Na Allawi kaboyo-Kibondo. Wadau wa elimu mkoani Kigoma wameombwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu ili kuleta uwiano sawa wa ufaulu na wavulana ili kusaidia kukomesha vitendo vya watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni na kuwapelekea kukatisha masomo yao. Wito huo umetolewa na afisa elimu wa mkoa huo mwl.Juma Kaponda alipokuwa anazungumza na walimu wa kata ya kibondo mjini katika hafla fupi ya kujipongeza kwa matokeo mazuri ya darasa la nne, darasa la saba na kidato cha pili pamoja na kidato cha nne…
Friday, 8 February 2019
SAKATA LA RAIS WA TFF KUMDHALILISHA TUNDU LISSU LATUA FIFA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania kimeandika barua kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino likimshtaki Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kutoa kauli za kibaguzi na unyanyasaji.Katika barua hiyo ya kurasa mbili, iliyosainiwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumain Makene imeonyesha masikitiko yake kwa kitendo cha Karia kutumia mchezo wa soka kuonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya Tundu Lissu ambaye Septemba 7, 2017 alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 jijini Dodoma.
"Tunaandika barua hii kuelezea masikitiko yetu na kupinga kauli iliyotolewa na Rais wa TFF, Wallace Karia ambayo inaunga mkono uvunjaji wa haki za binadamu, uhuru wa kuzungumza na kuchochea ubaguzi wa kisiasa jambo ambalo ni kinyume na miiko ya mchezo wa mpira wa miguu unaosimamiwa na Fifa," imeeleza sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo ambayo pia imeelekezwa kwa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) na Karia mwenyewe, imeambatanishwa pia na ushahidi wa kipande cha video kinachomuonyesha Rais huyo wa TFF akitoa kauli hiyo.
February 2 2019 shirikisho la soka Tanzania TFF lilifanya mkutano mkuu wa mwaka shirikisho hilo jijini Arusha na kujadili mambo mbalimbali, moja kati ya vitu vilivyoibuka katika mkutano mkuu ni kauli ya Rais wa shirikisho hilo Wallace Karia alipotaja jina la Tundu Lissu akimtolewa mfano Michael Wambura.
Michael Wambura alikuwa Makamu wa Rais wa TFF kabla ya kufungiwa maisha kujihusisha na soka, hivyo Wambura kwa sasa ni kama ana mpinga Karia kiasi cha Wallace Karia kumfananisha Wambura na Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu.
Karia alinukuliwa akisema kauli inayoeleza kuwa atawashughulikia wakina Tundu Lissu wa soka akimlenga Wambura, kitu ambacho hakijawafurahisha CHADEMA na sasa wameamua kuandika barua kuipeleka shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA kumshitaki Wallace Karia.
MAMA MPENDA 'LIMBWATA' APEWA TALAKA AKISAKA DAWA KWA SANGOMA MUME AMTII ZAIDI

Mwanamke mmoja mwenyeji wa Kagumo, Kirinyaga nchini Kenya amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutemwa na mumewe kutokana mume huyo kubaini kuwa mkewe alikuwa akitafuta nguvu za giza kwa mganga wa jadi akitaka kudumisha mapenzi kati yao ili mumewe aweze kumpenda na kumtii zaidi.
Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, mwanamke huyo aliamua kutafuta msaada wa mganga ili mapenzi yanoge na hata kupewa pesa nyingi na mumewe
Inadaiwa kuwa licha ya kumlipa mganga huyo na kumtembelea mara kadhaa, lengo la mwanamke huyo halikufanikiwa.
Siku ya kioja, mganga huyo ambaye alikuwa mnywaji wa pombe alikutana na mume wa mwanamke huyo kwenye baa, baada ya kubugia pombe na kulewa, alianza kumrushia mume huyo cheche za matusi huku akieleza kuhusu jinsi mkewe amekuwa akitafuta dawa za mapenzi 'Limbwata' kwake.
"Hata mkeo ni mteja wangu shupavu, hunitembelea kila mara kutafuta hirizi ya kunogesha mahaba kati yenu,’’ alisema.
Jamaa huyo alikasirika mno lakini akapata njia ya kujizuia. ''Wajua kuwa ndoa zina changamoto kadhaa na wanawake hawakosi vituko,’’ alimjibu mganga huyo.
Jamaa alipofika nyumbani alimfokea mkewe. "Kila ulichofanya gizani imebainika. Wewe na mganga mna uhusiano gani,’’ aliuliza kwa hasira.
Mwanamke huyo naye alimruka na kudai kuwa hamtoshelezi kimapenzi. ''Mume asiyemtosheleza mkewe unatarajia apelekwe wapi?,’’ alisema kwa dharau.
"Mganga huyo anayekutosheleza nenda kwake moja kwa moja,’’ Jamaa huyo" alisema huku akimfurusha mkewe.
Licha mwanamke huyo kumwomba msamaha, aligoma kumsamehe.
JAMAA AMUUA MCHEPUKO WA MKEWE BAADA YA KUWANASA WAKIFANYA MAPENZI KITANDANI KWAKE

Jamaa mmoja mwenyeji wa eneo la Bandari, Kisumu nchini Kenya anasakwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma ya kumuua mchepuko wa mkewe baada ya kuwanasa 'live' wakihondomola tendo la ndoa 'wakifanya mapenzi' kwenye kitanda chake.
Majirani wameeleza kuwa jamaa huyo ambaye ni Mwendesha boda boda alirudi nyumbani kutoka kwa mkewe mwingine usiku wa manane Februari 7,2019 na baada ya kuingia ndani alishangaa kuona simu asiyoijua pamoja na nguo zikiwa kwenye kiti.
Alichukua mwendesha bodaboda huyo baada ya kuona vitu hivyo aliingia moja kwa moja hadi chumba cha kulalia ili kushuhudia ni nini kilichokuwa kikiendelea.
Alikasirika baada ya kumuona jamaa huyo/mgoni akimmchovya mkewe kitandani akachukua kisu na kumdunga mara kadhaa na kumuua papo hapo.
"Alinaswa akiwa uchi, nguo zilikuwa kwenye kiti na simu yake ilikuwa mezani. Mumewe aliingia chumbani na kumpata mume huyo amemlalia mkewe. Mlango haukuwa umefungwa,’’ jirani moja alisimulia.
Hata hivyo, mkewe huyo aliweza kuponyoka akiwa uchi na kujinusuru ili kuepusha balaa zaidi kutokana na fumanizi hilo.
Inadaiwa kuwa muuaji huyo alichukua nafasi na kusafisha kisu chake kwa kutumia chupi ya jamaa huyo pole pole kabla ya kutoroka.
Polisi walifika eneo hilo na kuchukua mwili wa marehemu huku msako ukianzishwa kumkamata mume huyo muuaji.
HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 8,2019.
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 8, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.
Thursday, 7 February 2019
SIMBA SC YAREJEA TATU BORA LIGI KUU KWA KISHINDO BAADA YA KUICHAPA MWADUI FC 3-0

Simba SC imerejea ndani ya tatu bora kwenye Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 usiku wa leo dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 36 sawa na Lipuli FC baada ya kucheza mechi 15, lakini inapanda nafasi ya tatu kwa wastani wake mzuri wa mabao kuliko timu ya Iringa ambayo pia imecheza mechi tisa zaidi.
Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 55 za mechi 22, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 48 za mechi 21.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Alfred Vitalis wa Kilimanjaro aliyesaidiwa na washika vibendera, John Kanyenye wa Mbeya na Leonard Mkumbo wa Manyara hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere alianza kuifungia Simba bao la kwanza dakika ya 21 kwa kichwa akimalizia krosi ya Mzambia, Clatous Chama aliyenzishiwa kona fupi na kiungo mwenzake, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
Kiungo Muzamil Yassin akaifungia Simba SC bao la pili dakika ya 25 kwa shuti kali baada ya pasi ya Nahodha John Raphael Bocco kufuatia krosi ya beki Zana Coulibally kutoka Burkina Faso.
Mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco akaifungia Simba SC bao la tatu dakika ya 29 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya Niyonzima.
Kipindi cha pili, Simba ilipata pigo baada ya kiungo wake Muzamil Yassin kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jonas Mkude.
Mechi iliyotangulia jioni ya leo, Coastal Union ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wageni wakitangulia kwa bao la William Patrick dakika ya 37 kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia kwa Raizin Hafidh dakika ya 65.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Zana Coulibally, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, Pascal Wawa, James Kotei, Muzamil Yassin/Jonas Mkude dk60, Haruna Niyonzima, John Bocco, Meddie Kagere/Adam Salamba dk78 na Clatous Chama/Emmanuel Okwi dk70.
Mwadui FC: Mussa Mbisa, Revocatus Richard, Emanuel Kichiba, Frank Magingi, Joram Mgeveke, Iddy Mobby, Wallace Kiango, Abdallah Seseme, Fabian Gwanse/Ibrahim Irakoze dk87, Ditram Nchimbi na Gerard Mdamu/Salimu Aiyee dk46.
Via>>Binzubeiry blog
PESA ZA MBUNGE ROSE TWEVE ZAGEUKA LULU KWA AKINA MAMA WA KATA YA NZIHI IRINGA
Baadhi ya wajumbe wa kikundi cha Rose Tweve kilichopo kata ya Nzihi mkoaniri Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kikao chao cha kikatiba
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameendelea kuitunisha mifuko ya wanawake wa UWT mkoa wa Iringa kwa kukuza mtaji walipewa awali na mbunge huyo.
Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa kikundi cha Rose Tweve, Aulelia Mbembe amesema mbunge wa viti maalum Rose Tweve aliwapa mtaji wa shilingi laki tano(500,000/=) kwa kuanzia lakini waliunda kikundi na kukiita Rose Tweve kwa lengo la kumuuezi mbunge huyo kwa mchango wake kwa wanawake wa UWT kata ya Nzihi mkoani Iringa.
“Mbunge alitupa mtaji lakini tulijiongeza kwa kukopeshana kwa riba ndogo ambayo tulijipangia sisi wenyewe kwa kukopeshana na kukutana kwa mwezi mara moja kwa ajili ya kununua hisa pamoja na kubadilisha mawazo kwa lengo la kukuza mitaji na kufanya maendeleo yetu binafsi” ,alisema Mbembe.
Mbembe alisema mtaji wa kikundi cha Rose Tweve kimefanikiwa kukuza mtaji kutoka shilingi laki tano 500,000/=) hadi kufikia kiasi cha shilingi milioni kumi laki moja na nusu (10,150,000/=) kwa kipindi cha miaka mitatu kutoka mwaka 2017 hadi hii leo hapo ndio utajua kuwa ukimwezesha mwanamke unakuwa umeikomboa jamii.
‘’Kama kikundi tunategemea kuja kuwa na miradi yetu mikubwa itakayokuwa inaingiza faida kwetu na taifa kwa ujumla kupitia kulipa kodi kwa miradi hiyo ,lakini tunategemea kutembelea na kusaidia vikundi vya watu maalumu kama vile walemavu ,yatima ,wazee wasiojiweza,na waathirika wa vvu,yote haya ni mchango na matunda ya Mbunge Rose Tweve ,kwa kweli shukrani nyingi zifike kwake ,na viongozi wengine wachukue mfano wa mbunge dada Rose Tweve kwa kusaidia jamii kama Rose Tweve alivyotusaidia sisi kikundi cha akiba cha wanawake(UWT) Rose Tweve Nzihi”, alisema Aulilelia Mbembe mwenyekiti wa kikundi hicho.
“Hebu angalia ndugu mwandishi wa habari jinsi gani wanawake wa UWT kata ya Nzihi tulivyoweza kutumia vizuri fursa tuliyoipata kutoka kwa mbunge Rose Tweve kwa kutusaidia kubadilisha maisha yetu kwa kuweza kujikimu kimaisha tofauti na ilivyokuwa hapo awali hivyo tunamshukuru sana mbunge Rose Tweve”, alisema Mbembe.
Mery Msigara ni moja wa wajumbe wa kikundi cha akiba cha Rose Tweve alisema kuwa alikuwa anashinda nyumbani kwa kumtegemea mume wake kwa kila kitu lakini baada ya kujiunga kwenye kikukidi cha Rose Tweve amekuwa mjasiriamali anayeweza kufanya biashara ndogondogo na kupata faida kila kukicha huku familia yake ikipata maendeleo ukilinganisha na awali,yote haya ni matunda ya mbunge Rose Tweve.
Wajumbe katika kikundi hicho wameonekana kuwa na malengo makubwa katika kufanikiwa huku wakisema kwa mwanga waliooneshwa na mbunge Rose Tweve wanaamini watafikia malengo yao ya mbali kimafanikio kupitia kikundi hicho cha akiba cha Rose Tweve .
Hadi sasa mbunge Rose Tweve amefakiwa kuvifikia na kuvitembea jumla ya vikundi 92 vya mkoani iringa na kuviwezesha kama ilivyo kwa hiki kikundi cha kata ya Nzihi.
Na Fredy Mgunda - Iringa
SIMBA YAANZA NA MWADAUI YAICHAPA 3-0
Na Shabani Rapwi. Klabu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) ulipigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ushindi huo unaifanya Simba SC kufikisha jumla ya alama 36 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na michezo 6 mkononi, ikizidiwa alama 19 na kinara wa Ligi Yanga SC aliyefikisha alama 55 katika michezo 22. Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Meddie Kagera dakika ya 21′, Mzamiru Yassin dakika ya 26′ na John…
WALIOBAINIKA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE KUANZA KUBURUZWA MAHAKAMANI
Na.Amiri kilagalila Serikali mkoani Njombe inategemea kuanza kuwaburuza mahakamani siku ya kesho wale wote waliouhusika na mauaji ya watoto wadogo mkoani Njombe kutokana na upelelezi kukamilika kwa baadhi ya kesi Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka aliyasema hayo hii leo mbele ya makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Tanzania bara Philip Mangula katika mkutanao na mabalozi wa halmashauri ya mji mdogo wa makambako pamoja na viongozi wa chama hicho mkoa uliofanyika katika ukumbi wa shule ya secondari makambako mjini humo. “Tulijipanga vizuri tuliomba nguvu ya ziada kutoka makao…
CHADEMA WAMJIBU NDUGAI KAULI YAKE YA KUTAKA KUSITISHA MSHAHARA TUNDU LISSU
Tundu Lissu
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KAULI YA SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI KUTAKA KUSITISHA MSHAHARA WA MBUNGE TUNDU LISSU
Leo tarehe 07.02.2019 tumeisikia kauli nyingine tena ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa anasitisha mshahara na malipo yote ambayo Mhe.Tundu Lissu anastahili kulipwa kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu.
Spika ametoa tangazo hilo siku chache tangu alipotoa matangazo mengine mawili kuwa anafikiria kumfuta Ubunge na alishamlipa fedha za matibabu kiasi cha shillingi milioni 250, jambo ambalo ilikuja kuthibitika Kuwa ni uongo na Spika alisema amenukuliwa kimakosa!
Spika wa Bunge ametoa kauli hizi katika kipindi ambacho anapambana kuonyesha kuwa Bunge analoliongoza sio 'Dhaifu' kama ambavyo alinukuliwa akisema CAG na ambaye aliitwa kwenye kamati ya Bunge ili akathibitishe kauli yake kuwa 'Bunge ni dhaifu' na tangu alipoenda mbele ya Kamati Spika hajawahi kuelezea UMMA kama kamati ililubaliana na hoja za CAG kuwa Bunge ni dhaifu ama laa!
Tunapenda kumkumbusha Spika wa Bunge kuwa 'taasisi' isiyofuata Sheria na Kanuni ambazo imejiwekea na badala yake ikafuata kauli na matamko ya mtu yaliyo kinyume na sheria na kanuni za taasisi katika kujiendesha ni taasisi dhaifu Sana.
Tunamkumbusha Spika wa Bunge kuwa wapo wabunge wengi kwenye historia ya Bunge letu ambao wamewahi na wengine wapo kwenye matibabu na haijawahi kutokea tukashuhudia kiwango kikubwa cha chuki dhidi yao kama ambavyo sasa tunashuhudia kwa Mhe.Lissu ambaye jaribio la mauaji lilishindikana kwa miujiza ya Mungu.
Tunamtaka Spika wa Bunge ajue kuwa wabunge kama Prof. Mwandosya, Dr. Mwakyembe, Job Ndugai na Sasa Tundu Lissu na Nimrod Mkono ni miongoni mwa wabunge ambao wamelazwa hospitalini kwa kipindi kirefu na katika historia ya Bunge hatujawahi Kuona kauli za chuki kama ambavyo zinatolewa dhidi ya Mhe.Lissu.
Chadema tunasikitishwa Sana na kauli hizi kwani ni uthibitisho wa wazi kuwa Bunge lilipokataa kulipia matibabu ya Lissu walikuwa wana nia Mbaya dhidi ya maisha yake na walipoona watanzania wameendelea kulipia matibabu yake imewaumiza !
Chadema tunamtaka Spika wa Bunge asimamie sheria na kanuni za Bunge na ajue kuwa wabunge wana haki ambazo zipo kwa mujibu wa Sheria na hawafanyi kazi zao kwa kutegemea fadhila.
Tunawaomba Wanachama wetu wamuombee Spika pamoja na wabunge ili waachane na 'roho za chuki' dhidi ya mbunge !ambaye Mungu alimuokoa baada ya kupigwa risasi 16 zilizoingia ndani ya mwili wake.
Tunapenda kumkumbusha Spika Ndugai kuwa haki huinua Taifa.
Imetolewa na;
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
07 Februari, 2019
Ulimbukeni Mtandaoni : MUME AUAWA BAADA YA MKE KUCHUKUA MABUNDA YAKE YA PESA NA KUJIGAMBA NAYO FACEBOOK

Bwana mmoja raia wa Nigeria aitwaye Enango Gelsthorpe Sege ameuawa kwa kupigwa na majambazi waliojihami kwa silaha baada ya mke wake kujigamba mtandaoni /facebook akiwa na mabunda ya pesa zake.
Mtu anayedai kuwa kaka yake marehemu, kwa masikitiko makubwa alisema alipokea taarifa kuhusu kifo hicho Jumanne, Februari 5,2019.
Enango Gelsthorpe Sege aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi baada ya mke wake kujigamba mtandaoni akiwa na mabunda ya pesa.
Ibomo Rafeal Seimiengha, ambaye ni kaka ya marehemu alisema kwamba, Enango alishambuliwa na majambazi hao na hatimaye kupigwa risasi.
"Nilipata habari hizi za kutisha jana. Kaka yangu alipigwa risasi nyumbani kwake na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha. Ni makosa ya mke. Mke alichapisha picha Facebook akiwa na mabunda ya pesa. Kaka yangu alikuwa amelipwa na kampuni yake. Lala Salama Enango Gelsthorpe Sege.",alieleza.
Inaelezwa kuwa marehemu aliuawa akiwa nyumbani kwake na majambazi hao walivunja na kuingia bila ya yeye na mke wake kufahamu.
Kabla ya kifo chake, Enango alikuwa amelipwa na mwajiri wake na aliamua kwenda na mabunda ya noti nyumbani kwake.
Kisha mke wake aliyekuwa na furaha mpwitompwito alijipiga picha akiwa na mabunda ya noti hizo mkononi na kuzianika mtandaoni.
Katika picha hizo, ilikuwa bayana kwamba, mke wake Enango aliutaka ulimwengu mzima kuona jinsi walivyokuwa na utajiri wa pesa lakini mwisho ukawa mbaya sana.
SIMBA NA YANGA ZATUPWA NAFASI ZA SITA NA SABA

Hatimaye bodi ya ligi (TPLB) imeweka wazi kuwa moja ya tatizo kubwa linaliosababisha kubadilishwa kwa ratiba ya ligi kuu ni timu kutokuwa na viwanja vyake ambapo katika timu 20 za ligi kuu zinazomiliki viwanja ni tano pekee na Yanga na Simba si miongoni mwao.
Akiongea kwenye mahojiano maalum na www.eatv.tv, Mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura amesema tangu kuanza kwa msimu wa 2018/19 ni viwanja vitano pekee ambavyo havijabadilishiwa mechi.
''Suala la ligi kubadilika lipo tu na sio kwa matakwa yetu muda mwingine ni changamoto ya matumizi ya viwanja ambapo mnaweza kupanga vizuri ratiba lakini uwanja ukabadilishiwa matumizi na kwakuwa klabu haikumiliki lazima ikubali kupisha'', amesema.
Aidha Wambura amezitaja timu 5 zinazomiliki viwanja kuwa ni Azam FC (Azam Complex), Mtibwa Sugar (Manungu), Mwadui FC (Mwadui Complex), Ruvu Shooting (Mabatini) na JKT Tanzania (JKT Mbweni).
Wambura amesema kama timu zitamiliki viwanja vyake itapunguza ratiba kubadilika mara kwa mara tofauti na sasa ambapo mechi moja tu ikibadilika inakuwa na athari za moja kwa moja kwenye michezo mingine.
Chanzo - EATV
MBUNGE ATAKA MASHINE KUPIMA WABUNGE WENYE MKONO WA SWETA

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Ngonyani ametaka wabunge ambao hawajafanyiwa tohara kuchunguzwa na wakibainika wafanyiwe, akibainisha kuwa hiyo ni mbinu mojawapo kupambana na maambukizi ya Ukimwi.
Jackline ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 7, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa taarifa ya kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi.
Amesema kwa utafiti ambao umefanyika unaonyesha wanaume ambao hawajatahiriwa wamekuwa wakiambukiza magonjwa mbalimbali, ukiwemo Ukimwi kwa asilimia 60.
Mbunge huyo alikatishwa na mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini aliyempa taarifa kwamba hata Bunge la Kenya liliweka wataalam mbele ya mlango wa Bunge, wale waliobainika hawajatahiriwa walipata tiba.
“Ni sahihi kabisa Spika unaweza kuchukua utaratibu huo ili kuepuka maambukizi ya Ukimwi,” amesema Selasini.
Baada ya taarifa hiyo, Jackline aliendelea kuzungumza akibainisha kuwa zoezi hilo ni vyema lianzie kwa wabunge na watakaobainika hawajatahiriwa wafanyiwe tohara mara moja.
Amesema pia wasiofanyiwa tohara wamekuwa wakiambukiza kansa ya kizazi kwa wanawake.
Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia alimpa taarifa Jackline kuwa wakati akitoa hoja ya wabunge wanaume wapimwe mikono sweta, hawakuwepo ndani ya ukumbi wa Bunge ili waweze kuunga mkono hoja hiyo.
Ghasia amesema jambo la kusikitisha wasiofanyiwa tohara wanakwenda kuambukiza magonjwa wanawake.
Hata hivyo, mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku ‘Musukuma’ alitoa taarifa akisema si jambo jema kutaka wabunge wasiofanyiwa tohara waweze kutambulika na kufanyiwa.
“Lakini pia takwimu zinaonesha kuwa hata wanawake waliokeketwa pia wanachangia maambikizi ya Ukimwi. Hivyo tuwekewe mashine ili wakati tunapima wanaume wasiotahiriwa basi tupime na wanawake waliokeketwa,” amesema.
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
WAJASIRIAMALI DODOMA WAIPA SIKU 14 HALMASHAURI KUZUIA MAGARI YA MIZIGO SOKONI
Umoja wa wafanya Biashara wa Masoko Rasmi ya matunda, mboga mboga na samaki wabichi wametoa siku 14 kwa halmashauri ya jiji la dodoma kuhakikisha wanafanyia kazi matamko na matangazo ambayo yamekuwa yakitolewa na mamlaka hiyo kuhusu kutoruhusu magari ya mizigo na wauzaji jumla wa bidhaa hizo kuhakikisha wanashusha bidhaa hizo kwenye soko rasmi la bonanza na sio mahali pengine Akitoa tamko hilo la umoja huo wa wafanyabiashara saidi muumba katibu wa soko la tambukareli amesema kuwa tangu mwaka 2009 halmashauri ya jiji la dodoma lilizuia magari yakushusha bidhaa za samaki…
KAULI YA WAZIRI MKUU KUHUSU ONGEZEKO LA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA TANZANIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa, amewataka watumishi wa umma kuwa na subira kwa sababu Serikali inaendelea na mchakato wa kuwatambua watumishi wa umma halali na kufanya ulinganifu wa mishahara katika kada mbalimbali ili watumishi hao waanze kulipwa mishahara stahiki.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe Pascal Haonga, lililohoji juu ya ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma.
Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa mwanzoni nchi ilikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakilipwa mishahara na posho mbalimbali hivyo, ili kuwatambua watumishi halali Serikali iliamua kufanya uchunguzi na kuwagundua watumishi hao hewa.
Pia, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine wa kuwatambua watumishi wenye vyeti stahiki vya kufanya kazi mbalimbali Serikalini kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa baada ya kumaliza utambuzi wa watumishi halali, Rais Dkt. Magufuli aliunda Tume ya Mishahara na Motisha kwa ajili ya kufanya mapitio ya kada zote za Utumishi wa Umma na viwango vya mishahara ili kutambua ulinganifu kati ya stahiki ya mshahara na kada husika.
"Lengo la Rais Magufuli kuunda tume hiyo ni kufanya tathmini nzuri ili kutambua weledi wa kazi, uwajibikaji na tija inayopatikana mahala pa kazi, hivyo baada ya kukamilika Serikali itatoa taarifa," alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa rai kwa Watumishi wa Umma kuendelea kuiamini serikali kwani ina nia ya dhati kuhakikisha watumishi wote wanapata haki zao stahiki vile vile mpaka sasa mjadala kati ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi unaendelea vizuri.
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO





