Thursday, 14 February 2019

MAAJABU YA BENZEMA, LIGI YA MABINGWA ULAYA

Na Shabani Rapwi. Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Karim Benzema jana usiku amefunga goli moja katika ushindi wa magoli 2-1 iliopata timu yake ya Real Madrid dhidi ya Ajax katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ( UEFA Champions League) katika hatua ya 16 bora. Goli hilo alilofunga dakika ya 60′ na kuwa goli lake la 60 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, akishika nafasi ya nne ya wafungaji bora wa muda wote huku Cristiano Ronaldo akiwa ndiyo kinara wa ufungaji akiwa na magoli 121 nyuma ya Lionel…

Source

Share:

Ngoma Mpya : MAMA USHAURI - BHASIGANI


Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri anatualika kusikiliza ngoma yake mpya inaitwa Bhasigani..Isikilize hapa chini,ngoma kali balaa
Share:

WIZARA YA AFYA YATOA MSAADA WA KISAIKOLOJIA KWA FAMILIA ZILIZO ATHIRIKA NA MATUKIO YA MAUAJI NJOMBE

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii imetembelea kuwapa pole na kutoa msaada wa kisaikoloji na kijamii kwa Familia zilizoathirikana mauaji ya Watoto yalitokea mkoani Njombe. Timu hiyo imetembelea  Familia ya Bw. Gorden Mfugale inayoishi Mtaa wa Joshoni Kata ya Mji Mwema Halmashauri ya Mji Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto mmoja wa kiume Gidrack Mfugale (5) aliyepotea tarehe 04/02/2019 na kupatika tarehe 10/02/2019 akiwa amefariki dunia huku kiganja cha mkono kikiwa  na  mwili wake ulikutwa na majeraha kichwani katika  eneo la Shule…

Source

Share:

AUAWA AKIAMUA UGOMVI WA WANANDOA WALIOKUWA WANAPIGANA NDANI KWAO

Picha haihusiani na habari hapa chini

Mkazi wa Lizaboni Manispa ya Songea mkoani Ruvuma, Mohammed Hamim, ameuawa kwa kupigwa na kipande cha bomba la chuma kichwani alipokuwa akiamulia ugomvi wa mume na mke ambao ni majirani zake. 

Akizungumza na Nipashe jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tatu usiku katika mtaa wa Pacha Nne, kata ya Lizaboni .

Kamanda Mushy alisema siku hiyo ya tukio hilo, Hamim alikuwa amekwenda nyumbani kwa Soud Mdoka baada ya kusikia kelele zilizokuwa zikiashiria kuomba msaada na baada ya kufika, aliwakuta Mdoka na mke wake, Paulina Mlenga (35) wakiwa wanapigana.

Alisema baada ya kuona hivyo, Hamim alianza kuwaamulia jambo ambalo lilisababisha apigwe na kipande cha bomba la chuma kichwani na kumsababishia kifo papo hapo.

Mushy alisema Mdoka baada ya kubaini kuwa amemfanyia kitendo kibaya jirani yake kwa kumpiga na kufa papo hapo, alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Kutokana na kitendo hicho, Kamanda Mushy alisema Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamsaka Mdoka na akipatikana atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu mashtaka ya mauaji yanayomkabili.

Pia alisema mke wake, Paulina Mlenga, anashikiliwa na polisi katika jitihada za kumtafuta mume wake na mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea kwa uchunguzi.

Gideon Mwakanosya
Share:

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI NA ENDELEVU KATIKA SEKTA YA KILIMO

Na mwandishi wetu Dodoma Serikali imedhamiria kuendelea kujenga mazingira wezeshi na endelevu katika Sekta ya Kilimo kupitia sera imara na zenye kutekelezeka. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wakati akifungua Kongamano la Tano la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Sera Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa tarehe 13Februari, 2019. Waziri alieleza kuwa, dhamira ya Serikali inaenda sambamba na mchango wa sekta ya Kilimo katika uzalishaji pamoja na ukuaji wa…

Source

Share:

MWIGULU NCHEMBA ASIMULIA JINSI PUNDA WALIVYOTAKA KUMSABIBISHIA KIFO


Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani alipata ajali katika eneo la Migori wilayani Iringa katika Barabara ya Dodoma–Iringa ambako alikuwa safarini kutoka Iringa kwenda mkoani Singida jana asubuhi.

Akizungumza kwa taabu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini hapa, Mwigulu alimshukuru Mungu kwa kutoka mzima kwani dereva wake aligonga punda waliokuwa wakivuka barabara katika eneo hilo.

Akizungumzia mkasa huo, Mwigulu alisema: “Nilikuwa natoka Iringa nakwenda Singida, nilikuwa naenda kwenye kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa, sikuwa naangalia mbele nadhani nilikuwa nazungumza na simu kama sikosei… ghafla wakakatiza punda kama sikosei walikuwa watatu.”

Aliongeza: “Nilishtuka tu dereva alivyotoa ishara kwamba kuna kitu cha hatari kwa hiyo ilikuwa ni kitendo cha kufumbua macho hapo hapo na gari ikawa imepinduka. 

“Waligongwa wale punda watatu, mmoja alikuwa anamalizia barabara na mwingine alikuwa anaanza kuvuka barabara na mwingine alikuwa katikati, kwa hiyo hakukuwa na uwezekano wa kukwepa.

“Nilivyoona hivyo nilisikia kelele moja kubwa ya kugonga na baada ya hapo, sikuona tena mbele kwa sababu ghafla niliona mbele yangu pamekuwa padogo na kulikuwa na moshi unafuka. 

“Mwanzo sikuona kama nimeumia nikamuuliza mwenzangu unaendeleaje? Nikamwambia tunaweza kutoka akaniambia ngoja kwanza kwani moshi mkubwa ulikuwa unafuka nikawa naona kama vile kuna hitilafu kubwa ya moto kwani kulikuwa na moshi na nilikuwa nimebananishwa,” alisema. 

Alisema alipotoka ndani ya gari aliona kifua kinambana huku akisikia maumivu makali katika mguu wa kulia.

“Na nilipotoka kifua kilikuwa kinauma, kiuno na mguu, nashukuru nimepokewa hapa na nimepewa huduma haya maumivu ya kubana yaliyokuwa yakinisumbua naona sio sana yamebaki maumivu ya mwili tu,” alisema. 

Alimshukuru Mungu kwa kutoka salama kwani alikuwa akiona kifo kipo mbele yake. “Mungu ni mwema, Mungu ni mwema,” alisema mwanasiasa huyo kijana.

Akizungumzia dereva wake, alisema hali yake ni nzuri na aliwaagiza wasaidizi wake wampigie kujua hali yake. Mwigulu aliwataka Watanzania kuendelea kumuombea ili apone. “Naomba waniombee Mungu ni mwema ametunusuru, Mungu ni mwema ametunusuru,” alisema Mwigulu.

Kwa upande wake, dereva wa gari hiyo, Johnson Malesi akizungumza kwa njia ya simu na gazeti la Habarileo, alisema ajali hiyo ni kama ya maajabu kwani imetokea katika eneo la wazi.

 Alisema ilitokea saa 2.45 asubuhi katika eneo la Migori mkoani Iringa ambako alikuwa akikwepa punda waliotokea ghafla barabarani. 

“Ilikuwa saa 2.45 asubuhi tulikuwa tunatoka Iringa kupitia barabara ya Mtera na tulikuwa tumefika Migori na tulikuwa tumeachana na kijiji na kulikuwa hakuna makazi ya watu.
Share:

Wizara ya elimu: Korea Scholarships academic year 2019-2021

Wizara ya elimu: scholarships opportunities tenable in the republic of korea for academic year 2019-2021

1.0 Call for Application

The general Public is hereby informed that, the National Institute for International Education (NIIED) under the Ministry of Education of the Republic of Korea is offering Graduate study opportunity to a Tanzanian citizen for the academic year 2019 Global Korea Scholarship: Korean Government Scholarship Program for International Students for a Graduate Degree (2019 Graduate GKS).

2.0 Mode of Application

All applicants are required to complete application form and attach all requested documents. Instructions for this Scholarship are obtained in the following website>>>>CLICK HERE FOR MORE DETAILS

Application forms and attached documents should be submitted to the Korean Embassy not later than 7th March, 2019

PHYSICAL ADDRESS

19TH Floor Golden Jubilee Tower,

Ohio Street, City Centre,

O. Box 1154,
DAR ES SALAAM.

Issued by

Permanent Secretary,

Ministry of Education, Science and Technology,

College of Business Studies and Law,

University of Dodoma (UDOM) Building No. 10,

P.O. Box 10,
40479 DODOMA.

The post Wizara ya elimu: Korea Scholarships academic year 2019-2021 appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 14,2019

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 14, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Wednesday, 13 February 2019

LAZARUS MSIMBE ATEULIWA KUWA MSIMAMIZI WA KITUME MOROGORO


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Padre Msimbe, alikuwa ni Makamu wa Shirika la Mungu Mwokozi, maarufu kama Wasalvatoriani.

 Itakumbukwa kwamba, Mheshimiwa Padre Msimbe alizaliwa tarehe 27 Desemba 1963 huko Homboza, Jimbo Katoliki la Morogoro. Baada ya masomo yake ya msingi na sekondari, alijiunga na masomo ya falsafa kwenye Seminari kuu ya Kibosho, Jimbo Katoliki la Moshi.

Baadaye aliendelea na masomo ya taalimungu, Seminari kuu ya Segerea, iliyoko Jimbo kuu la Dar es Salaam. Baada ya majiundo yake ya kitawa, tarehe 8 Desemba, 1987, Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa daraja Takatifu ya Upadre tarehe 21 Juni 1998.

 Mheshimiwa Padre Msimbe aliendelea na masomo ya juu huko London, Uingereza na kujipatia Shahada ya Uzamili katika Sheria za Kanisa kutoka katika Chuo Kikuu cha Uingereza.

 Baadaye pia alijiendeleza na hatimaye kujipatia shahada kwenye Sheria za Kimataifa kutoka katika Chuo Kikuu cha West-England, kilichoko Bristol, Uingereza.

Baada ya kurejea nchini Tanzania, alipangiwa utume wa kuwa ni mlezi wa Wapostulanti na Wanovisi wa Shirika la Mungu Mwokozi.

 Kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2012 alichaguliwa kuwa Padre Mkuu wa Kanda ya Shirika la Mungu Mwokozi, nchini Tanzania. Baada ya kumaliza muda wake wa uongozi, ameendelea kuwa ni mlezi wa Shirika kimataifa katika nyumba ya malezi "Mater Salvatoris" iliyoko Jimbo Katoliki la Morogoro.

 Hadi kuteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Msimamizi wa kitume, mwenye kuwajibika moja kwa moja na Vatican katika masuala yote ya Jimbo la Morogoro, alikuwa ni Makamu mkuu wa Shirika la Mungu Mwokozi nchini Tanzania. 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Share:

LUGOLA MVAA TUNDU LISSU "KATELEKEZA KESI...KWANINI HATAKI KURUDI KWENYE KESI YAKE?"


Wakati mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akiendelea na ziara zake nchini Marekani, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Kangi Lugola amemtaka kurejea nchini ili kusaidia upelelezi wa tukio lake la kushambulikwa kwa risasi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Februari 13, 2019 jijini Arusha, Lugola amesema Lissu ndio mwenye kesi hiyo, “Serikali inashindwa kuendelea na upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwake kwa sababu haina mashahidi muhimu.”

Lissu alishambuliwa mchana wa Septemba 7, 2017 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake Area D, mjini Dodoma wakati akitoka kuhudhuria mkutano wa Bunge.

Alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali na siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi, Kenya.

Alipata matibabu katika hospitali hiyo hadi Januari 6, 2018 alipohamishiwa Ubelgiji.

Hivyo, tangu Septemba 7, 2017 hadi Desemba 31, 2018, mwanasheria huyo mkuu wa Chadema ametibiwa kwa kipindi cha siku 480 sawa na mwaka mmoja, miezi mitatu na siku 24. Siku hiyo ndio aliruhusiwa kutoka hospitali licha ya kuelezwa kuwa bado yupo katika matibabu. Katika gari hilo alikuwa pamoja na dereva wake Adam Bakari ambaye hakujeruhiwa na risasi na Lissu amekuwa akieleza jinsi alivyomuokoa.

“Hii ni kwa mara ya kwanza kutokea nchini mlalamikaji kutelekeza kesi. Kwanini hataki kurudi kwenye kesi yake, aache kuwaeleza Wazungu kwa sababu wanaopeleleza kesi ni sisi na sio wao,” amesema Lugola.

Waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Mwibara ameyataka mataifa ya kigeni kuja nchini kuwekeza na kuwapuuza watu wanaotoa taarifa potofu kuhusu amani na utulivu uliopo nchini.

Na Mussa Juma, Mwananchi 
Share:

WANAOMTUKANA RAIS MAGUFULI SASA KUSAKWA HADI WHATSAPP


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelitaka jeshi la polisi kwa kushirikiana na TCRA kuhakikisha mtu yoyote atakaye mtukana, kumdhihaki, ama kufanya uchochezi dhidi ya Rais Dkt John Magufuli achukuliwe hatua mara moja.

Akiongea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kangi amesema, "wanaomtukana Rais kuanzia sasa wasakwe popote pale walipo wakamatwe".

''Haiwezekani Rais akatukanwa, haiwezekani kabisa, iwe kwenye magroup ya WhatsApp, iwe kwenye ujumbe mfupi wa simu au blog na hata aina yoyote ya mawasiliano wachukuliwe hatua za kisheria'', amesisitiza.

SIKILIZA HAPA CHINI

Share:

DADA ASIMULIA ALICHOAMBIWA NA GODZILLA DAKIKA CHACHE KABLA YA KUFARIKI DUNIA

Dada wa msanii Godzilla, Joyce Mbunda, amefunguka juu ya kile alichoambiwa na marehemu Godzila, wakati umauti ukimkuta.

Joyce amesema wakati umauti ukimkuta mdogo wake, yeye na mama yake walikuwa wamemshika baada ya kumuona anatapatapa, na ndipo alipomwambia dada yake asimuachie kwani kuna watu wanamfuata.

“Alinifuata chumbani kwangu akaniambia, sister naomba nilale hapa kidogo, maana kule kuna watu, watu wengi sana wananifuata, na mimi sitaki, nikamuacha alale

"Dakika kumi hazijafika akatoka ananiambia naenda nje, nikamwambia twende wote, mama akamshika na mimi nikamshika, tunamzuia atulie maana anahangaika, tulivyomshika analegea huku anakaa chini, alikuwa ananiambia cha tu sister, nimemshikilia hivi, namwambia niambie kitu, anashindwa hata kuzungumza, mpaka analegea yuko mikononi mwangu”, amesema Joyce.

Joyce ameendelea kwa kusema kwamba Godzilla alikuwa mtu mwenye upendo, na mtu ambaye alikuwa karibu sana na familia yake.

Godzila amefariki alfajiri ya leo baada ya kuzidiwa, kutokana na maradhi ya sukari na presha iliyokuwa ikimsumbua.
Share:

SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA HUDUMA ZA AFYA

DODOMA. Mpango wa Taifa wa Damu salama umetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama. Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu…

Source

Share:

WODI YA WAZAZI HOSPITAL YA MPWAPWA YAZIDIWA NA WAGONJWA

Na Stephen Noel -Mpwapwa Akina mama wanaojifungua Katika wodi ya wazazi Hospital ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wanalazimika kulala wazazi wawili kwenye kitanda kimoja kutokana na uchache wa vitanda pamoja na udogo wa wodi hiyo Kauli hiyo imetolewa na Mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dkt, Hamza Mkingule alipo kuwa akitoa taarifa mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi Bi Laula Ngozi katika ziara yake aliyo ifanya wilayani hapa kwa lengo la kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama hicho. Dkt Mkingule amesema Hospital Hiyo iliyojengwa miaka…

Source

Share:

WANANCHI MAKAMBAKO WAISHUKIA HALMASHAURI KUHUSU FIDIA

Na Amiri kilagalila Baadhi ya Wakazi wa mtaa wa Makatani Kata ya Lyamkena halmashauri ya Mji wa Makambako wameitupia lawama halmashauri ya mji huo kwa kuchelewa kulipa fidia ya eneo lililochukuliwa na serikali tangu mwaka 2014 kwa ajili ya ujenzi wa soko la mazao hali ambayo imetajwa kukwamisha shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kudumu katika eneo hilo. Wakizungumzia kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo wakazi wa mtaa huo wamesema serikali imesababisha kuongezeka kwa ugumu wa maisha kwa wakazi wa mtaa huo ambao wameathiriwa na mpango wa ujenzi wa soko…

Source

Share:

Picha: BALOZI IDD AUNGURUMA SHINYANGA MJINI..AWATAKA WANA CCM KUACHANA NA SIASA ZA MAKUNDI



Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga amehutubia mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele ambaye ni Makamu wa Rais Bunge la Afrika.

Mkutano huo ambao ni sehemu ya kusherekea miaka 42 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi umefanyika leo Jumatano Februari 13,2019 katika Viwanja vya Zimamoto vilivyopo Mjini Shinyanga.

Akihutubia mkutano huo amewataka wanaCCM kuwa na umoja,kushirikiana na kuacha siasa makundi kwani makundi yanagawa chama.

“Tushirikiane,tushikamane ili chama chetu kiwe imara na tuweze kushinda kwenye uchaguzi,nawasihi muache siasa za makundi”,amesema Balozi Idd.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd  ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

PICHA NYINGI ZAIDI ZINAKUJA HIVI PUNDE
Share:

NDEGE YAANGUKA NA KUUA WATU WATANO KENYA

 Watano wamefariki dunia leo Jumatano Februari 13, 2019 baada ya ndege ndogo waliyokuwa wanasafiria kuanguka katika kaunti ya Kericho nchini Kenya.

Ndege hiyo ilianguka kwenye msitu wa Londiani ikiwa na abiria watano, mkuu wa kikosi cha anga, Kamanda Rodgers Mbithi amesema abiria wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wamefariki dunia.

Amesema waliopoteza maisha katika ndege hiyo Cesna 206-5-Y BSE ni wanaume watatu na wanawake wawili ambao hawajatambulika ni raia wa nchi gani.

Kwa mujibu wa kamanda wa kaunti ya Londiiani, Justus Munyao, ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Safari ambayo huchukua abiria kutoka Ol Kiombo kuelekea Kaunti ya Turkana.

Amesena tukio hilo lilitokea saa 5 asubuhi kwenye msitu wa Masaita.

Kamanda wa Kikosi cha Rift Valley, Edward Mwamburi amesema polisi wameshafika eneo la tukio.
Via Mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger