Saturday, 3 August 2019

DKT. MWANJELWA ATEMBELEA MKOA WA KAGERA KUKAGUA MIRADI YA TASAF...AWAFUNDA WALENGWA


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini(hawapo pichani) katika Manispaa ya Bukoba wakati wa ziara ya kikazi yenye kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipowatembelea kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikaribishwa na mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini, Manispaa ya Bukoba, Bibi Irene Mgongo katika nyumba aliyoijenga baada ya kupata ruzuku ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na moja ya kaya za Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Manispaa ya Bukoba.
Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Manispaa ya Bukoba, Bibi Irene Mgongo akimuonyesha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) shamba analolima kwa kutumia ruzuku ya TASAF ili kujiongezea kipato.

Na Estom Sanga- Kagera. 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. Dokta Mary Mwanjelwa amewahimiza Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kuthamini mchango huo wa serikali kwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kunufaika zaidi na kuboresha maisha yao. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti mwanzoni mwa ziara yake ya mkoani Kagera ambako amekutana na Walengwa wa TASAF na Watumishi wa Umma ,Dr. Mwanjelwa amesema Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanapaswa kutumia vizuri fursa hiyo adhimu waliyoipata ili waweze kuendelea kunufaika nayo kwa ukamilifu. 

Naibu Waziri huyo wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amesema utekelezaji wa Mpango huo ni miongoni mwa Mikakati ya Serikali ya kukabiliana na kero ya umaskini kwa Wananchi na hivyo akawahimiza kuitumia fursa hiyo kwa kuanzisha miradi ya kujiongezea kipato na kukuza uchumi wao na taifa kwa jumla. 

Aidha Dr. Mwanjelwa amepongeza mafanikio yaliyoanza kuonekana kwa Walengwa wa TASAF kuanza kuboresha maisha yao kwa kujenga nyumba,kuanzisha miradi ya kilimo, ufugaji na kukuza sekta ya elimu na afya ambayo amesema kwa kiwango kikubwa zimesaidia kukuza uwezo wa kuendesha maisha yao. 

Akizungumzia suala la baadhi ya vijiji kutojumuishwa kwenye Mpango, Dr, Mwanjelwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Magufuli ameagiza vijiji vyote vyenye Wananchi wanaostahili kujumuishwa kwenye Mpango huo vipewe fursa hi katika sehemu ya pili ya Mpango wa kunusuru Kaya Maskini inayotarajiwa kuanza hivi karibuni. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa ameonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio waliyoanza kupata Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Bukoba tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango huo hususani katika nyanja za elimu, afya, uzalishaji mali na uboreshaji wa makazi yaa. 

“Nimejionea namna walengwa wa TASAF mnavyotumia rukuzu mnayopata kuboresha maisha yenu hilo ni jambo zuri kwani mnaunga mkono nia njema ya serikali ya Awamu ya Tano kwa vitendo,” Amesisitiza Dkt. Mwanjelwa. 

Amesema, kwa kutambua mchango wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika maendeleo ya wananchi, Serikali imeamua kuendelea kuutekeleza Mpango huo katika sehemu ya pili ambapo mkazo utawekwa zaidi katika miradi itakayowawezesha Walengwa kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kupata ujira kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato. 

Akizungumzia suala la baadhi ya maeneo kutonufaika na huduma za Mpango huo , Naibu Waziri huyo amesema, Serikali imeamua kuwa katika sehemu ya pili ya Mpango huo inayotarajiwa kuanza hivi karibuni maeneo yote nchini ambako wananchi watakidhi vigezo wajumuishwe kwenye huduma za Mpango huo. 

“ Serikali hii haibagui wananchi wake, hivyo wale wote ambao watakidhi vigezo vya kuweko kwenye Mpango watapata fursa hiyo ili waweze kuitumia katika kuboresha maisha yao” Amefafanua Dkt Mwanjelwa. 

Dkt. Mwanjelwa yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi kujionea utekelezaji wa shughuli za TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma katika Halmashauri zote za mkoa huo. 

Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo takribani Kaya za Walengwa zipatazo Milioni MOJA na LAKI MOJA zimenufaika na huduma za Mpango huo katika sehemu yake ya Kwanza iliyoanza kutekelezwa mwaka 2012 kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba.
Share:

MBUNGE YOSEPHER KUFIKISHA KILIO CHA WANANCHI WA KIJIJI CHA UPARE WIZARA YA AFYA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoeji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziaraa yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
 Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoeji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziaraa yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba kushoto akichukua kero za wananchi  wa Kijiji cha Kijiji cha Upare Kitongoeji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga wakati wa ziaraa yake kusikiliza kero na kuona namna ya kuzitatua
 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge huyo
  Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba  kushoto akisalimiana na wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao wakati wa ziara yake


UKOSEFU wa Huduma za Afya kwenye Kijiji cha Upare Kitongoeji cha Kibaranga Kata ya Pande Darajani wilayani Muheza mkoani Tanga kumepelekea Mbunge wa Viti Maalumu mkoa huo (Chadema) Yosepher Komba kujitwisha mzigo huo na sasa anakusudia kwenda Wizara ya Afya ili kufikisha kilio hicho.

Hatua ya Mbunge huyo inatokana na kilio cha wananchi hao ambao walieleza kwamba idadi yao ni wakazi zaidi ya 600 wakati wa ziara yake wakieleza tatizo la kukosa zahanati na kulazimika kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Teule.

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kusikiliza kilio hicho alisema kwamba sheria ya Wizara ya Afya kila Kijiji kinapaswa kuwa na Zahanati hivyo ni jukumu la Serikali kuhakikisha kijiji hicho kinapatiwa huduma ya afya ili kuweza kunusuru afya za wananchi wa maeneo hayo hasa kinamama na watoto.

Mbunge huyo alisema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo atakwenda kukutana na Waziri Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ili kumueleza tatizo hilo kwani haiwezekani zaidi ya wananchi 600 katika kijiji hiki wanakosa huduma ya afya hii ni hatari kwa ustawa wa afya zao.

Alisema anashangazwa na viongozi wa Serikali wanaofanya ziara katika maeneo mbalimbali ya wilaya na wanajua tatizo hilo la kutokuwepo kwa huduma hiyo ya afya huku hakuna hatua zozote ziznazochukuliwa ili kuwasaidia wananchi hao.

Alisema ni jukumu la viongozi kutenda haki katika nyanja zote ili kutenda usawa wa huduma za kijamii na kuweka mazingira rafiki ya afya kwa wananchi hao kuliko kusubiria athari zitokee na kuanza kutafuta chanzo.

Awali wakizungumzia hali wananchi wa maeneo hayo alisema wanalazimika kutembea zaidi ya km 12 kuelekea Wilayani Muheza kupata huduma bora ya afya jambo ambalo linahatarisha maisha yao.

Mmoja wa wananchi hao Frednand Francis alisema ipo haja kwa Serikali kupitia Wizara yake kuwahurumia wananchi hao katika suala zima la afya ambayo ndio msingi wa maisha ya mwanadamu.

Francis alisema ni kitu cha ajabu kuona kijiji hicho kilichokuwa na wakazi zaidi ya 600 huku kikosa huduma hiyo ya afya jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao na watoto ambao ndio msingi wa Taifa lijalo.

Hata hivyo alimuomba kuwasaidia kufikisha kilio hicho kwa Waziri mwenye dhama juu ya hali mbaya kukosa huduma ya afya jambo ambalo ambalo linaweza kuleta madhara baadae kutokana na wananchi wengi kuathirika na maradhi.

Mwisho.
Share:

China yaahadi kulipa kisasi dhidi ya ushuru wa Marekani

China imesema  inajitayarisha kuchukua hatua za kulipa kisasi iwapo rais Donald Trump wa Marekani ataendelea na mipango yake ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 mwezi Septemba. 

Nyongeza hiyo ya ushuru wa asilimia 10 ambayo huenda itazilenga bidhaa za elektroniki na mavazi, itamaanisha kuwa karibu bidhaa zote za China zinapelekwa Marekani zitalipiwa kodi.

 Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa China, Hua Chunying, amesema pindi Marekani itaendelea na mipango yake ya kuongeza ushuru, China itajibu kwa kuchukua hatua sawa kulinda maslahi yake. 

Ingawa Chunying hakueleza hatua ambazo nchi hiyo itachukua, afisa huyo amesisitiza kuwa China haitokubali shinikizo, vitisho na ulaghai kutoka Marekani. 

Rais Trump ametishia mara kadhaa kuendelea kuongeza ushuru kwa bidhaa za China ikiwa rais Xi Jinping hatoharakisha mipango ya kufikia makubaliano ya kibiashara


Share:

BRELA KUTOA LESENI ZA BIASHARA DARAJA A KWA WASAFIRISHAJI WA MAZAO NA MIFUGO NJE YA NCHI KWENYE MAONYESHO YA NANE NANE

 Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo kulia akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wananchi aliyefika kwenye banda lao kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu

NAIBU Waziri wa Viwanda Mhandisi Stella Manyanya kulia akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) mara baada ya kutembelea banda lao




WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) wamesema kwamba wameamua kushiriki kwenye maonyesho ya kilimo ya nane nane yanayoendelea mkoani Simiyu kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje 

Hayo yalisemwa na Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela Suzana Senzo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika mkoani Simiyu. 

Alisema wameamua kushiriki kwenye maonyesho hayo hasa ukizingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya nane nane ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja dhima ya kujenga uchumi wa viwanda. 

Suzana alisema hivyo vyote vinaenda sambamba na uwezeshaji biashara huku akieleza lengo kubwa la mfumo ni kuhakikisha wakulima na wazalishaji wa bidhaa nchi wanapata taarifa za mahitaji ya masoko ya nje . 

“Kwa mfano mtu anataka kusafirisha bidhaa kupeleka Ulaya ,ni rahisi sana kupata taarifa hizi katika mfumo wa trade facilitation information module ambapo hapo awali haikuwepo kabisa”Alisema 

Alieleza kwamba wanataka wakulima,wafanyabishara wapate taarifa moja kwa moja kutoka mkoani Simiyu katika viwanja vya nane nane.

Aidha alisema kwa mkoa huo wafugaji wengi hivyo wafugaji ni wengi hivyo ukitaka kujua taarifa zinazohusu vibali na leseni mbalimbali katika kupeleka mifugo yake katika soko la nje ni rahisi kwasababu taarifa zipo ambazo zitamuwezesha kujua nini anahitaji, kwa gharama gani, itachukua muda gani, aendee taasisi gani na iko wapi. 

Aliongeza kwamba kwa mantiki hiyo mfumo huu ni mwarobaini wa tatizo la taarifa za kibiashara katika upatikanaji wa vibali na leseni mbalimbali nchini huku wakiwakaribisha wananchi kufika kwenye banda lao kupata huduma hizo. 

“Lakini pia BRELA tunatoa leseni za kundi A kama zilivyoainishwa katika sheria Leseni za Biashara ya Mwaka 1972 na marekebisho yake…. Leseni za kundi A ni zipi, ni zile leseni zinazotolewa kwa biashara zenye mlengo wa kitaifa, kimataifa na zenye usimamizi maalum, biashara hizi ni kama usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, uingizaji wa bidhaa ndani ya nchi na biashara za usimamizi maalum kama za madini, benki na zingine kama hizo. 

Awali akizungumza Afisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu wa Brela suzana Senso amesema wapo kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuwapasha habari wakulima na wafanyabiashara kupata huduma ya leseni hizi ili kuweza kutoa huduma hata katika masoko ya nje (internatinal market) . 

Hivyo bas mkulima / mfanyabiashara akifika BRELA anapata taarifa za kibishara zaidi katika biashara za kimataifa,asajili kampuni au jina la biashara na anapata leseni itakayomuwezesha kusafirisha bidhaa zake nje ya nchi. 

Hata hivyo alisemwa kwamba kwa matiki hiyo sasa Brela ni one stop shop mfanyabiashara akifika hapa anapata kila kitu kitakachomuwezesha kwenda kufanya biashara duniani. 

Naye kwa upande wake Eliabu Rwabiyago ambaye ni Afisa kutoka Brela amesema wakala pia ina kitengo cha kuwezesha biashara (trade facilitation section) ambacho kimejikita katika uwezeshaji biashara. 

Alisema kwa sasa wakala huo unaandaa portal inayoitwa trade facilitation information module , portal ambayo itajikita katika kutoa taarifa za kibiashara nchini. 

Alisema kwasababu wafanyabiashara wengi nchini na nje ya nchi wanataka kufanyabiashara lakini taarifa za kibiashara kwa maana ya vibali na leseni mbalimbali zinazohitajika zinapatikanaje na kwa muda gani hivyo kwa mtandao hayo maswali yote yamejibiwa. 

Alieleza kwamba kukamilika na kutumika kwa mfumo huu kutakuwa na faida nyingi sana katika uwezeshaji wa biashara ikiwemo kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma za umma, kuiongeza ushirikiano baina ya ofisi za umma na wafanyabiashara maana kwa kutumia mfumo watakuwa wanaweza kaundika maoni na maswali yao kujibiwa moja kwa moja, 

Alisisitiza pia kwamba pia mfumo huu unatumika kama promotional tool kwa maana bidhaa ambazo tunataka ziende duniani kirahisi zinawekwa katika mfumo na wafanyabiashara wanazipata kirahisi, kupunguza gharama za ufanyaji wa biashara na kuboresha mazingira ya biashara kwa ujumla. 

Mpaka sasa BRELA wameweza kuweka taarifa ya bidhaa 26 za kupeleka nje ya nchi (export) na 13 za kuingiza ndani ya nchi (import) 

Mwisho.

Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi 03 August





















Share:

Friday, 2 August 2019

Nuffic Scholarships 2020 for Training Courses at the Hague Academy in the Netherlands (Fully Funded)

Nuffic scholarships are available for short courses at The Hague Academy. Nuffic is a Dutch non-profit organisation which offers scholarships for training courses in The Netherlands. These scholarships seek to develop and strengthen the skills and abilities of professionals, in order to enable their organisations and communities to succeed in an ever-changing world. The Dutch Ministry of Foreign… Read More »

The post Nuffic Scholarships 2020 for Training Courses at the Hague Academy in the Netherlands (Fully Funded) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Holland Scholarships 2020/2021 for Bachelor’s or Masters Study in the Netherlands (5,000 Euros)

Holland Scholarships 2020/2021 for Bachelor’s or Masters Study in the Netherlands (5,000 Euros) The Holland Scholarship is meant for international students from outside the European Economic Area (EEA) who want to do their bachelor’s or master’s in the Netherlands. Are you ready for the chance of a lifetime? Apply for the Holland Scholarship! This scholarship is financed by… Read More »

The post Holland Scholarships 2020/2021 for Bachelor’s or Masters Study in the Netherlands (5,000 Euros) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

International Women’s Media Foundation (IWMF) Howard G. Buffett Fund for Women Journalists 2019 Round 2

International Women’s Media Foundation (IWMF) Howard G. Buffett Fund for Women Journalists 2019 Round 2 Promoting the work and advancing the role of women in the news media across the globe is critical to transparency and a diversity of voices. The Howard G. Buffett Fund for Women Journalists, the first funding initiative of its kind, enables the IWMF… Read More »

The post International Women’s Media Foundation (IWMF) Howard G. Buffett Fund for Women Journalists 2019 Round 2 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Rais Uhuru Kenyatta apokea Tausi wanne Aliopewa na Rais Magufuli

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana leo August 2 amemkabidhi Rais Uhuru Kenyatta zawadi ya Tausi 4 aliyopewa na Rais Magufuli alipomtembelea Chato.

Akipokea Tausi hao Kenyatta amesema hiyo ni ishara tosha ya umoja, upendo na undugu uliopo kati ya Kenya na Tanzania.


Share:

Mwanaharakati Stella Nyanzi Ahukumiwa Kifuyngo cha miezi 18 kwa kumtusi Rais Museveni Wa Uganda

Mwanaharakati msomi wa Uganda Dkt. Stella Nyanzi amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.

Nyanzi amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kimtandao dhidi ya Rais Yoweri Museveni na familia yake.

Dr. Nyanzi alikataa kumsikiliza hakimu akisoma hukumu dhidi yake na badala yake kufanya vurugu kwa kuvua nguo na kuonesha sehemu ya mwili wake.

Mwanaharakati huyo hakuwa mahakamani lakini hukumu dhidi yake ilitolewa kupitia video link kutoka jela.

Wakati kesi ikiendelea Bi. Stela alikataa kuomba dhamana na amekuwa katika gereza kuu la Uganda la Luzira kwa miezi minane. Sasa atazuiliwa gerezani kwa miezi tisa zaidi.


Share:

Marekani Yamuwekea Vikwazo Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania

Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Brigedia Jen. Mstaafu, Anselem Sanyatwe amewekewa vikwazo  na Marekani kufuatia kuhusika katika vifo vya raia 6 waliokuwa wakiandamana Agosti 2018 kushinikiza kutangazwa matokeo ya uchaguzi. 

Hata hivyo, Zimbabawe imeleza kutofurahishwa na  hatua hiyo  ya Marekani kumuekea vikwazo Anselem  Sanyatwe

Katika taarifa yake, serikali ya Harare imeitaja hatua hiyo ya Marekani kama inayodunisha uhuru wa taifa hilo na ambayo inashinikiza migawanyiko badala ya kuidhinisha uponyaji wa taifa na maelewano.

Wizara ya mambo ya nje Marekani ilitangaza vikwazo dhidi ya Balozi Sanyatwe, ambaye ni Brigedia mstaafu ya jeshi la kitaifa la ulinzi wa rais, kutokana na kuhusika kwake katika ukiukaji mkubwa wa haki za binaadamu.

Wizara hiyo Marekani imefafanua kuwa ina taarifa za kuaminika kwamba Anselem Sanyatwe alihusika katika msako mkali dhidi ya raia Zimbabwe ambao walikuwa hawakujihami wakati wa ghasia zilizozuka mnamo Agosti mosi mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu, uliosababisha vifo vya raia sita.


Share:

Lugola Apiga marufuku Bajaji na Bodaboda kulipishwa faini papo kwa papo

Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amepiga marufuku Bajaji na Bodaboda kulipishwa faini papo kwa papo wanapofanya makosa ya barabarani badala yake amewataka Polisi kutoa siku 7 kama wanavyofanya kwa magari

Lugola ameyasema hayo katika mkutano wa Wamiliki na Waendeshaji wa vyombo hivyo, Mjini Moshi, leo.


Share:

Spika Ndugai Aipigia Chapuo Utalii Wa Fukwe Za Pwani Ya Bahari Ya Hindi

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametoa wito kwa Serikali  kuendeleza utalii wa Pwani ya Bahari ya Hindi, hatua itakayosaidia kuchochea ukuaji wa  utalii nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana alhamisi (Agosti Mosi, 2019), Ndugai alisema Tanzania ina kila sababu ya kuendeleza fukwe hizo kutokana na ukweli kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi za fukwe na bahari zilizo bora kuliko nchi yoyote ndani ya bara la Afrika.

Spika Ndugai aliongeza kuwa uendelezaji wa fukwe hizo  utasaidia nchi kwa kiasi kikubwa kupiga hatua na  kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Sisi hapa Tanzania tuna pwani ya bahari nzuri zaidi kuliko pwani zingine popote pale Afrika, hizi ni hifadhi za mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, kuanzia Pangani mpaka Mtwara ambazo hazijatumika vizuri.” Alisema Spika Ndugai

Aidha Spika Ndugai aliongeza  fukwe hizo zikitumika vizuri zitasaidia kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kuoanishwa vizuri kwa utalii wa pwani na ule wa bara na hivyo kuifanya sekta ya utalii kuongeza wigo mwingine wa mtandao wa mapato nchini.

Akizitaja sababu zilizopelekea utalii kutoonekana vizuri, Spika Ndugai alisema moja ya sababu kubwa inayochangia sekta ya  utalii  kutokufanyika vizuri ni kwa kuwa utalii wa fukwe za bahari bado uko chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Aidha katika kuonyesha umuhimu wa kuendeleza fukwe hizo, Ndugai aliyataja maeneo ya Mombasa, Lamu na Malindi nchini Kenya kama maeneo ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendeleza fukwe katika Pwani zao, ambapo zimesaidia kuchochea ongezeko la watalii katika maeneo hayo.

“Kwenye Pwani zao kwa sasa kuna utalii maarufu unaofanyika baharini, unaofahamika kama ‘Marine Parks tourism’, ndio maana ukiangalia Pwani yao imejaa hotel, na sisi hapa kwetu tukitumia fukwe zetu vizuri tunaweza kuwa na utalii mzuri zaidi wa namna hii utakaosaidia kuongeza idadi ya watalii nchini”. Alisema Spika Ndugai.

Pia Spika Ndugai alimshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuamua kuipandisha hadhi iliyokuwa sehemu ya pori la akiba la Selous Game Reserve’ kuwa hifadhi kamili itakayojulikana kama Hifadhi ya Taifa ya Nyerere  au ‘Nyerere National Park’.

Akizungumzia kuhusu suala hilo Rais Magufuli alisema pendekezo la  kuendeleza fukwe  za pwani ya Bahari ya Hindi ni moja ya vipaumbele vya Serikali kwa sasa, na kumuagiza Waziri Mkuu , Kasim Majaliwa   kuangalia jinsi ya kuendeleza  fukwe zote kuanzia Moa hadi Msimbati.

MWISHO


Share:

Safari za mabasi masaa 24 kwa Baadhi ya Mikoa zasitishwa

Jeshi la Polisi nchini limezuia safari za saa 24 za mabasi kwa baadhi ya mikoa kwa sababu ya kiusalama na kuwataka wamiliki wa mabasi hayo kuzingatia maagizo yaliyotolewa ili kulinda usalama wa wananchi.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 2 na Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo, Liberatus Sabas ambapo amesema licha ya kuruhusu  mabasi yote nchini kutembea usiku bila kulala sehemu yoyote, Jeshi la polisi limebaini kuna baadhi ya maeneo zoezi hilo limebidi lisubiri kidogo ili wajipange kwa ajili ya usalama na watakapojiridhisha safari hizo zitaendelea kama kawaida.

Sabas amesema mabasi yanayotoka  Dar es Salaam kuelekea Mikoa ya Kagera, Kigoma, Katavi hayataruhusiwa kutembea saa 24 kutokana na sababu za kiusalama.

Kamishna Sabas amesema zuio hilo litahusu pia mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea wilaya mbalimbali za mkoani Tabora ambayo yatalazimika kusimama Tabora Mjini na baadaye kuendelea na safari wilayani.

Amesema  mabasi yanayotoka mikoa ya Kagera, Katavi, Kigoma kwenda Dar es Salaam yataruhusiwa kutembea saa 24 kama kawaida kutokana na eneo la Morogoro na Dar es Salaam kuwa salama wakati wote.

"Mabasi haya yalikuwa yakitoka kwenye mikoa hiyo yalikuwa yanalala Morogoro, lakini kutokana na hali nzuri ya kiusalama yataendelea na safari hadi Dar es Salaam," amesema Kamishna Sabas.

Amesema mabasi yanayotoka Dar es Salaam kuelekea katika mikoa hiyo yatalazimika kulala wilayani Kahama kisha kuendelea na safari.


Share:

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Atoa Maagizo Mazito Jeshi la Polisi

Na Mwandishi Wetu, MOHA
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuboresha mazingira ya huduma wanazotoa kwa wananchi.
 
Alisema ni wajibu wa jeshi hilo kutoa elimu kwa jamii iweze kufahamu hatua za kufuata pindi wanapotaka kuwawekea dhamana ndugu zao waliopo katika vituo vya polisi.
 
Kailima aliyasema hayo hayo jana alipofanya ziara ya kutembelea vituo vinne vya polisi mkoani Dodoma.
 
Lengo la ziara hiyo iliyoandaliwa na Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko Ndani ya Wizara hiyo ni kuangalia utendaji kazi wa jeshi hilo juu ya huduma wanazotoa kwa wananchi.
 
Vituo alivyotembelea ni vile vilivyopo katika Wilaya ya Dodoma Mjini ambavyo ni Kituo Kikuu (Central), Chang’ombe, Nkuhungu na Kikosi cha Usalama Barabarani.
 
Katika ziara hiyo, Kailima aliambatana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, Kamishna wa Polisi, Albert Nyamuhanga pamoja na Maafisa wengine wa kitengo hicho.

Akiwa kwenye kituo Kikuu cha Polisi (Central), Kailima alikuta idadi kubwa ya watu waliokuwa na shida mbalimbali, alitumia fursa hiyo kuzungumza nao na kuwataka waeleze kero zao.
 
Baada ya kuzungumza na wananchi, Kailima aliushauri uongozi wa kituo hicho kuweka mazingira mazuri ya kutoa huduma ili kuondoa mrundikano wa wananchi nje, ndani ya kituo.
 
“Wekeni mazingira mazuri ya mwananchi mmoja kuhudumiwa na askari mmoja kutokana na idadi ya askari ambao watakuwa zamu ili kupunguza msongamano,” alishauri.
 
Aliongeza kuwa; “Toeni elimu inayohusu dhamana kwa jamii ili wananchi wajipange kabla ya kuja kituoni, unakuta watu wengi wanakuja kuwawekea dhamana ndugu zao bila kujua taratibu hivyo kusababisha wajazane kituoni bila sababu,” alisisitiza.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Dodoma, Pipi Kayumba, alisema katika utendaji kazi wake, kila siku anapita kituoni hapo ili kuonana na wananchi anaowakuta kituoni, kusikiliza shida zao.
 
Alishauri ili jeshi hilo liweze kuboresha huduma zake, kuwepo vituo vya polisi katika njia zote za kuingia jijini Dodoma kwani jiji hilo limekuwa kubwa, idadi ya watu imeongezeka.
 
“Kwa sababu ya ongezeko kubwa la watu, hata utoaji huduma nao umekuwa mkubwa, kuanzishwa kwa vituo hivyo litakuwa jambo jema kwa Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla,” alisema.
 
Kwa upande wake, Kamishna Nyamuhanga alishauri Mkuu wa Kituo hicho, Kidwadi Karinga, aweke mkakati wa kuondoa malalamiko ya wananchi kwenye kituo hicho.
 
Kailima aliendelea na ziara yake kwenye Kituo cha Kikosi cha Usalama Barabarani, kuzungumza na wananchi waliodai kuna mtu ambaye si askari  alikuwa akitoa taarifa ya upotevu wa mali (loss report).
 
Mtu huyo alikuwa akitoa taarifa hiyo nje ya kituo hicho kwa gharama kubwa wakati gharama halisi ni sh. 500 tu, hulipwa kwa utaratibu uliowekwa na kupewa lisiti.
 
Kailima alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa lengo la ziara hiyo ni kujionea mazingira ya kazi za askari kwa jamii ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
 
Alimpongeza Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Nuru Selemani kwa kutekeleza agizo la Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola juu ya kuziondoa pikipiki zilizokamatwa kwa makosa mbalimbali.
 
“Wasisitize askari wako waache kuomba na kupokea rushwa, kutobambika kesi kwa wananchi, askari kutumia lugha nzuri, kuelimisha wananchi wanapofanya kosa, kutoa elimu katika  redio namna ya kuvuka kwenye zebra, kutoa taarifa kuhusu hali ya mji kila siku,” alisisitiza Kailima.
 
Aliwataka askari wa Usalama Barabarani wafanye operation kubwa mara moja kwa mwezi ili kufanya wepesi wa kukusanya maduhuli ya serikali, kutimiza wajibu wao wawapo kazini na wanaokwenda tofauti wachukuliwe hatua stahiki.
 
Alisisitiza suala la usalama hasa kipindi hiki ambacho kuna ugeni wa Mkutano wa SADC kuanzia Agosti 5, mwaka huu, hivyo kama chombo cha usalama wamuunge mkono Rais Dkt. John Magufuli.
 
Pia Kailima alitembelea Kituo cha Chang’ombe kinachohudumia kata tatu za Chamwino, Chang’ombe na Chinangali ambapo hali ya usalama si nzuri kutokana na matukio ya wizi, unyang’anyi.
 
Matukio hayo yamelifanya jeshi hilo kufanya msako mkali na tayari baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.
 
Kailima aliushaurio uongozi wa kituo hicho na askari kuitumia jamii au serikali za mitaa ili kupata taarifa za wahalifu.
 
Mkuu wa kituo hicho, Emanuel Mawi, alisema kuna doria inafanyika maeneo mbalimbali, pia wanashirikiana na jamii, changamoto waliyonayo ni udogo wa kituo ambacho kinahudumia eneo kubwa.
 
Akiwa kwenye Kituo cha Nkuhunga, Kailima aliambiwa kituo hicho kinahudumia kata mbili za Nkuhungu na Kizota.
 
Akiwa kituoni hapo, Kialima aliambiwa kituo hakilazi mahabusu ambao hupelekwa Kituo Kikuu (Central).
 
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Dodoma, Kayumba alisema changamoto waliyonayo ni uchache wa magari kwa ajili ya doria za kila siku.
 
Kailima aliwapongeza Kayumba na Karinga kwa kazi kubwa wanayoifanya.
 
Kwa upande wake, Kamishna Nyamuhanga, alimshukuru Kailima na kumuahidi kuwa, watatekeleza maelekezo yote aliyotoa katika ziara hiyo ili kuboresha utendaji kazi.
MWISHO.


Share:

AUAWA KWA KUPIGWA MSHALE SEHEMU ZA SIRI UGOMVI WA POMBE


Na Asha Shaban - Malunde1 blog Mara
Mtu mmoja ambae jina lake halijafahamika amefariki dunia kwa kupigwa na mshale sehemu zake za siri na wengine wawili kujeruhiwa kwa mishale hiyo na mtuhumiwa ajulikanae kwa jina la Mtunde kwa kosa la kunyimwa pombe kwenye sherehe huko katika kitongoji cha Nyamakendo wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Juma Ndaki alisema tukio hilo lilitokea Julai 28,2019 majira ya saa 2 usiku katika kitongoji hicho ambapo mtuhumiwa alitenda kosa hilo wakati wa sherehe ya ugeni kwa baba yake wa kufikia akiwa anadai kupewa pombe.

Alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo mtuhumiwa alishapewa pombe aina ya bia chupa mbili na kudai kuongezewa pombe hizo ndipo baba mlezi ajulikanae kwa jina Juma Joseph alipomkatalia na kumwambia pombe zilizobakia ni za wageni.

Aliongeza kusema kuwa "Baada ya kujibiwa hivyo mtuhumiwa huyo alichukia na kuanza kumfokea baba yake huyo kuwa ni mchoyo huku akisistiza kuwa kabila la kisukuma ni la uchoyo na kumtolea kauli ya kuwa utaona lakini kauli hiyo baba hakuiwekea maanani.

"Kijana huyo aliondoka na kisha kurejea majira hayo ya saa mbili usiku na kukuta watu wakiwa wamekaa wakiendelea na sherehe ndipo alipoanza kuirusha mishale hiyo kwa kutumia upinde na kufanikisha kumuua mwanamke huyo mmoja na kujeruhi wengine wawili",alieleza.

Alisema waliojeruhiwa katika tukio hilo ni baba mlezi wa kijana huyo Juma Joseph ambaye alipigwa mshale katika mguu wake wa kushoto mwingine aliyejeruhiwa alifahamika kwa jina moja la Meng'anyi (74),mkulima alijeruhiwa katika titi lake la kushoto na majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya DDH ya Wilayani Serengeti mkoni Mara.

Aidha kamanda ndaki alisema mtuhumiwa alipotenda kosa hilo alikimbilia nchi jirani ya Kenya ambapo alisema juhudi za kumsaka zinaendelea kwa kushirikiana na askari wa nchi jirani ya Kenya na pindi atakapokamatwa atafikishwa katika vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho kwa watu wengine.

Share:

MAJAMBAZI WAVAMIA MSIBA NA KUPORA FEDHA ZA KUNUNULIA JENEZA LA MAREHEMU

Familia moja katika eneo bunge la Kinangop, Kaunti ya Nyandarua,nchini Kenya iliyokuwa ikiomboleza ilipata majonzi zaidi baada ya kuvamiwa na majambazi walioiba Sh18,000 zilizokuwa zimetengewa ununuzi wa jeneza la kuzika marehemu. 

Kwa mujibu wa Taifa Leo, Rufa Thiga, mkewe na nduguye walivamiwa na majambazi sita mnamo Jumatano usiku, Julai, 27,2019 saa chache tu baada ya wageni waliofika kuomboleza kifo cha dada yao kuondoka.

Mke wa Thiga, Margaret Wambui na nduguye Benson Kigo walijeruhiwa kwenye kisa hicho. Thiga alisimulia jinsi alivyowasikia majambazi hao waking’ang’ana kuvunja lango kuu la kuingia boma lake na jinsi jaribio lake la kutorokea mlango wa nyuma lilivyogonga mwamba. 

“Nilipojaribu kutorokea mlango wa nyuma, watu wawili walinivamia kwa panga huku wengine wakiingia ndani ya nyumba na kumpiga mke wangu kwa silaha butu,” Thika alisema.

Simulizi hiyo inaendelea kwa kusema kuwa, baada ya hapo majambazi hao walimwagiza aingie ndani ya nyumba na awakabidhi pesa alizokuwa amekusanya kugharimia mazishi ya dadake.

 “Walinilazimisha kuingia ndani ya nyumba niwape pesa za matanga. Niliwapa KSh 18,000 ambazo zilikuwa zimetengewa ununuzi wa jeneza la marehemu,” akaongeza kusema. 

Wambui naye kwa masikitiko alisimulia jinsi majambazi hao walivyomfuata hadi kwenye bafu na kumpiga wakidai awape pesa.

“Walitishia kuua familia yote. Nilipata majeraha kwenye mikono, mgongo na kichwani,” akasema. Kigo naye alisema kuwa wezi hao walimlazimisha aingie ndani ya nyumba na akawapa KSh 3,000 ili kuyanusuru maisha yake.

 “Walinieleza kwamba walikuwa maafisa wa polisi kabla ya kunipiga kichwani na kuniamrisha nilale chini,” alisema. 

Haijulikani kufikia sasa ikiwa familia ya Thiga ilifanikiwa kupata pesa zingine na kuuzika mwili wa marehemu.
Via>>Tuko
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger