Monday, 12 August 2019

Unicef jobs tanzania 2019

Searches all vacancies related to unicef jobs: unicef jobs tanzania 2019, vacancies in embassies in tanzania, unicef tanzania, jobs in tanzania for foreigners, un volunteer jobs tanzania, ngo jobs in tanzania, unicef tanzania jobs 2019, jhpiego tanzania job opportunitiesunicef jobs, unicef current vacancies, unicef jobs for nurses, unicef jobs uk, unicef jobs tanzania 2019, how to work for… Read More »

The post Unicef jobs tanzania 2019 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

International Consultant to Support Training of Women Leaders and Aspirants

Location : Dar es Salaam, TANZANIA Application Deadline : 25-Aug-19 (Midnight New York, USA) Time left : 13d 17h 40m Type of Contract : Individual Contract Post Level : International Consultant Languages Required : English Starting Date : (date when the selected candidate is expected to start) 01-Sep-2019 Duration of Initial Contract : Three (3) months Expected Duration of… Read More »

The post International Consultant to Support Training of Women Leaders and Aspirants appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Programme Specialist, End Violence Against Women and Girls (EVAW/G)

Location : Dar es Salaam, TANZANIA Application Deadline : 26-Aug-19 (Midnight New York, USA) Time left : 14d 17h 46m Type of Contract : FTA Local Post Level : NO-C Languages Required : English Starting Date : (date when the selected candidate is expected to start) 01-Oct-2019 Duration of Initial Contract : One year   Background UN Women, grounded… Read More »

The post Programme Specialist, End Violence Against Women and Girls (EVAW/G) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi za kazi Tanzania Red Cross Society (Chaperones)

Nafasi za kazi Tanzania Red Cross Society (Chaperones) Chaperones (33) Positions Report to: Regional Coordinator. Location– Shinyanga (MC),Shinyanga DC, Kahama TC, Maswa DC, Nzega TC, Nzega DC , Kigoma MC, Urambo TC, Tabora MC, Kaliuwa DC, Musoma MC, Bunda DC, Tarime , Mc, Kasulu Dc, Geita DC TC. Mode of Employment: Temporary Contract for two months Job Summary:  The… Read More »

The post Nafasi za kazi Tanzania Red Cross Society (Chaperones) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Ikupa: Anayepingana Na Magufuli Anapingana Na Mungu Mwenyewe

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu Waziri kutoka   Ofisi ya Waziri mkuu,anayeshughulikia masuala ya watu wenye Ulemavu Mhe.Stella Ikupa  amewataka watanzania kuunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwa ni Pamoja na Kupiga vita Dawa za kulevya na kuwezesha wenye Ulemavu.
 
Mhe.Ikupa amesema hayo  jijini Dodoma wakati akifunga kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania [UWT]Kwa mkoa wa Dodoma.
 
Ikupa ametaja Nyanja mbalimbali ambazo Serikali ya awamu ya Tano imetekeleza ikiwa ni pamoja na kupambana na Dawa za kulevya ambazo zilikuwa zikipoteza vijana na kurudisha nyuma uchumi wa nchi,Uimarishaji wa Miundombinu ikiwa ni pamoja na Umeme,Barabara,Reli,Afya,Elimu bure  na Usafiri wa anga pamoja na uwezeshaji wa Mikopo kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
 
Hata hivyo ,Naibu Waziri huyo amechangia Jumla ya mabati 10 yenye thamani ya Tsh.360,000 Kwa UWT Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi  wa Elimu huku jumla ya Tsh.milioni moja ,laki nane na hamsini elfu zikichangiwa kwenye harambee ya baraza hilo.
 
Kwa upande wao Mjumbe wa Kamati kuu  Hadija Shalo [Keisha] na mjumbe wa Baraza kuu Taifa UWT,Chiku Mugo amempongeza  Rais Magufuli pamoja Naibu Waziri Ikupa Kwa Mchango huo huku wakiwapongeza wadau wengine kwa kuendelea kuiunga UWT Katika kufanikisha miradi mbalimbali ya Maendeleo


Share:

DOMINGOS:Tutaendelea Kuboresha, Kuimarisha na Kuhamasisha Biashara za Mazao ya Kilimo SADC.

NA.Mwandishi Wetu-MAELEZO
SEKRITARIETI ya Chakula, Kilimo na Malisili kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) imesema kuwa itaendelea kufanya kazi karibu na wananchi walioko kwenye ukanda wa Jumuiya hiyo  ili kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya  2015-2020 SADC hasa kwenye Sekta ya  Biashara kwa mazo mbalimbali ya Kilimo na  Mifugo.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Chakula, Kilimo na Maliasili, Domingos Dove alisema kuwa ni vyema kuhusisha vyombo vya habari kwenye sekta hiyo ili kutoa habari zilizohakikiwa, kuona changamoto wanazokumbana nazo, mafanikio  ili kili mmoja ajue sekritarieti inakoenda katika kuimarisha biashara na soko la SADC kwenye mazao ya Kilimo na Mifugo.
 
Alisema kuwa Sekritarieti ina dhamira kubwa ya kutoa wataalamu kwenye kutekeleza sera za Maendeleo za ukanda huo wa Afrika, ili kuhakikisha kunakuwepo na Maendeleo endeelevu kwa nchi wananchama wa Jumuiya hiyo.
 
“Kama Sekritarieti ya SADC tunafanya kazi kubwa kimkakati kwenye nchi wanachama na tunamatarajio makubwa ya kuona na kugusa sehemu zote kuanzia ngazi ya Taifa mpaka ngazi ya kanda na kazi hii inahakikisha kwamba sera zote kwenye nchi 16 za Jumuiya hii zinaunganishwa kisera ili kuwezesha kufanya kazi pamoja, hii ndiyo kazi yetu”, Domingos Gove, SADC.
 
Domingos alisema kuwa malengo ya Sekritarieti hiyo kwa nchi wanachama ni kutangaza, kuunganisha na kuwezesha uunganishwaji wa Sera  na miradi mbalimbali ya Maendeleo miongozi mwa nchi 16 wanachama wa SADC.
 
Domingos alitolea mfano kuwa kama Tanzania itakuwa na program ya Maendeleo kwenye sera ya kilimo, Sekritarieti itafanya kazi ya pamoja na Serikali ya Tanzania ili kuweza kuunganisha sera hiyo kwa nchi zingine 16 za ukanda huo wa afrika.
 
Alisema kuwa katika kutekeleza sera ya Maendeleo SADC, Sekritarieti hiyo inafanya kazi kwenye maeneo mengi yakiwemo, kuimarisha kilimo na uzalishaji wa mazo ya chakula, kuimarisha eneo la kutangaza biashara na kuwaunganisha wananchi kwenye nchi 16 za SADC ili kuweza kupata soko la watu zaidi ya milioni 300.
 
“Tunatakiwa kuwa na uwezo wa kutangaza na kuwahamasisha wananchi katika nchi wanachama wa SADC kuzalisha na kuchangamkia soko la zaidi ya watu 300 na hii ndiyo kazi yetu kama Sekritarieti na tutazidi kutangaza, kuboresha na kuhamasisha biashara miongoni mwa nchi wanachama kwenye mazo ya kilimo na Mifugo, kwa  hiyo wananchi wanatakiwa kuzalisha  kulingana na soko la SADC litakavyokuwa”, Domingos Gove, SADC.
 
Domingos aliongeza kuwa Sekritarieti hiyo inashughulikia pia  masuala ya usalama wa chakula pamoja na lishe bora kwa wananchi kutoka SADC, ili kuwezesha kuwepo na uchumi endelevu katika nchi 16 za Jumuiya hiyo, lengo kuu likiwa ni kuunganisha baadhi ya Sera za Utekelezaji miongoni mwa nchi wanachama.
 
Aidha, Domingos alisema kuwa Sekritarieti hiyo ina jukumu kubwa la kulinda maliasili zilizoko ukanda huo wa afrika na alitolea mfano kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ulinzi wa maliasili ikiwemo wanyama pori.
 
“Tunajivunia kuwa Serengeti na Kilimanjaro zipo kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika SADC na zinawavutia watu wengi kutoka nchi mbalimbali duniani, tunafurahi kuona Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa  kwa kiasi kikubwa kwenye ulinzi wa Maliasili ikiwemo mbuga za wanyama Serengeti na Ruaha”, Alisema Domingos Gove, SADC.
 
Aidha, Sekretarieti hiyo inajukumu la kutekezaji katika  kuangalia mabadiliko ya nachi katika ukanda huo wa Afrika kwani hiyo imekuwa ni changamoto kubwa miongoni mwa nchi wanachama wa SADC.
 
Mwisho.


Share:

Lori lingine la mafuta lateketea kwa moto

Lori  jingine la mafuta aina ya Scania, lenye namba ya usajili T 243 BCU, na tela T 685 DCV mali ya kampuni ya Njombe Filling Station, limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali katika Kijiji cha Ngadinda Halmashauri ya Madaba, Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma (RPC), Simon Maigwa Marwa, amethibitisha tukio hilo.

“Tukio la ajali ni kweli limetokea jana saa nne usiku (kuamkia leo Jumatatu) Songea Vijijini ambapo lori lilikuwa limebeba shehena petroli na likiendeshwa na Hubert Mpete ambaye bado hajajulikana alipo.  Lori hilo liliacha njia na kuingia porini kisha kugonga mti na kuwaka moto,  na kichwa (cabin) kiliungua chote,” alisema Marwa.


Share:

WATU 10 WANUSURIKA KIFO KWA BOTI MMOJA HAJULIKANI ALIPO JIJINI TANGA

WATU 10 wamenusurika kifo mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya boti waliyopanda kuzama kwenye bahari ya Hindi Jijini Tanga wakati wakiwa wanaenda kuangalia visiwa vilivyopo majini.
Akizungumza leo na Malunde Blog Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edward Bukombe alithibitisha kutoka kwa tukio hilo ambapo alisema lilitokea Agosti 11 mwaka ambao walikuwa wamepanda boti waliyokodi kutoka eneo la Yanchi Club.
Alisema kwamba baada ya watu hao kupanda boti hiyo walikuwa wakienda kutembelea visiwa mbalimbali vilivyopo kwenye bahari hiyo na ndipo upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi walipotoka ndipo ilipopinduka na kuwakwaga.
“Watu hao walikuwa wametokea eneo la Yanchi Club walikuwa wanakwenda kwenye kutembelea visiwa mbalimbali vya bahari ya hindi wakati wakiwa njiani upepo mkali uliwazuia kwenda mbele na walipotaka kugeuza kurudi wakapinduka “Alisema
Aidha kamanda Bukombe alisema kwenye boti hiyo iliyokuwa na watu 11 ambapo 10 kati yao waliweza kuokolewa kutokana na kuvaa maboya wakati wakiwa baharini na mwengine mmoja ambaye inadaiwa hakuwa nayo mpaka sasa hajulikani alipo.
“Nitoa wito kwa wananchi wanaotumia bahari kusafiria kuchukua
tahadhari wanapokuwa bahari kwa kuhakikisha wanavaa maboya ya kujiokolea ili wakati yanapotokea majanga kama hayo waweze kuona namna ya kujiokoa “Alisema Kamanda huyo.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu 12 August



























Share:

Sunday, 11 August 2019

'ZOEZI KIKAKA' YAFUNGWA.....WANAJESHI WAJIIMARISHA KULINDA MAPORI KIGOMA

Na Rhoda Ezekiel -Malunde1 blog  Kigoma

Mkuu wa Brigedi ya Magharibi 202 KV,Brigedia jenerali Jackobo Mkunda amewataka Wanajeshi wa Kikosi cha 24 Kj, kuhakikisha wanaendelea kukaa na kukagua ulinzi na usalama katika ofisi zao ambazo ni Mapori ya Mkoa wa Kigoma ili kuhakikisha mpaka wa magharibi unakuwa salama na hauvamiwi na watu waovu.

Wito huo aliutoa jana wakati wa akiahirisha Mafunzo ya siku 13 yaliyofahamika kama 'Zoezi Kikaka', yaliyohusisha kombania kujifunza namna ya kukabiliana na maadui, kuainisha matumizi ya silaha za kivita ,kutathimini utendaji kazi wa silaha za kikosi,kuimarisha utendaji kazi wa kikosi, kuwezesha maafisa kujua matumizi ya silaha za kivita katika nyakati zote na kuwajengea uwezo maafisa wa kutoa amri na matumizi ya redio nyakati za vita.

Alisema zoezi hilo litakuwa endelevu na hawatakubali kuona misitu na mapori yanavamiwa na raia kutoka nje ya nchi, wanaotumia mapori hayo kufanya uharifu na kuwatishia usalama wananchi wa Mkoa wa Kigoma, jeshi litahakikisha linalinda amani na usalama wa maeneo hayo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Brigedia Mkunda alisema ili kuhakikisha Wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli katika adhima yake ya uchumi wa viwanda ni lazima wahakikishe nchi iko salama na wananchi wanafanya shughuli zao bila kuwa na bugha yoyote na kuhakikisha amani inaendelea kuwepo.

"Kazi ya kuhakikisha ofisi zao ziko salama ni haki yao askari wa Jeshi la Wananchi hivyo kuzijua ofisi zao na wanapaswa kuzilinda na kuhakikisha muda wote ziko salama , kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kujiimarisha vizuri zaidi na zoezi hilo ni endelevu nipende kuwahakikishi Wwananchi kuwa eneo hilo ni salama na wafanye kazi kwa uhuru', alisema brigedia Mkunda.

Alisema suala la ulinzi na usalama sio la Jeshi pekee, bali kila taasisi pamoja na wananchi wanatakiwa kuwafichua Watu wote wanaoingia nchini bila vibali na kufanya uharifu pamoja na raia wanaoshirikiana nao katika vitendo hivyo.

Naye Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kikosi 202KV Kanali Wilson Ibuge alieleza kuwa mapori yanapoonekana hayana watu yana mwenyewe na mwenyewe ndiyo Jeshi la Wananchi na zoezi ndiyo kwanza limeanza, kazi ya jeshi ni vita hawapendi vita na iliwaweze kutekeleza vita lazima wajiandae na sehemu pekee ni mafunzo ya kivita na mazoezi.

Alisema matarajio ya brigedi siyo tu eneo la miliki ya kikosi cha 24 kj zoezi hilo ni endelevu na linapeleka salamu kwa wavamizi wa maeneo hayo na wakitaka salama ni kuacha kujihusisha na mambo ya kijangili na uharifu na pamoja na Wananchi wa Tanzania wanaoshirikiana na Warundi kufanya uharifu wote watashughulikiwa ipasavyo.

Aidha kamanda wa kikosi cha 24 KJ Meja Jonson Luhovyq alisema kuwa ndani ya siku kumi na tatu za mafunzo hayo askari wameweza kufanya zoezi hilo katika maeneo ya Malagarasi, Mvugwe, Kagerankanda, Busunzu,Nyarugusu na Kisogo pamoja na maeneo yanayo karibia kambi ya Kanembwa.

Alisema katika zoezi hilo waliweza kubaini baadhi ya raia kutoka nchi jirani ya Burundi, kuwepo katika eneo la mapori hayo wanaojihusisha na uvunaji wa mihogo baada ya hapo wanajihusisha na mambo mengine ya kihalifu.

Alisema watahakikisha wanalinda maeneo hayo pamoja na askari kufanya mafunzo hayo wataweza kushirikiana na Jeshi la polisi kulinda amani ha maeneo ya mpakani, na katika zoezi hilo matokeo makubwa yamepatikana na litakuwa endelevu.

Hata hivyo alisema changamoto waliyonayo ni ukosefu wa mafuta, endapo wakipata lita 300 kila mwezi, wataweza kuendelea na mazoezi hayo katika mapori ilikuhakikisha maeneo hayo yanakuwa salama na hakuna uharifu.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Hanange aliwapongeza askari kwa kazi kubwa walioifanya, na kuswma kwamba poti hilo lazima lilindwe kwa kuwa eneo kubwa la pori hilo ni chanzo cha mto Maragalasi linalomwaga maji katika Ziwa Tanganyika endapo litahaeibiwa litasababisha kuongezeka kwa joto ziwani na kusababisha madhara pamoja na samaki kukimbia.

Alisema serikali ina mpango wa kuboresha bandari ya mkoa wa Kigoma ni lazima zipwa liendelee kulindwa na kuwa la kisasa kwa kuwa bandari inategemea ziwa kazima msitu huo ulindwe, serikali itaendelea kushirikiaka na jeshi kuhakikisha katika mapori hayo hakuna kilimo kinachofanyika wala kuwepo na vitendo vya uharifu.


Share:

Rais Magufuli: Serikali Itagharamia Matibabu ya Waliojeruhiwa Ajali ya Moto Morogooro

Rais Magufuli amesema serikali itagharamia matibabu ya majeruhi wa ajali ya lori lililolipuka na kuwa moto mkoani Morogoro jana Jumamosi Agosti 10.

Aidha, Rais Magufuli pia amewataka Watanzania kutokuwa majaji na wepesi wa kuhukumu bila kufahamu chanzo cha ajali hiyo.

Rais Magufuli amesema hayo leo Jumapili Agosti 11, wakati alipowatembelea baadhi ya majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

“Niwaombe Watanzania tuendelee kuwaombea huu si wakati wa kulaumu kwa sababu nimesikia wengine wanasema walikuwa wameenda kuiba mafuta.

“Tusihukumu bila kufahamu chanzo kwa sababu kuna mmoja amesema alikuwa kwenye lori jingine alivyoona ajali akashuka ili akatoe msaada lakini aliungua, kwa hiyo si wote walikwenda kuiba mafuta wengine walikwenda kutoa msaada.

“Yupo mwingine alikuwa anasema anasafiri kwenda Mtwara wakazuiwa, akaungua. Sisi tusiwe majaji kwa sababu si kila mmoja alikuwa anakwenda kuiba mafuta wengine walikuwa wanapita njia tu,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, akiwa hospitalini hapo Rais Magufuli alipokea taarifa kuwa majeruhi waliofikishwa Muhimbili walikuwa 46 ambapo watatu kati yao wamefariki huku wengine 15 wakiendelea na matibabu mkoani Morogoro.

Rais Magufuli pia amewashukuru madktari na wauguzi hospitalini hapo kwa kuwahudumia wagonjwa hao kwa njia mbalimbali na kuokoa maisha yao ambao wengi wao wameungua vibaya.

“Muhimbili imebadilika sana huduma ni nzuri najua mna changamoto nyingi sana serikali tunatakiwa kuzitatua lakini tunaomba mjitahidi hivyo hivyo,” amesema.

Akiwa hospitalini hapo, Rais Magufuli amewatembelea majeruhi hao na kuwapatia Sh 500,000 kila mmoja na madaktari na wauguzi wanaowahudumia wagonjwa hao.


Share:

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari bin Zuberi Atoa Pole Kwa Wafiwa na Majeruhi Ajali ya Moto Morogoro

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari bin Zuberi ametoa salamu za pole kwa Rais, wafiwa na wote walioguswa na msiba kufuatia ajali ya moto mkoani Morogoro na kuagiza BAKWATA mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano wote utakaohitajika katika kipindi hiki.

Ajali hiyo imetokea jana Jumamosi Agosti 10, 2019   baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.

Wakati huohuo, Sheikh Abubakari bin Zuberi  amesema swala ya sikukuu ya Eid Agosti 12,kitaifa itaswaliwa katika kiwanja cha Masjid Kibadeni Chanika ikifuatiwa na baraza la Eid na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo.


Share:

Waziri Mkuu Aunda Tume Kuchunguza Ajali Ya Morogoro

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameunda tume maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali ya moto iliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 69 hadi mchana huu na wengine 70 kujeruhiwa wakati wakichota mafuta yaliyokuwa yakimwagika baada ya lori la mafuta kupinduka, mjini Morogoro.

“Hii tume inaanza kazi leo (Jumapili, Agosti 11, 2019), Hadi ijumaa inipe taarifa yake na hata kama mimi sijawajibika initaje. Ajali ya namna hii si mara ya kwanza ilitokea Mbeya eneo la Mbalizi. Naomba niwasihi Watanzani pale gari linapoanguka tusitume kama fursa twende tukaokoe binadamu waliopo pale”.

Waziri Mkuu ameunda tume hiyo leo (Jumapili, Agosti 11, 2019), wakati akizungumza na waombolezaji waliofika katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao. Niko mbele yenu nikimwakilisha Rais Dkt. John Magufuli aliyenituma kuja kuungana nanyi kwenye siku hii ya huzuni”.

Waziri Mkuu amesema lazima wajiridhishe kama Serikali ilitekeleza vizuri jukumu lake kwa sababu ajali imetokea saa mbili asubuhi katikati ya mji, hivyo tunataka kujua ajalj ilipotokea kila mmoja alitumiza jukumu lake.

Amesema ajali imetokea karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi na kuna polisi sasa je hawa wananchi waliopata ajali walienda na madumu ya kuchotea mafuta inamaana waliamka asubuhi wakijua ajali itatokea. “Najua pale ajali inapotokea trafiki wana wahi haraka hata kama kwa gari la kukodi. Watu walikuja na madumu, wengine kuchomoa betri nani aliwazuia.Je lilipoanza kuungua gari la zima moto lilikuja kwa wakati gani”.

Waziri Mkuu amesema lazima wajiridhishe ndani ya Serikali kama wamewajibika. “Kuna vitu vingi lazima tuviangalie tujue nani hakutimiza majukumu yake. Nadhani ujumbe mnaupata si vyema tutakimbilia vitu badala ya watu. Tunasikitika sana kwa yaliyotukuta hata upande wa Serikali tunasikitika kuwapoteza Watanzania”.

Pia, Waziri Mkuu amezungumzia kuhusu jitihada za kuokoa waliopata majeraha kwamba zinaendelea vizuri na jukumu lao kubwa kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani na pia wawaombee wajeruhi waweze kupona.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Magufuli tayari ameshatoa kibali cha kutolewa fedha kwa ajili ya kununuliwa vifaa tiba na dawa zinazohitajika.

Akizungumzia kuhusu idadi ya vifo na majeruhi waliotokana na ajali hiyo ambayo inatangazwa kupitia vyombo mvalimvali vya habari, Waziri Mkuu amesema ni vema takwimu hizo wakaacha zikatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Stephen Kebwe.

“Kwenye vyombo vya habari tuelewane kwenye takwimu za vifo na majeruhi. Msiseme suala la takwimu anayetoa ni Mkuu wa Mkoa na matukio haya yapo chini yake. Nimeamua kusema hivi hizi takwimu zikitajwa nyinginyingi mnajenga hofu na taharuki kwa wananchi. Hili halikubaliki mkitaka taarifa mtafuteni mkuu wa mkoa”.

 Wakati Huo huo, amesema Rais Dkt. Magufuli alipokea taarifa mapema ya ajali ya lori la mafuta na kusababisha vifo vya Watanzania 69, ambapo alimtaka aende mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwasilisha salamu za pole kwa wananchi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla kufuati tukio hilo la kuhuzunisha.

Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anawaombea marehemu na majeruhi lakini pia amawataka wafiwa na wananchi wote wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na wapendwa wao.
 
“Mheshimiwa Rais amehuzunishwa sana na msiba huu ndio maana amenituma nilete ujumbe huu kwenu.Lakini pia nimekuja na salamu za pole kutoka kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. Jambo hili si dogo ni kubwa kwani tumepoteza ndugu zetu wengi. Kwa idadi hii kubwa ya ndugu zetu waliotangulia mbele za haki na wale waliopo kwenye maumivu si jambo la faraja”.

Waziri Mkuu amesema wananchi wasipeleke miili kwanza makaburini ili waweze kupitia na kutambua ndugu na rafiki kwa ajili ya  kuwa na kumbukumbu ya kudumu. “Hali si nzuri ndugu zetu wameungua sana wapo wengine mnaweza msiwatambue lakini mnaweza kutambua kwa alama. Wapo wengine walivaa bangili, heleni, mkanda havijaungua”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kama hawajawatambua Serikali imeweka utaratibu wa vipomo vya vinasaba, ambapo  kumbukumbu hizo zimechukuliwa na wataalamu wetu wa afya. “Kama ukipita ukishindwa kumuona bado tunakuruhusu kukupima vinasaba na kulinganisha na vyakwako. Bado haki ya kumpata ndugu yako iko pale pale madaktari wapo, mitambo ipo tutachukua vinasaba na kuainisha tutatoa nafasi leo hadi saa 10 kufanya utambuzi”.

Amesema Serikali inaratibu vizuri jambo hilo lakini kuanzia saa 10 itaruhusu wale waliotambuliwa kuchukua mwili lakini kama hawajajipanga vizuri itauzika na kama kuna jina litaliandika na kama hakuna jina wataandika namba ya vinasaba ili kutoa fursa kwa ndugu siku nyingine waende wakapimwe na kuoneshwa kaburi la ndugu yao.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019.


Share:

Vijana Mkoani Ruvuma Wachangamkia Fursa Ya Mafunzo Ya Ujasiriamali

Na; Mwandishi Wetu
Vijana Mkoa wa Ruvuma wamefurahia fursa ya mafunzo ya ujasiriamali na usimamaizi wa biashara yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatawawezesha vijana hao kukuza na kurasimisha shughuli zao za kiuchumi.

Akifungua Mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa alieleza kuwa mafunzo hayo ya ujasiriamali ni muhimu sana na yanalenga kuwawezesha vijana wanaomiliki biashara wanapata mbinu za kuendeshaji na kusimamia biashara zao.

“Mafunzo haya ya ujasiriamali yameleta tija kwa vijana na wameweza kujiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi zenye faida,” alisema Issa

Alieleza kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa hizo zinapojitokeza ili waweze kuunganishwa na fursa za mitaji na mitandao ya huduma za biashara, pia kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa kujiamini na kuweza kuweza kupata faida.

“Vijana mnapaswa kutambua ninyi ndio nguvukazi ya Taifa, hivyo kuwa wabunifu ni jambo la msingi katika biashara zenu mkitambua fursa mlizonazo ili muweze kushindana katika biashara,” alisema Issa

Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali watakayopatiwa vijana hao yakiwemo masuala ya uchambuzi wa masoko, dhana ya ujasiriamali, uchambuzi wa mahitaji ya mteja, kutambua ushindani wa soko, mkakati na uendeshaji biashara, utambuzi wa masoko, usimamizi wa fedha, vihatarishi vya biashara na namna ya kuvikabili, usimamizi wa biashara na rasilimali watu, urasimishaji wa biashara na vyanzo vya mitaji.

Aliongeza kuwa Programu hii ya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana itawawezesha kutambua mapungufu waliyonayo na kutumia mwanya huo kuangalia fursa walizo nazo katika ushindani wa biashara zao.

“Ni muhimu vijana mkawekeza katika biashara mnazozimudu kimtaji, kiusimamizi kwa ushindani na kufanya maamuzi sahii,” alieleza Issa

Alieleza kuwa kila Mkoa una fursa zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali katika kujiendeleza kiuchumi, vijana wanatakiwa kuchangamkia fursa hizo ili waweze kunufaika kwa njia mbalimbali.

Alifafanua kuwa Ofisi yake imekuwa ikiendesha mafunzo ya aina hii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi za Umma, Wadau wa Mendeleo, Sekta binafsi na jamii kwa ujumla.

“Zaidi ya Vijana 10,000 wameweza kufikiwa na programu mbalimbali za mafunzo ikiwemo Kijana jiajiri, Ajira yangu, Kliniki ya vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu, mifuko ya uwezeshaji na watoa huduma,” alisema Issa

Aidha, alitoa shukrani zake kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona haja ya kuwekeza kwa vijana kwa kuwapatia ujuzi ili waweze kujiajiri, kuajiri na kuchangia katika pato la taifa.

Kwa Upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Hakimu Mafuru amewahimiza vijana wa Mkoa huo kuchangamkia fursa za mafunzo kama hayo yanayotolewa na Serikali pamoja na wadau mbalimbali kwa kuwa yatawawezesha kujitambua na kujisimamia wenyewe na kuongeza tija kwenye biashara zao.

Mmoja wa Vijana walioshiriki katika Mafunzo hayo, Bi. Pudencia Msangawale alieleza kuwa mafunzo hayo yatajibu changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kama wajisiriamali ikiwemo masuala ya ujuzi, maarifa, kurasimisha biashara, namna bora ya kuhudumia wateja na utafutaji wa masoko.

“Ninawashukuru Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa elimu waliyotupatia yametuwezesha kujitambua, kuwa wabunifu, waaminifu na kuweza kujisimamia katika biashara,” alisema Msangawale.

Mafunzo hayo yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo yatafanyika katika Mikoa nane (8) ya Tanzania Bara ikiwemo Dodoma ambapo tayari yamekisha fanyika, Ruvuma, Geita, Mwanza, Lindi, Mbeya, Tanga na Arusha.

MWISHO


Share:

Kutana na Mohamedi Buruhani Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH .....Anauwezo wakufanya Dua mbalimbali Na Kutafsiri Ndoto

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Mohamedi Buruhani Mtabibu wa Nyota za Binadamu  Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mohamed Buruani Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie ..Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Mohamed Buruhan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN, Anatafsiri Ndoto. ,KUSAFISHA NYOTA, Mvuto wa Mwili na BIASHARA, ...MIGUU Kufa GANZI na mengi zaidi (+255  715971688 au (+255  756914036

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...


Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992. WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Share:

Full Video: Rais Magufuli Alivyowajulia Hali Majeruhi Wa Ajali Ya Moto Muhimbili

Rais Magufuli amewatembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na ajali ya moto iliyotokana na mlipuko wa mafuta yaliyokuwa yamebebwa kwenye lori la kubeba mafuta lililopata ajali jana mkoani Morogoro.

Tazama hapo chini


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger