Tuesday, 12 February 2019

SIMBA WALIPA KISASI...WAWACHAPA WAARABU AL AHLY 1 - 0


Dakika 90 za Mchezo kati ya Simba SC na Al Ahly zimemalizika kwa Simba kuwachapa Al Ahly 1-0

Dakika ya 90 + 3 Kagere anadondoka, mpira unaendelea
Dakika ya 90 Waarabu wanapaisha mpira mawinguni wakiwa eneo la hatari.
Dakika nne zinaongezwa Taifa, Simba wameacha kukaba
Dakika ya 90 mwarabu anakosa bao la wazi
Dakika ya 89 Kotei anapiga mpira nje kwa waarabu
Dakika ya 88 Waarabu wanaanza safari kwa Manula baada ya Dilunga kucheza faulo.
Dakika ya 87 Manula anaamka na mpira unaanza kwenda kwa Waarabu.
Dakika ya 85 Manula alikwenda hewani wakati anashuka anaangukia mgongo.
Dakika ya 84 Simba wanaanza mashambulizi kwenda kwa Mwarabu, Mpira unatolewa nje anarusha Zimbwe, Kagere, wanadaka Waarabu.
Dakika ya 83 Mkude anauza kwa waarabu.
Dakika ya 82 Waarabu wanapata faulo inachezwa vizuri ila kichwa cha Mwarabu kinapaa Mawinguni.
Dakika ya 81 Bocco anatolewa nafasi yake inachukuliwa na Dilunga.
Dakika ya 81 Chama anapoteza Mpira kwa waarabu wanaanza safari kwa Manula sasa, Juuko anacheza rafu 
Dakika ya 80 Manula ananyanyuka, Waarabu wanaanza safari kumfuata sasa.
Dakika ya 79 bado Manula anagangwagangwa Uwanjani.
Dakika ya 77 Zana anakaba,ila bado waarabu wanamuwinda Manula anaokoa baada ya mabeki kukabia kwa macho na kumuumiza Manula.
Dakika ya 76 Kagere alipata pasi kutoka kwa Kotei akapaisha mpira mawinguni.

Dakika ya 75 Waarabu wanamchezea rafu Kotei
Dakika ya 75 bado waarabu wapo kwa mshikaji Manula
Dakika ya 74 waarabu wanaanza safari kwenda kwa Manula wao karibu na eneo la hatar sasa
Dakika ya 73 waarabu wanaanza safari kwa Manula
Dakika ya 72 Kotei anacheza rafu kwa waarabu wanapata faulo haziai matunda.
Dakika ya 71 Okwi anarejea Uwanjani kuwavaa waarabu.
Dakika ya 69 Okwi anatolewa akiwa kwenye machela.

Dakika ya 67, Mkude, Bocco mchezaji wa Simba anapata majeraha dakika ya 68 Okwi baada ya kuanguka na kupoteza fahamu kwa muda wa dakika kadhaa.

Dakika ya 66 Chama anatoa Mpira nje
Dakika ya 64 Kagere anaandika bao tamu na kumyayua Mohamed 'Mo' akitumia pasi ya Bocco ya kifua baada ya kupokea pasi ya mmwaga maji Zana.
Dakika ya 63 Waarabu wanamfuata Manula , Wawa anaanua hatari.

Dakika ya 62 Bocco anatoa Boko akiwa eneo la hatari baada ya kupewa pasi na Okwi
Dakika ya 61 Simba wanarusha kwa kumtumia Mohamed 
Dakika ya 60 Zana aliingiza majaro ya hatari eneo la hatari ila mira ukababatizwa ukatoka nje goal kick.

Dakika ya 59 Juuko anapoteza kwa waarabu, Wawa anafanya yake, Chama, Kagere anapoteza.
Dakika ya 58 Mkude anamsumbua Mwarabu na kumchezea faulo.

Dakika ya 57 Waarabu wanaanza safari kwa Manula Juuko anaanua
Dakika ya 57 Wawa anauza kwa waarabu.
Dakika ya 56 Juuko Murshid anagangwa gangwa guu lake la kushoto.

Dakika ya 55 Okwi anamchezea faulo Mwarabu karibu na eneo la hatari, Waarabu wanatumia nafasi ila mpira unapaa mawinguni.
Dakika ya 54 Zana anauza kwa Waarabu
Dakika ya 53 waarabu wanaanza safari kwenda kwa Manula, wanarejea nyumbani kisha wanaendela kupitia kwa Mohamed, Ramadhan, Khalid, Junior Wawa anazuia.
Dakika ya 52 Kager anashindwa kutumia nafasi ya mpira wa Zana.

Dakika ya 51 Waarabu wanapata faulo na mlinda mlango wao anapata hudua ya kwanza.

Kipindi cha pili Simba wanakosa nafasi za wazi tatu, dakika ya 45 Okwi, dakika ya 46 Okwi na dakika ya 49 Bocco.

Dakika 45 zinakamilika huku Simba wakishindwa kutumia nafasi walizozipata pamoja na Al Ahly nao wanakwenda mapumziko wakiwa ngoma droo.

Dakika ya 45 Waarabu wanaanua kona wanalifuata lango la Manula, Zana anachezewa faulo na waarabu.

Dakika ya 45, Chama anakataliwa na Warabu, Zana, Chama, Mkude, Chama, Kagere, kona.

Dakika ya 44 Waarabu wanalifuata lango la Manula kama hawana haraka hivi leo.
Dakika ya 43 Waarabu wote wanarudi langoni.
Dakika 42 Mohamed Hussen anafanya shambuliz mlinda mlango anadaka.
Dakika ya 42 Okwi anaangushwa eneo la hatari mwamuzi anapeta.
Dakika ya 41 Waarabu wanaliandama lango la Manula, Wawa anaosha majalo huko.

Dakika ya 40 Kagere anahindwa kutumia pasi ya Chama akiwa eneo la hatari na kuifanya iwe kona baada ya mlinda mlango kudakia nje.
Dakika ya 40 Waarabu wanaliandama lango la Manula.

Dakika ya 39 Kwasi anatoka anaingia Mohamed Hussen wa Simba.

Dakika ya 38 Kona haizai matunda, Kagre anatumia nguvu mpira unatoka nje.
Dakika ya 38 Kona inapigwa kwa sasa na Okwi.

Dakika ya 36 Simba wanapata kona baada ya Kwasi kupiga shuti eneo la hatari, Kwasi anazidiwa misuli inakaza anapewa huduma ya kwanza.
Dakika ya 35 Waarabu wanaendelea kuliandama lango la Manula, anaokoa sasa Simba wamezidiwa nguvu eneo la ulinzi muda huu hatari sana.
Dakika ya 33 waarabu wanafanya Counter attack, All Manashira, Amri, Mohamed,Mohamed, Mahanuz wanatoa nje ya hatari wachezaji wa Simba wanakabia macho hapa.
Dakika ya 33 Wawa, Chama, Mkude, Okwi, Chama, Kwasi, Bocco waarabu wanatoa mpira nje.
Dakika ya 32 Kagere anazidiwa ujanja na waarabu
Dakika ya 31 James Kotei, Bocco anazuiliwa na Mohamed Ally.

Dakika ya 31 waarabu wanafanya shambulizi kwa Manula anaokoa.

Dakika ya 30 Kwasi anatoa pasi kwa warabu akiwa eneo la hatari la waarabu.

Dakika ya 29 waarabu wanaanza mpira kwa kurusha kwenda kwa Manula.

Dakika ya 29 Chama anashindwa kupeleka mashambuliz kwa waarabu baada ya mbele kukosekana wachezaji.

Dakika ya 28 Waarabu wanakwenda lango la Manula wakiwa na Ramadhani, Okwi anazuia.
Dakika ya 27 Chama anafanyiwa faulo baada ya kuzidisha mbwembwe.

Dakika ya 26 Waarabu wanaingia eneo la Simba Kwasi anazuia.

Dakika ya 25 Manula anaanzisha mpira, Kagere, Chama, Okwi, Kwasi, Chama waarabu wanatoa.

Dakika ya 24 Wawa anaanzisha mashambulizi kwa Jonas Mkude anampa Kwasi, Kotei, Mkude, Okwi anakosa bao kwa kupaisa mpira mawinguni.

Dakika ya 22 Juuko Murshid anaosha hatari eneo lao.

Dakika ya 22 Kagere anamchezea rafu mchezaji wa Al Ahly.

Dakika ya 21 Al Ahly wanafanya jaribio la kwanza kwa Simba wanakosa
Dakika ya 20 Al Ahly wanapata faulo baada ya mchezaji wa Simba kucheza rafu
Dakika ya 19 Simba wanaanza mashambulizi kupitia kwa Zana Coulibaly
Dakika ya 18 Bocco anapaisha mpira mawinguni akiwa karibu na eneo la hatari
Dakika ya 18 Al Ahly wanarusha kwenda Simba
Dakika ya 17  Simba wanarusha
Dakika ya 16 Wawa anaanzisha mashambulizi kwenda kwa Al Ahly
Share:

WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Na.Amiri kilagalila Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe imesikiliza kesi ya mauaji namba moja ya mwaka 2019 dhidi ya jamhuri na watuhumiwa watatu waliohusioka na mauaji ya watoto watatu katika kijiji cha ikando kata ya kichiwa wilayani Njombe. Akisoma kesi hiyo mbele ya mahakama wakili mwandamizi wa serikali Ahmed Seif,alisema kuwa mtuhumiwa namba moja Joel joseph Nziku mbena (35)dreva anaisha Magegere mjini Makambako,mshatakiwa namba mbili Nasson Alfredo kaduma (39) mkulima anaishi kijiji cha Ibumila na mtuhumiwa namba tatu Alphonce Edward Danda (51)naye anaishi katika kijiji cha Ibumila wote wanashtakiwa…

Source

Share:

Picha : MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ATEMBELEA MGODI WA BUZWAGI KAHAMA

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amefanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Februari 11,2019,Balozi Idd ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga alipongeza viongozi wazawa wanaoendesha mgodi huo kwa kuwekeza miundombinu ya huduma za elimu afya na barabara.

"Zamani nilikuwa nasikia tu Buzwagi Buzwagi nashukuru sana Mkuu wa Mkoa nashukuru sana Meneja Mkuu wa Mgodi kwa fursa hii ya kuja kutembelea katika Mgodi wenu lakini kitu kinachonifurahisha ni huduma kwa jamii ya hapa Kahama mmenionyesha skuli ‘shule’mlizokarabati,barabara,na kadhlika.

Pia nimeambiwa kuna hospitali mnajenga hayo yote kwa kweli ni kitu kizuri kwamba rasilimali hii inafaidisha vile vile wanajamii nawapongezeni sana muendelee ili Wana Kahama na sehemu nyingine za Mkoa wa Shinyanga waendelee kunufaika na rasilimali yao",aliongeza.

Akimkaribisha Mgodini hapo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack alisema "Mheshimiwa Makamu wa Rais Zanzibar leo tupo kwenye Mgodi huu wa Buzwagi ambao ni pamoja na mali zilizopo kwenye Mkoa ambao wewe ni mlezi tumesema upite kwenye mgodi huu ili kwa kuwa wewe ni Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga ni muhimu uone na rasilimali zilizomo hivyo pamoja na ujumbe ulioambatana nao mtaangalia pamoja na mambo mengine uzalishaji wa Dhahabu".

Naye Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu alimshukuru Makamu wa Rais kwa kufanya ziara hapo Mgodini.

"Tumefarijika sana kupata ugeni huu tunashukuru sana, tukipata ugeni kama huu tunafurahi sana karibuni sana na kwa fursa kama hii ambavyo umeambatana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi tunaona ni vyema tupate nafasi kukuonyesha jinsi mgodi umeshiriki katika maendeleo ya jamii na namna tunavyozalisha dhahabu",alisema Busunzu.
Kulia ni Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd wakati akifanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akimwelezea Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kuhusu shughuli za uzalishaji zinazofanyika mgodini.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiuliza jambo.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akifafanua jambo kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd 
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akiongoza msafara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kutembelea mgodi wa Buzwagi.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza alipofanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akizungumza katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akishikana mkono na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akiwakaribisha wageni mbalimbali walioambatana na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kutembelea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alipotembelea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa, katikati ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Meneja Mahusiano ya Jamii wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Dr. Zumbi Musiba akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Meneja Mahusiano ya Jamii wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Dr. Zumbi Musiba akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ukitoka mgodini
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi Bw. Benedict Busunzu akipunga mkono kumuaga Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd

Picha kwa hisani ya kitengo cha Mawasiliano Buzwagi
Share:

MSIMU WA SITA WA COKE STUDIO WAZINDULIWA


Mkurungezi mkuu wa Coca cola Kwanza Basil Gadzios akizungumza na wageni waliofika kuhudhuria uzinduzi wa msimu wa Sita wa Coke Studio iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa mauzo na masoko, wa CocaCola Kwanza, Josephine Msalilwa akizungumza na wageni waliofika kuhudhuria uzinduzi wa msimu wa Sita wa Coke Studio iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Msanii Nandy akiimba huku akicheza na Mkurungezi mkuu wa Coca cola Kwanza Basil Gadzios wakati wa azinduzi huo.
Msanii Harmonize akizungumza katika uzinduzi huo. Wengine ni Rayvan, Jux na Nandy.
Wageni waalikwa wakifuatilia.
Msanii Jux akitoa burudani.
Wageni waalikwa wakifurahia.
Msanii Harmonize akifanyiwa mahojiano na wanahabari.
Mtangazaji wa Times Redio, Lil Ommy akipata selfie na msanii Jux.
Dj D-Ommy akitoa burudani huku shabiki akijiachia.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Msimu Mpya wa Coke Studio Africa umezinduliwa rasmi Tanzania katika halfa iliyofanyika klabu ya burudani Lifepark Mwenge.

Tanzania itawasikilishwa na wasanii watano watakaotumbuiza katika msimu wa sita wa Coke Studio.

Akizungumza mbele ya wageni waalikwa Mkurungezi mkuu wa Coca cola Kwanza Basil Gadzios amekiri kufurahishwa vipaji na uwezo wa wasanii watanzania watakao shiriki kwenye msimu huu mpya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mauzo na masoko wa Cocacola Kwanza, Josephine Msalilwa, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wasanii hao kuwa ni Faustina Charles' Nandy', Raymond Mwakyusa'Rayvanny', Rajabu Abdul'Harmonize', Juma Jux na Mimi Mars.

Amesema wasanii hao wataungana na wasanii wengine 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kutimiza idadi ya wasanii 25 watakaokuwa katika msimu wa mwaka huu.

"Nchi nyingine msanii huchukuliwa mmoja lakini kwa Tanzania imekuwa tofauti kidogo, hii yote inaonesha ni namna gani muziki Watanzania yani bongo fleva umekuwa ukikubalika na wasanii wake kupendwa," amesema Josephine.

Nao wasanii akiwemo Rayvanny amesema anashukuru kuwa mmoja wasanii watakaotumbuiza katika msimu huu huku akieleza hii ni mara yake ya pili.

Msanii Nandy amesema kushiriki Coke Studio 2019 kunakusaidia kukutana na wasanii kutoka Africa wenye vipaji lukuki... nafasi hii kwa msanii yoyote ni kitu cha kujivunia sana na pia inasaidia kutengeneza kazi tofauti na kufanya jina au brand ya msanii kuimarika na nguvu katika soko la muziki Afrika na dunia nzima.

"Coke Studio ni kitu kikubwa, na hakuwahi kutegemea kukutana na msanii mkubwa kama Skales kutoka nchini Nigeria ambaye ameurudia wimbo wake wa Ninogeshe na kunuelezea kuwa ni msanii ambaye ana ushirikiano mzuri," amesema.
Share:

WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE WAPANDISHWA MAHAKAMANI

Washukiwa watatu wa utekaji na mauaji ya watoto wa chini ya miaka 10 wilayani Njombe, wamepandishwa mahakamani hii leo.

Watuhumiwa hao waliowekwa wazi kwa mara ya kwanza hii leo ni Nasson Kaduma, Joel Nziku na Alphonce Danda.

Wote wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe.

Nje ya mahakama hiyo ulinzi mkali wa polisi umeimarishwa na msafara wa watuhumiwa hao ukisindikizwa na magari sita ya polisi.

Watoto takribani 10 wameshauawa toka visa hivyo vya kutamausha kuanza kuripotiwa mwezi Disemba.

Miili ya watoto hao imekutwa ikiwa imenyofolewa baadhi ya viungo kama matumbo, vidole, pua na macho, wauaji hao pia wamekuwa wakinyofoa viungo vya siri vya watoto hao.

Mamlaka nchini Tanzania zimekuwa zikihusisha mauaji hayo na imani za kishirikina, waganga wa kienyeji wanalaumiwa kwa kuwaaminisha watu kuwa viungo vya binaadamu vinavuta bahati na utajiri.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Ijumaa aliliambia Bunge kuwa tayari watu 29 wameshakamatwa kutokana na matukio hayo, na kusema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Miongoni mwa waliokamatwa ni wafanyabiashara maarufu wa eneo hilo pamoja na waganga wa jadi.

Chanzo:Bbc
Share:

MTOTO WA MIAKA 6 AAPISHWA KUWA POLISI

Askari Polisi wa Marekani ametokwa machozi wakati akimwapisha kwa heshima mtoto Abigail Arias (6) kuwa polisi.

Mtoto huyo anayesumbuliwa na saratani ya kibofu kwa miaka miwili sasa alihudhuria hafla hiyo ya kuapishwa akiwa na familia yake, huku akisema anaipenda kazi hiyo na ataifanya kwa weledi.

Polisi wa Texas, walituma taarifa za kumwapisha mtoto huyo katika hafla iliyofanyika mjini Texas kuwa polisi wa mji wa Freeport wenye watu 12,000 uliopo maili 50 kutoka Kusini mwa Houston.

Polisi amwaga machozi

Ofisa wa polisi aliyekuwa akimwapisha mtoto huyo alishindwa kujizuia na kuanza kulia kwa kwikwi huku akimkumbatia baada ya kumaliza kumwapisha.

“Nitapambana na wahalifu’’ hayo ni maneno ya mtoto huyo aliyotoa baada ya kuapishwa huku akishangaza wengi waliokuwa wamehudhuria hafla hiyo

Wakati akiapishwa mtoto huyo alikuwa amevalia vazi la polisi ambalo lilimpendeza na kumfanya kuwa na faraja wakati wote wa hafla hiyo iliyokuwa imehudhuriwa na familia yake pia na maofisa kadhaa wa polisi.

Mama mzazi wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la Ilene Arias, aliliambia Shirika la Habari la CNN kwamba huu ni muda wa kufurahia maisha ya mtoto huyo kwani watalia wiki chache zijazo.

Mama huyo alitoa kauli hiyo huku akiwa anabubujikwa na machozi mbele ya waandishi wa habari, akimaanisha kwamba mtoto wake huyo hawezi kuendelea kuishi kwa muda mrefu.

Kilio cha mama huyo kinakwenda sawa na polisi aliyekuwa akimwapisha ambaye alishindwa kujizuia na kuanza kulia Kamanda huyo wa Freeport, Raymond Garivey, alisema mtoto huyo anaishi kwa nguvu za Mungu tu.

“Tunatakiwa kumuombea mtoto huyu kwa sababu inafahamika anaumwa kitu gani hapa anaishi kwa miujiza tu, hivyo tumuombee,’’ alisema.

“Nataka kuhakikisha ndoto zake zinatimia na kuwa za kweli hivyo leo tumemwapisha kuwa askari kamili wa Marekani kwa sababu ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu,’’ alisema.

Baada ya kuapishwa kuwa askari Arias alikabidhiwa ofisi na bunduki kama walivyo askari wengine huku akionyesha tabasamu.

Via Mwananchi
Share:

WAFANYABIASHARA MITANDAONI KUSAKWA ILI WALIPE KODI

Serikali ya Mkoa wa Iringa imetangaza kuwasaka wafanyabiashara wa mitandaoni kama moja ya mkakati wake wa siku 90 hadi Mei 7, mwaka huu, unaolenga kila anayefanya biashara mkoani humo alipe kodi au awe na kitambulisho cha machinga.

Mkakati huo ulitangazwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi baada ya kupokea taarifa ya ugawaji wa vitambulisho 25,000 vya awali vya machinga katika hafla iliyohusisha ugawaji wa nyongeza ya vitambulisho vingine 35,000 kwa halmashauri tano za mkoa huo.

Taarifa hiyo inaonesha tangu vitambulisho hivyo vya awali 25,000 vianze kugaiwa kwa Sh 20,000 kwa wafanyabiashara ndogo wa halmashauri hizo Desemba mwaka jana, vitambulisho zaidi ya 9,000 vilikuwa vimeshachukuliwa hadi wiki iliyopita. 


Akitangaza mkakati huo ambao lengo lake pia ni kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, Hapi alisema; “Ndani ya mkoa wa Iringa hatutaki kuwa na mjasiriamali ambaye hayupo katika moja kati ya mifumo mitatu inayoiwezesha serikali kuwatambua.”

Alitaja mifumo hiyo kuwa ni ule wa leseni za biashara zinazotambuliwa na halmashauri, unaopitia Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo vilivyoanza kutolewa hivi karibuni na Rais John Magufuli. 


Alisema anayefanya biashara bila kuwa na moja kati ya vitu hivyo vitatu, huyo hana tofauti na mhujumu uchumi na ni lazima atafutwe ili afuate utaratibu.

“Wanauza nguo, keki, vyakula, bidhaa za tiba za jadi na biashara yoyote ile mkoani kwetu kupitia mitandao ya kijamii, katika simu za mikononi na vifaa vingine vinavyotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano, watatafutwa ili wasajiliwe katika moja ya mifumo hiyo,” alisema.

Alisema mzigo wa kuendesha nchi hii ni wa kila Mtanzania mwenye shughuli halali inayomuingizia kipato na akataja watu wengine ambao hawapaswi kusahaulika katika utaratibu huo kuwa ni wale wanaoendesha vikundi vya kuweka na kukopa fedha. 


“Wanaokopa kwenye Vicoba kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali lazima watafutwe na wapewe vitambulisho na kama biashara zao zina sifa za juu ya vitambulisho waingizwe kwenye utaratibu wa kulipa kodi kupitia TRA,” alisema.

Alisema mkoa umetoa muda wa miezi mitatu kwa wajasiriamali wote kuingia katika moja ya mifumo hiyo na “baada ya hapo tutafanya oparesheni kubwa ya kuwasaka wasio kwenye mfumo wowote kati ya hiyo.”


Aidha Mkuu wa Mkoa aliiagiza TRA kutumia pia siku hizo 90 kufanya msako wa wafanyabiashara walio katika mfumo wa Malipo ya Kielektroniki (EFDs); wanaouza bidhaa na huduma bila kutoa risiti za mashine
Share:

URUSI KUZIMA MTANDAO WA INTANETI KUJILINDA NA MAADUI

Urusi chini ya Rais Vladimir Putin imekuwa ikilaumiwa vikali na nchi wanachama wa Nato kwa mashambulizi ya kimtandao.

Urusi inajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda, na hivyo kujitoa kwenye mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.

Zoezi hilo litafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.

Rasimu ya sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana.

Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe mosi Aprili, lakini siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.


Rasimu hiyo ya sheria, iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga Urusi.

Nchi wanachama wa Nato na washirika wake wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.

Njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.

Chanzo:Bbc
Share:

RAMSEY AMESAINI MAKUBALIANO KUJIUNGA NA JUVENTUS

Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey ametia saini makubaliano ya awali ya kujiunga na klabu ya Juventus msimu ujao kwa kitika cha pauni £400,000 kwa wiki.

Nyota huyo wa miaka 28 amekubali mkataba wa miaka minne utakaomwezesha kujiunga na ligi ya champions ya Italia bila malipo baada ya kuwa Arsenal kwa miaka 11.

Ramsey alifuzu sehemu ya kwanza ya uchunguzi wa kimatibabu mwezi Januari, na kuchagua Juve baada ya kushauriana na wadau kadhaa wa klabu hiyo.


Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales unakamilika Juni 30 na Gunners hawatapokea malipo yoyote atakapo ondoka.

Ikithibitisha mpango huo, Juventus imesema italipa ada ya pauni milioni £3.2 lakini haikuelezea ada hiyo ni ya nini.

Arsenal imesema mchango wa Ramsey ulikuwa mkubwa sana katika klabu hiyo na kuongeza kuwa atasalia katika kumbu kumbu ya historia ya mashabiki.

Akiandika katika mtandao wake Instagram, Ramsey aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kusema kuwa ataendelea kuwaunga mkono 100%".

"Nasikitika kuondoka baada ya miaka 11 ya ufanisi sijui nielezee vipi hisia zangu muda huu. Asanteni."  Aliandika Ramsey

Tovuti ya Juventus imemkaribisha Ramsey kwa kuandika kwamba atakuwa mkazi wa Wales wa tatu kuiwakilisha klabu hiyo baada ya John Charles na Ian Rush.

Chanzo:Bbc
Share:

TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA 12 02 2019 SALAH KUHAMIA JUVENTUS MWISHONI MWA MSIMU

Juventus wanajipanga kutoa kitita cha pauni milioni 175 ili kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 26. (Sky Arabia)

Mustakabali wa Maurizio Sarri kama kocha wa Chelsea utaamuliwa ndani ya wiki mbili zijazo. (Telegraph)

Wachezaji wa Chelsea walifanya kikao maalum cha kurekebishana katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham jana Jumatatu kufuatia kipigo walichopata cha 6-0 dhidi ya Manchester City. (Mail)

Kocha wa Derby Frank Lampard amepuuzia uvumi kuwa huenda akarithi mikoba ya Maurizio Sarri endapo Chelsea itaamua kumfukuza. (Evening Standard)

Beki wa Tottenham Juan Foyth, 21, amefichua kuwa alikataa kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain ili ajiunge na Spurs mwaka 2017. (Goal)

Barcelona wamefikia makubaliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili mshambuliaji wao raia wa Serbia Luka Jovic, 21, mwishoni mwa msimu. (Diario Sport)

Mshambuliaji wa Juventus raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, anakaribia kufikia makubaliano ya kuhamia Real Madrid mwishoni mwa msimu. (AS)

Kiungo wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot, 23, amekuwa akihusishwa na klabu kadhaa na sasa Man United wameingia kwenye mbio za kumsajili

Manchester United wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot, 23,mwishoni mwa msimu. (AS - via Mirror)

Chanzo:Bbc
Share:

TAHA WAJIPANGA KUIFIKISHA TANZANIA OLIPINKI 2025

Na Stephen Noel Mpwapwa -Michezo. BARAZA la michezo Tanzania imetakiwa kuongeza nguvu Katika kuwekeza kwenye mchezo midogo midogo Kama mpira wa mikono (Handball) ili kuweza kumudu kuitangaza Tanzania Katika ulimwengu wa kimichezo sehemu mbalimbali ya ndani na nje ya nchi. Kauli hiyo imetolewa Mwenyekiti wa baraza la michezo na katibu tawala wa wilaya ya Mpwapwa Bi Salah Komba alipo kuwa akifunga Kongamano la mpira wa mikono lililo fanyika kwa siku tano wilayani Mpwapwa Kongamano hilo lililo andaliwa na Chama cha mpira wa mikono Tanzania (TAHA) kwa kuwajengea uwezo walimu wa…

Source

Share:

KATIBU MKUU VIJANA CCM ASHANGAZWA NA WANASIASA WANAOICHAFUA NCHI UGHAIBUNI

Na Amiri kilagalila Viongozi mbali mbali wa chama cha mapinduzi CCM wamewataka wanasiasa na watanzania kwa ujumla kuungana kwa pamoja katika kupambana na vitendo vinavyoendelea katika baadhi ya maeneo nchini yakiwemo mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe kuliko kuendelea na siasa za uchochezi katika mataifa ya ughaibuni. Hayo yalisemwa na katibu mkuu wa umoja wa vijana Taifa ndg.Raymond Mwangwala wakati akizungumza na baadhi ya wazee na viongozi wa dini katika ukumbi wa Turbo uliopo Njombe mjini. “Wazazi wangu tumepoteza watoto hatuelewi ni nani alikuwa Rais katika hao,hatuelewi nani alikuwa mchungaji…

Source

Share:

SERIKALI YATANGAZA KUZIMA INTANETI ILI KUJILINDA NA MAADUI

Serikali ya Urusi chini ya Rais Vladimir Putin inajipanga kuzima mtandao wa intaneti kwa muda, na hivyo kujitoa kwenye mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.

Zoezi hilo litafanya mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya ya kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.

Rasimu ya sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana.

Jaribio hilo linatarajiwa kufanyika kabla ya tarehe mosi Aprili, lakini siku rasmi ya kuzimwa mtandao haijatajwa.

Mvurugano mkubwa

Rasimu hiyo ya sheria, iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga Urusi.

Nchi wanachama wa Nato na washirika wake wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.

Njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.
Kwa sasa, kuna taasisi 12 zinzoshughulikia suala la utolewaj na matumizi ya anuani hizo na hakuna hata moja iliyopo Urusi.

Hata hivyo tayari kuna chapa nyingi za mfumo huo wa DNS nchini Urusi hali inayoonesha kuwa nchi hiyo inaweza kuendelea na shughuli zake za kimtandao hata ikitokea imetengwa leo.

Watoa huduma za intaneti wanatarajiwa kuelekeza mawasiliano yote yanayopita kwao kwenye vituo vya serikali kwenye zoezi hilo. Mawasiliano yote ya ndani ya Urusi yataruhusiwa kuendelea lakini yale yatokayo nje ya nci yataminywa.

Mwishowe, serikali ya Urusi itakuwa na ubavu kama wa China wa kupanga mawasiliano gani raia wake wapate kutoka nje ya nchi.

Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa watoa huduma za intaneti nchini humo wanakubaliana na mabadiliko hayo lakini wanatofautiana kwenye namna gani utekelzwaji wake uwe. Wanaamini jaribio hilo litazaa "mvurugano mkubwa" kwa matumizi ya mtandao ya nchi hiyo, umeandika mtandao wa ZDNet.
Serikali ya Urusi inawapa fedha watoa huduma ya intaneti nchini humo ili kuboresha miundombinu yao kuendana na mipango yake ya baadae.

Hata hivyo, kuna uwezekano wa watu kuchupa mazuio hayo ya serikali kwa kutumia mitandao binafsi (VPNs) - ambayo hudanganya mahala kompyuta ama simu janja ilipo na hivyo vidhibiti kushindwa kuzizui kupata mawasiliano yaliyokatazwa.

Hata hivyo, baadhi ya nchi kama China zimekuwa wakali kwa wale wanaotumia tenkolojia hiyo. Ukikutwa unatumia ama kusambaza bila kibali teknolijia hiyo nchini China unaweza kutupwa jela.

Mara chache, nchi hujikuta zimejitoa kwenye mawasiliano ya intaneti kwa bahati mabaya - ilitokea hivyo mwaka 2018 nchini Mauritania kwa siku mbili baada ya nyaya ya chini ya bahari inayopeleka mawasiliano hayo kukatika. Meli ya kuvua samaki inasadikiwa kusababisha ajali hiyo.

Chanzo- BBC
Share:

AMUUA MWANAFUNZI KWA KUMCHINJA NA SIME KISA PETE

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kereto Likoko [Mmasai] kwa madai ya kumuua Mwanafunzi Samson Conradi anayesoma katika Chuo cha Faraja kwa kumkata na sime shingoni kwa madai ya kushindwa kumlipa fedha ya pete ambayo alikuwa akiuza.

Akizungumza jana Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,”amesema Kamanda Issah
Share:

OFISA TAKUKURU MATATANI KWA TUHUMA YA KUMBAKA MTOTO WA DADA YAKE

Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Rukwa, Jonas Jackson (34) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kisha kumlawiti mtoto wa dada yake aliyekuwa akiishi naye.

Ofisa huyo alikamatwa Februari 7, 2019 baada ya mtoto huyo kwenda kuripoti kituo kikuu cha polisi mjini Sumbawanga kufuatia kuchoka kufanyiwa vitendo hivyo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa jana Jumatatu Februari 11, 2019 baada ya mlalamikaji mwenye umri miaka 18, kwenda polisi kutoa taarifa ya vitendo vya unyanyasaji anavyofanyiwa.

Msichana huyo amedai amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo na mjomba wake tangu Septemba, 2018.

Amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo mara kwa mara anapotoka kwenye starehe zake na kurejea nyumbani akiwa amekunywa pombe alikuwa na tabia ya kumnywesha pombe, kuanza kumbaka na kumwingilia kinyume na maumbile.

Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi na muda wowote atafikishwa mahakamani.
Share:

MKURUGENZI WA MABASI YA MWENDO KASI KORTINI KWA KUSABABISHA HASARA YA BILIONI 2

Mkurugenzi wa UDART, Robert Kisena(46) na wenzake watatu wamesomewa mashitaka 19 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo utakatishaji fedha wa Mil.603 na kuisababishia hasara UDART ya Bil.2.41.


Mbali ya Kisena, Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Cheni Shi (32).

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali, George Barasa, Ester Martin, Moza Kasubi na Imani Imtumezizi.

Barasa alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka hayo likiwamo moja la kuongoza uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa, wizi wakiwa wakurugenzi, mashtaka manne ya utakatishaji fedha, manne ya kughushi, manne ya kutoa nyaraka za uongo, mawili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la kuisababishia mamlaka hasara.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 kwa mamlaka waliyokuwa nayo waliusababishia mradi wa UDART hasara ya Sh.bilioni 2.41.

Katika shtaka lingine, ilidaiwa kuwa mshtakiwa wa kwanza na wanne, Robert na Shi, wanadaiwa kati ya Mei 26, 2016, wakiwa benki ya NMB tawi la Ilala, wakiwa wakurugenzi wa Kampuni Longway Engineering huku Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART walifanya muamala wa Sh. milioni 603 kupitia akaunti ya benki ya UDART kisha kuzihamishia fedha hizo katika akaunti ya Longway na baada ya siku mbili wakijua fedha ni za kughushi.

Katika shtaka lingine, ilidaiwa kuwa Mei 30, 2016, Robert na Shi katika benki ya NMB tawi la Ilala, walijipatia nyaraka kwa njia ya udanganyifu kutoka katika benki hiyo ikiwa na jina la Fund Transfer Request Form ikiwa na tarehe ya Aprili 6, 2016, kwa lengo la kuonyesha Sh. milioni 750 zimelipwa na Kampuni ya Longway kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kituo cha UDART Kimara, Kivukoni, Ubungo na Morocco, huku wakijua ni uongo.

Martin alidai shtaka la Robert na Shi, Juni 8, 2016, katika benki ya NMB tawi la Ilala walijipatia kwa njia ya udanganyifu Sh. milioni 595.92 kutoka UDART kwa kuonyesha zimelipwa na kampuni ya Longway ambayo imehusika katika kutengeneza vitu mbalimbali vya mradi huo, huku wakijua ni uongo.

Ilidaiwa kuwa Aprili 6, 2016 katika benki ya NMB tawi ya Ilala, Robert, alighushi nyaraka hiyo kwa lengo la kuonyesha Sh. milioni 594 zimelipwa kwa kampuni ya Longway ambayo imejihusisha na uandaaji, utengenezaji wa vitu mbalimbali wakati ni uongo.

Katika shtaka la kutakatishaji fedha linalowakibili washtakiwa wote wanne, wanadaiwa kuwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 wakiwa jijini Dar es Salaam kwa nia ovu walibadilisha thamani ya mafuta ya zaidi ya Sh. bilioni 1.21 kuwa fedha ya thamani hiyo baada ya kuyauza mafuta hayo, huku wakijua mafuta hayo ni zao la kosa la wizi.

Kosa lingine ni la kujenga kituo cha mafuta bila kuwa na vibali vya EWURA ambalo linamkabili Robert na Kulwa ambao wanadaiwa walilitenda Januari 1, 2015 na Desemba 31, 2017 maeneo ya Jangwani Ilala.

Inadaiwa kuwa washtakiwa Robert na Kulwa wakiwa wakurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil na Gas Ltd kwa pamoja walijenga kituo hicho cha mafuta bila kuwa na kibali cha EWURA.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na kibali cha kusikiliza kesi hiyo.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na uliomba tarehe ya kutajwa.

Hakimu Simba alisema kesi hiyo itatajwa Februari 23, mwaka huu na washtakiwa walipelekwa rumande kwa sababu mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.
Share:

WASANII WATAJWA KUWA WAATHIRIKA NAMBA MOJA WA MADAWA YA KULEVYA

Mamlaka ya Kupambana na kuzuia Dawa za Kulevya nchini imepanga kukutana na wasanii mbalimbali ili kuwapa elimu ya madhara ya dawa za kulevya ikiwa wao ni miongoni mwa wa waathirika wa dawa hizo kwa kutumia au kutumiwa kama wabebaji.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya utafiti uliofanywa na mamlaka hiyo kugundua kuwa wasanii ni waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya hivyo wamepanga kutoa vipeperushi vya kila aina ya dawa za kulevya vinavyoeleezea athari zake lengo ikiwa ni kufikisha taarifa kwa watu wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Rodgers Sianga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Jumatatu Februari 11, ambapo amesema wamepanga kukutana na wasanii hao Jumatano Februari 13 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Uingizwaji wa dawa nchini umepungua, tulipodhibiti nchi kavu walihamia katika njia za bahari ambapo kwa mwaka jana pekee tulikamata tani 9, 000 za dawa za kulevya zilizotaka kuingizwa nchini kwa njia ya majini na kwa nchi kavu tulikamata kilo 1, 000 za dawa kwa kushirikiana na majeshi ya majini bila hivyo hali yetu ingekuwa mbaya sana.

“ Kuhusu matumizi hatujajua yamepungua kiasi gani hivyo tunapanga mwishoni mwa mwaka huu kufanya tafiti ili tujue yamepungua kwa kiasi gani upatikanaji wake na matumzi yake kwa waathirika wa dawa ya kulevya na ndiyo sababu ya kuwaita wasanii ili watusaidie kufiklisha elimu kwa watu wengi” amesema.

Aidha Kamishna Sianga amesema wamejipanga kuhamishia nguvu katika mipaka ya Kusini ili kudhibiti uingizwaji wa dawa kutokea nchini Msumbiji kupitika katika ya mikoa ya kusini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger