Monday, 11 February 2019

KAZI YA SARRI MATATANI DARAJANI

Maurizio Sarri alikuwa katika filamu ambayo watazamaji wa Chelsea hawajaiona , na kitendo cha mwisho hakikuisha vizuri kwa mkufunzi huyo wa Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge.

Sarri alikuwa kama mtu aliyekuwa anawindwa sawa na watangulizi wake kama vile Felipe Scholari na Adre Villas Boas alipokabiliwa na kichapo cha sita bila mbele ya mikono ya Manchester City - ikiwa ni kipigo kikali tangu Chelsea iliposhindwa 7 mtungi na klabu ya Nottingham Forest mnamo mwezi Aprili 1991.

Alikiri kuwa kazi yake huwa hatarini kila mara huku akisisitiza kuwa hajui iwapo yuko hatarini kwa sasa.

Klabu hiyo ya Sarri imefungwa magoli 10 bila jibu katika kipindi cha mechi mbili za ugenini, baada ya kupoteza 4-0 dhidi ya Bournemouth mnamo tarehe 30.

Chelsea iliojulikana kuwa na safu kali ya ulinzi ilifungwa magoli 4 katika kipindi cha pili dhidi ya kikosi cha Eddie Howe katika kipindi cha dakika 25 za kwanza.

Kufikia sasa wameshuka hadi nafasi ya sita katka ligi ya Uingereza wakiwa nyuma ya Manchester United kwa pointi moja ambayo iko katika nafasi ya nne baada ya kuwa mbele ya mabingwa hao wa zamani kwa pointi 11 wakati Mourinho alipoondoka mwezi Disemba.

Chanzo:Bbc
Share:

MTOTO ALIYEKATWA KOROMEO NJOMBE AFARIKI

Mtoto aliyejulikana kwa jina la Meshack Myonga mwenye umri wa miaka 4 mkazi wa Mji Mwema mkoani Njombe ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa koromeo amefariki dunia mwishoni mwa juma hili akiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya alipolazwa lwa ajili ya matibabu.

Mtoto huyo ambaye aliokotwa barabarani jirani na pori akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa koromeo Desemba 23, 2019 majira ya saa 4 asubuhi mtaa wa Mji Mwema.

Akizungumza kwenye mazishi ya mtoto huyo jana katika kijiji cha Ngalanga Mjini Njombe, mjomba wa marehemu Gisbeth Mlelwa, amesema mtoto huyo alizidiwa kwa majeraha makali tangu alipovamiwa na watu wasiojulikana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo, Alanus Mwalongo ameonesha kusikitishwa na tukio la kifo cha mtoto huyo na kueleza kuwa jambo hilo linapaswa kupingwa na kila mmoja.

Hivi karibuni, Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Liberatus Sabas, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renata Mzinga wameanzisha zoezi la kuwasaka wahalifu wa matukio ya mauaji ya watoto ambapo walikagua mapori ya Nundu na Tanwat mkoani Njombe.

Chanzo:Eatv
Share:

AMBER RUTTY AKANA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE


Serikali imekamilisha upelelezi wa kesi ya kufanya ngono kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary ‘Amber Ruth’ na mumewe Said Mtopali kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Leo tarehe 11 Februari Faraji Nguka, Wakili wa Serikali, ameeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Augustine Rwizile. Hata hivyo washtakiwa wamekana kufanya ngono kinyume na maumbile.

Wakili Nguka amedai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 7 Machi 2019.

Amber Ruth na mumewe walifikishwa mahakamani hapo tarehe 2 Novemba 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na wawili hao, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya ngono kinyume cha maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa ametenda kati ama baada ya tarehe 25 Oktoba 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya 25 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam alifanya ngono na Amber Ruth kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya 25 Oktoba 2018 alisambaza video za ngono kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo WhatSapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati 25 Oktoba 2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii (Whatsapp). Kosa ambalo wamesema si kweli.
Chanzo- Mwanahalisionline
Share:

KATIBU MKUU CCM AMUOMBA JPM ATIBU UGONJWA WA DEKO NA KIBURI UNAOMSUMBUA TUNDU LISSU

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), anaumwa ugonjwa wa deko huku akimuomba Rais Dk. John Magufuli aanze kutibu ugonjwa huo.

Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Kilosa mkoani Morogoro, katika ziara yake ya kazi ikiwa ni sehemu ya maadhimino ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM.

Dk. Bashiru alidai Lissu amekuwa akisema uongo katika nchi za Ulaya huku akiota siku moja atakuwa Rais wa Tanzania.

Wakati mtendaji huo wa juu wa CCM akiyasema hayo, Lissu amekuwa akiendelea na ziara yake katika nchi za Ulaya.

Kwa sasa yupo Marekani akieleza kile alichodai hali ya demokrasia nchini na kupigwa kwake risasi.

Dk. Bashiru alidai dalili za ugonjwa wa aina ya Tundu Lissu ni kusema uongo, dharau, deko, uonevu, kiburi, majivuno.

“Ila shukrani ya punda ni mateke. Namuomba Rais wetu (Dk. John Magufuli) aanze kutibu ugonjwa wa deko unasomesha watu wanazunguka kutukana nchi yao na Rais wao kisa ugonjwa wa deko.

“Yupo msomi mmoja anaitwa Tundu Lissu ameugua ugonjwa wa deko, anadeka hajui jembe kwa maisha yake, hajui mpunga unalimwaje wala samaki wanavuliwaje.

“Hajapanda bodaboda muda mrefu na watoto wake hawasomi shule hizi anazunguka dunia nzima kutuchafua.

“Tunao Tundu Lissu wengi Serikalini tumewaamini tumewapa dhamana ila ukiwatembelea ofisini wanadeka, mara nyingine hawapo, wanajipendelea wao,” alisema Dk. Bashiru na kuongeza:

“Ugonjwa huu unaambukizwa na tumeulea na wauguzi na madaktari wa ugonjwa huu ni Watanzania nyie wenyewe. Huu ugonjwa hatari, unaambukizwa ni hatari kuliko Ukimwi. 

Anasema tumeweka Kifungu kwenye Katiba ya CCM cha kuzuia watu kugombea urais siyo kweli ni uongo”.

Dk. Bashiru alisema dalili za ugonjwa huo wa deko ni ubinafsi, kuota urais wa Tanzania kuwa na kiburi na kwenda Ulaya kuzungumza lugha za wakoloni lakini sasa anayemwita dikteta amefuta mashamba kwa ajili ya wanyonge.

“Nilipomskiliza nikasema ni muongo na kwa sababu anaumwa ugonjwa unaitwa Tundu Lissu, basi yupo kwenye hali mbaya.

“Ugonjwa wa Tundu Lissu ni hatari ila unaponyeka, amuache Rais (Dk. John Magufuli) atumikie wanyonge.

“Watendaji wote wa serikali ambao hawataki kupona ugonjwa huu watafute serikali nyingine, ajira ni hiyari waandike barua waseme chama hiki hakipendi dhurlma, mimi nadhulumu, hakipendi uongo mimi muongo, uachie madaraka,” alisema.
Share:

ZANTEL YAANZISHA MPANGO WA WAFANYAKAZI WAKE KUSHIRIKI KUFANYA MAZOEZI YA KUJENGA AFYA ZAO

Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakishiriki kufanya mazoezi ya viungo chini ya mpango ulioanzishwa na kampuni ili kuimarisha afya za wafanyakazi na kuongeza ufanisi kazini yaliyonduliwa katika ofisi za makao makuu ya kampuni jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya mawasiliano ya Zantel imeanzisha mpango, unaowawezesha wafanyakazi wake wote kushiriki kufanya mazoezi ya mwili baada ya saa za kazi kwa ajili ya kujenga afya zao.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu kutoka Zantel Joan Makwaia Kazimoto amesema mazoezi hayo yanafanyika mara tatu kwa wiki baada ya saa za kazi, na wanafanya mazoezi ya viungo ya kucheza (Zumba), kutembea na aerobics.

“Zantel siku zote inawajali wafanyakazi wetu kama ambavyo inavyowajali wateja wake, ndio maana tumeanzisha mpango kama huu wa mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya za wafanyakazi wetu wote sambamba na kuleta tija na ufanisi, tunaamini wafanyakazi wenye afya bora wanatekeleza majukumu yao ya kazi ya kila siku vizuri”,alisema Joan.

Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel walipohojiwa waliuelezea mpango huo kuwa ni mzuri kwa afya zao pia unadhihirisha jinsi kampuni inavyowajali wafanyakazi wake kama ambayo imekuwa ikiwajali wateja wake.

Akiongea wakati wa mazoezi hayo, mmoja wa wafanyakazi wa Zantel, Gamdad Murad aliushukuru uongozi wa Zantel kwa kujali afya zao kwani ni muhimu zaidi hasa kazini na katika familia zao pia.

“Mazoezi haya yanatuhamasisha kubadilisha mfumo wetu wa maisha na pia kuanza kuwazoesha watoto wetu kufanya mazoezi katika umri mdogo ili kuepukana na magonjwa yanayoletwa na uzito kupita kiasi,” alisema Murad.
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakishiriki kufanya mazoezi ya viungo chini ya mpango ulioanzishwa na kampuni ili kuimarisha afya za wafanyakazi na kuongeza ufanisi kazini yaliyonduliwa katika ofisi za makao makuu ya kampuni jijini Dar es Salaam.
Share:

SHEIKH PONDA ALAANI KITENDO CHA KUSITISHA UJENZI WA MSIKITI UDOM

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeeleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuamua kusitisha ujenzi wa msikiti uliokuwa ukijengwa katika chuo hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Jumuiya hiyo Sheikh Issa Ponda alisema, mwaka 2016 uongozi wa chuo hicho uliwapatia ekari 10 baada ya kukubali ombi la jumuiya hiyo la kutaka kujenga msikiti huo. Ponda alisema, walianza kushughulikia vibali vya ujenzi katika mamlaka za chuo hicho na nje na walifanikiwa kuvipata vyote na mwaka jana waliwasilisha…

Source

Share:

RAIS MUSEVENI APIGA MARUFUKU KUWATUMIA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA KUVUTIA WATALII

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hataruhusu mwanamke hata mmoja kutoka nchini humo kuonyesha mwili wake kwa umma kama njia moja ya kuwavutia watalii.

 Akiwa kwenye mkutano na wawekezaji katika Ikulu Alhamisi Februari 7,2019 Museveni alilaani pendekezo hilo la kutaka kuwatumia wanawake wenye makalio makubwa kama kivutio cha utalii. 

Museveni alidai kuwa pendekezo hilo lililotolewa na waziri wa Utalii Godfrey Kiwanda halikuwa limejadiliwa na baraza la mawaziri  huku akitaka wanawake waheshimiwe.


Aidha, Rais Museveni pia alisema hakuna uhakika kwamba wanawake kuonyesha makalio yao itavutia watalii Uganda.

 "Huu haukuwa uamuzi wa baraza la mawaziri, watu hawapaswi kuja hapa kuona wanawake, sijafurahishwa na pendekezo hilo hata kidogo. Hiyo ni kama kuwauza wanawake wetu kwa watalii," Museveni alisema.

 Museveni pia alisema wanawake wanapaswa kuheshimiwa na kushughulikiwa ipasavyo ila sio kuwaanika mitandaoni kama njia moja ya kuwauza.

 "Lazima tujipe muda wa kujadili suala hili, niko na maoni yangu binafsi na tayari nishayazungumzia, siwezi wakubali wajukuu wangu kuonyesha miili yao kwa umma eti kwa ajili ya kukuza utalii, ningependa tumtumie Abenakyo, Miss World Africa kuuza Uganda kwa mataifa mengine," Museveni aliongezea.

Mapema mwezi huu, Wizara ya Utalii nchini Uganda ilikuwa imetangaza kuwa itawatumia wanawake wenye makalio makubwa kama kivutio cha utalii. 

Share:

Wimbo mpya : PETER MSECHU - UMEJUA KUNIFURAHISHA

Share:

Video Mpya : RAMSO STAR Ft INSPECTOR HAROUN - POKEA

Ramso Star Ft Inspector Haroun - Pokea
Advertisement
Share:

RONALDO JUVENTUS KUMENOGA

Na Shabani Rapwi. Mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo amezidi kuwa tishia ndani ya Juventus baada ya usiku wa jana kutupia goli moja katika ushindi wa 3-0 iliyopata timu yake ya Juventus dhidi ya Sassuola, Sami Khedira ndiyo alikuwa wa kwanza kufunga goli dakika ya 23′, huku dakika ya 70′ Ronaldo akapachika goli la pili na Emre Can dakika ya 86′ akapachika goli la tatu. Ronaldo anakuwa kinara wa ufungaji wa magoli katika Ligi Kuu ya Italia akiwa na magoli 18 akifuatiwa na Fabio Quagliarella katika nafasi ya pili…

Source

Share:

AZAM FC KUIVAA LIPULI HII LEO, SAMORA

Na Shabani Rapwi. Klabu ya Azam FC leo Jumatatu, Februari 11, 2019 itakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaofanyika Saa 10: 00 Jioni Uwanja wa Samora, Iringa. Azam FC leo itakosa huduma ya mlinda mlango wake namba moja Razak Abalora ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Alliance. Timu hizo (Azam na Lipuli) zilikutana mara nne kwenye mechi za Ligi, katika mechi tatu zilizopita Azam FC ilishinda mara moja huku mechi mbili wakienda sare, mara ya mwisho kukutana kwenye uwanja…

Source

Share:

Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme 2019 for Refugees and Displaced Persons in Africa (Fully Funded) (Deadline: 30 April 2019)

Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme 2019 for Refugees and Displaced Persons in Africa (Fully Funded) (Deadline: 30 April 2019)

The Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme was launched in 2007 with the aim to contribute in the production and retention of high level African human resources for sustainable development of the continent incritical development areas, while promoting regional integration through intra-Africa mobility of students.

The Scholarship Scheme is intended to enable young Africans to study in reputable African Universities with a binding agreement that beneficiaries will work in any African country for at least the same duration of scholarship period after graduation.The African continent hosts one of the largest number of displaced persons in the world. Over a third of the world’s forcibly displaced persons are found in Africa, including 6.3 million refugees and 14.5 million internally displaced persons.

Access to higher education for many refugees has remained a challenge due to a number of reasons including the high cost of higher education and lack of appropriate documentation to facilitate enrollment of refugees into various institutions of higher learning.Only 1% of refugees and displaced people get access to higher education.

Promoting access to higher education is essential to enable refugees and forcibly displaced persons build their capacity to lead a normal life and contribute to regional integration and sustainable development in Africa. It is therefore necessary to enhance opportunities to effectively educate and integrate refugees and displaced persons.

To encourage the participation of young African Refugees and Internally Displaced Persons at Masters programmes in the fields of Natural Sciences, Agriculture, Health, Education, Engineering,and Social Sciences;the African Union Commission is offering a Call for Scholarship Applications.

The 2019 Scholarship offer is aimed to provide an important opportunity for enhancing the knowledge, professional skills and capacity of refugees and displaced persons;and there by streamline their integration to contribute for sustainable development in Africa.

Eligibility Requirements:

To be eligible for the Scholarship, a candidate must:

i.Be a Citizen of an African Union Member State.

ii.Be a formally registered refugee/displaced person with a UNHCR registration number or be able to demonstrate confirmed refugee status in an African Union Member State.

iii.Be under the age of thirty five (35) years.

iv.Be a holder of a Bachelor’s Degree in the relevant field, at least at the level of Upper Second Class Honours. The degree must be from a recognised University.

v.Have demonstrated outstanding academic achievement as evidenced by academic transcripts, and academic awards if any.

vi.Have proof of admission to undertake a full time Masters programme in a recognised university in an African Union Member State.

vii.Be willing to commit to work in an African Union Member State on completion of studies for at least three (3) years. No application will be considered without an admission letter from a university, and an official registration as a refugee or displaced person.

ELIGIBLE FIELDS OF STUDY

The following fields of study are eligible:Natural Sciences, Agriculture, Health, Education, Engineering,and Social Sciences

Scholarship Worth:

The scholarship award covers the following:

Tuition Fees:

According to an official invoice from the Host University.

Stipend:

500 US$monthly,to support living expenses such as housing, food, utilities, local transportation and medication.

Book Allowance:

An allowance of 500US$per year for the purchase of books.Air ticket: A round-trip economy fare (as applicable).

Travel Allowance:

One-off payment of 250 US$ to contribute towards ground transportation and settling-in costs

One-off payment of 350US$ to assist with shipping and other terminal expenses; upon departure from the host Institution after successful completion of the study.

Computer Allowance:

One-off payment of1,000 US$ for the purchase of laptop computer and accessories.Note:Candidates must complete their study within the specified period of the programme as the scholarship cannot be extended.

Application Procedure:

Applicants can submit their applications by post after completing the Scholarship Application Form, which is available on the Africa Union website:http://bit.ly/2DZJzz6

The application documents should include the following:

i.Completed application form

ii.A proof of refugee/displaced person status,indicating citizenship

iii.Recent passport-size photograph

iv.CV indicating applicant’s academic background and work experience

v.Certified copies of academic certificates and transcripts

vi.Copy of admission letter from a recognised African University

vii.Two (2) Reference Letters with contact addresses and telephone numbers.

viii.A Letter of Motivation of not more than 500words (maximum 2 pages) that explains why the candidate has chosen the particular field of study and its importance to Africa’s development

Applicants applying on-line should produce electronic copies of the above documents and submit as attachments.Applicants who submit their applications by post should make two (2) sets of hard copies of all the above documents.

The Application must be sent to the address below:

Department of Human Resources, Science and Technology
African Union Commission
P.O. Box 3243
Addis Ababa, Ethiopia

For More Information:

Visit the Official Webpage of the Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme 2019

The post Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme 2019 for Refugees and Displaced Persons in Africa (Fully Funded) (Deadline: 30 April 2019) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Sunday, 10 February 2019

DC MSAFIRI ASHIRIKI IBADA YA MFUNGO KUOMBEA MKOA WA NJOMBE

Na.Amiri kilagalila Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameshiriki katika ibada ya kuhitimisha mfungo na Maombi yakuombea mkoa wa Njombe yaliyofanyika kwa wiki moja katika kanisa la Tanzania Assemblies of God T.A.G lililopo mtaa wa Melinze halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo. Akiwa katika ibada hiyo Msafiri amewataka wakristo mkoani Njombe kuendelea kuombea mkoa wa Njombe kutokana na matatizo ya mauaji ya watoto yaliyojitokeza hivi karibuni huku akiwataka kuto kusahau kuombea maswala ya uchumi na familia kwa ujumla. “Naendelea kuwategemea sana watu wa Mungu hatutafika bila kuinua uchumi…

Source

Share:

MAN CITY WAIPA KIPIGO CHA MBWA KOKO CHELSEA.... NI 6-0 AGUERO AKIVUNJA REKODI YA SHEARER

Mshambuliaji Sergio Aguero amefikia rekodi Allan Shearer ya kupiga hat trick 11, akiiongoza Manchester City kuichakaza Chelsea kwa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Etihad.

Mshambuliaji Aguero ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya pili katika mechi tatu alizocheza na kuiongoza Manchester City kurudi kileleni kwa Ligi Kuu.

City ilikuwa mbele kwa mabao 4-0 katika dakika 25 za kwanza, Raheem Sterling alifunga bao la kwanza kabla ya Aguero kufunga bao la pili kwa shuti la umbali wa mita 30.

Aguero alifunga bao tatu akimalizia mpira uliorudishwa nyuma na beki wa Chelsea, Ross Barkley naye Ilkay Gundogan alifunga bao tatu kwa shuti la umbali wa mita 18 kabla ya mapumziko.

Aguero alifikia rekodi ya Alan Shearer ya kufunga hat-tricks 11 katika Ligi Kuu England akifunga penalti kabla ya Sterling' kuhitimisha kwa kufunga bao la sita.

Wakati Aguero anakwenda kuchukua mpira mwamuzi Mike Dean aliuficha mpira huo nyuma hadi alipomkaribia ndipo aliutoa mgongoni na kumpa.

Mshambuliaji huyo wa Argentina alikosa bao akiwa yeye na goli kabla ya kuweka rekodi yake ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Manchester City akiwa amefunga mabao 160 na kuivunja rekodi ya Eric Brook aliyekuwa amefunga mabao 158.

City sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya mabao tisa kwa Liverpool, wenye mchezo moja mkono.
Via Mwanaspoti
Share:

TUME YAENDESHA WARSHA VYUO VYA ARDHI KUHUSU DHANA YA USHIRIKISHWAJI KATIKA UPANGAJI WA MATUMIZI YA ARDHI


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi akitoa mada wakati wawarsha ya ushirikishwaji wa wananchi katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.
Bwana Kent Nillson kutoka Taasisi ya Lantmateriet nchini Sweeden akitoa mada juu ya uzoefu wa nchini kwao kuhusu upangaji wa matumizi ya ardhi.
Mwanafunzi wa mwaka wa pili Ngeze Valentina wa kozi ya RDP akichangia mada wakati wa majadiliano juu ya
ushirikishwaji wa wananchi katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.
Mshiriki wa warsha Kiteri Sophia kutoka
Chuo Kikuu cha Ardhi akitoa maoni yake juu ya ushiriki wa wanawake katika hatua za upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.
Baadhi ya washiriki wa warsha wakifuatilia
kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa warsha ya upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Lantmateriet ya nchini Sweden kupitia ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweeden(SIDA) imeendesha warsha katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam na Chuo cha Ardhi mjiji Morogoro iliyohusu ushirikishwaji wa wananchi hasa makundi maalum katika upangaji, usimamizi na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi nchini.

Katika warsha iliyofanyika Chuo Kikuu Ardhi na kuhudhuriwa na Wakufunzi pamoja na Wanafunzi
wa chuo hicho, wawezeshaji walikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume Dkt. Stephen Nindi; Bw. Kent Nillson kutoka Taasisi ya Lantmateriet na Bi. Lilian Looloitai kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la CORDS ambalo hufanya kazi zake katika
Wilaya za Monduli na Longido Mkoani Arusha.

Akitoa mada katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume alielezea namna gani Sheria, na miongozo mbalimbali inayohusu upangaji wa matumzi ya ardhi inavyotambua na kuhimiza ushirikishwaji wa wananchi na kutaja makandi maalum kama vile wanawake kupewa kipaumbele katika hatua zote za upangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi. 

Pia, Dkt. Nindi alitolea mfano wa Mwongozo Shirikishi wa Upangaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji (Participatory Land Use Management Guidelines) ambao umetamka bayana juu ya uundwaji wa kamati za upangaji na
usimamizi wa mipango ya matumizi ya ardhi za vijiji kuwa lazima ziwe na wajumbe wanawake wasiopungua watatu.

Wakielezea uzoefu wao juu ya ushirikishwaji katika upangaji wa matumizi ya ardhi, Bw. Kent Nillson kutoka Taasisi ya Lantmateriet amesema kuwa Sweden ilianza kupangwa toka mwaka 1692 ambapo hadi hivi sasa ushiriki wa wananchi katika shughuli za upangaji na umiliki wa ardhi umeimarika kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wa mwezeshaji kutoka Asasi ya Kiraia ya CORDS, Bi. Lilian Looloitai amesema kuwa, kwa muda
mrefu sasa CORDS wamejikita katika uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika Wilaya ya Monduli ambapo ushiriki wa wanawake katika zoezi hilo unaonyesha kufanikiwa. Bi. Lilian amesema kuwa kwa sasa kumekuwepo na ongezeko la idadi ya wanawake wanaoshiriki na kutoa maoni katika mikutano ya kijiji pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Warsha kama hii pia imefanyika Chuo cha Ardhi mjini Morogoro ambapo imekuwa chachu ya majadiliano
juu ya upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa njia ya ushirikishwaji pamoja na kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya kusimamia sekta ya ardhi kwa kuzingatia
masilahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Share:

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA MISA TAKATIFU YA DOMINIKA YA 5 YA MWAKA C KANISA LA MTAKATIFU PETRO DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki na waumini wengine katika Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Mwaka C katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa amani na masista na waumini wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Mwaka C katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Mkate wa Sakramenti Takatifu toka kwa Paroko wa Parokia ya Oysterbay Padri Dkt. Alister Makubi wakati wa Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Mwaka C katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Paroko wa Parokia ya Oysterbay Padri Dkt. Alister Makubi baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya 5 ya Mwaka C katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam leo February 10, 2019. Katikati ni mmoja wa viongozi wa kanisa hilo Dkt. Adelhelm James Meru . PICHA NA IKULU
Share:

COCA- COLA YAZINDUA KAMPENI YA KUTUNZA FUKWE NA MAZINGIRA 'MCHANGA PEKEE'


Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios (kulia) amesema kuwa kampeni ya hiyo ni ya pekee na tayari kampuni ya Coca-Cola Kwanza imefikia makubaliano na serikali (upande wa halmashauri) kwa kufanya usafi wa fukwe ya Coco (coco beach) kama eneo la kuanzia huku lengo ni kufikia fukwe zote zilizopo nchini Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Daniel Chongolo akiipongeza kampuni ya Coca Cola Kwanza kwa kampeni yao ya 'Mchanga Pekee'. Pia ameipongeza kampuni ya EcoAct Tanzania kwa ubunifu wa kutengeneza vibao vya alama za barabarani kutumia Plastic tofauti na chuma ambazo watu huzing'oa na kwenda kuuza vyuma chakavu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania Leodegar Tenga, akitoa pongezi kwa Coca Cola Tanzania kuweza kuanzisha kampeni ya 'Mchanga Pekee' yenye lengo la kuelimisha, kufundisha na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ya jamii zetu ikiwa imejikita katika ukusanyaji wa plastiki na usafishaji wa fukwe zetu.
Msanii na Balozi wa Coca Cola Kwanza Mrisho Mpoto (Mjomba) akitoa burudani na ujumbe kwa jamii iliyojitokeza katika zoezi la usafi.

Christian Mwijage Managing Director EcoAct Tanzania akielezea jinsi wanavyotumia Chupa za Plastic kutengenezea bidhaa mbalimbali, ikiwemo vibao vya tahadhari vya barabarani.
Mrisho Mpoto (kushoto) Basil Gadcious, Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola Tanzania (Kati) na Tania Hamilton (Kulia) wakijadilia jambo.
Tania Hamilton, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio akishiriki kusafisha fukwe ya Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu waliofika wakiendelea na usafi pembezoni mwa fukwe ya Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Kampuni ya Coca-Cola kwanza na Kampuni Tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa wameanzisha kampeni ya Mchanga Pekee yenye malengo na madhumuni ya kuelimisha, kufundisha na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ya jamii zetu ikiwa imejikita katika ukusanyaji wa plastiki na usafishaji wa fukwe zetu.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Mchanga Pekee, Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios amesema kuwa kampeni ya hiyo ni ya pekee na tayari kampuni ya Coca-ColaKwanza imefikia makubaliano na serikali (upande wa halmashauri) kwa kufanya usafi wa fukwe ya Coco (coco beach) kama eneo la kuanzia huku lengo ni kufikia fukwe zote zilizopo nchini Tanzania.

"Coca Cola Kwanza itaajiri na kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwapa vitendea kazi na posho ya kufanya usafishaji wa fukwe kwa kipindi chote kwa mwaka mzima kwa awamu ya kwanza ya mradi ambapo watakuwa na jukumu la msingi la kuhakikisha fukwe inakuwa katika hali ya usafi muda wote na kuhamasishautalii wa fukwe kwa kuwezesha wale wanao tembelea fukwe kufurahia mandhari ya fukwe hizo katika mazingira yalio safi na salama," amesema.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amesema wilaya ya Kinondoni imekuja na mpango maalum wa kuimarisha mazingira ya Bahari, tunazo na imetenga Bilioni 28 kwa ajili ya miradi miwili ya kuimarisha mazingira; zikiwemo fukwe za Osterbay zinazojumuisha eneo hili la Coco pamoja na kuimarisha mazingira ya soko la Tandale," Amesema.

Mbali na fedha hizo za miradi miwili, Serikali mwaka jana ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ukarabati wa soko la Magomeni, Jijini Dar Es Salaam zoezi ambalo linaendeleo mpaka sasa, aidha Chongolo alitoa wito kwa jamii kuhusu kuendeleza na kuzitunza fukwe za bahari ili kutengeneza mazingira mazuri ya wananchi kupumzika pia kubarizi.

Kampeni ya Mchanga Pekee ina lengo la kutunza usafishaji wa fukwe na kuziweka katika mandhari salama,endelevu na zenya kuvutia yaani kuubakiza mchanga peke yake kwenye fukwe kwa kuondoa vitu visivyostahili kuwepo (uchafu-plastiki) na pia kampeni itajikita katika ukusanyaji wa chupa za plastiki katika mazingira yetu kuwezesha mazingira kuwa salama na yenye kuweza kuhifadhi ekolojia ya mazingira iliopo.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger