Thursday, 9 May 2019

Picha : MAREHEMU DR MENGI AZIKWA NYUMBANI KWAO MACHAME - MOSHI


Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi umezikwa katika makaburi ya familia yao yaliyopo nyumbani kwa wazazi wake, Nkuu, Machame, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, leo Alhamisi, Mei 9, 2019.

Mazishi ya Dkt. Mengi ambayo yameanza na ibada katika Kanisa la KKKT, Usharika wa Moshi Mjini, yamehudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika Job Ndugai, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge, viongozi wa dini, siasa na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.

Mengi ameacha simanzi kubwa kwa Watanzania wengi kutokana na ukarimu wake katika kuwasaidia watu mbalimbali wakiwemo wenye ulemavu, vijana, wazee na maskini ili kujikwamua katika wimbi la umaskini.

Akihubiri wakati wa ibada ya kuaga mwili huo, Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo amemtaka Spika Job Ndugai, Bunge na wote wenye mamlaka wakatende haki kwa watu wote.

“Nashukuru Mheshimiwa Ndugai uko hapa. Kazi ya Bunge ni kutetea maslahi ya wananchi. Teteeni maslahi ya wananchi mnaowawakilisha, kama kweli tunasema tumejifunza kutoka kwa Dk Mengi,” amesema Dkt. Shoo.

Mengi alifariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, Mei 2, 2019, nchini Dubai katika Falme za Kiarabu na mwili wake uliwasili nchini Jumatatu, Mei 6 kabla kuagwa Karimjee na kusafirishwa kwenda Machame ambako umezikwa leo.

Ameacha mjane, Jacqueline Ntuyabilwe, watoto wanne ambapo watatu ni wa kiume na mmoja wa kike.


Share:

Tahadhari Kwa Umma Kuhusu Homa Ya Dengue Yazidi Kutolewa

NA WAJMW-DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezidi kutoa tahadhari ya  kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue nchini hususani katika Jiji la Dar Es Salaam na Tanga.
 
Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo zilizoko jijini Dodoma.
 
Prof. kambi amesema hadi kufikia tarehe 6 Mei 2019, kati ya watu waliopimwa, wagonjwa 1237 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugonjwa wa Dengue na kati yao 1150 ni kutoka Dar Es Salaam, 86 ni kutoka Tanga na mtu mmoja kutoka Singida.
 
Aidha, Prof Kambi amesema takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2019 zinaonesha mwenendo wa ugonjwa huu kuwa na idadi ya wagonjwa 1237, vifo vya watu wawili na kuongeza kuwa waliofariki walikua na maradhi mengine.
 
Pamoja na hayo Mganga Mkuu huyo wa Serikali amelipongeza jiji la Dar Es Salaam kwa kuanza kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu ili kupambana na ugonjwa huu.
 
Vile vile amesema Wizara inaelekeza Mikoa na Halmashauri zote nchini kuendelea kuchukua hatua katika kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi ya maji, kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi, kuondoa vitu vinavyosababisha mazalia ya mbu, kufyeka vichaka, kufunika mashimo ya maji taka kwa mifuniko pamoja kusafisha gata za paa la nyumba na kutoruhusu maji kusimama.
 
Prof. Kambi amesema Wizara kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri zote nchini itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuangamiza mazalia ya mbu na viluwiluwi, kuweka mpango wa dharura wa miezi sita kuanzia Mei mpaka Oktoba ili kukabiliana na ugonjwa huu. 

Pia amesema Serikali imenunua Vitendanishi vyenye uwezo wa kupima wagonjwa 1870 na vimesambazwa kwenye vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu nchini kote.
 
Mwisho Prof. Kambi amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga kuumwa na mbu kwa kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu, kutumia dawa za kufukuza mbu na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi ili kukabiliana na ugonjwa huu.


Share:

Waziri Hasunga Aagiza Kufikia Julai 2019 Rasimu Ya Sheria Ya Kilimo Kuwa Imekamilika

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 9 Mei, 2019 ameiagiza Timu ya wataalamu wa wizara ya Kilimo ambao wametuama kuandaa rasimu ya sheria ya kilimo na kufikia mwezi Julai 2019 iwe imekamilika.

Alisema kuwa ipo haja ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazomkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla hivyo ili kufikia malengo hayo ni lazima kuwa na ukomo wa ukamilishaji wa mpango kazi huo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 9 Mei 2019 wakati wa kikao na Menejimenti ya Wizara ya Kilimo, kikao kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe.

“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kuboreshwa ili iweze kuendana na mabadiliko mbalimbali ya kisera na wakati, ambapo lazima tuwe na rasimu yake kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Mei” amesema

Mhe. Hasunga ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa vigumu.

Mazao yaliyo katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho, Pareto, Mkonge, Sukari na Tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) alisema kikao hicho ni cha kipekee kwakuwa kitapelekea kuimarisha mkakati wa pamoja wa Wizara ya kilimo kuwa na uelekeo katika utatuzi wa kero za wakulima kisheria.

Aidha, alipendekeza kuwa ni vyema sekta ya ushirika ikatajwa kwa umuhimu wake kwenye sera ya kilimo sambamba na Zana ndogo za Kilimo.


Share:

Kutana na Sheikh Omary Mwenye Uwezo wakufanya Dua mbalimbali za Matatizo Yako Na Kutafsiri Ndoto kwa kutumia Vitabu vya QUR-AN

Sheikh Omary Ni bigwa wa kutatua matatizo kwa haraka, ni mtu aliye jaliwa kubuli Shufaa pia anatoa Duah  za Ruhia. Ukija na Maradhi yanaondoka hapo hapo bila kungoja kesho,  UKIPEWA MKONO  na Sheikh Omary .
 
Wasiliana na Mtaalam Huyu Kwani yeye hufaulu Pale wote waliko Shindwa na Pia Humaliza kazi zilizo Shindikana ama Zilizo Achwa ndani ya Siku Moja 1.
 
Sheikh Omary ni Mtaalamu wa Nyota za Binadamu  Mwenye Uwezo wa Kubaini Tatizo lako tu Pindi Utakapo Fanya Mawasiliano Kupitia Wasaa Husika.
 
Je una NUKSI  zisizo kwisha.!? JE umekimbiwa na Mume/Mke na Anaishi na Mtu Mwingine..!? Muone Akutatulie,
 
Una kosa bahati ya wanaume au mume wa kukuoa..Unataka nyota ing'ae Au huna hamu na Mkeo/ Mumeo.
 
Jini mahaba. Kama Unakasirika ovyo ukiwa na bwana au mwanamke wako na  kumchukia Mpaka  kushindwa kufanya nae tendo la ndoa.
 
Njoo umuone Sheikh Omary  na ujuwe  yanayo kusibu.Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN

Mawasiliano: Sheikh Omary 0673531992 WhatsApp/Call
Tembelea Page ya @Mtabibu_Omar  @Mtabibu_Omar
Usome Makala Tofauti Tofauti Kama.


Share:

Askofu Mkuu Dk. Shoo Awaonya Viongozi, Matajiri......Asema wasitumie nafasi zao kunyanyasa wengine, akemea ubaguzi

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Mkuu Dk. Ferdinand Shoo amewaonya viongozi wa Tanzania na kuwataka watumie nafasi zao kuwasaidia wengine hasa wale wenye uhitaji.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 9, 2019) wakati akitoa mahubiri kwenye ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni za IPP, Dkt. Reginald Mengi iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT, Usharika wa Moshi mjini.

Amesema kuna watu wakipata vyeo ama utajiri kidogo tu, wanatumia nafasi zao kunyanyasa wengine na akaonya Watanzania wasie wepesi wa kuhukumu, kunyanyasa wengine au kubagua wengine.

Katika mahubiri yake, Dk. Shoo amesema kama kuna dhambi ambayo binadamu anapaswa kuifanyia toba ni ile ya kubaguana na kama Watanzania wanahitaji Taifa lipokee baraka kutoka kwa Mungu, ni vema wakaacha kufanya hivyo. Amesema dhambi nyingine inayopaswa kufanyiwa toba ni ile ya watu wenye nafasi kuwakanyaga wengine.

“Ndugu zangu tukiwa na cheo, tukiwa matajiri, tukiwa na uwezo tuvitumie kuwasaidia wengine, tuache ubinafsi, tuache kiburi, tuache kujitutumua hasa kwa viongozi wa umri mdogomdogo. Kuna mahali mmefika mnajitutumua kama chatu, acheni kabisa. Naomba tuwe unyenyekevu ndugu zangu.”

“Wale wanaopata utajiri, acheni kukumbatia mali zenu, toeni na kuwasaidia wenye uhitaji kwani mnapata satisfaction kwa kufanya hivyo. Huu ni ujumbe kwetu sote na Mungu atusaidie tulishike hili. Muendelee kuiombea familia na yale mazuri mengi tuliyojifunza kwake tukayatende tukayatende, tuyaenzi,” amesema.

Akimuelezea Dkt. Mengi, Askofu Mkuu huyo amesema: “Aliwahi kusema kuwa, mali na utajiri ambao Mungu amempatia siyo kwa sababu yeye ni bora kuliko wengine, bali alimpa ili awe kama bomba la kufikisha baraka kwa wengine.”


“Leo mtu anapata vimilioni kadhaa tu anataka atembee juu ya migongo ya watu, anapata ka-cheo sijui ni diwani, Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya, halafu unaona wenzako si kitu. Tuache na tutubu, acha kiburi namuomba Mungu atujalie roho hiyo ya unyenyekevu,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Dkt. Mengi atakumbukwa kwa kitendo chake cha kuuchukia umaskini na zaidi kwa kazi mbalimbali ambazo alishiriki.

“Bila shaka kila mmoja wetu ameguswa kwa namna ya kipekee na mchango wa Dkt. Mengi. Kiukweli, marehemu Dkt. Mengi, atakumbukwa kama mwanahabari, mwanaviwanda na mfanyabiashara maarufu ambaye alitumia elimu, maarifa na utajiri wake kwa ajili ya manufaa ya wote hususan watu wenye mahitaji maalum,” amesema Waziri Mkuu.

Amewaomba wanafamilia wasimamie makampuni ambayo Dkt. Mengi aliyaanzisha na kama watakwama wasisite kuomba msaada serikalini kwani iko pamoja nao.

Akielezea wasifu wa baba yake, mtoto wa marehemu, Bw. Abdiel mengi alisema siyo rahisi kuyazungumzia yote kwa wakati mmoja mambo ambayo yamefanywa na Dkt. Mengi bali aliwashukuru waombolezaji wote, viongozi wa Serikali na wafanyakazi wa makampuni ya IPP kwa upendo wao.

“Mambo yote aliyoyafanya naweza kumwelezea katika sifa tatu kubwa ambazo ni alikuwa mzalendo, mwenye uthubutu na mwenye kupenda breakthrough. Alikuwa nafikiria tofauti na wengine. Kwanza anajiuliza kwa nini nifanye jambo hili, na nifanyeje ilikuwa ni suala la pili,” alisema.

Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia alfajiri ya Mei 2, mwaka huu akiwa kwenye matibabu huko Dubai, Falme za Kiarabu, amezikwa katika makaburi ya familia huko Nkuu Sinde - Kisereni, Machame, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. Ameacha mke na watoto wanne.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, MEI 9, 2019.


Share:

Katibu Mkuu CCM Dk. Bashiru amuombea radhi Makonda Kwa Kauli Zake.....Askofu Shoo ampatanisha na Mbowe

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amemuombea msamaha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutokana na kauli yake aliyoitoa wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni tanzu za IPP, Dk. Reginald Mengi katika viwanja vya Karimjee.

Katika kauli yake iliyozua sintofahamu, Makonda alisema hajawahi kuona mtu yeyote wa kabila la wachaga akitoa msaada au fedha kwa walemavu.

Kauli ambayo haikuwapendeza watu wengi akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ambaye wakati akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kuaga mwili wa Dk. Mengi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro leo Alhamisi Mei 9, alikumbushia suala hilo na kuwataka Watanzania kutogawanywa kwa kauli na vitendo vya kibaguzi zinazotolewa na viongozi.

Akizungumza wakati akitoa salamu za rambirambi, Dk. Bashiru amesema kauli za Makonda zimesababishwa na wao kama walezi kushindwa kutoa malezi ya kutengeneza viongozi bora.

Dk. Bashiru amesema hayo baada ya kauli ya Askofu Mkuu wa KKKT Usharika wa Kaskazini, Fredrick Shoo kuzungumzia umuhimu wa kuwaandaa viongozi bora, watiifu na wanyeyekevu.

“Naomba nitumie fursa hii kumuombea msamaha kijana wangu Makonda, mimi namfahamu na hii ni mara yangu ya pili nimemsema hadharani, mara ya kwanza nilimsema Simiyu akaja analia ofisini nikamwambia ubadilike na kwa kweli ameanza kubadilika.

“Bado ni kijana mzuri shupavu na bado tunahitaji, lakini tunahitaji kuwasaidia vijana wetu,” amesema Dk. Bashiru.

Hata hivyo baada ya Dk. Bashiru kumaliza kuzungumza, Askofu Shoo alimuita Makonda na kumuombea msamaha kisha akawapatanisha na Mbowe.

“Makonda uko wapi? njoo tunakutangazia msamaha hapa hapa na nimekusamehe na hapa ni madhabahuni nimewaita kw ajili ya upatanisho,” alisema Askofu Shoo.

Aidha baada ya kuombewa msamaha Makonda aliwashukuru Dk. Bashiru na Askofu Shoo kwa kumuombea msamaha.

“Kwanza nashukuru kwa maelekezo na maonyo ya baba Askofu, na nashukuru kwa Katibu wangu Mkuu kwa kusimama na kuomba msamaha kwa niaba yangu lakini pia namshukuru kaka yangu Mbowe mimi na yeye tunafahamiana kwa muda mrefu na mbele ya baba yetu Mengi kwa kutamka yale yaliyomkwaza naye pengine angeweza kukaa kimya.

“Nahisi tafsiri inaweza kuwa tatizo naomba radhi kwa kumsifia mchaga katikati ya wachaga na si mchaga kati ya wengine na nitaendelea kumshukuru kwa yote aliyoyafanya katika mkoa wetu hususani kusaidia walemavu,” amesema Makonda.


Share:

BOBI WINE, BESIGYE WATENGENEZA JEMBE MOJA LA KUMLIMIA MUSEVENI


Mbunge wa upinzani nchini Uganda ambaye pia ni msanii wa muziki, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, ameungana na mwanaharakati wa kisiasa Dkt. Kizza Besigye ili kukiondoa madarakani chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni.

Taarifa iliyotolewa na wapinzani hao wenye nguvu zaidi nchini Uganda, imeeleza kuwa baada ya mazungumzo kati yao, wamekubaliana kuhusu masuala kadhaa ya kushirikiana kisiasa dhidi ya Museveni kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2021.

Akizungumza na waandishi habari jana, Bobi Wine alisema wamekuwa wakishauriana katika mikutano kadhaa na vyama tofuati vya kisiasa nchini kikiwemo cha Democratic Party maarufu DP na kiongozi wa People’s Government, Dkt. Kizza Besigye.

Bobi ambaye hana chama, ni mgombea huru na kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Kyadondo,

NRM kimekuwa madarakani tangu 1986.
Share:

Ufahamu Ugonjwa Wa Ngiri Na Tiba Yake

Tatizo la Ngiri Linavyosababisha Upungufu wa Nguvu za Kiume na Maumbile Kusinyaa.
 
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.

Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;

Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Tiba ya Ngiri
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji , ama kutumia dawa za asili ili kupona kabisa tatizo hilo. Wasiliana Nami Kwa Ushauri zaidi wa Tatizo hili. Simu: 0714006521


Share:

MUME NA MKE WANUSURIKA KICHAPO KWA KUZIKA MAITI BANDIA

Mtu na mke wake huko Homa Bay nchini Kenya wamenusurika kipigo  baada ya jamaa zao kugundua walikuwa wakitaka kuzika watoto bandia.
 
Tukio hilo limetokea siku ya  Jumatano, Mei 8,2019

Beryl Akinyi, na mume wake Benson Onyango, 38, hatimaye walitiwa mbaroni na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Mbita huku polisi wakianzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho. 

 Onyango ambaye ni seremala alitengeneza majeneza mawili na kuyapeleka uwanja mdogo wa ndege wa Kabunde alikokuwa akitarajiwa mke na ‘maiti’. 

 Ilivyoripotiwa katika The Standard, wawili hao walidai pacha wao waliaga dunia mara baada ya kuzaliwa na kuongeza kuwa Akinyi alipatwa na matatizo wakati akijifungua pacha wao. 

“Tunachunguza kisa hiki ili kupata ukweli,” alisema afisa wa polisi anayehusika na uchunguzi wa kisa hicho.

 “Tunataka kufahamu ikiwa mke alimhadaa mume wake kuhusu ujauzito wake au la. Ama ikiwa walishirikiana kufanya ukora huo tutajua tu ” aliongeza kusema. 

Wananchi walisema walifukua ‘miili’ mara baada ya kuzikwa na kugundua ni kweli haikuwa maiti bali watoto bandia waliokuwa wamefungwa katika shuka. 

Shemeji yake Akinyi, Wycliffe Ogembo, alisema alitoka nyumbani siku kadhaa na kudai alikuwa akienda kujifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay lakini aliwaarifu alishauriwa kwenda Hospitali ya Aga Khan, Kisumu.

Ogembo alisema walishuku madai ya Akinyi ambaye alikuwa amedai alijifungua mtoto wa kwanza kupitia upasuaji Homa Bay kisha kuhamishiwa Kisumu.

 “Haiwezekani yeye kuwa Homa Bay, Agha Khan na alikuwa amelazwa Hospitali Kuu ya Kenyatta,” Ogembo alisema.

 Siku kadhaa baadaye, Akinyi na Onyango walidai pacha wao waliaga dunia walipokuwa wakizaliwa na hali hiyo iliwashangaza sana na ndipo wakaanza kujiuliza maswali.

Jumanne, Mei 7,2019 mume ambaye ni fundi seremala alitengeneza majeneza mawili na kuyapeleka uwanja mdogo wa ndege wa Kabunde alikokuwa akitarajiwa kuwasili mke na ‘maiti’.

Inadaiwa walisafirisha ‘maiti’ ndani ya Toyota Probox, na walipofika nyumbani wakaamua kuzika bila ya kuwafahamisha jamaa zao. 

Haijabainika wazi ikiwa Akinyi, aliyeonekana na ujauzito alijifungua au la ingawa inashukiwa aliwauza watoto wake madai ambayo bado hayajathibitishwa.

 Kamanda wa Polisi Homa Bay, Esther Seroney, alithibitisha tukio hilo na kusema watampeleka Akinyi hospitalini kuthibitisha madai yake. 
Share:

ASKOFU SHOO ATUMIA MSIBA WA MENGI KUWACHANA WENYE VIMILIONI NA VIONGOZI WENYE KIBURI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amesema kama kuna dhambi ambayo binadamu anapaswa kuifanyia toba ni ile ya kubaguana na kama Watanzania wanahitaji Taifa lipokee baraka kutoka kwa Mungu, ni vyema wakaacha kufanya hivyo.

Amesema dhambi nyingine inayopaswa kufanyiwa toba ni ile ya watu wenye nafasi kuwakanyaga wengine.

Dk Shoo ameyasema hayo leo, Alhamisi, Mei 9, 2019 katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti mtendaji wa kampuni za IPP, Reginald Mengi inayofanyika katika KKKT Usharika wa Moshi mjini.

Amesema jamii inapaswa kujifunza kupitia kwa Mengi kwa sababu alikuwa na nafasi ya kufanya mambo mengi ikiwemo kununua haki za watu wengine.

“Kama kuna kitu tunaweza kumuenzi (Mengi) ni kuiga roho yake ya upendo, kutokuwabagua watu kutokana na matabaka au kabila, nimemsikia mbunge wetu Freeman Mbowe akisema jambo fulani ambalo wakati mwingine huenda tunaongea kwa ndimi kuteleza, tunaomba sana Mungu atusaidie,” amesema Askofu Shoo.

Amesema, “tusibaguane kwa misingi yoyote ile, nimefuatilia malumbano yanayoendelea katika mitandao ya kijamii kati ya watu wa chama kimoja na chama kingine nakuta maneno, hadi najiuliza hivi ni Watanzania wameweza kufika mahali kwa namna hiyo.”

Kisha, Askofu Shoo akasema, “mwenyekiti Mengi alithamini sana maneno ya maridhiano kati ya Watanzania wote licha ya tofauti zetu, matajiri, maskini wenye mamlaka wasiokuwa na mamlaka kabila hili na kabila lile.”

“Leo bwana mtu anapata vimilioni kadhaa tu anataka atembee juu ya migongo ya watu, anapata ka-cheo sijui ni diwani, mkuu wa mkoa, waziri halafu unaona wenzako si kitu. Acha, acha kiburi namuomba Mungu atujaalie roho hiyo ya unyenyekevu.”


“Ndugu zangu tukiwa na cheo, tukiwa matajiri, tukiwa na uwezo tuutumie kuwasidia watu wengine tuache ubinafsi, tuache kiburi, tuache kujitutumua hasa kwa viongozi wa umri mdogomdogo, kuna mahali mnafika mnajitutumua kama chatu, acheni, unyenyekevu ndugu zangu (ni muhimiu).”

Amesema, “(Mtu) usitumie nafasi yako kunyanyasa wengine, kufarakanisha na usiwe mwepesi wa kuhukumu.”

Dk Shoo amesema baada ya kutokea kwa msiba wa Mengi kuna watu walianza kuweka machapisho katika mitandao ya kijamii na kuanza kuhukumu, akawaonya kuwa walikuwa wakikosea na kuhoji kuwa wao ni kina nani kwani kwa utaratibu wa kanisa mtu akitambua dhambi zake na kutubu anarudishwa kundini.

“Mtu akisharudishwa kundini wewe mwanadamu mwenye dhambi kama mimi una nini zaidi ya kusemea hapo acha,” amesema.

Amesema matajiri wanapaswa kuacha kukumbatia mali zao kwa kuwapa wengine, huku akiwataka watu wanaowatetea wananchi wenye haki na masilahi bungeni kufanya kazi yao ipasavyo.

“Huu ukawe ni ujumbe kwetu sote na Mungu atusaidie mkalishike hili, mkaendelee kuiombea familia na yale mazuri mengi tuliyojifunza kwake tukayatende,”amesema Dk Shoo.
Na Aurea Simtowe,mwananchi 
Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Mkoani Mbeya Kuhusu Mdude Nyagali

Mnamo Mei 04, 2019 majira kati ya saa 19:00 na 20:00 usiku huko Vwawa, Wilaya ya Mbozi na Mkoa wa Songwe, Mtu mmoja aitwaye MDUDE MPALUKE NYAGALI [31] ilibainika kuwa amechukuliwa na watu ambao hakuweza kuwatambua na kupelekwa mahali pasipojulikana.

Taarifa zilifikishwa Polisi Mkoa wa Songwe na ufuatiliaji ulianza mara moja na mnamo tarehe 08 Mei, 2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Inyala katika Kijiji cha Mtakuja kilichopo Mkoa wa Mbeya alionekana mtu anaomba msaada, ndipo Dereva wa Pikipiki @ Bodaboda aitwaye EMMANUEL KANAMGONDE na mwenzake AYUB WILSON walimbeba na Pikipiki hadi kwa uongozi wa serikali wa Kijiji cha Mtakuja.

Mhanga wa tukio hili baada ya kufikishwa kwa viongozi wa Kijiji hicho alijitambulisha kuwa yeye anaitwa MDUDE MPALUKE NYAGALI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na akaomba wajulishwe viongozi wake. Kisha Mhanga alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili.


Share:

CHADEMA YATISHIA KUTOA TAARIFA YA KUTEKWA MDUDE POLISI WAKINYAMAZA


 Chadema imelitaka Jeshi la Polisi kueleza kilichomtokea Mdude Nyagali maarufu Mdude Chadema aliyepatikana jana usiku baada ya kutekwa kwa siku tano.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema amesema leo, Mei 9, 2019 kuwa polisi isipotoa taarifa hiyo mapema, Chadema wataeleza.

Mrema amesema kwa sasa hawataki kuingilia kazi ya polisi kwani wanaamini watafanya kwa uadilifu, lakini ni muhimu wakaueleza umma kinachoendelea.

“Wameshamhoji Mdude na tuna taarifa kuwa katika uchunguzi wao kuna watu wengine kule Songwe wamehojiwa, basi waondoe hii taharuki kwa kuweka wazi angalau kidogo kuhusu suala hili,” amesema Mrema.

Amesema, “wakishindwa kufanya hivyo kwa haraka, basi sisi hatutanyamaza tutaweka wazi kile ambacho Mdude aliwaambia polisi maana wakati anahojiwa viongozi wa chama walikuwepo.”
Na Elizabeth Edward, Mwananchi 

Share:

Iran yatishia kurejea katika matumizi ya nyuklia

Baraza la Usalama la Taifa la Iran limeamua kusitisha mara moja baadhi ya ahadi zake ilizozitoa chini ya mkataba wake wa nyuklia na nyengine katika siku 60 zijazo, iwapo hakutakuwa na hatua zozote kushughulikia mkwamo wa kiuchumi unaolikabili taifa hilo. 

Katika barua yake kwa mataifa yaliyoendelea kusalia kwenye makubaliano hayo ambayo Marekani ilijitoa, Iran imelalamikia kusitasita kwa makampuni ya mataifa hayo kufanya biashara nayo. 

Viongozi wa China, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Urusi wamepokea barua hiyo, lakini walengwa zaidi ni viongozi wa mataifa ya Ulaya walioshindwa kutimiza ahadi zao ambazo zingesaidia kufufua uchumi wa Iran. 

Wataalamu wameliambia shirika la habari la AFP kwamba mkataba huo wa nyuklia unazitaka nchi zilizoweka saini kuimarisha uchumi wa Iran, lakini makampuni ya nchi za Ulaya bado yanaogopa kufanya biashara na Iran kwa hofu ya kuwekewa vikwazo na Marekani.


Share:

Korea Kaskazini yarusha kombora huku mjumbe wa Marekani akiwasili Korea Kusini

Korea Kusini imesema jirani yake Korea Kaskazini imerusha kombora lingine leo ikiwa ni mara ya pili wiki hii. 

Kombora hilo limerushwa ikiwa ni masaa machache kabla baada ya kuwasili mjini Seoul, Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Korea Kaskazini, Stephen Biegun, kwa mazungumzo na maafisa wa Korea Kusini kuijadili Korea Kaskazini na mpango wake wa makombora na silaha za nyuklia. 

Jumamosi iliyopita, Korea Kaskazini pia ilifanya zoezi la kijeshi na kurusha makombora kadhaa, mojawapo likiaminiwa kuwa ni la masafa mafupi. 

Ni ziara ya kwanza ya Biegun mjini Seoul, tangu mkutano wa kilele wa Hanoi kati ya Marekani na Korea Kaskazini kumalizika bila ya mafanikio. 

Katika mkutano huo, Kim Jong-un alisema atasitisha mpango wake wa nyuklia pale Marekani itakapoiondolea nchi yake vikwazo.


Share:

Rais Magufuli Akutana Na Ujumbe Kutoka Wizara Ya Ulinzi Ya Ujerumani, Ikulu Jijini Dar Es Salaam




Share:

Mbowe Awataka Watanzania Kutogombanishwa.....Awataka waige Mfano wa Reginald Mengi

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewataka Watanzania kutogombanishwa na kauli za viongozi hasa za kikabila na kidini huku akiwataka viongozi kutafakari maneno kabla ya kuyaongea kwani yanaweza kugawa watu na kuleta machafuko.

Aidha, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai,  amemuelezea aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni Tanzu za IPP, Dk. Reginald Mengi alikuwa ni mtu asiyekata tamaa.

Mbowe ameyasema hayo Mei 9, alipokuwa akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni tanzu za IPP, Dk. Reginald Mengi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.

“Kuna kauli zinasemwa sana watu na kwa ukweli zinakera kwa vile mimi si mnafiki lazima niseme na nitasema hapa hapa mbele za watu.

“Tuna nchi moja ambayo tunastahili kupendana na kusaidiana, na kila mtu ana haki ya kumsaidia mwenzie, tusikubali kauli za viongozi zitugawe na hasa za kidini na kikabila, kauli ya kusema kuna makabila hayawezi kuwasaidia walemavu si nzuri na haikutupendeza kwa kweli, tujitafakari tunapotaka kuongea maneno,” amesema Mbowe.

Aidha Mbowe ametoa wito kwa kila aliyeguswa na msiba wa Dk. Mengi kuyaenzi yale yate aliyokuwa akiyatenda enzi za uhai wake kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kumuenzi.

“Mzee Mengi ameshatangulia mbele za haki haitajalisha tuzungumze mema kiasi gani kumuhusu hatutamrejesha, ila tujitafakari na kuyaenzi yale aliyokuwa akiyafanya, alikuwa mnyeyekevu na kauli zake zilijenga, kupatanisha na kuleta matumaini lakini pia hakuwahi kukata tamaa,” amesema Mbowe.


Share:

Mamia ya Waombolezaji Wajitokeza Kushiriki Ibada ya Mazishi ya Reginald Mengi

Mamia ya waombolezaji leo Alhamisi Mei 9, 2019 wamejitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini kushiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi.

Baadhi ya waliofika kanisani hapo ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, mbunge wa kuteuliwa, Anne Kilango  na mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ndo ataongoza ujumbe wa Serikali katika mazishi ya Mengi aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 Dubai, Falme za Kiarabu.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger