Sunday, 26 May 2019

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo Na Rais Wa Afrika Kusini Ikulu Ya Pretoria

Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumapili Mei 26, 2019, amekutana na kufanya mazungujza na Rais  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Ikulu Jijini Pretoria.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amempongeza Rais huyo kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amemhakikishia kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria na nchi hiyo.

 Rais Magufuli amaesema uhusiano wa Tanzania na nchi hiyo uliasisiwa na Baba wa Taifa wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Nyerere na hayati Nelson Mandela kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ANC (African National Congress).

Amemwambia kuwa ni matarajio yake kuona uhusiano huo unaimarishwa zaidi katika nyanja za uchumi na kukuza lugha ya  Kiswahili.

Rais huyo wa Tanzania, amemshukuru Ramaphosa kwa kumkaribisha na kufanya naye mazungumzo ya siku moja baada ya kuapishwa kwake.

Kwa upande wake, Rais Ramaphosa naye amemshukuru Magufuli kwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake na amemhakikishia kuwa Afrika Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika ukombozi wa Taifa hilo.

Hivyo, amemuahidi katika kipindi chake cha uongozi atauendeleza na kukuza zaidi uhusiano huo.

Rais Ramaphosa amesema kufuatia uamuzi wa Afrika Kusini kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo katika shule za msingi na sekondari.

Aidha, ameahidi kufanya ziara rasmi ya Tanzania kabla ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), uliopangwa kufanyika Agosti 2019 nchini Tanzania. Pia, atahudhuria mkutano huo.

Kabla ya mazungumzo hayo,  Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alimkabidhi Ramaphosa zawadi ya vitabu vya kusoma na kufundishia lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Marais hao wawili wamefanya  mazungumzo hayo ikiwa ni kabla ya  Rais Ramaphosa hajatangaza Baraza lake la Mawaziri.

Kesho, Rais Magufuli ataondoka Afrika Kusini kuelekea nchini Namibia ambako atafanya ziara rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Namibia, Hage Geingob.


Share:

MAFURIKO YALETA KIZAAZAA BUKOBA


Mvua iliyonyesha leo asubuhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera ukiwemo Mji wa Bukoba, imesababisha maafa makubwa ikiwamo kuingia katika makazi ya watu, na madaraja kujaa maji hali iliyosababisha wananchi kushindwa kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine.

Maeneo yaliyozingirwa na maji ni pamoja na Omukigusha, Kyakailabwa, Hamugembe, Buyekera na Kagondo, lakini hadi sasa hasara iliyosababishwa na mvua hiyo bado haijafahamika, huku mali zinazoonekana kuathirika zaidi zikiwa ni nyumba na vitu vya ndani.

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba wamesema mafuriko hayo yametokana na baadhi ya wananchi kujenga kandokando ya mito hivyo kubana mkondo wa maji matokeo yake maji kushindwa kutiririka vizuri.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo amesema hivi sasa wamezuia wananchi wasijaribu kuvuka kwenye madaraja yaliyojaa maji kwenda popote ili kuepuka madhara zaidi.
Share:

Picha : RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA IKULU YA PRETORIA NCHINI AFRIKA KUSINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchiniAfrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifanya Mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya wanyama Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili na Kiingereza pamoja na vitabu vya Kiswahili Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa kwa ajili ya kujifunza lugha hiyo ya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu vitabu hivyo vya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza RaiswaAfrikaKusiniMheshimiwa Cyril RamaphosamarabaadayamazungumzoyaokatikaIkuluya Pretoria nchiniAfrikaKusinileo Mei 26, 2019 ikiwanisikumojabaadayakuapishwakuwaRaiswaNchihiyonakablahajateuaBaraza lake la Mawaziri. 







 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa
 PICHA NA IKULU
Share:

WANAFUNZI WAWILI SHULE SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WATEULIWA KULIWAKILISHA TAIFA KONGAMANO LA DUNIA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Festo Mgina (kulia) akiwakabidhi bendera ya Taifa jana wanafunzi wa shule ya msingi Southern Highlands Mafinga kwa ajili ya wenzao wawili walioteuliwa kuliwakilisha Taifa katika kongamano la mazingira duniani linalofanyika nchini Finland nkushoto kwake ni mkurugenzi wa shule hiyo ambae ni mkuu wa msafara wa wanafunzi hao Kitova Mungai
**

Na Francis Godwin, Iringa 

Uongozi wa serikali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umesema umepokea kwa heshima kubwa mwaliko wa wanafunzi wawili wa shule ya msingi Southern Highlands Mafinga ambao wamepata mwaliko wa kuliwakilisha Taifa nchini Finland katika kongamano la wanafunzi dunia wanaojali mazingira.

Akizungumza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa wanafunzi hao na kiongozi wao jana kwa niba ya serikali ya wilaya ya wilaya ya Mufindi mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi Festo Mgina alisema kuwa heshima ambayo shule hiyo ya Southern Highnalnds Mafinga imepata ni kubwa kwa wilaya ,mkoa na Taifa kwa ujumla. .
“ Huu ni mwaliko wa heshima kubwa kwa wilaya yetu na mkoa lakini kwa Taifa letu kualikwa katika kongamano kubwa kama hili la kujadili masuala ya mazingira duniani heshima hii sisi kama viongozi tunajivunia na tunapongeza shule kwa kuteuliwa kuwakilisha Taifa “ alisema Mgina.

Kuwa mwaliko huo umekuja wakati Taifa liko katika harakati ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hata kuanza mchakato wa kuondoa sokoni mifuko ya rambo ambayo ni moja ya vikwazo vya mazingira .

HIvyo aliagiza wakuu wa shule za msingi katika wilaya ya Mufindi kuhakikisha wanafika katika shule ya Southern Highnalnds Mafinga ili kujifunza yale ambayo wanafunzi hao wawili watarudi nayo kutoka katika mkutano huo mkubwa nchini Finland.

“tunataka elimu na aagizo ambayo yatatolewa katika mkutano huo wa dunia nchini Finland vijana hao wakirudi basi kuweza kusambaza kwa wenzao kwenye shule zetu zote za Mufindi ikiwa ni pamoja na wakuu wa shule kufika kujifunza ili kila shule kuweza kujifunza elimu hiyo kwa faida ya mazingira ya maeneo yao “ alisema Mgina.

KIongozi wa wanafunzi hao nchini Finland ,mkurugenzi wa shule hiyo ya Southern Highnalnds Mafinga Kitova Mungai alisema kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule wanachama wa Klabu za mazingira duniani na kuteuliwa kwa wanafunzi hao kumetokana na ziara ya waratibu wa kongamano hilo ambao walifika kupema uwezo wa klabu zote nchini.

Hivyo baada ya kuvutiwa na jitihada zinazofanywa na klabu ya shule yake katika utoaji wa elimu ya mazingira na ufundishaji wa masomo ya ujasiliamali kwa wanafunzi ndipo wameweza kutuma mwaliko kwa wanafunzi wawili na kiongozi mmoja ambao watakwenda kushiriki kongamano hilo kwa muda wa siku 10 safari ambayo itaanza jumanne wiki hii.

‘’ Tunategemea kukutana na wawakilishi kutoka nchi mbali mbali duniani kama china ,Japan, Brazil ,Marekani ,China ,Uganda , Kenya na nchi nyingine nyingi ila tunaimani kubwa ya kuwakilisha vema Tanzania kwani watoto ambao wamechaguliwa kwenda katika kongamano hilo wanauwezo mkubwa sana katika elimu ya mazingira “ alisema Mungai.

Alisema watoto hao na wenzao wamekuwa mbele kuhifadhi mazingira ya Shule ikiwa ni pamoja na uoteshaji wa miche ya miti na kuipata shuleni hapo na majumbani kwao na kwao suala la uhifadhi wa mazingira ni shughuli yao ambao hata wakipewa nafasi ya kufundisha wenzao wamekuwa wakifanya vizuri.

Mungai alisema kuwa Tanzania ni imekuwa mbele katika vita dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi na kuwa hata mkakati wa serikali wa kuzuia mifuko ya rambo ni mkakati ambao wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa namna ya kutunza mazingira pasipo kutumia mifuko hatarishi ya mazingira na kuwa kupitia kongamano hilo watapata kuwasilisha mbinu mbali mbali za utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wao wanafunzi watakaowakilisha Taifa katika kongamano hilo Maria Wambura na Stephen Sanga ambao ni wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo walisema kuwa kuteuliwa kwao katika kongamano hilo si nafasi ya bahati mbaya kwani wanauhakika wa kuliwakilisha vizuri Taifa katika kongamano hilo na kile ambacho watakipata watakuja kutumia kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao nchini .
Share:

JIMAMA LAFUMANIWA LIVE LIKIHONDOMOLA TENDO LA NDOA NA MTOTO WA DARASA LA SABA

Kizaazaa kimeshuhudiwa katika kijiji cha Mwangorisi, eneo bunge la Mugirango Magharibi, Kaunti ya Nyamira nchini Kenya baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 45 kufumaniwa akishiriki uroda na mvulana mwenye umri wa miaka 14. 

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, Angeline Osebe ambaye anafahamika kuwa kahaba alimnyemelea mvulana huyo wa darasa la 7 katika nyumba yao ya kulala Alhamisi, Mei 23 kisha kumshawishi kushiriki naye tendo hilo.

Wakazi waliokuwa na hasira walimvamia na kumpiga Osebe kabla ya kuokolewa na Wasamaria wema.

Mkazi mmoja kwa jina Erick Omwenga alimwona mwanamke huyo akiingia katika nyumba ya mvulana huyo jioni na kuwafahamisha wanakijiji ambao walifika na kumfumania akiwa uchi kitandani na mvulana huyo mdogo wakihondomolana. 

"Huwalenga sana wavulana wadogo, mkazi wa hapa alimwona akiingia katika nyumba ya mvulana huyo jioni na hakutoka. 

Alituita na tulipofika tulimpata akishiriki ngono naye," Omwenga alisema. 

Inaelezwa kuwa, wazazi wa mvulana huyo hawakuwapo nyumbani wakati wa kisa hicho na Hata hivyo alipokea kichapo kidogo kutoka kwa.

 Kamishona wa kaunti ya Nyamira Bw. Amos Mariba alithibitisha kisa hicho cha fedheha na cha kushangaza na kumshauri mwanamke huyo kutafuta wanaume wa rika lake kushiriki nao ngono badala ya kufuata wavulana wadogo.

 Wanawake wanaofanya biashara ya ngono ni lazima kuacha kufuatana na wavulana wadogo. Watafute wanaume wa umri wao badala ya watoto wachanga," Mariba alisema. 

Kulingana na kamishna, Asebe atafikishwa kortini mara uchunguzi ukikamilka ili uwe mfano kwa wengine wenye tabia ya aina hiyo.

Uchunguzi zaidi kuhusu kisa hicho unaendelea kwa sasa huku mwanamke huyo akiendelea kukaa seli. 

Ripoti ya Edwin Mwanambee, Kaunti ya Nyamira. 
Chanzo - Tuko
Share:

CHUO CHA TANGANYIKA POLYTECHNIC ARUSHA CHAWAPA WAJASIRIAMALI MAFUNZO YA KUTENGENEZA MIFUKO YA KARATASI


Meneja wa Sido mkoa wa Arusha,Uongozi wa Chuo pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kutengeneza mifuko ya karatasi wakiwa katika picha ya pamoja. 
Wanakikundi kutoka eneo la Lemara jijini Arusha waliopata mafunzo ya muda mfupi ya kutengeneza mifuko ya karatasi ili kuendana na sera ya serikali kuondoa matumizi ya mifuko ya nailoni,mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic jijini Arusha. 
Wanakikundi kutoka eneo la Lemara jijini Arusha waliopata mafunzo ya muda mfupi ya kutengeneza mifuko ya karatasi ili kuendana na sera ya serikali kuondoa matumizi ya mifuko ya nailoni,mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic jijini Arusha. 
Mmoja wa walionufaika na mafunzo ya kutengeneza mifuko ya karatasi katika Chuo cha Tanganyika Polytechnic ,Bakari Juma akitoa ushuhuda namna inavyomwingizia kipato kutokana na mahitaji kuongezeka. 
Meneja wa shirika la Sido mkoa wa Arusha,Nina Nchimbi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali wa kutengeneza mifuko ya karatasi ,kushoto ni Mkurugenzi wa ubunifu wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic kilichota mafunzo hayo,Dk Richard Masika na Mkuu wa Chuo,Abdul Semvua. 
Mkurugenzi wa ubunifu wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic kilichopo Njiro,Dk Richard Masika akizungumza katika hafla hiyo. 
Share:

Mahakama yaamuru kura kuhesabiwa upya Malawi

Mahakama nchini Malawi imeiamuru tume ya uchaguzi kutotangaza matokeo ya uchaguzi wa rais wa Mei 21 kufuatia malalamiko ya wizi wa kura yaliyotolewa na upinzani. 

Katika amri hiyo, Mahakama Kuu ilitaka kusitishwa utangazaji wa matokeo ya kura ya rais na kuelekeza kuhesabiwa upya kwa kura za theluthi ya maeneo yaliyoshiriki uchaguzi. 

Tume ya uchaguzi nchini humo ilisimamisha kutangaza matokeo hayo baada ya kupokea malalamiko 147 kutoka kwa baadhi ya vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo wa Jumanne iliyopita. 

Chama kikuu cha upinzani cha Malawi Congress (MCP) kinachoongozwa na Lazarus Chakwera, kiliwasilisha malalamiko mahakamani juu ya kile ilichodai kuwa makosa yaliyojitokeza katika wilaya 10 kati ya 28 nchini humo. 

Ujumbe wa Waangalizi wa Umoja wa Ulaya uliueleza uchaguzi huo kuwa ulisimamiwa vizuri, ulikuwa na uwazi pamoja na ushindani mkali.


Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

Iran yaapa kujilinda kwa nguvu zote dhidi ya uchokozi

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Mohammad Javad Zarif, amesema nchi yake itajilinda kwa nguvu zote dhidi ya uchokozi wa kijeshi na kiuchumi, huku akizitolea wito nchi za Ulaya kuchukua hatua zaidi kuyanusuru makubaliano ya nyuklia waliyotia saini. 

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Baghdad, Iraq, hivi leo, Zarif amesema nchi yake inataka kujenga mahusiano ya usawa na jirani zake wa eneo la Ghuba na imekwishapendekeza kutiwa saini mkataba wa kuepuka uchokozi.

 Wakati huo huo, Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria kuwa Iran inaweza kuitisha kura ya maoni kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo kufuatia kuongezeka mvutano kati yake na Marekani. 

Rouhani amesema amewahi kupendekeza suala hilo kwa Kiongozi  Mkuu Ayotallah Ali Khamenei mwaka 2004 alipokua mjumbe mwandamizi kwenye mazungumzo ya nyuklia. 

Kura hiyo ya maoni itaipa serikali ya Iran uhalali wa kisiasa iwapo itaamua kuongeza urutubishaji wa madini ya urani unaozuiwa chini ya makubaliano ya 2015 na mataifa yenye nguvu.


Share:

Wakurugenzi wa Halmashauri 10 Watakiwa Kuhakikisha Mradi wa Timiza Ndoto Yako Unatekelezwa Kikamilifu

Na Mwandishi Wetu
Wakurugenzi 10 wa Halmashauri za Wilaya wametakiwa Kuhakikisha kuwa mradi wa timiza ndoto zako kwa wasichana Balehe waliopo mashuleni na walio nje ya mfumo wa elimu unatekelezwa kama ilivyopangwa na Serikali ili kuleta matokeo chanya.
 
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Mei 25, 2019 Wilayani Bahi mkoani Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Katibu Mkuu Ofisi hiyo anayeshughulikia Sera Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona mradi huo unaleta ukombozi wa kweli kwa mtoto wa kike.
 
“ Waliopo shuleni na nje ya mfumo wa elimu ni vyema mkatambua kuwa mradi huu ni fursa yakuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuepeuka vishawishi na maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwani Serikali inatambua kuwa kumuwezesha mtoto wa kike ni kuiwezesha jamii nzima”Alisema Bi. Doorthy.
 
Mradi huu unatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida ambapo jumla ya Halmashuri 10 katika mikoa hiyo zinanufaika.Utekelezaji wake unatokana na usaidizi wa fedha kutoka kutoka Mfuko wa Dunia kwa ajili ya kuendeleza
mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na athari zake.
 
Akifafanua amesema kuwa watekelezaji wa mradi huo wanalo jukumu la kuwajengea uwezo wanaufaika ili hata baada ya kipindi cha mradi waweze kujitegemea na kuondokana na utegemezi kutoka kwa serikali ambapo kwa sasa wanafunzi kutoka Kaya masikini wanawezeshwa kupata taulo za kujisitiri pamoja na mahitaji mengine ikiwemo sare za shule.
 
Aliongeza kuwa wanafunzi wote wanapaswa kutambua kuwa
Serikali inawekeza fedha nyingi katika mradi huo kwa kutambua umuhimu wa kundi hilo ili kujikwamua kielimu na kutumia vyema vipaji walivyo navyo.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanamisi
Mukunda akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amasema kuwa mradi huo umesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo, mahudhurio ya wanafunzi shuleni yameongezeka kwa kiwango kikubwa.
 
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutuletea mradi huu katika Wilaya yetu kwani umeonesha mafanikio makubwa kwa kipindi cha majaribio ambacho umetekelezwa kwani umewanufaisha Wanawake Vijana wenye umri wa kati ya miaka 10- 24”, alisisitiza Mhe. Mwanahamisi.
 
Akifafanua amesema kuwa mradi huo umefikia Kaya 265 na
wasichana 129 unawanufaisha wasichana balehe waliopo shuleni na wale wa nje ya shule 45.
 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa mradi huo ni wa miaka 3 na unatekelezwa katika mikoa 3 ambapo wanufaika wa mradi walio nje ya shule watajengwewa uwezo kwa kupewa stadi za maisha.
 
Alitaja sababu za kuwalenga wasichana wanaobalehe Dkt. Maboko amesema kuwa ni pamoja na kundi hilo hilo kuwa waathirika wakubwa ambapo asilimia 80 ya maambukizi ya VVU yamewaathiri vijana wa kundi hilo.

Mmoja wa wazazi wa wanafunzi walionufaika na mradi huo Bi Mayasa Mussa amesema kuwa wanafunzi wanafurahia mradi huo na ari ya kwenda shule imeongezeka kwani kila mwezi wanapokea elfu 25,000/- kwa mwezi kuwawezesha kukidhi mahitaji muhimu ya wanafunzi hao ikiwemo kupata taulo za kike, sare za shule na mahitaji mengine.
 
Mradi wa Timiza ndoto zako unatekelezwa katika mikoa 3 na
Halmashuri na Halmashuri 10 ukilenga kuwawezesha wasichana waliobalehe wakiwa mashuleni na wale walio nje ya mfumo wa elimu.


Share:

Jeshi la Yemen latekeleza mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi Saudia

Jeshi la Yemen limetekelza mashambulizi mapya ya kulipiza kisasi katika eneo la Jizan, kusini magharibi mwa Saudi Arabia.

Televisheni ya Al Masirah imeripoti leo Jumapili kuwa, Jeshi la Anga la Yemen na kamati za wananchi zimetumia ndege isiyo na rubani au drone kushambulia maeneo ya kuegeshea ndege za kivita za Saudia katika uwanja wa ndege wa Jizan.

Taarifa zinasema kuwa oparesheni hiyo imetekelezwa na drone ya kivita ya Yemen aina ya Qasef-K2 baada ya oparesheni ya upelelezi.

Hali kadhalika Jeshi la Yemen limetangaza kuitungua ndege ya kijasusi ya adui katika eneo la mashariki mwa Jabal al-Dudud katika eneo la Jizan.


Share:

Kocha Wa Simba Apewa Mkataba Wa Mwaka Moja

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuinoa timu hiyo.

Hatua hiyo ni baada ya kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Share:

Vijana Wawili Wa Tanzania Bara Na Zanzibar Waibuka Kidedea Tuzo Ya Kimataifa Ya Kuhifadhi Quran

VIJANA wawili wa Kitanzania, Zakaria Sheha Ally na Shamsi Mwalimu Said wamechukua nafasi ya kwanza na ya tatu kwenye fainali za 27 za tuzo ya kimataifa ya kuhifadhi Quran tukufu.

Zakaria Sheha Ally (16) kutoka Tanzania Bara na Shamsi Mwalimu Said (19) kutoka Zanzibar wameibuka na kitita cha dola za Marekani 5,000 na dola 3,000 kila mmoja baada ya kuwashinda wenzao nane waliofanikiwa kuingia fainali hizo ambao walitoka Afrika Kusini, Sudan, Malaysia, Uturuki, Yemen, Kenya, Burundi na Uingereza.

Nafasi ya pili imechukuliwa na kijana Gaffari Mohammed (14) kutoka Uingereza ambaye ameibuka na kitita cha dola za Marekani 4,000. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, mwaka huu yalishirikisha vijana 10 kutoka nchi 10 duniani.

Tuzo hizo zimetolewa leo (Jumapili, Mei 26, 2019) wakati wa kilele cha mashindano ya 27 ya Kimataifa ya Kuhifadhi na Kusoma Qur’an tukufu na utoaji tuzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya waumini wa Kiislamu waliofurika kushuhudia kilele cha Tuzo ya Kimataifa ya Quran iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran nchini, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuhifadhisha Quran kunapaswa kuwa msingi imara katika kujenga jamii bora.

“Tuendelee kuhimiza suala la malezi bora ya vijana wetu kwa lengo la kuwafanya wawe raia wema, wakweli, wazalendo na wenye manufaa kwa nchi yao. Quran inatusisitizia sana kuhusu suala la uadilifu. Kwa mfano, katika Quran 9:119, Mwenyezi Mungu Mtukufu anatukumbusha waumini kumuogopa Mungu na kuambatana na wale walio wakweli wa maneno na vitendo,” amesema Waziri Mkuu.

Amewataka wazazi wa Kiislamu wahakikishe wanawasimamia vema watoto wao na kuwahifadhisha Quran badala ya kutoa msukumo pekee kwenye elimu ya kimazingira. “Sote ni mashahidi kwamba vijana wetu wanao uwezo wa kuhifadhi Quran na wakati huohuo wakasoma na kuhitimu fani mbalimbali katika elimu ya mazingira.”

“Tukumbuke kwamba mafanikio ya duniani na akhera hayapatikani kwingine isipokuwa ni kupitia Quran. Hivyo basi, tuwafunze Quran vijana wetu ili waweze kukabiliana na changamoto nyingi zinazoibuka kwenye ulimwengu wa sasa hususan suala zima la mmomonyoko mkubwa wa maadili,” amesisitiza.

Amesema njia mojawapo ya kuwasaidia vijana kukabiliana na hali ya sasa ya dunia ya utandawazi ni kuwasomesha na kuwahifadhisha Quran. “Vijana waliosoma na kuihifadhi Quran ni vigumu kuenenda kinyume na maadili kwani Quran ndiyo njia pekee ya kuwachunga na kuwafanya waonyeke dhidi ya vitendo vinavyokwenda kinyume na uadilifu.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameipongeza Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran nchini kwa kuendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mwongozo na msingi wa maisha yao kupitia Quran kwani kwa kufanya hivyo wanakuwa wanawaongezea vijana hao uelewa sahihi wa dini yao na elimu ya kutosha ya mazingira (yaani circular education).

“Kwa kufanya hivyo, Jumuiya inalipatia Taifa la Tanzania nguvu kazi yenye uadilifu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yake sambamba na uwezo na kujiamini katika kuisoma na kuihifadhi Quran tukufu,” amesema.

Amewakumbusha viongozi wa taasisi hiyo watenge muda maalum wa mashindano hayo kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, kanda, kitaifa ndipo wawagawe kwenye makundi mawili makubwa. “Mkitoka hapo washindanishwe kwa bara la Afrika na kisha mashindano ya dunia. Siyo mnamaliza mashindano ya kimataifa halafu unasikia kuna mashindano ya wilaya au mkoa,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali alisema tuzo za leo zimethibitisha kuwa kusoma elimu ya mazingira hakuharibu elimu ya dini. “Iwe changamoto kwa Waislamu kwamba msingi wa elimu ya dini hauchafui elimu ya dini, kwani kuna watu hawataki kusoma elimu ya mazingira kwa kisingizio kuwa mtume hakusoma, sasa mtume atasoma kila kitu?” alihoji.

“Mambo ya uchumi, kijamii, sheria na ufundi yalielezwa na Mtume Muhammad (S.A.W) na Quran imeyazungumzia sana. Kusoma elimu ya mazingira ni muhimu kwa sababu zipo pia aya zaidi ya 70 katika Quran tukufu ambazo zinaelezea mambo hayo,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, Sheikh Othman Ali Kaporo alisema walilazimika kuanzisha taasisi ili kuwafundisha vijana maadili mema kwani miaka ya 80 - 90 ilikuwa shida kumpata kijana mwenye uwezo wa kuhifadhi hata juzuu tatu tu.

“Hivi sasa taasisi yetu ina vijana zaidi ya 1,000 katika sekta tofauti lakini hakuna hata mmoja aliyekutwa katika mambo ya dawa za kulevya, ufisadi au mambo ya hovyo. Quran ni kinga. Quran ndiyo mafanikio, na kwa malengo hayo, ndiyo maana tunafanya mashindano haya,” alisema.

(mwisho)


Share:

Dkt. Bashiru: Uwezo Wa Kuhifadhi Vitabu Vitakatifu Uwe Chachu Ya Ubunifu Katika Nyanja Ya Sayansi Na Teknolojia

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally, amewataka watanzania kutumia  uwezo wa kuhifadhi Vitabu vitakatifu kuongeza ubunifu katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia na nyingine ili kuendeleza jamii kwa kuipatia maendeleo stahiki.
 
Dkt. Bashiru ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyowashirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini. 
 
Alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa katika kuwekeza kwenye elimu kwa watoto, kwa kuwa watoto wakisoma si tu wanajengewa maarifa lakini pia wanaunganishwa na hivyo kuwa chachu ya kuweza kuisaidia jamii inayowazunguka. 
 
Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuibua vipaji vya watoto vya kusoma Kitabu Kitukufu cha Qur'an na kuwajengea vijana uwezo wa kuwa na ujasili katika kueleza wanayo yaamini yakiwemo mambo mazuri ambayo yanafanywa na Serikali. 
 
Pause: Dkt. Ashatu Kijaji-Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, alisema kuwa kazi zinazofanywa na Dkt. Ashatu Kijaji, ni zakupigiwa mfano hasa kwa wanawake na akawataka wazazi katika Wilaya ya Kondoa kumuunga mkono kwa kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kuinua elimu katika eneo hilo, kwa kuhakikisha wanawapeleka watoto katika makambi yaliyo na lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
 
Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Mustapher Shabaan, amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi Qur'an na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.
 
Mwisho


Share:

Masoko Mapya ya Madini Yaingiza Bilioni 34.3 Kwa Mwezi Mmoja

Na Frank Mvungi- MAELEZO
Dhahabu ya Bilioni 34.3 imeuzwa katika Kipindi cha mwezi mmoja kupitia katika masoko 21 yaliyoanzishwa kwa ajili ya kuuza madini katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
 
Akizungumza katika mahojiano maalum na idara ya habari MAELEZO, Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko amesema kuwa kuanzishwa kwa masoko hayo kumekuwa chachu ya kuongeza mchango wa sekta ya madini katika kukuza uchumi na pato la Taifa kwa ujumla.
 
“ Katika kipindi cha mwezi mmoja tu yaani Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu,jumla ya kilo 409.3 za dhahabu pekee zenye thamani ya shiilingi bilioni 34.3 imeuzwa kupitia katika maduka yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali” Alisisitiza Biteko.
 
“Katika kilo hizo,Mkoa wa Geita umeongoza kwa kufanya biashara ya jumla ya kilo 289,Kahama kilo 44,Mara kilo 13,lakini cha kufurahisha zaidi ni kwa Wilaya ya Chunya ambako jumla ya kilo 52 zimeuzwa katika soko hilo zikiwa nia siku chache toka kufunguliwa kwake ,”,aliongeza, mheshimiwa Biteko.
 
Aidha mheshimiwa Biteko, katika mahojiano hayo maalum,ameeleza kuridhishwa na biashara inayofanyika katika maduka hayo ya madini kote nchini na kueleza kuwa licha ya mafanikio hayo yaliyofikiwa katika kipindi kifupi,serikali inashughulikia changamoto ndogondogo ikiwemo wafanyakazi,mashine za XRF na idadi ya watoa vibali.
 
Akifafanua amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona sekta hiyo inatoa mchango stahiki katika kujenga uchumi na kuchangia maendeleo hapa nchini ndio sababu mkazo umewekwa katika kusimamia sekta hii.
 
Pia aliwataka wachimbaji wadogo na madalali wa madini kuhakikisha kuwa wanatumia masoko hayo kikamilifu na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni jambo alilosema serikali haipendi,
 
Akizungumzia mikakati ya kusimamia sekta hiyo Mhe. Biteko amesema kuwa ni pamoja na kushirikisha wachimbaji wadogo katika kuhakikisha kuwa vitendo vya utoroshaji wa madini unakomeshwa ili kulinda mapato ya Serikali.
 
Aliongeza kuwa hatua nyingine ni usimamizi wa karibu katika maeneo yote ya uzalishaji wa madini ya aina mbalimbali na kuchukua hatua za kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo.

Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Waziri Biteko amebainisha kuwa masoko mengine 7 yanatarajiwa kufunguliwa.
 
Baadhi ya Mikoa ambayo imeshafungua masoko ya kuuza madini ni pamoja na Geita, Dodoma, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Morogoro, Mbeya, ambapo tayari mikoa 21 imeshafungua maduka hayo hadi sasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa kwa wakuu wa mikoa wote hapa nchini.


Share:

WILLIAM BUNDALA AFARIKI DUNIA,AZIKWA KIJIJINI KWAO ULOWA USHETU


Babu wa Mtangazaji maarufu nchini William Bundala maarufu Kijukuu cha Bibi K, Mzee William Bundala Ndabihizye (89) amefariki dunia.


Mzee Bundala amefariki dunia juzi majira ya saba mchana kufuatia kuugua ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo.

Kwa mujibu wa Mjukuu wake William Bundala (Kijukuu cha bibi K) ambaye sasa anafanya kazi Kahama Fm ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio Free Africa Willima Bundala ameiambia Malunde 1 blog kuwa babu yake alianza kuugua tangu tarehe 15/5/2019 na kufariki dunia Mei 24,2019.

Mzee William Bundala Ndabihizye ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la ardhi na mwenyekiti wa kitongoji cha Kangeme B kwa kipindi cha miaka 20, amezikwa kijijini kwao Kangeme kata ya Ulowa halmshauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga.

Alizaliwa mwaka 1930 katika kijiji cha Ubagwe,ameacha mjane,watoto 9,wajukuu 33,vitukuu 10.
Mzee William Bundala enzi za uhai wake
William Bundala maarufu Kijukuu cha Bibi K akiwa kwenye kaburi la Babu yake Mzee William Bundala Ndabihizye.
William Bundala maarufu Kijukuu cha Bibi K akiaga mwili wa Babu yake Mzee William Bundala.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Mzee William Bundala.



Share:

RAIS MSTAAFU AJIUNGA NA CHAMA CHA UPINZANI


Rais mstaafu wa Botswana, Ian Khama amejiengua katika chama tawala kilichoongoza nchi hiyo tangu uhuru miaka 53 iliyopita, akieleza tofauti kubwa baina yake na Rais aliyerithi kiti chake.

Hii ni mara ya kwanza kwa Botswana kuona rais mstaafu anakitosa chama cha tawala cha Botswana Democratic Party (BDP).

Khama mwenye umri wa miaka 57, alisema hakuwa na chama chochote lakini ataunga mkono chama cha upinzani cha Umbrella for Democratic Change (UDC) kupambana na BDP.

Khama aliyeingia madarakani Aprili Mosi 2008 akimrithi Festus Mogae, aliwaeleza maelfu ya wafuasi wake katika mji wa nyumbani kwake wa Serowe jana kwamba alifanya makosa katika kumteua Mokgweetsi Masisi kuwa rais.

Nimekuja hapa leo kuwaeleza kwamba ninaachana na BDP. Ninaitupa kadi yangu ya uanachama wa BDP,” alisema Khama huku akitupa kadi yake. “Siitambui BDP tena,” aliongeza.

Maelfu ya watu waliofurika katika mkutano huo, pia walirusha kadi zao za BDP.

Khama na mrithi wake wamekuwa wakilumbana waziwazi kutokana na Masisi kubadili sera zilizoanzishwa na mtangulizi wake, ikiwamo ya hivi karibuni ya kuondoa zuio la uwindaji wa tembo.

Tangazo la kuondoa zuio hilo lilitolewa Machi mwaka huu na Khama alimshutumu ‘kijana wake’ kwa usaliti.

Botswana ina ukomo wa vipindi viwili vya urais. Masisi alichukua madaraka baada ya Khama kujiuzulu Machi mwaka jana.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger