Saturday, 10 August 2019

WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC YAHITIMISHWA KWA KISHIDO


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza wakati akifunga maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yaliyokuwa yakifanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam pamoja na viwanja vya Karimjee jijini. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

 RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ally Mohammed Shein amesisitiza waafrika hasa walio katika Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kupenda bidhaa zinazozalishwa katika ukanda huo ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

 Akifunga maonyesho ya nne wiki ya viwanda ya SADC jijini Dar es Salaam jana, Dk. Shein alisema juhudi kubwa inayofanywa na viongozi wa nchi wanachama kuimarisha uzalishaji kwa viwanda vya ndani inatakiwa isipotee bure kwa kuunga mkono juhudi hizo.

 Alisema, inawezekana kabisa kukuza masoko na kuongeza ajira kwa kutumia bidhaa za ndani kwa sababu msisitizo mkubwa ni kuona waafrika wanapenda vya kwao bila kuwa tegemezi wa bidhaa za kimagharibi.

 “Kazi iliyo mbele yetu sasa ni kuhakikisha kwamba kila mmoja wetu anaunga mkono utelekezaji wa maazimio yaliyopitshwa katika vikao vilivyofanyika pamoja na mikakati ya Serikali zetu zote ya kuendeleza viwanda kwa kununua na kuzipenda bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe,” alisema na kuongeza:

 “Vile vile, tujenge utamaduni wa kuwapenda na kuwatumia wataalamu wetu wa ndani na tuondokane na utegemezi wa wataalamu wa nje, sambamba na kujenga misingi imara ya kuendeleza teknolojia yetu wenyewe.

 “Kufanya hivyo, ni kutafsiri kivitendo ile dhamira ya nchi zetu kuunda umoja wa SADC kwa ajili ya kuongeza fursa ya masoko na ajira. Tutaweza kuongeza masoko na ajira ikiwa tunanunua bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe vinavyoendeshwa na wataalamu wazalendo.

 “Kwa msingi huo, nasisitiza haja na umuhimu wa kuzingatia falsafa na hekima za Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar kwa kuzingatia maneno aliyoyasema kwamba “Tukuza kilicho chako hadi usahau cha mwenzako”. Wakati umefika wa kuhakiksha kwamba tunapenda kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu wenyewe.

” Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema anaamini maonesho hayo aliyoyafunga jana yamesaidia na yatakuwa na mchango mkubwa katika utekelezaji wa mipango na mikakati tuliyonayo ya kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa viwanda katika nchi zote 16 wanachama wa SADC.

 Taaluma, ujuzi na maarifa yaliyopatikana katika maadhimisho na maonesho haya itatumika katika kukuza ubunifu wa kuendeleza viwanda, utafutaji wa masoko pamoja na kukuza uhusiano baina ya wazalishaji, wanunuzi, wasafirishaji, na watumiaji bidhaa zinazozalishwa na viwanda vilivyomo ndani ya nchi Wanachama wa Jumuiya hii.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la SADC Peter Varndell akizungumza wakati wa hitimisho la Maonesho ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika SADC  lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la SADC Octavian Mshiu wakati akifunga maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yaliyokuwa yakifanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam pamoja na viwanja vya Karimjee jijini.
Meza kuu.
Katibu Mkuu wa SADC Mhe. Dr. Stergomena Tax, wakati wa ufungajin wa Maonesho ya Nne ya Wiki ya Maonesho ya Viwanda ya SADC leo Jijini Dar es Salaam.yaliofanyika katika ukumbi wa Juluis Nyerere. Vile vile, anaamini maonesho hayo yamepanua fursa ya ushirikiano kati ya wenye viwanda ndani ya nchi za SADC na wamiliki wa viwanda na watoa huduma mbali mbali wa mataifa mengine nje ya umoja wa SADC.

 Hata hivyo, alishauri wazalishaji katika nchi wanachama ikiwa wanataaka kuingia kwenye ushindani watalazimika waongeze ubora wa bidhaa za viwandani, ili ziweze kushindana na zile ambazo watu wengine hupenda kuzinunua. Ubora katika utengenezaji na ubunifu wa hali ya juu utakaoweza kuwavutia wanunuzi wengi.

Hali hii itaweka mazingira mazuri ya kupata masoko ya kutosha na ya uhakika pamoja na mitaji ya kujiendesha na kukuza ajira. “Naamini kwamba uwezo wa kufanya hivyo tunao, linalohitajika ni kushirikiana katika kuongeza ujuzi na bidii zaidi katika kazi zetu viwandani pamoja na kujiamini, kwamba tunaweza kuingia katika ushindani wa viwango na kuibuka washindi.

Katika utafutaji wa masoko tuweke mkazo katika Technolojia ya Habari na Mawasiliano, ili tuweze kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokana na utandawazi,” alisema Dk. Shein.

 Akigusia kaulimbiu ya Maadhimisho na Maonesho ya SADC kwa mwaka huu wa 2019 ambayo imeweka msisitizo katika uwekaji wa mazingira mazuri kwa maendeleo ya viwanda, ili ilete manufaa mapana zaidi kwa jamii, alisema inakwenda sambamba na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali zote mbili za kuimarisha viwanda.

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kuiimarisha sekta binafsi kwa lengo la kuhakikisha kwamba inaongeza fursa za ajira kwa vijana wetu wanaomaliza masomo yao katika ngazi zote.


 Serikali zote mbili zinaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kisera na za kimkakati katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na kuifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kufikia hadhi ya nchi ya Uchumi wa Kati, kama ilivyoelezwa katika Mipango Mikuu ya Maendeleo ya Taifa.
Kaimu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe akizungumza wakati wa mkutano wa Ufungaji wa Wiki ya Nne ya Maonesho ya Viwanda ya SADC Jijini Dares Salaam.
Mawaziri wakitambulishwa...
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa akitoa neno la Shukurani kwa Washiriki wa Wiki ya Viwanda kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, (hawapo pichani), Kuhusu maonesho ya Viwanda yaliyofungwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Wageni waalikwa.
Wageni wakifurahia.
Picha za pamoja za viongozi. Alisema, utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo Miradi ya umeme, barabara, reli, bandari na viwanja vya ndege unalenga katika kujenga misingi imara ya ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara ambazo ni muhimu katika kutatua changamoto za ajira pamoja na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi. Katika hatua nyingine, Dk. Shein aligusia umuhimu wa kutumia lugha ya Kiswahili katika nchi wanachama wa SADC ambapo alidai itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mtangamano kwa kuwa ndiyo lugha iliyotumika katika harakati za ukombozi. “Ni jambo jema kuona kwamba kuna wazo la kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa ni miongoni mwa lugha rasmi za mawasiliano katika majukwaa ya SADC. Hii ni hatua muhimu katika kuimarisha umoja na mshikamano kwa Wanachama wa Jumuiya hii pamoja na kukuza shughuli za biashara na viwanda. “Historia inatuonesha kwamba Kiswahili kimeweza kuwaunganisha Watanzania kuwa wamoja, licha ya kwamba Watanzania wanazo lugha tofauti za makabila mbali mbali. Aidha, Kiswahili kimekuwa na mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa Afrika. “Hivi sasa, Kiswahili kimerahisisha mawasiliano na kukuza biashara katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na tayari Umoja wa Afrika umekikubali Kiswahili kiwe ni Lugha rasmi. Kwa hivyo, wazo la kukifanya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha rasmi za SADC ni muhimu na vyema tukaungana katika kulifanyia kazi suala hili,” alisema Dk. Shein. Awali Katibu Mtendaji wa SADC, Dk. Stegomena Tax alisema maadhimisho hayo ya wiki ya nne ya viwanda yamekuja katika wakati muafaka ambapo Serikali ya Tanzania inaimarisha uchumi wa viwanda. Alisema, biashara ikikuzwa vema wananchi watapata faida na ajira pamoja na bidhaa zenye ubora ambazo zinazweza kuuzika hata nje ya mipaka ya nchi za SADC. “Ushiriki wenu katika wiki hii inamaanisha utayari mlio nao katika kukuza uchumi wa SADC, umuhimu wa kuzitambua fursa na kuhamasisha kuzichangamkia ni jambo la msingi katika ukombozi wa nchi za kiafrika kiuchumi, kijamii na kisiasa,” alisema Dk. Tax. Aidha, Dk. Tax alisisitiza umuhimu wa kuwepo mkakati madhubuti wa kuimarisha miundombinu ili kurahisisha usafirishaji bidhaa zitakazozalishwa kwenye viwanda vya nchi wanachama. Ambapo, wakati wa ufunguzi wa wiki hiyo ya viwanda Rais Dk. John Magufuli alisisitiza haja ya kuwa na miundombinu imara kwa kuunganisha nchi za SADC. Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Innocent Bashungwa alisema zaidi ya washiriki 5352 kutoka nchi wanachama wamehudhuria wiki hiyo ya viwanda, huku waonyeshaji bidhaa 585 walionyesha bidhaa mbalimbali kutoka nhci wanachaa 14 za SADC. “Katika waonyeshaji hao kulikuwa na taasisi 61, viwanda 69, taasisi za fedha 65, Umoja wa Mataifa pia walishiriki na wajasiriamali 405. Huku watu waliotembelea maonyesho haya wanafikia 4767, hii ni ishara ya kukubalika na itasaidia kuongeza fursa kwa wazalishaji wa ndani kupata mtandao mkubvwa wa kuuza bidhaa zao,” alisema Bashungwa. Leo katika ratiba ya SADC washiriki kutoka nchi wanachama watatembelea viwanda mbalimbali nchini ili kuona namna bidhaa zinavyozalishwa na kutoa ushauri pamoja na kujifunza masuala mbalimbali katika sekta ya viwanda Tanzania Bara na Zanzibar. SADC inaundwa na nchi 16 ambazo ni Tanzania, Zambia, Malawi, Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Eswatini, Botswana, Lesotho, Mauritius, Comoro, Ushelisheli, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Namibia na Zimbabwe.
Share:

DED AAGIZWA KUCHUKUA ZA HARAKA KUZUIA BIASHARA YA NGONO MWAKITOLYO....NGONO INAUZWA WANAITA ' KUCHEMSHA MASHINE'

Na Suleiman Abeid, Shinyanga
Mkurugenzi mtendaji katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Hoja Mahiba ameagizwa kuchukua hatua za haraka kuzuia vitendo vya uasherati vinavyofanywa na baadhi ya wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika kata ya Mwakitolyo wilayani humo.


Agizo hilo limetolewa mapema wiki hii katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kutolewa kwa taarifa ya kukithiri kwa biashara ya wanawake wanaojiuza kiasi cha wanaume kupanga foleni wakisubiri kupatiwa huduma.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mmoja wa madiwani iliwashitua madiwani wengine ambao walisema iwapo hali hiyo haitadhibitiwa haraka ipo hatari ya kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa wakazi wa wilaya hiyo na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla.

“Mheshimiwa mwenyekiti, binafsi nilipopata taarifa hii mimi mwenyewe niliamua kwenda Mwakitolyo kujiridhisha, na kweli nilichokikuta hakikunifurahisha, nilishuhudia mwenyewe katika nyumba zilizopangwa na wanawake hao kuna foleni za vijana wa kiume wengi wakisubiri huduma,”

“Niliuliza kuna biashara gani inayofanyika, jibu lilinishitua, ilibidi na mimi nipange foleni nikaone kule ndani kama kweli biashara hiyo ndiyo inayofanyika, lakini hata kabla sijaingia ndani nilishangaa kuona watu wanagonga milango wakisema, muda, muda, dakika zimekwisha tupishe na sisi,” alieleza diwani Isack Sengerema.

Akifafanua Sengerema ambaye ni diwani wa kata ya Iselamagazi, alisema biashara hiyo imekuwa ikifanyika wakati wote bila kujali muda wa kazi ambapo vijana wengi wafanyabiashara na wachimbaji madini ya dhahabu katika kata hiyo wamebuni msemo wa kwenda “kuchemsha mashine.”

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu, Azza Hilal alikiri kuwepo kwa vitendo hivyo ambapo alisema yeye binafsi kama mwanamke amesikitishwa na hali hiyo na kushauri kuchukuliwa kwa hatua za haraka kuwadhibiti wanawake ambao wameamua kufanya biashara hiyo chafu.

“Mheshimiwa mwenyekiti, ni kweli kabisa haya yanayoelezwa hapa ndiyo yanayotokea kule kwenye kata ya Mwakitolyo, nimeshuhudia hali hiyo, na imenisikitisha sana kama mama, ninachoshauri tuchukue hatua haraka, na nafikiri tuangalie uwezekano wa kuwapatia mikopo wanawake wanaofanya biashara hiyo,”

“Vitendo hivyo si aibu kwa wanaovifanya peke yao bali hata wilaya yetu inachafuliwa, nimeona wengi wanaofanya biashara hiyo ni mabinti, huenda ni ugumu wa maisha ndiyo unasababisha wajiuze, hivyo wakihamasishwa kujiunga kwenye vikundi na kukopeshwa fedha, naamini wataacha,” alieleza Azza.

Hata hivyo hoja ya kuwapatia mikopo ilipingwa na madiwani ambao walisema sehemu kubwa ya wakazi wa Mwakitolyo ni watu wanaotoka maeneo ya nje ya wilaya ya Shinyanga ambao wamekwenda pale kufanya biashara ya madini na hawana anuani maalumu.

Baada ya mjadala mrefu, madiwani hao walimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuchukua hatua za haraka za kudhibiti vitendo hivyo na pia kuwaomba madiwani wa viti maalumu kwenda kutoa elimu  kwa wanawake wenzao wanaofanya vitendo hivyo kwa kuwaeleza madhara wanayoweza kuyapata.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Mboje Ngassa aliagiza kazi ya kwenda kutoa elimu kwa watu wanaofanya biashara hiyo ifanyike mapema wiki ijayo ambapo amemuomba mbunge wa viti maalumu, Azza Hilal ashirikiane na madiwani wa viti maalum katika suala hilo.

“Ni vitendo vinavyosikitisha, inaonesha ni ukosefu wa elimu kwa wenzetu hawa walioamua kujitoa ufahamu, hawajui madhara ya kile wanachokifanya, sasa tukawaelimisha, nafikiri wataacha, kwa suala la mikopo, litakuwa gumu kidogo maana wengi wao si wakazi wa wilaya ya yetu,” alieleza Ngassa.
Mwisho.
Share:

WAZIRI MKUU ATOA ONYO LA MWISHO KWA MKURUGENZI MANISPAA YA SHINYANGA KUGOMBANA NA WENZIE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geoffrey Mwangulumbi pamoja na Mwekahazina wa Manispaa hiyo, Pascal Makoye, ambapo amewataka wabadilike na waache kugombana na badala yake watekeleze majukumu yao.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo Agosti 9, 2019, wakati akizindua nyumba 10 za Askari Polisi katika Manispaa ya Shinyanga eneo la Kambarage, mradi ambao umetokana na fedha kiasi cha sh. milioni 225.

Waziri Mkuu amesema viongozi hao wameshindwa kutekeleza majukumu yao, ikiwemo kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji wa mapato, na kutoa kazi hiyo kwa kampuni zisizokuwa na uwezo.

“Mkurugenzi na wenzako nawaonya kwa mara ya mwisho badilikeni na hakikisheni mnatekeleza majukumu yenu ipasavyo yakiwemo ya ukusanyaji wa mapato.” amesema Waziri Mkuu.

Kuhusu nyumba za Askari Polisi, Waziri Mkuu amesema lengo la ujenzi wa nyumba hizo ni kuhakikisha askari wanaishi katika mazingira mazuri.
Share:

Breaking: Lori la Mafuta Laripuka Na Kuua Idadi Kubwa ya Watu Morogoro

Idadi kubwa ya Watu wanasadikiwa kufariki Duania  baada ya kuungua na moto kufuatia Lori la mafuta kulipuka eneo la Msamvu mjini Morogoro. 

Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakiiba mafuta kwenye Lori hilo ambalo lilipata ajali majira ya saa 1:00 Asubuhi leo Aug 10.

Endelea kuwa nasi kwa habari kamili


Share:

Breaking : WATU ZAIDI YA 50 WASADIKIWA KUFA BAADA YA LORI LA MAFUTA KUWAKA MOTO MORO

Watu zaidi ya 50 wanasadikiwa wamekufa baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto eneo la Msamvu mkoani Morogoro. Inadaiwa chanzo ni watu kutaka kuiba betri kutoka kwenye tenka hio iliyokuwa imepinduka huku wengine wakiba mafuta ndipo moto ukalipuka. Juhudi za kuopoa miili zinaendelea.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi August 10




Share:

Friday, 9 August 2019

Wizara Ya Ardhi Kwa Kushirikiana Na TAKUKURU Yaunda Tume Ya Uchunguzi Dhidi Ya Watumishi 183

Na.Faustine     Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, WILIAM LUKUVI, amesema Wizara hiyo imeunda timu  ya uchunguzi ambayo itakuwa chini ya TAKUKURU, ikijumuisha vyombo vya ulinzi na usalama, kuwachunguza watumishi 183 waliosimamishwa kwa kuingilia mfumo wa kukadilia na kukusanya kodi ya pango la ardhi.
 
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, kutolea ufafanuzi juu ya kusimamishwa kwa watumishi 183 wa wizara hiyo amesema serikali ilitilia shaka mfumo huo  na kufanya uhakiki.
 
Uhakiki huo wa miezi sita umebaini kuna watu walitakiwa kulipa kiwango  cha kodi ya pango lakini  kiwango kilichoingia hazina ni kidogo ukilinganisha na kiwango kilichofutwa katika mfumo wa malipo ikionesha kiwango hicho kimelipwa.
 
Amesema kutokana na matokeo ya uhakiki huo Wizara kupitia kwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo wanaunda timu ambayo itakuwa chini ya TAKUKURU na vyombo vingine vya usalama kuchunguza jambo hilo na makosa mengine yatakayoonekana katika uchunguzi huo.
 
Waziri Lukuvi ametumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi hususan Wa wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na Mkoani Mtwara  kwa kuonesha  ushirikiano wa kutoa taarifa dhidi ya watumishi wa ardhi waiokuwa waaminifu.

Aidha waziri Lukuvi amewatoa hofu wana nchi kutokana na idadi kubwa ya maafisa ardhi waliosimamishwa amesema Shughuri za kiserikali katika Ofisi hizo zitaendelea kama kawaida.
 
Pia amewataka wananchi kutumia mfumo wa kielecronic kulipia kodi ya pango ili kuepusha vitendo vya rushwa, na amesema kwa wale wote ambao fedha za malipo ya pango zilifutwa bila malipo kuonekana katika mfumo na wale ambao yameingia malipo pungufu wote watalipa kiasi kilichobaki kukamilisha malipo hata kama wamelipa.
 
Hata hivyo,Waziri Lukuvi ametolea Mfano suala la Mmiliki wa  Mbeya Hotel ambapo alipunguziwa ukubwa wa eneo  lililokuwa na Ukubwa wa Mita za Mita za mraba 20,234 lakini kwenye mfumo wa malipo akawa analipia gharama ya   Mita za Mraba  502 badala ya 20,234 tangu mwaka 2002 baada ya kufanyiwa ujanja na mtumishi wa ardhi .
 
Hivyo alitakiwa kulipa zaidi ya  Tsh.Milioni 6  kwa Mwaka, kutokana na ujanja amepatana na mtu wa mfumo  badala yake wanamtoza zaidi ya 63 elfu pekee tangu mwaka 2002 pekee kwa mwaka na kwa malipo halisi serikali inamdai zaidi ya Tsh.Milioni 68.

Timu hiyo ya Uchunguzi itaanza kufanya kazi kuanzia Wiki ijayo Siku ya Jumanne ambapo itafanya uchunguzi kwa muda wa siku 30.


Share:

Mbunge Wa CHADEMA Akubali Utendaji Kazi Wa Rais John Pombe Magufuli.

NA Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini kupitia chama cha Demokrasia na maendelelo (CHADEMA) Mh Wilfredy Muganyizi Rwakatale amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania   Dk John Pombe Magufuri kwakuendelea kukarabati meli ya abiria na mizigo itakayokuwa inafanya safari zake Bukoba-Mwanza.
 
Mh Rwakatale amesema hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo la Bukoba  Mjini uliofanyika  August 7 2019 katika kata ya Hamugembe manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wenye lengo la kuzungumzia miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyofanyika kwa kipindi cha miaka minne kwenye uongozi wake wa  jimbo na kuongeza kuwa jitihada za ukarabati wa meli hiyo unaendelea kwa kasi chini ya uongozi wa awamu ya tano unaoongozwa na Dk John Magufuri.
 
Aidha mh Rwakatale amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera ususani jimbo lake la manispaa ya Bukoba kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo meli inaendelea kutengenezwa na itakapo kuwa imekamilika itawaondolea usumbufu wa kuendelea kusafiri kwa kutumia mabasi kwenda mkoani Mwanza.
 
Katika miaka minne ya uongozi wake mh Rwakatale ameweza kutekeleza miradi mbalimnbali ya kimaendeleo katika jimbo lake ikiwemo kuchangia shilingi milioni 16 kuwezesha ukarabati wa uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kashai, mabati 56 kwa ajili ya kuezeka shule ya msingi Nyamkazi, ametoa shilingi milioni 2 kila kata kwenye kata 14 ili kuwezesha utengenezwaji wa madawati na mengine mengi.
 
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh Conchesta Rwamulaza amewaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kujitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ili waweze kushiriki katika ushaguzi wa serikari za mitaa utaotarajia kufanyika mnamo mwaka huu.
 
Mh Rwamulaza ameongeza kuwa ili wananchi  wapate  kiongozi bora inabidi washiriki katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ambapo zoezi ilo kwa upande wa mkoa wa kagera limetajwa kuanza kufanyika mnamo mwezi wa tisa  mwaka huu.


Share:

Tiba Halisi ya Tatizo la Nguvu za Kiume

*NKOLOMIJE*/
√Ni dawa bora ya mitishamba yenye kuimarisha, kurefusha na kukufanya uwe imara hata kama umelala pia huimarisha na kukuza  maumbile yaliyosinyaa na kuwa regevu

*📌SUPER GAFINA MIX*/
Ni dawabora ya nguvu za kiume yenye mchanganyiko wa miti shamba 10 yenye maajabu yafuatayo:/
🔖(1)Inatibu upungufu wa nguvu za kiume mara dufu na kuimarisha misuri ya uume ulio legea na kusinyaa wakati wa tendo la ndoa/
🔖(2)Kuongeza hamu ya tendo kukufanya uweze kurudia tendo hadi mara tatu bila kuchoka
🔖(3)Itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15-30 kwa tendo la Kwanza na utakuwa na uwezo wa Kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3-4 bila hamu kuisha na inatibu kabisa/
.
*MATATIZO HAYA HUSABABISHWA NA*/
🔖(1)Tumbo kujaa gesi, na kuunguruma chini ya kitovu/
🔖(2) Choo kuwa kama Cha mbuzi/
🔖(3)Ngiri/
🔖(4)Kama umejichua sana punyeto/
🔖(5)Kisukari/
🔖(6)Presha ya kupanda na kushuka/
🔖(7)Vidonda vya tumbo,/


Bado hujachelewa

Pia tuna tibu  KISUKARI,PRESHA,VIDONDA VYA TUMBO N.K/
._______________________
ANAPATIKANA  DAR ES SALAAM  AU UNAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO SIMU NO:/
*📞0752723508*


Share:

Jeshi la Polisi Lamtia Mbaroni Afisa Usalama wa Taifa FEKI

Jeshi la polisi nchini kupitia kikosi chake cha viwanja vya ndege jijini Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili katika uwanja wa Mwl. JK Nyerere kwa makosa tofauti.


Share:

Mfanyakazi TAKUKURU Makao Makuu adakwa akiomba na kupokea Rushwa

Mchunguzi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyita (44), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania  akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kuomba rushwa ya Sh200 milioni na kutakatisha fedha.

Batanyita ambaye ni mkazi wa Chamazi, Dar es Salaam amefikishwa mahakamani hapo, leo Ijumaa Agosti 9, 2019 na kusomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina.

Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi akisaidiana kusomewa mashtaka yake na Wankyo Simon amedai mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 76/2019.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili mshtakiwa huyo ni kushawishi, kuomba rushwa na kutakatisha fedha, ambapo anadaiwa kuyatenda kati ya Februari  9, 12 na 24, 2019.

Katika shtaka la kuomba rushwa, Batanyita anadaiwa Februari 9, 2019 eneo la Upanga, Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa Takukuru alishawishi na kuomba rushwa ya Sh200 milioni kutoka kwa Hussein Gulamal Hasham ili aweze kuharibu ushahidi katika kesi ya ukwepaji wa kodi iliyokuwa inamkabili Hasham.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 23, 2019 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa  rumande.


Share:

Mkongo: Kibongo ya Tatizo la Nguvu za Kiume

********************************
SUPER MKONGO MPYA,
_______________________________
********************************
Ni dawa bora ya kutibu na kumaliza matatizo yote ya nguvu za kiume na sababu zake zote kama vile,

- kuwahi kufika kileleni dakika moja ushakojoa
- maumbile kusinyaa na kulegea wakati wa tendo
- kukosa hamu ya tendo la ndoa
- kushindwa kurudia tendo la ndoa
- maumbile kusimama kwa kulegea
-  kulegea katikati ya tendo
- kuathirika kwa kujichua kwa muda mrefu
- kuishiwa nguvu kutokana na punyeto.

Epuka aibu hii leo kwa kutumia SUPER MCONGO MPYA, kiboko ya matatizo haya.
_______________________________
Kwanza fahamu sababu zinazopelekea kuwa na upungufu wa nguvu za kiume
_______________________________
(1) kujichua (punyeto) kwa muda mrefu maana hupelekea misuli ya uume kulegea.
(2) ngiri
(3) kuugua chango la uzazi kwa muda mrefu.
(4) kupungukiwa hormone za testosterone.
(5) ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na visivyo na virutubisho  vya kutosha.
(6) kutokufanya mazoezi na mwenendo wa maisha.
(7) kisukari.
(8) tumbo kuunguruma na kujaa gesi.
(9) maumivu ya kiuno nk.
_______________________________

WASILIANA NA:
DR. MCONGOMANI
SIMU NO:
📞0658816558
📞0682323682
Popote ulipo huduma hii inakufikia


Share:

BOT Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarships 2019/2020

BOT Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarships 2019/2020 SCHOLARSHIP ANNOUNCEMENT (6 Scholarships) MWALIMU JULIUS NYERERE MEMORIAL SCHOLARSHIP FUND The Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund is announcing Scholarships for the 2019/2020 academic year. The primary objective of the Fund is to promote interest and excellence in Mathematics and Science courses among female students in the United Republic of Tanzania.… Read More »

The post BOT Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarships 2019/2020 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

African Development Bank (AFDB) Technology Incubation Hackathon 2019 for African Women

Tech Incubation Program Hackathon 2019 Frankfurt School of Finance & Management is implementing AfDB’s Technology Incubation Program: A gendered approach in Sudan and Rwanda, with support from Korea-Africa Economic Cooperation (KOAFEC). Young Tech aspiring Entrepreneurs (targeting 70% female) will be selected based on performance and idea bankability over five hackathons (episodes). The selected teams comprising 12 innovators will… Read More »

The post African Development Bank (AFDB) Technology Incubation Hackathon 2019 for African Women appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

IBM Digital Nation Africa Internship 2019 for young Nigerians

IBM Digital Nation Africa Internship 2019 for young Nigerians IBM Digital-Nation Africa is a cloud-based learning and innovation platform, providing digital competency and nurturing innovation. IBM Digital-Nation Africa curriculum content is designed for the following audiences: Explorer: People keen on learning about the new emerging technologies Innovator: Designed to help accelerate innovation and enable would-be innovators to bring… Read More »

The post IBM Digital Nation Africa Internship 2019 for young Nigerians appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Taarifa ya Mfumuko Wa Bei Kwa Mwezi Julai 2019

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini ambapo pamoja na mambo mengine mfumuko wa bei ya mwezi Julai 2019, umebakia kuwa asilimia 3.7 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2019.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari leo Ijumaa (Agosti 9, 2019) Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja alisema kiwango hichi kubakia kuwa sawa kwa kiwango hicho kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisizo za chakula kwa kipindi kilichoisha Julai 2019.

Aidha Minja alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2019 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 2.9 kutoka asilimia 2.3 ilivyokuwa kwa mwezi Juni 2019.

“Baadhi ya bidhaa zilizoongezeka bei kwa mwezi Julai zikilinganishwa na Julai 2018 ni pamoja na unga wa mahindi (6.0%), unga wa mhogo (4.0%), mafuta ya kupikia (8.9%), na mbogamboga (4.6%) ambapo kwa uoande wa bidhaa zisizokuwa za vyakula ni pamoja na vifaa vya kieletroniki, majiko ya gesi pamoja na vifaa pamoja na bidhaa za huduma”.

Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki, taarifa inaonyesha kuwa Nchi ya Kenya ilikuwa na Kiwango cha juu cha mfumuko wa bei kwa mwezi Julai 2019, ambapo kiwango chake kilifikia asilimia 6.27 ikilinganishwa na asilimia 5.70 kwa mwaka ulioishia Juni 2019.

Akifafanaua zaidi Minja alisema taarifa ya mfumuko wa bei katika Nchi ya Uganda katika mwaka ulioishia Julai 2019, taarifa zinaonyesha kuwa Nchi hiyo ilikuwa na kiwango kidogo cha mfumuko wa mdogo bei kilichofikia asilimia 2.6 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia Juni, 2019.

MWISHO.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger