Wednesday, 28 August 2019

Video : MAANDAMANO YA KUSHINIKIZA KUACHIWA KWA NDEGE YA AIR TANZANIA ILIYOKAMATWA AFRIKA KUSINI YAANZA DAR

Umati wa watu umejitokeza leo nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini jijini Dar es Salaam ukishinikiza kuachiwa kwa ndege ya Air Tanzania iliyoshikiliwa nhini Afrika kusini kufuatia kesi ya fidia inayomhusu Bwana Hermanus Steyn wa nchi hiyo na Serikali ya Tanzania.



Ndege hiyo ya ATCL aina ya Airbus A220-300, ilizuiliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg mwishoni mwa wiki iliyopita kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng nchini humo.

Baada ya ndege hiyo kushikiliwa, serikali ilituma jopo la wanasheria nchini Afrika Kusini likiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi kufuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiliwe haraka na kuendelea na safari zake kama kawaida. 




Video kwa hisani ya Azam tv


Share:

Airport Services Agent | Qatar Airways | Zanzibar

QR22059 – Airport Services Agent | Qatar Airways | Zanzibar Qatar Airways Welcome to a world where ambitions fly high. From experienced pilots to dynamic professionals embarking on new careers, Qatar Airways is searching for talented individuals to join our award-winning team. We take pride in our people—a dynamic and culturally diverse workforce is essential to why we… Read More »

The post Airport Services Agent | Qatar Airways | Zanzibar appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Franchise Manager Tanzania -The Coca-Cola Company

Franchise Manager Tanzania Location: Dar-es-Salaam, Dar es Salaam – TW Job ID: R-33078 Time Type: Full time Post Date: 8/27/2019 Post End Date: 8/27/2019 Represents the company to the bottlers in a country or group of countries; manages the day to day operations of the franchise incl. marketing and finance; provides commercial and franchise leadership to bottlers; partners… Read More »

The post Franchise Manager Tanzania -The Coca-Cola Company appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waliosafirisha madini ya Bilioni 2 Walipa Faini ya Milioni 341 Kukwepa Kifungo Gerezani

Madereva wawili na Wafanyabiashara wanne wa Madini ya Dhahahu wamenusurukika kwenda jela miaka 20, baada ya kulipa faini ya zaidi ya Shilingi Milioni 341, baada ya kukiri kosa la kusafirisha la madini ya yenye thmanai ya zaidi ya Shilingi bilioni 2.
 
Katika fedha hiyo wa Mil. 341, kiasi cha Sh.Mil 125 ni faini na Sh.Mil 216.5 ni fidia wanayotakiwa kulipa kutokana na kuisababishia Serikali hasara.

Hukumu hiyo imetolewa na  Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam, Janeth Mtega baada ya washtakiwa hao kwa ujumla wao kukiri makosa yao na Mahakama ikawatia hatiani na kuwahukumu.

Akiwasomea hukumu hiyo Hakimu Mtega amesema washtakiwa kwa pamoja walishiriki genge la uhalifu, kusafirisha madini nje ya nchi, kuuza madini kinyume na sheria, kushindwa kulipa mrabaha na kuisababishia hasara Serikali.


Share:

Waziri Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi Ashiriki Mkutano Wa Mawaziri Wa TICAD Jijini Yokohama, Japan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi  tarehe 27 Agosti 2019 ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Pacifico jijini Yokohama, Japan.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine unatarajiwa kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Azimio hilo litakalowasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaoanza tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019 kwa ajili ya kuridhiwa.

Akifungungua mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Kono Taro amezipongeza nchi za Afrika kwa kupiga hatua katika maendeleo kupitia ushirikiano na Japan na kwamba nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na nchi hizo ili kuziwezesha kufikia malengo ikiwemo mapinduzi ya viwanda.

Mhe. Taro alisema kuwa, ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia mpango wa TICAD umeendelea kuimarika tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 1993 na kwamba ni matarajio yake Mkutano wa Saba utakuwa wa tija zaidi kwa pande hizo mbili.

“Nawakaribisha Mawaziri wenzangu Yokohama ambapo maandalizi ya mkutano wa saba wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika yanaendelea. Jukumu letu ni kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango kazi wake ili hatimaye litunufaishe sote pale litakapopitishwa na Wakuu wa nchi” alisema Mhe. Taro.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. Sameh Shoukry ameipongeza Japan kwa kuendelea kuandaa mikutano hiyo ambayo ina nia ya kuifikisha Afrika katika mapinduzi ya viwanda na kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na umaskini.

Kwa upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ambao ni miongoni mwa waandaaji wa Mkutano wa Saba wa TICAD, Bw. Kwesi Quartey amesema kuwa, mkutano huo unafanyika wakati Umoja wa Afrika unaendelea kutekeleza agenda 2063. Agenda hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuziwezesha nchi za Afrika kufikia maendeleo ya hali ya juu kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, teknolojia na miundombinu.

Kadhalika Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika, Bw. Lamin Manneh alisema kuwa ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia TICAD umekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Bara la Afrika. Aliongeza kuwsema kuwa, Shirika lake ambalo linasimamia maendeleo linaridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya Japan na Afrika ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa.

Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Ushirikiano na Afrika pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

Mkutano huu ambao umewashirikisha Mawaziri kutoka nchi za Afrika, na wadau mbalimbali wa maendeleo unafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama, Japan.



Share:

Katibu Mkuu CCM Dkt. Bashiru ampongeza Askari aliyegoma kutumia salamu ya CCM

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amempongeza askari polisi wa mkoani Pwani ambaye siku za hivi karibuni aligoma kutumia salamu ya ‘Kidumu Chama cha Mapinduzi’ inayotumiwa na chama hicho tawala nchini.

Askari huyo aliombwa kutoa salamu hiyo na mjumbe wa halmashauri Kuu Taifa ya chama hicho, Haji Jumaa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Vianzi wilayani Mkuranga, kabla ya kueleza kero za kufungwa kituo cha polisi muda wa kazi.

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo Jumanne Agosti 27, 2019 katika mkutano wa wanachama wa CCM wilaya ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya ziara yake iliyoanza ya kukagua uhai wa chama, miradi ya maendeleo na kuzindua mashina.

Akitolea mfano wa tukio hilo, Dkt. Bashiru amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kuwa chombo cha nidhamu kwa watumishi wa umma.

“Nampongeza yule askari aliyegoma kufuata maelekezo nataka nimjue hata IGP nilimpigia simu kuhusu tukio hilo. Polisi hapokei maelekezo ya chama chochote cha siasa iwe CCM au CUF. Kama una jambo usibwatuke tu, sitaki kusikia amri au maelekezo yoyote, tukiendelea na tabia hiyo tutakuwa tunajenga nchi isiyofuata sheria,” amesema Dkt. Bashiru.

Amebainisha kuwa watumishi wa umma wana vyombo vyao vya kuwajibishana na wakati mwingine hupeana adhabu.

Hata hivyo, askari huyo aligoma akisema maadili ya kazi yake hayaruhusu kutoa salamu hiyo, akidai ni kosa kimaadili.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano 28 August























Share:

Tuesday, 27 August 2019

Jiji La Dodoma Latia Saini Katika Utekelezaji Wa Miradi Mikubwa Ya Maendeleo Ikiwa Ni Pamoja Na Mradi Wa Dodoma City Hotel

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jiji la Dodoma kwa siku ya leo Agosti 27,2019 limevunja Historia baada ya Kusaini miradi Mikubwa ya Maendeleo itakayokuwa inaratibiwa na jiji hilo.
 
Akizungumza katika utiaji saini wa Miradi hiyo,Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema Jumla ya Miradi itakayotekelezwa ni Saba yenye thamani zaidi ya Tsh.Bil.60 lakini kwa sasa wataanza na miradi miwili yenye thamani ya zaidi ya Tsh.Bil.27.
 
Kunambi ameitaja miradi miwili ya kuanzia  kwa awamu ya kwanza ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa Dodoma City Hotel utakaogharimu Bilioni 9.9  lenye ghorofa 11 na Mradi wa pili ni jengo la Uwekezaji litakalokuwa mji wa Kiserikali litakalogharimu zaidi ya Tsh.Bilioni 18.
 
Aidha,Kunambi amebainisha kuwa utekelezaji wa miradi hiyo,unapaswa kutekelezwa ndani ya Mwaka mmoja kuanzia sasa na Miongoni wa Wabia wa Maendeleo watakaochukua tenda hiyo kuwa ni pamoja na Mohammad Builders LTD na Stecol Corporation huku akiwaasa Wadau wengine wa Maendeleo kuchangamkia Fursa hizo.
 
Katibu tawala mkoa wa Dodoma Kessy Maduka amesema miradi hiyo ni ujenzi wa uchumi wa viwanda wa jiji la Dodoma na linatakiwa liangaliwe katika uwekezaji huku mkuu wa mkoa huo,Dkt.Binilith Mahenge akibainisha kuwa uwekezaji huo unazidi kumuunga Mkono Rais Dokt.John Pombe Magufuli azma ya Makao Makuu na akitoa ombi kwa serikali uboreshaji wa ujenzi wa Shule za Kimataifa.

Kwa Upande wake Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo amesema lengo la Mradi huo ni kutoa unyafuzi wa Mapato ambapo jiji la Dodoma kwa Sasa lina uwezo wa kuwalipa watumishi wake  bila utegemezi wa mfuko kutoka hazina kuu huku akibainisha kuwa ujenzi wa majengo hayo ya kisasa itakuwa ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara.
 
Aidha,Waziri Jafo amewakumbusha  watumishi wa Serikali kufanya Kazi kwa Bidii na kuacha maigizo katika utendaji wa kazi.
 
“Badala ya kufanya kazi watumishi wanajiposti kwenye mitandao ya kijamii wakitaka sifa,hatutaki watendaji wa namna hii”amesema.
 
Hata hivyo ,Waziri Jafo ametahadharisha kwa wakandarasi wazembe na wababaishaji na hawana nafasi katika serikali ya awamu ya tano.
 
Katika hatua nyingine,Waziri Jafo amesikitishwa kutokana na wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kushindwa kutekeleza agizo lake ambapo hivi karibuni alitoa agizo kuwa Wilaya hiyo ilitakiwa iwe imeshakamilisha upimaji wa Maeneo hadi kufikia Julai 30,2019 lakini mpaka sasa maeneo yaliyo mengi hayajapimwa na fedha za upimaji serikali ilishatoa.
 
“Chamwino mnamwaibisha mkuu wa Wilaya,nilitoa maagizo kufikia Mwezi Julai,30,2019 maeneo yote yapimwe wapewe wawekezaji lakini mpaka leo bado.Mnamwaibisha mkuu wetu wa Wilaya ,tena ni eneo la Ikulu sifurahishwi na kitendo hiki.Kwa hiyo nikuagize Dc wa Chamwino uende ukawasimamie wataalam wako na uwachukulie hatua.Maana hakuna kisingizio chochote na Fedha za Upimaji tulishatoa sisi kama serikali.”Amesema Waziri Jafo.
 
Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia , kazi, vijana  ajira,Mhe.Anthony Mavunde amesema katika kutekeleza adhma  ya Serikali ya awamu ya tano ya uwekezaji,mkoa wa Dodoma umeanza  utalii wa Mashamba ya Mizabibu.


Share:

Jela Miaka 30 jela kwa kubaka Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 na kumpa mimba.

NA SALVATORY NTANDU
Mkazi wa kijiji cha Mpunze Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ramadhani Mohamedi (23) amekuhumiwa kwenda jela miaka 30 na Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa kosa la  kubaka na kumpa mimba mwanafunzi (17).

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo Ushindi Swalo na kusema kuwa Mahakama imeridhika na Ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri ambao umemtia hatiani Ramadhani pasipo shaka yeyote.

Amesema Mahakama imepitia ushahidi wote wa upande wa jamhuri na kujiridhisha kuwa anahatia ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi huyo hivyo atatumikia adhabu hiyo ili iwefundisho kwake na kwa watu wengine.

Awali akisoma shauri hilo Mahakamani hapo Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Evodia Baimo amedai kuwa Ramadhani katika kosa la kwanza la ubakaji amekiuka kifungu namba 130 (1) (2) na 131 (1) sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.

Kosa la pili Ramadhani amekiuka kifungu 60 (a) (3) sura ya 353 ya sheria ya elimu ya mwaka 2016 na kuimba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwake ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Ramadhani alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza hoja ambayo imetupiliwa mbali na Mahakama.

Tayari ameshaaanza kutumikia adhabu yake na haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ipo wazi ndani ya siku 60.


Share:

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHE. UMMY MWALIMU , AZINDUA CHAMA CHA UREMBO NA VIPODOZI


Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu alipotembelea moja ya meza za vipodozi lipotemelea meza ya kutengeneza mawigi katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Amesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa ya ini, figo, moyo na saratani ambapo kwa mwaka 2015 wagonjwa wa kansa walikuwa 2416 hadi kufikia wagonjwa 7649 kwa mwaka 2018 na sababu mojawapo inayosababisha ni matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu vikali na amewashauri watengenezaji wa vipodozi kutengeneza mazingira bora ya biashara kwa kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango huku akiahidi ushirikiano katika suala zima la upatikanaji wa masoko.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa ongezeko la wagonjwa wa Kansa kutoka taasisi ya Kansa Ocean road imefikia wagonjwa 7649 mwaka 2018 ukilinganisha na wagonjwa 2416 mwaka 2015.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa chama Cha urembo na vipodozi nchini (TCA), Waziri Ummy amesema kuwa amesukumwa sana mapinduzi yanayofanywa katika sekta ya urembo na vipodozi na amesukumwa zaidi kuhudhuria ufunguzi huo na akiwa mwanamke mwenye dhamana katika Wizara inayosimamia jinsia pia ameona hilo ni jambo jema la kuungwa mkono hasa sekta hiyo inahusisha afya pia.
Waziri Ummy amewapongeza waanzilishi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wao Shekha Nasser kufanikisha kuanzishwa kwa chama hicho na wao kama Wizara watahakikisha wanatengeneza mazingira bora ya biashara ili kuendeleza ujenzi wa viwanda pamoja na kuuza na kufanya biashara nje ya nchi.Vilevile amewashauri Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) pamoja na baraza la taifa la elimu ya ufundi (NACTE) kuweka sehemu ya mafunzo katika sekta urembo katika mitaala ya elimu ili hata watu kutoka nje ya nchi waweze kuja kujifunza masuala ya urembo nchini na kuzidi kuipa thamani sekta hiyo, pia amewahakikishia wanachama hao kuwa serikali itaendelea kukuza sekta hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Vilevile ametoa rai watengenezaji na wauzaji wa vipodozi na urembo kufuata kanuni na taratibu pamoja na kuwashauri watanzania kukitumia chama hicho ili kuwe na sauti moja ya kuwasiliana na kufanya maamuzi kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Awali akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa chama hicho Shekha Nasser amesema kuwa tasnia hiyo inakua haraka duniani, barani Afrika na nchini Tanzania na kwa mwaka 2017 pekee ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 532 duniani huku ikitegemewa kufikia dola bilioni 863 kwa mwaka 2024 kwa ukuaji wa asilimia 7 kwa mwaka.
Amesema kuwa kuanzishwa kwa chama hicho kumelenga kufanikisha malengo mbalimbali yakiwemo kuwaunganisha wadau wote wa sekta ya vipodozi na urembo pamoja na kukusanya maoni na kuyapeleka kwa serikali yakiwa na sauti moja na hiyo ni pamoja na kuendeleza viwanda vidogo, vya Kati na vikubwa na vinachangia sana katika kukuza ajira kwa vijana, kulipa kodi na mapato kwa serikali.
Baadhi ya wadau wa urembo wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa taasisi ya urembo na vipodozi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Shekha amesema kuwa Tanzania inapata asilimia 3 pekee katika soko la dunia huku wanufaika wakubwa wakiwa ni nchi za Afrika kusini, Kenya na Nigeria.

Share:

Ugonjwa wa Zinaa wa Kisonono (gonorrhea) : Dalili Zake, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kujikinga

Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi sana duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono. 

Vitendo hivi vya ngono vinaweza kuwa kujamiana, kupiga denda (kissing), vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral genital sex), kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe kwa mwanamume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators). 

Magonjwa ya zinaa huathiri sana watu walio katika umri wa miaka 15 – 24 lakini hata kwa watu wengine ambao wana umri chini au zaidi ya huu niliotaja pia yanaonekana kwa wingi.

Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya ishirini yanayotambulika duniani, baadhi ya magonjwa ya zinaa ni
  1.  Kisonono (Gonorrhoea – “Gono” kama wengi wanavyopenda kuita kwa kifupi).
  2.     Chlamydia
  3.     Kaswende (Syphillis)
  4.     Human papilloma virus (HPV)
  5.     HIV/AIDS (Ukimwi/Upungufu wa kinga mwilini)
  6.     Hepatitis B, C, A
  7.     Herpes virus
  8.     Trichomoniasis
  9.     Bacteria Vaginosis
  10.     Pubic lice (chawa kwenye nywele za kinena)
  11.     Chancroid
Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba ya uhakika kama HPV, Hepatitis B na C, na HIV. Mengine yameanza kuwa sugu kutokana na matumizi ya dawa za antibiotics bila mpangilio, magonjwa hayo ni kama gono (gonorrhoea) na nk.
 
Visababishi vya magonjwa ya zinaa
  1. Vitendo vya ngono kama nilivyoeleza hapo awali
  2. Kuanza vitendo vya ngono mapema au wakati wa umri mdogo
  3. Kuwa na wapenzi wengi
  4. Kufanya mapenzi ambao sio salama
  5. Maambukizi kupitia michibuko au sehemu zilizokatika kwenye ngozi kwa kugusana na majimaji ya aina yoyote yanayotoka kwa mtu mwenye ugonjwa wa zinaa kama damu, shahawa nk. Hii inaweza kutokea bila mtu kujua kwani mara nyingi dalili za magonjwa ya zinaa zinakuwa hazionekani kwa wanawake na hata baadhi ya wanaume.
Watu wengi huhisi kitendo cha kula denda (kissing) ni salama lakini si kama wanavyofikiria kwani baadhi ya magonjwa kama kaswende, herpes nk, yanaweza kuambukizwa kupitia njia hii. 

Soma pia: Tatizo la Kutokwa na usaha Wakati wa Kukojoa 

Kondomu husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama gono, Chlamydia lakini sio kinga muafaka dhidhi ya magonjwa ya zinaa kama kaswende, genital herpes, genital warts, na magonjwa ya upungufu wa kinga mwilini (AIDS).

Kisonono (gonorrhea) ni nini?
Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi (cervix). 

Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15 – 29, wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 – 24 wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
 
Ugonjwa huu huambukizwa vipi?
Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum). 

Soma Pia: Ugonjwa wa Zinaa wa Kaswende (Syphilis) : Dalili Zake, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kujikinga 

Ugonjwa wa gono huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya kulevya.
 
Dalili za ugonjwa wa kisonono
Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7 baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili ni kama zifuatazo

Kwa wanaume
  1. Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation)
  2. Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana
  3. Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
  4. Maambukizi yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.
Kwa wanawake
Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote
  1. Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
  2. Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu
  3. Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika.
  4. Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa
  5. Kichefuchefu
  6. Homa (fever)
  7. Kutapika
Vipimo vya ugonjwa wa kisonono
  1. Swab for culture – Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono.
  2. Polymerase Chain Reaction (PCR) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.
Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?
Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. 

Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano.

Soma Pia:  Saratani ya tezi dume : Madhara Yake, Dalili Zake, Chanzo na Tiba Yake

Fuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito (mfano doxycyclin). Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za ugonjwa huu.
 
Madhara ya ugonjwa wa kisonono
  1. Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
  2. Huweza kuathiri moyo (heart valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
  3. Madhara kwenye sehemu za maungio au jointi (joint inflammation)
  4. Kwa wanawake wale ambao hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
  5. Wale wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor).
  6. Kwa wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu (blindness), homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).
Kinga ya kisonono
  1. Kutumia kondomu wakati wa kujamiana
  2. Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
  3. Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
  4. Kwa wanawake wajawazito – Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwengine wowote.
  5. Wanawake wajawazito wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha kuwa kipofu.
  6. Epuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono.


Share:

Tatizo la Kutokwa na usaha Wakati wa Kukojoa

Bila shaka wapo wengi ambao wana tatizo kama hili. Naomba tuwe pamoja kwenye makala hii ili ujifunze kuhusu tatizo la mtu kutokwa usaha wakati wa kukojoa.

Tatizo la Kuwepo kwa chembechembe za usaha au usaha kwenye mkojo hujulikana kama pyuria ambapo linaweza kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope) au kama tatizo ni kubwa linaweza kuonekana kwa macho.

Visababishi vya tatizo la Kutokwa Usaha Wakati wa Kukojoa ni nini?

Visababishi vya tatizo hili ni kama vifuatavyo;
  1. Ugonjwa wa mfumo wa mkojo (UTI)-Maambukizi kwenye figo, kwenye mrija wa mkojo na kwenye kibofu cha mkojo (cystitis- amabayo huonekana sana)
  2. Magonjwa ya Zinaa-Kama ugonjwa wa kisonono au ‘’gono’’ kama wengi wanavyoita, ugonjwa wa Chlamydia na Trichomoniasis
  3. Sumu inayotokana na kemikali (Chemical poisoning) kama 4-Aminodiphenyl inayotumika kwenye maabara na kwa ajili ya tafiti
  4. Tatizo linajulikana kama Reiter’s syndrome
  5. Pyelonephritis-Maambukizi ya bakteria kwenye sehemu za figo zinazojulikana kama calyces, renal pelvis na tishu za figo
  6. Madhara ya pyelonephritis ambayo husabababisha ugonjwa unaojulikana kama renal abscess
  7. Maambukizi kwenye tezi dume-Prostatitis (Kwa wanaume)
  8. Upungufu wa kinga mwilini
  9. Mcharuko (Inflammation) kutokana kuwa na mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
  10. Mzio (Allergy) au kuota uvimbe sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo
Viashiria vya tatizo hili ni;
  1. Maumivu makali ya kuchoma (Painful burning sensation) wakati wa kukojoa
  2. Maumivu chini ya kitovu
  3. Homa
  4. Kutapika
Tatizo hii likidumu kwa muda mrefu husababisha kupungua uzito kwa mgonjwa

Vipimo vya uchunguzi
  1. Urinalysis – Kipimo cha mkojo
  2. Urine for culture and sensitivity - Kipimo cha kuangalia bakteria kwenye mkojo
  3. Complete blood count – Kipimo cha kuangalia wingi wa damu na chembechembe za damu (husaidia  kuonyesha kama kuna maambukizi kwenye mwili)
  4. Blood culture - Kuangalia kama kuna maambukizi kwenye damu
  5. Prostate –Specific Antigen (PSA) Test-Kipimo cha tezi dume
  6. Kipimo cha mionzi ya X-ray - Huonyesha kama tatizo ni kubwa sana
  7.  Kipimo cha ultrasound
  8. Kipimo cha CT scan au MRI - Husaidia kuonyesha kama tatizo hili lipo ndani ya tishu za figo  (Intra-renal abscess) au nje ya tishu za figo (Extra-renal abscess)
Vichagizi vya Tatizo la Kutokwa Usaha Wakati wa  Kukojoa (Predisposing Factors)

Vichagizi vya tatizo hili ni;
  1. Kutosafisha vizuri sehemu za siri baada ya kujisaidia haja ndogo
  2. Kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa wowote wa zinaa
  3. Ugonjwa wa kisukari
  4. Madhara yanayotokana na kutumia mpira wa mkojo - Kwa wale wote waliowekewa mpira huu wa mkojo (catheter)
  5. Saratani ya kwenye mfumo wa mkojo au sehemu za siri
  6. Matumizi ya dawa za jamii aina ya Non-steoridal anti-inflammatory drugs (NSAIDS) au madawa yanayopunguza kinga mwilini (Immuno-suppressant medications) kwa muda mrefu
  7.  Kuvimba kwa tezi dume
Matibabu
  1. Tiba hutegemea na chanzo cha tatizo hili
  2. Dawa za kutibu vimelea (antibiotics)
  3. Matibabu ya mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
  4. Kunywa maji kwa wingi mara kwa mara ili kusaidia kutoa chembechembe za usaha kupitia njia ya haja ndogo-Ikumbukwe ya kwamba maji sio tiba
Angalizo:-mgonjwa Atahitaji Kumuona Daktari Ili Apate Tiba Stahiki  Kulingana Na Chanzo Cha Tatizo La Kutoka  Usaha  Wakati Wa Kukojoa


Share:

Bara La Afrika Lataka Kuwezeshwa Kujitegemea

Nchi za Bara la Afrika, Tanzania ikiwemo zimesema wakati umefika sasa kwa Nchi zilizoendelea kuisaidia Afrika kujitegemea na kuliwezesha kutumia rasilimali zake yenyewe kwa maendeleo ya watu wake badala ya kulifanya Bara hilo kama eneo la kupata malighafi ya kuhudumia viwanda vya nchi zilizoendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo baada ya kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Pacifico jijini Yokohama, Japan.

Ameongeza kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine umesisitiza umuhimu ya uwepo wa miundombinu ambayo inaunganisha Nchi za Kiafrika ili kuliwezesha bara la Afrika kuwa na miundo mbinu ya usafirishaji imara na zenye kuleta tija kwa wote.

Aidha Prof. Kabudi ameongeza kuwa ni mkutano huo pia umeazimia kuzitaka nchi zilizoendelea kuongeza fedha zaidi kwa ajili ya kutoa huduma za kijamii hususani katika nyanja za afya hususani katika kupambana na malaria,kifua kikuu na ukimwi sambamba na Afrika kuwajibika kuchukiua hatua zote za kuhakikisha uwepo wa utawala bora,usalama na Amani.

Akifungungua mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Kono Taro amezipongeza nchi za Afrika kwa kupiga hatua katika maendeleo kupitia ushirikiano na Japan na kwamba nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na nchi hizo ili kuziwezesha kufikia malengo ikiwemo mapinduzi ya viwanda.

Mhe. Taro amesema kuwa, ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia mpango wa TICAD umeendelea kuimarika tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 1993 na kwamba ni matarajio yake Mktano wa Saba utakuwa wa tija zaidi kwa pande hizo mbili.

“Nawakaribisha Mawaziri wenzangu Yokohama ambapo maandalizi ya mkutano wa saba wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika yanaendelea. Jukumu letu ni kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango kazi wake ili hatimaye litunufaishe sote pale litakapopitishwa na Wakuu wa nchi” alisema Mhe. Taro.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. Sameh Shoukry ameipongeza Japan kwa kuendelea kuandaa mikutano hiyo ambayo ina nia ya kuifikisha Afrika katika mapinduzi ya viwanda na kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na nyingine nyingi.

Kwa upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamishenii ya Umoja wa Afrika ambao ni miongoni mwa waandaaji wenza wa Mkutano wa Saba wa TICAD, Bw. Kwesi Quartey amesema kuwa, mkutano huo unafanyika wakati Umoja wa Afrika unaendelea kutekeleza agenda 2063. Agenda hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuziwezesha nchi za Afrika kufikia maendeleo ya hali ya juu kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, teknolojia na miundombinu.

Kadhalika Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika, Bw. Lamin Manneh alisema kuwa ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia TICAD umekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Bara la Afrika.

Mkutano wa Saba pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

Mkutano huu ambao umewashirikisha Mawaziri kutoka nchi za Afrika, na wadau mbalimbali wa maendeleo unafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.


Share:

Wimbo wa TETEMA Wa Rayvanny na Diamond Platnumz Wapigwa Marufuku Kenya

Wimbo Tetema wa msanii Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz umepigwa marufuku kupigwa katika maeneo ya wazi  nchini Kenya.

Mbali na Tetema, wimbo mwingine uliopigwa marufuku kupigwa maeneo hayo ni  Wamlabez wa msanii Sailors wa nchini Kenya.


Kiongozi wa  Bodi ya Filamu nchini Kenya (KFCB),  Ezekiel Mutua amesema sababu ya kuzizuia nyimbo hizo  ni  kuwa na maudhui yanayokwenda kinyume na maadili.

"Nyimbo za Tetema na Wamlambez zinazuiwa kuchezwa nje ya vilabu na baa. Inatia aibu kuwaona hata viongozi wa kitaifa wakidensi na kuimba nyimbo za aibu mbele ya hadhara.

"Maneno katika nyimbo hizo ni uchafu na hayafai kusikilizwa hadharani hususan mahali ambapo kuna watoto wanaoweza kuwa wanasikiliza maneno au kuona mtu akicheza. Nyimbo zote mbili ni ponografia halisi ," ameandika bwana Mutua.

"Japo hatuzipigi marufuku kwasababu zinaimbwa kwa mtindo wa mafumbo , ni muhimu kwa umma kufahamu kuwa nyimbo hizi ni chafu, na hazifai kuchezwa mahala penye mchanganyiko wa watu wa rika tofauti. Acha zipigwe kwenye vilabu , kwa ajili ya watu wazima pekee !" aliandika.

Hata hivyo haijafahamika ni vipi agizo la Bwana Mutua litatekelezwa na bodi ya udhibiti wa maudhui ya kiusanii.



Share:

Usisumbuke Tena na Tatizo la Nguvu za Kiume....Soma hii

Super Mkunyati Mix; ni dawa bora ya mitishamba yenye uwezo wa kutibu na kumaliza matatizo yote ya ukosefu wa nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile:-
 
  -kuwai kufika kileleni ndani ya dakika chache tu.
 -Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa muda mrefu.
 -Kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu(punyeto) husababisha kuishiwa au kupungukiwa na nguvu za kiume.

Epuka matatizo haya kwa kutumia dawa bora ya asili ya Super Mkunyati Mix ni kiboko ya matatizo haya yanayowasumbua baadhi ya wanaume wengi.
 
Pia kuna dawa ya kutibu Presha,miguu kufa ganzi, tumbo kuuma chini ya kitovu, kisukari,ngiri, chango aina zote na nk, matatizo haya nayo uchangia matatizo haya ya ukosefu wa nguvu za kiume na kuwa na maumbile madogo na uume mfupi.
 
JABABILA;- ni dawa ya mvuto wa mapenzi ,mchumba, mke, mume aliyekuacha .
 
ITALIGULA;- ni dawa ya biashara  .

Ofisi zetu zinapatikana DAR ES SALAAM, SONGEA - BOMBAMBILI, SHINYANGA - KAHAMA MJINI. na pote pale ulipo utaipata huduma hii,kama huna nafasi utaletewa hulipo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na DR. MACHIMKENDA simu no, 0717 339 771AU 0763 172 670whatsApp 0621998653


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger