nikosa langu kwa kiasi fulani " Bwana Smith aliliambia gazeti la Star Telegram kuhusu ni kwanini aliamua kuwaita polisi waangalie hali yake . "Nisingewaita polisi kwa simu angelikuwa bado anaishi ."
Chanzo - BBC
Share:

KUTANA NA MREMBO KIKONGWE

Mrembo wa miaka zaidi ya 70 kutoka nchini Nigeria ameiambia BBC namna anavyotunza mwili wake

Abimbola Olayinka Idowu, ambaye anajulikana kama Segilola Grey, anasema kuwa hana siri yoyote inayomfanya kuendelea kuwa mrembo hata katika umri wake wa uzee.

Mzee huyo anasema kuwa huwa hafanyi chochote cha zaidi zaidi ya kuwa anafanana na mama yake, anakula vizuri na anapumzika.
Miaka mitatu iiyopita anasema kuwa mtoto wake alikuja na wazo la kumtaka awe mwanamitindo kwa kupiga picha cha mavazi mbalimbali.

Bibi huyo anasema kuwa anafurahia kufanya kazi hiyo na anaona kuwa ni jambo zuri kulifanya katika jamii.

Kama yeye mzee ameweza hata akina mama wadogo wanaweza pia, muhimu ni kujitunza na kupumzika vya kutosha.Segilola Grey anapenda kutangaza mavazi zaidi

Mtoto wake mwenye umri wa miaka 29 Tosin Idowu, anasema kuwa mama yake ni mrembo ndio maana aliamua kumtumia katika mradi wake wa picha.

Tosin Idowu a nasema kuwa ni jambo la kipekee kwa mama yake kufanya kazi hiyo na anaona kuwa watu wanampenda na wanapenda kazi yake nchini Nigeria.

Tosin anasema kuwa mpaka sasa hajawahi kupata lawama yoyote kwa kumtumia mama yake kuwa mwanamitindo.
Chanzo - BBC
Share:

Ndege mpya Dreamliner ya ATCL yafanyiwa majaribio Marekani

Ndege  mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Boeing 787-8 5H-TCJ Dreamliner ipo katika hatua za mwisho nchini Marekani kuja nchini, ambako inaundwa.

Jana, ofisa wa kitengo cha habari cha kampuni ya Boeing, Jennifer Schuld alituma picha za ndege hiyo aina ya Boeing 787-8 na kueleza kuwa ipo kwenye majaribio.

“Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania imeanza majaribio ya kuruka leo. Ndege hii 787 inaitwa Rubondo Island,” aliandika ofisa huyo kwenye ujumbe alioutuma kwenye akaunti yake ya Twitter ikiwa sambamba na picha kadhaa za ndege hiyo.


Share:

Mvua Yaleta Maafa Tanga....Watoto Watano Wafariki Dunia, Mamia Wakosa Makazi

Watoto watano wamekufa maji kutokana na mafuriko wilayani Korogwe mkoani Tanga na kufikisha idadi ya waliofariki kufikia 12 mkoani hapa kutokana na mvua.

Aidha, kaya zaidi ya 300 zimekosa makazi kutokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha kwa takribani wiki mbili sasa katika maeneo mbalimbali ya mkoani Tanga.

Pia daraja la Mto Mandera lililopo Kata ya Segera mpakani mwa Wilaya za Handeni na Korogwe mkoani Tanga limekata mawasiliano ya barabara kati ya mikoa mitano ya Tanga, Dar e Salaam, Arusha, Pwani na Manyara na kusababisha magari zaidi ya 200 kukwama kwa zaidi ya saa 36, huku abiria takribani 800 wakilala nje.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Kissa Gwakisa, alisema mafuriko hayo yametokea katika Kitongoji cha Magunga - Mzia Kata ya Foroforo baada ya nyumba iliyokuwa na watu wanane wa familia moja nyumba yao kuanguka nawatoto watano kati yao kusombwa na maji ambapo kati yao miili yote mitano imepatikana.

Kufuatia hali hiyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Korogwe ilifika katika kijiji hicho pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambapo kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kufukua miili ya watoto hao iliyofunikwa na mchanga usiku wa kuamkia jana.

Gwakisa alisema watu 120 ambao makazi yao yamezingirwa na maji wamehifadhiwa katika kambi maalum kijijini hapo, na ametoa tamko la watu kutokurudi katika makazi yao hadi tamko la serikali hata kama hali itarejea kuwa ya kawaida.



Share:

LIVE: Kilele Cha Mbio Za Mwenge Wa Uhuru, Kumbukumbu Ya Baba Wa Taifa Mwalimu JK Nyerere Mkoani Lindi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli anahudhuria maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Wiki ya Vijana Kitaifa katika Uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi


Share:

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA NA DC KOROGWE WATEMBELEA ENEO LA MANDERA KUONA MAFURIKO YALIYOSABABISHA BARABARA KUFUNGWA KWA MUDA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa wametembelea eneo la Mandera linalounganisha wilaya za Korogwe na Handeni na kujionea mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda
Katibu Tawala  wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi (aliyesimama mbele kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi alipotembelea kuona athari za mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa na kusababisha barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya kaskazini kufungwa kwa muda, kulia mbele  ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa. Octoba 13,2019
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa.(Kulia mbele) akiwapa pole wakazi wa wilaya ya Korogwe pamoja na wananchi wote walioshindwa kuendelea na Safari kutokana na maji kujaa katika eneo hilo la Mandera kushoto mbele ni Katibu Tawala  wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
 Hili ndilo eneo la Mandera ambapo daraja lilifungwa kwa muda 
Maji yakiwa yamezidi daraja , ingawa hapa maji yanaonekana kupungua kiasi
Hali ya mafuriko ilivyokuwa katika eneo la Mandera
Mhe. Kissa G. Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe (wa tatu kutoka kushoto) akimonesha jambo Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi walipotembelea eneo la mafuriko.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi akisisitiza  jambo walipotembelea eneo la mafuriko.

Picha na Fredy Njeje - Korogwe

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger